كِتَابُ الزَّكاة
Kitabu Cha Zakaah
بُلُوغُ الْمَرام
Buluwgh Al-Maraam
كِتَابُ اَلزَّكَاةُ
Kitabu Cha Zakaah[1]
Mlango Wa Zakaah Ya Mali
483.
عَنِ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا: {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم بَعَثَ مُعَاذًا رضى الله عنه إِلَى اَلْيَمَنِ...} فَذَكَرَ اَلْحَدِيثَ، وَفِيهِ: {أَنَّ اَللَّهَ قَدِ اِفْتَرَضَ عَلَيْهِمْ صَدَقَةً فِي أَمْوَالِهِمْ، تُؤْخَذُ مِنْ أَغْنِيَائِهِمْ، فَتُرَدُّ فِي فُقَرَائِهِمْ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ، وَاللَّفْظُ لِلْبُخَارِيِّ
Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimtuma Mu’aadh (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) kuenda Yaman.” Akaitaja Hadiyth yote, miongoni mwa maneno yaliyomo: “Allaah Aliifanya Zakaah kuwa ni jambo la fardhi kwao, katika mali zao, huchukuliwa kutoka kwa matajiri wao na kupewa masikini wao.”[2] [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni Al-Bukhaariy]
484.
وَعَنْ أَنَسٍ رضى الله عنه أَنَّ أَبَا بَكْرٍ اَلصِّدِّيقَ رضى الله عنه كَتَبَ لَهُ {هَذِهِ فَرِيضَةُ اَلصَّدَقَةِ اَلَّتِي فَرَضَهَا رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم عَلَى اَلْمُسْلِمِينَ، وَاَلَّتِي أَمَرَ اَللَّهُ بِهَا رَسُولَهُ فِي أَرْبَعٍ وَعِشْرِينَ مِنَ اَلْإِبِلِ فَمَا دُونَهَا اَلْغَنَمُ فِي كُلِّ خَمْسٍ شَاةٌ، فَإِذَا بَلَغَتْ خَمْسًا وَعِشْرِينَ إِلَى خَمْسٍ وَثَلَاثِينَ فَفِيهَا بِنْتُ مَخَاضٍ أُنْثَى فَإِنْ لَمْ تَكُنْ فَابْنُ لَبُونٍ ذَكَرٍ فَإِذَا بَلَغَتْ سِتًّا وَثَلَاثِينَ إِلَى خَمْسٍ وَأَرْبَعِينَ فَفِيهَا بِنْتُ لَبُونٍ أُنْثَى، فَإِذَا بَلَغَتْ سِتًّا وَأَرْبَعِينَ إِلَى سِتِّينَ فَفِيهَا حِقَّةٌ طَرُوقَةُ اَلْجَمَلِ فَإِذَا بَلَغَتْ وَاحِدَةً وَسِتِّينَ إِلَى خَمْسٍ وَسَبْعِينَ فَفِيهَا جَذَعَةٌ فَإِذَا بَلَغَتْ سِتًّا وَسَبْعِينَ إِلَى تِسْعِينَ فَفِيهَا بِنْتَا لَبُونٍ، فَإِذَا بَلَغَتْ إِحْدَى وَتِسْعِينَ إِلَى عِشْرِينَ وَمِائَةٍ فَفِيهَا حِقَّتَانِ طَرُوقَتَا اَلْجَمَلِ، فَإِذَا زَادَتْ عَلَى عِشْرِينَ وَمِائَةٍ فَفِي كُلِّ أَرْبَعِينَ بِنْتُ لَبُونٍ، وَفِي كُلِّ خَمْسِينَ حِقَّةٌ، وَمَنْ لَمْ يَكُنْ مَعَهُ إِلَّا أَرْبَعٌ مِنَ اَلْإِبِلِ فَلَيْسَ فِيهَا صَدَقَةٌ إِلَّا أَنْ يَشَاءَ رَبُّهَا.
وَفِي صَدَقَةِ اَلْغَنَمِ سَائِمَتِهَا إِذَا كَانَتْ أَرْبَعِينَ إِلَى عِشْرِينَ وَمِائَةِ شَاةٍ شَاةٌ، فَإِذَا زَادَتْ عَلَى عِشْرِينَ وَمِائَةٍ إِلَى مِائَتَيْنِ فَفِيهَا شَاتَانِ، فَإِذَا زَادَتْ عَلَى مِائَتَيْنِ إِلَى ثَلَاثمِائَةٍ فَفِيهَا ثَلَاثُ شِيَاهٍ فَإِذَا زَادَتْ عَلَى ثَلَاثِمِائَةٍ فَفِي كُلِّ مِائَةٍ شَاةٌ، فَإِذَا كَانَتْ سَائِمَةُ اَلرَّجُلِ نَاقِصَةً مِنْ أَرْبَعِينَ شَاةٍ شَاةً وَاحِدَةً فَلَيْسَ فِيهَا صَدَقَةٌ، إِلَّا أَنْ يَشَاءَ رَبُّهَا.
وَلَا يُجْمَعُ بَيْنَ مُتَفَرِّقٍ وَلَا يُفَرَّقُ بَيْنَ مُجْتَمِعٍ خَشْيَةَ اَلصَّدَقَةِ، وَمَا كَانَ مِنْ خَلِيطَيْنِ فَإِنَّهُمَا يَتَرَاجَعَانِ بَيْنَهُمَا بِالسَّوِيَّةِ، وَلَا يُخْرَجُ فِي اَلصَّدَقَةِ هَرِمَةٌ وَلَا ذَاتُ عَوَارٍ، إِلَّا أَنْ يَشَاءَ اَلْمُصَّدِّقُ، وَفِي اَلرِّقَةِ رُبُعُ اَلْعُشْرِ، فَإِنْ لَمْ تَكُنْ إِلَّا تِسْعِينَ وَمِائَةً فَلَيْسَ فِيهَا صَدَقَةٌ إِلَّا أَنْ يَشَاءَ رَبُّهَا، وَمَنْ بَلَغَتْ عِنْدَهُ مِنَ اَلْإِبِلِ صَدَقَةُ اَلْجَذَعَةِ وَلَيْسَتْ عِنْدَهُ جَذَعَةٌ وَعِنْدَهُ حِقَّةٌ، فَإِنَّهَا تُقْبَلُ مِنْهُ اَلْحِقَّةُ، وَيَجْعَلُ مَعَهَا شَاتَيْنِ إِنِ اِسْتَيْسَرَتَا لَهُ، أَوْ عِشْرِينَ دِرْهَمًا، وَمَنْ بَلَغَتْ عِنْدَهُ صَدَقَةُ اَلْحِقَّةِ وَلَيْسَتْ عِنْدَهُ اَلْحِقَّةُ، وَعِنْدَهُ اَلْجَذَعَةُ، فَإِنَّهَا تُقْبَلُ مِنْهُ اَلْجَذَعَةُ، وَيُعْطِيهِ اَلْمُصَّدِّقُ عِشْرِينَ دِرْهَمًا أَوْ شَاتَيْنِ} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ
Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kwamba Abuu Bakr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alimuandikia barua kuwa: “Hii ni Swadaqah ya fardhi ambayo Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliifaridhisha kwa Waislam[3] na ambayo Allaah Alimuamrisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aiamrishe.[4] Kwa kila ngamia ishirini na nne au zaidi, kondoo mmoja atolewe kwa kila tano. Wakitimia kati ya ishirini na tano mpaka thelathini na tano, atolewe ngamia jike wa mwaka wa pili.[5] Iwapo hakuna ngamia jike, basi atolewe ngamia dume wa mwaka wa tatu. Wakitimia thelathini na sita hadi arubaini na tano, atolewe ngamia jike wa mwaka wa tatu. Wakitimia arubaini na sita hadi sitini, atolewe ngamia jike wa mwaka wa nne[6] ambaye yu tayari kupandwa. Wakitimia sitini na moja hadi sabini na tano, atolewe ngamia jike wa mwaka wa tano. Wakitimia sabini na sita hadi tisini, watolewe ngamia wawili majike wa mwaka wa tatu, wakitimia tisini na moja hadi mia na ishirini, watolewe ngamia wawili majike wa mwaka wa nne, ambao wako tayari kupandwa. Wakizidi idadi ya mia na ishirini, ngamia mmoja jike wa mwaka wa tatu atolewe kwa kila arubaini, na ngamia mmoja jike wa mwaka wa nne atolewe kwa kila hamsini. Iwapo mtu anao ngamia wanne tu, hatozwi Swadaqah isipokuwa kama mwenye ngamia anataka kutoa.
Kuhusu Swadaqah ya kondoo wanaolishwa, wakitimia idadi ya arubaini hadi mia moja na ishirini, atolewe kondoo mmoja. Wakizidi mia moja na ishirini hadi mia mbili, watolewe kondoo wawili. Wakiwa zaidi ya mia mbili hadi mia tatu, watolewe kondoo watatu. Wakiwa zaidi ya mia tatu, kondoo mmoja atolewe kwa kila mia moja. Mtu akiwa na idadi ya kondoo chini ya arubaini, hatozwi Swadaqah isipokuwa kama mwenye kondoo hao anapenda.
Wala hawakusanywi waliotawanyika na waliokusanyika wasitenganishwe[7] kwa sababu ya kuogopa Swadaqah. Na wanaomilikiwa na washirika wawili, watadaiana walipane kwa usawa.[8] Kondoo mzee au kondoo mwenye chongo au kondoo dume asitolewe Swadaqah isipokuwa ikiwa mkusanyaji anataka hivyo.[9] Katika fedha: kwa Dirham mia mbili,[10] ilipwe moja ya arubaini, lakini zikiwepo mia moja na tisini tu, hailipii Zakaah isipokuwa kama mwenye fedha hiyo anataka kutoa. Endapo mtu yeyote mwenye idadi ya ngamia ambayo inahitaji kulipia Zakaah ya ngamia jike wa mwaka wa tano lakini hana ngamia huyo ila anaye ngamia wa mwaka wa nne,[11] mtu huyo alipe ngamia huyu pamoja na kondoo wawili iwapo anaweza kuwapata, vinginevyo alipe Dirham ishirini. Ikiwa mtu ana idadi ya ngamia ambayo inahitaji kulipa ngamia jike wa mwaka wa nne,[12] na hana ngamia kama huyu ila anaye ngamia jike wa mwaka wa tano, amtoe ngamia huyu na mkusanyaji lazima amrudishie Dirham ishirini au kondoo wawili.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]
485.
