(Mabustani Ya Swalihina)
كتاب عيادة المريض وتشييع الميت والصلاة عليه وحضور دفنه
06-Kitabu Cha Kumzuru Mgonjwa, Jeneza;
Kumswalia Maiti Na Kuhudhuria Mazishi Yake
Alhidaaya.com [2]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب عيَادة المريض وَتشييع المَيّت
والصّلاة عليه وَحضور دَفنهِ وَالمكث عِنْدَ قبرهِ بَعدَ دَفنه
01-Mlango Wa Kutembelea Mgonjwa Kufuata Jeneza, Kumswalia Maiti, Kuhudhuria Mazishi Yake na Kukaa Kwenye Kaburi Lake Kwa Muda
Alhidaaya.com [4]
Hadiyth – 1
عن البَرَاءِ بن عازِبٍ رضي الله عنهما ، قَالَ : أمَرَنَا رسولُ الله صلى الله عليه وسلم بعِيَادَةِ الْمَريضِ ، وَاتِّبَاعِ الجَنَازَةِ ، وَتَشْمِيتِ العَاطِسِ ، وَإبْرَارِ الْمُقْسِمِ ، وَنَصْرِ المَظْلُومِ ، وَإجَابَةِ الدَّاعِي ، وَإفْشَاءِ السَّلاَمِ . متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Al-Baraa' bin 'Aazib (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: "Ametuamuru sisi Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuzuru wagonjwa, kufuata jeneza, kumwombea dua anapochemua mtu, kutekeleza viapo, kumnusuru aliyedhulumiwa, kuitikia mwaliko na kueneza salamu za amani." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 2
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( حَقُّ المُسْلِمِ عَلَى المُسْلِمِ خَمْسٌ : رَدُّ السَّلاَمِ ، وَعِيَادَةُ المَرِيضِ ، وَاتِّبَاعُ الجَنَائِزِ ، وَإجَابَةُ الدَّعْوَةِ ، وَتَشْمِيتُ العَاطِسِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Haki ya Muislamu kwa Muislamu mwenziwe ni Tano: Kurudisha salamu (anapokusalimia kwa Assalaamu 'Alaykum), kumzuru mgonjwa, kufuata jeneza, kuitikia mwaliko na kumwombea dua anapochemua mmoja wenu." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 3
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( إنَّ اللهَ عز وجل يَقُولُ يَومَ القِيَامَةِ : يَا ابْنَ آدَمَ ، مَرِضْتُ فَلَمْ تَعُدنِي ! قَالَ : يَا رَبِّ ، كَيْفَ أعُودُكَ وَأنْتَ رَبُّ العَالَمِينَ ؟! قَالَ : أمَا عَلِمْتَ أنَّ عَبْدِي فُلاَناً مَرِضَ فَلَمْ تَعُدْهُ ! أمَا عَلِمْتَ أنَّكَ لَوْ عُدْتَهُ لَوَجَدْتَني عِنْدَهُ ! يَا ابْنَ آدَمَ ، اسْتَطْعَمْتُكَ فَلَمْ تُطْعِمنِي ! قَالَ : يَا رَبِّ ، كَيْفَ أطْعِمُكَ وَأنْتَ رَبُّ العَالَمِينَ ؟! قَالَ : أمَا عَلِمْتَ أنَّهُ اسْتَطْعَمَكَ عَبْدِي فُلانٌ فَلَمْ تُطْعِمْهُ ! أمَا عَلِمْتَ أنَّكَ لَوْ أطْعَمْتَهُ لَوَجَدْتَ ذَلِكَ عِنْدِي ! يَا ابْنَ آدَمَ ، اسْتَسْقَيْتُكَ فَلَمْ تَسْقِنِي ! قَالَ : يَا رَبِّ ، كَيْفَ أسْقِيكَ وَأنْتَ رَبُّ العَالَمينَ ؟! قَالَ : اسْتَسْقَاكَ عَبْدِي فُلاَنٌ فَلَمْ تَسْقِهِ ! أمَا عَلِمْتَ أنَّكَ لَوْ سَقَيْتَهُ لَوَجَدْتَ ذَلِكَ عِنْدِي ! )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika Allaah 'Azza wa Jalla Atasema Siku ya Qiyaamah: "Ee mwanadamu! Nimeumwa hukunizuru." Atasema: "Ee Rabb wangu! Vipi nitakuzuru nawe ni Rabb wa viumbe vyote?" Atasema: "Je, hukujua kuwa mja wangu fulani ameumwa hukumzuru?, Hukujua lau ungemzuru ungenikuta kwake?, Ee mwanadamu! Nilikuomba chakula hukunilisha." Akasema: "Ee Rabb wangu! Vipi natakulisha nawe ni Rabb wa viumbe?", Atasema: "Hukujua mja wangu fulani alikuomba chakula hukumlisha?, Hukujua lau ungemlisha ungepata hilo kwangu?, Ee mwanadamu! Nilikuomba maji hukunipa." Atasema: "Ee Rabb wangu! Vipi nitakunywesha Nawe ni Rabb wa viumbe?", Allaah atasema: "Mja wangu fulani alikuomba maji hukumpa. Hukujua lau ungempa ungepata ujira wako Kwangu?" [Muslim].
Hadiyth – 4
وعن أَبي موسى رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( عُودُوا المَريضَ ، وَأطْعِمُوا الجَائِعَ ، وَفُكُّوا العَانِي )) رواه البخاري
Imepokewa kwa Abu Muwsaa Al-'Ash'ariy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mtembeleeni mgonjwa, na mlisheni mwenye njaa msameheni mwenye makosa mateka." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 5
وعن ثوبان رضي الله عنه ، عن النبي صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إنَّ المُسْلِمَ إِذَا عَادَ أخَاهُ المُسْلِمَ ، لَمْ يَزَلْ في خُرْفَةِ الْجَنَّةِ حَتَّى يَرْجِعَ )) قِيلَ : يَا رَسولَ الله ، وَمَا خُرْفَةُ الجَنَّةِ ؟ قَالَ : (( جَنَاهَا )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Thawbaan (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika Muislamu anapomzuru nduguye Muislamu aliye mgonjwa huwa miongoni pamoja na Khurfah ya Peponi mpaka arudipo." Pakasemwa: "Ee Rasuli wa Allaah! Na Khurfah ya Peponi ni nini?" Akasema: "Matunda yake." [Muslim]
Hadiyth – 6
وعن عليّ رضي الله عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ، يَقُولُ : (( مَا مِنْ مُسْلِم يَعُودُ مُسْلِماً غُدْوة إِلاَّ صَلَّى عَلَيْهِ سَبْعُونَ ألْفَ مَلَكٍ حَتَّى يُمْسِي ، وَإنْ عَادَهُ عَشِيَّةً إِلاَّ صَلَّى عَلَيْهِ سَبْعُونَ ألْفَ مَلَكٍ حَتَّى يُصْبحَ ، وَكَانَ لَهُ خَرِيفٌ في الْجَنَّةِ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Kutoka kwa 'Aliy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Hakuna Muislamu anayemtembelea Muislamu mwenziwe aliye mgonjwa baina ya Swalaah ya Alfajiri na kuchomoza jua isipokuwa wanamuombea yeye Malaika elfu sabiini mpaka kuingie jioni. Na akimtembelea mwisho wa mchana huwa wanamuombea yeye Malaika elfu sabiini mpaka kupambazuke. Na anapatiwa bustani la matunda Peponi." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]
Hadiyth – 7
وعن أنسٍ رضي الله عنه ، قَالَ : كَانَ غُلاَمٌ يَهُودِيٌّ يَخْدُمُ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم ، فَمَرِضَ ، فَأتَاهُ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم يَعُودُهُ ، فَقَعَدَ عِنْدَ رَأسِهِ ، فَقَالَ لَهُ : (( أسْلِمْ )) فَنَظَرَ إِلَى أبِيهِ وَهُوَ عِنْدَهُ ؟ فَقَالَ : أَطِعْ أَبَا القَاسِمِ ، فَأسْلَمَ ، فَخَرَجَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم ، وَهُوَ يَقُولُ : (( الحَمْدُ للهِ الَّذِي أنْقَذَهُ منَ النَّارِ )) رواه البخاري .
Amesema Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu): Kulikuwa na kijana wa kiyahudi aliyekuwa akimtumikia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Alishikwa na ugonjwa na hivyo Nabiy alimzuru na akakaa karibu na kichwa chake na akamwambia: "Silimu." Kijana alimtizama babake aliye naye. Babake Akamwambia: "Mtii Abul Qaasim (yaani Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Kijana alisilimu, naye Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alitoka nyumbani kwao na huku anasema: "Sifa zote anastahiki Allaah aliyemuepusha na moto." [Al-Bukhaariy].
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب مَا يُدعى به للمريض
02-Mlango Wa Duaa za Kumuombea Mgonjwa
Alhidaaya.com [4]
Hadiyth – 1
عن عائشة رضي الله عنها : أنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم ، كَانَ إِذَا اشْتَكى الإنْسَانُ الشَّيْءَ مِنْهُ ، أَوْ كَانَتْ بِهِ قَرْحَةٌ أَوْ جُرْحٌ ، قَالَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم بِأُصْبُعِهِ هكَذا – وَوَضَعَ سُفْيَانُ بْنُ عُيَيْنَة الرَّاوي سَبَّابَتَهُ بِالأَرْضِ ثُمَّ رَفَعَها – وقال : (( بِسمِ اللهِ ، تُرْبَةُ أرْضِنَا ، بِرِيقَةِ بَعْضِنَا ، يُشْفَى بِهِ سَقِيمُنَا ، بإذْنِ رَبِّنَا )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwake 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anaposhtakiwa na mtu kwa maumivu asikiayo au jipu au jeraha, alikuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akifanya hivi kwa kidole chake cha shahada, na akaweka Sufyaan bin 'Uyaynah, mpokezi wa Hadiyth hii kidole chake cha shahada kwenye ardhi, kisha anakinyanyua na akasema: "BismiLLaah Turbatu Ardhina Biriiqati Ba'dhina Yushfaa bihi Saqiimuna Biidhni Rabbina - Kwa jina la Allaah, huu ni mchanga wa ardhiyetu, kwa mate ya baadhi yetu, anaponywa mgonjwa wetu kwa idhini ya Rabb wetu." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 2
عن عائشة رضي الله عنها : أنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ يَعُودُ بَعْضَ أهْلِهِ يَمْسَحُ بِيدِهِ اليُمْنَى ، ويقولُ : (( اللَّهُمَّ رَبَّ النَّاسِ ، أذْهِب البَأسَ ، اشْفِ أنْتَ الشَّافِي لاَ شِفَاءَ إِلاَّ شِفاؤكَ ، شِفَاءً لاَ يُغَادِرُ سَقماً )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuwa akimtembelea mtu wa familia yake mgonjwa. Alikuwa akimgusa kwa mkono wake wa kulia na kusema: "Allaahumma Rabban Naas Adhhibul Ba'sa washfi Antash Shaafi Laa Shifaa' illaa Shifaa'uka Laa Yughaadiru Saqama - Ee Rabb wangu! Rabb wa watu, ondoa ubaya na ponyesha, Wewe Ndiye Mponyeshaji, hakuna ponyo isipokuwa ponyo lako, ponyo lisiloacha ugonjwa." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 3
وعن أنسٍ رضي الله عنه أنه قَالَ لِثابِتٍ رحمه اللهُ : ألاَ أرْقِيكَ بِرُقْيَةِ رسول الله صلى الله عليه وسلم ؟ قَالَ : بَلَى ، قَالَ : (( اللَّهُمَّ رَبَّ النَّاسِ ، مُذْهِبَ البَأسِ ، اشْفِ أنْتَ الشَّافِي ، لاَ شَافِيَ إِلاَّ أنْتَ ، شِفَاءً لاَ يُغَادِرُ سَقماً )) رواه البخاري .
Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) Alimwambia Thaabit: "Nikufanyie Ruqyah ya Rasuli wa Allaah?" Akasema: "Ndio." Akasema: "Ee Rabb wangu! Rabb wa watu, Mwenye kuondoa ubaya, ponyesha, Wewe ni Mponyaji, hakuna Mponyaji isipokuwa Wewe, ponyo lisiloacha ugonjwa." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 4
وعن سعدِ بن أَبي وقاصٍ رضي الله عنه ، قَالَ : عَادَنِي رسول الله صلى الله عليه وسلم ، فَقَالَ : (( اللَّهُمَّ اشْفِ سَعْداً ، اللَّهُمَّ اشْفِ سَعْداً ، اللَّهُمَّ اشْفِ سَعْداً )) رواه مسلم .
Amesema Sa'd bin Abu Waqqaas: Alinitembelea Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kumuombea: Ee Rabb wangu! ponyeshe Sa'd. Ee Rabb wangu! Mponyesha Sa'd. Ee Rabb wangu! Mponyeshe Sa'd." [Muslim]
Hadiyth – 5
وعن أَبي عبدِ الله عثمان بنِ أَبي العاصِ رضي الله عنه : أنّه شَكَا إِلَى رسول الله صلى الله عليه وسلم وَجَعاً ، يَجِدُهُ في جَسَدِهِ ، فَقَالَ لَهُ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( ضَعْ يَدَكَ عَلَى الَّذِي يَألَم مِنْ جَسَدِكَ وَقُلْ : بسم اللهِ ثَلاثاً ، وَقُلْ سَبْعَ مَرَّاتٍ : أعُوذُ بِعِزَّةِ الله وَقُدْرَتِهِ مِنْ شَرِّ مَا أجِدُ وَأُحَاذِرُ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu 'Abdillaah 'Uthmaan bin Abil 'Aas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba alimshitakia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa maumivu anayoyasikia katika mwili wake. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia: "Weka mkono wako katika sehemu inayokuuma kwenye mwili wako kisha useme: 'BismiLLaah (Thalaath - mara tatu) na useme mara saba: A'uudhu Bi'izzati Llaahi wa Qudratihi min sharri maa Ajidu wa Uhaadhir (Najilinda kwa Nguvu za Allaah na Kudura Yake kwa shari iliyo ninayoiona na ambayo ninaiogopa." [Muslim]
Hadiyth – 6
وعن ابن عباسٍ رضي الله عنهما ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مَنْ عَادَ مَرِيضاً لَمْ يَحْضُرْهُ أجَلُهُ ، فقالَ عِنْدَهُ سَبْعَ مَرَّاتٍ : أسْأَلُ اللهَ العَظيمَ ، رَبَّ العَرْشِ العَظيمِ ، أنْ يَشْفِيَكَ ، إِلاَّ عَافَاهُ اللهُ مِنْ ذَلِكَ المَرَضِ )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) ، وقال الحاكم : (( حديث صحيح عَلَى شرط البخاري )) .
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kumtembelea mgonjwa ambaye ajali yake haijafika na akasema mbele yake mara saba: 'As'alu Llaahal 'Adhiym Rabbal 'Arshil 'Adhiym an Yashfiyaka - Namuomba Allaah Al-'Adhiym, Rabb wa 'Arshi (Kiti cha enzi) Al-'Adhiym akupony)', isipokuwa Allaah hmuondolea maradhi hayo." [Abuu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan. Na akasema Al-Haakim: "Hii ni Hadiyth Swahiyh kwa sharti za Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 7
وعن ابن عباسٍ رضي الله عنهما : أنَّ النبي صلى الله عليه وسلم دَخَلَ عَلَى أعْرَابِيٍّ يَعُودُهُ ، وَكَانَ إِذَا دَخَلَ عَلَى مَنْ يَعُودُهُ ، قَالَ : (( لاَ بَأسَ ؛ طَهُورٌ إنْ شَاءَ اللهُ )) رواه البخاري .
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimtembelea Mbedui mgonjwa. Na alikuwa akimtembelea mgonjwa husema: "Laa ba's Twahuur in shaa Allaah (Hakuna ubaya, ugonjwa wako ni tohara yako Allaah Akitaka)." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 8
وعن أَبي سعيد الخدري رضي الله عنه : أن جِبريلَ أتَى النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم ، فَقَالَ : يَا مُحَمَّدُ ، اشْتَكَيْتَ ؟ قَالَ : (( نَعَمْ )) قَالَ : بِسْمِ الله أرْقِيكَ ، مِنْ كُلِّ شَيْءٍ يُؤْذِيكَ ، مِنْ شَرِّ كُلِّ نَفْسٍ أَوْ عَيْنِ حَاسِدٍ ، اللهُ يَشْفِيكَ ، بِسمِ اللهِ أُرقِيكَ . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Jibriyl alikuja kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Akasema: "Ee Muhammad! Unaumwa?" Akasema: "Ndio." Akasema: "BismiLlaah Arqiyk, min kuli Shay'in Yu'dhiyk, min kuli nafsin aw 'ayni haasid, Allaahu Yashfiyk, BismiLlaah Arqiyk (Kwa jina la Allaah nanakutibu kila kinacho kuudhi, kutokana na shari ya kila nafsi au jicho la hasid. Allaah akuponye, kwa jina la Allaah ninakutibu)." [Muslim]
Hadiyth – 9
وعن أَبي سعيد الخدري وأبي هريرة رضي الله عنهما : أنَّهُمَا شَهِدَا عَلَى رسول الله صلى الله عليه وسلم ، أنّه قَالَ : (( مَنْ قَالَ : لاَ إلهَ إِلاَّ اللهُ وَاللهُ أكْبَرُ ، صَدَّقَهُ رَبُّهُ ، فَقَالَ : لاَ إلهَ إِلاَّ أنَا وأنَا أكْبَرُ . وَإِذَا قَالَ : لاَ إلهَ إِلاَّ اللهُ وَحدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ ، قَالَ : يقول : لاَ إلهَ إلاَّ أنَا وَحْدِي لا شَريكَ لِي . وَإِذَا قَالَ : لاَ إلهَ إِلاَّ اللهُ لَهُ المُلْكُ وَلَهُ الحَمْدُ ، قَالَ : لاَ إلهَ إِلاَّ أنَا لِيَ المُلْكُ وَلِيَ الحَمْدُ . وَإِذَا قَالَ : لاَ إله إِلاَّ اللهُ وَلاَ حَوْلَ وَلاَ قُوَّةَ إِلاَّ باللهِ ، قَالَ : لاَ إلهَ إِلاَّ أنَا وَلاَ حَوْلَ وَلاَ قُوَّةَ إِلاَّ بي )) وَكَانَ يقُولُ : (( مَنْ قَالَهَا في مَرَضِهِ ثُمَّ مَاتَ لَمْ تَطْعَمْهُ النَّارُ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) na Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) wao wanashuhudia kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kusema: Hapana Mola ila Allaah, Allaah ni Mkuu.' Allaah anamjibu Anasema: "Hapana Mola ila Mimi, na Mimi ni Mkuu.' Na anaposema: 'Hapana Mola ila Allaah, Peke yake hana mshirika.' Amesema: Anasema: 'Hapana Mola ila Mimi, Peke Yangu sina mshirika.' Na anaposema: 'Hapana Mola ila Allaah, ni Wake Ufalme, ni Kwake kuhimidiwa.' Amesema: 'Hapana Mola ila Mimi, Mimi ni Mfalme na Mimi ni mwenye kusifiwa.' Na anaposema: 'Hapana Mola ila Allaah, hakuna hila wala nguvu ila kwa Allaah.' Amesema: 'Hapana Mola ila Mimi, wala hila wala nguvu isipokuwa Kwangu.' Na Nabiy alikuwa akisema: Mwenye kuyasema katika maradhi yake kisha akafa Moto hautamla." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب استحباب سؤال أهل المريض عن حاله
03-Mlango Wa Kupendeza Kuulizia Hali ya Mgonjwa Kupitia kwa Watu Wake
Alhidaaya.com [4]
عن ابن عباسٍ رضي الله عنهما : أنَّ عليَّ بْنَ أَبي طالب رضي الله عنه ، خَرَجَ مِنْ عِنْدِ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم ، في وَجَعِهِ الَّذِي تُوُفِّيَ فِيهِ ، فقالَ النَّاسُ : يَا أَبَا الحَسَنِ ، كَيْفَ أصْبَحَ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم ؟ قَالَ : أصْبَحَ بِحَمْدِ اللهِ بَارئاً . رواه البخاري .
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba 'Ali bin 'Abi Twaalib (Radhwiya Allaahu 'anhu) alitoka katika chumba cha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuwa anaugua kwa ugonjwa aliokufa nao. Watu walimuuliza: "Ee Abul Hasan! Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amelala (na kuamka) vipi?" Akasema: "Sifa zote anastahiki Allaah ameamka katika hali nzuri." [Al-Bukhaariy]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب مَا يقوله مَن أيس من حياته
04-Mlango Wa Anachosema Mwenye Kukata Tamaa ya Maisha Yake
Alhidaaya.com [4]
Hadiyth – 1
عن عائشة رضي الله عنها ، قالت : سَمِعْتُ النبيَّ صلى الله عليه وسلم وَهُوَ مُسْتَنِدٌ إلَيَّ ، يَقُولُ : (( اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي وارْحَمْنِي ، وأَلْحِقْنِي بالرَّفِيقِ الأَعْلَى )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Amesema 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): Nimemsikia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wakati alipokuwa amejipumzisha juu yake (kabla ya kuaga kwake dunia) akisema: "Ee Mola wangu! Nisamehe na unirehemu na unikutanishe na Rafiki yangu (Mtukufu) Aliye juu." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 2
وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : رَأيتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم وَهُوَ بِالمَوْتِ ، عِنْدَهُ قَدَحٌ فِيهِ مَاءٌ ، وَهُوَ يُدْخِلُ يَدَهُ في القَدَحِ ، ثُمَّ يَمْسَحُ وَجْهَهُ بالماءِ ، ثُمَّ يَقُولُ : (( اللَّهُمَّ أعِنِّي عَلَى غَمَرَاتِ المَوْتِ أَوْ سَكَرَاتِ المَوْتِ )) رواه الترمذي .
