Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب الحياء وفضله والحث على التخلق به
01-Mlango Wa Haya na Fadhila Zake na Kuhimizwa Kuwa na Maadili Hayo
Alhidaaya.com [4]
Hadiyth – 1
عن ابن عمر رضي الله عنهما : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم مَرَّ عَلَى رَجُلٍ مِنَ الأنْصَار وَهُوَ يَعِظُ أخَاهُ في الحَيَاءِ ، فَقَالَ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( دَعْهُ ، فَإنَّ الْحَيَاءَ مِنَ الإيمَانِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipota kwa mtu fulani miongoni mwa Answaar, naye alikuwa anamuonya ndugu yake katika haya. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Mwache kwani kuwa na haya ni katika Iymaan." [Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy, Abu Daawuud, An-Nasai na Malik].
Hadiyth – 2
وعن عمران بن حصينٍ رضي الله عنهما ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( الْحَيَاءُ لاَ يَأْتِي إِلاَّ بِخَيْرٍ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
وفي رواية لمسلمٍ : (( الحياءُ خَيْرٌ كُلُّهُ )) أَوْ قَالَ : (( الْحَيَاءُ كُلُّهُ خَيْرٌ )) .
Imepokewa kutoka kwa 'Imraan bin Huswayn (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Haya haileti isipokuwa kheri." [Al-Bukhaariy, Muslim na Abu Daawuud].
Katika Riwaayah ya Muslim: "Haya ni kheri yote" au amesema: "Haya yote ni kheri."
Hadiyth – 3
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( الإيمَانُ بِضْعٌ وَسَبْعُونَ أَوْ بِضْعٌ وَسِتُّونَ شُعْبَةً : فَأفْضَلُهَا قَوْلُ : لاَ إلهَ إِلاَّ الله ، وَأدْنَاهَا إمَاطَةُ الأَذَى عَنِ الطَّرِيقِ ، وَالحَيَاءُ شُعْبَةٌ مِنَ الإيمَانِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Iymaan ina sehemu sitini. Iliyo bora zaidi ni kauli ya Laa Ilaaha Illa Allaah (Hapana anayepasa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah) na ya chini kabisa ni kuondosha chenye kuudhi njiani. Na kuwa na haya ni sehemu ya Iymaan." [Al-Bukhaariy na Muslim].
Hadiyth – 4
وعن أَبي سعيدٍ الخدري رضي الله عنه ، قَالَ : كَانَ رسول الله صلى الله عليه وسلم أشَدَّ حَيَاءً مِنَ العَذْرَاءِ في خِدْرِهَا ، فَإذَا رَأَى شَيْئاً يَكْرَهُهُ عَرَفْنَاهُ في وَجْهِه . متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iyd Al-Khudhry (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikua ni mtu mwenye haya sana kuliko mwanamwari chumbani kwake, akiona kitu anachokichukia tunajua kupitia usoni mwake." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
بابُ حفظ السِّر
02-Mlango Wa Kuhifadhi Siri
Alhidaaya.com [4]
قَالَ الله تَعَالَى:
وَأَوْفُوا بِالْعَهْدِ ۖ إِنَّ الْعَهْدَ كَانَ مَسْئُولًا ﴿٣٤﴾
Na timizeni ahadi; hakika ahadi itakuwa ni ya kuulizwa. [Al-Israa: 34]
Hadiyth – 1
وعن أَبي سعيد الخدري رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( إنَّ مِنْ أشَرِّ النَّاسِ عِنْدَ اللهِ مَنْزِلَةً يَوْمَ القِيَامَةِ الرَّجُلَ يُفْضِي إِلَى الْمَرْأةِ وتُفْضِي إِلَيْهِ ، ثُمَّ يَنْشُرُ سِرَّهَا )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika watu waovu kabisa kwa daraja mbele ya Allaah Siku ya Qiyaamah ni mtu aliyejamiiana na mkewe na mke aliyestarehe na mumewe kisha mmoja wao akatangaza siri hiyo." [Muslim]
Hadiyth – 2
وعن عبدِ الله بن عمر رضي الله عنهما : أنَّ عمرَ رضي الله عنه حِيْنَ تأيَّمَتْ بِنْتُهُ حَفْصَةُ ، قَالَ : لَقِيتُ عُثْمَانَ بْنَ عَفّانَ رضي الله عنه ، فَعَرَضْتُ عَلَيْهِ حَفْصَةَ ، فَقُلْتُ : إنْ شِئْتَ أَنْكَحْتُكَ حَفْصَةَ بِنْتَ عُمَرَ ؟ قَالَ : سأنْظُرُ فِي أمْرِي . فَلَبِثْتُ لَيَالِيَ ثُمَّ لَقِيَنِي ، فَقَالَ : قَدْ بَدَا لِي أنْ لاَ أتَزَوَّجَ يَوْمِي هَذَا . فَلَقِيتُ أَبَا بَكْرٍ رضي الله عنه ، فقلتُ : إنْ شِئْتَ أنْكَحْتُكَ حَفْصَةَ بنْتَ عُمَرَ ، فَصَمتَ أَبُو بَكْرٍ رضي الله عنه ، فَلَمْ يَرْجِعْ إلَيَّ شَيْئاً ! فَكُنْتُ عَلَيْهِ أوْجَدَ مِنِّي عَلَى عُثْمَانَ ، فَلَبِثَ لَيَالِيَ ثُمَّ خَطَبَهَا النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم ، فَأنْكَحْتُهَا إيَّاهُ . فَلَقِيَنِي أَبُو بَكْرٍ ، فَقَالَ : لَعَلَّكَ وَجَدْتَ عَلَيَّ حِيْنَ عَرَضْتَ عَلَيَّ حَفْصَةَ فَلَمْ أرْجِعْ إِلَيْكَ شَيْئاً ؟ فقلتُ : نَعَمْ ، قَالَ : فَإنَّهُ لَمْ يَمْنَعْنِي أنْ أرْجِعَ إِلَيْك فِيمَا عَرَضْتَ عَلَيَّ إِلاَّ أنِّي كُنْتُ عَلِمْتُ أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم ذَكَرَهَا ، فَلَمْ أكُنْ لأُفْشِيَ سِرَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، وَلَوْ تَرَكَهَا النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم لَقَبِلْتُهَا . رواه البخاري .
Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah bin 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) ya kwamba pindi Hafswah bint 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhaa) alipoachwa mjane (kufa mumewe), 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) alikutana na 'Uthmaan bin 'Affaan (Radhwiya Allaahu 'anhu) na kumwambia: "Ukitaka nitakuoza bint yangu, Hafswah." Akasema: "Nitaangalia jambo hilo." Akakaa kwa siku kadhaa, kisha akakutana na 'Umar na kumwambia: "Nimefikiria juu ya mas-ala hayo na naona kuwa sitaowa hivi karibuni." Baada ya hapo nilikutana na Abu Bakr (Radhwiya Allaahu 'anhu) nikasema: "Ukitaka nitakuoza Hafswah bint 'Umar." Abu Bakr alikaa kimya na wala hakunijibu chochote. Jambo hili liliniuma zaidi kuliko jawabu la 'Uthmaan. Nilikaa kwa siku chache mara Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaleta posa na mimi nukamuozesha. Akakutana nami Abu Bakr, ambaye aliniambia: "Huenda ukawa hukufurahi wakati ulipotaka nimuoe Hafswah, nami sikukujibu lolote." Nikasema: "Ndio." Akasema: "Hakika hakuna kilicho nizuia mimi kukubali hilo ila nilijua ya kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa tayari amemtaja (kwa nia ya kumuoa). Na sikuweza kutoa siri ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na lau Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) asingemuoa basi mimi ningekubali maombi yako hayo." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 3
وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : كُنَّ أزْوَاجُ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم عِنْدَهُ ، فَأقْبَلَتْ فَاطِمَةُ رضي الله عنها تَمْشِي ، مَا تُخْطِئُ مِشيتُها مِنْ مشْيَةِ رسول الله صلى الله عليه وسلم شَيْئاً ، فَلَمَّا رَآهَا رَحَّبَ بِهَا ، وقال : (( مَرْحَباً بابْنَتِي )) ، ثُمَّ أجْلَسَهَا عَنْ يَمِينِهِ أَوْ عَنْ شِمَالِهِ ، ثُمَّ سَارَّهَا فَبَكتْ بُكَاءً شَديداً ، فَلَمَّا رَأى جَزَعَهَا ، سَارَّهَا الثَّانِيَةَ فَضَحِكَتْ ، فقلتُ لَهَا : خَصَّكِ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم مِنْ بَيْنِ نِسَائِهِ بالسِّرَارِ ، ثُمَّ أنْتِ تَبْكِينَ ! فَلَمَّا قَامَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم سَألْتُهَا : مَا قَالَ لَكِ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم ؟ قالت : مَا كُنْتُ لأُفْشِي عَلَى رسول الله صلى الله عليه وسلم سِرَّهُ ، فَلَمَّا تُوُفِّيَ رسول الله صلى الله عليه وسلم قُلْتُ : عَزَمْتُ عَلَيْكِ بِمَا لِي عَلَيْكِ مِنَ الحَقِّ ، لَمَا حَدَّثْتِنِي مَا قَالَ لَكِ رسول الله صلى الله عليه وسلم ؟ فقالتْ : أمَّا الآن فَنَعَمْ ، أمَّا حِيْنَ سَارَّنِي في المَرَّةِ الأُولَى فأخْبَرَنِي أنّ جِبْريلَ كَانَ يُعَارِضُهُ القُرآنَ في كُلِّ سَنَةٍ مَرَّةً أَوْ مَرَّتَيْنِ ، وَأنَّهُ عَارَضَهُ الآنَ مَرَّتَيْنِ ، وَإنِّي لا أُرَى الأجَلَ إِلاَّ قَدِ اقْتَرَبَ ، فَاتَّقِي اللهَ وَاصْبِرِي ، فَإنَّهُ نِعْمَ السَّلَفُ أنَا لَكِ ، فَبَكَيْتُ بُكَائِي الَّذِي رَأيْتِ ، فَلَمَّا رَأى جَزَعِي سَارَّنِي الثَّانِيَةَ ، فَقَالَ : (( يَا فَاطِمَةُ ، أمَا تَرْضَيْنَ أنْ تَكُونِي سَيِّدَةَ نِسَاءِ المُؤُمِنِينَ ، أَوْ سَيَّدَةَ نِساءِ هذِهِ الأُمَّةِ ؟ )) فَضَحِكتُ ضَحِكِي الَّذِي رَأيْتِ . متفقٌ عَلَيْهِ ، وهذا لفظ مسلم .