وَعَنْ مُعَاذِ بْنِ جَبَلٍ رضى الله عنه {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم بَعَثَهُ إِلَى اَلْيَمَنِ، فَأَمَرَهُ أَنْ يَأْخُذَ مِنْ كُلِّ ثَلَاثِينَ بَقَرَةً تَبِيعًا أَوْ تَبِيعَةً، وَمِنْ كُلِّ أَرْبَعِينَ مُسِنَّةً، وَمِنْ كُلِّ حَالِمٍ دِينَارًا أَوْ عَدْلَهُ مُعَافِرَ} رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ، وَاللَّفْظُ لِأَحْمَدَ، وَحَسَّنَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ وَأَشَارَ إِلَى اِخْتِلَافٍ فِي وَصْلِهِ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ، وَالْحَاكِمُ
Kutoka kwa Mu’aadh bin Jabal (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimtuma kuenda Yaman, na akamuamrisha achukue ndama wa ng’ombe mwenye umri wa mwaka mmoja, dume au jike kwa kila ng’ombe telathini, na amchukue ng’ombe jike mmoja wa mwaka wa tatu[13] kwa kila arubaini, na Dinari moja kwa kila mtu mzima asiyekuwa Muislam (kama Jizya),[14] au nguo zenye thamani sawa zilizotengenezwa Yaman.” [imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) na tamshi hili ni la Ahmad, na At-Tirmidhiy amesema ni Hasan, na akataja kuwa kuna kutofautiana iwapo hii ni Mawswuwl au laa. Na wakaisahihisha Ibn Hibbaan na Al-Haakim]
486.
وَعَنْ عَمْرِو بْنِ شُعَيْبٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {تُؤْخَذُ صَدَقَاتُ اَلْمُسْلِمِينَ عَلَى مِيَاهِهِمْ} رَوَاهُ أَحْمَدُ
وَلِأَبِي دَاوُدَ: {وَلَا تُؤْخَذُ صَدَقَاتُهُمْ إِلَّا فِي دُورِهِمْ}
Kutoka kwa ‘Amr bin Shu’ayb kwa upokezi wa baba yake kutoka kwa babu yake (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Swadaqah za Waislamu zipokewe kwenye manywesheo yao (maji).” [Imetolewa na Ahmad]
Na katika Riwaayah ya Abuu Daawuwd: “Swadaqah zao zipokewe majumbani mwao tu.”
487.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {لَيْسَ عَلَى اَلْمُسْلِمِ فِي عَبْدِهِ وَلَا فِي فَرَسِهِ صَدَقَةٌ} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ
وَلِمُسْلِمٍ: {لَيْسَ فِي اَلْعَبْدِ صَدَقَةٌ إِلَّا صَدَقَةُ اَلْفِطْرِ}
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Muislamu hana Swadaqah katika mtumwa wake au farasi wake.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]
Na katika Riwaayah ya Muslim: “Hakuna Swadaqah kwa mtumwa isipokuwa Swadaqatul-Fitwr.”
488.
وَعَنْ بَهْزِ بْنِ حَكِيمٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {فِي كُلِّ سَائِمَةِ إِبِلٍ: فِي أَرْبَعِينَ بِنْتُ لَبُونٍ، لَا تُفَرَّقُ إِبِلٌ عَنْ حِسَابِهَا، مَنْ أَعْطَاهَا مُؤْتَجِرًا بِهَا فَلَهُ أَجْرُهُ، وَمَنْ مَنَعَهَا فَإِنَّا آخِذُوهَا وَشَطْرَ مَالِهِ، عَزْمَةً مِنْ عَزَمَاتِ رَبِّنَا، لَا يَحِلُّ لِآلِ مُحَمَّدٍ مِنْهَا شَيْءٌ} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَأَبُو دَاوُدَ، وَالنَّسَائِيُّ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ، وَعَلَّقَ اَلشَّافِعِيُّ اَلْقَوْلَ بِهِ عَلَى ثُبُوتِهِ
Kutoka kwa Bahz bin Hakiym[15] kutoka kwa baba yake[16] naye kwa upokezi wa babu yake[17] amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Kwa ajili ya ngamia arubaini wanaolishwa,[18] atolewe ngamia mmoja jike wa mwaka wa tatu. Hao ngamia wasitenganishwe wakati wa kuwahesabu. Mtu anayelipa Zakaah kwa kutaka thawabu atapata thawabu na mwenye kuzuia Zakaah sisi tutaichukua pamoja na nusu ya mali yake kama fidia ile Aliyoiweka Rabb wetu. Si halali humo chochote kwa Muhammad.” [Imetolewa na Ahmad, Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy, na akaisahihisha Al-Haakim]
Ash-Shaafi’iyy[19] amesema ameongezea kauli juu ya uthibitisho wa kutwaa nusu ya mali ya mtu aliyeikwepa Zakaah.
489.
وَعَنْ عَلِيٍّ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {إِذَا كَانَتْ لَكَ مِائَتَا دِرْهَمٍ وَحَالَ عَلَيْهَا اَلْحَوْلُ فَفِيهَا خَمْسَةُ دَرَاهِمَ، وَلَيْسَ عَلَيْكَ شَيْءٌ حَتَّى يَكُونَ لَكَ عِشْرُونَ دِينَارًا، وَحَالَ عَلَيْهَا اَلْحَوْلُ، فَفِيهَا نِصْفُ دِينَارٍ، فَمَا زَادَ فَبِحِسَابِ ذَلِكَ، وَلَيْسَ فِي مَالٍ زَكَاةٌ حَتَّى يَحُولَ عَلَيْهِ اَلْحَوْلُ} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ، وَهُوَ حَسَنٌ، وَقَدِ اِخْتُلِفَ فِي رَفْعِهِ
وَلِلتِّرْمِذِيِّ، عَنِ اِبْنِ عُمَرَ: {مَنِ اِسْتَفَادَ مَالًا، فَلَا زَكَاةَ عَلَيْهِ حَتَّى يَحُولَ اَلْحَوْلُ} وَالرَّاجِحُ وَقْفُهُ
Kutoka kwa ‘Aliy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Ukiwa na Dirham mia mbili zikapitiwa na mwaka, utazilipia Dirham tano, na hupaswi kulipa chochote mpaka umemiliki Dinari ishirini kwa muda wa mwaka mzima ambapo utazilipia nusu Dinari,[20] kinachozidi idadi hiyo kitahesabiwa hivyo hivyo. Na hakuna katika mali ya Zakaah mpaka ipitiwe na mwaka.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd. Ni Hasan na wanazuoni wametofautiana kama ni Marfuw’ au la]
Na At-Tirmidhiy alipokea hivi kutoka kwa ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ): “Mtu anayepata mali hapaswi kuilipia Zakaah mpaka mwaka umepita.” [Hadiyth hii imepewa daraja la Mawquwf]
490.
وَعَنْ عَلِيٍّ رضى الله عنه قَالَ:{لَيْسَ فِي اَلْبَقَرِ اَلْعَوَامِلِ صَدَقَةٌ} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ، وَاَلدَّارَقُطْنِيُّ، وَالرَّاجِحُ وَقْفُهُ أَيْضًا
Kutoka kwa ‘Aliy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Hakuna Swadaqah kwa ng’ombe anayefanyishwa kazi.”[21] [Imetolewa na Abuu Daawuwd na Ad-Daaraqutwniyy, na ikaitwa Maawquwf]
491.
وَعَنْ عَمْرِو بْنِ شُعَيْبٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ، عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ عَمْرِوٍ، أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: {مِنْ وَلِيَ يَتِيمًا لَهُ مَالٌ، فَلْيَتَّجِرْ لَهُ، وَلَا يَتْرُكْهُ حَتَّى تَأْكُلَهُ اَلصَّدَقَةُ} رَوَاهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَاَلدَّارَقُطْنِيُّ، وَإِسْنَادُهُ ضَعِيفٌ
وَلَهُ شَاهِدٌ مُرْسَلٌ عِنْدَ اَلشَّافِعِيِّ
Kutoka kwa ‘Amr bin Shu’ayb kwa upokezi wa baba yake kutoka kwa babu yake ‘Abdullaah bin ‘Amr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Endapo waliy wa yatima mwenye mali, ni lazima aifanyie biashara, asiiache tu mpaka imalizwe na Zakaah.”[22] [Imetolewa na At-Tirmidhiy na Ad-Daaraqutwniyy kwa Isnaad dhaifu]
Ina tafsiri inayoiunga mkono ambayo ni Mursal iliyosimuliwa na Ash-Shaafi’iyy
492.
وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ أَبِي أَوْفَى رضى الله عنه قَالَ: {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم إِذَا أَتَاهُ قَوْمٌ بِصَدَقَتِهِمْ قَالَ: "اَللَّهُمَّ صَلِّ عَلَيْهِمْ"} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Abiy Awfaa (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Watu walipoleta Swadaqah zao kwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akisema: Ee Allaah! Wabaarik hawa.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
493.
وَعَنْ عَلِيٍّ رضى الله عنه أَنَّ اَلْعَبَّاسَ رضى الله عنه {سَأَلَ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم فِي تَعْجِيلِ صَدَقَتِهِ قَبْلَ أَنْ تَحِلَّ، فَرَخَّصَ لَهُ فِي ذَلِكَ} رَوَاهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَالْحَاكِمُ
Kutoka kwa ‘Aliy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ): “Alimuomba Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kuharakiza kutoa Swadaqah yake kabla ya wakati, naye akamruhusu[23] kuilipa.” [Imetolewa na At-Tirmidhiy na Al-Haakim]
494.
وَعَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اَللَّهِ رضى الله عنه عَنْ رَسُولِ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: {لَيْسَ فِيمَا دُونَ خَمْسِ أَوَاقٍ مِنَ اَلْوَرِقِ صَدَقَةٌ، وَلَيْسَ فِيمَا دُونَ خَمْسٍ ذَوْدٍ مِنَ اَلْإِبِلِ صَدَقَةٌ، وَلَيْسَ فِيمَا دُونَ خَمْسَةِ أَوْسُقٍ مِنَ اَلتَّمْرِ صَدَقَةٌ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ
وَلَهُ مِنْ حَدِيثِ أَبِي سَعِيدٍ: {لَيْسَ فِيمَا دُونَ خَمْسَةِ أَوْسَاقٍ مِنْ تَمْرٍ وَلَا حَبٍّ صَدَقَةٌ}
وَأَصْلُ حَدِيثِ أَبِي سَعِيدٍ مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Jaabir bin ‘Abdullaah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Hakuna Swadaqah chini ya Uqiya[24] tano (yaani gramu 595) za fedha, na chini ya ngamia watano, na kwa idadi chini ya kapu (Wasaq)[25] tano (gramu 652) za tende.”[26] [Imetolewa na Muslim]
Na Abuu Sa’iyd alisimuliwa kuwa: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Hakuna Swadaqah (Zakaah) chini ya kapu tano za tende au nafaka.”[27]
495.
