كِتابُ اللِّباسِ وَالزِّينَةِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo
الزِّيْنَةُ للمَرْأَةِ المُسْلِمَةِ
Pambo La Mwanamke Wa Kiislamu
Abu Maalik Kamaal Bin As-Sayyid Saalim
Imetarjumiwa na 'Abdullaah Mu'aawiyah (Abu Baasim)
Alhidaaya.com
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo
الزِّيْنَةُ للمَرْأَةِ المُسْلِمَةِ
Pambo Kwa Mwanamke Wa Kiislamu
Alhidaaya.com [3]
001-Mambo Mawili Muhimu Kuyajua:
Imeshaelezwa nyuma kwamba mwanamke haruhusiwi kuonyesha pambo lake isipokuwa kwa mumewe, au maharimu zake, au wanawake wenzake na wengineo wote waliotajwa. Katika suala hili, yamebakia mambo mawili ambayo ni lazima yajulikane:
La kwanza: Ni kwamba pambo ambalo mwanamke analionyesha kwa watajwa hawa linatofautiana na kuzidiana. Pambo analolionyesha kwa mumewe si sawa na analolionyesha kwa baba yake au kaka yake, na analolionyesha kwa baba yake na kaka yake si sawa na analolionyesha kwa mume wa baba yake na kuendelea. Jambo hili bila shaka liko wazi.
La pili: Kujipamba kwake kwa mumewe kuna mipaka, hakuachiwa ajipambe tu. Kwa mfano, haruhusiwi kujipamba kwa kitu kilichoharamishwa, au cha kujifananisha na wanaume, au chenye kugeuza uumbaji wa Allaah, au kilicho maalum kwa mapambo ya wanawake wa kikafiri na vitakavyobainika katika yanayokuja.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo
الزِّيْنَةُ للمَرْأَةِ المُسْلِمَةِ
Pambo Kwa Mwanamke Wa Kiislamu
Alhidaaya.com [3]
02-Aina Za Mapambo Ambayo Mwanamke Anajipambia
1-Pambo La Nywele:
Inapendeza kwa mwanamke kuzitunza vyema nywele zake kwa kuzichana, kuzitia mafuta, kuziosha na mfano wa hivyo ili aonekane mbele ya mumewe kwa mandhari inayomfurahisha. Na bila shaka kumfurahisha mume ni jambo linalotakiwa kisharia. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipoulizwa kuhusu mwanamke bora kabisa alijibu:
"الَّتِي تُطِيعُهُ إِذَا أَمَرَ، وتَسُرُّهُ إِذَا نَظَرَ، وَتَحْفَظُهُ فِي نَفْسِهَا وَمَالِهِ"
“Ni yule ambaye anamsikiliza anapomwamrisha, anamfurahisha anapomwangalia, na anamlinda kwa kuuhifadhi mwili wake (na machafu) na mali yake. [An-Nasaaiy: (6/68) kwa Sanad Swahiyh].
Na kwa sababu hii, Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anawakataza Maswahaba wake wanaporudi kutoka safari kuingia nyumbani kwa wake zao usiku kwa kuchelea mtu kumkuta mkewe katika mandhari isiyoridhisha. Alikuwa akisema:
"أَمْهِلُوا حَتَّى لا نَدْخُلَ لَيْلاً ، كَىْ تَمْتَشِطَ الشَّعِثَةُ وَتَسْتَحِدَّ الْمُغِيبَةُ "
“Vuteni muda tusipate kuingia (majumbani) usiku, ili mwenye nywele zilizokaa ovyo ovyo apate muda wa kuzitengeneza, na anyoe kinena ambaye mumewe amekuwa mbali naye”. [Al-Bukhaariy (579) na Muslim (715)]
Na Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anasema:
"مَنْ كَانَ لَهُ شَعْرٌ فَلْيُكْرِمْهُ"
“Mwenye nywele, basi azienzi na kuzitunza”. [Abu Daawuwd (4163) kwa Sanad Hasan].
Miongoni Mwa Adabu Za Kuchana Nywele:
1- Kuanza upande wa kulia wa kichwa
Ni kwa Hadiyth ya ‘Aaishah:
"كَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يُحِبُّ التَّيَمُّنَ مَا اسْتَطَاعَ فِي طُهُورِهِ وَتَنَعُّلِهِ وَتَرَجُّلِهِ"
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapenda kuanzia kulia kiasi awezavyo wakati anapojitwaharisha, anapovaa viatu na anapochana nywele zake”. [Sunan An-Nasaai (26)]
2- Kuzitia mafuta na kuzilainisha kwa maji kama zimetutumka
Ni kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wakati alipomwona mtu mwenye nywele zilizosimama vibaya:
"أَمَا يَجِدُ هَذَا مَا يُسَكِّنُ بِهِ شَعْرَهُ "
“Je, hawezi kupata huyu chochote akazilainisha nywele zake?!” [Abu Daawuwd (4062) na An-Nasaaiy (8/183) kwa Sanad Swahiyh]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo
الزِّيْنَةُ للمَرْأَةِ المُسْلِمَةِ
Pambo Kwa Mwanamke Wa Kiislamu
Alhidaaya.com [3]
03-Hairuhusiwi Kuunganisha Nywele Asili Na Za Bandia (Kuvaa Wigi):
Asmaa (Radhwiya Allaah ‘anhaa) amesema:
"لَعَنَ اللَّهُ الْوَاصِلَةَ وَالْمُسْتَوْصِلَةَ"
“Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amemlaani msusi wa kuunganisha nywele bandia na mwenye kutaka kuunganishiwa”. [Al-Bukhaariy (5936) na Muslim (2122)]
Kuvaa wigi kunaingia pia ndani ya duara la uharamu hata kama mwanamke ana tatizo la kukatika nywele zake. Na hii ni kwa riwaayah nyingine ya Asmaa (Radhwiya Allaah ‘anhaa):
"أَنَّ امْرَأَةً جَاءَتْ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَتْ: إِنِّي أَنْكَحْتُ ابْنَتِي، ثُمَّ أَصَابَهَا شَكْوَى فَتَمَرَّقَ رَأْسُهَا، وَزَوْجُهَا يَسْتَحِثُّنِي بِهَا، أَفَأَصِلُ رَأْسَهَا؟ فَسَبَّ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الْوَاصِلَةَ وَالْمُسْتَوْصِلَةَ"
“Kwamba mwanamke mmoja alikuja kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kumwambia: Mimi nimemwoza binti yangu, kisha amepatwa na ugonjwa wa kunyonyoka nywele, na mumewe amenishikilia nimtafutie namna. Je, naweza kumuunganishia nywele bandia? Hapo hapo Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamlaani muunganishaji na anayetaka kuunganishiwa nywele bandia. [Al-Bukhaariy 5935) na Muslim (2122)]
Na imesimuliwa pia kwamba Mu’aawiyah bin Abu Sufyaan alichukua furushi la nywele lililokuwa mkononi mwa mmoja wa walinzi wake akasema:
"أَيْنَ عُلَمَاؤُكُمْ؟ سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَنْهَى عَنْ مِثْلِ هَذِهِ وَيَقُولُ: "إِنَّمَا هَلَكَتْ بَنُو إِسْرَائِيلَ حِينَ اتَّخَذَتْ هَذِهِ نِسَاؤُهُمْ"
“Wako wapi ‘Ulamaa wenu? Mimi nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akikataza mfano wa hii akisema: “Hakika waliangamia Baniy Israaiyl wanawake wao walipoanza kutumia hili”. [Al-Bukhaariy (5933) na Muslim (2127)]
Kiufupi, mwanamke haruhusiwi kuunganisha nywele zake na nywele zingine au kuvaa wigi, ni sawasawa iwe kwa ajili ya mumewe au kwa mwingine, kwa kuwa ni haramu.
Je, Inafaa Kuunganisha Nywele Kwa Nyuzi Za Hariri Au Sufi Na Mfano Wa Hivi Ambavyo Si Nywele?
Kauli yenye nguvu kati ya kauli mbili za ‘Ulamaa inasema kwamba inaruhusiwa mwanamke kuunganisha nywele zake kwa nyuzi za hariri, au za sufi, au za kitambaa ambazo hazifanani na nywele. Kutumia hizi hakuzingatiwi kama kuunganisha, na wala hakuingii ndani ya maana kusudiwa ya kuunganisha, bali ni kujipamba na kujiremba. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi. [An-Nawawiy ameinukulu toka kwa Al-Qaadhwiy ‘Ayyaadh. Ahmad bin Hanbal amepondokea kwenye kauli hii]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo
الزِّيْنَةُ للمَرْأَةِ المُسْلِمَةِ
Pambo Kwa Mwanamke Wa Kiislamu
Alhidaaya.com [3]
04-Kunyoa Kinena Na Kunyofoa Nywele Za Kwapa Ni Katika Sunnah Za Maumbile Asilia (Fitwrah):
Kinena ni sehemu inayounganisha mapaja na fumbatio, na ndipo zinapoota nywele pembezoni mwa utupu. Inapendeza kwa mwanamke ajijengee mazoea ya kunyoa nywele za kinena na kwapa, kwani hilo ni katika Sunan za maumbile asilia zinazopendeza azifanye.