Na amesema 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): Nilimuona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa katika hali ya mauti. Alikuwa na kikombe cha maji anatia mkono wake ndani yake, kisha anapangusa uso wake na maji. Kisha anasema: "Ee Mola wangu! Nipunguzie ulevi wa mauti, na uchungu kwani mauti yana ulevi." [At-Tirmidhiy]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب استحباب وصية أهل المريض
ومن يخدمه بالإحسان إليه واحتماله والصبر عَلَى مَا يشق من أمره
وكذا الوصية بمن قرب سبب موته بحد أَوْ قصاص ونحوهما
05-Mlango Wa Kuwausia Watu wa Familia Yenye Mgonjwa na Wanaomuangalia Kumfanyia Wema na Kumfanyia Hisani Aliye katika Uchungu wa Mauti au Aliyehukumiwa Kunyongwa
Alhidaaya.com [4]
عن عِمْران بن الحُصَيْنِ رضي الله عنهما : أنَّ أمْرَأَةً مِنْ جُهَيْنَةَ أتَت النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم وَهِيَ حُبْلَى مِنَ الزِّنَا ، فَقَالَتْ : يَا رسول الله ، أصَبْتُ حَدّاً فَأقِمْهُ عَلَيَّ ، فَدَعَا رسولُ الله صلى الله عليه وسلم وَلِيَّهَا ، فَقَالَ : (( أحْسِنْ إِلَيْهَا ، فَإذَا وَضَعَتْ فَأتِنِي بِهَا )) فَفَعَلَ ، فَأمَرَ بِهَا النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم ، فَشُدَّتْ عَلَيْهَا ثِيَابُهَا ، ثُمَّ أمَرَ بِهَا فَرُجِمَت ، ثُمَّ صَلَّى عَلَيْهَا . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa 'Imraan bin Huswayn (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba mwanamke wa kabila la Juhaynah alikuja kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa na mimba ya zinaa, akasema: "Ee Rasuli wa Allaah! MImi nimezini hivyo nisimamishie adhabu." Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwita walii wake akamwambia: "Mtendee wema, atakapozaa mlete kwangu' Akafanya hivyo. Nabiy aliamuru afungwe kwa nguo zake, kisha akaamuru apigwe mawe. Kisha Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamswalia (Swala ya Jeneza)." [Muslim]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب جواز قول المريض : أنَا وجع ، أَوْ شديد الوجع
أَوْ مَوْعُوكٌ أَوْ وارأساه ونحو ذلك . وبيان أنَّه لا كراهة في ذلك
إِذَا لَمْ يكن عَلَى سبيل التسخط وإظهار الجزع
06-Mlango Wa Kuruhusiwa Mgonjwa Kusema: Ninaumwa au Ninaumwa Sana, Lakini ni Karaha Kusema Hivyo kwa Kukata Tamaa
Alhidaaya.com [4]
Hadiyth – 1
عن ابن مسعود رضي الله عنه ، قَالَ : دَخَلْتُ عَلَى النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم وَهُوَ يُوعَكُ ، فَمَسسْتُهُ ، فَقلتُ : إنَّكَ لَتُوعَكُ وَعَكاً شَديداً ، فَقَالَ : (( أجَلْ ، إنِّي أُوعَكُ كَمَا يُوعَكُ رَجُلانِ مِنْكُمْ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba, nilimzuru Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wakati alipokuwa na homa, nikamwambia: "Ee Rasuli wa Allaah! Hakika wewe una homa kali." Akasema: "Ndio, mimi huumwa kwa maumivu yaliyo sawa na watu wawili miongoni mwenu." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 2
وعن سعدِ بن أَبي وقاصٍ رضي الله عنه ، قَالَ : جَاءني رسولُ الله صلى الله عليه وسلم يَعُودُنِي مِنْ وَجَعٍ اشْتَدَّ بِي ، فقلتُ: بَلَغَ بِي مَا تَرَى ، وَأنَا ذُو مَالٍ ، وَلاَ يَرِثُنِي إِلاَّ ابْنَتِي .. وذَكر الحديث . متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Sa'd bin Waqqaas amesema kwamba: "Alikuja kunizuru mimi Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) nikiwa mgonjwa sana." Nikamwambia: "Ee Rasuli wa Allaah! Umenifikia mimi ugonjwa huu kama unavyoniona na mimi ni tajiri na hakuna anayenirithi isipokuwa binti yangu mmoja"... Na akaitaja Hadiyth. [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 3
وعن القاسم بن محمد، قَالَ : قالت عائشةُ رضي الله عنها : وَارَأسَاهُ ! فَقَالَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم : (( بَلْ أنَا ، وَارَأسَاهُ ! )) ... وذكر الحديث . رواه البخاري .
Na imepokewa kutoka kwa Al-Qaasim bin Muhammad kwamba 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) alisema: "Ah, kichwa changu." Hapo Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Bali, ni kichwa changu"... Na akaitaja Hadiyth. [Al-Bukhaariy]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب تلقين المحتضر : لا إله إِلاَّ اللهُ
07-Mlango Wa Kumlakinia Anayekata Roho kwa Kalima "Laa ILaaha Illa Allaah"
Alhidaaya.com [4]
Hadiyth – 1
عن معاذ رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ كَانَ آخِرَ كَلامِهِ لاَ إلهَ إِلاَّ اللهُ دَخَلَ الجَنَّةَ )) رواه أَبُو داود والحاكم ، وقال : (( صحيح الإسناد )) .
Imepokewa kutoka kwa Mu'aadh (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Yeyote yatakayokua maneno yake ya mwisho Laa ilaaha illa Allaah (Hapana Mola anayepasa kuabudiwa kwa haki ila Allaah) ataingiya peponi." [Abuu Daawuwd na Al-Haakim, na akasema Isnaad yake ni Swahiyh]
Hadiyth – 2
وعن أَبي سعيد الخدري رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( لَقِّنُوا مَوْتَاكُمْ لاَ إلهَ إِلاَّ اللهُ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Walakinieni mauti wenu kwa neno, Laa ilaaha illa Allaah." [Muslim]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب مَا يقوله بعد تغميض الميت
08-Mlango Wa Anayosema Baada ya Kumfumba Macho Maiti
Alhidaaya.com [4]
عن أُم سلمة رضي الله عنها ، قالت : دَخَلَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم عَلَى أَبي سَلَمة وَقَدْ شَقَّ بَصَرُهُ ، فَأغْمَضَهُ ، ثُمَّ قَالَ : (( إنَّ الرُّوحَ إِذَا قُبِضَ ، تَبِعَهُ البَصَرُ )) فَضَجَّ نَاسٌ مِنْ أهْلِهِ ، فَقَالَ : (( لاَ تَدْعُوا عَلَى أنْفُسِكُمْ إِلاَّ بِخَيْرٍ ، فَإنَّ المَلاَئِكَةَ يَؤمِّنُونَ عَلَى مَا تَقُولُونَ )) ثُمَّ قَالَ : (( اللَّهُمَّ اغْفِرْ لأَبِي سَلَمَة ، وَارْفَعْ دَرَجَتْهُ في المَهْدِيِّينَ ، وَاخْلُفْهُ في عَقِبهِ في الغَابِرِينَ ، وَاغْفِرْ لَنَا وَلَهُ يَا رَبَّ العَالَمِينَ ، وَافْسَحْ لَهُ في قَبْرِهِ ، وَنَوِّرْ لَهُ فِيهِ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwake Ummu Salamah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amesema: Aliingia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa Abu Salamah (Radhwiya Allaahu 'anhu) macho yake yapo wazi (alipofariki) akayafumba kisha akasema: "Roho inapotolewa macho huifuata." Watu katika watu wake wakapiga, kelele, Nabiy akawambia: "Msiombee nafsi zenu isipokuwa kheri, kwani Malaaikah wanaitikia Aamiyn kwa hayo mnayosema." Kisha akasema: "Ee Mola wangu! Msamehe Abu Salamah na inua daraja yake katika walioongoka, na mbadilishie kizazi chake katika waliopita. Na utusamehe sisi na yeye ee Mola wa Ulimwengu, na mkunjulie kaburi lake, na linawirishe ndani yake." [Muslim]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب ما يقال عند الميت وَمَا يقوله من مات له ميت
09-Mlango Wa Kinachosemwa kwa Mtu Anayekaribia Kufa na Wanayoambiwa Wafiwa
Alhidaaya.com [4]
Hadiyth – 1
عن أُم سَلَمة رضي اللهُ عنها ، قالت : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( إِذَا حَضَرتُمُ المَرِيضَ أَو المَيِّتَ ، فَقُولُوا خَيْراً ، فَإنَّ المَلائِكَةَ يُؤَمِّنُونَ عَلَى مَا تَقُولُونَ )) ، قالت: فَلَمَّا مَاتَ أَبُو سلَمة، أتَيْتُ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم ، فقلت : يَا رسولَ الله ، إنَّ أَبَا سَلَمَة قَدْ مَاتَ، قَالَ : (( قُولِي: اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي وَلَهُ، وَأعْقِبْنِي مِنْهُ عُقْبى حَسَنَةً )) فقلتُ ، فَأعْقَبنِي اللهُ مَنْ هُوَ خَيْرٌ لِي مِنْهُ : مُحَمَّداً صلى الله عليه وسلم . رواه مسلم هكَذا : (( إِذَا حَضَرتُمُ المَريضَ ، أَو المَيِّتَ )) ، عَلَى الشَّكِّ ، ورواه أَبُو داود وغيره : (( الميت )) بلا شَكّ .
Imepokewa kutoka kwa Ummu Salamah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mtakapo kuwepo mahali alipo mgonjwa au maiti basi semeni yaliyo ya kheri kwani Malaaikah huitikia Aamiyn kwa hayo mnayoyasema." Akasema (Radhwiya Allaahu 'anhaa): "Alipoaga dunia Abu Salamah nilikuja kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) nikamwambia: "Ee Rasuli wa Allaah! Hakika Abu Salamah ameaga dunia." Akasema: "Sema: "Allaahummaghfirli wa lahu wa A'qibniy minhu 'uqbaa hasanah (Ee Mola nisamehe na umsamehe yeye na unipatie mimi mbadala mwema)." Nikaomba dua hiyo na Allaah akanibadilishia kwa aliye bora kuliko yeye (yaani Abu Salamah), naye ni Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)." [Muslim]. Na imenukuliwa hivi "Mtakapo kuwepo mahali alipo mgonjwa" au "maiti" juu ya shaka, lakini amepokea Abu Daawuwd na wengineo: "Maiti", bila ya shaka yoyote.
