كِتابُ اللِّباسِ وَالزِّينَةِ وَأَحْكامِ النَّظَر
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia
اللِّبَاسُ وَالزِّيْنَةُ للرِّجَالِ
Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume
Abu Maalik Kamaal Bin As-Sayyid Saalim
Imetarjumiwa na 'Abdullaah Mu'aawiyah (Abu Baasim)
Alhidaaya.com
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ وَأَحْكَامُ النَّظَرِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia
اللِّبَاسُ وَالزِّيْنَةُ للرِّجَالِ
Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume
Alhidaaya.com [3]
001-Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume: Wajibu Wa Kusitiri Uchi:
Maana ya uchi katika lugha, ni kila kasoro inayohofiwa kufichuka kutokana na mwanya au mvujo. Na uchi ni sehemu ya kufichwa vizuri isiweze kuonekana kirahisi, na uchi wa mwanaume na mwanamke ni tupu zao mbili. [Lisaanul ‘Arab 4/416].
Ama katika istilahi, uchi ni kila ambacho Allaah Ta’aalaa Ameharamisha kukionyesha mbele ya mtu ambaye si halali kwake kukiangalia. [Nihaayatul Muhtaaj (2/5) na Tafsiyrul Qurtubiy (7/182)].
Sharia imewajibisha kuhifadhi na kusitiri nyuchi zisionekane na mtu ambaye si halali kwake kuziona.
1- Allaah Ta’aalaa Amesema:
"يَا بَنِي آدَمَ خُذُوا زِينَتَكُمْ عِندَ كُلِّ مَسْجِدٍ وَكُلُوا وَاشْرَبُوا وَلَا تُسْرِفُوا ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُسْرِفِينَ ﴿٣١﴾"
31. Enyi wana wa Aadam! Chukueni mapambo yenu katika kila Masjid. Na kuleni na kunyweni na wala msifanye israfu. Hakika Yeye (Allaah) Hapendi wanaofanya israfu. [Al-A’araaf 31].
Waarabu wakati wa enzi ya ujahili, walikuwa wakitufu Al-Ka’abah uchi, mpaka Allaah Alipomtuma Muhammad (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Aayah hii ikateremka. Mpiga mbiu wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) akatangaza na kusema:
"أَنْ لَا يَطُوفَ بِالْبَيْتِ عُرْيَان"
“Asitufu yeyote Nyumba akiwa uchi”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (369) na Muslim (1347)].
Al-Qurtubiy (Rahimahul Laah) amesema: “Agizo katika Aayah hii linawahusu watu wote ingawa mlengwa hapo ni wale waliokuwa wakitufu Nyumba uchi miongoni mwa Waarabu. Agizo hilo ni jumuishi kwa kila Msikiti wanaposwalia watu, kwa kuwa linalozingatiwa ni ujumuishi kuwahusisha wote, na si sababu kutokana na watu maalum”. [Al-Jaami’u Liahkaamil Qur-aan (7/189)].
2- Allaah Ta’aalaa Amewakataza watu kufunua nyuchi zao na Akaliita hilo fitna. Amesema Ta’aalaa:
"يَا بَنِي آدَمَ لَا يَفْتِنَنَّكُمُ الشَّيْطَانُ كَمَا أَخْرَجَ أَبَوَيْكُم مِّنَ الْجَنَّةِ يَنزِعُ عَنْهُمَا لِبَاسَهُمَا لِيُرِيَهُمَا سَوْآتِهِمَا"
“Enyi wana wa Aadam! Asikufitinisheni kabisa shaytwaan kama alivyowatoa wazazi wenu katika Jannah huku akiwavua nguo zao ili awaonyeshe sehemu zao za siri”. [Al-A’araaf: (28)].
3- Kutokana na umuhimu wa kusitiri uchi na hadhi yake katika Uislamu, Allaah Ameliambatanisha hili sambamba na taqwa pale Aliposema:
“يَا بَنِي آدَمَ قَدْ أَنزَلْنَا عَلَيْكُمْ لِبَاسًا يُوَارِي سَوْآتِكُمْ وَرِيشًا ۖ وَلِبَاسُ التَّقْوَىٰ ذَٰلِكَ خَيْرٌ"
“Enyi wana wa Aadam! Kwa yakini Tumekuteremshieni libasi inayositiri tupu zenu (nguo), na libasi ya mapambo. Na libasi ya taqwa ndiyo bora zaidi”. [Al-A’araaf (26)].
4- Toka kwa Bahz bin Hakiym toka kwa baba yake toka kwa babu yake, amesema, nilisema:
"يَا رَسُولَ اللَّهِ ، عَوْرَاتُنَا مَا نَأْتِي مِنْهَا وَمَا نَذَرُ؟ قَالَ: "احْفَظْ عَوْرَتَكَ إِلاَّ مِنْ زَوْجَتِكَ أَوْ مِمَّا مَلَكَتْ يَمِينُكَ" . فَقَالَ: الرَّجُلُ يَكُونُ مَعَ الرَّجُلِ؟ قَالَ: "إِنِ اسْتَطَعْتَ أَنْ لاَ يَرَاهَا أَحَدٌ فَافْعَلْ"
“Ee Rasuli wa Allaah! Kuhusu nyuchi zetu, ni zipi ambazo tunaweza kuzifunika, na ni zipi ambazo tunaweza kuziachia? Akasema: Uhifadhi uchi wako isipokuwa kwa mkewe au watumwa wako. Nikasema: Ee Rasuli wa Allaah! Vipi mwanaume akiwa na mwanaume mwenzake? Akasema: Ukiweza asiuone yeyote, basi fanya. Nikasema: Na mwanamume akiwa peke yake? Akasema: Allaah Ana haki zaidi ya kuonewa haya kuliko watu”. [Hadiyth Hasan. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (7/40), At-Tirmidhiy (2769) na Ibn Maajah (1920)].
5- Abu Sa’iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaah ‘anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"لَا يَنْظُرُ الرَّجُلُ إِلَى عَوْرَةِ الرَّجُلِ وَلَا الْمَرْأَةُ إِلَى عَوْرَةِ الْمَرْأَةِ ، وَلَا يُفْضِي الرَّجُلُ إِلَى الرَّجُلِ فِي ثَوْبٍ وَاحِدٍ وَلَا تُفْضِي الْمَرْأَةُ إِلَى الْمَرْأَةِ فِي ثَوْبٍ وَاحِدٍ "
“Mwanaume haruhusiwi kuangalia uchi wa mwanaume mwenzake, wala mwanamke kuangalia uchi wa mwanamke mwenzake. Na mwanaume asigusane ngozi kwa ngozi na mwanaume mwenzake ndani ya nguo moja, na mwanamke pia asigusane ngozi kwa ngozi na mwanamke mwenzake ndani ya nguo moja”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (338), At-Tirmidhiy (2793) na Abu Daawuwd (4018)].
6- Ni pamoja na dalili nyingine lukuki kuhusiana na wajibu wa kuinamisha chini macho, kuharamisha kuangalia uchi, wajibu wa kupiga hodi na mfano wa hayo ambayo yatakuja kufafanuliwa katika sehemu husika In Shaa Allaah.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ وَأَحْكَامُ النَّظَرِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia
اللِّبَاسُ وَالزِّيْنَةُ للرِّجَالِ
Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume
Alhidaaya.com [3]
002- Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume: Mpaka Wa Uchi Wa Mwanaume:
Hakuna makhitilafiano yoyote kati ya ‘Ulamaa kuhusiana na wajibu wa kuusitiri uchi ili usionekane na watu isipokuwa ule uliovuliwa na dalili. Lakini, ni upi mpaka wa uchi kwa upande wa mwanaume?
‘Ulamaa katika hili wana kauli nyingi ambazo zinaweza kuchujwa na kuwa kauli mbili tu:
Ya kwanza: Uchi wa mwanaume ni kati ya kitovu na magoti.
Wenye kauli hii ni madhehebu ya Jumhuwr na wengineo. Lakini pia wanavutana katika kuingia kitovu na magoti ndani ya duara la uchi. Dalili zao ni:
1- Hadiyth ambayo Al-Bukhaariy ameifanya “Mu’allaq” -ikiwa na anuani “Kuuguza”- toka kwa Ibn ‘Abbaas, Jarhad, na Muhammad bin Jahsh toka kwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"الفَخْذُ عَوْرَةٌ"
“Paja ni uchi”. [Hadiyth Mu’allaq. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy].
2- ‘Aliyy (Radhwiya Allaah ‘anhu): Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliniambia:
"لَا تُبْرِزْ فَخِذَكَ ، وَلَا تَنْظُرْ إِلَى فَخِذِ حَيٍّ وَلَا مَيِّتٍ"
“Usiliwache wazi paja lako, na wala usiangalie paja la aliye hai wala la maiti”.
Lakini Hadiyth hii ni Dhwa’iyf sana. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (3140, 4015), Ibn Maajah (2/228) na Al-Bayhaqiy (2/228).
3- Yaliyosimuliwa toka kwa ‘Amri bin Shu’ayb, toka kwa baba yake, toka kwa babu yake, kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"فَإِنَّ مَا تَحْتَ السُّرَّةِ إلى رُكْبَتِهِ مِنَ العَوْرَةِ"
“Kwani sehemu iliyo chini ya kitovu hadi kwenye goti lake ni uchi”. [Al-Albaaniy ameihasinisha. Imekharijiwa na Ahmad (2/187) na Ad-Daaraqutwniy (1/230). Angalia Al-Irwaa (271)].
4- Al-Musuwr bin Makhramah (Radhwiya Allaah ‘anhu) amesema:
"أَقْبَلْتُ بِحَجَرٍ ثَقِيلٍ أَحْمِلُهُ وَعَلَىَّ إِزَارٌ خَفِيفٌ ، فَانْحَلَّ إِزَارِي وَمَعِيَ الْحَجَرُ لَمْ أَسْتَطِعْ أَنْ أَضَعَهُ حَتَّى بَلَغْتُ بِهِ إِلَى مَوْضِعِهِ ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ : "ارْجِعْ إِلَى ثَوْبِكَ فَخُذْهُ وَلاَ تَمْشُوا عُرَاةً"
“Nilikakamia kulibeba jiwe zito nikiwa nimejifunga chini kipande hafifu cha shuka (izari). Mara kipande hicho kikafunguka na kudondoka na jiwe nimeshalibeba, na sikuweza kulitua, nikaenda nalo hivyo hivyo mpaka nikalifikisha sehemu yake husika. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaniambia: “Rejea ukaichukue nguo yako, na wala msitembee uchi”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (341) na Abu Daawuwd (4016)].
Kauli ya pili: Uchi ni nyeti ya mbele na ya nyuma tu.
Ni riwaayah nyingine ya Ahmad, na riwaayah katika madhehebu ya Maalik, na ni kauli ya Adh-Dhwaahiriyyah. Wametoa dalili kwamba paja si uchi kwa haya yafuatayo:
1- Hadiyth ya Anas bin Maalik (Radhwiya Allaah ‘anhu):
"أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ غَزَا خَيْبَرَ ، فَصَلَّيْنَا عِنْدَهَا صَلاَةَ الْغَدَاةِ بِغَلَسٍ ، فَرَكِبَ نَبِيُّ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَرَكِبَ أَبُو طَلْحَةَ وَأَنَا رَدِيفُ أَبِي طَلْحَةَ ، فَأَجْرَى نَبِيُّ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي زُقَاقِ خَيْبَرَ ، وَإِنَّ رُكْبَتِي لَتَمَسُّ فَخِذَ نَبِيِّ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ، ثُمَّ حَسرَ الإِزَارُ عَنْ فَخِذِه حَتَّى إِنِّي أَنْظُرُ إِلَى فَخِذِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ"
“Kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliivamia Khaybar. Tukaswali hapo Swala ya Alfajiri mwanzo wa wakati giza likiwa bado limetanda. Halafu Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akampanda mnyama wake, na Abu Twalha naye akampanda wake, nami akanipakia nyuma. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwendesha kwa kasi mnyama wake kwenye vichochoro vya Khaybar. Goti langu lilikuwa likigusa paja la Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Halafu izari yake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ilishuka kidogo ikaliwacha wazi paja lake kiasi cha mimi kuweza kuliona”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (371) na Muslim (1365)].
Ibn Hazm amesema: “Imekuwa wazi bayana kwa hili kwamba paja si uchi. Na kama lingekuwa ni uchi, basi Allaah ‘Azza wa Jalla Asingeliwacha likamfunuka Rasuli Wake aliyetwaharishwa na kulindwa kutokana na watu katika Unabii na Urasuli wake, na wala Asingelimfanya Anas wala mwingine yeyote aweze kuliona. Na Yeye Allaah Alimlinda uchi wake usionekane tokea utotoni na kabla ya kupewa Utume”. [Al-Muhallaa (3/272)].
Lakini Ibn Hazm anajibiwa akiambiwa kwamba hili lina uwezekaniko wa kuwa izari ilishuka yenyewe, na si kwa kitendo cha yeye kuishusha wala kukusudia kufanya hivyo. Na hili linathibitishwa na riwaayah ya “Swahiyhayn” isemayo:
"فَانْحَسَرَ الإِزَارُ"
“Izari ikashuka”.