Imepokewa kutoka kwake 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amesema: Sote wake wa Nabiy (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) tuko naye wakati mmoja mara akaja Faatwimah. Utembeaji wake ulikuwa kama ule wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Alipomuona alimkaribisha kwa kumwambia: "Karibu, bint yangu." Kisha akamkalisha uapande wake wa kulia au wa kushoto kisha kumnong'oneza kitu ambacho kilimliza sana. Alipomwuona na huzuni kubwa, alimnog'oneza mara ya pili, naye akacheka. Nikamuliza: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amewapuuza wakeze wote na kuzungumza nawe kwa siri, kisha wewe ukalia." Alipoondoka Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) nilimuuliza: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekuambia nini?" Akasema: "Siwezi kutoa siri ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)." Alipoaga dunia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) nilimuuliza: "Nakuomba kwa jina la Allaah kwa ile haki niliyo nayo juu yako, uniambie ni jambo gani alilokuambia Rasuli wa Allaah?" Akasema: "Ama sasa naweza kukuambia. Hakika pale aliponionong'oneza mara ya kwanza alinipasha habari kuwa: 'Jibriyl alikuwa kila mwaka akimsomea na kisha akimsikiliza Qur-aan mara moja au mara mbili. Na ama sasa anafanya hivyo mara mbili. Na hakika naona kuwa wakati wangu umefika. Hivyo, mche Allaah na usubiri, kwani hakika mimi ni mtangulizi mwema kwako. Nililia kilio changu ulivyoona. Alipoona huzuni yangu, aliniong'oneza mara ya pili akasema: "Ee Faatwimah! Huridhiki kuwa wewe bibi wa ummah huu?' Nikacheka kicheko changu ulivyoona." [Al-Bukhaariy na Muslim, na hii ni lafdhi ya Muslim]
Hadiyth – 4
وعن ثَابِتٍ ، عن أنس رضي الله عنه ، قَالَ : أتَى عَلَيَّ رسول الله r وَأنَا ألْعَبُ مَعَ الغِلْمَانِ ، فَسَلمَ عَلَيْنَا ، فَبَعَثَني إِلَى حاجَةٍ ، فَأبْطَأتُ عَلَى أُمِّي . فَلَمَّا جِئْتُ ، قالت : مَا حَبَسَكَ ؟ فقلتُ : بَعَثَني رسولُ الله صلى الله عليه وسلم لِحَاجَةٍ ، قالت : مَا حَاجَتُهُ ؟ قُلْتُ : إنَّهاَ سرٌّ . قالت : لا تُخْبِرَنَّ بِسرِّ رسول الله صلى الله عليه وسلم أحَداً ، قَالَ أنَسٌ : وَاللهِ لَوْ حَدَّثْتُ بِهِ أحَداً لَحَدَّثْتُكَ بِهِ يَا ثَابِتُ . رواه مسلم وروى البخاري بعضه مختصراً .
Imepokewa kutoka kwa Thaabit kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Alinijia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) nilikuwa ninachezsa na watoto, Alitusalimia akanituma haja, hivyo nikachelewa kwa mamangu. Nilipofika nyumbani , akaniuliza: "Nini kimekuchelewesha?" Nikasema: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alinituma haja." Akasema: "Ni haja gani?" Nikasema: "Hiyo ni siri." Akaniambia: "Usimwambie yoyote siri ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ." Akasema Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu): "Naapa kwa Allaah! Lau ningekuwa ni mwenye kufichua siri hiyo kwa yeyote basi ningekueleza wewe, ee Thaabit." [Muslim, na Al-Bukhaariy amenukuu baadhi yake kwa mukhtasar]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب الوفاء بالعهد وَإنجاز الوَعد
03-Mlango Wa Kutekeleza Ahadi
Alhidaaya.com [4]
قَالَ الله تَعَالَى:
وَأَوْفُوا بِالْعَهْدِ ۖ إِنَّ الْعَهْدَ كَانَ مَسْئُولًا ﴿٣٤﴾
Na timizeni ahadi; hakika ahadi itakuwa ni ya kuulizwa. [Al-Israa: 34]
وَأَوْفُوا بِعَهْدِ اللَّـهِ إِذَا عَاهَدتُّمْ ﴿٩١﴾
Na timizeni ahadi ya Allaah mnapoahidi. [An-Nahl: 91]
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَوْفُوا بِالْعُقُودِ ۚ ﴿١﴾
Enyi walioamini! Timizeni mikataba. [Al-Maaidah: 1]
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لِمَ تَقُولُونَ مَا لَا تَفْعَلُونَ﴿٢﴾ كَبُرَ مَقْتًا عِندَ اللَّـهِ أَن تَقُولُوا مَا لَا تَفْعَلُونَ﴿٣﴾
Enyi walioamini! Kwanini mnasema yale msiyoyafanya? Ni chukizo kubwa mno mbele ya Allaah kwamba mnasema yale msiyoyafanya. [Asw-Swaff: 2-3]
Hadiyth – 1
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( آيَةُ المُنَافِقِ ثَلاَثٌ : إِذَا حَدَّثَ كَذَبَ ، وَإِذَا وَعَدَ أخْلَفَ ، وَإِذَا اؤْتُمِنَ خَانَ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Alama za mnafiki ni tatu: Anapozungumza anasema uwongo; na anapoahidi huvunja ahadi; na anapoaminiwa hufanya hiyana." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 2
وعن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( أرْبَعٌ مَنْ كُنَّ فِيهِ كَانَ مُنَافِقاً خَالِصاً ، وَمَنْ كَانَتْ فِيهِ خَصْلَةٌ مِنْهُنَّ كَانَتْ فِيهِ خَصْلَةٌ مِنَ النِّفَاقِ حَتَّى يَدَعَهَا : إِذَا اؤْتُمِنَ خَانَ ، وَإِذَا حَدَّثَ كَذَبَ ، وَإِذَا عَاهَدَ غَدَرَ ، وَإِذَا خَاصَمَ فَجَرَ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa 'Abdilaah bin 'Amruu bin Al-'Aas (Radhwiya Allahu 'anhumaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mtu yeyote akiwa na mambo manne atakuwa mnafiki hasa, na kama atakuwa na moja katika hayo manne: atakuwa na sifa ya unafiki mpaka aliache. Akiaminiwa hufanya hiyana; na akizungumza anaongopa; na anapotoa ahadi huvunja na anapogombana anaiacha haki kuwa jeuri." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 3
وعن جابر رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ لي النبيُّ صلى الله عليه وسلم : (( لَوْ قَدْ جَاءَ مَالُ الْبَحْرَيْنِ أعْطَيْتُكَ هكَذَا وَهَكَذَا وَهكَذَا )) فَلَمْ يَجِئْ مَالُ الْبَحْرَينِ حَتَّى قُبِضَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم ، فَلَمَّا جَاءَ مَالُ الْبَحْرَيْنِ أمَرَ أَبُو بَكْرٍ رضي الله عنه فَنَادَى : مَنْ كَانَ لَهُ عِنْدَ رسول الله صلى الله عليه وسلم عِدَةٌ أَوْ دَيْنٌ فَلْيَأتِنَا ، فَأتَيْتُهُ وَقُلْتُ لَهُ : إنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم قَالَ لي كَذَا وَكَذَا ، فَحَثَى لي حَثْيَةً فَعَدَدْتُهَا ، فَإذَا هِيَ خَمْسُمِئَةٍ ، فَقَالَ لِي : خُذْ مِثْلَيْهَا . متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema aliniambia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Lau mali ya Bahrayn itakuja basi nitakupatia hivi na hivi." Mali ya Bahrayn haikuja mpaka akafariki Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Ilipokuja mali kutoka Bahrayn Abu Bakr (Radhwiya Allaahu 'anhu) aliamuru kutangazwe: 'Ambaye ana ahadi kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), au anayemdai aje kwetu. Nilifika kwake na kumwambia: "Hakika Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliniambia hivi na vile." Abu Bakr alinichotea fedha Nilipozihesabu zilikuwa ni Dirhamu mia tano. Kisha akaniambia: "Chukua mfano wake mara mbili." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب المحافظة عَلَى مَا اعتاده من الخير
03-Mlango Wa Kuhifadhi Aliyozoea Katika Mambo ya Kheri
Alhidaaya.com [4]
قَالَ الله تَعَالَى:
إِنَّ اللَّـهَ لَا يُغَيِّرُ مَا بِقَوْمٍ حَتَّىٰ يُغَيِّرُوا مَا بِأَنفُسِهِمْ ۗ ﴿١١﴾
Hakika Allaah Habadilishi yale yaliyoko kwa watu mpaka wao wenyewe wabadilishe yale yaliyomo katika nafsi zao. [Ar-Ra'd: 11]
وَلَا تَكُونُوا كَالَّتِي نَقَضَتْ غَزْلَهَا مِن بَعْدِ قُوَّةٍ أَنكَاثًا ﴿٩٢﴾
Na wala msiwe kama yule mwanamke aliyezongoa uzi wake vipande vipande baada ya (kuusokota na) kuwa mgumu [An-Nahl: 92]
وَلَا يَكُونُوا كَالَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلُ فَطَالَ عَلَيْهِمُ الْأَمَدُ فَقَسَتْ قُلُوبُهُمْ ۖ ﴿١٦﴾
Na wala wasiwe kama wale waliopewa Kitabu kabla, ukawatawilikia muda, kisha zikawa ngumu nyoyo zao? [Al-Hadiyd: 16]
فَمَا رَعَوْهَا حَقَّ رِعَايَتِهَا ۖ ﴿٢٧﴾
Lakini hawakuuchunga ipasavyo kuchungwa. [Al-Hadiyd: 27]
Hadiyth – 1
وعن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما ، قَالَ : قَالَ لي رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( يَا عبْدَ الله ، لاَ تَكُنْ مِثْلَ فُلانٍ ، كَانَ يَقُومُ اللَّيْلَ فَتَرَكَ قِيَامَ اللَّيْلِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah usiwe mfano wa fulani ambaye alikuwa akiswali Swalaah ya usiku kisha akaacha kisimamo hicho cha usiku." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب استحباب طيب الكلام وطلاقة الوَجه عند اللقاء
05-Mlango Wa Kupendeza Kuzungumza Vizuri na Kuwa na Bashasha Wakati wa Kukutana na Mtu
Alhidaaya.com [4]
قَالَ الله تَعَالَى:
وَاخْفِضْ جَنَاحَكَ لِلْمُؤْمِنِينَ﴿٨٨﴾
Na inamisha bawa lako kwa Waumini (kuwahurumia). [Al-Hijr: 88]
وَلَوْ كُنتَ فَظًّا غَلِيظَ الْقَلْبِ لَانفَضُّوا مِنْ حَوْلِكَ ۖ ﴿١٥٩﴾
Na lau ungelikuwa mjeuri mwenye moyo mgumu wangelitawanyika mbali nawe. [Aal-'Imraan: 159]
Hadiyth – 1
وعن عدي بن حاتمٍ رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( اتَّقُوا النَّارَ وَلَوْ بِشِقِّ تَمْرَةٍ فَمَنْ لَمْ يَجِدْ فَبِكَلِمَةٍ طَيِّبَةٍ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa 'Adiyy bin Haatim (Radhwiya Allaahu 'anhu) Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Jiepusheni au jikingeni na moto japokuwa kwa kutoa kipande cha tende moja." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 2
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( وَالكَلِمَةُ الطَّيِّبَةُ صَدَقَةٌ )) متفقٌ عَلَيْهِ
Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Na maneno mazuri ni swadaqah." [Al-Bukhaariy na Muslim].
Hadiyth – 3
وعن أَبي ذَرٍّ رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ لي رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( لاَ تَحْقِرَنَّ مِنَ الْمَعْرُوفِ شَيْئاً ، وَلَوْ أنْ تَلْقَى أخَاكَ بوَجْهٍ طَلْقٍ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Dharr (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Msichukie jema lolote hata ikiwa ni kukutana na ndugu yako kwa uso wa tabasamu na bashasha." [Muslim]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب استحباب بيان الكلام وإيضاحه للمخاطب وتكريره ليفهم إذا لَمْ يفهم إِلا بذلك
06-Mlango Wa Kupendeza Kubainisha Maneno na Kuweza Wazi kwa Mwenye Kusikiliza na Kuyakariri Ili Apate Kufahamu Ikiwa Hatafahamu Ila Kwayo
Alhidaaya.com [4]
Hadiyth – 1
عن أنسٍ رضي الله عنه : أنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ إِذَا تَكَلَّمَ بِكَلِمَةً أعَادَهَا ثَلاَثاً حَتَّى تُفْهَمَ عَنْهُ ، وَإِذَا أتَى عَلَى قَوْمٍ فَسَلَّمَ عَلَيْهِمْ سَلَّمَ عَلَيْهِمْ ثَلاثاً . رواه البخاري .
Amesema Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuwa akizungumza alikuwa akirudia maneno mara tatu mpaka afahamike. Na alipokuwa akija kwa watu na kuwasalimia husalimia mara tatu." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 2
وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : كَانَ كَلاَمُ رسول الله صلى الله عليه وسلم كَلاماً فَصْلاً يَفْهَمُهُ كُلُّ مَنْ يَسْمَعُهُ . رواه أَبُو داود .
Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)Alikuwa akizungumza kwa uwazi kabisa hivyo akifahamika na kila mmoja mwenye kumsikia." [Abu Daawuud]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب إصغاء الجليس لحديث جليسه الذي ليس بحرام واستنصات العالم والواعظ حاضري مجلسه
07-Mlango Wa Mtu Kumsikiliza aliyekaa Nae Ambayo Sio Haramu, na Kumsikiliza Mwanazuoni na Mtoa Waadhi Mbele ya Mkutano Wake
Alhidaaya.com [4]
عن جرير بن عبدِ اللهِ رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ لي رسول الله صلى الله عليه وسلم في حَجَّةِ الْوَدَاعِ : (( اسْتَنْصِتِ النَّاسَ )) ثُمَّ قَالَ : (( لاَ تَرْجِعُوا بَعْدِي كُفّاراً يَضْرِبُ بَعْضُكُمْ رِقَابَ بَعْضٍ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Jariyr bin 'Abdillaah (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Aliniambia mimi Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika Hajjatul Wadaa'i (Hijjah ya kuaga): "Wanyamazishe watu." Kisha akasema: "Msirudi baada yangu katika ukafiri kwa kuuana nyinyi kwa nyinyi." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
بابُ الوَعظ والاقتصاد فِيهِ
08-Mlango Wa Kutorefusha Mawaidha
Alhidaaya.com [4]
قَالَ الله تَعَالَى:
ادْعُ إِلَىٰ سَبِيلِ رَبِّكَ بِالْحِكْمَةِ وَالْمَوْعِظَةِ الْحَسَنَةِ ۖ ﴿١٢٥﴾
Lingania katika njia ya Rabb wako kwa hikmah na mawaidha mazuri. [An-Nahl: 125]
Hadiyth – 1
وعن أَبي وائلٍ شقيقِ بن سَلَمَةَ ، قَالَ : كَانَ ابنُ مَسْعُودٍ رضي الله عنه يُذَكِّرُنَا في كُلِّ خَمِيسٍ ، فَقَالَ لَهُ رَجُلٌ : يَا أَبَا عَبْدِ الرَّحْمانِ ، لَوَدِدْتُ أنَّكَ ذَكَّرْتَنَا كُلَّ يَوْمٍ ، فَقَالَ : أمَا إنَّهُ يَمْنَعُنِي مِنْ ذَلِكَ أنَّي أكْرَهُ أنْ أُمِلَّكُمْ ، وَإنِّي أتَخَوَّلُكُمْ بِالْمَوْعِظَةِ ، كَمَا كَانَ رسول الله صلى الله عليه وسلم يَتَخَوَّلُنَا بِهَا مَخَافَةَ السَّآمَةِ عَلَيْنَا . متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Wa'il Shaqiyq bin Salamah amesema: Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) Alikuwa akitupatia mawaidha kila siku ya Alkhamisi. Mtu mmoja akamwambia yeye: "Ee Abu 'Abdur-Rahman! Natamani uwe unatupatia mawaidha kila siku." Akasema: "Hakika linalo nikataza mimi kufanya hivyo ni kuogopea kuwachosha kwa mawaidha. Mimi ninafanya kama alivyokuwa akifanya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa kutuogopea tusije tukachoka." [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]
Hadiyth – 2
وعن أَبي اليقظان عمار بن ياسر رضي الله عنهما ، قَالَ : سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( إنَّ طُولَ صَلاَةِ الرَّجُلِ ، وَقِصَرَ خُطْبَتِهِ ، مَئِنَّةٌ مِنْ فِقههِ ، فأطِيلُوا الصَّلاَةَ وَأقْصِرُوا الْخُطْبَةَ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abul Yaqdhaan 'Ammaar bin Yaasir (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Hakika mtu kurefusha Swalaah na kufupisha khutbah inayonyesha umahiri na alama ya ujuzi wake. Hivyo refusheni Swalaah na fupisheni khutbah." [Muslim]
Hadiyth – 3
وعن مُعاوِيَة بن الحكم السُّلَمي رضي الله عنه ، قَالَ : بَيْنَا أنَا أُصَلّي مَعَ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، إذْ عَطَسَ رَجُلٌ مِنَ القَوْمِ ، فَقُلْتُ : يَرْحَمُكَ اللهُ ، فَرَمَانِي القَوْمُ بِأبْصَارِهِمْ ! فَقُلْتُ : وَاثُكْلَ أُمِّيَاهُ ، مَا شَأنُكُمْ تَنْظُرُونَ إلَيَّ ؟! فَجَعَلُوا يَضْرِبُونَ بأيديهم عَلَى أفْخَاذِهِمْ ! فَلَمَّا رَأيْتُهُمْ يُصَمِّتُونَنِي لكِنّي سَكَتُّ ، فَلَمَّا صَلّى رسول الله صلى الله عليه وسلم ، فَبِأبِي هُوَ وَأُمِّي ، مَا رَأيْتُ مُعَلِّماً قَبْلَهُ وَلاَ بَعْدَهُ أحْسَنَ تَعْلِيماً مِنْهُ ، فَوَاللهِ مَا كَهَرَني ، وَلاَ ضَرَبَنِي ، وَلاَ شَتَمَنِي . قَالَ : (( إنَّ هذِهِ الصَّلاَةَ لاَ يَصْلُحُ فِيهَا شَيْءٌ مِنْ كَلامِ النَّاسِ ، إنَّمَا هِيَ التَّسْبِيحُ وَالتَّكْبِيرُ ، وَقِراءةُ القُرْآنِ )) ، أَوْ كَمَا قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم . قلتُ : يَا رسول الله ، إنّي حَدِيثُ عَهْدٍ بِجَاهِلِيَّةٍ ، وَقَدْ جَاءَ اللهُ بِالإسْلاَمِ ، وَإنَّ مِنّا رِجَالاً يَأتُونَ الْكُهّانَ ؟ قَالَ : (( فَلاَ تَأتِهِمْ )) قُلْتُ : وَمِنّا رِجَالٌ يَتَطَيَّرُونَ ؟ قَالَ : (( ذَاكَ شَيْء يَجِدُونَهُ في صُدُورِهِمْ فَلاَ يَصُدَّنَّهُمْ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Mu'awiyah bin Al-Hakam As-sulamiy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: "Nikiwa naswali pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mtu katika jamaa akacheua nikasema: "yarhamuka Allaah (Allaah Akurehemu)." Watu wakanikodolea macho. Nikasema: "Mama zenu wapotee! Mna nini mnaniangalia hivi?", wakawa wanapiga kwa mikono mapaja yao. Nilipowaona wakininyamazisha, basi nilinyamaza. Alipomaliza Swalaah Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), baba yangu na mama yangu wawe fidia kwake, sijaona mwalimu mzuri kuliko yeye kabla wala baada yake. Naapa kwa Allaah! Hakunilaumu wala hakunipiga wala hakunitukana. Alisema: "Hakika hii Swalaah, haifai ndani yake maneno ya watu. Kwa hakika hiyo ni tasbihi , takbiri na kusoma Qur-aan", au kama alivyosema: "Ee Rasuli wa Allaah! Hakika mimi ni hivi karibuni tu nimetoka katika Ujahiliyah, na Allaah ametuletea Uislaamu. Na katika sisi kuna watu wanaendea makuhani." Akasema: "Msiende kwao." Nikasema: "Miongoni mwetu wako wanao ongozwa na bahati." Akasema: "Hilo ni jambo wanaolipata katika vifua vyao (na akili zao). Wasiwazuie." [Muslim]
Hadiyth – 4
وعن العِرْباض بن ساريَةَ رضي الله عنه ، قَالَ : وَعَظَنَا رسول الله صلى الله عليه وسلم مَوْعِظَةً وَجِلَتْ مِنْهَا القُلُوبُ ، وَذَرَفَتْ مِنْهَا العُيُونُ ... وَذَكَرَ الحَدِيثَ وَقَدْ سَبَقَ بِكَمَالِهِ في باب الأمْر بِالمُحَافَظَةِ عَلَى السُّنَّة ، وَذَكَرْنَا أنَّ التَّرْمِذِيَّ ، قَالَ : (( إنّه حديث حسن صحيح )) .
Imepokewa kutoka kwa 'Irbaadh bin Saariyah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: "Alituaidhia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mawaidha yaliyozifanya nyoyo zikaingia hofu na macho yakabubujikwa na machozi. Na akitaja hiyo Hadiyth ambayo imetangulia kutafsiriwa katika mlango wa kuhifadhi Sunnah, [At-Tirmidhiy amesema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب الوقار والسكينة
09-Mlango Wa Heshima na Utulivu
Alhidaaya.com [4]
قَالَ الله تَعَالَى:
وَعِبَادُ الرَّحْمَـٰنِ الَّذِينَ يَمْشُونَ عَلَى الْأَرْضِ هَوْنًا وَإِذَا خَاطَبَهُمُ الْجَاهِلُونَ قَالُوا سَلَامًا ﴿٦٣﴾
Na waja wa Ar-Rahmaan ni wale wanaotembea katika ardhi kwa unyenyekevu na upole, na majahili wanapowasemesha, wao husema: Salaam! [Al-Furqaan: 63]
وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : مَا رَأيْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم مُسْتَجْمِعاً قَطُّ ضَاحِكاً حَتَّى تُرَى مِنهُ لَهَوَاتُهُ ، إنَّمَا كَانَ يَتَبَسَّمُ . متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amesema: "Sijamuona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akicheka sana mpaka nyama ya ndani kabisa katika mdomo ikaonekana. Hakika alikuwa anatabasamu tu." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب الندب إِلَى إتيان الصلاة والعلم ونحوهما من العبادات بالسكينة والوقار
10-Mlango Wa Kupendeza Kuja Katika Swalaah na 'Ibaadah Nyinginezo Kwa Utulivu na Kwa Unyenyekevu
Alhidaaya.com [4]
قَالَ الله تَعَالَى:
وَمَن يُعَظِّمْ شَعَائِرَ اللَّـهِ فَإِنَّهَا مِن تَقْوَى الْقُلُوبِ ﴿٣٢﴾
Na yeyote anayeadhimisha Ishara za Allaah, basi hayo ni katika taqwa ya nyoyo. [Al-Hajj: 32]
Hadiyth – 1
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( إِذَا أُقِيمَتِ الصَّلاَةُ ، فَلاَ تَأتُوهَا وَأنْتُمْ تَسْعَونَ ، وَأتُوهَا وَأنْتُمْ تَمْشُونَ ، وَعَلَيْكُمُ السَّكِينَةُ ، فَمَا أدْرَكْتُم فَصَلُّوا ، وَمَا فَاتكُمْ فَأَتِمُّوا )) متفقٌ عَلَيْهِ .
زاد مسلِمٌ في روايةٍ لَهُ : (( فَإنَّ أحَدَكُمْ إِذَا كَانَ يَعْمِدُ إِلَى الصَّلاَةِ فَهُوَ في صَلاَةٍ )) .
Imepokewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Inapokimiwa Swalaah, msiijie hali nyie mnakimbia, lendeeni mkiwa mnatembea, na juu yenu utulivu. Mlichopata swalini, mlichokosa timizeni." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Muslim amezidisha katika riwaayah yake: "Kwa hakika mmoja wenu anapokusudia kuswali basi yupo katika Swalaah."
Hadiyth – 2
وعن ابن عباس رضي الله عنهما : أنَّهُ دَفَعَ مَعَ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم يَوْمَ عَرَفَةَ فَسَمِعَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم وَرَاءهُ زَجْراً شَديداً وَضَرْباً وَصَوْتاً للإِبْلِ ، فَأشَارَ بِسَوْطِهِ إلَيْهِمْ ، وقال : (( يَا أيُّهَا النَّاسُ ، عَلَيْكُمْ بالسَّكِينَةِ ، فَإنَّ الْبِرَّ لَيْسَ بالإيضَاعِ )) رواه البخاري ، وروى مسلم بعضه .