وَعَنْ سَالِمِ بْنِ عَبْدِ اَللَّهِ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: {فِيمَا سَقَتِ اَلسَّمَاءُ وَالْعُيُونُ، أَوْ كَانَ عَثَرِيًّا: اَلْعُشْرُ، وَفِيمَا سُقِيَ بِالنَّضْحِ: نِصْفُ اَلْعُشْرِ} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ
وَلِأَبِي دَاوُدَ: {أَوْ كَانَ بَعْلًا: اَلْعُشْرُ، وَفِيمَا سُقِيَ بِالسَّوَانِي أَوِ اَلنَّضْحِ: نِصْفُ اَلْعُشْرِ}
Kutoka kwa Saalim bin ‘Abdillaah amesimulia kutoka kwa baba yake (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Katika kilichonyeshewa na mvua au chemchem, au kwa unyevu ni moja ya kumi, na katika kilichonyeshewa kwa njia ya umwagiliaji ni moja ya ishirini au ngamia wa ukame ni moja ya ishirini.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]
Na katika Riwaayah ya Abuu Daawuwd: “Iwapo hayo mazao ya shambani yatakuwa yalimwagiliwa maji na unyevu wa maji ya chini ya ardhi yatalipiwa moja ya kumi; lakini iwapo yatakuwa yamemwagiliwa kwa mifereji ya umwagiliaji, magurudumu ya maji, au ngamia wa ukame yatalipiwa moja ya ishirini.”
496.
وَعَنْ أَبِي مُوسَى اَلْأَشْعَرِيِّ، وَمُعَاذٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا، أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم قَالَ لَهُمَا: {لَا تَأْخُذَا فِي اَلصَّدَقَةِ إِلَّا مِنْ هَذِهِ اَلْأَصْنَافِ اَلْأَرْبَعَةِ: اَلشَّعِيرِ، وَالْحِنْطَةِ، وَالزَّبِيبِ، وَالتَّمْرِ} رَوَاهُ اَلطَّبَرَانِيُّ، وَالْحَاكِمُ
وَلِلدَّارَقُطْنِيِّ، عَنْ مُعَاذٍ: {فَأَمَّا اَلْقِثَّاءُ، وَالْبِطِّيخُ، وَالرُّمَّانُ، وَالْقَصَبُ، فَقَدْ عَفَا عَنْهُ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم} وَإِسْنَادُهُ ضَعِيفٌ
Kutoka kwa Abuu Muwsaa Al-Ash’ariyy na Mu’aadh (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) wamesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema kuwaambia: “Msikusanye Swadaqah ila kwa aina hizi nne tu zifuatazo: shayiri, ngano, zabibu kavu, na tende.” [Imetolewa na Atw-Twabaraaniyy na Al-Haakim
Na katika tafsiri ya pili ya Ad-Daaraqutwniyy kwa upokezi wa Mu’aadh amesema: “Ama matango, matikiti, makomamanga na miwa ilisamehewa na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) isilipiwe Swadaqah.” [Isnaad yake ni dhaifu]
497.
وَعَنْ سَهْلِ بْنِ أَبِي حَثْمَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: أَمَرَنَا رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {إِذَا خَرَصْتُمْ، فَخُذُوا، وَدَعُوا اَلثُّلُثَ، فَإِنْ لَمْ تَدَعُوا اَلثُّلُثَ، فَدَعُوا اَلرُّبُعَ} رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ إِلَّا اِبْنَ مَاجَهْ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ، وَالْحَاكِمُ
Kutoka kwa Sahl bin Abuu Hatmah[28] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah alituamrisha: “Mnapokadiria Swadaqah ya matunda kama tende, chukueni na muache theluthi moja, basi acheni robo ya Swadaqah inayokadiriwa kwa wamiliki wake.”[29] [Imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ahmad) isipokuwa Ibn Maajah, na akaisahihisha Ibn Hibbaan na Al-Haakim]
498.
وَعَنْ عَتَّابِ بنِ أُسَيْدٍ رضى الله عنه قَالَ: أَمَرَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {أَنْ يُخْرَصَ اَلْعِنَبُ كَمَا يُخْرَصُ اَلنَّخْلُ، وَتُؤْخَذَ زَكَاتُهُ زَبِيبًا} رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ، وَفِيهِ اِنْقِطَاعٌ
Kutoka kwa ‘Attaab bin Usayd[30] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amessema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliamrisha Zakaah ya mizabibu ikadiriwe kama inavyokadiriwa mitende, na Zakaah yake ilipwe kwa zabibu zilizokaushwa kama Zakaah ya mitende ilipwavyo kwa tende zilizokaushwa.” [Imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) lakini ina katika Isnaad]
499.
وَعَنْ عَمْرِو بْنِ شُعَيْبٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ، {أَنَّ اِمْرَأَةً أَتَتِ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم وَمَعَهَا اِبْنَةٌ لَهَا، وَفِي يَدِ اِبْنَتِهَا مِسْكَتَانِ مِنْ ذَهَبٍ، فَقَالَ لَهَا: "أَتُعْطِينَ زَكَاةَ هَذَا؟" قَالَتْ: لَا. قَالَ: "أَيَسُرُّكِ أَنْ يُسَوِّرَكِ اَللَّهُ بِهِمَا يَوْمَ اَلْقِيَامَةِ سِوَارَيْنِ مِنْ نَارٍ؟". فَأَلْقَتْهُمَا.} رَوَاهُ اَلثَّلَاثَةُ، وَإِسْنَادُهُ قَوِيٌّ
وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ: مِنْ حَدِيثِ عَائِشَةَ
Kutoka kwa ‘Amr bin Shu’ayb kwa upokezi wa baba yake kutoka kwa babu yake amesema: Mwanamke mmoja alikuja kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), alikuwa pamoja na binti yake aliyevaa bangili za dhahabu mkononi mwake. Akamuambia: “Unalipa Zakaah ya bangili hizo?” Akasema: “Hapana.” Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Je, utafurahi[31] iwapo Allaah Atakuwekea bangili mbili za moto badala yake?” Akazitupa. [Imetolewa na Ath-Thalaathah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd) na Isnaad yake ni imara. Imethibitishwa na Al-Haakim kutokana na Hadiyth ya ‘Aaishah]
500.
وَعَنْ أُمِّ سَلَمَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا، {أَنَّهَا كَانَتْ تَلْبَسُ أَوْضَاحًا مِنْ ذَهَبٍ فَقَالَتْ: يَا رَسُولَ اَللَّهِ! أَكَنْزٌ هُوَ؟ فَـقَالَ: "إِذَا أَدَّيْتِ زَكَاتَهُ، فَلَيْسَ بِكَنْزٍ"} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ، وَاَلدَّارَقُطْنِيُّ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ
Kutoka kwa Ummu Salamah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema kuwa: “Yeye alikua akivaa bangili za dhahabu[32] akauliza: Ee Rasuli wa Allaah! Hii ni hazina? Akasema: “Si hazina iwapo utailipia Zakaah yake.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na Ad-Daaraqutwniyy na akaisahihisha Al-Haakim]
501.
وَعَنْ سَمُرَةَ بْنِ جُنْدُبٍ رضى الله عنه قَالَ: {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَأْمُرُنَا; أَنْ نُخْرِجَ اَلصَّدَقَةَ مِنَ اَلَّذِي نَعُدُّهُ لِلْبَيْعِ} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ، وَإِسْنَادُهُ لَيِّنٌ
Kutoka kwa Samurah bin Jundub (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akituamrisha tutoe Swadaqah katika vitu tunavyo viandaa kwa biashara.”[33] [Imetolewa na Abuu Daawuwd, na Isnaad yake ni dhaifu]
502.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه {أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: "وَفِي اَلرِّكَازِ: اَلْخُمُسُ"} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Na katika hazina iliyofukiwa chini hutozwa moja ya tano.”[34] [Al-Bukhaariy, Muslim]
503.
وَعَنْ عَمْرِو بْنِ شُعَيْبٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ، {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم قَالَ فِي كَنْزٍ وَجَدَهُ رَجُلٌ فِي خَرِبَةٍ: "إِنْ وَجَدْتَهُ فِي قَرْيَةٍ مَسْكُونَةٍ، فَعَرِّفْهُ، وَإِنْ وَجَدْتَهُ فِي قَرْيَةٍ غَيْرِ مَسْكُونَةٍ، فَفِيهِ وَفِي اَلرِّكَازِ: اَلْخُمُسُ "} أَخْرَجَهُ اِبْنُ مَاجَهْ بِإِسْنَادٍ حَسَنٍ
Kutoka kwa ‘Amr bin Shu’ayb amemnukuu baba yake, kuwa babu yake (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesimulia kuwa: Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema kuhusu hazina alioipata mtu mahala pasipotumika: “Ukiipata kwenye makazi ya watu, lazima uwajulishe. Ukiipata pasipo makazi na katika hazina iliyozikwa basi ni moja ya tano.” [Imetolewa na Ibn Maajah kwa Isnaad nzuri]
504.
وَعَنْ بِلَالِ بْنِ اَلْحَارِثِ رضى الله عنه { أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَخَذَ مِنَ اَلْمَعَادِنِ اَلْقَبَلِيَّةِ اَلصَّدَقَةَ} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ
Kutoka kwa Bilaal bin Al-Haarith[35] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipokea Swadaqah ya machimbo ya Al-Qabaliyyah.”[36] [Imetolewa na Abuu Daawuwd]
[1] Maana ya Zakaah ni “Kuongezeka na kutakasika.” Kwa sababu malipo ya Zakaah hupelekea kuongezeka kwa mali na kwa hivyo huhesabika kuwa ni sababu ya kutakasika kwake, wajibu huu umepewa jina la Zakaah na Shariy’ah. Zakaah ilifaradhishwa mwaka wa 2 A.H., kabla ya amri ya Swawm.