2- Hadiyth ya ‘Aaishah:
"أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ جَالِسًا كَاشِفًا عَنْ فَخِذِهِ ، فَاسْتَأْذَنَ أَبُو بَكْرٍ فَأَذِنَ لَهُ وَهُوَ عَلَى حَالِهِ ، ثُمَّ اسْتَأْذَنَ عُمَرُفَأَذِنَ لَهُ وَهُوَ عَلَى حَالِهِ ، ثُمَّ اسْتَأْذَنَ عُثْمَانُ فَجَلَسَ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم وَسَوَّى ثِيَابَهُ ، فَلَمَّا خَرَجَ قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللهِ، دَخَلَ أَبُو بَكْرٍ فَلَمْ تَهَشَّ وَلَمْ تُبَالِهِ، ثُمَّ دَخَلَ عُمَرُ فَلَمْ تَهَشَّ وَلَمْ تُبَالِهِ، ثُمَّ دَخَلَ عُثْمَانُ فَجَلَسْتَ وَسَوَّيْتَ ثِيَابَكَ؟ قَالَ: أَلاَ أَسْتَحِي مِنْ رَجُلٍ تَسْتَحِي مِنْهُ الْمَلاَئِكَةُ؟"
“Kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa ameketi huku akiwa amelifunua paja lake. Abu Bakr akapiga hodi, akamruhusu kuingia akiwa hivyo hivyo (akazungumza naye akatoka). Kisha ‘Umar naye akapiga hodi, akamruhusu kuingia akiwa hivyo hivyo (akazungumza naye akatoka). Halafu ‘Uthmaan akapiga hodi, na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaketi sawa, akaiweka vizuri nguo yake. Alipoondoka nilimuuliza: Ee Rasuli wa Allaah! Abu Bakr ameingia, ukabaki ulivyokuwa wala hukujali, kisha ‘Umar akaingia, ukabaki hivyo hivyo, lakini ‘Uthmaan alipoingia, uliketi sawa na kuiweka vizuri nguo yako. Akasema: “Iwaje nisimwonee haya mtu ambaye Malaika wanamwonea haya?!” [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (2401)].
3- Jaabir amesema:
"احْتَجَمَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَلَى وَرِكِهِ مِنْ وَثْءٍ كَانَ بِهِ"
“Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alifanya hijama sehemu ya juu ya paja lake kutokana na vilio la damu lililompata”. [Hadiyth Dhwa’iyf. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (3763)].
Hili linajibiwa: Kwamba kufunua Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) sehemu ya juu ya paja lake kwa mfanyaji hijama, haionyeshi kwamba si paja si uchi, kwa kuwa alilifunua kutokana na udharura wa kupatiwa tiba, na hili linajuzu kwa makubaliano ya ‘Ulamaa wote.
Kauli yenye nguvu:
Linaloonekana ni kuwa dalili za Jumhuwr (ambazo ni za maneno ya Rasuli) zinazatitiana zenyewe kwa zenyewe na zinapanda kufikia ngazi ya kuwa hoja thibitishi. Na kwa muktadha huu, dalili hizi zinapewa kipaumbele na kutangulizwa kabla ya dalili za kundi la pili, kwa kuwa dalili zao ni matukio ya kibinafsi yaliyomhusu Nabiy pekee na wala hayahusishwi na watu wote. Na katika kesi kama hii, kauli ya Rasuli hutangulizwa kabla ya kitendo chake.
Na kama itaulizwa: Kwa nini mmepita mrengo wa “tarjiyh” (kuzipa uzito dalili kadhaa zinazoonekana kuwa na nguvu zaidi na kuziacha zingine) na wala hamkufanya “jam-‘u” (kuzikusanya dalili zote na kuzifanyia kazi), pamoja na kwamba kuzitumia dalili zote zilizopo ni bora zaidi kuliko kuzitelekeza zingine?
Jibu ni: Kwamba paja, ima liwe uchi au lisiwe, hakuna namna ya tatu, na kwa hivyo imebidi kufanya “tarjiyh”. Na kwa picha hii, inajulikana kwamba Hadiyth alizozikusanya Ibn Al-Qayyim katika Kitabu cha “Tahdhiyb As-Sunan” na Al-Albaaniy (Rahimahul Laahu) akapendezwa na hilo katika “Al-Irwaa” (1/301), Hadiyth ambazo zinagusia kwamba uchi ni wa aina mbili: Uchi mwepesi na uchi mzito. Mzito ni tupu mbili; ya mbele na nyuma, na mwepesi ni mapaja mawili. Na hakuna makinzano baina ya amri ya kuinamisha macho chini kutoyaangalia mapaja mawili kwa kuwa kwake ni uchi, na kati ya kuyaacha wazi kwa kuwa kwake ni uchi mwepesi. Hili halina mwelekeo . Na Allaah Ndiye Ajuaye zaidi.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ وَأَحْكَامُ النَّظَرِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia
اللِّبَاسُ وَالزِّيْنَةُ للرِّجَالِ
Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume
Alhidaaya.com [3]
003- Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume: Vivazi Vinavyoruhusiwa Na Vinavyopendeza Zaidi Kuvaliwa Na Wanaume:
· Nguo Nzuri Zaidi Ni Nyeupe
1- Samurah: Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"الْبَسُوا مِنْ ثِيَابِكُمُ الْبَيَاضَ ، فَإِنَّهَا أَطْهَرُ وَأَطْيَبُ ، وَكَفِّنُوا فِيهَا مَوْتَاكُمْ"
“Vaeni katika nguo zenu zilizo nyeupe, kwani ndizo zenye utwahara zaidi na zilizo nzuri zaidi, na wakafinieni kwazo maiti wenu”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na An-Nasaaiy (4/8-34), Ibn Maajah (3567) na Ahmad (5/12,20)].
Na katika riwaayah:
"عَلَيْكُمْ بِالْبَيَاضِ مِنَ الثِّيَابِ ، فَلْيَلْبَسْهَا أَحْيَاؤُكُمْ وَكَفِّنُوا فِيهَا مَوْتَاكُمْ ، فَإِنَّهَا مِنْ خَيْرِ ثِيَابِكُمْ"
“Shikamaneni na nguo nyeupe, wazivae walio hai wenu na wakafinieni kwazo maiti wenu, kwani hizo ndizo nguo zenu zilizo bora zaidi”.
Ash-Shawkaaniy (Rahimahul Laah) amesema: “Ama kuwa kwake zinapendeza zaidi, hilo liko wazi. Ama kuwa kwake ni twaharifu zaidi, ni kwa kuwa zikipatwa na chochote hata kiwe kidogo, basi kitaonekana haraka na nguo itasafishwa, na kikiwa ni najisi, nguo itatwaharishwa. Na amri tajwa katika Hadiyth si ya wajibu kutokana na yaliyothibiti toka kwake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba alivaa nguo za rangi nyingine. Lakini pia, Maswahaba wengi walivaa nguo zisizo nyeupe, na Rasuli pia aliwakubalia Maswahaba wengi kuvaa nguo za rangi tofauti”. [Naylul Awtwaar kwa marekebisho madogo].
2- Sa’ad kasema:
"رَأَيْتُ بِشِمَالِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَبِيَمِينِهِ رَجُلَيْنِ عَلَيْهِمَا ثِيَابٌ بِيضٌ يَوْمَ أُحُدٍ، مَا رَأَيْتُهُمَا قَبْلُ وَلاَ بَعْدُ"
“Niliwaona kushotoni na kuliani mwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) watu wawili wenye nguo nyeupe Siku ya Uhud. Sikuwahi kuwaona kabla (ya Siku hiyo) wala baada yake”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5826)].
3- Abu Dharri amesema:
"أَتَيْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَعَلَيْهِ ثَوْبٌ أَبْيَضُ وَهُوَ نَائِمٌ"
“Nilimwendea Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam), nikamkuta amelala akiwa amevaa nguo nyeupe”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5827)].
· Hakuna Ubaya Kuvaa Nguo Isiyo Nyeupe
1- Al-Baraa kasema:
" كَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مَرْبُوعًا، وَقَدْ رَأَيْتُهُ فِي حُلَّةٍ حَمْرَاءَ مَا رَأَيْتُ شَيْئًا أَحْسَنَ مِنْهُ"
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa na kimo cha wastani. Niliwahi kumwona akiwa amevaa vazi jekundu la juu na chini, sijapata kuona kitu kizuri zaidi kuliko yeye. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5848). Ina Hadiyth mwenza ya Jaabir iliyoko kwa At-Tirmidhiy (2811)].
2- ‘Aaishah kasema:
"خَرَجَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ذَاتَ غَدَاةٍ وَعَلَيْهِ مِرْطٌ مُرَحَّلٌ مِنْ شَعَرٍ أَسْوَدَ "
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitoka asubuhi moja akiwa amevaa nguo ya chini (ya Yemen) ya sufi nyeusi yenye michoro ya kiti cha kukalia ngamia”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (2081), At-Tirmidhiy (2813) na Abu Daawuwd (402)].
3- Qataadah amesema:
"قُلْنَا لأَنَسٍ: أَىُّ اللِّبَاسِ كَانَ أَحَبَّ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم؟ قَالَ: "الْحِبَرَةُ"
“Tulimuuliza Anas: Ni kivazi gani alichokuwa akikipenda zaidi Rasuli wa Allaah? Akasema: Ni “Alhibarah”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5812) na Muslim (2081)].
“Alhibarah” ni vazi lenye marembo na mistari, hutengenezwa kwa kitani au sufi.
4- Abu Rimthata amesema:
"رَأَيْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَخْطُبُ وَعَلَيْهِ بُرْدَانِ أَخْضَرَانِ"
“Nilimwona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anakhutubu akiwa amevaa vishali viwili vya kijani”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na At-Tirmidhiy (2813), Abu Daawuwd (4206), An-Nasaaiy (8/204) na Ahmad (2/227)].
5- Vazi la kijani litavaliwa zaidi na watu wa Peponi. Allaah Ta’aalaa Amesema:
"عَالِيَهُمْ ثِيَابُ سُندُسٍ خُضْر"
“Watavaa nguo za hariri nyororo za kijani”. [Al-Insaan: 21].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ وَأَحْكَامُ النَّظَرِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia
اللِّبَاسُ وَالزِّيْنَةُ للرِّجَالِ
Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume
Alhidaaya.com [3]
004- Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume: Vivazi Vinavyoruhusiwa Na Vinavyopendeza Zaidi Kuvaliwa Na Wanaume: Kanzu Ndio Vazi Bora Zaidi
Ummu Salamah amesema:
"كَانَ أَحَبُّ الثِّيَابِ إِلَى رَسُوْلِ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ القُمُصُ"
“Vazi alilokuwa akilipenda zaidi Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni kanzu”. [Hadiyth Hasan. Imekharijiwa na At-Tirmidhiy (1762, 1763), Abu Daawuwd (4025), An-Nasaaiy katika Al-Kubraa (9668), Abu Ya’alaa (7014) na Al-Bayhaqiy (2/239)].
· Suruali Inaruhusiwa Kuvaa
Kuvaa suruali kunaruhusiwa kwa makubaliano ya ‘Ulamaa wote. Na asili ya kuruhusiwa ni Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas kwamba Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"مَنْ لَمْ يَجِدْ إِزَارًا فَلْيَلْبَسْ سَرَاوِيلَ، وَمَنْ لَمْ يَجِدْ نَعْلَيْنِ فَلْيَلْبَسْ خُفَّيْنِ"
“Asiyepata nguo ya kujifunga chini (izari), basi avae suruali, na asiyepata viatu viwili, basi avae khufu mbili”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (1841, 5804), An-Nasaaiy (2672) na Ibn Maajah (2931)].
Suruali inayovaliwa inatakikana iwe pana isiyochora uchi, na kama si pana, basi ni lazima ivaliwe juu yake kanzu ndefu inayositiri uchi. Abu Umaamah amesema:
"قُلْنَا : يَا رَسُوْلَ اللهِ، إِنَّ أَهْلَ الكِتَابِ يَتَسَرْوَلُوْنَ ولاَ يَأْتَزِرُوْنَ، فَقَالَ رَسُوْلُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ : "تَسَرْوَلُوْا واتَّزِرُوْا"
“Tulisema: Ee Rasuli wa Allaah! Mayahudi na Manaswara wanavaa suruali na hawavai vikoi (izari). Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: Vaeni suruali, vaeni vikoi”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Ahmad (5/264) na At-Twabaraaniy (5/121)].
Angalizo:
Baadhi ya ‘Ulamaa wanaoheshimika katika enzi yetu ya leo, wameegemea mrengo wa kusema kuwa kuvaa suruali na kuswalia nayo ni karaha ya uharamu. Sababu wanasema ni kujifananisha na makafiri!! Wamesahau kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameshaeleza ni ipi nguo ya kikafiri. Hii ni pale mtu mmoja alipomjia akiwa amevaa nguo ya rangi ya zafarani akamwambia:
"هَذِهِ مِنْ ثِيَابِ الْكُفَّارِ فَلاَ تَلْبَسْهَا"
“Hii ni katika nguo za makafiri, usizivae”. [Hadiyth Swahiyh. Takhriyj yake iko njiani].
Ninasema: “Kuvaa suruali hakuwapambanui tena makafiri kuwa ndio kivazi chao na alama yao mpaka kuharamishwe kwa hoja ya kujifananisha nao. Bali linaloshurutishwa ni hilo tulilolieleza nyuma kidogo kuwa iwe pana isiyochora uchi. Lakini pamoja na hayo, kuacha kuivaa na kuvaa kanzu ni bora zaidi. Allaah Ndiye Mjuzi zaidi”.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ وَأَحْكَامُ النَّظَرِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia
اللِّبَاسُ وَالزِّيْنَةُ للرِّجَالِ
Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume
Alhidaaya.com [3]
005- Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume: Vivazi Vinavyoruhusiwa Na Vinavyopendeza Zaidi Kuvaliwa Na Wanaume: Inapendeza Kuvaa Kilemba
Toka kwa Jaabir:
" أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ دَخَلَ مَكَّةَ يَوْمَ الفَتْحِ وَعَلَيْهِ عِمَامَةٌ سَوْداءُ"
“Kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliingia Makkah Siku ya Ukombozi akiwa amevalia kilemba cheusi”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (1358), At-Tirmidhiy (1735), An-Nasaaiy, (2869) Abu Daawuwd (4076) na Ibn Maajah (2822)].