Ni karaha kwa mwanamke na hata kwa mwanaume kuziachia nywele za sehemu hiyo kumea hadi kuwa refu, kwa kuwa kufanya hivyo, kutatoa nafasi ya kukusanyika uchafu na kuwa chanzo cha harufu mbaya itakayomkimbiza mke na mume.
Na kwa ajili hiyo, Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam), ameelekeza nywele hizi zisiachwe kwa zaidi ya siku 40. Anas amesema:
"وُقِّتَ لَنَا فِي قَصِّ الشَّارِبِ وَتَقْلِيمِ الْأَظْفَارِ وَنَتْفِ الْإِبِطِ وَحَلْقِ الْعَانَةِ أَنْ لَا تُتْرَكَ أَكثر من أَرْبَعِينَ لَيْلَة"
“Tumewekewa muda wa kukata sharubu, kukata kucha, kunyofoa nywele za kwapa na kunyoa kinena, kwamba zisiachwe kwa zaidi ya siku 40”. [Muslim(258), Abu Daawuwd (420), At-Tirmidhiy (2759), An-Nasaaiy (1/15) na Ibn Maajah (295)]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo
الزِّيْنَةُ للمَرْأَةِ المُسْلِمَةِ
Pambo Kwa Mwanamke Wa Kiislamu
Alhidaaya.com [3]
05- "النَّمْصُ" Ni Haramu:
"النَّمْصُ" ina maana mbili. Ya kwanza ni kuondosha nywele za uso wote, na ya pili ni kuondosha nyusi au kuzichonga, si uso wote. Maana hii ya pili ndiyo iliyonukuliwa toka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaah ‘anhaa), na yeye ndiye ajuaye zaidi mfano wa jambo kama hili kuliko mwingine yeyote.
Kuchonga nyusi ni haramu, ni sawa kwa ajili ya mume au kwa mwingine, kwa idhini yake au bila idhini, kwa kuwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"لَعَنَ النَّامِصَةَ وَالْمُتَنَمِّصَةَ"
“Amemlaani mchonga nyusi na mwenye kuchongwa”. [Al-Bukhaariy (5948), Muslim (2125) na wengineo]
Rasuli amekilaani kitendo hiki kwa kuwa ni ubadilishaji wa uumbaji wa Allaah, na hivyo kinakuwa ni haramu kwa mchongaji na mchongwa.
Lakini pamoja na laana hii ya Allaah na Rasuli Wake kwa wanaofanya jambo hili, tunaona -kwa masikitiko makubwa- kuwa jambo hili limeenea sana kwa wanawake wa Kiislamu na hata kwa wanaovaa hijabu kufikia mpaka wa kuonwa ajabu kwa wasiolifanya na kuchezwa shere.
Mwanamke Akitokezewa na Nywele Za Sharubu Au Ndevu Basi Aziondoshe:
Katika baadhi ya hali ambazo si za kawaida, huota kwa baadhi ya wanawake nywele za sharubu au ndevu hadi kutisha. Ikiwa hivyo, anatakikana aziondoshe, kwa sababu atakuwa anarejesha umbile katika asili yake na si kulibadilisha.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo
الزِّيْنَةُ للمَرْأَةِ المُسْلِمَةِ
Pambo Kwa Mwanamke Wa Kiislamu
Alhidaaya.com [3]
06-Pambo La Meno:
Uislamu umehimiza kuyatunza meno, na kwa ajili hiyo, umesunisha kutumia mswaki.
Abu Hurayrah: Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"لَوْلاَ أَنْ أَشُقَّ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ لأَمَرْتُهُمْ بِتَأْخِيرِ الْعِشَاءِ وَبِالسِّوَاكِ عِنْدَ كُلِّ صَلاَةٍ"
“Lau si kuhofia kuwafanyia uzito Waumini, ningeliwaamuru waicheleweshe ‘Ishaa na wapige mswaki wakati wa kila Swalaah”. [Al-Bukhaariy (887) na Muslim (252) na tamshi ni lake]
Ni Haramu Kupasua Mwanya Katika Meno
Hii inafanyika kuonyesha kwamba mtu ana umri mdogo au kwamba meno yake ni mazuri. Kufanya hivi bila kuwa kunahitajika kwa tiba ni haramu, kwa kuwa ni ubadilishaji wa uumbaji wa Allaah na kudanganya.
Rasuli (Swalla Allaah ‘Alayhi wa aalihi wa sallam):
"لَعَنَ الْمُتَفَلِّجَاتِ لِلْحُسْنِ، الْمُغَيِّرَاتِ لخَلْقِ اللَّهِ"
“Amewalaani wanawake wenye kupasua mwanya wa meno ili waonekane wazuri, hao wanabadilisha uumbaji wa Allaah”. [Al-Bukhaariy (4886) na Muslim (2125)]
Akifanya hivi kwa ajili ya matibabu, basi itaruhusiwa. Inaruhusiwa vile vile kuyakaza meno kwa dhahabu kama yatahofiwa kutoka, na pia kupandikiza meno na magego. Haya yote yanaruhusiwa kutokana na dharura. [Al-Mughniy (3/15,16)]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo
الزِّيْنَةُ للمَرْأَةِ المُسْلِمَةِ
Pambo Kwa Mwanamke Wa Kiislamu
Alhidaaya.com [3]
07-Kutumia Mafuta Mazuri:
Kutumia mafuta mazuri ni katika madh-hari ya pambo lililoruhusiwa kwa mwanamke kwa ajili ya mumewe. Anaweza kutumia mafuta yoyote ayapendayo.
Zaynab bint Salamah amesema:
"دَخَلْتُ عَلَى أُمِّ حَبِيبَةَ زَوْجِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ حِينَ تُوُفِّيَ أَبُوهَا أَبُو سُفْيَانَ بْنُ حَرْبٍ، فَدَعَتْ أُمُّ حَبِيبَةَ بِطِيبٍ فِيهِ صُفْرَةٌ خَلُوقٌ أَوْ غَيْرُهُ فَدَهَنَتْ مِنْهُ جَارِيَةً، ثُمَّ مَسَّتْ بِعَارِضَيْهَا، ثُمَّ قَالَتْ وَاللَّهِ مَا لِي بِالطِّيبِ مِنْ حَاجَةٍ، غَيْرَ أَنِّي سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: "لاَ يَحِلُّ لاِمْرَأَةٍ تُؤْمِنُ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الآخِرِ أَنْ تُحِدَّ عَلَى مَيِّتٍ فَوْقَ ثَلاَثِ لَيَالٍ، إِلاَّ عَلَى زَوْجٍ أَرْبَعَةَ أَشْهُرٍ وَعَشْرًا"
“Niliingia kwa Ummu Habiybah mke wa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wakati alipofariki baba yake Abu Sufyaan bin Harb. Ummu Habiybah akaagiza aletewe manukato yenye unjano wa khalouwq na akampaka kijakazi aliyekuwepo, naye akajipaka kidogo mashavuni, halafu akasema: Wallaah, mimi sina haja na mafuta mazuri isipokuwa tu kwa vile nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Si halali kwa mwanamke anayemwamini Allaah na Siku ya mwisho kumuomboleza maiti kwa zaidi ya siku tatu, isipokuwa kwa mumewe, ni miezi minne na siku kumi ”. [Al-Bukhaariy (5334) na Muslim (1486)]
Mwanamke Anaweza Kutumia Mafuta Mazuri Ya Kiume Na Mwanamume Anaweza Kutumia Ya Kike:
Hii ni kwa Hadiyth ya ‘Aaishah:
"أَنَّ امْرَأَةً، سَأَلَتِ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ غُسْلِهَا مِنَ الْمَحِيضِ، فَأَمَرَهَا كَيْفَ تَغْتَسِلُ قَالَ " خُذِي فِرْصَةً مِنْ مِسْكٍ فَتَطَهَّرِي بِهَا ". قَالَتْ كَيْفَ أَتَطَهَّرُ قَالَ " تَطَهَّرِي بِهَا ". قَالَتْ كَيْفَ قَالَ " سُبْحَانَ اللَّهِ تَطَهَّرِي ". فَاجْتَبَذْتُهَا إِلَىَّ فَقُلْتُ تَتَبَّعِي بِهَا أَثَرَ الدَّمِ"
“Kwamba mwanamke mmoja alimuuliza Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) namna ya kuoga josho la hedhi. Rasuli akamwelekeza namna ya kuoga akimwambia: Chukua kipande cha kitambaa kilichotiwa miski ujipanguse nacho (kwenye utupu). Akauliza: Nijipanguse nacho vipi? Akamwambia: Jisafishe nacho. Akauliza: Vipi? Akasema: Subhaanal Laah! Jisafishe. Nikamvutia kwangu nikamwambia: Kipitishe sehemu ilipo athari ya damu”. [Swahiyh Al-Bukhaariy (314)]
Hapa Rasuli amemwelekeza mwanamke yule atumie kitambaa kilichotiwa mafuta ya miski, na mafuta haya ni mahsusi kwa wanaume.
