Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
01-Kiumbe Bora Kabisa Wa Kwanza Kufufuliwa
Na Kwanza Kuomba Ash-Shafaa’ah
Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni kiumbe bora kabisa, na wa kwanza kufufuliwa na wa kwanza atakayeruhusiwa kuomba Ash-Shafaa’ah (uombezi) Siku ya Qiyaamah:
عن أَبُي هُرَيْرَةَ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "أَنَا سَيِّدُ وَلَدِ آدَمَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَأَوَّلُ مَنْ يَنْشَقُّ عَنْهُ الْقَبْرُ وَأَوَّلُ شَافِعٍ وَأَوَّلُ مُشَفَّعٍ " رواه مسلم
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema: ((Mimi ni Bwana wa mtoto wa Aadam Siku ya Qiyaamah, na (mimi) wa kwanza ambaye kaburi lake litapasuka, na wa kwanza wa kushufai, na wa kwanza ambaye atakayeombewa Ash-Shafaa’ah)) [Muslim]
An-Nawawiy akasema katika Sharh Swahiyh Muslim: “Hadiyth hii ni dalili ya ubora wake Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam juu ya viumbe wote wengineo kwa sababu madhehebu ya Ahlus-Sunnah wanawafikiana kwamba bin Aadam ni bora kuliko Malaika, naye Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam ni bora kuliko bin Aadam wengineo.”
Links
[1] http://www.alhidaaya.com
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9418&title=01-Fadhila%20Za%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%3A%20Kiumbe%20Bora%20Kabisa%20Wa%20Kwanza%20Kufufuliwa%20Na%20Kwanza%20Kuomba%20Ash-Shafaa%E2%80%99ah