Inakuwa vizuri zaidi kilemba kiteremke kati ya mabega mawili. Na hii ni kwa Hadiyth ya ‘Amri bin Hurayth aliyesema:
"كَأَنِّيْ أَنْظُرُ إِلى رَسُوْلِ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَلَى المِنْبَرِ وَعَلَيْهِ عِمَامَةٌ سَوْدَاءٌ قَدْ أَرْخَى طَرَفَيْهَا بَيْنَ الكَتِفَيْنِ"
“Kana kwamba mimi namwangalia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa amevaa kilemba cheusi, huku amening’iniza ncha zake mbili baina ya mabega yake mawili”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (1359) na Ibn Maajah (2821)].
Ibn ‘Umar amesema:
"كَانَ رَسُوْلُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا اعْتَمَّ سَدلَ عِمَامَتَهُ بَيْنَ كَتِفَيْهِ"
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapopiga kilemba, hukiachilia kilemba chake baina ya mabega yake mawili”. [Hadiyth Hasan Lighayrih. Imekharijiwa na At-Tirmidhiy (1736), Ibn Hibaan (6397) na At-Twabaraaniy (12/379)].
An-Nawawiy kasema: “Inajuzu kuvaa kilemba kwa kuzitupia ncha zake mbili au kwa kutozitupia, na wala hakuna ukaraha wa kimoja kati ya viwili, na hakuna tamshi lolote sahihi lililokataza kutotupia. Ama kuzitupia kwa kuvuka sana mpaka, hilo litakuwa ni haramu kwa wenye kujiona, na kwa wengine itakuwa ni makruhu”. [Al-Majmuw’u (4/457)]
.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ وَأَحْكَامُ النَّظَرِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia
اللِّبَاسُ وَالزِّيْنَةُ للرِّجَالِ
Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume
Alhidaaya.com [3]
006- Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume: Vivazi Vilivyokatazwa Kwa Wanaume Kuvivaa: Kuvaa Mavazi Mahsusi Kwa Wanawake:
Jumhuwr ya ‘Ulamaa wanasema kwamba ni haramu mwanaume kujifananisha na mwanamke katika mavazi ambayo ni mahsusi kwa wanawake na kinyume chake. Kuna Hadiyth kadhaa zilizothibiti ambazo zinaharamisha kiujumla kila jinsia kujifananisha na nyingine katika mambo maalum yanayohusiana na kila upande. Na hii inajumuisha kujifananisha katika mavazi, mapambo, uzungumzaji, utembeaji na mfano wa hayo. Kati ya Hadiyth hizo ni:
1- Ibn ‘Abbaas amesema:
"لَعَنَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الْمُتَشَبِّهِينَ مِنَ الرِّجَالِ ِبِالنِّسَاءِ ، والْمُتَشَبِّهَاتِ مِنَ النِّسَاءِ بِالرِّجَالِ"
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amewalaani wanaume wanaojifananisha na wanawake, na wanawake wanaojifananisha na wanaume”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5885), At-Tirmidhiy (2784), Abu Daawuwd (4097) na Ibn Maajah (1904)].
2- Abu Hurayrah:
" أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لَعَنَ الرَّجُلَ يَلْبَسُ لِبْسَ الْمَرْأَةِ ، وَالْمَرْأَةَ تَلْبَسُ لِبْسَ الرَّجُلِ"
“Kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amemlaani mwanaume anayevaa kivazi cha kike, na mwanamke anayevaa kivazi cha kiume”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (4098) na Ahmad (2/325)].
Na laana haiwi isipokuwa kwa jambo lililoharamishwa, na hii ni kauli ya Jumhuwr.
Ash-Shaafi’iy amesema: “Haikatazwi, bali ni makruhu!! Lakini Hadiyth tajwa zinamjibu kauli yake hii. Na kwa ajili hiyo, An-Nawawiy (Rahimahul Laah) amesema: “Lililo sawa ni kwamba wanawake kujifananisha na wanaume na kinyume chake ni haramu kutokana na Hadiyth Swahiyh”. [Al-Majmuw’u (4/335)].
· Kushusha Nguo Chini Ya Vifundo Vya Miguu Na Kuiburura Kwa Kiburi Ni Haramu
1- Ibn ‘Umar: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"لَا يَنْظُرُ اَللَّهُ إِلَى مَنْ جَرَّ ثَوْبَهُ خُيَلَاءَ"
“Allaah Hamwangalii mwenye kuiburura nguo yake kwa kiburi na kujiona”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5784) na Muslim (2085)].
Abu Hurayrah: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"لَا يَنْظُرُ اَللَّهُ يَوْمَ القِيَامَةِ إِلَى مَنْ جَرَّ إِزَارَهُ بَطَرًا"
“Allaah Hatomwangalia Siku ya Qiyaamah mwenye kuburuza kikoi chake kwa kiburi”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5788) na Muslim (2087)].
Abu Hurayrah (pia): Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"بَيْنَمَا رَجُلٌ يَمْشِي فِي حُلَّةٍ، تُعْجِبُهُ نَفْسُهُ مُرَجِّلٌ جُمَّتَهُ، إِذْ خَسَفَ اللَّهُ بِهِ، فَهُوَ يَتَجَلَّلُ إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ"
“Katika wakati ambapo mtu mmoja alikuwa anatembea akiwa amevalia maridadi kabisa, akijiona yeye ndiye yeye hakuna zaidi yake, amezichana vizuri kabisa nywele zake, mara ghafla Allaah Akamzamisha chini. Naye anadidimia na kuendelea kuzama mpaka Siku ya Qiyaamah”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5789) na Muslim (2088)].
Hadiyth hizi zote pamoja na nyinginezo, zinaashiria uharamu wa kuburuza nguo kwa kiburi na kujiona, na kwamba mwenendo huo ni katika madhambi makubwa.
· Hukmu Ya Kuteremsha Nguo Chini Ya Vifundo Vya Miguu Bila Kukusudia Kiburi:
Abu Hurayrah: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"مَا أَسْفَلَ مِنَ الْكَعْبَيْنِ مِنَ الْإِزَارِ فِي النَّارِ"
“Sehemu ya kikoi (nguo) iliyo chini ya vifundo viwili vya miguu, itaadhibiwa motoni”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5787), An-Nasaaiy (5331), Abu Daawuwd (4093) na Ibn Maajah (3573)].
Al-Khattwaabiy amesema: “(Rasuli) anamaanisha hapa kwamba sehemu ambayo inafikiwa na kikoi (nguo) baada ya vifundo viwili vya miguu, ndiyo ambayo itakuwa kwenye moto. Nguo imefanywa kinaya kwa mwili wa mvaaji. Na maana yake ni kuwa sehemu hiyo ya mguu iliyo chini ya vifundo viwili ndiyo itakayounguzwa motoni.. ”. [Fat-hul Baariy (10/257)].
Ibn ‘Umar: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"مَنْ جَرَّ ثَوْبَهُ خُيَلَاءَ لَمْ يَنْظُرِ اللَّهُ إِلَيْهِ يَوْمَ الْقِيَامَة"، فَقَالَ أَبُو بَكْرٍ : يَا رَسُولَ اللَّهِ ، إِنَّ أَحَدَ شِقَّىْ إِزَارِي يَسْتَرْخِي، إِلاَّ أَنْ أَتَعَاهَدَ ذَلِكَ مِنْهُ، فَقَالَ: "إِنَّكَ لَسْتَ مِمَّنْ يَفْعَلُ ذلِكَ خُيَلَاء"َ
“Mwenye kuiburuza nguo yake kwa kiburi na kujiona, Allaah Hatomtazama Siku ya Qiyaamah”. Abu Bakr akasema: Ee Rasuli wa Allaah, upande mmoja wa izari yangu unateremka chini, nami nalichunga hilo kwa kuupandisha. Akasema: “Lakini wewe si katika ambaye anafanya hivyo kwa kiburi na kujiona”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5784), An-Nasaaiy (3553) na Abu Daawuwd (4085)].
Kundi la baadhi ya ‘Ulamaa limeshika msimamo wa kuharamisha kuteremsha nguo chini ya mafundo mawili ya mguu ikiwa ni kwa kiburi na kujiona, na kama itakuwa kwa jingine, basi ni makruhu. Wanasema kwamba Hadiyth zilizokuja kuhusiana na katazo la kushusha nguo chini ya vifundo ni “Mutwlaq” (yaani hazikuainisha kama ni kwa kibr au la), hivyo basi ni lazima ziainishwe kwa kufungamanishwa na kuteremsha nguo kwa kiburi na kujiona tu!! Hivi ndivyo Ash-Shaafi’iy alivyoeleza juu ya makundi. [Sharhu Muslim cha An-Nawawiy (14/62)].
Lakini wengine wameshika mrengo wa kwamba haijuzu kwa mwanaume kuishusha nguo yake chini ya vifundo, halafu adai na kusema: “Mimi siibururi kwa ajili ya kiburi na kujiona, mimi sina sifa hiyo”. Madai haya hayakubaliki, bali hata kurefusha tu nguo yake ikagusa chini kunaonyesha kwamba ana kibr”. [Fat-hul Baariy (10/263)].
Ninasema: “Mrengo huu wa mwisho una nguvu zaidi, nao unatiliwa nguvu na Hadiyth ya Jaabir bin Sulaym At-Twawiyl ambapo Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"وَارْفَعْ إِزَارَكَ إِلَى نِصْفِ السَّاقِ ، فَإِنْ أَبَيْتَ فَإِلَى الْكَعْبَيْنِ ، وَإِيَّاكَ وَإِسْبَالَ الإِزَارِ فَإِنَّهَا مِنَ الْمَخِيلَةِ، وَإِنَّ اللَّهَ لاَ يُحِبُّ الْمَخِيلَةَ"
“Na nyanyua izari yako hadi kwenye nusu ya muundi, na kama huwezi, basi hadi kwenye vifundo vya miguu. Na tahadhari na kuteremsha izari chini ya vifundo vya miguu, kwani kufanya hivyo ni kiburi na kujiona, na Allaah kwa hakika Hapendi kiburi na mtu kujiona”. [Swahiyh Bituruqihi. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (4084), Ibn Hibaan (522), An-Nasaaiy katika Al-Kubraa (9691) na Ahmad (5/63)].
Hapa Rasuli amekufanya kule tu kushusha nguo chini ya vifundo ni kiburi na kujiona kulikoharamishwa. Hivyo basi, ujumbe hapa ni kuwa, kuteremsha nguo chini ya vifundo viwili vya mguu ni haramu, na afanyaye hivyo, atastahiki kuadhibiwa sehemu iliyo chini ya vifundo vya miguu miwili motoni (kama ilivyoeleza Hadiyth ya Abu Hurayrah). Lakini pamoja na hivyo, kitendo hiki hakiingii ndani ya duara la madhambi makubwa ambayo yatamkosesha mtu kuangaliwa na Allaah Siku ya Qiyaamah isipokuwa tu kama atakusudia kiburi na kujiona kwa kufanya hivyo.
Ama Hadiyth ya Abu Bakr, inavyoonekana ni kuwa, yeye hakuwa anaiteremsha izari yake chini ya vifundo, bali ilikuwa yenyewe inashuka na yeye anaipandisha, hivyo Hadiyth haiwezi kuleta utata kwa yaliyotangulia.
· Je, Kurefusha Mikono Ya Kanzu Zaidi Ya Kipimo Kunaingia Kwenye Hukmu Ya Kushusha Izari Chini Ya Vifundo?
Inavyoonekana ni kwamba mwenye kurefusha mikono ya kanzu (nguo) ikapitiliza kuliko ilivyozoeleka, basi anaingia ndani ya hukmu ya kushusha nguo chini ya vifundo vya miguu. ‘Ayyaadh amenukuu toka kwa ‘Ulamaa wakisema kwamba ni karaha kwa kila kilichopitiliza ada, pamoja na urefu na upana uliozoeleka kwenye mavazi.
Ninasema: “Haya yanatiliwa nguvu na Hadiyth ya Ibn ‘Umar, kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"الْإِسْبَالُ فِي الْإِزَارِ وَالْقَمِيصِ وَالْعِمَامَةِ ، مَنْ جَرَّ مِنْهَا شَيْئًا خُيَلَاءَ لَمْ يَنْظُرِ اللَّهُ إِلَيْهِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ"
“Kuteremsha nguo zaidi ya mpaka unaotakiwa (isbaal), kunajumuisha izari, kanzu (shati) na kilemba. Basi yeyote atakayeburuza chochote katika hivi kwa kiburi na kujiona, basi Allaah Hatomwangalia Siku ya Qiyaamah”. [Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (4094), An-Nasaaiy (5334), na Ibn Maajah (3576). Angalia Al-Mishkaat (4332)].
Na Ibn Al-Qayyim ameeleza kwamba haikuwa katika mwenendo wa Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuvaa mikono mipana na mirefu kupitiliza, kamwe hakuvaa yeye wala yeyote katika Maswahaba wake. Kufanya hivyo ni kwenda kinyume na Sunnah yake, kama ambavyo kujuzisha hilo hakubebi vigezo vyovyote imara, hiyo ni sehemu ya kiburi na kujiona tu na si vinginevyo, lakini pia ni upotezaji mali, kwani anaweza kushona nguo nyingine kutokana na ziada za mikono hiyo.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ وَأَحْكَامُ النَّظَرِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia
اللِّبَاسُ وَالزِّيْنَةُ للرِّجَالِ
Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume
Alhidaaya.com [3]
007- Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume: Vivazi Vilivyokatazwa Kwa Wanaume Kuvivaa: Kuvaa Hariri Safi Isiyochanganywa:
Jumhuwr ya ‘Ulamaa -bali baadhi yao wamenukuu ‘Ijmaa- kwamba ni haramu kuvaa hariri safi kwa wanaume -isipokuwa kwa dharura- kutokana na Hadiyth zinazoeleza wazi kuhusu uharamu wa hilo. Kati ya Hadiyth hizo ni:
1- Hadiyth ya Anas, kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"لاَ تَلْبَسُوا الْحَرِيرَ ، فَإِنَّهُ مَنْ لَبِسَهُ فِي الدُّنْيَا لَمْ يَلْبَسْهُ فِي الآخِرَة"
“Msivae hariri, kwa sababu, mwenye kuivaa duniani, hatoivaa akhera”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5833) na Muslim (2069)].
