SWALI:
Assalam alikum warahma tullahi taala wabarakatu,
Ni nini unatakiwa kufanya ili umsilimishe mtu?... Naombeni jibu, kwasababu nina rafiki yangu ambaye ananiya ya kuingia kwenye uislamu ila sina uhakika wa taratibu ya kusilimisha mtu asiye muislamu. Shukran nategemea jibu hivi karibuni... wabillahi tauri
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Kumsilimisha mtu ni jambo jepesi kabisa ila baada ya kumsilimisha kuna ya muhimu ya kuzingatia ambayo tunakuwekea maelezo chini ya hizi taratibu za kumsilimisha.
Kwanza kabisa
Ash-hadu an laa ilaaha illa-Allaah, wa ashhadu anna Muhammadar Rasuulu-Allaah. (Nakiri na kutamka kuwa hapana apasaye kwa dhati kuabudiwa ila Allaah, na nakiri kuwa Muhammad ni Mjumbe Wake)
(Haya tuliyopigia mstari unaweza kumtaka atamke ingawa si lazima
(Na nakiri kuwa 'Iysa (Yesu) ni Mjumbe wa Allaah na si mungu au mwana wa mungu.'
Wa ash-hadu anna ‘Iysa Rasuulu-Allaah
Akitamka yote hayo hapo juu basi tayari ameshakuwa Muislamu.
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa alihi wa sallam) alimuamrisha Kafiri mwanamume aliyesilimu: ((Nyoa nywele za ukafiri na fanya tohara [jando])). [Abu Daawuud, na imepewa daraja ya Hasan na Shaykh Al-Albaaniy]
Tanbihi: Nywele za kwapani na sehemu za siri zisikae zaidi ya siku arubaini bila ya kunyolewa au kupunguzwa kwa Waislam wote.
Mambo muhimu kutekeleza baada ya kumsimilisha Muislamu
Usimuache baada ya hapo, bali mpe vitabu vya Dini, mfundishe Dini vizuri, ikiwa wewe hujui mtafutie Mwalimu japo umlipe aweze kumfundisha Uislam. Makosa makubwa yanafanywa sana na Waislam, ni kuwa baada ya kumsilimisha mtu humwacha akaenda zake na hawamfuatilizii wala hawamsaidii kumfundisha Dini wala kujua kama anaswali, anafunga n.k. Jaribu kumsaidia kwa hali na mali kadiri uwezavyo ili kumpa moyo na kumuonyesha undugu wa Kiislamu.
Pia makosa makubwa yanatokea kwa kuwa wale wanaowasilimisha watu au kusababisha wasilimu, wao wenyewe hawatekelezi mafundisho ya Dini, hawaswali, hawana tabia njema za Kiislam na hata hawaijui Dini
Tunatumai ndugu yetu humo katika tabia hizo. Na ikiwa ni mtu ambaye hufuati mafunzo ya dini yako kamili, basi hukuchelewa sana, tunakunasihi, uanze kutekeleza na kujifunza kwa kusoma au kuhudhuria madarsa na mihadhara ya Dini n.k. kwani usipofanya hivyo ujue kuwa mtu huyu unayemsilimisha atasilimu jina tu lakini kivitendo hatopata mafunzo na mifano kutoka kwako atabaki kama alivyokuwa katika ukafiri wake kwani atakuwa anakutegemea sana wewe khaswa kwa kupata mafunzo ya dini yake.
Na Allaah Anajua zaidi
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/101
[2] http://www.alhidaaya.com/sw/node/257
[3] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F3016&title=Jinsi%20Ya%20Kumsilimisha%20Mtu%20Kuingia%20Uislamu