[2] Hadiyth inatufundisha kuwa Zakaah ni lazima kwa matajiri miongoni mwa Waislam. Zakaah hii ni ya kuwapa msaada Waislam maskini, na hawapewi wasiokuwa Waislam. Tunafunzwa zaidi kuwa, Zakaah inayokusanywa katika mji mmoja sharti wagawiwe maskini wa mji huo huo.
[3] Wakati wa Abuu Bakr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alipomteua Anas kuwa Gavana wa Bahrayn kwa niaba yake, alimpa maagizo haya yanayohusu Zakaah kwa maandishi.
[4] Kuhusu usahihi wa Hadiyth hii, yaani Isnaad ni sahihi kabisa. Kuhusu maandishi, nayo ni wazi kabisa, na kuna maafikiano ya pamoja ya Maswahaba wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kuhusu usahihi wake. Hakuna Swahaba hata mmoja wa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliyewahi kuikanusha Hadiyth hii.
[5] بِنْتُ مَخَاضٍ (Bint Makhaadhw) ni neno linalotumika kwa ngamia mwenye umri wa mwaka mmoja na ameingia katika mwaka wa pili wa umri wake.
[6] حِقَّةٌ (Hiqqah) ni neno linalotumika kwa ngamia mwenye umri wa miaka mitatu na ameingia katika mwaka wa nne wa umri wake, na ana uwezo wa kupandwa.
[7] Mfano wa kuunganisha mali ya Zakaah zilizotengana ni kama ifuatavyo: “Kuna watu wawili wana kundi la mbuzi hamsini kila mmoja wao, kwa hivyo wanatakiwa kutoa mbuzi mmoja kila mtu kutoka katika hisa zao. Endapo watu hawa wawili wataunganisha makundi yao mawili kuwa kundi moja, watapata faida ya kutoa mbuzi mmoja tu kwa pamoja kama Zakaah ya mbuzi mia moja, kwa sababu Zakaah ya mbuzi mia moja ni mbuzi mmoja tu.” Mfano wa kutenganisha kesi za Zakaah zilizoungana ni kama ifuatavyo: “Watu wawili wanamiliki kundi moja la mbuzi hamsini kwa ubia wa sawa kwa sawa. Kwa hivyo Zakaah ya mbuzi hawa hamsini itakuwa ni mbuzi mmoja. Lakini wakiligawanya kundi lao na kuwatenganisha ili kila mmoja awe na mbuzi ishirini na tano tu, wataepuka kutoa Zakaah kwa kuwa idadi ya mbuzi wa kila mmoja ni chini ya mbuzi arubaini. Hali kadhalika mkusanyaji wa Zakaah asithubutu kuunganisha wala kutenganisha mali za watu, yaani akiwakuta watu wawili wakiwa na mbuzi thelathini kila mmoja na kwa hivyo wanasamehewa kutoa Zakaah, mkusanyaji hana ruhusa ya kuunganisha hayo makundi mawili mbalimbali ya watu hao wawili na kulifanya liwe kundi moja ili adai wale watu walipe mbuzi mmoja.”
[8] Kwa mfano watu wawili wanamiliki mbuzi mia moja na arubaini. Mmoja anamiliki arubaini wakati mwenziwe anamiliki mia moja. Zakaah hapa inakuwa mbuzi wawili. Lakini ikiwa mmiliki wa mbuzi arubaini anamuambia mwenziwe hivi: “Ni bora ulipe Zakaah ya mbuzi mmoja na nusu, na mimi nilipe nusu ya mbuzi mmoja.” Hivyo haitakuwa sahihi. Shariy’ah yataka mmiliki wa mbuzi arubaini alipe mbuzi mmoja kamili, na mmiliki wa mbuzi mia pia naye alipe mbuzi mmoja tu kamili kama Zakaah yake.
[9] Hii inamaanisha kwamba, mtu anayetaka kutoa Zakaah asijaribu kutoa vitu vyenye dosari, wala mkusanyaji au mpokeaji naye asijaribu kuchukua vitu vizuri zaidi kuliko vyote. Vitu vitolewe vile vyenye thamani ya wastani.
[10] Moja ya kumi na mbili ya Uqiya moja ya dhahabu, kwa thamani.
[11] جَذَعَةٌ (Jadha’ah) ni neno linalotumika kwa ngamia jike ambaye ana miaka mine na ameingia mwaka wa tano wa umri wake.
[12] حِقَّةٌ (Hiqqah) ni neno linalotumika kwa ngamia jike wa miaka mitatu na ameingia mwaka wa nne wa umri wake.
[13] Ng’ombe na nyati ni jamii moja ya wanyama. Wote hao, wa jinsia zote mbili, wanajumuishwa katika hesabu. Mtu anayemiliki chini ya ng’ombe thelathini hatozwi Zakaah, wakitimia thelathini, hutozwa ndama mwenye umri wa mwaka mmoja. Wanyama anaowamiliki mtu wakiwa kati ya arubaini na sitini na tisa, Zakaah itakuwa ndama wa miaka miwili. Wakitimia sabini Zakaah ni ile ile, yaani ndama mmoja wa miaka miwili pamoja na ndama mmoja wa mwaka mmoja.
[14] Jizyah ni kodi ya kichwa anayoilipa mtu asiyekuwa Muislam anayeishi katika nchi ya Kiislam.
[15] Bahz bin Hakiym ndiye Abuu ‘Abdil-Maalik Bahz bin Hakiym bin Mu’aawiya bin Haida Al-Qushayr Al-Basri. Alikuwa Taabi’i wa daraja la sita. Uaminifu au utegemewaji wake umekanushwa. Abuu Daawuwd amesema: “Ahaadiyth zake ni sahihi.” Pia Ibn Maa’in, Ibn Al-Madiniy, na An-Nasaaiy walimkubali. Lakini Abuu Haatim amesema: “Huyo siyo mtaalam wa Hadiyth.” Naye Ibn Hibbaan amesema: “Alikuwa na makosa mengi katika Hadiyth.” Alikufa baada ya miaka ya 140 A.H. au kabla ya miaka sitini.
[16] Na huyu babake Bahz pia ni Taabi’i ambaye Ibn Hibbaan alimhesabu kuwa ni mpokezi na msimuliaji mwaminifu wa Hadiyth.
[17] Babu yake ni Mu’aawiyah bin Hayda bin Mu’aawiya bin Qushayr bin Ka’b Al-Qushayr, na alikuwa Swahaba aliyelowea Basra na alikuwa anazo Ahaadiyth.
[18] Hali ya Zakaah ya ng’ombe ni kwamba sharti wawe wazima na nguvu za kutosha kijilisha wao wenyewe. Hali hii ilitajwa hususan kwa mbuzi na ngamia. Na kanuni hiyo hiyo imeamriwa kwa ajili ya ng’ombe na nyati.
[19] Hadiyth hii inadhihirisha kwamba, iwapo mtu halipi Zakaah kwa hiari yake, Serikali ya ya Kiislam inaweza kumtoza faini yenye thamani ya nusu ya bidhaa zake na wanaweza kuichukua kwa nguvu. Kutozwa hivyo kwa nguvu kutakidhi deni alilonalo huyo mtu, lakini atanyimwa thawabu.
[20] Hadiyth hii inaongelea Zakaah inayotozwa katika dhahabu na fedha. Uzito wa fedha ni kuanzia Dirham mia mbili na zaidi. Uzito hasa wa fedha unaostahili kulipiwa Zakaah ni tola hamsini na nusu (sawa na gramu 611.5) na Zakaah inayotozwa kwa kiasi itakuwa moja ya arubaini. Halikadhalika kiasi cha dhahabu ipaswayo kutolewa Zakaah ni tola saba na nusu (sawa na gramu 87), Zakaah ipaswayo kulipwa kwa kiasi hiki ni moja ya arubaini pia. Na hata kwa pesa za noti hulipiwa hiyo hiyo 1/40.
[21] Ng’ombe wafanyao kazi za kulima, kuchota na kumwagia maji, na wasafirishaji, ndio wanaohusika.
[22] Kuna tofauti za maoni ya Wanazuoni kuhusu iwapo mali ya yatima itolewe Zakaah au laa. Juu ya kuwepo kukhitilafiana, ni bora kuilipia Zakaah.
[23] Siku na nyakati za Hajj, Swalaah na Swawm zote zimepangwa wazi. Lakini kuhusu Zakaah hakuna wakati maalumu. Ulipaji wake unaweza kuahirishwa au pia unaweza kulipwa mapema, ingawa huwa inakuwa deni baada ya muda wa mwaka mmoja tu.
[24] Kwa kuwa thamani ya Uqiya moja ni Dirham 40 (au gramu 128), basi Waqiya tano zitakuwa sawa sawa na Dirham 200.
[25] Takribani kilo kumi na mbili unusu.
[26] Kwa mujibu wa vipimo vya siku hizi, kiasi cha Zakaah ipasavyo kulipwa kwa kila maund 20 za nafaka (yaani quintal 8), itakuwa maund moja ya nafaka (yaani takribani kilo 40). Iwapo kiasi cha nafaka ni chini ya quintal 8, hakuna kuilipia hiyo Zakaah hiyo. Quintal 8 ni sawa na Wasq 5 ambayo imetajwa katika Hadiyth hii. Endapo mtu atamiliki zaidi ya gramu 87 za dhahabu, huyo analazimika ailipie Zakaah. Na endapo mtu atamiliki zaidi ya gramu 611.5, basi huyu pia inapaswa ailipie Zakaah.
[27] Nafaka yoyote inayoweza kuhifadhiwa kwa mwaka mmoja, inapaswa ilipiwe Zakaah. Ngano, shayiri, mpunga, mtama, mahindi ya Kihindi, mahindi jamii ya kunde na choroko n.k. vyote vinaingia katika kundi hili. Zakaah ya hivi hutegemea kiasi cha kazi na adha itokanayo na kuzalisha hivi. Mazao ya ardhi ambayo yamemwagiliwa maji na ya mafuriko, au mbubujiko wa asili au mito, yatalipiwa moja ya kumi ya kazi ya kuyazalisha. Ikiwa ardhi imemwagiliwa na maji ya kisima au kwa kulipia pesa maji yale kama maji ya mifereji, basi mazao yake yatalipiwa Zakaah ya moja ya ishirini tu ya jumla yake.
[28] Sahl bin Abiy Hatmah, jina lake halisi ni ‘Abdullaah au ‘Aamir bin Sa’ida bin ‘Aamir Al-Answaar Al-Khazraj Al-Madaniy. Alikuwa Swahaba aliyezaliwa mnamo mwaka wa 3A.H. alilowea Kufa na anahesabika kuwa yu mkazi wa Al-Madiynah ambako alifia wakati wa ugavana wa Mus’ab bin Az-Zubayr.