Ni dhahiri kwamba kutoivaa akhera ni kinaya cha kutoingia mvaaji Peponi. Kwani Allaah Ta’aalaa Amesema kuhusiana na watu wa Peponi:
"وَلِبَاسُهُمْ فِيهَا حَرِيرٌ"
“Na mavazi yao humo ni hariri”. [Al-Hajji: 23].
2- Hudhayfah bin Al-Yamaan: Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"لَا تَلْبَسُوا الْحَرِيرَ وَلَا الدِّيبَاجَ ، وَلَا تَشْرَبُوا فِي آنِيَةِ الذَّهَبِ وَالْفِضَّةِ ، وَلَا تَأْكُلُوا فِي صِحَافِهَا، فَإِنَّهَا لَهُمْ فِي الدُّنْيَا ، وَلَنَا فِي الْآخِرَةِ"
“Msivae hariri wala dibaji (brocade), na wala msinywee chombo cha dhahabu au fedha, na wala msilie katika sahani zake, kwani hizo ni zao hapa duniani, na za kwetu huko akhera”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5426) na Muslim (2067)].
3- ‘Umar bin Al-Khattwaab: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إِنَّمَا يَلْبَسُ الْحَرِيرَ فِي الدُّنْيَا مَنْ لَا خَلَاقَ لَهُ فِي الْآخِرَة"
“Hakika si vinginevyo, anayevaa hariri hapa duniani, ni yule asiye na fungu lolote akhera”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5835) na Muslim (2068)].
4- Abu Muwsaa Al-Ash-‘ariyy: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"حُرِّمَ لِبَاسُ الْحَرِيرِ وَالذَّهَبِ عَلَى ذُكُورِ أُمَّتِي وَأُحِلَّ لإِنَاثِهِمْ"
“Kuvaa hariri na dhahabu kumeharamishwa kwa wanaume wa umati wangu, lakini kwa wanawake wao kumehalalishwa”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (4057), At-Tirmidhiy (1720), An-Nasaaiy (8/160) na Ibn Maajah (3595)].
Na kwa upande mwingine, baadhi ya watu wamenukuliwa wakisema kwamba ni halali wanaume kuvaa hariri. Dalili zao ni:
1- Hadiyth ya ‘Uqbah bin ‘Aamir, amesema:
"أُهْدِيَ لِرَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَرُّوجُ حَرِيرٍ، فَلَبِسَهُ، ثُمَّ صَلَّى فِيهِ، ثُمَّ انْصَرَفَ فَنَزَعَهُ نَزْعًا شَدِيدًا كَالْكَارِهِ لَهُ ثُمَّ قَالَ : لاَ يَنْبَغِي هَذَا لِلْمُتَّقِينَ"
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipewa zawadi ya “Farruji” la hariri, akalivaa, kisha akaswali nalo. Alipomaliza kuswali, alilivua kwa haraka sana kama vile amelichukia, kisha akasema: Hili halifai kwa wamchao Allaah.” [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (375) na Muslim (2075)].
“Farruji” ni nguo iliyobana mikono na kiuno, na nyuma imepasuliwa.
Hili linajibiwa: Kwamba alilivaa kabla ya kuharamishwa, kwani haiwezekani idhaniwe kuwa Rasuli anaweza kulivaa baada ya kuharamishwa, ni sawa iwe kwenye Swalaah au kwengineko.
2- Hadiyth ya Al-Mis-war bin Makhramah kwamba:
"أَنَّهَا قُدِّمَتْ لِلنَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَقْبِيَةٌ ، فَذَهَبَ هُوَ وَأَبُوْهُ إِلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لِشَيْءٍ مِنْهَا ، فَخَرَجَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَعَلَيْهِ قُبَاءٌ مِنْ دِيْبَاجٍ مُزَرَّرَةٌ بِالذَّهَبِ، فَقَالَ :"يَا مَخْرَمَة ،خَبَأْنَا هَذَا لَكَ" ، وَجَعَلَ يُرِيْهِ مَحَاسِنَهُ ، وَقَالَ: أَرَضِيَ مَخْرَمَةٌ؟
“Kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliletewa majoho kadhaa ya hariri. Akaenda yeye (Mis-war) na baba yake kwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ili kuambulia chochote katika majoho hayo. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akatoka akiwa amevaa joho fupi la hariri lenye vifungo vya dhahabu. Akasema: Ee Makhramah! Tumekuwekea hili”. Akaanza kumuonyesha lilivyo zuri, na akauliza: Makhramah amelifurahia? [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (3127), Al-Bayhaqiy (3/273) na At-Twahaawiy (4/243)].
Hadiyth hii inajibiwa: Kwamba Hadiyth nyingine ziko wazi katika kuharamisha, juu ya msingi wa kwamba hakuna mvutano kuwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anavaa hariri, kisha uharamisho ukawa ni mwisho wa mambo mawili. [Ahkaamul ‘Awrat cha Musaa’id Al-Faalih (uk. 183)].
· Kiasi Cha Hariri Kinachoruhusiwa Katika Nguo
Mwanaume anaruhusiwa kuvaa nguo ikiwa na mstari wa hariri wa kiasi cha vidole vinne na chini ya hapo kwa mujibu wa kauli ya Jumhuwr ya ‘Ulamaa. Ni kwa Hadiyth ya Abu ‘Uthmaan:.
"كَتَبَ إِلَيْنَا عُمَرُ وَنَحْنُ بِأَذْرَبِيجَانَ : أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ نَهَى عَنْ لُبْسِ الْحَرِيرِ إِلاَّ هَكَذَا ، وَصَفَّ لَنَا النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِصْبَعَيْهِ. وَرَفَعَ زُهَيْرٌ الْوُسْطَى وَالسَّبَّابَةَ"
‘Umar bin Al-Khattwaab alituandikia barua tukiwa Azerbaijan isemayo: “Kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kuvaa hariri isipokuwa kwa kiasi hiki, na Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaashiria vidole vyake viwili”. Na Zuhayr akanyanyua cha kati na cha shahada. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5829) na Muslim (2069)].
Na katika tamko la Muslim:
"نَهَى عَنْ لُبْسِ اَلْحَرِيرِ إِلَّا مَوْضِعَ إِصْبَعَيْنِ، أَوْ ثَلَاثَةٍ، أَوْ أَرْبَعَةٍ"
“Amekataza kuvaa hariri isipokuwa kwa kiasi cha vidole viwili, au vitatu, au vinne”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (2069)].
Ikiwa kiasi cha hariri katika nguo kitazidi vidole vinne, basi itakuwa ni haramu.
· Inaruhusiwa Kuvaa Hariri Wakati Wa Dharura
[Ibn ‘Aabidiyna (5/224), Al-Khurashiy (1/252), Al-Majmuw’u (4/440), Al-Mughniy (2/306) na Zaadul Ma’aadiy (3/103)].
Jumhuwr ya ‘Ulamaa -kinyume na Wamaalik na riwaayah toka kwa Ahmad- wamejuzisha kuvaa hariri wakati wa dharura kama katika hali ya ugonjwa, au kuwashwa ngozi na mfano wake. Ni kwa Hadiyth ya Anas aliyesema:
"رَخَّصَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم لِلزُّبَيْرِ وَعَبْدُ الرَّحْمنِ في لُبْسِ الحَرِيْرِ لِحَكَّةٍ بِهِمَا"
“Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwaruhusu Zubayr na ‘Abdulrahmaan kuvaa hariri kutokana na upele uliokuwa ukiwasumbua”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5839) na Muslim (2076)].
Kwa upande wa Wamaalik, wao wanasema kwamba haijuzu kuvaa hariri kwa ajili ya upele na mfano wake, na kwamba ruksa hiyo ilikuwa mahsusi kwa Maswahaba hao wawili tu (Radhwiya Allaah ‘anhumaa)!!
Lililo sahihi ni kauli ya Jumhuwr, kwa kuwa asili ni kutohusisha watu pasi na wengine, na ruksa inapotolewa kwa baadhi ya watu kwa sababu fulani, basi ruksa hiyo itavuka kwenda kwa kila ambaye imepatikana kwake sababu hiyo, kwa kuwa hukmu inaenea kwa kuenea sababu yake. Allaah Ndiye Ajuaye zaidi.
· Hairuhusiwi Kutandika Hariri
Hudhayfah amesema:
"نَهَانَا النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنْ نَشْرَبَ فِي آنِيَةِ الذَّهَبِ وَالْفِضَّةِ وَأَنْ نَأْكُلَ فِيهَا ، وَعَنْ لُبْسِ الْحَرِيرِ وَالدِّيبَاجِ وَأَنْ نَجْلِسَ عَلَيْهِ"
“Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametukataza kunywea au kulia chombo cha dhahabu au fedha, na kuvaa au kukalia hariri na dibaji (brocade). [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5837)].
Haya ndiyo waliyosema Jumhuwr -kinyume na Abu Haniyfah-, kwa kuwa sababu ya kuharamisha kuvaa ipo pale pale katika kukalia, na kwa kuwa pia kuvaa kukiharamishwa -nalo ni jambo la lazima kwa mtu- basi jinginelo linastahiki uharamu zaidi. Na hii ni hukmu inayowahusu wanaume tu. Ama wanawake, wao inajuzu kuvaa.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ وَأَحْكَامُ النَّظَرِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia
اللِّبَاسُ وَالزِّيْنَةُ للرِّجَالِ
Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume
Alhidaaya.com [3]
008- Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume: Vivazi Vilivyokatazwa Kwa Wanaume Kuvivaa: Ni Haramu Kuvaa Nguo Ya Kipekee Ili Kuonekana Tofauti (Vazi La Umashuhuri):
Ibn ‘Umar amesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"مَنْ لَبِسَ ثَوْبَ شُهْرَةٍ فيٍ الدُّنْيَا أَلْبَسَهُ اللَّهُ ثَوْبَ مَذَلَّةٍ يَوْمَ الْقِيَامَةِ" [ثُمَّ أَلْهَبَ فِيْهِ نَارًا]
“Mwenye kuvaa nguo ya kutaka yeye pekee aonekane tofauti na wengine hapa duniani, Allaah Atamvisha nguo ya udhalili Siku ya Qiyaamah [Kisha Atamwashia ndani yake moto]. [Hadiyth Hasan. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (4029), Ibn Maajah (3606) na Ahmad (2/92), iko kwenye Swahiyhul Jaami’i (6526)].
Ibn Al-Athiyr amesema: “Nguo hii, ni nguo ya mtu kutaka umashuhuri kati ya watu, rangi yake iwe tofauti na rangi ya nguo zao (au mshono, kitambaa n.k) kiasi cha kuwafanya watu wanyanyue macho yao kuiangalia huku akitamba kwa kiburi na kujiona yeye ni yeye, hakuna zaidi yake”.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ وَأَحْكَامُ النَّظَرِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia
اللِّبَاسُ وَالزِّيْنَةُ للرِّجَالِ
Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume
Alhidaaya.com [3]
009- Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume: Vivazi Vilivyokatazwa Kwa Wanaume Kuvivaa: Je, Ni Karaha Kwa Mwanaume Kuvaa Vazi Jekundu?:
‘Ulamaa wamekhitalifiana kwa kauli nyingi juu ya hukmu ya mwanaume kuvaa nguo nyekundu. Al-Haafidh amezidhibiti katika kauli saba ambazo zinaweza kuchujwa na kuwekwa katika kauli mbili:
Kauli ya kwanza: Ni karaha kuvaa nguo nyekundu, nayo ni madhehebu ya Hanafiy na Hanbali. Dalili zao ni:
1- Hadiyth ya Al-Baraa bin ‘Aazib: amesema:
"أَمَرَنَا النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِسَبْعٍ وَنَهَانَا عَنْ سَبْعٍ – فَذَكَرَ مِنْهَا- المَيَاثِرُ الحُمُرُ"
“Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametuamuru mambo saba na ametukataza mambo saba -kati ya aliyoyakataza- ni matandiko myekundu (ya kukalia juu ya mnyama)”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5849) na Muslim (2066)].
Katika riwaayah ya Hadiyth ya ‘Imraan bin Haswiyn imekuja:
"نَهَى عَنْ مِيثَرَةِ الأُرْجُوَان"
“Amekataza tandiko la hariri la rangi nyekundu iliyokoza (la kukalia juu ya mnyama)”.
2- Yaliyosimuliwa toka kwa ‘Abdullaah bin ‘Umar aliyesema:
"مَرَّ عَلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ رَجُلٌ عَلَيْهِ ثَوْبَانِ أَحْمَرَانِ فَسَلَّمَ عَلَيْهِ فَلَمْ يَرُدَّ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم عَلَيْهِ"
“Mtu mmoja alipita mbele ya Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa amevaa nguo mbili nyekundu, akamsalimia, lakini Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakumjibu”. Lakini ni Dhwa’iyf. [Hadiyth Dhwa’iyf. Imekharijiwa na At-Tirmidhiy (2807) na Abu Daawuwd (4069)].