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) walirudi pamoja na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) siku ya 'Arafah, akasikia nyuma yake zogo kali, pigo na sauti ya ngamia. Akawaashiria kwa mjeledi wake, Akasema: "Enyi watu! Ni juu yenu utulivu, kwani utiifu si kwa kufanya haraka." [Al-Bukhaariy, na Muslim ameipokea baadhi yake].
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب إكرام الضيف
11-Mlango Wa Kumkirimu Mgeni
Alhidaaya.com [4]
قَالَ الله تَعَالَى:
هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ ضَيْفِ إِبْرَاهِيمَ الْمُكْرَمِينَ﴿٢٤﴾ إِذْ دَخَلُوا عَلَيْهِ فَقَالُوا سَلَامًا ۖ قَالَ سَلَامٌ قَوْمٌ مُّنكَرُونَ﴿٢٥﴾ فَرَاغَ إِلَىٰ أَهْلِهِ فَجَاءَ بِعِجْلٍ سَمِينٍ﴿٢٦﴾ فَقَرَّبَهُ إِلَيْهِمْ قَالَ أَلَا تَأْكُلُونَ﴿٢٧﴾
Je, imekufikia hadithi ya wageni wahishimiwao wa Ibraahiym? Walipoingia kwake wakasema: Salaam! Akasema: Salaam watu wasiotambulikana. Akaondoka bila kuhisiwa kuelekea kwa ahli yake akaleta ndama aliyenona. Akawakurubishia; akasema: Mbona hamli? [Adh-Dhaariyaat: 24 - 27]
وَجَاءَهُ قَوْمُهُ يُهْرَعُونَ إِلَيْهِ وَمِن قَبْلُ كَانُوا يَعْمَلُونَ السَّيِّئَاتِ ۚ قَالَ يَا قَوْمِ هَـٰؤُلَاءِ بَنَاتِي هُنَّ أَطْهَرُ لَكُمْ ۖ فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَلَا تُخْزُونِ فِي ضَيْفِي ۖ أَلَيْسَ مِنكُمْ رَجُلٌ رَّشِيدٌ﴿٧٨﴾
Wakamjia kaumu yake wakimkimbilia na kabla ya hapo walikuwa wakitenda maovu. (Luutw) Akasema: Enyi kaumu yangu! Hawa ni mabinti zangu, wao wametwaharika kwenu (kuwaoa kihalali) Basi mcheni Allaah, na wala msinifedheheshe mbele ya wageni wangu. Je, hakuna miongoni mwenu mtu muongofu? [Huwd: 78]
Hadiyth – 1
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاللهِ وَاليَوْمِ الآخِرِ فَلْيُكْرِمْ ضَيْفَهُ ، وَمَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاللهِ وَاليَومِ الآخِرِ ، فَلْيَصِلْ رَحِمَهُ ، وَمَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاللهِ وَاليَومِ الآخِرِ ، فَلْيَقُلْ خَيْراً أَوْ لِيَصْمُتْ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kumuamini Allaah na Siku ya Mwisho amkirimu mgeni wake; na mwenye kumuamini Allaah na Siku ya Mwisho na aunganishe kizazi; na mwenye kumuamini Allaah na Siku ya Mwisho na aseme kheri au anyamaze." [Al-Bukhaariy na Muslim].
Hadiyth – 2
وعن أَبي شُرَيْح خُوَيْلِدِ بن عَمرو الخُزَاعِيِّ رضي الله عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، يقول: (( مَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاللهِ وَاليَوْمِ الآخِرِ فَلْيُكْرِمْ ضَيْفَهُ جَائِزَتَهُ ))
قالوا : وَمَا جَائِزَتُهُ ؟ يَا رسول الله ، قَالَ : (( يَوْمُهُ وَلَيْلَتُهُ ، وَالضِّيَافَةُ ثَلاَثَةُ أيَّامٍ ، فَمَا كَانَ وَرَاءَ ذَلِكَ فَهُوَ صَدَقَةٌ عَلَيْهِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
وفي رواية لِمسلمٍ : (( لاَ يَحِلُّ لِمُسْلِمٍ أنْ يُقِيمَ عِنْدَ أخِيهِ حَتَّى يُؤْثِمَهُ )) قالوا : يَا رسول الله ، وَكيْفَ يُؤْثِمُهُ ؟ قَالَ : (( يُقِيمُ عِنْدَهُ وَلاَ شَيْءَ لَهُ يُقْرِيه بِهِ )) .
Imepokewa kutoka kwa Abuu Shurayh Khuwaylid bin 'Amru Al-Khuzaa'iy (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Mwenye kumwamini Allaah na Siku ya Mwisho na amkirimu mgeni wake Jaa'izatahu." Wakauliza: "Ee Rasuli wa Allaah! Jaa'izatahu ni nini?" Akasema: "Ni siku moja (mchana na usiku wake) na ugeni ni siku tatu. Zaidi ya siku hizo (tatu) ni swadaqah kwake." [Al-Bukhaariy na Muslim].
Katika riwaayah ya Muslim: "Haifai kwa Muislamu kukaa siku nyingi kwa nduguye (mwenyeji wake) mpaka akamtia katika dhambi." Wakasema: "Ee Rasuli wa Allaah! Na vipi atamtia katika dhambi?" Akasema: "Anakaa kwake na ilihali mwenyeji hana cha kumkirimu mgeni wake."
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب استحباب التبشير والتهنئة بالخير
12-Mlango Wa Kupendeza Kutoa Bishara na Kupongeza Kwa Kufikiwa na Kheri
Alhidaaya.com [4]
قَالَ الله تَعَالَى:
فَبَشِّرْ عِبَادِ ﴿١٧﴾ الَّذِينَ يَسْتَمِعُونَ الْقَوْلَ فَيَتَّبِعُونَ أَحْسَنَهُ ۚ ﴿١٨﴾
Basi wabashirie waja Wangu.Wale wanaosikiliza kwa makini kauli, wakafuata yaliyo mazuri yake zaidi. [Az-Zumar: 17-18]
يُبَشِّرُهُمْ رَبُّهُم بِرَحْمَةٍ مِّنْهُ وَرِضْوَانٍ وَجَنَّاتٍ لَّهُمْ فِيهَا نَعِيمٌ مُّقِيمٌ﴿٢١﴾
Rabb wao Anawabashiria kwa rahmah kutoka Kwake na radhi na Jannaat, watapata humo neema zenye kudumu. [At-Tawbah: 21]
وَأَبْشِرُوا بِالْجَنَّةِ الَّتِي كُنتُمْ تُوعَدُونَ﴿٣٠﴾
Na pokeeni bishara njema ya Jannah ambayo mlikuwa mkiahidiwa. [Fusw-swilat: 30]
فَبَشَّرْنَاهُ بِغُلَامٍ حَلِيمٍ ﴿١٠١﴾
Basi Tukambashiria ghulamu mvumilivu. [Asw-Swaffaat: 101]
وَلَقَدْ جَاءَتْ رُسُلُنَا إِبْرَاهِيمَ بِالْبُشْرَىٰ ﴿٦٩﴾
Na kwa yakini walimjia Ibraahiym Wajumbe Wetu kwa bishara. [Huwd: 69]
وَامْرَأَتُهُ قَائِمَةٌ فَضَحِكَتْ فَبَشَّرْنَاهَا بِإِسْحَاقَ وَمِن وَرَاءِ إِسْحَاقَ يَعْقُوبَ﴿٧١﴾
Na mkewe amesimama wima, akacheka; Tukambashiria Is-haaq na baada ya Is-haaq ni Ya’quwb. [Huwd: 71]
فَنَادَتْهُ الْمَلَائِكَةُ وَهُوَ قَائِمٌ يُصَلِّي فِي الْمِحْرَابِ أَنَّ اللَّـهَ يُبَشِّرُكَ بِيَحْيَىٰ ﴿٣٩﴾
Basi mara Malaika akamwita (Zakariyyaa) naye akiwa amesimama anaswali katika chumba kwamba: Hakika Allaah Anakubashiria Yahyaa. [Aal-'Imraan: 39]
إِذْ قَالَتِ الْمَلَائِكَةُ يَا مَرْيَمُ إِنَّ اللَّـهَ يُبَشِّرُكِ بِكَلِمَةٍ مِّنْهُ اسْمُهُ الْمَسِيحُ ﴿٤٥﴾
Na pale Malaika waliposema: Ee Maryam! Hakika Allaah Anakubashiria Neno (la Kun!) kutoka Kwake (umzae mtoto), jina lake ni Al-Masiyhu. [Aal-'Imraan: 45]
Hadiyth – 1
عن أَبي إبراهيم ، ويقال : أَبُو محمد ، ويقال : أَبُو معاوية عبد اللهِ بن أَبي أوفى رضي الله عنهما : أنّ رسول الله صلى الله عليه وسلم بَشَّرَ خَدِيجَةَ رضي اللهُ عنها ببَيْتٍ في الجَنَّةِ مِنْ قَصَبٍ ، لاَ صَخَبَ فِيهِ ، وَلاَ نَصَبَ . متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Ibraahiym na panasemwa Abu Muhammad, na panasemwa Abu Mu'awiyah 'Abdillaah bin Abu Awf (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimbashiria Khadiyjah (Radhwiyah Allaahu 'anhaa) kuwa atapat nyumba Peponi iliyotengenezwa na lulu, ambako hakutakuwa na makelele wala taabu." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 2
وعن أَبي موسى الأشعري رضي الله عنه : أَنَّهُ تَوَضَّأ في بَيْتِهِ ، ثُمَّ خَرَجَ ، فَقَالَ : لأَلْزَمَنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، وَلأَكُونَنَّ مَعَهُ يَوْمِي هَذَا ، فَجَاءَ الْمَسْجِدَ ، فَسَألَ عَنِ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم، فَقَالُوا وجَّهَ هاهُنَا، قَالَ : فَخَرَجْتُ عَلَى أثَرِهِ أسْألُ عَنْهُ ، حَتَّى دَخَلَ بِئْرَ أريسٍ، فَجَلَسْتُ عِندَ البَابِ حتَّى قضى رسول الله صلى الله عليه وسلم حاجتهُ وتوضأ ، فقمتُ إليهِ ، فإذا هو قد جلسَ على بئرِ أريسٍ وتوَسَّطَ قُفَّهَا ، وكشَفَ عنْ ساقيهِ ودلاّهُما في البئرِ ، فسلمتُ عَليهِ ثمَّ انصَرَفتُ ، فجلستُ عِندَ البابِ ، فَقُلْتُ : لأَكُونَنَّ بَوَّابَ رسولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم الْيَوْمَ ، فَجَاءَ أَبُو بَكْرٍ رضي الله عنه فَدَفَعَ الْبَابَ ، فقلتُ : مَنْ هَذَا ؟ فَقَالَ : أَبُو بَكْرٍ ، فقُلتُ : عَلَى رِسْلِكَ ، ثُمَّ ذَهبْتُ ، فقلتُ : يَا رسول الله ، هَذَا أَبُو بَكْرٍ يَستَأْذِنُ ، فَقَالَ : (( ائْذَنْ لَهُ وَبَشِّرْهُ بِالْجَنَّةِ )) فَأقْبَلْتُ حَتَّى قُلْتُ لأَبي بَكْرٍ : ادْخُلْ وَرسول الله صلى الله عليه وسلم يُبَشِّرُكَ بِالجَنَّةِ ، فَدَخَلَ أَبُو بَكرٍ حَتَّى جَلَسَ عَنْ يَمينِ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم مَعَهُ في القُفِّ ، وَدَلَّى رِجْلَيْهِ في البِئْرِ كَمَا صَنَعَ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، وَكَشَفَ عَنْ سَاقَيْهِ ، ثُمَّ رَجَعْتُ وَجَلَسْتُ ، وَقَدْ تَرَكْتُ أخِي يَتَوَضَّأ وَيَلْحَقُنِي ، فقلتُ : إنْ يُرِدِ الله بِفُلانٍ – يُريدُ أخَاهُ – خَيْراً يَأتِ بِهِ . فَإذَا إنْسَانٌ يُحَرِّكُ الْبَاب ، فقلتُ : مَنْ هَذَا ؟ فَقَالَ : عُمَرُ بن الخَطّابِ ، فقلتُ : عَلَى رِسْلِكَ ، ثُمَّ جِئْتُ إِلَى رسول الله صلى الله عليه وسلم ، فَسَلَّمْتُ عَلَيْهِ وَقُلْتُ : هَذَا عُمَرُ يَسْتَأذِنُ ؟ فَقَالَ : (( ائْذَنْ لَهُ وَبَشِّرْهُ بالجَنَّةِ )) فَجِئْتُ عُمَرَ ، فقلتُ : أَذِنَ وَيُبَشِّرُكَ رسول الله صلى الله عليه وسلم بِالجَنَّةِ ، فَدَخَلَ فَجَلَسَ مَعَ رسول الله صلى الله عليه وسلم في القُفِّ عَنْ يَسَارِهِ وَدَلَّى رِجْلَيْهِ في البِئرِ ، ثُمَّ رَجَعْتُ فَجَلَسْتُ ، فَقُلتُ : إنْ يُرِدِ اللهُ بِفُلاَنٍ خَيْراً – يَعْنِي أخَاهُ – يَأْتِ بِهِ ، فَجَاءَ إنْسَانٌ فَحَرَّكَ الْبَابَ . فَقُلتُ : مَنْ هَذَا ؟ فَقَالَ : عُثْمَانُ بن عَفَّانَ . فقلتُ : عَلَى رِسْلِكَ ، وجِئْتُ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم فأخْبَرْتُهُ ، فقالَ : (( ائْذَنْ لَهُ وَبَشِّرْهُ بِالجَنَّةِ مَعَ بَلْوَى تُصِيبُهُ )) فَجِئْتُ ، فقلتُ : ادْخُلْ وَيُبَشِّرُكَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم بِالجَنَّةِ مَعَ بَلْوَى تُصيبُكَ ، فَدَخَلَ فَوجَدَ الْقُفَّ قَدْ مُلِئَ ، فجلس وِجَاهَهُمْ مِنَ الشِّقِّ الآخرِ . قَالَ سَعيدُ بْنُ الْمُسَيَّبِ : فَأوَّلْتُهَا قُبُورَهُمْ . متفقٌ عَلَيْهِ .