Katika Hadiyth ya Abu Sa’iyd, amezungumzia kupendeza mwanaume ajitie mafuta mazuri Siku ya Ijumaa “hata kama ni ya wanawake”. Hadiyth inasema:
"غُسْلُ يَوْمِ الْجُمُعَةِ عَلَى كُلِّ مُحْتَلِمٍ وَسِوَاكٌ وَيَمَسُّ مِنَ الطِّيبِ مَا قَدَرَ عَلَيْهِ " [وَلَوْ مِنْ طِيبِ الْمَرْأَةِ" ]
“Ni juu ya kila aliyebaleghe kuoga Siku ya Ijumaa na kupiga mswaki, na ajitie mafuta mazuri anayoweza kuyapata [hata kama ni ya wanawake]. [Swahiyh Muslim (846), An-Nasaaiy (1375) na Abu Daawuwd (344)]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo
الزِّيْنَةُ للمَرْأَةِ المُسْلِمَةِ
Pambo Kwa Mwanamke Wa Kiislamu
Alhidaaya.com [3]
08- Kutumia Mafuta Mazuri Yenye Mchanganyo Wa Alcohol (Cologne)
Harufu nyingi za mafuta mazuri zijulikanazo kama “cologne” au “paravan” zinakuwa na mchanganyo wa mada ya alcohol (Ethil). Imethibiti toka kwa madaktari wenye uzoefu na utaalamu kwamba mada hii inalewesha, na kwa mintarafu hiyo, hairuhusiwi kutumia katika manukato kutokana na Kauli Yake Ta’aalaa:
"يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْخَمْرُ وَالْمَيْسِرُ وَالْأَنصَابُ وَالْأَزْلَامُ رِجْسٌ مِّنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ فَاجْتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ"
“Enyi walioamini! Hakika pombe na kamari na masanamu na kutazamia kwa mishale ya kupigia ramli, ni najisi na chukizo kutokana na kazi ya shaytwaan. Basi jiepusheni navyo, mpate kufaulu”. [Al-Maaidah: 90]
Allaah Ta’alaa Ameiita pombe najisi na Akaamuru kuiepuka. Katazo hili la kujiepusha nayo ni jumuishi, kwa maana kwamba hairuhusiwi kunufaika na chochote chenye kulewesha. Na hii ndiyo sababu ya Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuamuru pombe imwagwe baada ya kushuka Aayah ya kuiharamisha. Na lau kama kungelikuwa na manufaa ndani yake, basi Rasuli angebainisha na asingeliamuru imwagwe kama alivyobainisha ruhusa ya kunufaika na ngozi ya mnyama mfu.
Baadhi ya ‘Ulamaa wameruhusu kutumia mafuta haya ikiwa kiwango cha alcohol ni kidogo, na hii itategemea maelezo ya wataalamu wa nyanja hii. Lakini kiakiba ni bora kutoyatumia, au kutumia yasiyo na mchanganyo wa alcohol. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo
الزِّيْنَةُ للمَرْأَةِ المُسْلِمَةِ
Pambo Kwa Mwanamke Wa Kiislamu
Alhidaaya.com [3]
09-Mwanamke Ampake Mumewe Mafuta:
‘Aaishah:
"كُنْتُ أُطَيِّبُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِأَطْيَبِ مَا نَجِدُ حَتَّى أَجِدَ وَبِيصَ الطِّيبِ فِي رَأْسِهِ وَلِحْيَتِهِ"
“Nilikuwa nampaka Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mafuta mazuri zaidi tuliyonayo mpaka naona mng’ao wa mafuta kwenye kichwa chake na ndevu zake”. [Al-Bukhaariy (5923) na Muslim (1190)]
Katika Hadiyth hii, tutagundua kwamba wanaume hawapaki au kupakwa na wake zao mafuta usoni kinyume na wanawake, wao ndio maumbile yao ya kujipodoa uso na kujipamba kwa mafuta mazuri na vinginevyo kinyume na wanaume, wao kufanya hayo ni marufuku ili wasijifananishe na wanawake. [Fat-hul Baariy (10/366)]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo
الزِّيْنَةُ للمَرْأَةِ المُسْلِمَةِ
Pambo Kwa Mwanamke Wa Kiislamu
Alhidaaya.com [3]
10-Mwanamke Akitoka Nyumbani Kwake Kwenda Nje Ni Lazima Aondoshe Harufu Ya Mafuta Mazuri:
Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"أَيُّما امرَأَةٍ اسْتَعْطَرَتْ فَمَرَّتْ بِقَوْمٍ لِيَجِدُوا رِيْحَهَا فَهِيَ زَانِيَةٌ"
“Mwanamke yeyote aliyejitia mafuta mazuri kisha akajipitisha kwa wanaume ili waisikie harufu yake, basi anakuwa ni mwenye kuzini”. [Takhriyj yake imetajwa nyuma]
Na anasema tena Rasuli:
"إِذَا شَهِدَتْ إِحْدَاكُنَّ الْمَسْجِدَ فَلَا تمَسَّ طِيْبًا"
“Akihudhuria mmoja wenu masjid, basi asiguse mafuta mazuri”. [Muslim (334) na An-Nasaaiy katika Al-Kubraa (9425)]
Sheikh Al-Albaaniy (Rahimahul Laah) amesema: “Ikiwa hili ni haramu kwa mwanamke anayekwenda masjid, basi vipi itakuwa hali kwa mwenye kwenda sokoni, au kupita vichochoroni na mabarabarani?! Bila shaka itakuwa ni haramu zaidi na madhambi makubwa zaidi”.
Al-Haythamiy ameeleza katika “Az-Zawaajir” kwamba mwanamke kutoka nyumbani kwake akiwa amejipamba na kujitia mafuta mazuri, ni katika madhambi makubwa hata kama mumewe atamruhusu.
Ninasema: “Ni lazima mwanamke amalizane na harufu za manukato kabla hajatoka nyumbani kwake kwa njia yoyote awezayo kama kuosha na kadhalika”.
Angalizo:
Mwanamke anaweza kutoka nyumbani kwake bila kuwa amejitia manukato lakini akawa amembeba mwanaye ambaye amemtia manukato. Hili halifai, kwa kuwa sababu ya kuvuta macho ya wanaume kwake kutokana na harufu nzuri itakuwa bado iko, na hivyo basi hukmu ya kuwa ni haramu inabakia palepale. Atanabahi kwa hili, na Allaah Ndiye Ajuaye zaidi.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo
الزِّيْنَةُ للمَرْأَةِ المُسْلِمَةِ
Pambo Kwa Mwanamke Wa Kiislamu
Alhidaaya.com [3]
11-Hairuhusiwi Kutumia Mafuta Mazuri, Si Kwa Mume Wala Kwa Mwengine Yeyote Katika Hali Tatu:
Ya kwanza: Baada ya kuhirimia Hajji au ‘Umrah:
Ni kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusiana na aliyehirimia Hajji au ‘Umrah:
"وَلاَ تَلْبَسُوا مِنَ الثِّيَابِ شَيْئًا مَسَّهُ الزَّعْفَرَانُ وَلاَ الْوَرْسُ"
“Wala msivae nguo yoyote iliyoingiwa na zafarani wala wars”…. [Al-Bukhaariy. Takhriyj yake iko kwenye mlango wa Hijja]
Hikma ya kuzuiwa mwanamke aliyehirimia, ni kuwa harufu ya mafuta haya ni katika vichangamshi na vichochezi vya jimai ambayo inaharibu ihraam.
Ya pili: Katika eda
Mwanamke anakatazwa kutumia mafuta mazuri wakati wa eda ya kufiwa na mumewe.
