SW
A. Aleykum! Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 21 na hapa karibuni nimepata mchumba anataka kunioa lakini kuna tatizo moja kabila, na wazazi wangu nauhakika hawatakubali mimi kuolewa naye..Nampenda huyo kijana maana Allaah habagui rangi wa kabila sisi wote ni wa kwake..Sheikh sipendi kuwaudhi wazazi wangu nawapenda na kuwaheshimu
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Kwanza kabla hatujajibu swali lako, tunakukumbusha kuwa unapoandika Salaam hazifai kufupishwa kwa kuandikwa (A.A) au (A.A.W.W.) au kama ulivyoandika kwani haijafundishwa hivyo na pia ni kujikosesha fadhila za Salaam
Shukran zetu za dhati kwa swali lako kuhusu posa na ndoa kwa kijana asiyekuwa kabila lako. Na kulikuwa hakuna haja kwako kuomba msamaha kwa Kiswahili ulichoandika kwani swali
Utata uliopo ni kuwa tayari wewe umeamua kuwa wazazi watakataa posa ya kijana huyo hata kabla ya wazazi wake kuja kuposa. Inatakiwa dada yetu hata kabla ya kuwa na rai hiyo umwambie huyo kijana awaambie wazazi wake wakapeleke posa rasmi kwenu. Nyinyi lenu ni kungojea majibu yatakayotoka huko. Hatujui maoni yako umeyatoa kwa sababu alikuja mtu wa kabla jingine akakataliwa au maoni yako yamefungamanishwa kwa kuwajua kuwa wazazi wako ni wabaguzi? Mara nyingi huwa tunakosea katika
Waache wazazi wakatae baada ya kuwa wazazi wa kijana wamekwenda kwa njia ya halali. Wala wewe usichukue hatua yoyote kwa wakati wote huo na uwe ni mwenye kuwatii kwa yote. Hata hivyo, labda tukuulize swali kidogo kuhusu
Pia, je huyo kijana mwenyewe anataka kukuoa au wewe unamlazimisha?
Kuwa na maisha mazuri katika ndoa ni lazima kijana mwenyewe awe naye anakupenda, ikiwa ni kinyume na hivyo, kijana huyo atakutumia bure.
Ikiwa kijana ameshika Dini na anataka kuja kuposa sio kukuchezea na kisha kukutupa, tutaweza kukupatia ushauri katika
Tunalohofia ikiwa uko sawa kutowafuata wazazi si laana kwani laana ya batili haimfikii mtu, lakini ni kutokuwa na kinga wewe kijana wa kike. Wanaume wanaeleweka, wengi wao ni wazuri na wengi pia ni wabaya wasiokuwa na misimamo ya sawa na ya kidini. Mwanamme kawaida anamdharau mwanamke ambaye amewaasi wazazi na kumfuata yeye. Tumepata mashtaka mengi ya kuteswa wanawake
Hata ndoa ikifaulu watoto wenu watakuwa na raha gani ikiwa hawawezi kuwazuru mababu na mabibi zao. Kuwa makini, wewe kutoolewa na kijana huyo sio mwisho wa ulimwengu. Wakikataa wazazi wewe hutalaumiwa na Allaah Aliyetukuka bali wao ndio watakaopata madhambi kwa
Usifanye uamuzi wa haraka na tunamuomba Allaah Aliyetukuka ikiwa mume huyo ana kheri nawe Akusahilishie mambo yako na aifanye harusi na tangamano la kheri. Ikiwa si kheri nawe basi Akuepushie mbali
Na Allaah Anajua zaidi
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/56
[2] http://www.alhidaaya.com/sw/nasiha_kiislamu
[3] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F2863&title=Nataka%20Kuolewa%20Na%20Kijana%20Nimpendaye%20Lakini%20Wazazi%20Hawatakubali%20Kwa%20Ajili%20ya%20Ukabila%20Na%20Rangi.