3- Mwanamke mmoja wa Baniy Asad amesema:
"كُنْتُ يَوْمًا عِنْدَ زَيْنَبَ امْرَأَةِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَنَحْنُ نَصْبُغُ ثِيَابًا لَهَا بِمَغْرَةٍ ، فَبَيْنَمَا نَحْنُ كَذَلِكَ إِذْ طَلَعَ عَلَيْنَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ، فَلَمَّا رَأَى الْمَغْرَةَ رَجَعَ ، فَلَمَّا رَأَتْ ذَلِكَ زَيْنَبُ عَلِمَتْ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَدْ كَرِهَ مَا فَعَلَتْ فَأَخَذَتْ فَغَسَلَتْ ثِيَابَهَا وَوَارَتْ كُلَّ حُمْرَةٍ ، ثُمَّ إِنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ رَجَعَ فَاطَّلَعَ ، فَلَمَّا لَمْ يَرَ شَيْئًا دَخَلَ"
“Nilikuwa siku moja kwa Zaynab mke wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Tulikuwa tunaitia nguo yake rangi kwa kutumia poda nyekundu. Na wakati tukiwa tunaendelea na shughuli hiyo, mara Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaingia. Alipoona poda nyekundu alirudi, hakuingia. Zaynab alipoona hivyo, akajua kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amechukia hayo anayoyafanya. Akaichukua nguo yake akaiosha hadi wekundu wote ukaondoka. Kisha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alirejea tena, akachungulia, alipoona hakuna kitu, aliingia”. Hadiyth hii ni Dhwa’iyf. [Imekharijiwa na Abu Daawuwd (4071), Ibn Abiy ‘Aaswim katika Al-Aahaad (3096) na At-Twabaraaniy (24/25-57/185)].
4- Yaliyopokelewa Marfuw’an toka kwa Raafi’u bin Yaziyd Ath-Thaqafiy:
"إِنَّ الشَّيْطَانَ يُحِبُّ الحُمْرَةَ ، وَإِيَّاكُمْ وَالحُمْرَةَ وَكُلَّ ثَوْبٍ ذِيْ شُهْرَةٍ"
“Hakika shetani anapenda rangi nyekundu, basi tahadharini na wekundu na kila kivazi cha kutafutia umashuhuri”. Hii pia ni Dhwa’iyf. [At-Twabaraaniy ameikhariji katika Al-Awsatw (7708)].
Kauli ya pili: Inafaa kuvaa nguo nyekundu. Haya ni madhehebu ya Maalik na Shaafi’iy. Dalili zao ni:
1- Hadiyth ya Al-Baraa:
" كَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مَرْبُوعًا، وَقَدْ رَأَيْتُهُ فِي حُلَّةٍ حَمْرَاءَ مَا رَأَيْتُ شَيْئًا أَحْسَنَ مِنْهُ"
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa na kimo cha wastani. Niliwahi kumwona akiwa amevaa vazi jekundu la juu na chini, sijapata kuona kitu kizuri zaidi kuliko yeye. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5848). Ina Hadiyth mwenza ya Jaabir iliyoko kwa At-Tirmidhiy (2811)].
2- Jaabir bin Samurah:
رَأَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فِي لَيْلَةٍ إِضْحِيَانٍ فَجَعَلْتُ أَنْظُرُ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَإِلَى الْقَمَرِ وَعَلَيْهِ حُلَّةٌ حَمْرَاءُ فَإِذَا هُوَ عِنْدِي أَحْسَنُ مِنَ الْقَمَرِ"
“Nilimwona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika usiku angavu wa mbalamwezi. Nikaanza kumwangalia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) huku nikiuangalia mwezi naye akiwa amevaa vazi jekundu, nikamwona kwa hakika ni mzuri kuliko mwezi. [Hadiyth Dhwa’iyf. Imekharijiwa na At-Tirmidhiy (2811), An-Nasaaiy katika Al-Kubraa (9640), Abu Ya’alaa (7477) na Al-Haakim (4/207)].
Wa kauli ya mwanzo wenye kusema ni karaha kuvaa nyekundu wamejibu wakisema kwamba vazi jekundu alilolivaa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) halikuwa jekundu lote, bali lilichanganyika na rangi nyingine.
Kauli Yenye Nguvu:
Ninaloliona mimi ni kuwa dalili za kundi la mwanzo wanaosema ni karaha kuvaa nyekundu, hazina nguvu. Kwa msingi huo, hakuna ubaya kuvaa nyekundu. Lakini, lau mtu ataacha kuvaa nyekundu iliyokoza ambayo haikuchanganyika na rangi yoyote, itakuwa bora na akiba zaidi ili kutoka nje ya duara la mvutano. Allaah Ndiye Mjuzi zaidi.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ وَأَحْكَامُ النَّظَرِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia
اللِّبَاسُ وَالزِّيْنَةُ للرِّجَالِ
Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume
Alhidaaya.com [3]
010- Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume: Vivazi Vilivyokatazwa Kwa Wanaume Kuvivaa: Nguo Ya Rangi Ya Zafarani:
‘Abdullaah bin ‘Amri amesema:
"رَأَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَلَىَّ ثَوْبَيْنِ مُعَصْفَرَيْنِ فَقَالَ : "إِنَّ هَذِهِ مِنْ ثِيَابِ الْكُفَّارِ فَلاَ تَلْبَسْهَا"
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliniona nimevaa nguo mbili za rangi ya zafarani. Akaniambia: Hakika hizi ni katika nguo za makafiri, basi usizivae”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (2077)].
Na katika riwaayah amesema:
"أَأُمُّكَ أَمَرَتْكَ بِهَذَا؟" قُلْتُ أَغْسِلُهُمَا. قَالَ: "بَلْ أَحْرِقْهُمَا"
“Je, ni mama yako amekuamuru kufanya hivi?! Nikasema: Nitazitoa rangi. Akasema: Bali zichome moto”.
Maana ya swali la (Rasuli): Je, ni mama yako aliyekuamuru kufanya hivi?!, ni kuwa haya ni katika mavazi ya wanawake, mapambo yao na tabia zao. Ama amri ya kuzichoma moto, ‘Ulamaa wamesema ni adhabu na shadidio ili aonyeke na waonyeke wengineo kufanya mfano wa kitendo hicho. [Sharhu Muslim].
Imepokelewa toka kwa ‘Aliy bin Abiy Twaalib:
أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ نَهَى عَنْ لُبْسِ الْقَسِّيِّ ، والمُعَصْفَرِ، وَعَنْ تَّخَتُّمِ الذَّهَبِ ، وَعَنْ قِرَاءَةِ القُرْآنِ في الرُّكُوْعِ"
“Kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametukataza kuvaa nguo iliyotengenezwa kwa kitani na hariri, nguo ya rangi ya zafarani, kuvaa pete ya dhahabu, na kusoma Qur-aan kwenye rukuu”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (2078), At-Tirmidhiy (264) na An-Nasaaiy (1041)].
‘Ulamaa wamekhitilafiana kuhusu suala la nguo ya zafarani, nayo ni ile yenye rangi ya kinjano. Jumhuwr ya ‘Ulamaa wamejuzisha kuvaa akiwemo Shaafi’iy, Maalik na Abu Haniyfah!! Ama kundi jingine la ‘Ulamaa, wao wamesema ni makruhu karaha hafifu “tanziyh” kutokana na yaliyothibiti toka kwa Ibn ‘Umar akisema:
"رَأَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَصْبُغُ بِالصُّفْرَةِ"
“Nilimwona Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akitia rangi ya kinjano”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5851) na Muslim (1187)].
Ama Al-Khattwaabiyy, yeye amesema katazo linaelekezwa kwenye nguo iliyotiwa rangi hiyo baada ya kufumwa. Ama ile ambayo nyuzi zake zimetiwa rangi kisha ikafumwa, basi hiyo haiingii kwenye katazo.
Kadhalika, ‘Ulamaa wengine wamelichukulia katazo kwa aliyehirimia Hajji au ‘Umrah ili liowane na Hadiyth ya Ibn ‘Umar kuhusiana na yaliyoharamishwa kuvaa kwa aliyehirimia. [Sharhu Muslim (14/54)].
Ninasema: “Linaloonekana kuwa na nguvu, ni kwamba haijuzu kuvaa nguo iliyotiwa rangi ya kinjano kutokana na Hadiyth zilizothibiti na hususan ikiwa rangi yenyewe imekoza sana hadi kufanana na nguo za akina mama. Na kwa ajili hiyo, Al-Bayhaqiy (Rahimahul Laah) amesema: “Lau kama Hadiyth hizi zingelimfikia Ash-Shaafi’iy, basi angelizisema..”.
Ama Hadiyth ya Ibn ‘Umar, Hadiyth hii haikutaja ni kitu gani alichokitia rangi Rasuli, je ni nguo, au nywele au ndevu. Hivyo, inaweza kuchukulika kwamba Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitia rangi nywele zake au nguo zake. Lakini pia, unjano unaozungumziwa kwenye Hadiyth ya Ibn ‘Umar unaweza kuchukuliwa kuwa si ule wa kukoza wa kufanana na nguo za wanawake. Allaah Ndiye Mjuzi zaidi”.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ وَأَحْكَامُ النَّظَرِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia
اللِّبَاسُ وَالزِّيْنَةُ للرِّجَالِ
Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume
Alhidaaya.com [3]
011- Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume: Vivazi Vilivyokatazwa Kwa Wanaume Kuvivaa: Nguo Yenye Msalaba:
Toka kwa ‘Aaishah:
"أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لَمْ يَكُنْ يَتْرُكُ فِي بَيْتِهِ شَيْئًا فِيهِ تَصَالِيبُ إِلَّا نَقَضَهُ"
“Kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakuwa akiacha chochote ndani ya nyumba yake chenye umbo (au mchoro) la msalaba ila hukiharibu”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5952].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ وَأَحْكَامُ النَّظَرِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia
اللِّبَاسُ وَالزِّيْنَةُ للرِّجَالِ
Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume
Alhidaaya.com [3]
012- Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume: Vivazi Vilivyokatazwa Kwa Wanaume Kuvivaa: Nguo Iliyotengenezwa Kwa Ngozi Ya Wanyama Wakali:
Ni kama simba, chui, duma na kadhalika. Ni haramu kuvaa nguo au viatu vilivyotengenezwa kwa ngozi za wanyama hawa kutokana na neno lake Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"لَا تَرْكَبُوا الْخَزَّ وَلَا النِّمَارَ"
“Msikalie hariri wala ngozi ya chui”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (4129) na Ibn Maajah (3656)].
Rasuli amekataza kutumia vitu hivi kutokana na kuwa ni mapambo, na kuwa vinajenga kiburi kwa mtumiaji, lakini pia ni nguo za watu wasio na asili ya Uarabu (Waajemi). [‘Awnul Ma’abuwd (11/188)]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ وَأَحْكَامُ النَّظَرِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia
اللِّبَاسُ وَالزِّيْنَةُ للرِّجَالِ
Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume
Alhidaaya.com [3]
013- Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume: Adabu Za Kuvaa:
1- Kuwa na hima ya kuvaa vivazi vizuri kwa mwenye uwezo
Al-Ahwasw alimnukulu baba yake akisema:
"أَتَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَعَلَى ثَوْبٌ دُونٌ ، فَقَالَ لِي: أَلَكَ مَالٌ؟ قُلْتُ: نَعَمْ. قَالَ: مِنْ أَيِّ الْمَالِ؟ قُلْتُ: مِنْ كُلِّ الْمَالِ قَدْ أَعْطَانِي اللَّهُ منَ الإِبلِ وَالْبَقَرِ وَالْخَيْلِ وَالرَّقِيقِ. قَالَ: فَإِذَا آتَاكَ اللَّهُ مَالًا فَلْيُرَ أَثَرُ نِعْمَةِ اللَّهِ عَلَيْكَ وَكَرَامَتِهِ"
“Nilimwendea Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) nikiwa nimevaa nguo duni. Akaniuliza: Je, una mali? Nikasema: Na’am. Akauliza: Ni mali ya aina gani? Nikasema: Ni za aina zote, Allaah Ameniruzuku ngamia, ng’ombe, farasi na watumwa. Akasema: Allaah Akikuruzuku mali, basi athari ya Neema ya Allaah ionekane kwako pamoja na na Hisani Yake”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (4063) na An-Nasaaiy (5224). Ina Hadiyth wenza toka kwa ‘Abdullaah bin ‘Amri, Abu Hurayrah, ‘Imraan bin Haswiyn, Ibn Mas-‘uwd na wengineo].
Na Allaah Amesema:
قُلْ مَنْ حَرَّمَ زِينَةَ اللَّـهِ الَّتِي أَخْرَجَ لِعِبَادِهِ وَالطَّيِّبَاتِ مِنَ الرِّزْقِ ۚ قُلْ هِيَ لِلَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا خَالِصَةً يَوْمَ الْقِيَامَةِ
“Sema: Nani aliyeharamisha Mapambo ya Allaah ambayo Amewatolea Waja Wake na vilivyo vizuri katika riziki? Sema: Hivyo ni kwa ajili ya wale walioamini katika uhai wa dunia; makhsusi (kwa Waumini) Siku ya Qiyaamah”. [Al-A’araaf: 32].