Ya tatu: Anapotoka nyumbani
Na hii ni hata kama atamkusudia mumewe kama tulivyotangulia kugusia hili nyuma kidogo.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo
الزِّيْنَةُ للمَرْأَةِ المُسْلِمَةِ
Pambo Kwa Mwanamke Wa Kiislamu
Alhidaaya.com [3]
12-Pambo La Wanja:
Inapendeza kwa mwanamke ajitie wanja ili kujipamba kwa mumewe. Pia kwa ajili ya dawa kama atasumbuliwa na maumivu ya jicho.
Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"وَإِنَّ خَيْرَ أَكْحَالِكُمُ الإِثْمِدُ، يَجْلُو الْبَصَرَ، وَيُنْبِتُ الشَّعْرَ"
“Na hakika wanja wenu ulio bora zaidi ni wa “al-ithmid”, unasafisha macho, unaotesha kope”. [Hadiyth Hasan. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (3878), At-Tirmidhiy (994), An-Nasaaiy (8/15) na Ibn Maajah (3497)].
Mwanamke haruhusiwi kujitia wanja wakati wa eda ya kufiwa na mumewe.
Haijuzu Kutumia Kichupa Cha Wanja Cha Dhahabu Au Silva
Katika mlango wa vyombo, tulieleza kwamba haijuzu kutumia vyombo vya dhahabu au silva kwa kuwa kufanya hivyo ni sehemu ya israfu, kibri, kuvunja nyoyo za masikini na mfano wa hayo.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo
الزِّيْنَةُ للمَرْأَةِ المُسْلِمَةِ
Pambo Kwa Mwanamke Wa Kiislamu
Alhidaaya.com [3]
13-Pambo La Kutia Rangi:
Haijuzu kwa mwanamke wala mwanamume kunyofoa mvi. Ni kutokana na neno lake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"لاَ تَنْتِفُوا الشَّيْبَ، مَا مِنْ مُسْلِمٍ يَشِيبُ شَيْبَةً فِي الإِسْلاَمِ إِلاَّ كَانَتْ لَهُ نُورًا يَوْمَ الْقِيَامَةِ "
z
“Msinyofoe mvi, kwani hakuna Muislamu yeyote anayeota mvi akiwa ndani ya Uislamu, isipokuwa zitakuwa ni nuru kwake Siku ya Qiyaamah”. [Abu Daawuwd (4202) kwa Sanad Hasan]
Lakini, pamoja na katazo hilo, inaruhusiwa kuzitia nywele rangi njano au nyekundu. Ni kwa Hadiyth ya Abu Hurayrah (Radhwiya Allaah ‘anhu) kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إِنَّ الْيَهُودَ وَالنَّصَارَى لَا يَصْبِغُوْنَ فَخَالِفُوْهُمْ"
“Hakika Mayahudi na Manaswara hawatii rangi nywele, basi wakhalifuni”. [Al-Bukhaariy (3462) na Muslim (2103)]
Kibora zaidi cha kubadilisha rangi nywele ni hina na “katam”. “Katam” ni majani ya mti wa salam (mimosa tree).
Abu Dharr:
"إِنَّ أَحْسَنَ مَا غَيَّرْتُمْ بِهِ الشَّيْبَ الْحِنَّاءُ وَالْكَتَمُ"
“Hakika kizuri zaidi mnachobadilishia kwacho rangi mvi, ni hina na katam”. [At-Tirmidhiy (1573), An-Nasaaiy (8/139) na Ibn Maajah (3622). Kuna mvutano kwenye Sanad yake]
Hina inajulikana na wote, na katam ni mmea ambao hutumiwa kutilia rangi.
Kutia nywele rangi nyeusi ni haramu. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipoona nywele na ndevu za Abu Quhaafah nyeupe mithili ya hisopo siku ya ukombozi wa Makkah alisema:
"غَيِّرُوا هَذَا بِشَيْءٍ وَاجْتَنِبُوا السَّواد"
“Badilisheni hii kwa chochote, lakini epukeni nyeusi”. [Muslim (2102), An-Nasaaiy (5076) na Abu Daawuwd (4204)]
Inaruhusiwa Kupaka Hina Au Katam Wakati Wa Hedhi:
Toka kwa Mu’aadhah:
"أَنَّ امْرَأَةً سَأَلَتْ عَائِشَةَ: تَخْتَضِبُ الخَائِضُ؟ فَقَالَت: قَدْ كُنَّا عِنْدَ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ نَخْتَضِبُ، فَلَمْ يَكُنْ يَنْهَانَا عَنْهُ"
“Kwamba mwanamke mmoja alimuuliza ‘Aaishah kama mwenye hedhi anaweza kupaka hina (au rangi). Akasema: Tulikuwa tunapaka tukiwa na Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na hakuwa akitukataza hilo”. [Ibn Maajah (656) kwa Sanad Swahiyh]
Kadhalika, inaruhusiwa wakati wa twahara, lakini ni lazima aiondoshe akitaka kutawadha kama itakuwa inazuia maji kufika kwenye ngozi. Ibn ‘Abbaas amesema:
"كُنَّ نِسَاءَنَا يَخْتَضِبْنَ بِاللَّيْلِ، فَإِذَا أَصْبَحْنَ، فَتَحْنَهُ فَتَوَضَّأْنَ وَصَلَّيْنَ، ثُمَّ يَخْتَضِبْنَ بَعْدَ الصَّلَاةِ، فَإِذَا كَانَ عِنْدَ الظُّهْرِ، فَتَحْنَهُ فَتَوَضَّأْنَ وَصَلَّيْنَ فَأَحْسَنَّ خِضَابًا، وَلَا يَمْنَعُ مِنَ الصَّلَاةِ "
“Wake zetu walikuwa wakijitia hina (au katam) usiku, na wanapopambaukiwa wanaitoa, wakatawadha na kuswali, kisha baada ya kuswali hujitia tena. Inapofika adhuhuri wanaitoa tena, wakatawadha na kuswali, tena wanaitia vizuri kabisa, na haliwazuii hilo kuswali”. [Ad-Daaramiy (1093) kwa Sanad Swahiyh]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo
الزِّيْنَةُ للمَرْأَةِ المُسْلِمَةِ
Pambo Kwa Mwanamke Wa Kiislamu
Alhidaaya.com [3]
14-Vipodozi Na Poda Za Kujipambia Mwili:
Mwanamke anaruhusiwa kutumia aina yoyote ya vipodozi aipendayo kwa ajili ya kujipamba kwa mumewe. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"....وَخَيْرَ طِيبِ النِّسَاءِ مَا ظَهَرَ لَوْنُهُ وَخَفِيَ رِيحُهُ"
“… na mafuta mazuri zaidi kwa mwanamke ni yale yenye rangi inayoonekana, yasiyo na harufu”. [At-Tirmidhiy (2788) na Abu Daawuwd (2174). Ni Hadiyth Hasan Lighayrih]
Kati ya linalotilia nguvu hili, ni Hadiyth ya Anas:
"أَنَّ عَبْدَ الرَّحْمَنِ بْنَ عَوْفٍ جَاءَ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَبِهِ أَثَرُ صُفْرَةٍ ، فَسَأَلَهُ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَأَخْبَرَهُ أَنَّهُ تَزَوَّجَ امْرَأَةً مِنَ الأَنْصَارِ"
“Kwamba ‘Abdurrahmaan bin ‘Awf alikuja kwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa na athari ya rangi njano. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamuuliza imekuwaje? Akamweleza kwamba ameowa mwanamke wa Kianswaar”. [Swahiyhul Bukhaariy (5153)]
Unjano huo ulimganda toka kwa mkewe kwa mujibu wa kauli ya An-Nawawiy.
Haya yote ni dalili ya kujuzu mwanamke kujipaka vipodozi na poda za kujipamba mwili wake.
Kiufupi, ni ruksa kwa mwanamke kutumia vipodozi madhali tu havionyeshi ila kwa wale tu alioruhusiwa kufanya hivyo, wala isiwe kwa ajili ya kudanganya au kuficha kitu, na wala visisababishe madhara kwa ngozi yake. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi. [Jaami’u Ahkaamin Nisaa (4/418). Na hivi ndivyo walivyofutu Bin Baaz na Bin ‘Uthaymiyn (Rahimahumal Laah]
Angalizo:
Baadhi ya madaktari wanasema kwamba vipodozi vina madhara kwa ngozi. Ikiwa hili litathibiti, basi haitoruhusiwa kuvitumia. Dk. Mustwafa Husayn ‘Abdul Maqsoud mbobezi wa magonjwa ya ngozi na uzazi katika Chuo Kikuu cha Tanta nchini Misri amesema:
“Vipodozi vinavyotengenezwa hivi sasa vina madhara makubwa sana kwa ngozi kama ifuatavyo:
Kwanza: Madhara ya vipodozi
1- Husababisha ngozi kudumaa na kusinyaa, na hii hupelekea kuzeeka ngozi mapema.