وزاد في رواية : وأمرني رسولُ الله صلى الله عليه وسلم بحفظِ الباب . وَفيها : أنَّ عُثْمانَ حِيْنَ بَشَّرَهُ حَمِدَ اللهَ تَعَالَى ، ثُمَّ قَالَ : اللهُ المُسْتَعانُ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Muwsaa Al-'Ash'ariy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa yeye alitawadha nyumbani kwake kisha akatoka huku akisema: Leo nitajilazimisha kuwa pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Hivyo Alifika Msikitini na kumuulizia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) naye akaambiwa kuwa amepita njia fulani. Akasema: Nilifuata nyayo zake na huku naulizia kwa watu mpaka nikafika sehemu inayoitwa Bi'r Ariys. Nikasimama kwenye mlango mpaka Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamaliza haja yake (haja ndogo) na akatawadha, nilienda kwake na kumuona kuwa amekaa kwenye ukingo wa kisima cha Ariys. Alikuwa amekunja kikoi chake na miguu yake inaeleaelea kisimani. Nikamsalimia kisha nikaondoka na kusimama mlangoni. Nikasema: "Nitakuwa ni mlinzi wa mlango kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) leo." Akaja Abu Bakr (Radhwiya Allaahu 'anhu) na kusukuma mlango, nami nikamuuliza: "Ni nani huyo?" Alijibu: "Ni mimi Abu Bakr." Nikamwambia: "Ngoja kidogo." Kisha nilikwenda na kusema: "Ee Rasuli wa Allaah! Abu Bakr amekuja na anomba ruhusa kuingia." Akasema: "Mpe ruhusa na umbashirie Pepo." Nilirudi mlangoni na kumfungulia Abu Bakr na kumpa bishara ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa ataingia Peponi. Aliingia Abu Bakr (Radhwiya Allaahu 'anhu)na kukaa upande wa kulia wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) juu ya ukingo ule wa kisima na akanyoosha miguu yake kisimani kama alivyofanya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na akainyanyua nguo yake mpaka miundi ikawa inaonekana. Kisha nilirudi na kukaa mlangoni, kwani nilikuwa na ndugu yangu niliyemwacha nyumbani akitawadha na alikuwa aje kwangu. Nikasema: "Ikiwa allaah anamtakia kheri fulani - akikusudia ndugu yake, basi atamleta hivi sasa." Mara kukawa na mtu aliyekuwa akiusukuma mlango, nami nikauliza: "Ni nani huyo?" Naye akajibu: "Ni mimi 'Umar bin Al-Khattwaab." Nikamwambia: "Ngoja kidogo." Nilikwend na kumsalimia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kusema: "Ee Rasuli wa Allaah! 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) amekuja na anaomba ruhusa kuingia." Akasema: "Mpe ruhusa na umbashirie Pepo." Nilirudi mlangoni na kumfungulia 'Uamar (Radhwiya Allaahu 'anhu) na kumpa bishara ya Rasuli wa Allaah (Swaalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa ataingia Peponi. Aliingia na kukaa upande wa kushoto wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) juu ya ukingo ule wa kisima. Kisha nilirudi na kukaa mlangoni, nikasema: "Ikiwa Allaah anamtakia kheri fulani - akikusudia ndugu yake, basi atamleta hivi sasa." Mara kukawa na mtu aliyekuwa akiusukuma mlango, nami nikauliza: "Ni nani huyo?" Naye akajibu: "Ni mimi 'Uthmaan bin 'Affaan." Nikamwambia: "Ngoja kidogo." Nilikwenda na kumpasha habari Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) naye akasema: "Mpe ruhusa na umbashirie Pepo pamoja na balaa itakayomfika." Nilirudi mlangoni na kumwambia: "Ingia na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anakupa bishara ya kuingia Peponi pamoja na balaa itakayokufika." Aliingia na kukuta kuwa ule ukingo umejaa, hivyo alikaa ule upande mwengine akielekeana nao. Amesema Sa'iyd bin Al-Musayyab: "Huu mpangilio waliokaa hawa watu wa mwanzo yatakuwa karibu." [Al-Bukhaariy na Muslim].
Na imezidishwa katika riwaayah: "Na akaniamuru Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kutunza mlango. Na hapo pia: Hakika pindi 'Uthmaan alipobashiriwa, alimuhimidi Allaah Ta'aalaa, kisha akasema: Allaah ndiye msaidizi."
Hadiyth – 3
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : كُنَّا قُعُوداً حَوْلَ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم ، وَمَعَنَا أَبُو بَكرٍ وَعُمَرُ رضي الله عنهما في نَفَرٍ ، فَقَامَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم مِنْ بَيْنِ أظْهُرِنَا فَأبْطَأ عَلَيْنَا ، وَخَشِينَا أنْ يُقْتَطَعَ دُونَنَا وَفَزِعْنَا فَقُمْنَا ، فَكُنْتُ أَوَّلَ مَنْ فَزِعَ ، فَخَرَجْتُ أبْتَغِي رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ، حَتَّى أتَيْتُ حَائِطاً للأنصَارِ لِبَني النَّجَارِ ، فَدُرْتُ بِهِ هَلْ أجِدُ لَهُ بَاباً ؟ فَلَمْ أجِدْ ! فَإذَا رَبيعٌ يَدْخُلُ في جَوْفِ حَائِطٍ مِنْ بِئْرٍ خَارِجَهُ – وَالرَّبِيعُ : الجَدْوَلُ الصَّغِيرُ – فَاحْتَفَرْتُ ، فَدَخَلْتُ عَلَى رسول الله صلى الله عليه وسلم، فَقَالَ: (( أَبُو هُرَيْرَةَ ؟ )) فقلتُ : نَعَمْ ، يَا رسول اللهِ ، قَالَ : (( مَا شأنُكَ ؟ )) قُلْتُ : كُنْتَ بَيْنَ أظْهُرِنَا فَقُمْتَ فَأبْطَأتَ عَلَيْنَا ، فَخَشِينَا أنْ تُقْتَطَعَ دُونَنَا ، ففزعنا ، فَكُنْتُ أوّلَ مَنْ فَزِعَ ، فَأتَيْتُ هَذَا الحَائِطَ ، فَاحْتَفَرْتُ كَمَا يَحْتَفِرُ الثَّعْلَبُ ، وهؤلاء النَّاسُ وَرَائِي . فَقَالَ : (( يَا أَبَا هُرَيرَةَ )) وَأعْطَانِي نَعْلَيْهِ ، فَقَالَ : (( اذْهَبْ بِنَعْلَيَّ هَاتَيْنِ ، فَمَنْ لَقِيتَ مِنْ وَرَاءِ هَذَا الحَائِطِ يَشْهَدُ أنْ لا إله إِلاَّ الله مُسْتَيْقِنَاً بِهَا قَلْبُهُ ، فَبَشِّرْهُ بِالجَنَّةِ ... )) وَذَكَرَ الحديثَ بطوله ، رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Tulikuwa tumekaa huku tumemzunguka Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na pamoja nasi yupo Abu Bakr na 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa). Akasimama Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) baina yetu na kutoka nje. Akakawia sana bila ya kurudi, hivyo tukawa na wasiwasi mkubwa kuhusu usalam wake. Nilikuwa wa kwanza kuhisi hivyo, nami nikatoka kumfuata Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mpaka nikafika katika ukuta wa Answaar kutoka kwa ukoo wa An-Najjar. Nilizunguka ukuta huo kutafuta mlango lakini bila mafanikio. mara nikaona kijimto kilichokuwa kikileta maji kutoka katika kisima nje ya bustani kikipitia katika ukuta. Nikajikunja mpaka nikaweza kupita kwenye kishimo na kumfikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), ambaye aliponiona alimaka kwa kusema: "Ee Abu Hurayrah!" Nikasema: "Naam (ndio)! Ee Rasuli wa Allaah." Akasema: "Una nini (ni kitu gani kilichokuleta hapa)?" Nikasema: "Ulikuwa pamoja nasi, na kwa ghafla ukaondoka na ukakawia kurudi, hivyo tukawa na wasiwasi kuwa huenda umefikwa na jambo bila ya sisi kuwepo. Mimi nilikuwa wa kwanza kubabaika, hivyo nikaja kwenye ukuta wa bustani hili na nikajikunja kama anavyojikunja mbwa mwitu ili niweze kupita katika shimo. Wengine wapo nyuma yangu." Akasema: "Ee Abu Hurayrah!" na akanipa viatu vyake na kuniambia: "Nenda na viatu vyangu hivi na yeyote utakayekutana naye nyuma ya ukuta huu anashuhudia ya kwamba hapana anayepaswa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah akiwa na yakini katika moyo wake, mpe bishara njema kuwa ataingia Peponi." Baada ya hayo Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) aliieleza Hadiyth hii kwa urefu wake." [Muslim]
Hadiyth – 4