Kuvaa nguo nzuri haimaanishi mtu ana kibri. Toka kwa Ibn Mas-‘uwd: Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"لاَ يَدْخُلُ الْجَنَّةَ مَنْ كَانَ فِي قَلْبِهِ مِثْقَالُ ذَرَّةٍ مِنْ كِبْرٍ . قَالَ رَجُلٌ: إِنَّ الرَّجُلَ يُحِبُّ أَنْ يَكُونَ ثَوْبُهُ حَسَنًا وَنَعْلُهُ حَسَنَةً . قَالَ : إِنَّ اللَّهَ جَمِيلٌ يُحِبُّ الْجَمَالَ ، الْكِبْرُ بَطَرُ الْحَقِّ وَغَمْطُ النَّاسِ"
“Haingii Peponi mtu ambaye ndani ya moyo wake kuna kibri cha uzito wa sisimizi. Mtu mmoja akasema: Je ikiwa mtu anapenda nguo zake kuwa nzuri na viatu vyake kuwa vizuri?. Akasema: Hakika Allaah Ni Mzuri, Anapenda vitu vizuri, lakini kibri ni kuikataa haki na kudharau watu”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (91), Abu Daawuwd (4092) na wengineo].
2- Asinunue mtu mavazi ya ziada bila kuhitajia
Allaah Ta’aalaa Amesema:
يَا بَنِي آدَمَ خُذُوا زِينَتَكُمْ عِندَ كُلِّ مَسْجِدٍ وَكُلُوا وَاشْرَبُوا وَلَا تُسْرِفُوا ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُسْرِفِينَ ﴿٣١﴾
31. Enyi wana wa Aadam! Chukueni mapambo yenu katika kila Masjid. Na kuleni na kunyweni, na wala msifanye israfu. Hakika Yeye (Allaah) Hapendi wanaofanya israfu. [Al-A’araaf: 31].
Na Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"كُلُوا وَاشْرَبُوا وَتَصَدَّقُوا وَالْبَسُوا مَا لم يُخَالِطْهُ إِسْرَافٌ وَلَا مَخِيْلَة"ٌ
“Kuleni, kunyweni, toeni sadaka na vaeni, mradi tu isiwepo israfu wala majivuno ndani yake”. [Hadiyth Hasan. Al-Bukhaariy ameifanya Mu’allaq kwenye Kitabu Cha Mavazi, na An-Nasaaiy kaifanya Mawswuul (2559) na Ibn Maajah kwa Sanad Hasan].
3- Kuomba du’aa wakati wa kuvaa nguo mpya
Abu Sa’iyd Al-Khudriyy amesema:
"كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا اسْتَجَدَّ ثَوْبًا سَمَّاهُ بِاسْمِهِ عِمَامَةً أَوْ قَمِيصًا أَوْ رِدَاءً ، ثُمَّ يَقُولُ : اللَّهُمَّ لَكَ الْحَمْدُ أَنْتَ كَسَوْتَنيهِ ، أَسْأَلُكَ خَيْرَهُ وَخَيْرَ مَا صُنِعَ لَهُ ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّهِ وَشَرِّ مَا صُنِعَ لَهُ"
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapopata nguo mpya huipa jina lake, ikiwa kilemba au kanzu au shuka ya juu, kisha husema: Ee Allaah! Ni Yako himdi, Wewe Ndiye Umenivisha, nakuomba kheri yake na kheri iliyotengenezewa, na najilinda Kwako na shari yake na shari iliyotengenezewa”. [Hasan Lishawaahidihi. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (4020), At-Tirmidhiy (1767), na An-Nasaaiy (1382). Ina Hadiyth mwenza inayoizatiti].
4- Kuanza kuvaa kwa upande wa kulia
‘Aaishah amesema:
"كَانَ اَلنَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يُعْجِبُهُ اَلتَّيَمُّنُ فِي تَنَعُّلِهِ، وَتَرَجُّلِهِ، وَطُهُورِهِ، وَفِي شَأْنِهِ كُلِّهِ"
“Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kulikuwa kunampendeza kuanza kwa kulia akivaa viatu, akichana nywele, akijitwaharisha, na katika mambo yake yote”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (426) na Muslim (268)].
5- Asitembee mtu kwa kiatu kimoja
Abu Hurayrah: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"لَا يَمْشِي أَحَدُكُمْ فِي نعلٍ واحدةٍ ، لِيَنْعَلْهُمَا جَمِيعًا ، أَوْ لِيُحْفِيَهُمَا جَمِيعًا"
“Mmoja wenu asitembee kwa kiatu kimoja. Ima avivae vyote viwili, au avivue vyote viwili”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5855) na Muslim (2097)].
“Mmoja wenu asitembee kwa kiatu kimoja. Ima avivae vyote viwili, au avivue vyote viwili”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5855) na Muslim (2097)].
Ukaraha katika katazo hili -na Allaah Ndiye Ajuaye zaidi- ni kwa ajili ya kuepuka mtu kuonekana wa kipekee, kwa kuwa kitendo hiki huvuta macho ya watu, na Rasuli amekataza kuvaa kivazi cha kuonekana mtu wa kipekee (cha umashuhuri). Kitu chochote kinachomfanya mhusika wake kuonekana tofauti na wengine, basi kinastahiki kuepukwa.
6- Mtu asilale chali na kuweka mguu mmoja juu ya mwingine kama hajavaa suruali ya ndani
Jaabir bin ‘Abdillaah: “Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"لاَ يَسْتَلْقِيَنَّ أَحَدُكُمْ ثُمَّ يَضَعُ إِحْدَى رِجْلَيْهِ عَلَى الأُخْرَى"
“Asilale kabisa chali mmoja wenu kisha akaweka mguu wake mmoja juu ya mwingine”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (2099)].
Wakati wa katazo hili unakuwa pale mtu anapokuwa hajavaa ndani suruali ya kusitiri uchi wake. Abu Sa’iyd amesema:
"نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنْ يَحْتَبِيَ الرَّجُلُ فِي ثَوْبٍ وَاحِدٍ ، لَيْسَ عَلَى فَرْجِهِ مِنْهُ شَىْءٌ"
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza mtu kukaa kikao cha “ihtibaa” akiwa na nguo moja tu, na hana chochote cha kusitiri utupu wake”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (367), An-Nasaaiy (5340), na Abu Daawuwd (3377). Iliyoko kwa Al-Bukhaariy imetoka kwa Abu Hurayrah, na iliyoko kwa Muslim imetoka kwa Jaabir].
“Ihtibaa” ni kunyanyua mtu miguu yake miwili wakati amekaa, akaambatisha mapaja yake na tumbo lake na kifua, kisha akaizungushia nguo, au akaiviringisha mikono yake miwili au kishali.
Ama ikiwa amevaa nguo ya ndani ya kusitiri utupu wake, basi hakuna ubaya. Imepokelewa toka kwa ‘Abdullaah bin Zayd kwamba:
"رَأَى رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مُسْتَلْقِيًا فِي الْمَسْجِدِ وَاضِعًا إِحْدَى رِجْلَيْهِ عَلَى الأُخْرَى"
“Alimwona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa amelala chali Msikitini huku ameweka mguu wake mmoja juu ya mwingine”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (475) na Muslim (2100)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ وَأَحْكَامُ النَّظَرِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia
اللِّبَاسُ وَالزِّيْنَةُ للرِّجَالِ
Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume
Alhidaaya.com [3]
014- Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume: Pambo La Nywele:
Inapendeza kwa mwenye nywele azihifadhi kwa kuzisafisha na kuziweka kwenye mwonekano mzuri, azienzi, azichane, azipake mafuta na kadhalika.
Bibi ‘Aaishah amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إِذَا كَانَ لأَحَدِكُمْ شَعْرٌ فَلْيُكْرِمْهُ"
“Mmoja wenu akiwa na nywele, basi azienzi na kuzitunza”. [Hadiyth Hasan. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (4163) na An-Nasaaiy (8/183)].
Haitakikani mtu aziachilie nywele zake mpaka ziwe kwenye hali mbaya, bali azipake mafuta, azilainishe kwa maji na mfano wake na azichane. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwona mtu mmoja nywele zake zimemsimama akasema:
"أَمَا كَانَ يَجِدُ هَذَا مَا يُسَكِّنُ بِهِ شَعْرَهُ"
“Je hawezi huyu kupata chochote cha kulainishia nywele zake?”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (4062) na An-Nasaaiy (8/183)].
Imesuniwa mtu anapochana nywele zake aanzie upande wa kulia wa kichwa chake kutokana na Hadiyth ya ‘Aaishah iliyotangulia.
"كَانَ اَلنَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يُعْجِبُهُ اَلتَّيَمُّنُ فِي تَنَعُّلِهِ، وَتَرَجُّلِهِ، وَطُهُورِهِ، وَفِي شَأْنِهِ كُلِّهِ"
Na ikiwa anazitunza vyema nywele zake, basi itapendeza aziwache ziwe ndefu na aziteremshie hadi kwenye mabega yake. Anas amesema:
"أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ يَضْرِبُ شَعْرَ رَأْسِهِ مَنْكِبَيْهِ"
“Kwamba nywele za Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) zilikuwa zikigusa mabega yake mawili”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5904)].
‘Aaishah kasema:
"كَانَ لِرَسُوْلِ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ شَعْرٌ دُونَ الْجُمَّةِ وَفَوْقَ الوَفْرَةِ"
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa na nywele zilizoning’inia juu kidogo ya mabega mawili, na chini kidogo ya ndewe za masikio”. [Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh. Imekharijiwa na Ibn Maajah (3635) na At-Tirmidhiy (1755)].
Haitakikani nywele kuwa ndefu zaidi ya kipimo hiki, na hii ni kwa sababu mbili:
Ya kwanza: Kunamuingiza mtu katika duara la kujifananisha na wanawake.
Ya pili: Ni kwa yaliyopokelewa toka kwa Sahl bin Al-Handhwaliyyah, amesema: Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"نِعْمَ الرَّجُلُ خُرَيْمٌ الْأَسْدِيُّ ، لَوْلَا طُولُ جُمَّتِهِ وَإِسْبَالِ إِزَارِهِ ، فَبَلَغَ ذَلِكَ خُرَيْمًا ، فَأَخَذَ شَفْرَةً فَقَطَعَ بِهَا جُمَّتَهُ إِلَى أُذُنَيْهِ ، وَرَفَعَ إِزَارَهُ إِلَى أَنْصَافِ سَاقَيْهِ"
“Khuraym Al-Asdiyyu angelikuwa ni mtu bora kabisa lau kama si kurefusha nywele zake chini ya ndewe na kuburuza izari yake. Khuzaym akasikia habari hiyo, hapo hapo akachukua mkasi akakata nywele zake hadi kufikia masikioni, na akanyanyua izari yake hadi kwenye miundi”. [Isnaad Layyin. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (4089), Ahmad (4/179), na At-Twabaraaniy (6/94)].
· Angalizo:
Ama yaliyothibiti kwamba:
"نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنِ التَّرَجُّلِ إِلاَّ غِبًّا"
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kuchana sana nywele isipokuwa muda baada ya muda”. [Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh. Imekharijiwa na An-Nasaaiy (8/132), At-Tirmidhiy (1756) na Abu Daawuwd (4159). Iko kwenye Swahiyhul Jaami’u (6870)].
Makusudio ya hili ni mtu asipumbazike sana na nywele na kupoteza wakati mwingi kuzishughulikia. Allaah Ndiye Ajuaye zaidi.
· Kunyofoa Mvi Ni Haramu:
Toka kwa ‘Amri bin Shu’ayb, toka kwa baba yake toka kwa babu yake toka kwa Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"لَا تَنْتِفُوا الشَّيْبَ ، فَإِنَّهُ نُورُ الْمُسْلِمِ يَوْمَ القِيَامَةِ"
“Msinyofoe mvi, kwani mvi ni nuru ya Muislamu Siku ya Qiyaamah”. [Hadiyth Hasan. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (4202) na At-Tirmidhiy (2821)].
Toka kwa Anas:
"كُنَّا نَكْرَهُ أَنْ يَنْتِفَ الرَّجُلُ الشَّعْرَةَ الْبَيْضَاءَ مِنْ رَأْسِهِ وَلِحْيَتِهِ"
“Tulikuwa hatupendi mwanaume kunyofoa mvi za kichwa chake na ndevu zake”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (2341)].
· Kutia Rangi Nywele:
Inaruhusiwa kubadili rangi ya mvi, lakini si kwa rangi nyeusi. Toka kwa Jaabir, amesema:
"أُتِيَ بِأَبِي قُحَافَةَ يَوْمَ فَتْحِ مَكَّةَ وَرَأْسُهُ وَلِحْيَتُهُ كَالثُّغَامَةِ بَيَاضًا ، فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: غَيِّرُوا هَذَا بِشَيْءٍ وَاجْتَنِبُوا السَّوَادَ"
“Abu Quhaafah aliletwa Siku Makkah ilipokombolewa kichwa chake na ndevu zake zikiwa nyeupe mithili ya hisopo. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: Badilisheni hizi kwa kitu chochote, lakini epukeni rangi nyeusi”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (2102), An-Nasaaiy (5076) na Abu Daawuwd (4204)].
Na Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliamuru kwenda kinyume na Mayahudi na Manaswara akisema:
"إِنَّ الْيَهُودَ وَالنَّصَارَى لاَ يَصْبُغُونَ فَخَالِفُوهُمْ"
“Hakika Mayahudi na Manaswara hawatii rangi nywele (wala ndevu), basi nendeni kinyume nao”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5899) na Muslim (2103)].
Rangi inabadilishwa kwa kutumia hina, “katam” (mimosa flava) na mfano wake. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إِنَّ أَحْسَنَ مَا غُيِّرَ بِهِ الشَّيْبُ الْحِنَّاءُ وَالْكَتَمُ"
“Hakika kitu bora zaidi cha kubadilishia rangi mvi ni hina na “katam (mimosa flava)”. [Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh katika Asw-Swahiyhah (1509). Imekharijiwa na At-Tirmidhiy (1573), An-Nasaaiy (8/139), na Ibn Maajah (3622). Kuna mvutano kwenye Sanadi yake].