2- Husababisha ngozi kukauka na kupasuka.
3- Husababisha ngozi kuvimba, kuwashwa na kupata ukurutu (eczema).
4- Husababisha kubadilika rangi ya ngozi, ima kwa kuongezeka rangi yake na kutokeza mabaka meusi, au kwa kupungua rangi na kutokeza madoa meupe.
5- Baadhi ya rangi za vipodozi hufyonza miale na kusababisha mwasho wa kimiale kwenye ngozi au kuota nywele nyingi usoni.
6- Viambata vya vipodozi vinaweza kupelekea kubadilika muundo wa seli za ngozi, na hii inaweza kusababisha kansa.
7- Krimu huziba vitundu vya kutolea jasho kwenye ngozi na husababisha kumea vipele na chunusi.
8- Vipodozi husababisha chunusi kupwita vikali kwa walionazo na kuchelewesha kuondoka.
Pili: Rangi ya mdomo (Lipstick)
1- Husababisha midomo kukauka na kunyauka, na hatimaye huwasha vikali.
2- Kutumia mara kwa mara husababisha ukurutu (eczima) na kuwashwa, na kunaweza kusababisha kansa kwenye midomo.
3- Mada yenye kutoa rangi hunyonya miale ambayo hujikita kwenye midomo, na hii huongeza rangi na kusawidika midomo kuzungukia kinywa. Haya ni malalamiko ya akina mama wengi wanaotumia rangi za mdomo.
4- Ikichanganyika na chakula au kinywaji, inaweza kufyonza baadhi ya mada ambazo zinaweza kuleta madhara makubwa kwa mwili. [Jarida la Al-Wa-’ayul Islaamiyy la Kuwait toleo nambari 140, ukurasa 93]
Dk. Wajiyh Zaynul ‘Aabidiyna aliandika makala kwenye jarida la Al-Wa-‘ayu Al-Islaamiy akisema:
“Pambo la nywele kwa sasa kwa msichana ni kuzitia mada telezi ijulikanayo “spray” ili zisimame. Mada hii inaweza kusababisha nywele kukatika na kunyonyoka, au inaweza kusababisha madhara kwa konea ya jicho ikiwa italigusa moja kwa moja au kwa namna nyingine. Na huenda matibabu yake yakaendelea kwa miezi kadhaa.
Ama poda na vipodozi vya uso, hivi huleta lengelenge za uso na maambukizi kwenye ngozi. Hali hii huifanya ngozi kuwa na mikunjano kunjano na kuzeeka haraka, na mikunjano hii huacha mstari mkubwa chini ya jicho. Na msichana anapobaleghe baada ya miaka 20, anakuja kusumbuliwa mara kwa mara na mwasho kwenye vigubiko vya jicho (eyelid) kutokana na kope bandia, au mwasho kwenye vigubiko vya jicho kutokana na rangi zinazopakwa juu yake.
Rangi nyekundu ya mdomo inaweza kusababisha uvimbe au kunyauka ngozi yake laini, kwa sababu rangi hii huondosha tabaka lenye kulinda mdomo. Kadhalika, rangi za kucha husababisha wakati mwingine kucha kukatika, au kuvunjika, au kuharibika, au hata maradhi sugu.
Bila shaka mwanadamu kwa maumbile yake ni lazima apate himaya kutokana na viathiri vya nje anavyokabiliana navyo katika maisha yake ya hapa ardhini. Na ngozi ndiyo mstari wa kwanza wa kinga, na kwa kiasi cha tunavyoichunga ndivyo ambavyo tunafaidika zaidi na nguvu yake ya ulinzi. Lakini kwa masikitiko makubwa, ustaarabu wa kisasa unaiharibu nguvu hii ya ulinzi kwa utumiaji wa kupitiliza wa madawa ya kujiremba na viambata vyake”.
Naye Dk. Naadiyah ‘Abdul Hamiyd Swaaleh ambaye ni bingwa wa magonjwa ya macho anasema:
“Vipodozi vya jicho vina viambata vya kemikali kali zinazosababisha madhara kwa macho, kutoka kope, mwasho, majipu kwenye ngozi ya kufunika jicho pamoja na kutokeza vifuko vya duhuni kwenye ngozi hiyo na kukunjana pia. Hatimaye macho huja kuonekana yamechoka, yamekauka, sambamba na kutokeza weusi pembezoni mwa ngozi ya kufunika jicho”.
Dk. Naadiyah anatahadharisha pia kupasiana vipodozi hivi kati ya mtu na mwingine. Tabia hii inapelekea kuambukizana magonjwa ya macho kupitia kalamu na brashi.
Na kwa upande mwingine, madaktari wanasema kwamba mada ambazo wanawake wanapaka kwenye kope zao za asili zina viambata vya chumvi za nickel, au mpira bandia. Mada hizi husababisha mwasho kwenye ngozi ya jicho na kung’ooka kope.
Ama rangi wanazotumia akina mama kupaka pembezoni mwa jicho, madaktari wamefichua ukweli wake wa kitaaluma, nao ni:
1- Rangi nyeusi ni kaboni nyeusi na oksidi nyeusi ya chuma.
2- Rangi bluu ni “bruce” na kemikali buluu.
3- Rangi kijani inatokana na "chromium oxide".
4- Rangi ya kahawia ni "iron oxide" iliyounguzwa.
5- Rangi ya njano ni "iron oxide".
Mada zote hizi ni kemikali, nazo husababisha madhara hatari kwa jicho na sehemu za pembezoni mwake.
Kadhalika, madaktari wameeleza kwamba kati ya michanganyiko yake ni mada zinazosababisha athari sugu ya sumu kama “chlorophyll hexate” na “pheniylenediamine”. Athari hii hupelekea vidonda kwenye konea na maambukizi kwenye jicho na hatimaye kope hudondoka.
Ninasema: “Ikiwa mambo ni hivi, basi utumiaji wa vipodozi hivi ni haramu. Lakini ikithibiti kutokuwa na madhara yoyote, basi ni halali. Allaah Ndiye Ajuaye zaidi”.
Angalizo:
Rangi za kucha hazina ubaya kuzitumia kama hazina madhara ya mada za kemikali. Lakini tatizo lake ni kuwa zinazuia maji ya wudhuu kufika kwenye kucha. Kama zitaondoshwa wakati wa kutawadha, basi hakuna ubaya.
Na hapa tunapenda kuwakumbusha akina mama kwamba ni muhimu kukata kucha zao, wasiziachie kurefuka kama wanavyofanya wasichana wengi. Hili ni kinyume na Sunnah ya maumbile asili (fitwrah).
Vile vile, hairuhusiwi kuunganisha kucha na kucha nyingine bandia zilizo ndefu kuliko za asili. Kufanya hivyo ni kubadili umbile la Allaah, kujifananisha na makafiri, na kwenda kinyume na umbile salama.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo
الزِّيْنَةُ للمَرْأَةِ المُسْلِمَةِ
Pambo Kwa Mwanamke Wa Kiislamu
Alhidaaya.com [3]
15-Pambo La Madini:
Mwanamke anaruhusiwa kujipamba kwa aina zote za dhahabu na fedha. ‘Aliyy bin Abiy Twaalib amesema:
"أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَخَذَ حَرِيرًا فَجَعَلَهُ فِي يَمِينِهِ، وَأَخَذَ ذَهَبًا فَجَعَلَهُ فِي شِمَالِهِ، ثُمَّ قَالَ: إِنَّ هَذَيْنِ حَرَامٌ عَلَى ذُكُورِ أُمَّتِي"
“Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alichukua hariri akaiweka kuliani mwake, na akachukua dhahabu akaiweka kushotoni mwake, kisha akasema: Hakika viwili hivi ni haramu kwa wanaume wa umati wangu”. [Abu Daawuwd (4057), An-Nasaaiy (8/160) na Ibn Maajah (3595). Ni Hadiyth Swahiyh]
Mwanamke anaruhusiwa kujipamba kwa bangili, hereni, pete, mkufu wa shingoni, kidani na kadhalika.
