KUIREFUSHA RUKUU
Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akifanya rukuu yake, kisimamo chake baada ya rukuu, na sujuud yake na kikao baina sajda mbili, karibu sawa kwa urefu.([1])
KUKATAZWA KUSOMA QUR-AAN KATIKA RUKUU
Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akikataza kusoma Qur-aan katika rukuu na sujuud.([2])
Alikuwa akisema: ((Hakika mimi nimekatazwa kusoma Qur-aan hali ya kuwa nimerukuu au nimesujudu. Hivyo basi katika rukuu mtukuzeni Mola (عزوجل), na (ama) katika sujuud, jitahidini kwa du'aa, kwani ni karibu kukubaliwa humo)).([3])
[1] Al-Bukhaariy na Muslim. Imetolewa katika Irwaa Al-Ghaliyl (331).
[2] Muslim na Abu 'Awaanah. Makatazo ni ya ujumla, hivyo inahusisha Swalah za Faradhi na Sunnah. Ziada ya Ibn 'Asaakir (17/299/1): "Ama Swalah za Sunnah, hakuna ubaya", ni (aidha) shaadhah au munkar. Ibn 'Asaakir ameashiria dosari humo, hivyo haijuzu kufanyiwa kazi.
[3] Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni.
Links
[1] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F3564&title=034-Sifa%20Ya%20Swalah%20Ya%20Mtume%20%28Swalla%20Allaahu%20%27Alayhi%20Wa%20Aalihi%20Wa%20Sallam%29%3A%20Kuirefusha%20Rukuu%20Na%20Kukatazwa%20Kusoma%20Qur-aan%20Katika%20Rukuu