Ama kutia rangi nyeusi, hili haliruhusiwi, ni marufuku kabisa. Ni kwa Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaah ‘anhumaa) aliyesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"يَكُونُ فِي آخِرِ الزَّمَانِ قَوْمٌ يَخْضِبُونَ بِالسَّوَادِ كَحَوَاصِلِ الْحَمَامِ ، لَا يَرِيحُونَ رَائِحَةَ الْجَنَّةِ"
“Watakuja watu zama za mwisho, watatia nywele zao (na ndevu) rangi nyeusi mithili ya vifua vya njiwa, hao hawatainusa harufu ya Pepo”. [Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (4212), An-Nasaaiy (8/138), na Ahmad (1/273). Iko katika Swahiyhul Jaami’i (8153)].
Na pia kwa Hadiyth nyingine iliyotangulia:
"غَيِّرُوا هَذَا بِشَيْءٍ وَاجْتَنِبُوا السَّواد"
“Badilisheni hizi kwa kitu chochote, lakini epukeni rangi nyeusi”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (2102), An-Nasaaiy (5076) na Abu Daawuwd (4204)].
Faida:
Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kunyofoa mvi lakini hakukataza kuzitia rangi, kwa kuwa kunyofoa kunabadili umbile lake la asili kinyume na kutia rangi ambako hakugeuzi umbile kwa mwenye kuziangalia.
Baadhi ya ‘Ulamaa wamesema kwamba sharia imeruhusu kuzificha mvi kwa kuzitia rangi kwa ajili ya maslaha mengine ya kidini, nayo ni kuwavunja nguvu maadui na kuwaonyesha ukakamavu na ungangari mbele yao. [‘Awnul Ma’abuwd (11/171)].
· Ni Haramu Kunyoa Ndevu:
Kunyoa ndevu kwa wanaume ni haramu kwa ‘Ijmaa ya ‘Ulamaa. Kwa kuwa kuzinyoa ni kubadili uumbaji wa Allaah, kumtii shetani, kukhalifu agizo la Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) la kuzifuga na kuziachilia, kujifananisha na makafiri, na kujifananisha pia na wanawake. Dalili juu ya hayo zimetajwa kwenye Kitabu Cha Twahara.
· Kukata Sharubu Na Kulipunguza:
Kukata sharubu na kulipunguza ni katika sunnah za maumbile asilia, lakini pia ni ukamilisho wa pambo la mwanaume. Abu Hurayrah amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"الْفِطْرَةُ خَمْسٌ : الْخِتَانُ، وَالاِسْتِحْدَادُ، وَنَتْفُ الإِبْطِ، وَتَقْلِيمُ الأَظْفَارِ، وَقَصُّ الشَّارِبِ"
“Maumbile asili ni katika (mambo) matano: Kutahiriwa, kunyoa kinena, kunyofoa kikwapa, kukata kucha na kukata sharubu”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5891) na Muslim (257)].
Na Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"أَحْفُوا الشَّوَارِبَ"
“Punguzeni sharubu”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5892) na Muslim (259)].
Na katika riwaayah:
"جُزُّوا الشَّوَارِبَ"
“Kateni masharubu”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (260)].
Pia amesema:
"مَنْ لَمْ يَأْخُذ مِنْ شَارِبِهِ فَلَيْسَ مِنَّا"
“Yeyote ambaye hapunguzi chochote katika sharubu lake, basi si katika sisi”. [Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh. Imekharijiwa na An-Nasaaiy (1/15), At-Tirmidhiy (2761) na Ahmad (4/368). Iko kwenye Swahiyhul Jaami’i (6533).
Makusudio hapa ni kukata sharubu zenye kuota juu ya mdomo wa juu na si kuzifyeka zote, na pia kuzikata kabisa toka kwa juu zile zinazoangukia kwenye wekundu wa mdomo kwa namna isiyosababisha kero kwa mlaji wala kukusanyika uchafu.
Imesemwa pia kwamba makusudio ni kuondosha nywele zote ziotazo kwenye mdomo wa juu. Kauli zote mbili zinabebwa na dalili, na pia hupatikana kwazo lengo la kuwakhalifu Wamajusi, mbali na kusalimika mlaji na adha ya nywele na kukusanyia uchafu. Allaah Ndiye Ajuaye zaidi.
Muislamu anatakikana asiache sharubu kwa zaidi ya siku 40. Na hii ni kwa Hadiyth ya Anas aliyesema:
"وُقِّتَ لَنَا فِي قَصِّ الشَّارِبِ وَتَقْلِيمِ الْأَظْفَارِ وَنَتْفِ الْإِبِطِ وَحَلْقِ الْعَانَةِ أَنْ لَا تُتْرَكَ أَكثر من أَرْبَعِينَ لَيْلَة"
“Tumewekewa sisi muda katika kukata sharubu, kukata kucha, kunyofoa nywele za kwapa, na kunyoa kinena kwamba visiachwe hivyo zaidi ya siku 40”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (257)].
· Ni Marufuku Kunyoa Denge (Panki)
Ibn ‘Umar amesema:
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kunyoa denge”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5920) na Muslim (113)].
Denge ni kunyoa sehemu ya kichwa na kuacha nyingine. Vijana wengi wa Kiislamu wameingia kwenye mtihani huu wakiwaiga kibubusa Mayahudi na Manaswara.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ وَأَحْكَامُ النَّظَرِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia
اللِّبَاسُ وَالزِّيْنَةُ للرِّجَالِ
Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume
Alhidaaya.com [3]
015- Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume: Pambo La Pete Na Mfano Wake:
· Wanaume Hawaruhusiwi Kuvaa Pete Ya Dhahabu
1- Ibn ‘Umar amesema:
"أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ اصْطَنَعَ خَاتَمًا مِنْ ذَهَبٍ ، فَكَانَ يَجْعَلُ فَصَّهُ فِي بَاطِنِ كَفِّهِ إِذَا لَبِسَهُ، فَصَنَعَ النَّاسُ خَوَاتِيمَ ، ثُمَّ إِنَّهُ جَلَسَ عَلَى الْمِنْبَرِ فَنَزَعَهُ، فَقَالَ : "إِنِّي كُنْتُ أَلْبَسُ هَذَا الْخَاتِمَ وَأَجْعَلُ فَصَّهُ مِنْ دَاخِلٍ ". فَرَمَى بِهِ ثُمَّ قَالَ "وَاللَّهِ لاَ أَلْبَسُهُ أَبَدًا". فَنَبَذَ النَّاسُ خَوَاتِيمَهُمْ"
“Kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitengeneza pete ya dhahabu. Alikuwa anapoivaa, huigeuza stoni yake kuwa ndani ya tumbo la kiganja chake. Watu walipomwona, nao pia wakatengeneza pete. Kisha baadaye alikuja akakaa juu ya mimbari, halafu akaitoa kwa nguvu na kusema: “Hakika mimi nilikuwa navaa pete hii na kuelekeza stoni yake kwa ndani”, kisha akaitupa. Halafu akasema: Wa Allaah! Sitoivaa tena kamwe”. Na watu nao wakazitupa pete zao”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (2090)].
2- Abu Hurayrah:
"أَنَّهُ نَهَى عَنْ خَاتَمِ الذَهّبِ"
“Kwamba (Rasuli) amekataza pete ya dhahabu”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5863)].
3- Abu Hurayrah:
"أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ رَأَى خَاتَمًا مِنْ ذَهَبٍ فِي يَدِ رَجُلٍ فَنَزَعَهُ فَطَرَحَهُ فَقَالَ: يَعْمِدُ أَحَدُكُمْ إِلَى جَمْرَةٍ مِنْ نَارٍ فَيَجْعَلُهَا فِي يَدِهِ؟ فَقَالُوْا لِلرَّجُلِ بَعْدَمَا ذَهَبَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: خُذْ خَاتَمَكَ فَانْتَفِعْ بِهِ. قَالَ: لَا، وَاللَّهِ لَا آخُذُهُ أَبَدًا وَقَدْ طَرَحَهُ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ"
“Kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliona pete ya dhahabu kwenye kidole cha mtu mmoja, akaitoa na kuitupa, kisha akamwambia: Inakuwaje mmoja wenu anakipania kijinga cha moto akakiweka kwenye mkono wake?! Watu wakamwambia mtu yule baada ya Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuondoka: Ichukue pete yako upate kunufaika nayo. Akasema: Hapana. Naapa kwa Allaah kwamba sitoichukua kamwe madhali Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameitupa”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (2090)].
4- Abu Umaamah: Kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"مَنْ كَانَ يُؤْمِنُ باللهِ وَاليَومِ الآخِرِ فَلَا يَلْبَسْ حَرِيْرًا وَلاَ ذَهَبًا"
“Yeyote ambaye anamwamini Allaah na Siku ya Mwisho, basi asivae hariri wala dhahabu”. [Hadiyth Hasan. Imekharijiwa na Ahmad (5/261), Al-Haakim (4/212) na At-Twabaraaniy (8/186)].
5- Hadiyth iliyotangulia ya ‘Aliy (Radhwiya Allaah ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"حُرِّمَ لِبَاسُ الْحَرِيرِ وَالذَّهَبِ عَلَى ذُكُورِ أُمَّتِي وَأُحِلَّ لإِنَاثِهِمْ"
“Kuvaa hariri na dhahabu kumeharamishwa kwa wanaume wa umati wangu, kumehalalishwa kwa wanawake wao”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (4057), At-Tirmidhiy (1720), An-Nasaaiy (8/160) na Ibn Maajah (3595)].
Kutokana na Hadiyth hizi na nyinginezo, tunapata kujua kwamba ni haramu kwa wanaume kuvaa pete ya dhahabu. Basi je baadhi ya Waislamu watayasikia haya na kuachana na pete za uchumba za dhahabu wanazozivaa kwa kuiga tamaduni za makafiri wanaodai kuwa hilo linaenzi maisha ya ndoa!!
· Hakuna Ubaya Kuvaa Pete Ya Fedha
Kuvaa pete ya fedha kunaruhusiwa kwa wanaume. Anas amesema:
"اتَّخَذَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ خَاتَمًا مِنْ فِضَّةٍ نَقْشُهُ : "مُحَمَّدٌ رَسُولُ اللَّهِ" ، فَكَأَنِّي بِوَبِيصِ -أَوْ بِبَصِيصِ - الْخَاتَمِ فِي إِصْبَعِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَوْ فِي كَفِّهِ"
“Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alichongesha pete ya fedha iliyotiwa nakshi isomekayo: “Muhammad Rasuli wa Allaah”, kana kwamba mimi naona mng’ao wa pete katika kidole cha Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) au katika kijanja chake”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5872) na Muslim (2092)].
· Ni Karaha Kwa Mwanaume Kuvaa Pete Kwenye Kidole Chake Cha Kati Au Cha Shahada
Abu Burdah: ‘Aliy (Radhwiya Allaah ‘anhu) amesema:
"نَهَانِي رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنْ أَتَخَتَّمَ فِي إِصْبَعِي هَذِهِ أَوْ هَذِهِ قَالَ: فَأَوْمَأَ إِلَى الْوُسْطَى وَالَّتِي تَلِيهَا"
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alinikataza kuvaa pete katika kidole changu hiki au hiki. Akaashiria cha kati na cha shahada”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (2078), Abu Daawuwd (4225), At-Tirmidhiy (1786) na An-Nasaaiy (5210)].
Na katika tamko jingine: “Akaashiria kidole chake cha shahada na cha kati”.
An-Nawawiy (Rahimahul Laah) amesema: “Waislamu wote wamekubaliana kwamba ilivyo sunnah, ni mwanaume kuvaa pete kwenye kidole kidogo cha mwisho. Ama mwanamke, yeye anavaa pete kwenye vidole vyake vyote. Ni karaha kwa mwanaume kuvaa kwenye kidole chake cha kati na cha shahada kutokana na Hadiyth hii, nayo ni karaha hafifu “tanziyh”. [Sharhu Muslim cha An-Nawawiy (14/71)].
· Je, Kutumia Dhahabu Kwa Dharura Kunaruhusiwa?
"عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ طَرَفَةَ أَنَّ جَدَّهُ عَرْفَجَةَ بن أَسْعَد قُطِعَ أَنْفُهُ يَوْمَ الْكُلَابِ ، فَاتَّخَذَ أَنْفًا مِنْ وَرِقٍ فَأَنْتَنَ عَلَيْهِ ، فَأَمَرَهُ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنْ يَتَّخِذَ أَنْفًا مِنْ ذَهَبٍ"
Toka kwa ‘Abdurrahmaan bin Twarafah toka kwa babu yake ‘Arfajah bin As-’ad: “Kwamba alikatwa pua katika vita vya Al-Kulaab (enzi ya ujahili). Akatengeneza pua ya silva, lakini ilimwozea. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwamuru atengeneze pua ya dhahabu”. [Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh. Imekharijiwa na Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy na An-Nasaaiy (4/164)].
Al-Khattwaabiy amesema: “Hadiyth hii inatufahamisha kwamba inaruhusiwa kutumia dhahabu kidogo kwa wanaume kutokana na dharura kama kukazia meno na mfano wa hayo”. [Tuhfat Al-Ahwadhiy (11/198)].
Na hii ni kauli ya ’Ulamaa wengi.
Ninasema: “Ama kwa jambo lisilo la dharura, uharamu utabakia pale pale kwa wanaume. Hairuhusiwi kuweka vifungo vya dhahabu kwenye nguo au kuvaa saa ya dhahabu, kwa kuwa hakuna dharura kwa mambo kama haya. Kufanya hivyo bila dharura, kunahesabiwa kuwa ni israfu, kibri, na kujiona. Allaah Ndiye Mjuzi zaidi”.