Toka kwa ‘Abdullaah bin ‘Amr:
" أَنَّ امْرَأَةً أَتَتْ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَبِنْتٌ لَهَا، فِي يَدِ ابْنَتِهَا مَسَكَتَانِ غَلِيِظَتَانِ مِنْ ذَهَبٍ فَقَالَ لَهَا: أَتُؤَدِّينَ زَكَاةَ هَذِه؟ قَالَتْ: لاَ. قَالَ: "أَيَسُرُّكِ أَنْ يُسَوِّرَكِ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ بِهِمَا يَوْمَ الْقِيَامَةِ سِوَارَيْنِ مِنْ نَارٍ"
“Kwamba mwanamke mmoja alikuja kwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa na binti yake. Binti huyu alikuwa amevaa bangili mbili nzito za dhahabu mkononi. Akamuuliza: Je, unazitolea hizi zaka? Akasema hapana. Akamwambia: Je, uko tayari Allaah Akuvishe badala yake bangili mbili za moto Siku ya Qiyaamah?!” [Abu Daawuwd (1563), At-Tirmidhiy (623) na An-Nasaaiy (5/38) kwa Sanad Hasan]
Katika tukio la Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwatolea wanawake mawaidha Siku ya ‘Iyd, Ibn ‘Abbaas anahadithia kwamba Rasuli alikuwa na Bilaal na akawaamuru akina mama watoe swadaqah. Kila mwanamke akaanza kutoa hereni na pete yake na kuitupia (kwenye kapu la swadaqah). [Imetajwa nyuma mara kadhaa]
Na katika Hadiyth ya Twawbaan:
"فَانْتَزَعَتْ فَاطِمَةُ سِلْسِلَةً فِي عُنُقِهَا مِنْ ذَهَبٍ وَقَالَتْ: هَذِهِ أَهْدَاهَا إِلَىَّ أَبُو حَسَنٍ"
“Faatwimah akautoa mkufu wa dhahabu shingoni mwake na kusema: Abul Hasan amenipa huu zawadi”. [An-Nasaaiy (5140) na Ahmad (21892) kwa Sanad Swahiyh]
Mwanamke anaruhusiwa vilevile kuvaa vikuku nyumbani kwake kwa mumewe. Haruhusiwi kuvionyesha kwa wasio maharimu wala kupiga chini miguu ili wanaume wajue kuwa amevivaa. Na hii ni kwa Kauli Yake Ta’aalaa:
"وَلَا يَضْرِبْنَ بِأَرْجُلِهِنَّ لِيُعْلَمَ مَا يُخْفِينَ مِن زِينَتِهِنَّ"
“Na wala wasipige miguu yao yakajulikana yale wanayoyaficha katika mapambo yao”. [An-Nuwr: 31]
Faida:
Mwanamke anaweza kuvaa pete kidole chochote apendacho, kinyume na mwanaume ambaye anakatazwa kuvaa kwenye kidole cha kati na cha shahada.
Katika Swahiyh Muslim (2078), ‘Aliyy amesema:
" نَهَانِي رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنْ أَتَخَتَّمَ فِي إِصْبَعِي هَذِهِ أَوْ هَذِهِ، فَأَوْمَأَ إِلَى الْوُسْطَى وَالَّتِي تَلِيهَا"
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alinikataza kuvaa pete katika kidole changu hiki au hiki. Akaashiria cha kati na kinachofuatia (cha shahada)”. [Ni Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (2078), At-Tirmidhiy (1786), An-Nasaaiy (5210) na Abu Daawuwd (4225)]
An-Nawawiy amenukuu ‘Ijmaa ya kwamba katazo hili linawahusu wanaume tu pasina wanawake ambao wanaruhusiwa kidole chochote kama ilivyotangulia.
Hakuna Neno Kuvaa Pete Ya Chuma:
Kwa kuwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia Swahaba aliyetaka kuoa na hakuwa na chochote cha kulipia mahari:
"الْتَمِسْ وَلَوْ خَاتَمًا مِنْ حَدِيدِ"
“Tafuta japokuwa pete ya chuma”. [Bukhaariy na Muslim]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo
الزِّيْنَةُ للمَرْأَةِ المُسْلِمَةِ
Pambo Kwa Mwanamke Wa Kiislamu
Alhidaaya.com [3]
16-Tojo (Tattoo) Ni Haramu:
Ibn Mas-‘uwd (Radhwiya Allaah ‘anhu) amesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"لَعَنَ اللَّهُ الْوَاشِمَاتِ وَالْمُسْتَوْشِمَاتِ، والنَّا مِصَاتِ وَالْمُتَنَمِّصَاتِ، وَالْمُتَفَلِّجَاتِ لِلْحُسْنِ، الْمُغَيِّرَاتِ خَلْقَ اللَّهِ"
“Allaah Amewalaani wanawake wenye kuwafanyia tattoo wengine na wenye kufanyiwa, na wenye kuwachonga nyusi wenzao na wenye kuchongwa, na wenye kupasua mwanya wa meno ili waonekane wazuri, hao ni wenye kubadili uumbaji wa Allaah”. [Al-Bukhaariy (4886) na Muslim (2125)]
Tojo kwa kawaida hufanywa kwa kuingiza sindano au mfano wake kwenye mgongo wa kiganja, au mdomo, au sehemu yoyote ya mwili wa mwanamke mpaka damu ikachuruzika, kisha mahala kusudiwa hujazwa hina au mfano wake mpaka pakawa kijani. Tojo hii athari yake inabakia, na haiondoki kwa kuosha au kupita wakati. Na kwa ajili hiyo, imekuwa ni haramu kwa mtendaji na mtendewa aliyetaka kwa hiari yake. Na anayemfanyia hivyo binti mdogo anapata yeye madhambi, lakini binti hapati kwa kuwa bado hajavunja ungo.
Hivi leo pameenea mtindo mpya kwa wasichana wa kuchorwa tojo kwenye kifua na tumbo. Wakati wa kuchorwa, mchoraji ni lazima afunuliwe sehemu hizo ambaye anaweza pia kuwa mwanaume kwenye masaluni ambayo baadhi yake yametenga chumba maalum cha kazi hiyo na kwa bei za juu kabisa!! Kama hiyo haitoshi, akitoka hapo, msichana huanika wazi sehemu hizo kwa watu ili waone michoro hiyo. Haya ndiyo mambo!!
Angalizo:
Ingawa Hadiyth ya Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) imewalenga wanawake tu, lakini pia hata kwa wanaume ni haramu kuchora tattoo. Kwa kuwa wanawake maumbile yao ni kujipamba na kujiremba, na maumbile hayo yamewapeleka hadi kufikia kwenye tattoo. Na mwanaume akifanya hilo, bila shaka itakuwa ni mbaya zaidi.
Faida: Athari Mbaya Za Kitiba Za Kuchora Tojo Kwenye Ngozi:
Bingwa wa magonjwa ya ngozi na uzazi Dk. ‘Abdul Haadiy Muhammad ‘Abdul Ghaffaar anasema kwamba mada ngeni ambazo zinaingia ndani ya ngozi husababisha aleji ya ngozi. Na kama mada hizo zitakuwa na mchanganyiko wa petroli, basi zitasababisha saratani ya ngozi na hatimaye ngozi itapoteza uhai wake. Na utumiaji wa sindano katika kuweka tojo husababisha maambukizi ya homa ya ini (hepatitis) na ukimwi ikiwa itatumiwa na zaidi ya mtu mmoja.
Angalizo:
Siku hizi pameibuka aina nyingine ya tojo ambayo huchorwa kwenye ngozi mfano wa hina, lakini hii inaweza kutoka kwa usahali. Hii kama haina madhara kwa ngozi, basi haina ubaya, kwa kuwa si ugeuzaji wa uumbaji wa Allaah, bali ni kama hina tu, lakini mwanamke anatakiwa asiruhusu kuonwa na yeyote zaidi ya mumewe ingawa kuacha inakuwa ni akiba zaidi ili awe mbali na kujifananisha na wanawake waliolaaniwa kwenye Hadiyth.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo
الزِّيْنَةُ للمَرْأَةِ المُسْلِمَةِ
Pambo Kwa Mwanamke Wa Kiislamu
Alhidaaya.com [3]
17-Hukmu Ya “Plastic Surgery”:
“Plastic Surgery” ina hali mbalimbali. Baadhi yake zinaruhusiwa, kuna ambazo ni lazima, na nyingine ni haramu.
1- Zinazoruhusiwa ni kama kuziba jeraha la kina kirefu, kukarabati jeraha lililopasuka, na kutia kiraka sehemu iliyoungua vibaya na hususan uso au sehemu za mwili zinazoonekana zaidi. Upasuaji wote huu unaingia ndani ya duara la kutengeneza kilichoharibika na kurejesha umbile la asili katika mwili. Haya yote hayana ubaya, bali baadhi yake yanaweza kuwa ni waajib.
2- Kuondosha kasoro ambazo huenda zikawa zimetokea wakati wa ujauzito kutokana na mjamzito kutumia madawa au vinginevyo. Pia kuondosha kilicho kinyume na maumbile ya kawaida kama kidole cha sita na mfano wake. Haya tunataraji kwamba hayana ubaya kwa kuwa hayaingii kwenye duara la kubadili uumbaji wa Allaah Subhaanahu wa Ta’aalaa.