[29] Maana ya neno la kiarabu “Kharsw” ni kubahatisha au kudhania, yaani kukisia kiasi cha matunda yanayoweza kuzaliwa baada ya kukomaa na kuiva. Mtu kama huyo ni sharti aifanye kazi yake kwa uaminifu mkubwa sana. Kanuni ya wakusanyaji Zakaah ni kiasi cha theluthi moja ya kiasi hicho alichokikadiria. Kama hakubaliani nacho basi lazima aache robo yake, au mara nyingine mmiliki anaweza kuwapa majirani zake baadhi yake.
[30] ‘Attaab bin Usayd bin Abiy Al-‘Ays bin Umayyah bin ‘Abd Shams Al-Umawi Al-Makki alikuwa Swahaba. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimteua aitawale Makkah katika mwaka wa kuiteka, kwa kuwa alikuwa akienda Humayn na akaendelea kuitawala hadi Abuu Bakr alipofariki. Inasemekana naye alifariki siku hiyo hiyo aliyofariki Abuu Bakr. Inasemwa pia kuwa aliishi hadi mwisho wa Ukhalifa wa ‘Umar.
[31] Suala la Zakaah ya mapambo ya dhahabu lina mvutano. Lakini rai ya wengi ni kuwa iyo Zakaah ni lazima ilipwe, na Hadiyth hii ni ushahidi wake.
[32] أوضاح (Awdhwaah) ni wingi wa وضع. Hiyo ilikuwa ni aina ya mapambo ambayo zamani yalikuwa yakitengenezwa kwa fedha. Kwa sababu ya kumeremeta kwake, ikaitwa أَوْضَاح, baadaye ikawa inatengenezwa kwa dhahabu pia. Kwa hivyo Hadiyth hii inathibitisha kuwa mapambo ya fedha na dhahabu yanapaswa kulipiwa Zakaah. Kuna mapambo mengine yasiyokuwa ya dhahabu na fedha, yasiyostahili kulipiwa Zakaah. Hayo ni mapambo ya lulu, zumaridi, johari, rubi, marijani na vito vingine.
[33] Kwa hivyo hii inatufahamisha, bidhaa zote za biashara hustahili kulipiwa Zakaah.
[34] Mali yoyote iliyofukuliwa kutoka ardhini ni اَلرِّكَازِ (Ar-Rikaaz), yaani ni hazina iliyofichwa ilimradi ni ya kutoka zama za wasiokuwa Waislam, na ni lazima kuweka moja ya tano ya mali hiyo katika hazina ya Kiislam. Hii haina lile sharti la kuwa hiyo moja ya tano iwekwe baada ya kupita mwaka mmoja.
[35] Alipewa jina la utani wa ‘Abdur-Rahmaan, na alikuwa miongoni mwa wajumbe wa kwanza kumzuru Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kule Al-Madiynah kutoka katika kabila la Muzaynah mnamo mwaka wa 5 A.H. alishika bendera ya Muzaynah wakati wa kuiteka Makkah. Aliishi nje ya Al-Madiynah na baadaye akahamia Basra. Alifariki mnamo mwaka wa 60 A.H. huku akiwa na miaka 80.
[36] Qabaliyyah ni jina la mahala iliyo pwani ya bahari umbali wa safari ya siku tano kwa kupanda ngamia kutoka Al-Madiynah.
بُلُوغُ الْمَرام
Buluwgh Al-Maraam
كِتَابُ اَلزَّكَاةُ
Kitabu Cha Zakaah
بَابُ صَدَقَةِ اَلْفِطْرِ
Mlango Wa Zakaatul-Fitwr
505.
عَنِ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {فَرَضَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم زَكَاةَ اَلْفِطْرِ، صَاعًا مِنْ تَمْرٍ، أَوْ صَاعًا مِنْ شَعِيرٍ: عَلَى اَلْعَبْدِ وَالْحُرِّ، وَالذَّكَرِ، وَالْأُنْثَى، وَالصَّغِيرِ، وَالْكَبِيرِ، مِنَ اَلْمُسْلِمِينَ، وَأَمَرَ بِهَا أَنْ تُؤَدَّى قَبْلَ خُرُوجِ اَلنَّاسِ إِلَى اَلصَّلَاةِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
وَلِابْنِ عَدِيٍّ مِنْ وَجْهٍ آخَرَ ، وَاَلدَّارَقُطْنِيِّ بِإِسْنَادٍ ضَعِيفٍ: {اغْنُوهُمْ عَنِ اَلطَّوَافِ فِي هَذَا اَلْيَوْمِ}
Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliamrisha Zakkaatul-Fitwr kwa mtumwa, mtu huru, mwanaume, mwanamke, kijana, na mzee miongoni mwa Waislam, pishi moja (sawa sawa na takribani kilogramu mbili na nusu) ya tende zilizokaushwa, au Swaa’ moja ya shayiri, na akaamrisha itolewe kabla watu hawajaondoka kuenda kuswali Swalaah ya ‘Iydul-Fitwr.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
Na Ibn ‘Adiyy na Ad-Daaraqutwniy alisimulia Hadiyth hiyo kwa Isnaad dhaifu: “Watosheni (wapeni mahitaji yao) dhidi ya kuenda njiani wakiombaomba katika siku hii.”
506.
وَعَنْ أَبِي سَعِيدٍ اَلْخُدْرِيِّ رضى الله عنه قَالَ: {كُنَّا نُعْطِيهَا فِي زَمَانِ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم صَاعًا مِنْ طَعَامٍ، أَوْ صَاعًا مِنْ تَمْرٍ، أَوْ صَاعًا مِنْ شَعِيرٍ، أَوْ صَاعًا مِنْ زَبِيبٍ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
وَفِي رِوَايَةٍ: {أَوْ صَاعًا مِنْ أَقِطٍ}
قَالَ أَبُو سَعِيدٍ: {أَمَّا أَنَا فَلَا أَزَالُ أُخْرِجُهُ كَمَا كُنْتُ أُخْرِجُهُ فِي زَمَنِ رَسُولِ اَللَّهِ}
وَلِأَبِي دَاوُدَ: {لَا أُخْرِجُ أَبَدًا إِلَّا صَاعًا}
Kutoka kwa Sa’iyd Al-Khudriyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Wakati alipokuwepo Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), tulikua tukitoa Pishi moja ya nafaka[1] kama Zakkaatul-Fitwr, au tende kavu, au shayiri, au zabibu kavu.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
Na katika Riwaayah nyingine inasema: “Au Swaa’ pishi moja ya jibini.”
Abuu Sa’iyd amesema: “Mimi sitaacha kutoa kama nilivyokuwa nikitoa (Pishi) wakati Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipokuwa hai.”
Na tafsiri ya Abuu Daawuwd inasema: “Sijawahi kutoa Swadaqah ila Pishi.”
507.
وَعَنِ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {فَرَضَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم زَكَاةَ اَلْفِطْرِ، طُهْرَةً لِلصَّائِمِ مِنَ اَللَّغْوِ، وَالرَّفَثِ، وَطُعْمَةً لِلْمَسَاكِينِ، فَمَنْ أَدَّاهَا قَبْلَ اَلصَّلَاةِ فَهِيَ زَكَاةٌ مَقْبُولَةٌ، وَمَنْ أَدَّاهَا بَعْدَ اَلصَّلَاةِ فَهِيَ صَدَقَةٌ مِنَ اَلصَّدَقَاتِ.} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ، وَابْنُ مَاجَهْ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ
Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliamrisha Zakkaatul-Fitwr iwe ndiyo utakaso wa mtu anayefunga Swawm dhidi ya maongezi ya kipuuzi na uchafu, pamoja na kuwa chakula kwa watu maskini. Mtu yeyote atailipa hiyo kabla ya Swalaah ya ‘Iydul-Fitwr itakubaliwa kama Zakaah. Lakini mtu akiilipa hiyo baada ya Swalaah ya ‘Iydul-Fitwr[2] itahesabika kuwa ni Swadaqah miongoni mwa Swadaqah zingine.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na Ibn Maajah na akaisahihisha Al-Haakim]
[1] Neno la Kiarabu: “طَعَامٍ” (Twa’aam) hutumika kwa aina mbalimbali za nafaka. Inaweza kutumika kwa ngano, shairi, na tende pia. Kwa ujumla yaweza kutumika kwa kila zao la kilimo.
[2] Hii inamaanisha kwamba, mtu akiilipa hiyo Zakaatul-Fitwr (Zakaah ya kufungulia Swawm), haimuondoshei wajibu wala hapati thawabu zinazohusiana na malipo hayo kama Zakaah. Hata hivyo ulipaji huu haupotei hivi hivi kwani atapata thawabu za tendo la kawaida tu la Swadaqah. Ni bora kulipa Pishi moja nzima (Kilo 2.6) kama Zakaatul-Fitwr, kwani ule usimulizi unaotaja nusu ya pishi siyo sahihi.
بُلُوغُ الْمَرام
Buluwgh Al-Maraam
كِتَابُ اَلزَّكَاةُ
Kitabu Cha Zakaah
بَابُ صَدَقَةِ اَلتَّطَوُّعِ
03-Mlango Wa Swadaqah Za Khiari
508.
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه عَنِ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: {سَبْعَةٌ يُظِلُّهُمُ اَللَّهُ فِي ظِلِّهِ يَوْمَ لَا ظِلَّ إِلَّا ظِلُّهُ....} فَذَكَرَ اَلْحَدِيثَ وَفِيهِ: {وَرَجُلٌ تَصَدَّقَ بِصَدَقَةٍ فَأَخْفَاهَا حَتَّى لَا تَعْلَمَ شِمَالُهُ مَا تُنْفِقُ يَمِينُهُ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Watu saba Allaah Atawafunika katika kivuli Chake tu, na akawataja miongoni mwao ni mtu anayetoa Swadaqah kwa siri hata mkono wake wa kushoto haujui mkono wake wa kuume umetoa nini.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
509.
وَعَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ رضى الله عنه قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: {كُلُّ اِمْرِئٍ فِي ظِلِّ صَدَقَتِهِ حَتَّى يُفْصَلَ بَيْنَ اَلنَّاسِ} رَوَاهُ اِبْنُ حِبَّانَ وَالْحَاكِمُ
Kutoka kwa ‘Uqbah bin ‘Aamir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema nilimsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema: “Kila mmoja atakuwa chini ya kivuli[1] cha Swadaqah yake hadi ihukumiwe baina ya watu.” [Imetolewa na Ibn Hibbaan na Al-Haakim]
510.
