Alhidaaya.com
Published on Alhidaaya.com (https://www.alhidaaya.com/sw)

Ukurasa Wa Kwanza > Yanayopasa Kufanywa Na Mwenye Mimba Na Baada Ya Kuzaa

Yanayopasa Kufanywa Na Mwenye Mimba Na Baada Ya Kuzaa

Maswali: Uzazi - Malezi [1]

SWALI:

Assaalam aleikum,

Ni mambo gani ya dini yanayompasa mwanamke mwenye mimba kufanya wakati wa hiyo miezi tisa na baada ya kuzaa. Asante.

 


JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Mwanamke Muislamu anayekuwa na mimba anapaswa kufanya yote aliyokuwa akifanya kabla ya kushika mimba. Katika mambo hayo ni kuswali kama kawaida, kufunga funga ya faradhi au ya Sunnah isipokuwa ikiwa kufunga kutamletea matatizo yeye au mtoto wake, kusoma Qur-aan, kuleta dhikri (kumtaja Allaah), kufanya kazi ikiwa ni muajiriwa au ana kazi yake mwenyewe na hata pia kujamiiana na mumewe na mengineyo.

Hakuna ibada haswa ya kufanya mwanamke anapokuwa mja mzito au baada ya kuzaa kama ndivyo ulivyokusudia kuuliza. Ibada zote za kawaida zilizo sahihi zinapaswa kutekelezwa.

Ingia katika viungo vifuatavyo upate maelezo upasayo kufanya kwa ajili ya mtoto:

Utaratibu Wa 'Aqiyqah Katika Sunnah [2]
Kufanya Aqiyqah Ni Lazima Au Sunnah? [3]
Fiqh Ya Kuwaita Majina Watoto [4]

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share [5]
www.alhidaaya.com

Source URL: https://www.alhidaaya.com/sw/node/711

Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/59
[2] http://alhidaaya.com/sw/node/749
[3] http://alhidaaya.com/sw/node/813
[4] http://alhidaaya.com/sw/node/257
[5] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F711&title=Yanayopasa%20Kufanywa%20Na%20Mwenye%20Mimba%20Na%20Baada%20Ya%20Kuzaa