3- Kila linaloingia kwenye duara la kubadili uumbaji wa Allaah linakuwa ni haramu. Allaah Ta’aalaa Ameumba watu wakiwa wametofautiana. Ameumba warefu, wafupi, weusi, weupe, wazuri na wabaya wa sura. Haya yote ni katika alama za kupwekeka Kwake na ubunifu Wake. Yeye Ndiye Mola Mwenye Kutia sura kama Alivyosema:
"هُوَ الَّذِي يُصَوِّرُكُمْ فِي الْأَرْحَامِ كَيْفَ يَشَاءُ ۚ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ "
“Yeye Ndiye Anayekusawirini umbo katika matumbo ya uzazi vile Atakavyo. Hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote. [Aal ‘Imraan: 06]
Na hakuna shaka kwamba kukiuka uumbaji wa Allaah kwa kubadili sura, au rangi, au umbo, kunaingia kwenye duara la kuingilia uumbaji wa Allaah ‘Azza wa Jalla. Hilo Amelikataza Aliposema:
"لَا تَبْدِيلَ لِخَلْقِ اللَّـهِ"
“Hakuna kubadilisha Uumbaji wa Allaah”. [Ar-Ruwm: 30]
Sehemu hii ya Aayah ni agizo, kwa maana kwamba msibadili uumbaji wa Allaah. Na Allaah Ashatujulisha kwamba ibliys atamwamuru mwanadamu abadili uumbaji wa Allaah pale Aliposema:
"إِن يَدْعُونَ مِن دُونِهِ إِلَّا إِنَاثًا وَإِن يَدْعُونَ إِلَّا شَيْطَانًا مَّرِيدًا ﴿١١٧﴾ لَّعَنَهُ اللَّـهُ ۘ وَقَالَ لَأَتَّخِذَنَّ مِنْ عِبَادِكَ نَصِيبًا مَّفْرُوضًا ﴿١١٨﴾ وَلَأُضِلَّنَّهُمْ وَلَأُمَنِّيَنَّهُمْ وَلَآمُرَنَّهُمْ فَلَيُبَتِّكُنَّ آذَانَ الْأَنْعَامِ وَلَآمُرَنَّهُمْ فَلَيُغَيِّرُنَّ خَلْقَ اللَّـهِ ۚ وَمَن يَتَّخِذِ الشَّيْطَانَ وَلِيًّا مِّن دُونِ اللَّـهِ فَقَدْ خَسِرَ خُسْرَانًا مُّبِينًا ﴿١١٩﴾"
“Hawaombi badala Yake isipokuwa miungu ya kike na hawaombi isipokuwa shaytwaan muasi • Allaah Amemlaani. Na (shaytwaan) akasema: Kwa hakika nitashika katika waja Wako sehemu maalumu ● Na hakika nitawapoteza, na nitawashawishi matamanio ya kulaghai, na nitawaamrisha. Basi watakata masikio ya wanyama (wawatukuze), na nitawaamrisha watabadili Uumbaji wa Allaah. Na atakayemfanya shaytwaan kuwa rafiki mwandani badala ya Allaah basi kwa yakini amekhasirika khasara bayana. [An-Nisaa: 117-119]
Na kati ya kazi za shaytwaan za kumpoteza mwanadamu ni kumwamuru abadili umbile la Allaah.
Na hakuna shaka yoyote kwamba operesheni ambazo zinalenga kubadili uumbaji wa Allaah kama kubadili jinsia ya mwanaume kuwa mwanamke na kinyume chake, au kubadilisha rangi (kama kujichubua n.k), au kubadilisha sura ya uso au kiungo chochote cha mwili, hayo yote ni matendo ya kumfuata shaytwaan ambaye kazi yake ni kumpoteza mwanadamu na kumchochea akiuke uumbaji wa Allaah kwa kuubadilisha na kuugeuza.
Hadiyth ya Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) imeyaainisha kwa uwazi baadhi ya mambo ya ubadilishaji uumbaji wa Allaah. Kati ya mambo hayo ni kuchonga meno kwa kuweka mwanya kati ya jino na jino, kuunganisha nywele, kuchonga nyusi zikawa nyembamba, na kuchora tattoo. Ni pale aliposema:
"لَعَنَ اللَّهُ الْوَاشِمَاتِ وَالْمُسْتَوْشِمَاتِ، والنَّا مِصَاتِ وَالْمُتَنَمِّصَاتِ، وَالْمُتَفَلِّجَاتِ لِلْحُسْنِ، الْمُغَيِّرَاتِ خَلْقَ اللَّهِ"
“Allaah Amewalaani wanawake wenye kuwafanyia tattoo wengine na wenye kufanyiwa, na wenye kazi ya kuchonga nyusi na wenye kuchongwa, na wenye kupasua mwanya wa meno ili waonekane wazuri, hao ni wenye kubadili uumbaji wa Allaah”. [Al-Bukhaariy (4886) na Muslim (2125)]
Sababu ya kuharamishwa mambo haya kwa mujibu wa Hadiyth hii ya Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam), ni kuwa yote ni ubadilishaji wa uumbaji wa Allaah, na kwa hivyo ni haramu kuyafanya.
Na hakuna shaka yoyote kwamba ubadilishaji wa uumbaji wa Allaah ulio haramu zaidi, ni kubadili jinsia ya mtu kutoka mwanamume kwenda mwanamke au kinyume chake. Na hii inakuwa kwa yule ambaye Allaah Amemuumba mwanaume kamili, kisha akataka mwenyewe awe mwanamke na kinyume chake. Ama yule ambaye ameumbwa akiwa na viungo vya kiume na kike (khuntha), huyu ni halali afanyiwe upasuaji wa kumweka katika jinsia iliyoelemea zaidi kwake. Upasuaji huu ni halali kwa kuwa hauingii kwenye duara la kubadili uumbaji wa Allaah, bali ni kurekebisha tatizo au kasoro.
Ama operesheni za kubadili jinsia kwa mtu ambaye ni mwanaume kamili ili awe mwanamke, au awe jinsia ya tatu kama inavyofanyika kwenye baadhi ya nchi hivi sasa ili kuunda jinsia isiyobeba ujauzito ili iweze kutumika kwa starehe tu, jambo hili ni dhambi chafu mno na uchafuzi mbaya sana katika ardhi. Huu ni uhalifu uliopandana, kwa kuwa kwanza ni ubadilishaji wa uumbaji wa Allaah ambao ndio ubadilishaji mkubwa zaidi katika mwili wa mwanadamu kuliko ubadilishaji mwingine wowote. Na pili, ni ubadilishaji wenye lengo la kuharibu jamii na kueneza machafu kwa njia mbaya kabisa za kuchukiza. Ni tendo ovu mno lenye upotevu zaidi kuliko hata hali waliyokuwa nayo kaumu Luwt (‘Alayhis Salaam).
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo
الزِّيْنَةُ للمَرْأَةِ المُسْلِمَةِ
Pambo Kwa Mwanamke Wa Kiislamu
Alhidaaya.com [3]
18-Hukmu Ya Kuvaa Lensi Za Rangi Kama Pambo Na Fasheni:
Sheikh Swaaleh bin Fawazaan aliulizwa hukmu ya kuvaa lensi za rangi kwa ajili ya kujipamba na kwenda na fasheni bila kusahau bei yake ya juu mno, naye akajibu akisema:
“Kuvaa lensi kutokana na dharura hakuna ubaya. Na kama hakuna dharura, basi kuacha inakuwa ni bora zaidi na hususan kama bei yake itakuwa ghali ili kujiepusha na israfu iliyoharamishwa. Mbali na hivyo, inakuwa ni udanganyifu, kwa kuwa inalionyesha jicho kinyume na uhalisia wake ulivyo.
