Alhidaaya.com
Published on Alhidaaya.com (https://www.alhidaaya.com/sw)

Ukurasa Wa Kwanza > Kuitikia Salaam Au Kumuamkia Asiye Muislam

Kuitikia Salaam Au Kumuamkia Asiye Muislam

Maswali: Shari'ah za Kiislamu [1]

 

Kuitikia Salaam Au Kumuamkia Asiye Muislam

 

Alhidaaya.com [2]

 

 

SWALI:

 

Asalaam Aleykoum Warahmatullah Wabarakatu.

 

Natumai kwa uwezo wa Allah mko katika kheri zake In Shaa Allah. Swali langu naomba mnifahamishe vipi kuitikia salam ya mtu ambaye si Muislam na vipi jinsi ya kumwamkia yeye katika sheria.

 

Wabilahi Tawfiq.

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Kuhusu salaam ambazo Muislamu anatolewa na asiye Muislamu ikiwa ni katika yale maamkuzi ya Kiislamu, yaani asiye Muislamu akikuamkia kwa

 

السَّلامُ عَلَيْكُم

 “Assalaamu ‘Alaykum”,

 

basi wewe unawajibika kumjibu kwa kusema

 وَعَلَيْكُمْ

“Wa ‘Alaykum” [Al-Bukhaariy na Muslim].

 

Ama ikiwa ni habari yako au habari ya asubuhi basi utamjibu kuwa ni nzuri au ni njema.

 

Bonyeza  kiungo kifuatacho upate faida na kwa sauti pia:

 

109-Hiswnul-Muslim: Namna Ya Kumrudishia Salaam Kafiri Anapokusalimia [3]

 

Ama kuanza kumuamkia asiye Muislamu kwa Assalaamu ‘Alaykum haifai kabisa [Ameitoa Imaam Muslim] kwani hiyo ni salaam ya Muislamu kwa mwenziwe. Lakini ikiwa ni zile habari za kawaida habari ya jioni au habari za asubuhi hakuna shida yoyote ile.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

 

 

 

Share [4]
www.alhidaaya.com

Source URL: https://www.alhidaaya.com/sw/node/4775

Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/101
[2] http://www.alhidaaya.com
[3] http://www.alhidaaya.com/sw/node/9842
[4] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F4775&title=Kuitikia%20Salaam%20Au%20Kumuamkia%20Asiye%20Muislam