وَعَنْ أَبِي سَعِيدٍ اَلْخُدْرِيِّ، عَنِ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: {أَيُّمَا مُسْلِمٍ كَسَا مُسْلِمًا ثَوْبًا عَلَى عُرْيٍ كَسَاهُ اَللَّهُ مِنْ خُضْرِ اَلْجَنَّةِ، وَأَيُّمَا مُسْلِمٍ أَطْعَمَ مُسْلِمًا عَلَى جُوعٍ أَطْعَمَهُ اَللَّهُ مِنْ ثِمَارِ اَلْجَنَّةِ، وَأَيُّمَا مُسْلِمٍ سَقَى مُسْلِمًا عَلَى ظَمَإٍ سَقَاهُ اَللَّهُ مِنْ اَلرَّحِيقِ اَلْمَخْتُومِ} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ وَفِي إِسْنَادِهِ لِينٌ
Kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Muislamu yeyote atakayemvisha Muislam aliye uchi, Allaah Atamvisha huyo nguo za kijani za Al-Jannah. Na Muislam yeyote atakayemlisha Muislam mwenye njaa, Allaah Atamlisha matunda ya Al-Jannah. Na Muislam yeyote atakayemnywesha Muislam mwenye kiu, Allaah Atamnywesha Ar-Rahiyq Al-Makhtuwm (kinywaji kizuri cha mvinyo Al-Jannah).” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na kuna udhaifu katika mlolongo wa wapokezi]
511.
وَعَنْ حَكِيمِ بْنِ حِزَامٍ رضى الله عنه عَنِ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: {اَلْيَدُ اَلْعُلْيَا خَيْرٌ مِنَ اَلْيَدِ اَلسُّفْلَى، وَابْدَأْ بِمَنْ تَعُولُ، وَخَيْرُ اَلصَّدَقَةِ عَنْ ظَهْرِ غِنًى، وَمَنْ يَسْتَعْفِفْ يُعِفَّهُ اَللَّهُ، وَمَنْ يَسْتَغْنِ يُغْنِهِ اَللَّهُ.} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ، وَاللَّفْظُ لِلْبُخَارِيِّ
Kutoka kwa Hakiym bin Hizaam (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mkono wajuu ni mbora kuliko wa chini, na anza kwa kuwapa Swadaqah wanaokutegemea.[2] Na Swadaqah bora ni inayotolewa kwa ajili ya kujitosha, na yeyote anayejizuia kuwaomba watu Swadaqah, Allaah Atamfanya aridhike, na kila anayeridhika na anachopewa na Allaah, basi Allaah Atamfanya awe anajitosheleza.” [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Al-Bukhaariy]
512.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ: {قِيلَ يَا رَسُولَ اَللَّهِ: أَيُّ اَلصَّدَقَةِ أَفْضَلُ؟ قَالَ: "جُهْدُ اَلْمُقِلِّ، وَابْدَأْ بِمَنْ تَعُولُ"} أَخْرَجَهُ أَحْمَدُ، وَأَبُو دَاوُدَ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَةَ، وَابْنُ حِبَّانَ، وَالْحَاكِمُ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliulizwa Swadaqah gani iliyokuwa bora zaidi? Akasema: “Ni juhudi ya mwenye mali kidogo sana anayoweza kutoa, na aanze na watu wanaomtegemea yeye.” [Imetolewa na Ahmad, na Abuu Daawuwd, na wakaisahihisha Ibn Khuzaymah, Ibn Hibbaan na Al-Haakim]
513.
وَعَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {" تَصَدَّقُوا " فَقَالَ رَجُلٌ: يَا رَسُولَ اَللَّهِ، عِنْدِي دِينَارٌ؟ قَالَ: " تَصَدَّقْ بِهِ عَلَى نَفْسِكَ " قَالَ: عِنْدِي آخَرُ، قَالَ: " تَصَدَّقْ بِهِ عَلَى وَلَدِكَ " قَالَ: عِنْدِي آخَرُ، قَالَ: " تَصَدَّقْ بِهِ عَلَى خَادِمِكَ " قَالَ: عِنْدِي آخَرُ، قَالَ: " أَنْتَ أَبْصَرُ ".} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ وَالنَّسَائِيُّ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ وَالْحَاكِمُ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema tena kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Toeni Swadaqah.” Mtu mmoja akasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Ninayo dinari moja tu.” Akasema: “Jitolee Swadaqah mwenyewe.” Yule mtu akasema: “Ninayo nyingine.” Akasema: “Mtolee Swadaqah mwanao.” Yule mtu akasema: “Ninayo nyingine.” Akasema: “Mtolee Swadaqah mkeo.” Yule mtu akasema tena: “Ninayo nyingine.” Akasema: “Mtolee Swadaqah mtumishi wako.” Yule mtu akasema: “Ninayo nyingine.” Akasema: “Wewe unajua zaidi uifanyie nini hiyo.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy, na wakaisahihisha Ibn Hibbaan na Al-Haakim]
514.
وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: قَالَ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم {إِذَا أَنْفَقَتِ اَلْمَرْأَةُ مِنْ طَعَامِ بَيْتِهَا، غَيْرَ مُفْسِدَةٍ، كَانَ لَهَا أَجْرُهَا بِمَا أَنْفَقَتْ وَلِزَوْجِهَا أَجْرُهُ بِمَا اِكْتَسَبَ وَلِلْخَازِنِ مِثْلُ ذَلِكَ، وَلَا يَنْقُصُ بَعْضُهُمْ أَجْرَ بَعْضٍ شَيْئًا} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwanamke akitoa Swaadaqah sehemu ya chakula cha nyumbani mwake bila ubadhirifu,[3] atapata thawabu kwa alichotoa, mumewe atapata thawabu kwa alichochuma, na aliyekihifadhi naye atapata sawa na hizo, wala hakuna atakayepunguziwa thawabu[4] zake.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
515.
وَعَنْ أَبِي سَعِيدٍ اَلْخُدْرِيِّ رضى الله عنه قَالَ: {جَاءَتْ زَيْنَبُ اِمْرَأَةُ اِبْنِ مَسْعُودٍ، فَقَالَتْ: يَا رَسُولَ اَللَّهِ، إِنَّكَ أَمَرْتَ اَلْيَوْمَ بِالصَّدَقَةِ، وَكَانَ عِنْدِي حُلِيٌّ لِي، فَأَرَدْتُ أَنْ أَتَصَدَّقَ بِهِ، فَزَعَمَ اِبْنُ مَسْعُودٍ أَنَّهُ وَوَلَدُهُ أَحَقُّ مَنْ تَصَدَّقْتُ بِهِ عَلَيْهِمْ، فَقَالَ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم "صَدَقَ اِبْنُ مَسْعُودٍ، زَوْجُكِ وَوَلَدُكِ أَحَقُّ مَنْ تَصَدَّقْتِ بِهِ عَلَيْهِمْ".} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ
Kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Alikuja Zaynab[5] (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) mke wa Ibn ‘Mas-‘uwd akasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Leo umeamrisha Swadaqah, nami nilikuwa na vito vyangu, kwa hivyo ninataka nivitoe hivyo kama Swadaqah, lakini Ibn Mas-‘uwd alidai kuwa yeye na watoto wake wana haki zaidi niwatolee wao Swadaqah.” Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Ibn Mas-‘uwd amesema kweli, kuwa mumeo na watoto wana haki zaidi ya kunufaishwa na Swadaqah[6] yako.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]
516.
وَعَنِ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم {مَا يَزَالُ اَلرَّجُلُ يَسْأَلُ اَلنَّاسَ حَتَّى يَأْتِيَ يَوْمَ اَلْقِيَامَةِ لَيْسَ فِي وَجْهِهِ مُزْعَةُ لَحْمٍ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mtu hataacha kuomba hadi aje siku ya Qiyaamah hana usoni mwake nyama.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
517.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {مَنْ سَأَلَ اَلنَّاسَ أَمْوَالَهُمْ تَكَثُّرًا، فَإِنَّمَا يَسْأَلُ جَمْرًا، فَلْيَسْتَقِلَّ أَوْ لِيَسْتَكْثِرْ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Anayeomba watu mali zao ili aongezee mali yake mwenyewe, huyo anajipalilia makaa ya moto; kwa hivyo hebu aombe kidogo au kingi (na adhabu itamsubiri).”[7] [Imetolewa na Muslim]
518.
وَعَنِ اَلزُّبَيْرِ بْنِ اَلْعَوَّامِ رضى الله عنه عَنِ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: {لَأَنْ يَأْخُذَ أَحَدُكُمْ حَبْلَهُ، فَيَأْتِي بِحُزْمَةِ اَلْحَطَبِ عَلَى ظَهْرِهِ، فَيَبِيعَهَا، فَيَكُفَّ اَللَّهُ بِهَا وَجْهَهُ، خَيْرٌ لَهُ مِنْ أَنْ يَسْأَلَ اَلنَّاسَ أَعْطَوهُ أَوْ مَنَعُوهُ} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ
Kutoka kwa Az-Zubayr bin Al-‘Awwaam (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mmoja wenu kuchukua kamba yake, alete mzigo wa kuni mgongoni kwake, auuze, kwa huo, Allaah Ahifadhie heshima yake ni bora, kuliko kuombaomba watu, wawe wanakupa au wanakunyima.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]
519.
وَعَنْ سَمُرَةَ بْنِ جُنْدُبٍ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {اَلْمَسْأَلَةُ كَدٌّ يَكُدُّ بِهَا اَلرَّجُلُ وَجْهَهُ، إِلَّا أَنْ يَسْأَلَ اَلرَّجُلُ سُلْطَانًا، أَوْ فِي أَمْرٍ لَا بُدَّ مِنْهُ} رَوَاهُ اَلتِّرْمِذِيُّ وَصَحَّحَهُ
Kutoka kwa Samurah bin Jundub (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Kuomba ni mikwaruzo inayoharibu uso wa mtu isipokuwa akimuomba mtawala,[8] au katika hali ambayo hana budi nayo.” [Imetolewa na At-Tirmidhiy ambaye pia aliisahihisha]
[1] Hicho ‘Kivuli’ kinamaanisha kuwa kila Swadaqah inayotolewa itageuka kuwa mwavuli kwa mtoaji Swadaqah ambao utamkinga dhidi ya jua lichomalo sana Siku ya Qiyaamah. Moja ya faida za Swadaqah ya khiari ni kuwa itakuwa kama dawa ya mapungufu katika Zakaah ya fardhi.