Hadiyth – 2
عن أُم سَلَمة رضي اللهُ عنها ، قالت : سَمِعْتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( مَا مِنْ عَبْدٍ تُصيبُهُ مُصِيبَةٌ ، فَيَقُولُ : إنّا للهِ وَإنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ ، اللَّهُمَّ أُجِرْنِي في مُصِيبَتي وَاخْلفْ لِي خَيراً مِنْهَا ، إِلاَّ أَجَرَهُ اللهُ تَعَالَى في مُصِيبَتِهِ وَأخْلَفَ لَهُ خَيْراً مِنْهَا )) قالت : فَلَمَّا تُوُفِّيَ أَبُو سَلَمَة قلتُ كَمَا أمَرَني رسولُ الله صلى الله عليه وسلم ، فَأخْلَفَ اللهُ لِي خَيْراً مِنْهُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم . رواه مسلم .
Kutoka kwa Ummu Salamah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba amesema: Nimmsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Akisema: "Hakuna mtu anayepatwa na msiba na akasema: Hakika sisi ni wa Allaah, na kwake tunarudi. Ee Mola nilipe katika msiba wangu, na nipe mbadala bora zaidi yake", isipokuwa atalipwa na Allaah katika msiba wake huo na atampatia mbadala bora kuliko hiyo." Akasema: "Alipofariki Abu Salamah (Radhwiya Allaahu 'anhu) nikasema kama alivyoniamuru Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), na Allaah akanipa mbadala bora kuliko yeye yaani Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)." [Muslim]
Hadiyth – 3
وعن أَبي موسى رضي اللهُ عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إِذَا مَاتَ وَلَدُ العَبْدِ ، قَالَ اللهُ تَعَالَى لِمَلائِكَتِهِ : قَبَضْتُمْ وَلَدَ عَبْدِي ؟ فيقولونَ : نَعَمْ . فيقولُ : قَبَضْتُمْ ثَمَرَة فُؤَادِهِ ؟ فيقولونَ : نَعَمْ . فيقولُ : مَاذَا قَالَ عَبْدِي ؟ فيقولونَ : حَمدَكَ وَاسْتَرْجَعَ . فيقول اللهُ تَعَالَى : ابْنُوا لِعَبْدِي بَيْتاً في الجَنَّةِ ، وَسَمُّوهُ بَيْتَ الحَمْدِ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Imepokewa kutoka kwa Abu Muwsaa (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anapokufa mtoto wa mja, Allaah anauliza Malaaikah wake: "Mmefisha mtoto wa mja wangu?" Wanasema: "Ndio." Atasema: 'Mja wangu amesema nini?' Watasema: 'Amekuhimidi na akarejea, Atasema Allaah Ta'aalaa: 'Mjengeeni mja wangu nyumba Peponi, na iiteni Nyumba ya Kuhimidiwa." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]
Hadiyth – 4
وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( يقولُ اللهُ تَعَالَى : مَا لِعَبْدِي المُؤمِن عِنْدِي جَزَاءٌ إِذَا قَبَضْتُ صَفِيَّهُ مِنْ أهْل الدُّنْيَا ، ثُمَّ احْتَسَبَهُ إِلاَّ الجَنَّةَ )) رواه البخاري .
Imepokewa kutoka kwake Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Allaah Ta'aalaa, husema, 'Hakika mja Wangu Muumini ambaye anasubiri na akwa na matarajio ya thawabu pindi Ninapomchukua kipenzi chake katika watu wa dunia isipokuwa ni kumuingiza Peponi." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 5
وعن أسَامَة بن زَيدٍ رضي اللهُ عنهما ، قَالَ : أرْسَلَتْ إحْدى بَنَاتِ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم إِلَيْهِ تَدْعُوهُ وَتُخْبِرُهُ أنَّ صَبِيَّاً لَهَا – أَوْ ابْناً – في المَوْتِ فَقَالَ للرسول : (( ارْجِعْ إِلَيْهَا ، فَأخْبِرْهَا أنَّ للهِ تَعَالَى مَا أخَذَ وَلَهُ مَا أعْطَى ، وَكُلُّ شَيْءٍ عِنْدَهُ بِأجَلٍ مُسَمّى ، فَمُرْهَا ، فَلْتَصْبِرْ وَلْتَحْتَسِبْ )) ... وذكر تمام الحديث . متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwake Usamah bin Zayd (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) "Bint ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimtuma mtu kuja kumuita Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwani mtoto wake alikuwa katika utangulizi wa mauti." Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alituma salamu kwake na ujumbe ufuatao: "Kwa hakika mikononi mwa Allaah zipo Anazochukuwa na zile Anazotoa. Na kila kitu Kwake kina wakati maalumu, hivyo asubiri na atarajie thawabu (kutoka kwa Allaah)..." Na akataja Hadiyth kwa ukamilifu wake. [Al-Bukhaariy na Muslim]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب جواز البكاء عَلَى الميت بغير ندب وَلاَ نياحة
10-Mlango Wa Ruhusa ya Kulia Unapofiwa Bila Kuomboleza
Alhidaaya.com [4]
أمَّا النِّيَاحَةُ فَحَرَامٌ وَسَيَأتِي فِيهَا بَابٌ فِي كِتابِ النَّهْيِ ، إنْ شَاءَ اللهُ تَعَالَى . وَأمَّا البُكَاءُ فَجَاءتْ أحَادِيثُ بِالنَّهْيِ عَنْهُ ، وَأنَّ المَيِّتَ يُعَذَّبُ بِبُكَاءِ أهْلِهِ ، وَهِيَ مُتَأَوَّلَةٌ ومَحْمُولَةٌ عَلَى مَنْ أوْصَى بِهِ ، وَالنَّهْيُ إنَّمَا هُوَ عَن البُكَاءِ الَّذِي فِيهِ نَدْبٌ ، أَوْ نِيَاحَةٌ ، والدَّليلُ عَلَى جَوَازِ البُكَاءِ بِغَيْرِ نَدْبٍ وَلاَ نِياحَةٍ أحَادِيثُ كَثِيرَةٌ ، مِنْهَا :
Ama kuomboleza ni haramu kabisa na kutakuja mlango kuhusu hilo katika kitabu cha makatazo, Allaah akipenda. Na ama kulia zipo Hadiyth nyingi zinazokataza, na hakika ni kuwa maiti anaadhibiwa kwa kulia watu wake. Katazo ni kule kulia pamoja na kujipiga na kuomboleza. Na dalili za kujuzu kulia bila kujipiga au kuomboleza ni nyingi, miongoni mwazo:
Hadiyth – 1
عن ابن عمر رضي الله عنهما : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم عاد سَعْدَ بْنَ عُبَادَةَ، وَمَعَهُ عَبدُ الرَّحْمانِ بْنُ عَوفٍ، وَسَعدُ بْنُ أَبي وَقَّاصٍ، وَعَبْدُ اللهِ بْنُ مَسْعُودٍ رضي الله عنه، فَبَكَى رسولُ الله صلى الله عليه وسلم ، فَلَمَّا رَأى القَوْمُ بُكَاءَ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم بَكَوْا ، فَقَالَ : (( ألاَ تَسْمَعُونَ ؟ إنَّ الله لاَ يُعَذِّبُ بِدَمْعِ العَينِ ، وَلاَ بِحُزنِ القَلبِ ، وَلَكِنْ يُعَذِّبُ بِهذَا أَوْ يَرْحَمُ )) وَأشَارَ إِلَى لِسَانِهِ . متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimtembelea Sa'd bin 'Ubadah (Radhwiya Allaahu 'anhu) akiwa pamoja na 'Abdur-Rahmaan bin 'Awf na Sa'd bin Abi Waqqaas na 'Abdillaah bin Mas'uuwd (Radhwiya Allaah 'anhum) Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alilia kuiona hali yake na watu walipomuona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akilia nao pia wakalia. Akasema: "Sikilizeni! Hakika Allaah humuadhibu kwa kutokwa na machozi wala kwa huzuni ya moyo, lakini anaadhibu kwa hili au anawahurumia." Na hapo akaashiria mdomo wake." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 2
وعن أُسَامَة بن زَيدٍ رضي اللهُ عنهما : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم رُفِعَ إِلَيْهِ ابنُ ابْنَتِهِ وَهُوَ فِي المَوتِ ، فَفَاضَتْ عَيْنَا رسولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، فَقَالَ لَهُ سَعدٌ : مَا هَذَا يَا رسولَ الله ؟! قَالَ : (( هذِهِ رَحْمَةٌ جَعَلَهَا اللهُ تَعَالَى في قُلُوبِ عِبَادِهِ ، وَإنَّمَا يَرْحَمُ اللهُ مِنْ عِبَادِهِ الرُّحَمَاءَ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Usamah bin Zayd (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), alinyanyuliwa kwake mtoto wa binti yake akiwa katika hali ya mauti. Nabiy alibubijika machozi. Sa'd akasema: "Hii ni rehma Allaah ameiweka ndani ya nyoyo za waja Wake." Hakika Allaah anahurumia waja Wake wenye huruma." [Ahmad, Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 3
وعن أنسٍ رضي اللهُ عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم دَخَلَ عَلَى ابْنِهِ إبْرَاهيمَ رضي اللهُ عنه ، وَهُوَ يَجُودُ بِنَفسِهِ ، فَجَعَلَتْ عَيْنَا رسولِ الله صلى الله عليه وسلم تَذْرِفَان . فَقَالَ لَهُ عبدُ الرحمانِ بن عَوف : وأنت يَا رسولَ الله ؟! فَقَالَ : (( يَا ابْنَ عَوْفٍ إنَّهَا رَحْمَةٌ )) ثُمَّ أتْبَعَهَا بأُخْرَى ، فَقَالَ : (( إنَّ العَيْنَ تَدْمَعُ والقَلب يَحْزنُ ، وَلاَ نَقُولُ إِلاَّ مَا يُرْضِي رَبَّنَا ، وَإنَّا لِفِرَاقِكَ يَا إبرَاهِيمُ لَمَحزُونُونَ )) رواه البخاري ، وروى مسلم بعضه . والأحاديث في الباب كثيرة في الصحيح مشهورة ، والله أعلم .
Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliingia kwa mtoto wake Ibraahim akiwa katika hali ya kukata roho. Hapo macho ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) yakadondokwa na machozi. Akamwambia 'Abdir-Rahmaan bin 'Awf: "Hata wewe, ee Rasuli wa Allaah?" Akasema: "Ee Ibn 'Awf! Hakika hiyo ni huruma." Baada ya hapo akaanza kulia tena na akasema: "Hakika jicho linatoa machozi na moyo unahuzunika na hatusemi ila yanayomridhisha Rabb wetu, nasi kwa kufarikiana nawe Ibraahiym tumehuzunika." [Al-Bukhaariy, na Muslim amenukuu baadhi yake. Na Hadiyth katika mlango huu ni nyingi zilizo Swahiyh na mashuhuri. Na Allaah anajua zaidi].