Ama Sheikh Ibn ‘Uthaymiyn, yeye alisema kuhusiana na lensi za kugandisha na jicho kwamba ni lazima kumshauri daktari kujua kama zina madhara kwa jicho au la. Kama zitakuwa na madhara, basi ni haramu kuzitumia, na madhara yoyote yanayoweza kuupata mwili, ni lazima kuyaepuka kutokana na Neno Lake Ta’aalaa:
"وَلَا تَقْتُلُوا أَنفُسَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِكُمْ رَحِيمًا "
“Wala msijiue. Hakika Allaah Ni Mwenye Kuwarehemuni”. [An-Nisaa: 29]
Ama kama madaktari watasema kwamba hazina athari yoyote mbaya wala madhara, hapa itaangaliwa tena, je lensi hizi zinayafanya macho ya mwanamke kuwa kama ya wanyama mfano wa ya kondoo au ya sungura?. Ikiwa ni hivyo, basi hairuhusiwi, kwa kuwa itakuwa ni kujifananisha na wanyama. Kujifananisha na wanyama hakujaelezewa ila kwa sifa mbaya ya kukimbiza kama katika Kauli Yake Ta’aalaa:
"وَاتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ الَّذِي آتَيْنَاهُ آيَاتِنَا فَانسَلَخَ مِنْهَا فَأَتْبَعَهُ الشَّيْطَانُ فَكَانَ مِنَ الْغَاوِينَ ● وَلَوْ شِئْنَا لَرَفَعْنَاهُ بِهَا وَلَـٰكِنَّهُ أَخْلَدَ إِلَى الْأَرْضِ وَاتَّبَعَ هَوَاهُ ۚ فَمَثَلُهُ كَمَثَلِ الْكَلْبِ إِن تَحْمِلْ عَلَيْهِ يَلْهَثْ أَوْ تَتْرُكْهُ يَلْهَث"
“Na wasomee (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) khabari za yule Tuliyempa Aayaat (ishara, dalili) Zetu, akajivua nazo na shaytwaan akamfuata, na akawa miongoni mwa waliopotoka ● Na lau Tungelitaka Tungelimnyanyua kwazo (hizo Aayaat), lakini aligandamana na dunia na akafuata hawaa zake. Basi mfano wake ni kama mfano wa mbwa, ukimhujumu ananing’iniza ulimi nje na kuhema, na ukimwacha pia ananing’iniza ulimi nje na kuhema”. [Al-A’araaf: 175, 176]
Pia Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliposema:
"لَيْسَ لَنَا مَثَلُ السَّوْءِ، الْعَائِدُ فِي هِبَتِهِ كَالْكَلْبِ يَعُودُ فِي قَيْئِهِ"
“Haitakikani kwetu (sisi Waislamu) kuwa mfano wa sifa mbovu. Mwenye kurejelea zawadi aliyotoa ni kama mbwa anayerejea kula matapishi yake”. [Al-Bukhaariy (2589) na Muslim (1622)]
Na pia:
"مَنْ تَكَلَّمَ يَوْمَ الْجُمُعَةِ وَالْإِمَامُ يَخْطُبُ فَهُوَ كَمَثَلِ الْحِمَارِ يَحْمِلُ أَسْفَارًا"
“Anayezungumza Siku ya Ijumaa na imamu anakhutubu, basi ni kama punda anayebeba vitabu”. [Ahmad katika Al-Musnad kwa Sanad Dhwa’iyf. Angalia kwenye Al-Mishkaat nambari (1397)]
Hivyo basi, ikiwa lensi hizi zitalifanya jicho kuwa kama la mnyama, basi kuzivaa ni haramu. Ama ikiwa hazibadilishi umbo la jicho bali zinabadili rangi yake tu kutoka weusi uliokoza kuja weusi uliofifia na mfano wake, basi hakuna ubaya kuzitumia, kwa kuwa hali hii haizingatiwi kuwa ni ubadilishaji wa uumbaji wa Allaah, kwa sababu si hali ya kudumu muda mrefu kama ilivyo tojo. Zinakuwa ni kama miwani ambayo wakati wowote akitaka mtu huivua, ingawa tofauti ya viwili hivi ni kuwa miwani haigusani na jicho lakini lensi zinaligusa jicho moja kwa moja.
Alaa kulli hali, ikiwa mwanamke ataachana nazo, itakuwa ni vizuri na salama zaidi kwa macho yake.
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/284
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11640&title=09D-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20%D9%83%D9%90%D8%AA%D8%A7%D8%A8%D9%8F%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%91%D9%90%D8%A8%D8%A7%D8%B3%D9%90%20%D9%88%D9%8E%D8%A7%D9%84%D8%B2%D9%91%D9%90%D9%8A%D9%86%D9%8E%D8%A9%D9%90%20-%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20%D8%A7%D9%84%D8%B2%D9%91%D9%90%D9%8A%D9%92%D9%86%D9%8E%D8%A9%D9%8F%20%D9%84%D9%84%D9%85%D9%8E%D8%B1%D9%92%D8%A3%D9%8E%D8%A9%D9%90%20%D8%A7%D9%84%D9%85%D9%8F%D8%B3%D9%92%D9%84%D9%90%D9%85%D9%8E%D8%A9%D9%90%3A%20Pambo%20Kwa%20Mwanamke%20Wa%20Kiislamu%20
[3] http://www.alhidaaya.com/
[4] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11641&title=01-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%3A%20Pambo%20Kwa%20Mwanamke%20Wa%20Kiislamu%3A%20Mambo%20Mawili%20Muhimu%20Kuyajua%20%20
[5] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11642&title=02-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%3A%20Pambo%20Kwa%20Mwanamke%20Wa%20Kiislamu%3A%20Aina%20Za%20Mapambo%20Ambayo%20Mwanamke%20Anajipambia
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11643&title=03-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%3A%20Pambo%20Kwa%20Mwanamke%20Wa%20Kiislamu%3A%20Hairuhusiwi%20Kuunganisha%20Nywele%20Asili%20Na%20Za%20Bandia%20%28Kuvaa%20Wigi%29
[7] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11644&title=04-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%3A%20Pambo%20Kwa%20Mwanamke%20Wa%20Kiislamu%3A%20Kunyoa%20Kinena%20Na%20Kunyofoa%20Nywele%20Za%20Kwapa%20Ni%20Katika%20Sunnah%20Za%20Maumbile%20Asilia%20%28Fitwrah%29
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11645&title=05-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%3A%20Pambo%20Kwa%20Mwanamke%20Wa%20Kiislamu%3A%20%22%D8%A7%D9%84%D9%86%D9%91%D9%8E%D9%85%D9%92%D8%B5%D9%8F%22%20Ni%20Haramu
[9] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11646&title=06-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%3A%20Pambo%20Kwa%20Mwanamke%20Wa%20Kiislamu%3A%20Pambo%20La%20Meno%20
[10] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11647&title=07-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%3A%20Pambo%20Kwa%20Mwanamke%20Wa%20Kiislamu%3A%20Kutumia%20Mafuta%20Mazuri
[11] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11648&title=08-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%3A%20Pambo%20Kwa%20Mwanamke%20Wa%20Kiislamu%3A%20Kutumia%20Mafuta%20Mazuri%20Yenye%20Mchanganyo%20Wa%20Alcohol%20%28Cologne%29%20
[12] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11649&title=09-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%3A%20Pambo%20Kwa%20Mwanamke%20Wa%20Kiislamu%3A%20Mwanamke%20Ampake%20Mumewe%20Mafuta
[13] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11650&title=10-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%3A%20Pambo%20Kwa%20Mwanamke%20Wa%20Kiislamu%3A%20Mwanamke%20Akitoka%20Nyumbani%20Kwake%20Kwenda%20Nje%20Ni%20Lazima%20Aondoshe%20Harufu%20Ya%20Mafuta%20Mazuri
[14] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11651&title=11-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%3A%20Pambo%20Kwa%20Mwanamke%20Wa%20Kiislamu%3A%20Hairuhusiwi%20Kutumia%20Mafuta%20Mazuri%2C%20Si%20Kwa%20Mume%20Wala%20Kwa%20Mwengine%20Yeyote%20Katika%20Hali%20Tatu
[15] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11652&title=12-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%3A%20Pambo%20Kwa%20Mwanamke%20Wa%20Kiislamu%3A%20Pambo%20La%20Wanja
[16] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11653&title=13-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%3A%20Pambo%20Kwa%20Mwanamke%20Wa%20Kiislamu%3APambo%20La%20Kutia%20Rangi%20
[17] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11654&title=14-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%3A%20Pambo%20Kwa%20Mwanamke%20Wa%20Kiislamu%3A%20Vipodozi%20Na%20Poda%20Za%20Kujipambia%20Mwili
[18] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11655&title=15-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%3A%20Pambo%20Kwa%20Mwanamke%20Wa%20Kiislamu%3A%20Pambo%20La%20Madini
[19] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11656&title=16-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%3A%20Pambo%20Kwa%20Mwanamke%20Wa%20Kiislamu%3A%20Tojo%20%28Tattoo%29%20Ni%20Haramu%20
[20] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11657&title=17-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%3A%20Pambo%20Kwa%20Mwanamke%20Wa%20Kiislamu%3A%20Hukmu%20Ya%20%E2%80%9CPlastic%20Surgery%E2%80%9D
[21] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11658&title=18-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%3A%20Pambo%20Kwa%20Mwanamke%20Wa%20Kiislamu%3A%20Hukmu%20Ya%20Kuvaa%20Lensi%20Za%20Rangi%20Kama%20Pambo%20Na%20Fasheni%20