وعن ابن شِمَاسَة ، قَالَ : حَضَرْنَا عَمْرَو بنَ العَاصِ رضي الله عنه وَهُوَ في سِيَاقَةِ الْمَوْتِ ، فَبَكَى طَوِيلاً ، وَحَوَّلَ وَجْهَهُ إِلَى الجِدَارِ ، فَجَعَلَ ابْنُهُ ، يَقُولُ : يَا أبَتَاهُ ، أمَا بَشَّرَكَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم بكَذَا ؟ أمَا بَشَّرَكَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم بِكَذَا ؟ فَأقْبَلَ بِوَجْهِهِ ، فَقَالَ : إنَّ أفْضَلَ مَا نُعِدُّ شَهَادَةُ أنْ لا إلهَ إِلاَّ الله ، وَأنَّ مُحَمَّداً رسول اللهِ ، إنِّي قَدْ كُنْتُ عَلَى أطْبَاقٍ ثَلاَثٍ : لَقَدْ رَأيْتُنِي وَمَا أحَدٌ أشَدُّ بُغضاً لرسولِ الله صلى الله عليه وسلم مِنِّي ، وَلاَ أحَبَّ إليَّ مِنْ أنْ أكُونَ قدِ اسْتَمكنتُ مِنْهُ فَقَتَلْتُه ، فَلَوْ مُتُّ عَلَى تلكَ الحَالِ لَكُنْتُ مِنْ أهْلِ النَّارِ ، فَلَمَّا جَعَلَ اللهُ الإسلامَ في قَلْبِي أتَيْتُ النبيَّ صلى الله عليه وسلم ، فقُلْتُ : ابسُطْ يَمِينَكَ فَلأُبَايِعُك ، فَبَسَطَ يَمِينَهُ فَقَبَضْتُ يَدِي ، فَقَالَ : (( مَا لَكَ يَا عَمْرُو ؟ )) قلتُ: أردتُ أنْ أشْتَرِطَ ، قَالَ : (( تَشْتَرِط مَاذا ؟ )) قُلْتُ : أنْ يُغْفَرَ لِي ، قَالَ : (( أمَا عَلِمْتَ أن الإسلامَ يَهْدِمُ مَا كَانَ قَبْلَهُ ، وَأن الهِجْرَةَ تَهْدِمُ مَا كَانَ قَبلَهَا ، وَأنَّ الحَجَّ يَهْدِمُ مَا كَانَ قَبْلَهُ ؟ )) وَمَا كَانَ أحدٌ أحَبَّ إليَّ مِنْ رَسُولِ الله صلى الله عليه وسلم ، وَلاَ أجَلَّ في عَيني مِنْهُ وَمَا كُنْتُ أُطيقُ أن أملأ عَيني مِنْهُ ؛ إجلالاً لَهُ ، ولو سئلت أن أصفه مَا أطقت ، لأني لَمْ أكن أملأ عيني مِنْهُ ، ولو مُتُّ عَلَى تِلْكَ الحالِ لَرجَوْتُ أن أكُونَ مِنْ أهْلِ الجَنَّةِ ، ثُمَّ وَلِينَا أشْيَاءَ مَا أدْرِي مَا حَالِي فِيهَا ؟ فَإذَا أنَا مُتُّ فَلاَ تَصحَبَنِّي نَائِحَةٌ وَلاَ نَارٌ ، فَإذا دَفَنْتُمُونِي ، فَشُنُّوا عَليَّ التُّرابَ شَنّاً ، ثُمَّ أقِيمُوا حَوْلَ قَبْرِي قَدْرَ مَا تُنْحَرُ جَزورٌ ، وَيُقْسَمُ لَحْمُهَا ، حَتَّى أَسْتَأنِسَ بِكُمْ ، وَأنْظُرَ مَا أُرَاجعُ بِهِ رسُلَ رَبّي . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Ibn Shumaasah kuwa amesema: Tulimzuru 'Amruw bin Al-'Aaas (Radhwiya Allaahu 'anhu) akiwa katika uchungu wa kifo. Alilia sana na kwa muda mrefu mpaka akageuza uso wake ukutani. Kuona hivyo, mtoto wake akawa anamliwaza kwa kumwambia: "Ee baba yangu! Si rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikubashiria kadhaa na kadhaa? Si Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) alikubashiria kadhaa na kadhaa?" 'Amru (Radhwiya 'anhu) alituangalia na kusema: "Hakika matayarisho bora (kujiandaa kwa Aakhera) ni kuikariri shahada ya kwamba hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Rasuli wa Allaah. Hakika mimi nimepitiwa na wakati ambao hakuwa yeyote mwenye chuki zaidi kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuniliko na hakukuwa na kitu nilichokuwa nikipenda kama kumkamata na kumuua (yaani kumuua Nabiy). Lau ningekufa katika hali hiyo ningekuwa mtu wa motoni. Allaah Alipoujaalia Uislaamu katika moyo wangu nilikuja kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kumwambia: 'Tafadhali nyoosha mkono wako wa kulia ili nikubai'. Alinyoosha mkono wake wa kulia lakini nilirudisha mkono wangu. Akasema: 'Una nini ee 'Amruw?' Nikasema: 'Napenda kuweka sharti.' Akasema: 'Unaweka sharti gani?' Nikasema: 'Nisamehewe madhambi yangu yote.' Akasema: 'Je, hujajua ya kwamba Uislaamu unafuta madhambi yote yaliyofanywa kabla yake (yaani ya kusilimu); na Hijrah (kuhama/kugura kwa ajili ya Allaah) inafuta yote yaliokuwa kabla yake; na pia Hijjah inafuta yaliyokuwa kabla yake.' Baada ya hapo hakukuwa na yeyote niliyekuwa nikimpenda kuliko Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na wala hakukuwa na aliyekuwa mtukufu machoni pangu kuliko yeye. Na kwa ajili ya utukufu wake kwangu, sikuweza kumtizama uso wake mzima kwa makini na lau nitaulizwa nimsifu (au nimueleze) sitoweza kufanya hivyokwa kuwa sikuwahi kumwangalia kwa kitambo. Lau ningekufakatika hali hiyo basi nilikuwa na matumaini makubwa kuwa nitakuwa miongoni mwa watu wa Peponi. Kisha baada ya hapo tumetawalishwa mambo mengi na sijui hali yangu ndani yake? Hivyo, ninapofariki asifuate jeneza langu muombolezi wala moto. Mnaponizika tupeni mchanga kidogo kidogo, kisha kaeni pembezoni mwa kaburi langu kwa muda unaotosha kuchinja ngamia na kugawa nyama yake, ili nipate kujituliza kwa sababu ya kuwepo kwenu na kuanza kutafakari majibu kwa wajumbe wa Rabb wangu (yaani Malaaika)." [Muslim].
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب وداع الصاحب ووصيته عند فراقه للسفر وغيره والدعاء لَهُ وطلب الدعاء مِنْهُ
13-Mlango Wa Kumuaga Rafiki na Kumuusia Mnapotengana Kwa Ajili ya Safari na Kumuombea na Kutaka Akuombee Duaa
Alhidaaya.com [4]
قَالَ الله تَعَالَى:
وَوَصَّىٰ بِهَا إِبْرَاهِيمُ بَنِيهِ وَيَعْقُوبُ يَا بَنِيَّ إِنَّ اللَّـهَ اصْطَفَىٰ لَكُمُ الدِّينَ فَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنتُم مُّسْلِمُونَ ﴿١٣٢﴾
Na Ibraahiym akawausia hayo wanawe na (kadhalika) Ya’quwb (akawaambia): Enyi wanangu! Hakika Allaah Amekukhitarini nyinyi Dini; basi msife isipokuwa nyinyi ni Waislamu.
أَمْ كُنتُمْ شُهَدَاءَ إِذْ حَضَرَ يَعْقُوبَ الْمَوْتُ إِذْ قَالَ لِبَنِيهِ مَا تَعْبُدُونَ مِن بَعْدِي قَالُوا نَعْبُدُ إِلَـٰهَكَ وَإِلَـٰهَ آبَائِكَ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ إِلَـٰهًا وَاحِدًا وَنَحْنُ لَهُ مُسْلِمُونَ ﴿١٣٣﴾
Je, mlikuwa mashahidi wakati mauti yalipomfikia Ya’quwb alipowaambia wanawe: Mtaabudu nini baada yangu? Wakasema: Tutamwabudu Ilaaha wako (Allaah) na Ilaaha wa baba zako, Ibraahiym na Ismaa’iyl na Is-haaq; Ilaah Mmoja, nasi ni Waislamu (tunajisalimisha) Kwake. [Al-Baqarah: 132-133]
Hadiyth – 1
حديث زيد بن أرقم رضي الله عنه – الَّذِي سبق في بَابِ إكرام أهْلِ بَيْتِ رسول الله صلى الله عليه وسلم - قَالَ : قَامَ رسول الله صلى الله عليه وسلم فِينَا خَطِيباً ، فَحَمِدَ الله ، وَأثْنَى عَلَيْهِ ، وَوَعَظَ وَذَكَّرَ ، ثُمَّ قَالَ : (( أمَّا بَعْدُ ، ألاَ أيُّهَا النَّاسُ ، إنَّمَا أنَا بَشَرٌ يُوشِكُ أنْ يَأتِيَ رَسُولُ رَبِّي فَأُجِيبَ ، وَأنَا تَارِكٌ فِيكُمْ ثَقَلَيْنِ ، أوَّلَهُمَا : كِتَابُ اللهِ ، فِيهِ الْهُدَى وَالنُّورُ ، فَخُذُوا بِكِتَابِ اللهِ وَاسْتَمْسِكُوا بِهِ )) ، فَحَثَّ عَلَى كِتَابِ اللهِ ، وَرَغَّبَ فِيهِ ، ثُمَّ قَالَ : (( وَأَهْلُ بَيْتِي ، أذَكِّرُكُمُ اللهَ في أهْلِ بَيْتِي )) رواه مسلم ، وَقَدْ سَبَقَ بِطُولِهِ .
Na miongoni mwa Hadiyth ni ile ya Zayd bin Arqam ambayo tumeitaja katika mlango wa kuwakirimu Watu wa Nyumbani wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Naye amesema: "Alisimama Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mbele yetu siku moja kutuhutubia.' Kisha akasema: 'Ama baada:... Sikilizeni enyi watu! Hakika mimi ni mwanadamu, huenda akaja mjumbe kutoka kwa Rabb wangu nami nikamuitikia. Hivyo nimewaachia nyinyi vitu viwili vikubwa na muhimu, cha kwanza ni Kitabu cha Allaah ambacho ndani yake kuna uwongofu na nuru. Shikamaeni vilivyo na Kitabu cha Allaah. Akahimiza sana nukta hii na kututaka tukifuate. Kisha akasema: "Na familia yangu. Ninawakumbusha kwa jina la Allaah kuhusu familia yangu." [Muslim]
Hadiyth – 2
وعن أَبي سليمان مالِك بن الحُوَيْرِثِ رضي الله عنه، قَالَ : أَتَيْنَا رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ، وَنَحْنُ شَبَبَةٌ مُتَقَارِبُونَ، فَأقَمْنَا عِنْدَهُ عِشْرِينَ لَيْلَةً، وَكَانَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم رَحِيماً رَفيقاً ، فَظَنَّ أنّا قد اشْتَقْنَا أهْلَنَا ، فَسَألَنَا عَمَّنْ تَرَكْنَا مِنْ أهْلِنَا ، فَأخْبَرْنَاهُ ، فَقَالَ : (( ارْجِعُوا إِلَى أهْلِيكُمْ ، فَأقِيمُوا فِيهمْ ، وَعَلِّمُوهُم وَمُرُوهُمْ ، وَصَلُّوا صَلاَةَ كَذَا فِي حِيْنِ كَذَا ، وَصَلُّوا كَذَا في حِيْنِ كَذَا ، فَإذَا حَضَرَتِ الصَّلاَةُ فَلْيُؤَذِّنْ لَكُمْ أحَدُكُمْ وَلْيَؤُمَّكُمْ أكْبَرُكُمْ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
زاد البخاري في رواية لَهُ : (( وَصَلُّوا كَمَا رَأيْتُمُونِي أُصَلِّي ))
Imepokewa kutoka kwa Abu Sulaymaan Maalik bin Al-Huwayrith (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Tulikuja kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) tukiwa vijana na rika moja. Tulikaa kwake siku ishirini (20) na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa mpole mwenye huruma. Alidhania ya kwamba sisi tunahamu na familia zetu, hivyo alituuliza kuhusu wale tuliowaacha nyuma katika watu wa familia zetu, nasi tukampasha habari kuhusu hilo. akasema: "Rejeeni kwa familia zenu na muwe pamoja nao, na wafundisheni na muwaamrishe na Swalini Swalaah kadhaa wakati kadhaa, na Swalini Swalaah wakati kadhaa. Swalaah inapofika awaadhinie mmoja wenu na awaongoze mkubwa wenu katika Swalaah." [Al-Bukhaariy na Muslim].