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب الكف عن مَا يرى من الميت من مكروه
11-Mlango Wa Kuhifadhi Aibu Zinazoonekana kwa Maiti
Alhidaaya.com [4]
وعن أَبي رافع أسلم مولى رسول الله صلى الله عليه وسلم : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مَنْ غَسَّلَ مَيتاً فَكَتَمَ عَلَيْهِ ، غَفَرَ اللهُ لَهُ أربَعِينَ مَرَّة )) رواه الحاكم ، وقال : صحيح عَلَى شرط مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Raafi' Aslam (Radhwiya Allaahu 'anhu) mwacha huru wa Rasuli wa Allaah (Swalla Alllahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kumuosha maiti na akaficha siri yake, Allaah humsamehe mara arubaini." [Al-Haakim, na akasema ni Swahiyh kulingana na sharti iliyowekwa na Muslim].
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب الصلاة عَلَى الميت وتشييعه وحضور دفنه
وكراهة اتباع النساء الجنائز
12-Mlango Wa Kumswalia Maiti na Kufuata Jeneza na Kuhudhuria Kuzikwa Kwake na Karaha kwa Wanawake Kufuata Jeneza
Alhidaaya.com [4]
Hadiyth – 1
عن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ شَهِدَ الجَنَازَةَ حَتَّى يُصَلَّى عَلَيْهَا ، فَلَهُ قِيراطٌ ، وَمَنْ شَهِدَهَا حَتَّى تُدْفَنَ ، فَلَهُ قِيرَاطَانِ )) قِيلَ : وَمَا القِيرَاطانِ ؟ قَالَ : (( مِثْلُ الجَبَلَيْنِ العَظِيمَيْنِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kushuhudia jeneza mpaka likaswaliwa atakuwa na ujira wa Qiraati moja na mwenye kushuhudia mpaka akazikwa maiti, atakuwa na ujira wa Qiraati mbili." Akaulizwa: "Na Qiraati mbili ina maana gani?" Akasema: "Ni mfano wa majabali mawili makubwa." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy na An-Nasai']
Hadiyth – 2
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مَنِ اتَّبَعَ جَنَازَةَ مُسْلِمٍ إيماناً وَاحْتِسَاباً ، وَكَانَ مَعَهُ حَتَّى يُصَلَّى عَلَيْهَا وَيُفرَغَ مِنْ دَفْنِهَا ، فَإنَّهُ يَرْجعُ مِنَ الأَجْرِ بِقيراطَيْنِ كُلُّ قِيرَاطٍ مِثْلُ أُحُدٍ ، وَمَنْ صَلَّى عَلَيْهَا ، ثُمَّ رَجَعَ قَبْلَ أنْ تُدْفَنَ ، فَإنَّهُ يَرْجِعُ بِقيرَاطٍ )) رواه البخاري .
Kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kufuata jeneza la Muislamu kwa Imani nakutaraji radhi za Allaah, Atarejea na malipo ya Qiraati mbili, kila Qiraati nikama Mlima wa Uhud, na mwenye kuliswalia, kisha akarudi kabla ya kuzikwa atarudi na Qiraati moja." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 3
وعن أم عطية رضي الله عنها ، قالت : نُهِينَا عَنِ اتِّبَاعِ الجَنَائِزِ ، وَلَمْ يُعْزَمْ عَلَيْنَا . متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kwa Ummu Atwiyyah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amesema: "Tumekatazwa kufuata jeneza, na (hilo) halikuazimiwa kwetu sisi." [Al-Bukhaariy, Muslim na Abu Daawuwd]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب استحباب تكثير المصلين عَلَى الجنازة
وجعل صفوفهم ثلاثة فأكثر
13-Mlango Wa Kupenda Kuwa na Jamaa Kubwa Katika Swalaah ya Jeneza na Kuzifanya Safu Zake Tatu na Zaidi
Alhidaaya.com [4]
Hadiyth – 1
عن عائشة رضي الله عنها ، قالت : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( مَا مِنْ مَيتٍ يُصَلِّي عَلَيْهِ أُمَّةٌ مِنَ المُسْلِمِينَ يَبْلُغُونَ مِئَةً كُلُّهُمْ يَشْفَعُونَ لَهُ إِلاَّ شُفِّعُوا فِيهِ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwake 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakuna maiti yeyote anayeswaliwa na kikundi cha Waislaamu wanaofika mia moja wote wanamuombea isipokuwa Allaah anakubali maombi yao." [Muslim]
Hadiyth – 2
وعن ابن عباسٍ رضي الله عنهما ، قَالَ : سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( مَا مِنْ رَجُلٍ مُسْلِمٍ يَمُوتُ ، فَيقومُ عَلَى جَنَازَتِهِ أرْبَعُونَ رَجُلاً لاَ يُشْرِكُونَ بِاللهِ شَيْئاً ، إِلاَّ شَفَّعَهُمُ اللهُ فِيهِ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Hakuna mtu Muislaamu aliyefariki, wakasimama kwenye jeneza lake watu arubaini wasiomshirikisha Allaah na chochote isipokuwa Allaah humsamehe (maiti)." [Muslim]
Hadiyth – 3
وعن مرثدِ بن عبدِ الله اليَزَنِيِّ ، قَالَ : كَانَ مَالِكُ بن هُبَيْرَة رضي اللهُ عنه إِذَا صَلَّى عَلَى الجَنَازَةِ ، فَتَقَالَّ النَّاس عَلَيْهَا ، جَزَّأَهُمْ عَلَيْهَا ثَلاَثَةَ أجْزَاءٍ ، ثُمَّ قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ صَلَّى عَلَيْهِ ثَلاَثَةُ صُفُوفٍ فَقَدْ أوْجَبَ )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
imepokewa kutoka kwa Marthad bin 'Abdillaah Al-Yazaniyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: Alikuwa Maalik bin Hubayrah anaposwalia jeneza yenye watu kidogo anawagawa safu tatu, kisha anasema: "Mwenye kuswaliwa na safu tatu hakika imethibiti (yaani imewajibika kuingizwa Peponi)." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب مَا يقرأ في صلاة الجنازة
14-Mlango Wa Kisomo Katika Swalaah ya Jeneza
Alhidaaya.com [4]
إِنَّ اللَّـهَ وَمَلَائِكَتَهُ يُصَلُّونَ عَلَى النَّبِيِّ ۚ ﴿٥٦﴾
Hakika Allaah na Malaika Wake wanamswalia Nabiy. [Al-Ahzaab: 56]
فَإنَّهُ لاَ تَصحُّ صَلاَتُهُ إِذَا اقْتَصَرَ عَلَيْهِ ، ثُمَّ يُكَبِّرُ الثَّالِثَةَ ، وَيَدعُو للمَيِّتِ وَللمُسْلِمِينَ بِمَا سَنَذكُرُهُ مِنَ الأحاديث إنْ شَاءَ اللهُ تَعَالَى ، ثُمَّ يُكَبِّرُ الرَّابِعَةَ وَيَدْعُو . وَمِنْ أحْسَنِهِ : (( اللَّهُمَّ لاَ تَحْرِمْنَا أجْرَهُ ، وَلاَ تَفْتِنَّا بَعدَهُ ، وَاغْفِرْ لَنَا وَلَهُ )) . وَالمُخْتَارُ أنه يُطَوِّلُ الدُّعاء في الرَّابِعَة خلافَ مَا يَعْتَادُهُ أكْثَرُ النَّاس ، لحديث ابن أَبي أَوْفى الذي سَنَذْكُرُهُ إنْ شَاء اللهُ تَعَالَى .
Kwani haisihi Swalaah bila ya kusoma Suratul Faatihah. Kisha ataleta takbira ya tatu, na kumuombea maiti na Waislamu wote kwa jumla kama tutakavyo taja Hadiyth in shaa Allaah. Kisha atapiga tabiri ya nne, na aombe kwa dua tofauti, na zilizo bora ni: Allaahumma laa tahrimna ajrahu walaa taftinna ba'dahu waghfirlana walahu. Na inayopendeza ni aifanye dua ndefu katika takbira ya nne kinyume na walivyozoea watu wengi kwa mujibu wa Hadiyth ya Ibn Abu Awfaa ambayo tutaitaja in shaa Allaah.
Hadiyth – 1
عن أَبي عبد الرحمان عوف بن مالك رضي اللهُ عنه ، قَالَ : صَلَّى رسول الله صلى الله عليه وسلم عَلَى جَنازَةٍ ، فَحَفِظْتُ مِنْ دُعَائِهِ ، وَهُوَ يقُولُ : (( اللَّهُمَّ اغْفِرْ لَهُ وَارْحَمْهُ ، وَعَافِهِ وَاعْفُ عَنْهُ ، وَأكْرِمْ نُزُلَهُ ، وَوَسِّعْ مُدْخَلَهُ ، وَاغْسِلْهُ بِالمَاءِ وَالثَّلْجِ وَالبَرَدِ ، وَنَقِّه مِن الخَطَايَا كَمَا نَقَّيْتَ الثَّوْبَ الأَبْيَضَ مِنَ الدَّنَس ، وَأبدلْهُ دَاراً خَيْراً مِنْ دَارِهِ ، وَأهْلاً خَيراً مِنْ أهْلِهِ ، وَزَوْجَاً خَيْراً مِنْ زَوْجِهِ ، وَأدْخِلهُ الجَنَّةَ ، وَأعِذْهُ مِنْ عَذَابِ القَبْرِ ، وَمنْ عَذَابِ النَّارِ )) حَتَّى تَمَنَّيتُ أن أكُون أنَا ذَلِكَ الْمَيِّت . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu 'Abdir-Rahmaan 'Awf bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Alituswalisha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Swalaah ya jeneza, nikahifadhi katika dua yake akisema: "Ee Mola mdgufirie na umrehemu, na msalimishe na msamehe, na mkirimu kwa kushuka kwake, na kunjua kuingia kwake. Na muoshe kwa maji, theluji na barafu. Na safisha makosa yake kama inayosafishwa nguo nyeupe kutokana na uchafu. Na mbadilishie nyumba yake, na jamaa bora kuliko nyumba yake, na jamaa bora kuliko jamaa zake. na mwenza kuliko bora kuliko mwenza wake. Na mwepushe na adhabu ya kaburi, na adhabu ya moto. Mpaka nikatamani kuwa niwe huyo maiti." [Muslim]
Hadiyth – 2
وعن أَبي هريرة وأبي قتادة وَأبي إبراهيم الأشهلي ، عن أبيه – وأبوه صَحَابيٌّ – رضي اللهُ عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم : أنَّهُ صَلَّى عَلَى جَنَازَةٍ ، فَقَالَ : (( اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِحَيِّنَا وَمَيِّتِنَا ، وَصَغِيرنَا وَكَبيرنَا ، وَذَكَرِنَا وَأُنْثَانَا ، وشَاهِدنَا وَغَائِبِنَا ، اللَّهُمَّ مَنْ أحْيَيْتَهُ مِنَّا فَأحْيِهِ عَلَى الإسْلاَمِ ، وَمَنْ تَوَفَّيْتَهُ مِنَّا فَتَوفَّهُ عَلَى الإيمَان ، اللَّهُمَّ لاَ تَحْرِمْنَا أجْرَهُ ، وَلاَ تَفْتِنَّا بَعدَهُ )) رواه الترمذي
Imepokewa kwake Abu Hurayrah na Abu Qataadah na Abu Ibraahiym Al-Ashhaliyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kutoka kwa babake, na babake ni Swahaaba kutoka Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): kuwa aliswalisha Swalaah ya jeneza, akasema: "Ee Mola wasamehe walio hai miongoni mwetu na waliokufa, na watoto wetu na wazee wetu, na wanaume wetu na wanawake, na waliopo na wasio kuwepo. Ee Mola, yeyote miongoni mwetu utakaye mpatia uhai mfanye aishi juu ya Uislamu na utakaye mfisha miongoni mwetu mfishe katika Imani. Ee Mola usituharamishie ujira wake wala usitufitini baada yake." [At-Tirmidhiy]
Hadiyth – 3
وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( إِذَا صَلَّيْتُمْ عَلَى المَيِّتِ ، فَأخْلِصُوا لَهُ الدُّعاء )) رواه أَبُو داود .