[2] Imekatazwa kuwapa Swadaqah watu baki kama watu wa familia yako wana shida kubwa. Kwa mujibu wa Muslim, imesimuliwa na Thawbaan kuwa, sehemu bora ya pesa ni ima ile iliyotomika kwa familia yako, au pesa zilizotumika kwa ajili ya farasi aliyetumika katika vita vya Jihaad (vita ya kidini) au pesa zilizotumika kwa marafiki.
[3] Inamaanisha kuwa, ilimradi mke huyo hana dhamiri ya siri ya kuidhuru nyumba ya mumewe, anaweza kutoa Swadaqah kama ilivyo desturi. Anaweza kumpa muombaji maskini mikate au unga. Ikiwa inahitajika Swadaqah zaidi, basi ni sharti apate idhini kutoka kwa mume wake.
[4] Inamaanisha kwamba, Allaah (سبحانه وتعالى) Atampa kila mtu thawabu au zawadi kamili kwa Ukarimu Wake. Si kama Anayo zawadi moja tu anayoigawanya hiyo hiyo miongoni mwa watu wote. Hii inathibitisha kuwa mtu sharti umsaidie kila mtu kutenda matendo mema ili na yeye apate zawadi.
[5] Zaynab alikuwa anatoka kwa Banuw Thaqiyf, na babake aliitwa Mu’aawiyah, au ‘Abdullaah bin Mu’aawiyah, au Abuu Mu’aawiyah. Alisimulia kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), mume wake, ‘Umar bin Al-Khatwaab, mwanawe, mpwa wake, na wengine walisimuliwa kutoka kwake.
[6] Hilo neno Swadaqah linawahusu watu wote, iwe ni tendo la khiari au la Swadaqah au tendo la lazima la kulipa Zakaah au Swadaqatul-Fitrw. Qur-aan tukufu imelitaja neno hili la Swadaqah pale tu ilipokuwa ikieleza mambo kuhusu kugawanya na kusambaza fedha za Zakaah. Inapokuwa hiyo Swadaqah ya khiari siyo kubwa sana, basi kwa kawaida huashiria tendo la wajibu la kutoa Swadaqah (Zakaah). Hapa inaelekea kuwa ni ulipaji wa lazima wa Swadaqah kwani mtu hana haja ya kuomba ruhusa ya mtu yeyote kuhusu Swadaqah ya khiari. Wengi wa Wanazuoni wanaafikiana kuwa mke anaweza kumpa mumewe. Halikadhalika kuna maafikiano ya maoni kuwa mwanaume hawezi kumpa Zakaah mkewe.
[7] Iwapo mtu asiyestahili anakusanya pesa kwa kuombaomba, atapata fedheha na aibu Siku ya Qiyaamah na atakabiliwa na mateso ya motoni. Kuna aina tatu za watu wanaostahili kupewa pesa ya Zakaah:
(a) Mtu ambaye mali yake inateketezwa ghafla na balaa lisilotazamiwa kiasi kwamba hana kitu hata cha kula. Mtu kama huyo anaweza kuomba pesa za Zakaah ili ziweze kumkimu.
(b) Mtu ambaye ameadhibiwa kimaonezi, au mtu aliyemkingia kifua au alisaini dhamana au mkataba fulani kwa ajili ya mtu mwingine na sasa analazimishwa alipe pesa kwa ajili ya huyo mtu mwingine ingawa hana pesa za kutosha kulipia hilo. Mtu kama huyo ana haki ya kupewa pesa za Zakaah ili awe na pesa za kutosha kulipia deni hilo.
(c) Mtu ambaye anafanya kazi au anataka kwa dhati kufanya kazi kwa uaminifu na bidii zote lakini haipati kazi, au mwenye pato dogo kuliko kiwango kinachotosheleza matumizi yake na kwa hivyo analazimika kukabiliwa na njaa.
[8] Hii inatujulisha kwamba kumuendea mfalme na kumuomba msaada wa kipesa inaruhusiwa. Mfalme anaruhusiwa ima kumpa mtu Swadaqah kutoka katika malipo ya Zakaah, au kutoka katika Khumus (moja ya tano ya mali iliyotokana na ngawira za vita na kupangiwa ihifadhiwe katika hazina). Iwapo muombaji ni maskini sana, anaweza kupewa kutoka kwenye Zakaah. Lakini akiwa ni tajiri, asipewe pesa kutoka katika Zakaah, bali apewe kutoka katika Khumus (fedha kutoka hazina ya serikali).
بُلُوغُ الْمَرام
Buluwgh Al-Maraam
كِتَابُ اَلزَّكَاةُ
Kitabu Cha Zakaah
بَابُ قَسْمِ اَلصَّدَقَاتِ
04-Mlango Wa Ugawaji Wa Swadaqah
520.
عَنْ أَبِي سَعِيدٍ اَلْخُدْرِيِّ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {لَا تَحِلُّ اَلصَّدَقَةُ لِغَنِيٍّ إِلَّا لِخَمْسَةٍ: لِعَامِلٍ عَلَيْهَا، أَوْ رَجُلٍ اِشْتَرَاهَا بِمَالِهِ، أَوْ غَارِمٍ، أَوْ غَازٍ فِي سَبِيلِ اَللَّهِ، أَوْ مِسْكِينٍ تُصُدِّقَ عَلَيْهِ مِنْهَا، فَأَهْدَى مِنْهَا لِغَنِيٍّ} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَأَبُو دَاوُدَ، وَابْنُ مَاجَهْ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ، وَأُعِلَّ بِالْإِرْسَالِ
Kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Swadaqah si halali kwa anayejitosheleza isipokuwa kwa mambo matano: Mtu anayeikusanya, au mtu anayeinunua kwa pesa zake, au alielemewa, au mtu anayepigania Dini ya Allaah, au mtu masikini ambaye baada ya kupewa Swadaqah humpa sehemu yake mtu tajiri kama zawadi.”[1] [Imetolewa na Ahmad, Abuu Daawuwd na Ibn Maajah, na akaisahihisha Al-Haakim]
521.
وَعَنْ عُبَيْدِ اَللَّهِ بْنِ عَدِيِّ بْنِ اَلْخِيَارِ، {أَنَّ رَجُلَيْنِ حَدَّثَاهُ أَنَّهُمَا أَتَيَا رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَسْأَلَانِهِ مِنَ اَلصَّدَقَةِ، فَقَلَّبَ فِيهِمَا اَلْبَصَرَ، فَرَآهُمَا جَلْدَيْنِ، فَقَالَ: "إِنْ شِئْتُمَا، وَلَا حَظَّ فِيهَا لِغَنِيٍّ، وَلَا لِقَوِيٍّ مُكْتَسِبٍ".} رَوَاهُ أَحْمَدُ وَقَوَّاهُ، وَأَبُو دَاوُدَ، وَالنَّسَائِيُّ
Kutoka kwa ‘Ubaydullaah bin ‘Adiyy bin Al-Khiyaar[2] amesema kuwa: “Watu wawili walituarifu kuwa walikwenda kwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kuomba Swadaqah. Akawatazama juu mpaka chini, na alipowaona wako imara, akawaambia: “Mkitaka nitawapa, lakini kitu hicho hakipati mtu yeyote ambaye ni tajiri au mtu ambaye ana nguvu mwenye uwezo wa kuchuma.”[3] [Imetolewa na Ahmad na ikaimarishwa na Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy]
522.
وَعَنْ قَبِيصَةَ بْنِ مُخَارِقٍ اَلْهِلَالِيِّ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {إِنَّ اَلْمَسْأَلَةَ لَا تَحِلُّ إِلَّا لِأَحَدِ ثَلَاثَةٍ: رَجُلٌ تَحَمَّلَ حَمَالَةً، فَحَلَّتْ لَهُ اَلْمَسْأَلَةُ حَتَّى يُصِيبَهَا، ثُمَّ يُمْسِكَ، وَرَجُلٌ أَصَابَتْهُ جَائِحَةٌ، اِجْتَاحَتْ مَالَهُ، فَحَلَّتْ لَهُ اَلْمَسْأَلَةُ حَتَّى يُصِيبَ قِوَامًا مِنْ عَيْشٍ، وَرَجُلٌ أَصَابَتْهُ فَاقَةٌ حَتَّى يَقُومَ ثَلَاثَةٌ مِنْ ذَوِي الْحِجَى مِنْ قَومِهِ: لَقَدْ أَصَابَتْ فُلَانًا فَاقَةٌ; فَحَلَّتْ لَهُ اَلْمَسْأَلَةُ حَتَّى يُصِيبَ قِوَامًا مِنْ عَيْشٍ، فَمَا سِوَاهُنَّ مِنَ اَلْمَسْأَلَةِ يَا قَبِيصَةُ سُحْتٌ يَأْكُلُهَا صَاحِبُهَا سُحْتًا} رَوَاهُ مُسْلِمٌ، وَأَبُو دَاوُدَ، وَابْنُ خُزَيْمَةَ، وَابْنُ حِبَّانَ
Kutoka kwa Qabiyswah bin Mukhaariq Al-Hilaaliyy[4] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Kuomba hakuruhusiwi isipokuwa kwa moja kati ya matatu: (a) Mtu aliyeweka dhamana, ambaye huruhusiwa kuomba hadi amepata kisha ajizuie (b) Mtu ambaye mali zake zimeteketezwa na maafa yaliyomsibu. Ameruhusiwa kuomba hadi atakapopata kiasi cha kumkimu. (c) Mtu aliyefilisika na akawa maskini anayethibitishwa na watu watatu werevu, anaruhusiwa kuomba hadi atakapopata cha kumkimu. Sababu yoyote nyingine ya kuomba Ee Qabiyswah ni haramu na mtu anayeomba hivyo, atakuwa anakula haramu.” [Imetolewa na Muslim, Abuu Daawuwd, Ibn Khuzaymah na Ibn Hibbaan]
523.