Na haya yote ni kwa upande wa wanaume. Ama kwa wanawake, dhahabu kwao kiasili inaruhusiwa ijapokuwa bila dharura kama ilivyotangulia.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ وَأَحْكَامُ النَّظَرِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia
اللِّبَاسُ وَالزِّيْنَةُ للرِّجَالِ
Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume
Alhidaaya.com [3]
016- Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume: Wanaume Kujipaka Wanja:
Hakuna ubaya kwa wanaume kupaka wanja ikiwa ni kwa ajili ya kuimarisha nguvu ya kuona, kuondosha utando wa jicho, kulisafisha na kulitwaharisha, au kwa ajili ya tiba, na hususan ikiwa ni kwa wanja asili wa “Al-Ithmid”. Na hii ni kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"وَإِنَّ خَيْرَ أَكْحَالِكُمُ الإِثْمِدُ، يَجْلُو الْبَصَرَ، وَيُنْبِتُ الشَّعْرَ"
“Na hakika wanja wenu ulio bora zaidi ni wa “ithmid”, unasafisha macho, unaotesha kope”. [Hadiyth Hasan. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (3878), At-Tirmidhiy (994), An-Nasaaiy (8/15) na Ibn Maajah (3497)].
Ama kutia wanja kwa ajili ya kujipamba na kujitengeneza, kwa hili, hakuna Hadiyth yoyote iliyothibiti. Imesimuliwa kwamba: “Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akitia wanja kwenye jicho lake la kulia mara tatu, na la kushoto mara mbili”. Lakini Hadiyth hii haikuthibiti.
Inavyoonekana ni kwamba si katika Sunnah kama wanavyoitakidi watu wengi.
Al-‘Allaamah Ibn ‘Uthaymiyn amesema: “Ama wanaume, hapo ni pa kutafitiwa zaidi, na mimi siko huku wala kule. Lakini hata hivyo, suala hili linaweza kupambanuliwa kati ya kijana ambaye inahofiwa fitna kama atajipaka, huyu haruhusiwi, na kati ya mtu mzima ambaye hahofiwi lolote, huyu hakatazwi”. [Fataawaa Ziynatil Mar-at wat-Tajmiyl (uk.51)].
Ninasema: “Ama kwa mwanamke, hili linatakiwa na hususan kujipamba kwa ajili ya mumewe”.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ وَأَحْكَامُ النَّظَرِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia
اللِّبَاسُ وَالزِّيْنَةُ للرِّجَالِ
Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume
Alhidaaya.com [3]
017- Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume: Wanaume Kujipaka Zafarani Au Hina:
· Ni Marufuku Kujipaka Zafarani
Zafarani ni mmea wa kinjano ambao hutumika kwa kutia rangi nguo, na kama manukato kwa wanawake ambao hujipaka nao mwili. Haijuzu kwa mwanaume kuutumia.
Anas amesema:
"نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنْ يَتَزَعْفَرَ الرَّجُلُ"
“Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza mwanaume kutumia zafarani”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5846) na Muslim (1101)].
‘Ammaar bin Yaasir: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalhi wa sallam) amesema:
"ثَلَاثٌ لَا تَقْرَبُهُمُ الْمَلَائِكَةُ :جِيفَةُ الْكَافِرِ ، وَالْمُتَضَمِّخُ بِالْخَلُوقِ ، وَالْجُنُبُ إِلَّا أَنْ يتَوَضَّأ"
“Watu watatu hawakurubiwi na Malaika: Mzoga wa kafiri, mwenye kujipaka “khaluwq”, na mwenye janaba mpaka atawadhe”. [Hadiyth Hasan Lighayrihi. Imekharijiwa na Abu Daawuwd, iko kwenye Swahiyh Al-Jaami’i (3061)].
“Khaluwq” ni manukato ya kinjano yaliyotengenezwa kutokana na zafarani, hutumiwa na wanawake tu.
· Je, Mwanaume Anaruhusiwa Kujipaka Mikono Na Miguu Yake Hina Na Mfano Wake?
Abu Hurayrah:
"أُتِيَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِمُخَنَّثٍ قَدْ خَضَبَ يَدَيْهِ وَرِجْلَيْهِ بِالْحِنَّاءِ ، فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَا بَالُ هَذَا؟" . فَقِيلَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، يَتَشَبَّهُ بِالنِّسَاءِ . فَأُمِرَ بِهِ فَنُفِيَ إِلَى النَّقِيعِ ، فَقَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَلاَ نَقْتُلُهُ؟ فَقَالَ: "إِنِّي نُهِيتُ عَنْ قَتْلِ الْمُصَلِّينَ"
“Khanithi aliyekuwa amepaka mikono na miguu yake hina, aliletwa kwa Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akauliza: Ana nini huyu? Akaambiwa: Ee Rasuli wa Allaah, huyu anajifananisha na wanawake. Rasuli akaamuru apelekwe uhamishoni Naqiy. Wakasema: Ee Rasuli wa Allaah! Kwa nini tusimuue? Akasema: Nimekatazwa kuua wenye kuswali”. [Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh. Imekharijiwa na Abu Daawuwd].
Al-Haafidh amesema: “Ama kupaka mikono na miguu, hili haliruhusiwi kwa mwanamume ila kwa matibabu tu”. [Fat-hul Baariy (10/367].
Ninasema: “Na Hadiyth zinazokataza kujipaka zafarani zinatilia nguvu hilo. Ama Hadiyth ya Anas:
“Kwamba Abdurrahmaan bin ‘Awf alikuja kwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa na alama ya kinjano, Rasuli akamuuliza, naye akamweleza kwamba ameoa mwanamke wa Kianswaar”,.. Hadiyth hii haina ubavu wa kutolewa dalili juu ya kujuzu mwanaume kujipaka zafarani, na hasa pale An-Nawawiy alipoweka wazi zaidi kwa kusema: “Unjano huo ulimganda toka kwa mkewe”. [Sharhu Muslim]
Na kwa muktadha huu, wanalolifanya mabwana harusi wengi katika “Usiku Wa Hina” la kutia hina mikono na miguu kabla ya ndoa, jambo hili halijuzu. Allaah Ndiye Ajuaye zaidi.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ وَأَحْكَامُ النَّظَرِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia
اللِّبَاسُ وَالزِّيْنَةُ للرِّجَالِ
Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume
Alhidaaya.com [3]
018- Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume: Kutumia Manukato Mazuri:
Kutumia manukato (mafuta) mazuri kwa mwanaume ni katika mapambo yenye kupendelewa. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إِنَّ خَيْرَ طِيبِ الرِّجَالِ مَا ظَهَرَ رِيحُهُ وَخَفِيَ لَوْنُهُ ، وَخَيْرَ طِيبِ النِّسَاءِ مَا ظَهَرَ لَوْنُهُ وَخَفِيَ رِيحُهُ"
“Hakika manukato bora zaidi kwa wanaume ni yale yenye kusikika harufu, yasiyoonekana rangi yake, na manukato bora zaidi kwa wanawake ni yale yenye kuonekana rangi yake, yasiyosikika harufu”. [Hasanun Lighayrih. Imekharijiwa na At-Tirmidhiy (2788) na Abu Daawuwd (2174)].
Toka kwa ‘Aaishah:
"كُنْتُ أُطَيِّبُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِأَطْيَبِ مَا نَجِدُ حَتَّى أَجِدَ وَبِيصَ الطِّيبِ فِي رَأْسِهِ وَلِحْيَتِهِ"
“Nilikuwa nikimtia Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mafuta mazuri zaidi tunayokuwa nayo mpaka naona mng’ao wa mafuta kwenye kichwa chake na ndevu zake”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5923) na Muslim (1190)].
Ibn Battwaal amesema: “Tunafahamu kutokana na Hadiyth hii kwamba mwanaume hapaki mafuta mazuri usoni mwake kinyume na akina mama. Akina mama kwa maumbile yao hujipodoa nyuso zao na kujiremba kwa mafuta hayo na mengine kinyume na akina baba. Mwanaume haruhusiwi kisharia kujitia mafuta usoni ili asije kujifananisha na wanawake”. [Al-Fat-hu (10/366)].
Na kama alivyosema Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"أَطْيَبُ الطِّيبِ الْمِسْكُ"
“Manukato mazuri zaidi ni miski”. [Hadiyh Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (2252)].
· Usikatae Mafuta Mazuri Ukipewa
Anas alikuwa hakatai mafuta mazuri, na amesema:
"أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ لَا يَرُدُّ الطِّيبَ"
“Kwamba Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa hakatai mafuta mazuri”. [Hadiyh Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5929), na mfano wake iko kwenye Swahiyhul Jaami’i (4852)].
Na Rasuli (Swalla Allaah ‘alahyi wa aalihi wa sallam) amesema:
"مَنْ عُرِضَ عَلَيْهِ رَيْحَانٌ فَلَا يَرُدُّهُ فَإِنَّهُ خَفِيفُ الْمَحْمَلِ طَيِّبُ الرّيح"
“Atakayetunukiwa rayhani basi asiikatae, kwa kuwa inabebeka kirahisi, ina harufu njema”. [Hadiyh Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (2253), Abu Daawuwd, An-Nasaaiy, kwao iko “Twiyb” badala ya “Rayhani”].
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/284
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11188&title=09A-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20%D9%83%D9%90%D8%AA%D8%A7%D8%A8%D9%8F%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%91%D9%90%D8%A8%D8%A7%D8%B3%D9%90%20%D9%88%D9%8E%D8%A7%D9%84%D8%B2%D9%91%D9%90%D9%8A%D9%86%D9%8E%D8%A9%D9%90%20%D9%88%D9%8E%D8%A3%D9%8E%D8%AD%D9%92%D9%83%D8%A7%D9%85%D9%90%20%D8%A7%D9%84%D9%86%D9%91%D9%8E%D8%B8%D9%8E%D8%B1%20-%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%91%D9%90%D8%A8%D9%8E%D8%A7%D8%B3%D9%8F%20%D9%88%D9%8E%D8%A7%D9%84%D8%B2%D9%91%D9%90%D9%8A%D9%92%D9%86%D9%8E%D8%A9%D9%8F%20%D9%84%D9%84%D8%B1%D9%91%D9%90%D8%AC%D9%8E%D8%A7%D9%84%D9%90%20%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Kwa%20Wanaume%20
[3] http://www.alhidaaya.com/
[4] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11469&title=001-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Kwa%20Wanaume%3A%20Wajibu%20Wa%20Kusitiri%20Uchi%3A%20
[5] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11470&title=002-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Kwa%20Wanaume%3AMpaka%20Wa%20Uchi%20Wa%20Mwanaume%3A
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11471&title=003-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Kwa%20Wanaume%3A%20Vivazi%20Vinavyoruhusiwa%20Na%20Vinavyopendeza%20Zaidi%20Kuvaliwa%20Na%20Wanaume
[7] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11472&title=004-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Kwa%20Wanaume%3AVivazi%20Vinavyoruhusiwa%20Na%20Vinavyopendeza%20Zaidi%20Kuvaliwa%20Na%20Wanaume%3A%20Kanzu%20Ndio%20Vazi%20Bora%20Zaidi
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11473&title=005-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Kwa%20Wanaume%3AVivazi%20Vinavyoruhusiwa%20Na%20Vinavyopendeza%20Zaidi%20Kuvaliwa%20Na%20Wanaume%3A%20Inapendeza%20Kuvaa%20Kilemba
[9] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11474&title=006-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Kwa%20Wanaume%3A%20Vivazi%20Vilivyokatazwa%20Kwa%20Wanaume%20Kuvivaa%3A%20Kuvaa%20Mavazi%20Mahsusi%20Kwa%20Wanawake
[10] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11475&title=007-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Kwa%20Wanaume%3AVivazi%20Vilivyokatazwa%20Kwa%20Wanaume%20Kuvivaa%3A%20%20Kuvaa%20Hariri%20Safi%20Isiyochanganywa
[11] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11476&title=008-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Kwa%20Wanaume%3AVivazi%20Vilivyokatazwa%20Kwa%20Wanaume%20Kuvivaa%3A%20Ni%20Haramu%20Kuvaa%20Nguo%20Ya%20Kipekee%20Ili%20Kuonekana%20Tofauti%20%28Vazi%20La%20Umashuhuri%29
[12] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11477&title=009-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Kwa%20Wanaume%3AVivazi%20Vilivyokatazwa%20Kwa%20Wanaume%20Kuvivaa%3A%20%20Je%2C%20Ni%20Karaha%20Kwa%20Mwanaume%20Kuvaa%20Vazi%20Jekundu%3F
[13] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11478&title=010-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Kwa%20Wanaume%3AVivazi%20Vilivyokatazwa%20Kwa%20Wanaume%20Kuvivaa%3A%20%20Nguo%20Ya%20Rangi%20Ya%20Zafarani
[14] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11479&title=011-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Kwa%20Wanaume%3AVivazi%20Vilivyokatazwa%20Kwa%20Wanaume%20Kuvivaa%3A%20%20Nguo%20Yenye%20Msalaba
[15] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11480&title=012-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Kwa%20Wanaume%3AVivazi%20Vilivyokatazwa%20Kwa%20Wanaume%20Kuvivaa%3A%20%20Nguo%20Iliyotengenezwa%20Kwa%20Ngozi%20Ya%20Wanyama%20Wakali
[16] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11481&title=013-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Kwa%20Wanaume%3A%20Adabu%20Za%20Kuvaa
[17] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11482&title=014-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Kwa%20Wanaume%3A%20Pambo%20La%20Nywele
[18] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11483&title=015-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Kwa%20Wanaume%3APambo%20La%20Pete%20Na%20Mfano%20Wake
[19] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11484&title=016-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Kwa%20Wanaume%3AWanaume%20Kujipaka%20Wanja
[20] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11485&title=017-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Kwa%20Wanaume%3A%20Wanaume%20Kujipaka%20Zafarani%20Au%20Hina
[21] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11486&title=018-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Kwa%20Wanaume%3A%20Kutumia%20Manukato%20Mazuri