Na amesema Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Mnapo mswalia maiti basi ksudieni dua zenu kwa ikhlasi." [Abu Daawuwd]
Hadiyth – 4
وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم في الصَّلاَةِ عَلَى الجَنَازَةِ : (( اللَّهُمَّ أنْتَ رَبُّهَا ، وَأنْتَ خَلَقْتَهَا ، وَأنتَ هَدَيْتَهَا للإسْلاَمِ ، وَأنتَ قَبَضْتَ رُوحَهَا ، وَأنْتَ أعْلَمُ بِسرِّهَا وَعَلاَنِيَتِهَا ، وَقَدْ جِئنَاكَ شُفَعَاءَ لَهُ ، فَاغْفِرْ لَهُ )) رواه أَبُو داود .
Kutoka kwake Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliomba duaa ifuatayo katika Swalaah ya jeneza: "Ee Mola, Wewe ni Rabb wake, na Wewe umemuumba, na Wewe umemuongoza katika Uislamu, na Wewe unayejua siri na dhahiri yake, nasi tumekujia waombezi wake, basi msamehe." [Abu Daawuwd]
Hadiyth – 5
وعن وَاثِلَة بنِ الأَسْقَعِ رضي اللهُ عنه ، قَالَ : صَلَّى بِنَا رسول الله صلى الله عليه وسلم عَلَى رَجُلٍ مِنَ المُسْلِمِينَ ، فَسَمِعْتُهُ يَقُولُ : (( اللَّهُمَّ إنَّ فُلانَ ابْنَ فُلانٍ في ذِمَتِّكَ وَحَبْلِ جِوَارِكَ ، فَقِهِ فِتْنَةَ القَبْرِ ، وَعذَابَ النَّار ، وَأنْتَ أهْلُ الوَفَاءِ وَالحَمْدِ ؛ اللَّهُمَّ فَاغْفِرْ لَهُ وَارْحَمْهُ ، إنَّكَ أنْتَ الغَفُورُ الرَّحيمُ )) رواه أَبُو داود .
Amesema Waathilah bin Al-Asqa' (Radhwiya Allaahu 'anhu): Alituswalisha Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), kumswalia mtu miongoni mwa Waislamu, nikamsikia akisema: "Ee Mola, hakika fulani mtoto wa fulani yupo katika dhima Yako (kwenye ahadi Yako) na kamba ya ujirani wako, hivyo muhifadhi fitna ya kaburi na adhabu ya Moto. Nawe ni Bwana wa kulipa na kuhimidiwa. Ee Mola mghufurie na umrehemu, hakika Wewe ni Mwingi wa kusamehe Mwingi wa kurehemu." [Abu Daawuwd]
Hadiyth – 6
وعن عبدِ الله بنِ أبي أَوْفى رضي الله عنهما : أنَّهُ كَبَّرَ عَلَى جَنَازَةِ ابْنَةٍ لَهُ أرْبَعَ تَكْبِيرَاتٍ ، فَقَامَ بَعْدَ الرَّابِعَةِ كَقَدْرِ مَا بَيْنَ التَّكْبِيرَتَيْنِ يَسْتَغْفِرُ لَهَا وَيَدْعُو ، ثُمَّ قَالَ : كَانَ رسول اللهِ صلى الله عليه وسلم يَصْنَعُ هكَذَا .
وفي رواية : كَبَّرَ أرْبَعاً فَمَكَثَ سَاعَةً حَتَّى ظَنَنْتُ أنَّهُ سَيُكَبِّرُ خَمْساً ، ثُمَّ سَلَّمَ عَنْ يَمينِهِ وَعَنْ شِمَالِهِ . فَلَمَّا انْصَرَفَ قُلْنَا لَهُ : مَا هَذَا ؟ فَقَالَ : إنِّي لاَ أزيدُكُمْ عَلَى مَا رأيْتُ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يَصْنَعُ ، أَوْ : هكَذَا صَنَعَ رسول الله صلى الله عليه وسلم . رواه الحاكم ، وقال : (( حديث صحيح )) .
Imepokewa kutoka kwake 'Abdillah bin Abu Awfaa (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba alileta takbiri nne katika Swalaah ya jeneza ya binti yake. Baada ya takbiri ya nne alisimama kwa kitambo kirefu muda uliokuwa sawa na takbiri mbili huku akimuombea msamaha (maiti). Kisha akasema: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akifanya kama nilivyofanya."
Katika riwaya nyengine: "Alipiga ya nne akakaa kidogo hadi nikadhani kuwa atapiga ya tano, kisha akatoa salamu kulia kwake. Alipoondoka tulimwambia: "Nini hiki?" akasema: "Mimi sikuzidishieni juu ya nilivyomuona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akifanya, Au: Kama hivi amefanya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). [Al Haakim na akasema Hadiyth Swahiyh]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب الإسراع بالجنازة
15-Mlango Wa Kuharakisha Jeneza
Alhidaaya.com [4]
Hadiyth – 1
عن أَبي هريرة رضي الله عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( أسْرِعُوا بالجَنَازَةِ ، فَإنْ تَكُ صَالِحَةً ، فَخَيرٌ تُقَدِّمُونَهَا إِلَيْهِ ، وَإنْ تَكُ سِوَى ذَلِكَ ، فَشَرٌّ تَضَعُونَهُ عَنْ رِقَابِكُمْ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
وفي روايةٍ لمسلمٍ : (( فَخَيْرٌ تُقَدِّمُونَهَا عَلَيْهِ )) .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Liharakisheni jeneza (lipelekeni haraka), kama litakuwa la mwema basi mnalipeleka kwenye kheri na kama halikuwa hivyo basi mnajiodoshea mwovu shingoni mwenu." [Al-Bukhaariy, Muslim, Maalik, Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy na An-Nasaai]
Hadiyth – 2
وعن أَبي سعيد الخدري رضي الله عنه ، قَالَ : كَانَ النبي صلى الله عليه وسلم ، يقُولُ : (( إِذَا وُضِعَت الجَنَازَةُ ، فَاحْتَمَلَهَا الرِّجَالُ عَلَى أعنَاقِهمْ ، فَإنْ كَانَتْ صَالِحَةً ، قالتْ : قَدِّمُونِي ، وَإنْ كَانَتْ غَيْرَ صَالِحَةٍ ، قَالَتْ لأَهْلِهَا : يَا وَيْلَهَا أَيْنَ تَذْهَبُونَ بِهَا ؟ يَسْمَعُ صَوْتَهَا كُلُّ شَيْءٍ إِلاَّ الإنْسَانَ ، وَلَوْ سَمِعَ الإنسَانُ لَصَعِقَ )) رواه البخاري .
Amesema Abu Sa'iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Itakapokuwa tayari jeneza na ikabebwa na watu juu ya mabega yao, akiwa ni mtu mwema atasema: 'Nipelekeni mbele, nipelekeni mbele (yaani nifikisheni haraka katika kaburi langu). Na ikiwa si mwema atasema: 'Ee, ole wake! Munaipeleka wapi?' Sauti yake inasikika na kila kitu isipokuwa mwanadamu na lau angesikia (mwanadamu) basi angezimia." [Al-Bukhaariy]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب تعجيل قضاء الدَّين عن الميت
والمبادرة إِلَى تجهيزه إلا أن يموت فجأة فيترك حَتَّى يُتَيَقَّنَ مَوْتُه
16-Mlango Wa Kuharakisha Kumlipia Deni Maiti na Kuharakisha Kumuandaa Isipokuwa Mauti Yake Yathibitike
Alhidaaya.com [4]
Hadiyth – 1
عن أَبي هريرة رضي الله عنه ، عن النبي صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( نَفْسُ المُؤْمِنِ مُعَلَّقَةٌ بِدَيْنِهِ حَتَّى يُقْضى عَنْهُ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Imepokewa kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Nafsi ya Muumini hutundikwa kwa deni lake mpaka lilipwe." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]
Hadiyth – 2
وعن حُصَيْنِ بن وَحْوَحٍ رضي الله عنه : أنَّ طَلْحَةَ بْنَ البَرَاءِ بن عَازِبٍ رضي الله عنهما مَرِضَ ، فَأتَاهُ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم يَعُودُهُ ، فَقَالَ : (( إنِّي لاَ أرى طَلْحَةَ إِلاَّ قَدْ حَدَثَ فِيهِ المَوْتُ ، فآذِنُوني بِهِ وَعَجِّلُوا بِهِ ، فَإنَّهُ لاَ يَنْبَغِي لجِيفَةِ مُسْلِمٍ أنْ تُحْبَسَ بَيْنَ ظَهْرَانِيْ أهْلِهِ )) رواه أَبُو داود .