Al-Bukhaariy amezidisha katika riwaayah yake: "Na swalini kama mulivyoniona mimi nikiswali."
Hadiyth – 3
وعن عمرَ بن الخطاب رضي الله عنه ، قَالَ : اسْتأذَنْتُ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم في العُمْرَةِ ، فَأذِنَ ، وقال : (( لاَ تَنْسَانَا يَا أُخَيَّ مِنْ دُعَائِكَ )) فقالَ كَلِمَةً ما يَسُرُّنِي أنَّ لِي بِهَا الدُّنْيَا .
وفي رواية قَالَ : (( أشْرِكْنَا يَا أُخَيَّ في دُعَائِكَ )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Na imepokewa kutoka kwa 'Umar bin Al-Khattaab (Radhwiya Allaah 'anhu) ambaye alisema: "Nilimuomba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ruhusa ya kwenda kufanya Umrah, naye alinipatia idhini. Na akasema: 'Ee ndugu yangu! Usitusahau katika dua zako.' Akasema (Radhwiya Allaahu 'anhu): 'Hili ni neno ambalo sitataka kubadilishana hata na dunia yote."
Na katika riwaayah nyengine, alisema (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Ee ndugu yangu! Tushirikishe katika dua yako." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, ambaye amesema kuwa hii ni Hadiyth Hasan Swahiyh]
Hadiyth – 4
وعن سالم بنِ عبدِ الله بنِ عمر : أنَّ عبدَ اللهِ بن عُمَرَ رضي الله عنهما، كَانَ يَقُولُ للرَّجُلِ إِذَا أرَادَ سَفَراً: ادْنُ مِنِّي حَتَّى أُوَدِّعَكَ كَمَا كَانَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم يُوَدِّعُنَا ، فَيَقُولُ : (( أَسْتَوْدِعُ اللهَ دِينَكَ ، وَأمَانَتَكَ ، وَخَواتِيمَ عَمَلِكَ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Imepokewa kutoka kwa Saalimbin 'Abdillaah kwamba alikuwa 'Abdillaah bin 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) akimwambia mtu mwenye nia ya kusafiri: "Njoo karibu ili nikuage kama alivyokuwa akituaga Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa kusema: Astawdi'u Allaah Diynaka wa Amanataka wa Khawaatiyma 'Amalika: Ninakuweka katika dhima ya Allaah kwa Dini yako, na amana yako na hatima ya amali zako." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh].
Hadiyth – 5
وعن عبدِ الله بن يزيدَ الخطْمِيِّ الصحابيِّ رضي الله عنه ، قَالَ : كَانَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم إِذَا أرَادَ أنْ يُوَدِّعَ الجَيشَ ، قَالَ : (( أسْتَوْدِعُ اللهَ دِينَكُمْ ، وَأمَانَتَكُمْ ، وَخَواتِيمَ أعْمَالِكُمْ )) حديث صحيح ، رواه أَبُو داود وغيره بإسناد صحيح .
Amesema 'Abdillaah bin Yaziyd Al-Khatmiy (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye ni Swahaaba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipotaka kuiaga jeshi alikuwa akiwaambia: "Ninawaageni na kuwaweka katika dhamana ya Allaah katika Dini yenu, amana zenu na mwisho wa amali zenu." [Hadiyth Swahiyh, Abu Daawuwd na wengineo kwa Isnaad Swahiyh].
Hadiyth – 6
وعن أنسٍ رضي الله عنه ، قَالَ : جَاءَ رَجُلٌ إِلَى النبي صلى الله عليه وسلم ، فَقَالَ : يَا رسولَ الله ، إنّي أُرِيدُ سَفَراً ، فَزَوِّدْنِي ، فَقَالَ : (( زَوَّدَكَ الله التَّقْوَى )) قَالَ : زِدْنِي قَالَ : (( وَغَفَرَ ذَنْبَكَ )) قَالَ : زِدْنِي ، قَالَ : (( وَيَسَّرَ لَكَ الْخَيْرَ حَيْثُمَا كُنْتَ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Na amesema Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba alikuja mtu kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kumwambia: "Ee Rasuli wa Allaah! Mimi ninataka kusafiri, hivyo naomba unipatie cha kunisaidia (yaani uniombee)." Akasema: "Allaah akuzidishie uchaji Mungu (Taqwaa)." Akasema yule mtu: "Nizidishie." Akasema: "Na akusamehe dhambi zako." Akasema (tena): "Nizidishie." Akasema: "Na akusahilishie kufanya kheri na mema popote ulipo." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب الاستِخارة والمشاورة
14-Mlango Wa Kutaka Msaada wa Allaah na Ushauri
Alhidaaya.com [4]
قَالَ الله تَعَالَى:
وَشَاوِرْهُمْ فِي الْأَمْرِ ۖ ﴿١٥٩﴾
Na washauri katika mambo. [Aal-'Imraan: 159]
وَأَمْرُهُمْ شُورَىٰ بَيْنَهُمْ ﴿٣٨﴾
Na jambo lao hushauriana baina yao. [Ash-Shuwraa: 38]
Hadiyth – 1
وعن جابر رضي الله عنه ، قَالَ : كَانَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم يُعَلِّمُنَا الاسْتِخَارَةَ في الأمُورِ كُلِّهَا كَالسُّورَةِ مِنَ القُرْآنِ ، يَقُولُ : (( إِذَا هَمَّ أحَدُكُمْ بِالأمْرِ ، فَلْيَركعْ ركْعَتَيْنِ مِنْ غَيْرِ الفَرِيضَةِ ، ثُمَّ ليقل : اللَّهُمَّ إنِّي أسْتَخِيرُكَ بِعِلْمِكَ ، وَأسْتَقْدِرُكَ بِقُدْرَتِكَ ، وأسْألُكَ مِنْ فَضْلِكَ العَظِيْمِ ، فَإنَّكَ تَقْدِرُ وَلاَ أقْدِرُ ، وَتَعْلَمُ وَلاَ أعْلَمُ ، وَأنْتَ عَلاَّمُ الْغُيُوبِ . اللَّهُمَّ إنْ كُنْتَ تَعْلَمُ أنَّ هَذَا الأمْرَ خَيْرٌ لِي في دِينِي وَمَعَاشِي وَعَاقِبَةِ أمْرِي )) أَوْ قَالَ : (( عَاجِلِ أمْرِي وَآجِلِهِ ، فاقْدُرْهُ لي وَيَسِّرْهُ لِي ، ثُمَّ بَارِكْ لِي فِيهِ . وَإنْ كُنْتَ تَعْلَمُ أنَّ هَذَا الأَمْرَ شَرٌّ لِي في دِينِي وَمَعَاشِي وَعَاقِبَةِ أَمْرِي )) أَوْ قَالَ : (( عَاجِلِ أمْرِي وَآجِلِهِ ؛ فَاصْرِفْهُ عَنِّي ، وَاصْرِفْنِي عَنْهُ ، وَاقْدُرْ لِيَ الخَيْرَ حَيْثُ كَانَ ، ثُمَّ أرْضِنِي بِهِ )) قَالَ : (( وَيُسَمِّيْ حَاجَتَهُ )) رواه البخاري .
Imepokewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Alikuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akifundisha Istikhaarah (kutaka shauri kwa Allaah) katika mambo yote kama alivyokuwa akitufundisha Suwrah katika Qur-aan, akisema: "Anapotaka kufanya jambo mmoja wenu na aswali rakaa mbili zisizo za faradhi kisha asema: 'Allaahumma inniy Astakhiyruka Bi'ilmika wa Astaqdiruka Biqudratika wa As'aluka min Fadhwlikal 'Adhiym. Fainnaka Taqdiru walaa Aqdiru wa Ta'alamu walaa A'lamu wa Anta 'Allaamul Ghuyuub. Allaahumma in Kunta Ta'lamu anna hadhaal amru khayrul liy fiy Diyniy wa Ma'aashiy wa 'Aqibati Amriy (au alisema 'Aaajili amriy wa Aajilihi) Faqdurhu liy wa Yassirli Thumma Baarik liy Fiyhi. Wa in Kunta Ta'lamu anna Hadhaal amra Sharrul liy fiy Diyniy wa Ma'aashiy wa 'Aaqibati Amriy (au alisema 'Aajili amriy wa Aajilihi) Faswrifuhu wa swrifni 'anhu waqadur liyal Khayyra haythu kaana Thumma Radhdhiniy Bihi' (yaani Ee Allaah! Nakuomba uongozi kutokana na Ilimu Yako. Na nakuomba uniwezeshe kwa uwezo Wako. Na nakuomba katika Fadhila Zako kubwa, kwani Wewe una uwezo nami sina uwezo, Nawe unajua lakini mimi sijui, Nawe ni Mjuzi wa ghayb. Ee Allaah! Kama jambo hili (hapa unataja jambo lenyewe), Unalilijua, ni kheri kwangu katika Dini yangu na maisha yangu na marejeo yangu (au alisema katika Dunia yangu na Aakhera yangu). Basi niamuliye nilifanye na Nisahilishie kisha unibarikie kwa hilo. Na kama Unavyofahamu likiwa jambo hili (utalitaja tena jambo lenyewe) ni shari kwangu katika Dini yangu na maisha yangu na marejeo yangu (au alisema katika Dunia yangu na Aakhera yangu), basi liepushe nami, na uniepushe nalo, na Uniamulie lenye kheri popote litakapokuwa kisha Uniridhishe nalo." Amesema: "Kisha hutaja haja yake." [Al-Bukhaariy].
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب استحباب الذهاب إِلَى العيد وعيادة المريض والحج والغزو والجنازة ونحوها من طريق ، والرجوع من طريق آخر لتكثير مواضع العبادة
15-Mlango Wa Kupendeza Kwenda Kwenye Swalaah ya Iyd na Kuwazuru Wagonjwa, Hijja, Jihadi (Vita), Kufuata Jeneza na Mfano Wake Katika Njia Moja na Kurudi Kwa Njia Fursa za 'Ibaadah
Alhidaaya.com [4]
Hadiyth – 1
عن جابر رضي الله عنه ، قَالَ: كَانَ النبي صلى الله عليه وسلم إِذَا كَانَ يومُ عيدٍ خَالَفَ الطَّريقَ . رواه البخاري .
Amesema Jaabir (Radhwiya Allahu 'anhu): "Alikuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) itakapofika siku ya Iyd hubadilisha njia." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 2
وعن ابن عُمَرَ رضي الله عنهما : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم كَانَ يَخْرُجُ مِنْ طَريق الشَّجَرَةِ ، وَيَدْخُلُ مِنْ طَريقِ الْمُعَرَّسِ ، وَإِذَا دَخَلَ مَكَّةَ ، دَخَلَ مِن الثَّنِيَّةِ الْعُلْيَا ، وَيَخْرُجُ مِنَ الثَّنِيَّةِ السُّفْلَى . متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anatoka mji wa Madiynah kupitia njia ya Shajarah na anaingia kupitia Makkah kutokea Thaniyyatul 'Ulya na akatoka kupitia Thaniyyatus Suflaa (Thaniyyatul ni njia nyembamba baina ya majabali mawili). [Al-Bukhaariy na Muslim]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب استحباب تقديم اليمين في كل مَا هو من باب التكريم
16-Mlango Wa Kuanza kwa Upande wa Kulia Katika Kila Lenye Kupendeza Kama Kutawadha, Kuoga, Kutayamam, Kuvaa na Kuingia Msikitini
Alhidaaya.com [4]
كالوضوءِ وَالغُسْلِ وَالتَّيَمُّمِ ، وَلُبْسِ الثَّوْبِ وَالنَّعْلِ وَالخُفِّ وَالسَّرَاوِيلِ وَدُخولِ الْمَسْجِدِ ، وَالسِّوَاكِ ، وَالاكْتِحَالِ ، وَتقليم الأظْفار ، وَقَصِّ الشَّارِبِ ، وَنَتْفِ الإبْطِ ، وَحلقِ الرَّأسِ ، وَالسّلامِ مِنَ الصَّلاَةِ ، وَالأكْلِ ، والشُّربِ ، وَالمُصافحَةِ ، وَاسْتِلاَمِ الحَجَرِ الأَسْوَدِ ، والخروجِ منَ الخلاءِ ، والأخذ والعطاء وغيرِ ذَلِكَ مِمَّا هُوَ في معناه . ويُسْتَحَبُّ تَقديمُ اليسارِ في ضدِ ذَلِكَ ، كالامْتِخَاطِ وَالبُصَاقِ عن اليسار ، ودخولِ الخَلاءِ ، والخروج من المَسْجِدِ ، وخَلْعِ الخُفِّ والنَّعْلِ والسراويلِ والثوبِ ، والاسْتِنْجَاءِ وفِعلِ المُسْتَقْذرَاتِ وأشْبَاه ذَلِكَ .