وَعَنْ عَبْدِ اَلْمُطَّلِبِ بْنِ رَبِيعَةَ بْنِ اَلْحَارِثِ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {إِنَّ اَلصَّدَقَةَ لَا تَنْبَغِي لِآلِ مُحَمَّدٍ، إِنَّمَا هِيَ أَوْسَاخُ اَلنَّاسِ}
وَفِي رِوَايَةٍ: {وَإِنَّهَا لَا تَحِلُّ لِمُحَمَّدٍ وَلَا آلِ مُحَمَّدٍ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa ‘Abdul Mutwalib bin Rabiy’ah bin Al-Haarith[5] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Hizi Swadaqah hazifai kwa watu wa Rasuli wa Allaah kwani hizo uchafu wa watu.”[6]
Katika Riwaayah nyingine: “Hizo si halaal kwa Muhammad wala familia yake.” [Imetolewa na Muslim]
524.
وَعَنْ جُبَيْرِ بْنِ مُطْعِمٍ رضى الله عنه قَالَ: {مَشَيْتُ أَنَا وَعُثْمَانُ بْنُ عَفَّانَ رضى الله عنه إِلَى اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَقُلْنَا: يَا رَسُولَ اَللَّهِ، أَعْطَيْتَ بَنِي اَلْمُطَّلِبِ مِنْ خُمُسِ خَيْبَرَ وَتَرَكْتَنَا، وَنَحْنُ وَهُمْ بِمَنْزِلَةٍ وَاحِدَةٍ، فَقَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم "إِنَّمَا بَنُو اَلْمُطَّلِبِ وَبَنُو هَاشِمٍ شَيْءٌ وَاحِدٌ".} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ
Kutoka kwa Jubayri bin Mutw’im (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “’Uthmaan bin ‘Affaan (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) na mimi tulimuendea Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) tukamuambia: “Ee Rasuli wa Allaah! Umewapa wana wa Al-Mutwalib Khumus (moja ya tano) ya ngawira ya vita vya Khaybar na hukutupa sisi, na sisi na wawo ni daraja moja.”[7] Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Wana wa ‘Abdul-Mutwalib na wana wa Haashim wote ni wamoja tu.”[8] [Imetolewa na Al-Bukhaariy]
525.
وَعَنْ أَبِي رَافِعٍ رضى الله عنه {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم بَعَثَ رَجُلًا عَلَى اَلصَّدَقَةِ مِنْ بَنِي مَخْزُومٍ، فَقَالَ لِأَبِي رَافِعٍ: اِصْحَبْنِي، فَإِنَّكَ تُصِيبُ مِنْهَا، قَالَ: حَتَّى آتِيَ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم فَأَسْأَلَهُ. فَأَتَاهُ فَسَأَلَهُ، فَقَالَ: " مَوْلَى اَلْقَوْمِ مِنْ أَنْفُسِهِمْ، وَإِنَّا لَا تَحِلُّ لَنَا اَلصَّدَقَةُ ".} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَالثَّلَاثَةُ، وَابْنُ خُزَيْمَةَ، وَابْنُ حِبَّانَ
Kutoka kwa Abuu Raafi’[9] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimtuma mtu wa Banuw Makhzuwm kwenda kukusanya Swadaqah na akamtaka Abuu Raafi’ aende naye ili akapate sehemu ya hiyo. Abuu Raafi’ akasema: “Hapana siendi hadi nikamuulize Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Alipokwenda kumuuliza Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Swadaqah imeharamishwa kwetu sisi, na mtumwa[10] wa watu ni mmoja wapo.” [Imetolewa na Ahmad, na Ath-Thalaathah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd), Ibn Khuzaymah na Ibn Hibbaan]
526.
وَعَنْ سَالِمِ بْنِ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ عُمَرَ، عَنْ أَبِيهِ، {أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم كَانَ يُعْطِي عُمَرَ اَلْعَطَاءَ، فَيَقُولُ: أَعْطِهِ أَفْقَرَ مِنِّي، فَيَقُولُ: "خُذْهُ فَتَمَوَّلْهُ، أَوْ تَصَدَّقْ بِهِ، وَمَا جَاءَكَ مِنْ هَذَا اَلْمَالِ، وَأَنْتَ غَيْرُ مُشْرِفٍ وَلَا سَائِلٍ فَخُذْهُ، وَمَا لَا فَلَا تُتْبِعْهُ نَفْسَكَ".} رَوَاهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Saalim bin ‘Abdillaah bin ‘Umar kwa upokezi wa baba yake amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimpa zawadi ‘Umar, naye akamuambia: “Mpe mtu ambaye ni maskini kuliko mimi.” Aliposikia hivyo, Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aksema: “Wewe chukua, na uifanye mali yako, au uigawe kama Swadaqah. Chukua kinachokuja katika mali hii wala wewe huna uroho wala huombi, lakini isiyokuwa hiyo usiuache moyo wako uitamani.” [Imetolewa na Muslim]
[1] Imekatazwa kwa mtu tajiri kuchukua pesa zozote kutoka katika Zakaah lakini ikiwa mtu maskini atapata pesa za Zakaah, akanunua kitu kwa pesa hizi na akampa hicho mtu tajiri, inaruhusiwa.
[2] ‘Ubaydullaah bin ‘Adiyy bin Al-Khiyaar alikuwa Mkuraishi kutoka Banuw Nawfal. Alizaliwa wakati Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) bado yu hai, lakini anahesabika miongoni mwa Taabi’iyn. Alisimulia Hadiyth kutoka kwa ‘Umar na ‘Uthmaan na wengine. Inasemekana kuwa babake aliuawa kule Badr kama kafiri. ‘Ubaydullaah anasemekana kuwa alikuwa kijana mkubwa wakati Makkaah ilipotekwa, na kwa hivyo alikuwa Swahaba. Alikuwa miongoni mwa utawala wa Al-Waliyd bin Abdil-Maalik mnamo mwaka wa 90 A.H.
[3] Watu wengine wanaitafsiri Hadiyth hii kwamba, mtu anayeweza kufanya kazi ya kipato, hata kama yeye ni maskini, asipokee Swadaqah. Tafsiri hii siyo sahihi. Hadiyth nyingine inaweka wazi kwa kusema, mtu ambaye yuko karibu na kufa kwa njaa anaweza kuomba Swadaqah.
[4] Qabiyswah bin Mukhaariq Al-Hilaaliyy ndiye Abuu Bishr Qabiyswah bin Al-Mukhaariq bin ‘Abdillaah bin Shaddaad Al-‘Aamir Al-Hilaal, alikuwa ni Swahaba aliyelowea Basra. Alimzuru Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) na akasimulia Hadiyth kutoka kwake. Yeye ni msimulizi wa Hadiyth sita.
[5] ‘Abdul Mutwalib bin Rabiy’ah bin Al-Haarith ndiye mwana wa ‘Abdul-Mutwalib bin Haashim Al-Qurayashiy. Alilowea Al-Madiynah, kisha akahamia Damascus ambako alifia.
[6] Imekatazwa kwa kila kizazi cha Muhammad (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kukubali malipo ya Zakaah. Hukmu hii imeafikiwa. Hata hivyo, kuna tofauti ya maoni juu ya hali ya Swadaqah ya khiari. Hawa siyo vizazi vya Muhammaad (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) peke yake wanaoharamishiwa kupokea malipo za Zakaah, bali wamo pia vizazi vya ‘Aliy, ‘Abbaas, Ja’far, ‘Aaqil, ‘Abdul-Mutwalib bin ‘Abd-Manaaf ambayo inamaanisha kuwa wote hawa wamo katika familia ya Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ).
[7] Usemi wa Jubayr bin Mutw’im na ‘Uthmaan (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) kuwa wao wako sawa au daraja zao sawa una maana mbili: (a) Wote wanamtii Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kwa njia ile ile kama vizazi vya Al-Mutwalib wanavyomtii. (b) Banuw Mutwalib hawawapiti wao katika kustahili kutokana na miungano ya mahusiano na udugu kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). ‘Uthmaan baki ya kupewa heshima ya kuwa mkwe wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) pia anatoka katika ukoo wa Banuw Umayiyyah. Banuw Umayiyya na Banuw Haashim walihisabika kuwa makabila yaliyo sawa kwa mujibu wa hadhi yao miongoni mwa vizazi vya Maquraishi.
[8] Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) Amesema hivi: “Hakuna ubishi kuwa kuhusu daraja, na ukoo, Banuw Haashim na Banuw Umayiyyah wako sawa kabisa. Lakini Banuw Mutwalib waliungana na upande wa Waislam, wakati Banuw Nawfal na Banuw Abdish-Shams waliwapinga Waislam. Kwa sababu hiyo Banuw Haashim na Banuw Mutwalib wako sawa, na wakati ulipofika, walipewa Khumus ya pesa lakini ninyi hamkupewa chochote.”
[9] Abuu Raafi’ alikuwa mtumwa wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), na jina lake ni Aslam au Hurmuz au Thaabit au Ibraahiym. Alikuwa Mkipti wa Misri na alimilikiwa na Al-‘Abbaas aliyemzawadia Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Alisilimu kabla ya Badr, na hakuwahi kuishuhudia vita ile. Alishuhudia vita za Uhud na zilizofuata. Al-‘Abbaas aliposilimu, Abuu Raafi’ ndiye aliyempa habari hizo njema Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) ambaye alimuacha huru. Alikufa mwanzo mwanzo wa Ukhalifa wa ‘Aliy mnamo mwaka wa 36 A.H. kule Al-Madiynah.
[10] Mtu ambaye kaharamishiwa kupokea Zakaah hata mtumwa wake ni haraam kupokea
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/277
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9152&title=04-Buluwgh%20Al-Maraam%3A%20Kitabu%20Cha%20Zakaah%20-%20%20%20%D9%83%D9%90%D8%AA%D9%8E%D8%A7%D8%A8%D9%8F%20%D8%A7%D9%8E%D9%84%D8%B2%D9%91%D9%8E%D9%83%D9%8E%D8%A7%D8%A9
[3] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9153&title=01-Buluwgh%20Al-Maraam%3A%20Kitabu%20Cha%20Zakaah%3A%20Mlango%20Wa%20Zakaah%20Ya%20Mali
[4] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9154&title=02-Buluwgh%20Al-Maraam%3A%20Kitabu%20Cha%20Zakaah%3A%20Mlango%20Wa%20Zakaatul-Fitwr
[5] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9155&title=03-Buluwgh%20Al-Maraam%3A%20Kitabu%20Cha%20Zakaah%3A%20Mlango%20Wa%20Swadaqah%20Za%20Khiari
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9156&title=04-Buluwgh%20Al-Maraam%3A%20Kitabu%20Cha%20Zakaah%3A%20Mlango%20Wa%20Ugawaji%20Wa%20Swadaqah