Imepokewa kutoka kwa Huswayn Wahwah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Twalhah bin Al-Baraa' alishikwa na ugonjwa na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaja kumzuru na kusema: "Hakika mimi nadhania kuwa Twalhah yu karibu na umauti, hivyo anapofariki nifahamisheni na fanyeni haraka kumzika, kwani haifai kwa maiti ya Muislaamu kubaki kwa familia yake bila sababu yeyote." [Abuu Daawuwd]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب الموعظة عند القبر
17-Mlango Wa Mawaidha Kwenye Kaburi
Alhidaaya.com [4]
عن عَلِيٍّ رضي الله عنه ، قَالَ : كُنَّا فِي جَنَازَةٍ في بَقيعِ الغَرْقَدِ ، فَأتَانَا رسولُ الله صلى الله عليه وسلم فَقَعَدَ ، وَقَعَدْنَا حَوْلَهُ وَمَعَهُ مِخْصَرَةٌ فَنَكَّسَ وَجَعَلَ يَنْكُتُ بِمِخْصَرَتِهِ ، ثُمَّ قَالَ : (( مَا مِنْكُمْ مِنْ أحَدٍ إِلاَّ وَقَدْ كُتِبَ مَقْعَدُهُ مِنَ النَّارِ وَمَقْعَدُهُ مِنَ الجَنَّةِ )) فقالوا : يَا رسولَ الله ، أفَلا نَتَّكِلُ عَلَى كِتَابنَا ؟ فَقَالَ : (( اعْمَلُوا ؛ فكلٌّ مُيَسرٌ لِمَا خُلِقَ لَهُ ... )) وذكَر تَمَامَ الحديث . متفقٌ عَلَيْهِ .
'Aliy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Tulikuwa na jeneza makaburi ya Baqi' Al-Gharqad. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akatujia akakaa, tukakaa pembeni yake akiwa na bakora, Akainamisha kichwa chake na anakwaruza ardhi kwa fimbo yake. Kisha akasema: "Hakuna yoyote miongoni mwenu ila ameandikiwa kikao chake motoni na kikao chake Peponi." Wakauliza: "Ee Rasuli wa Allaah! Tutegemee katika vitabu vyetu?", Akasema: "Fanyeni kwani kila mmoja amerahisishiwa alioumbiwa (na kukuduriwa)." Na akataja Hadiyth hiyo kwa ukamilifu wake. [Al-Bukhaariy na Muslim]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب الدعاء للميت بعد دفنه والقعود عند قبره
ساعة للدعاء لَهُ والاستغفار والقراءة
18-Mlango Wa Kumuombea Dua Maiti Baada ya Kuzikwa na Kukaa Kwenye Kaburi Lake kwa Muda
Alhidaaya.com [4]
Hadiyth – 1
وعن أَبي عمرو - وقيل : أَبُو عبد الله ، وقيل : أَبُو ليلى - عثمان بن عفان رضي الله عنه ، قَالَ : كَانَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم إِذَا فُرِغَ مِن دَفْنِ المَيِّتِ وَقَفَ عَلَيْهِ ، وقال : (( اسْتَغْفِرُوا لأخِيكُمْ وَسَلُوا لَهُ التَّثْبِيتَ ، فَإنَّهُ الآنَ يُسألُ )) رواه أَبُو داود .
Amesema Abu 'Amruw (Radhwiya Allaahu 'anhu) na panasemwa Abu 'Abdillaah - na panasemwa Abu Laylaa 'Uthmaan bin 'Affaan (Radhwiya Allaahu 'anhu): Alikuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisimama kwnye kaburi baada ya kumzika maiti na kusema: "Muombeeni msamaha ndugu yenu na mupmbeeni uthabiti kwani yeye sasa hivi anaulizwa." [Abuu Daawuwd]
Hadiyth – 2
وعن عمرو بن العاص رضي الله عنه ، قَالَ : إِذَا دَفَنْتُمُونِي ، فَأقِيمُوا حَوْلَ قَبْرِي قَدْرَ مَا تُنْحَرُ جَزُورٌ ، وَيُقَسَّمُ لَحمُهَا حَتَّى أَسْتَأنِسَ بِكُمْ ، وَأعْلَمَ مَاذَا أُرَاجِعُ بِهِ رُسُلَ رَبِّي . رواه مسلم .
Imepokewa kwa 'Amruw bin Al-'Aas amesema: Mtakaponizika simameni pembeni ya kaburi langu kiasi cha kuchinjwa ngamia, na kugawanywa nyama yake, ili nijiliwaze nanyi, nijue nini nitawajibu wajume wa Rabb wangu." [Muslim]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب الصدقة عن الميت والدعاء لَهُ
19-Mlango Wa Kumtolea Swadaqah Maiti na Kumuombea Dua
Alhidaaya.com [4]
قَالَ الله تَعَالَى:
وَالَّذِينَ جَاءُوا مِن بَعْدِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالْإِيمَانِ ﴿١٠﴾
Na wale waliokuja baada yao wanasema: Rabb wetu! Tughufurie na ndugu zetu ambao wametutangulia kwa iymaan. [Al-Hashr: 10]
Hadiyth – 1
وعن عائشة رضي الله عنها : أنَّ رجلاً قَالَ للنبيِّ صلى الله عليه وسلم : إنَّ أُمِّي افْتُلِتَتْ نَفْسُهَا وَأُرَاهَا لَوْ تَكَلَّمَتْ تَصَدَّقَتْ ، فَهَلْ لَهَا أجْرٌ إنْ تَصَدَّقْتُ عَنْهَا ؟ قَالَ : (( نَعَمْ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) alisema mtu fulani alimwambia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Mama yangu amekufa nadhani lau angesema angetoa sadaka. Je, anapata thawabu nikimtolea sadaka?" Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema: "Ndiyo." [Al-Bukhaariy na muslim]
Hadiyth – 2
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إِذَا مَاتَ الإنْسَانُ انْقَطَعَ عَمَلُهُ إِلاَّ مِنْ ثَلاثٍ : صَدَقةٍ جَاريَةٍ ، أَوْ عِلْمٍ يُنْتَفَعُ بِهِ ، أَوْ وَلَدٍ صَالِحٍ يَدْعُو لَهُ )) رواه مسلم .
Imepokewa kwake Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anapokufa mwanadamu hukatika amali yake isipokuwa mambo matatu: Sadaka endelevu, au elimu yenye manufaa au mtoto mwema anamuombea dua." [Muslim]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب ثناء الناس عَلَى الميت
20-Mlango Wa Maiti Anayesifiwa na Watu
Alhidaaya.com [4]
Hadiyth – 1
عن أنسٍ رضي الله عنه ، قَالَ : مَرُّوا بِجَنَازَةٍ ، فَأَثْنَوْا عَلَيْهَا خَيْراً ، فَقَالَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم : (( وَجَبَتْ )) ثُمَّ مَرُّوا بِأُخْرَى ، فَأثْنَوْا عَلَيْهَا شَرّاً ، فَقَالَ النبي صلى الله عليه وسلم : (( وَجَبَتْ )) ، فَقَالَ عمر بن الخطاب رضي الله عنه : مَا وَجَبَت ؟ فَقَالَ : (( هَذَا أثْنَيْتُمْ عَلَيْهِ خَيْراً ، فَوَجَبتْ لَهُ الجَنَّةُ ، وهَذَا أثْنَيْتُمْ عَلَيْهِ شَرّاً ، فَوَجَبَتْ لَهُ النَّار ، أنْتُمْ شُهَدَاءُ اللهِ في الأَرضِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Lilipita jeneza, watu wakamsifu maiti. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Imethibiti." Kisha likapita jengine wakamsema vibaya. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Imethibiti." Umar bin Al-Khatwaab (Radhwiya Allaahu 'anhu) akauliza: "Nini kilichothibiti?" Akamjibu: "Huyu mmemsifia kheri, imethibiti kwake Pepo; na huyu mmeeleza ubaya wake, umethibiti kwake Moto. watu ni mashahidi wa Allaah ardhini." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 2
وعن أَبي الأسْوَدِ ، قَالَ : قَدِمْتُ المَدِينَةَ ، فَجَلَسْتُ إِلَى عُمَرَ بنِ الخَطَّاب رضي الله عنه فَمَرَّتْ بِهمْ جَنَازَةٌ ، فَأُثْنِيَ عَلَى صَاحِبِهَا خَيْراً ، فَقَالَ عُمَرُ : وَجَبَتْ ، ثُمَّ مُرَّ بَأُخْرَى فَأُثْنِيَ عَلَى صَاحِبِهَا خَيْراً ، فَقَالَ عُمرُ : وَجَبَتْ ، ثُمَّ مُرَّ بِالثَّالِثَةِ ، فَأُثْنِيَ عَلَى صَاحِبِهَا شَرّاً ، فَقَالَ عُمر : وَجَبَتْ ، قَالَ أَبُو الأسودِ : فقلتُ : وَمَا وَجَبَتْ يَا أمْيرَ المُؤمِنينَ ؟ قَالَ : قُلْتُ كما قَالَ النبي صلى الله عليه وسلم : (( أيُّمَا مُسْلِمٍ شَهِدَ لَهُ أرْبَعَةٌ بِخَيرٍ ، أدْخَلَهُ اللهُ الجَنَّةَ )) فقُلْنَا : وَثَلاثَةٌ ؟ قَالَ : (( وَثَلاثَةٌ )) فقلنا : وَاثْنَانِ ؟ قَالَ : (( وَاثْنَانِ )) ثُمَّ لَمْ نَسْأَلْهُ عَن الواحِدِ . رواه البخاري .