Pia kupiga msuwaki, kupaka wanja, kukata kucha, kupunguza masharubu, kung'oa nywele za makapwani na kunyoa nywele. Na pia kutoa salamu ya kumaliza Swalaah, kula na kunywa, kupeana mikono, kulibusu Hajaril Aswad (Jiwe jeusi katika Al-Ka'abah) na kutoka chooni, kupokea na kupeana kitu na shughuli nyengine zilizo sawa na hizo. Na inapendeza kutanguliza kushoto katika mambo yaliyo kinyume na hayo kama kutoa makamasi na kutema mate upande wa kushoto, kuingia chooni, kutoka Msikitini, kuvua soksi na viatu, suruali na nguo, kuosha sehemu za siri baada ya kumaliza haja na kufanya kazi chafu na mfano wake...
قَالَ الله تَعَالَى:
فَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ بِيَمِينِهِ فَيَقُولُ هَاؤُمُ اقْرَءُوا كِتَابِيَهْ﴿١٩﴾
Basi ama yule atakayepewa kitabu chake kuliani mwake; atasema: Hebu chukueni someni kitabu changu! [Al-Haaqah: 19]
فَأَصْحَابُ الْمَيْمَنَةِ مَا أَصْحَابُ الْمَيْمَنَةِ ﴿٨﴾
Basi watu wa kuliani; je, ni nani watu wa kuliani?
وَأَصْحَابُ الْمَشْأَمَةِ مَا أَصْحَابُ الْمَشْأَمَةِ ﴿٩﴾
Na watu wa kushotoni; je, ni nani watu wa kushotoni? [Al-Waaqi'ah: 8-9]
Hadiyth – 1
وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : كَانَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم يُعْجِبُهُ التَّيَمُّنُ في شَأنِهِ كُلِّهِ : في طُهُورِهِ ، وَتَرَجُّلِهِ ، وَتَنَعُّلِهِ . متفقٌ عَلَيْهِ .
'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anha) amesema: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapenda kuanza kuliani katika mambo yake yote: Katika kijitwahirisha kwake, kuchana nywele zake na kuvaa viatu vyake." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 2
وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : كَانَتْ يَدُ رسول الله صلى الله عليه وسلم اليُمْنَى لِطُهُورِهِ وَطَعَامِهِ ، وَكَانَتِ الْيُسْرَى لِخَلائِهِ وَمَا كَانَ مِنْ أذَىً . حديث صحيح ، رواه أَبُو داود وغيره بإسنادٍ صحيحٍ .
'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anha) amesema: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akitumia mkono wake wa kuume kwa kujitwahirisha na kulia chakula. Na alikuwa anautumia mkono wake wa kushoto kujisafisha anapoingia haja (chooni) na mambo mengine kama hayo." [Hadiyth Swahiyh, Abu Daawuwd na wengineo kwa Isnaad iliyo Swahiyh].
Hadiyth – 3
وعن أم عطية رضي الله عنها : أنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم قَالَ لهن في غَسْلِ ابْنَتِهِ زَيْنَبَ رضي الله عنها : (( ابْدَأنَ بِمَيَامِنِهَا ، وَمَوَاضِعِ الوُضُوءِ مِنْهَا )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Ummu 'Atwiyyah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba Nabiy (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwaambia walipokuwa wanamuosha binti yake, Zaynab (Radhwiya Allaahu 'anhaa): "Anzeni kuliani kwake na sehemu za udhu wake." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 4
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إِذَا انْتَعَلَ أحَدُكُمْ فَلْيَبْدَأْ بِالْيُمْنَى ، وَإِذَا نَزَعَ فَلْيَبْدأْ بِالشِّمَالِ . لِتَكُنْ اليُمْنَى أوَّلَهُمَا تُنْعَلُ ، وَآخِرُهُمَا تُنْزَعُ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mmoja wenu anapovaa viatu aanze kwa mguu wa kulia na anapovua aanze kwa mguu wa kushoto. Hivyo, uwe mguu wa kulia wa mwanzo kuvaa nao viatu na wa mwisho kuvua viatu." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 5
وعن حفصة رضي الله عنها : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم كَانَ يجعل يَمينَهُ لطَعَامِهِ وَشَرَابِهِ وَثِيَابِهِ ، وَيَجْعَلُ يَسَارَهُ لِمَا سِوَى ذَلِكَ . رواه أَبُو داود والترمذي وغيره .
Imepokewa kutoka kwa Hafswah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) ya kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliujaalia mkono wake wa kulia ni wa kulia chakula, na kunywea kinywaji na kuvulia nguo. Na aliutumia mkono wake wa kushoto kwa mambo mengine yasiyokuwa hayo." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy na wengineo]
Hadiyth – 6
وعن أَبي هُريرة رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إِذَا لَبِسْتُمْ ، وَإِذَا تَوَضَّأتُمْ ، فَابْدَأوا بأيَامِنِكُمْ )) حديث صحيح ، رواه أَبُو داود والترمذي بإسناد صحيح .
Imepokewa kutoka kwa Ahu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Alllahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anzeni kwa mkono wenu wa kulia mnapovaa nguo na mnapo tawadha." [Hadiyth Swahiyh, Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy kwa Isnaad Swahiyh]
Hadiyth – 7
وعن أنس رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم أتى مِنىً ، فَأتَى الْجَمْرَةَ فَرَمَاهَا ، ثُمَّ أتَى مَنْزِلَهُ بِمِنَىً ونحر ، ثُمَّ قَالَ لِلحَلاَّقِ : (( خُذْ )) وأشَارَ إِلَى جَانِبهِ الأَيْمَنِ ، ثُمَّ الأَيْسَرِ ، ثُمَّ جَعَلَ يُعْطِيهِ النَّاسَ . متفقٌ عَلَيْهِ .
وفي رواية : لما رمَى الجَمْرَةَ ، وَنَحَرَ نُسُكَهُ وَحَلَقَ ، نَاوَلَ الحَلاَّقَ شِقَّهُ الأَيْمَنَ فَحَلَقَهُ ، ثُمَّ دَعَا أَبَا طَلْحَةَ الأنْصَارِيَّ رضي الله عنه ، فَأعْطَاهُ إيَّاهُ ، ثُمَّ نَاوَلَهُ الشِّقَّ الأَيْسَرَ ، فَقَالَ : (( احْلِقْ )) ، فَحَلَقَهُ فَأعْطَاهُ أَبَا طَلْحَةَ ، فَقَالَ : (( اقْسِمْهُ بَيْنَ النَّاسِ )) .
Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alifika Mina, akalielekea Jamarah na kutupa vijiwe. Baada ya hapo alirudi kwenye hema lake hapo Mina na kuchinja mnyama wake. Kisha alimwambia kinyozi: "Chukua (yaani amnyoe)." Akamuashiria upande wa kuliani (mwa kichwa chake) na kisha kushoto. Akawa anawapatia nywele zake watu (aliponyolewa). [Al-Bukhaariy, Muslim, abu Daawuwd na At-Tirmidhiy]
Na katika riwaayah nyingine: Baada ya kurusha vijiwe kwenye Jamarah na kuchinja mnyama wake na akajitayarisha kunyolewa, alimuonyesha kinyozi upande wa kulia naye akamnyoa. Kisha alimuita abu Twalhah Al-Ansaariyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) na akampatia hizo nywele. Baada ya hilo, alimuonyehsa kinyozi upande wa kushoto, na akanyolewa upande huo pia. akampatia Abu Twalhah nywele hizo na kumwambia: "Wagawanyie watu."
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/280
[2] http://www.alhidaaya.com/sw/
[3] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10315&title=01-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Kitabu%20Cha%20Nidhamu%20-%20%D9%83%D9%90%D8%AA%D8%A7%D8%A8%D9%8F%20%D8%A7%D9%84%D8%A3%D8%AF%D9%8E%D8%A8%20
[4] http://www.alhidaaya.com/
[5] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10828&title=01-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Haya%20na%20Fadhila%20Zake%20na%20Kuhimizwa%20Kuwa%20na%20Maadili%20Hayo
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10829&title=02-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kuhifadhi%20Siri
[7] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10830&title=03-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kutekeleza%20Ahadi
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10831&title=04-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kuhifadhi%20Aliyozoea%20Katika%20Mambo%20ya%20Kheri
[9] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10832&title=05-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kupendeza%20Kuzungumza%20Vizuri%20na%20Kuwa%20na%20Bashasha%20Wakati%20wa%20Kukutana%20na%20Mtu
[10] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10833&title=06-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kupendeza%20Kubainisha%20Maneno%20na%20Kuweza%20Wazi%20kwa%20Mwenye%20Kusikiliza%20na%20Kuyakariri%20Ili%20Apate%20Kufahamu%20Ikiwa%20Hatafahamu%20Ila%20Kwayo
[11] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10834&title=07-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Mtu%20Kumsikiliza%20aliyekaa%20Nae%20Ambayo%20Sio%20Haramu%2C%20na%20Kumsikiliza%20Mwanazuoni%20na%20Mtoa%20Waadhi%20Mbele%20ya%20Mkutano%20Wake
[12] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10835&title=08-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kutorefusha%20Mawaidha
[13] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10872&title=09-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Heshima%20na%20Utulivu
[14] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10875&title=10-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kupendeza%20Kuja%20Katika%20Swalaah%20na%20%27Ibaadah%20Nyinginezo%20Kwa%20Utulivu%20na%20Kwa%20Unyenyekevu
[15] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10876&title=11-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kumkirimu%20Mgeni
[16] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10901&title=12-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kupendeza%20Kutoa%20Bishara%20na%20Kupongeza%20Kwa%20Kufikiwa%20na%20Kheri
[17] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10910&title=13-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kumuaga%20Rafiki%20na%20Kumuusia%20Mnapotengana%20Kwa%20Ajili%20ya%20Safari%20na%20Kumuombea%20na%20Kutaka%20Akuombee%20Duaa
[18] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10911&title=14-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kutaka%20Msaada%20wa%20Allaah%20na%20Ushauri
[19] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10912&title=15-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kupendeza%20Kwenda%20Kwenye%20Swalaah%20ya%20Iyd%20na%20Kuwazuru%20Wagonjwa%2C%20Hijja%2C%20Jihadi%20%28Vita%29%2C%20Kufuata%20Jeneza%20na%20Mfano%20Wake%20Katika%20Njia%20Moja%20na%20Kurudi%20Kwa%20Njia%20Fursa%20za%20%27Ibaadah
[20] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10913&title=16-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kuanza%20kwa%20Upande%20wa%20Kulia%20Katika%20Kila%20Lenye%20Kupendeza%20Kama%20Kutawadha%2C%20Kuoga%2C%20Kutayamam%2C%20Kuvaa%20na%20Kuingia%20Msikitini