Mlango Wa 54
بَابٌ لا يَقُولُ عَبْدِي وَأَمَتِي
Asiseme Mtu “Mja Wangu”, “Mjakazi Wangu”
فِي اَلصَّحِيحِ عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ) أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((لاَ يَقُلْ أَحَدُكُمْ: أَطْعِمْ رَبَّكَ وَضِّئْ رَبَّكَ وَلْيَقُلْ سَيِّدِي وَمَوْلايَ وَلا يَقُلْ أَحَدُكُمْ: عَبْدِي وَأَمَتِي، وَلْيَقُلْ فَتَايَ وَفَتَاتِي َغُلامِي))
Katika Swahiyh (Al-Bukhaariy) kutoka kwa Abuu Hurayrah(رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Asiseme mmoja wenu: Mlishe Rabbaka [Rabb wako]. Mtawadhishe Rabbaka, bali aseme: Sayyidiy au Mawlaayi [Bwana wangu][1] Na asiseme mtu: ‘Abdiy au Amatiy [mjakazi wangu], bali aseme: Fataay, na Fataatiy [kijana wangu] na ghulaamiy [mvulana wangu])) [Al-Bukhaariy]
Masuala Muhimu Yaliyomo:
1-Kukatazwa kusema: "Mtumwa wangu" au "mjakazi wangu.”
2-Mtumwa asiseme: "Rabb wangu” wala asiambiwe: "Mlishe Rabb wako.”
3-Kumfundisha bwana aseme badala ya hayo: "kijana wangu” “ee bint”, “ee mvulana”
4-Kumfundisha mtumwa kusema badala ya hayo: “sayyidiy” au “bwana wangu.”
5-La muhimu hapa ni kufafanua Tawhiyd kwa ukamilifu, hata kama ni katika maneno, majina na istilahi.
Links
[1] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7910&title=54-Kitaab%20At-Tawhiyd%3A%20Asiseme%20Mtu%20%E2%80%9CMja%20Wangu%E2%80%9D%2C%20%E2%80%9CMjakazi%20Wangu%E2%80%9D