Amesema Abil Aswad: Nilikuja Madiynah na nikakaa na 'Umar bin Al-Khatwaab (Radhwiya Allaahu 'anhu) likapita jeneza na watu wakamsifu maiti. 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) akasema: "Imethibiti." Kisha likapita jengine wakamsifu kwa wema. 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) akasema: "Imethibiti." Kisha likapita la tatu wakasema vibaya. 'Umar akasema: "Imethibiti." Akasema Abul Aswad: Nikasema: "Ni nini kilichothibiti ee Amiri wa Waumini?" Akasema: "Nimesema kama alivyosema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): 'Muislamu yeyote anayeshuhudiwa na watu wanne kwa kheri, Allaah atamuingiza Peponi." Tukauliza: Je, na watatu?" Akasema: "Nawatatu." Tukauliza: Je, na wawili?" Akasema: "Na wawili pia." Kisha hatukuuliza kuhusu mtu mmoja." [Al-Bukhaariy]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب فضل من مات لَهُ أولاد صغار
21-Mlango Wa Ubora wa Kufiwa na Watoto Wachanga
Alhidaaya.com [4]
Hadiyth – 1
وعن أنسٍ رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَا مِنْ مُسْلِمٍ يَمُوتُ لَهُ ثَلاَثَةٌ لَمْ يَبْلُغوا الحِنْثَ إِلاَّ أدْخَلَهُ اللهُ الجَنَّةَ بِفَضْلِ رَحْمَتِهِ إيَّاهُمْ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakuna Muislamu yeyote anayefiwa na watoto watatu ambao hawaja baleghe isipokuwa Allaah atamuingiza Peponi kwa fadhila ya rehma Yake kwao (yaani watoto)." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 2
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( لاَ يَمُوتُ لأَحَدٍ مِنَ المُسْلِمينَ ثَلاَثَةٌ مِنَ الوَلَدِ لاَ تَمسُّهُ النَّارُ إِلاَّ تَحِلَّةَ القَسَمِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Moto hautamgusa Muislamu aliyefiwa na watoto watatu ila hadiya kwa kutekeleza yamini." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 3
وعن أَبي سعيد الخدري رضي الله عنه، قَالَ : جَاءتِ امْرأةٌ إِلَى رسولِ الله صلى الله عليه وسلم ، فَقَالَتْ : يَا رسولَ الله ، ذَهبَ الرِّجَالُ بِحَدِيثكَ ، فَاجْعَلْ لَنَا مِنْ نَفْسِكَ يَوْماً نَأتِيكَ فِيهِ تُعَلِّمُنَا مِمَّا عَلَّمَكَ اللهُ ، قَالَ : (( اجْتَمِعْنَ يَوْمَ كَذَا وَكَذَا )) فَاجْتَمَعْنَ ، فَأَتَاهُنَّ النبيُّ صلى الله عليه وسلم فَعَلَّمَهُنَّ مِمَّا عَلَّمَهُ اللهُ ، ثُمَّ قَالَ : (( مَا مِنْكُنَّ مِنِ امْرَأةٍ تُقَدِّمُ ثَلاَثَةً مِنَ الوَلَدِ إِلاَّ كَانُوا لَهَا حِجَاباً مِنَ النَّارِ )) فقالتِ امْرَأةٌ : وَاثْنَينِ ؟ فَقَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( وَاثْنَيْنِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Amesema Abu Sa'iyd Al-Khudriy: mwanamke Alikuja kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kusema: "Ee Rasuli wa Allaah! Wanaume wametutangulia kwa Hadiyth zako, hivyo tuwekee siku ambayo tutakuja kwako ili utufundishe aliyo kufundisha Allaah." Akasema: "Kusanyikeni siku kadha wa kadha." Wanawake wakakusanyika siku iliyopangwa na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaja kwao na kuwafundisha aliyofunuliwa na Allaah, kisha akasema: "Hakuna yeyote miongoni mwenu ambaye atawatanguliza (atafiwa) watoto watatu isipokuwa watakuwa ni kinga kwake na Moto." Mwanamke mmoja Akasema: "je, na wawili?" Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Na wawili pia." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب البكاء والخوف عِنْدَ المرور بقبور الظالمين
ومصارعهم وإظهار الافتقار إِلَى الله تَعَالَى
والتحذير من الغفلة عن ذلك
22-Mlango Wa Kulia Kuwa na Hofu Wakati wa Kupita Kwenye Makaburi ya Madhalimu, Kunyenyekea kwa Allaah na Onyo kwa Kughafilika na Hilo
Alhidaaya.com [4]
عن ابن عمرَ رضي الله عنهما : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ لأصْحَابِهِ - يعْني لَمَّا وَصَلُوا الحِجْرَ - دِيَارَ ثَمُودَ - : (( لاَ تَدْخُلُوا عَلَى هَؤُلاَءِ المُعَذَّبِينَ إِلاَّ أنْ تَكُونُوا بَاكِينَ ، فَإنْ لَمْ تَكُونُوا بَاكِينَ ، فَلاَ تَدْخُلُوا عَلَيْهِمْ ، لاَ يُصِيبُكُمْ مَا أصَابَهُمْ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
وفي روايةٍ قَالَ : لَمَّا مَرَّ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم بِالحِجْرِ ، قَالَ : (( لاَ تَدْخُلُوا مَسَاكِنَ الَّذِينَ ظَلَمُوا أنْفُسَهُمْ ، أنْ يُصِيبَكُمْ مَا أصَابَهُمْ ، إِلاَّ أنْ تَكُونُوا بَاكِينَ )) ثُمَّ قَنَّع رسولُ الله صلى الله عليه وسلم ، رَأسَهُ وأسْرَعَ السَّيْرَ حَتَّى أجَازَ الوَادِي .
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwaambia Sahaaba zake (yaani walipowasili Hijr), nyumba na ardhi ya Thamuwd: "Musiingie kwa hawa watu wanaoadhibiwa isipokuwa mkiwa mnalia (kwa kuonyesha huzuni na hofu); Ikiwa hamtalia, basi musiingie kabisa katika sehemu hiyo musije mukafikiwa na yale yaliowakumba wao." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Katika riwaayah nyingine amesema: Alipopita Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Hijr alisema: "Musiingie katika makazi ya wale waliodhulumu nafsi zao ili musifikiwe na yale yalio wafika ila ikiwa mtakuwa ni wenye kulia." Kisha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alijifunika kichwa chake kwa nguo na akakaza mwendo hadi akapita bonde hilo.
Links
[1] http://alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/280
[2] http://www.alhidaaya.com/sw/
[3] https://www.addtoany.com/share#url=http%3A%2F%2Falhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10320&title=06-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Kitabu%20Cha%20Kumzuru%20Mgonjwa%2C%20Jeneza...%20-%20%D9%83%D8%AA%D8%A7%D8%A8%20%D8%B9%D9%8A%D8%A7%D8%AF%D8%A9%20%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%B1%D9%8A%D8%B6%20%D9%88%D8%AA%D8%B4%D9%8A%D9%8A%D8%B9%20%D8%A7%D9%84%D9%85%D9%8A%D8%AA%20%D9%88%D8%A7%D9%84%D8%B5%D9%84%D8%A7%D8%A9%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%AD%D8%B6%D9%88%D8%B1%20%D8%AF%D9%81%D9%86%D9%87
[4] http://www.alhidaaya.com/
[5] https://www.addtoany.com/share#url=http%3A%2F%2Falhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11049&title=01-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kutembelea%20Mgonjwa%20Kufuata%20Jeneza%2C%20Kumswalia%20Maiti%2C%20Kuhudhuria%20Mazishi%20Yake%20na%20Kukaa%20Kwenye%20Kaburi%20Lake%20Kwa%20Muda
[6] https://www.addtoany.com/share#url=http%3A%2F%2Falhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11050&title=02-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Duaa%20za%20Kumuombea%20Mgonjwa
[7] https://www.addtoany.com/share#url=http%3A%2F%2Falhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11051&title=03-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kupendeza%20Kuulizia%20Hali%20ya%20Mgonjwa%20Kupitia%20kwa%20Watu%20Wake
[8] https://www.addtoany.com/share#url=http%3A%2F%2Falhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11052&title=04-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Anachosema%20Mwenye%20Kukata%20Tamaa%20ya%20Maisha%20Yake
[9] https://www.addtoany.com/share#url=http%3A%2F%2Falhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11053&title=05-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kuwausia%20Watu%20wa%20Familia%20Yenye%20Mgonjwa%20na%20Wanaomuangalia%20Kumfanyia%20Wema%20na%20Kumfanyia%20Hisani%20Aliye%20katika%20Uchungu%20wa%20Mauti%20au%20Aliyehukumiwa%20Kunyongwa
[10] https://www.addtoany.com/share#url=http%3A%2F%2Falhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11054&title=06-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kuruhusiwa%20Mgonjwa%20Kusema%3A%20Ninaumwa%20au%20Ninaumwa%20Sana%2C%20Lakini%20ni%20Karaha%20Kusema%20Hivyo%20kwa%20Kukata%20Tamaa
[11] https://www.addtoany.com/share#url=http%3A%2F%2Falhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11055&title=07-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kumlakinia%20Anayekata%20Roho%20kwa%20Kalima%20%22Laa%20ILaaha%20Illa%20Allaah%22
[12] https://www.addtoany.com/share#url=http%3A%2F%2Falhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11056&title=08-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Anayosema%20Baada%20ya%20Kumfumba%20Macho%20Maiti
[13] https://www.addtoany.com/share#url=http%3A%2F%2Falhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11057&title=09-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kinachosemwa%20kwa%20Mtu%20Anayekaribia%20Kufa%20na%20Wanayoambiwa%20Wafiwa
[14] https://www.addtoany.com/share#url=http%3A%2F%2Falhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11058&title=10-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Ruhusa%20ya%20Kulia%20Unapofiwa%20Bila%20Kuomboleza
[15] https://www.addtoany.com/share#url=http%3A%2F%2Falhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11059&title=11-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kuhifadhi%20Aibu%20Zinazoonekana%20kwa%20Maiti
[16] https://www.addtoany.com/share#url=http%3A%2F%2Falhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11060&title=12-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kumswalia%20Maiti%20na%20Kufuata%20Jeneza%20na%20Kuhudhuria%20Kuzikwa%20Kwake%20na%20Karaha%20kwa%20Wanawake%20Kufuata%20Jeneza
[17] https://www.addtoany.com/share#url=http%3A%2F%2Falhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11061&title=13-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kupenda%20Kuwa%20na%20Jamaa%20Kubwa%20Katika%20Swalaah%20ya%20Jeneza%20na%20Kuzifanya%20Safu%20Zake%20Tatu%20na%20Zaidi
[18] https://www.addtoany.com/share#url=http%3A%2F%2Falhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11062&title=14-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kisomo%20Katika%20Swalaah%20ya%20Jeneza
[19] https://www.addtoany.com/share#url=http%3A%2F%2Falhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11064&title=15-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kuharakisha%20Jeneza
[20] https://www.addtoany.com/share#url=http%3A%2F%2Falhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11065&title=16-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kuharakisha%20Kumlipia%20Deni%20Maiti%20na%20Kuharakisha%20Kumuandaa%20Isipokuwa%20Mauti%20Yake%20Yathibitike
[21] https://www.addtoany.com/share#url=http%3A%2F%2Falhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11066&title=17-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Mawaidha%20Kwenye%20Kaburi
[22] https://www.addtoany.com/share#url=http%3A%2F%2Falhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11067&title=18-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kumuombea%20Dua%20Maiti%20Baada%20ya%20Kuzikwa%20na%20Kukaa%20Kwenye%20Kaburi%20Lake%20kwa%20Muda
[23] https://www.addtoany.com/share#url=http%3A%2F%2Falhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11068&title=19-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kumtolea%20Swadaqah%20Maiti%20na%20Kumuombea%20Dua
[24] https://www.addtoany.com/share#url=http%3A%2F%2Falhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11069&title=20-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Maiti%20Anayesifiwa%20na%20Watu
[25] https://www.addtoany.com/share#url=http%3A%2F%2Falhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11070&title=21-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Ubora%20wa%20Kufiwa%20na%20Watoto%20Wachanga
[26] https://www.addtoany.com/share#url=http%3A%2F%2Falhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11071&title=22-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kulia%20Kuwa%20na%20Hofu%20Wakati%20wa%20Kupita%20Kwenye%20Makaburi%20ya%20Madhalimu%2C%20Kunyenyekea%20kwa%20Allaah%20na%20Onyo%20kwa%20Kughafilika%20na%20Hilo