Alhidaaya.com
Published on Alhidaaya.com (https://www.alhidaaya.com/sw)

Ukurasa Wa Kwanza > Shaykh Fawzaan: Sha'baan: Je Laylatul-Qadr Inatokea Katika Nisfwu Sha'baan?

Shaykh Fawzaan: Sha'baan: Je Laylatul-Qadr Inatokea Katika Nisfwu Sha'baan?

Shaykh Fawzaan [1]

 

Je, Laylatul-Qadr Inatokea Katika Nisfwu Sha'baan?

 

Shaykh Swaalih bin Fawzaan Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)

 

Alhidaaya.com [2]

 

 

 

 

SWALI:

 

Je, Laylatul-Qadr inakuwa tarehe 15 Sha'baan?

 

 

JIBU:

 

Hapakuthibiti fadhila yoyote katika usiku wa Niswfu Sha´baan inayotofautiana na masiku wala usiku wowote wa mwezi wa Sha´baan. Hapakuthibiti lolote katika hili.

 

Vilevile wanasema kuwa Laylatul-Qadr inakuwa katika usiku wa Niswfu Sha´baan, si kweli. Laylatul-Qadr inakuwa katika Ramadhwaan. Kwa sababu Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)  Amesema:

إِنَّا أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةِ الْقَدْرِ ﴿١﴾

1. Hakika Sisi Tumeiteremsha Qur-aan katika Laylatil-Qadr (usiku wa Qadar). [Al-Qadr: 01]

 

Laylatul-Qadr inakuwa katika masiku kumi ya mwisho ya Ramadhwaan. Hili ni kwa Ijmaa´. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anaitafuta katika Ramadhwaan na hakuwa anaitafuta katika mwezi wa Sha´baan.

 

Wapi wametoa haya kwamba Laylatul-Qadr inakuwa katika usiku wa Niswfu Sha´baan?

 

 

[Al-Mawqi’ Ar-Rasmiy li-Ma’aaliy Ash-Shaykh Ad-Duktuwr Swaalih bin Fawzaan Bin ‘Abdillaah Al-Fawzaan] [3]

 

 

Share [4]
www.alhidaaya.com

Source URL: https://www.alhidaaya.com/sw/node/9069

Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/208
[2] http://www.alhidaaya.com/
[3] http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/liqo-24-07-1435-01.mp3
[4] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9069&title=Shaykh%20Fawzaan%3A%20Sha%27baan%3A%20Je%20Laylatul-Qadr%20Inatokea%20Katika%20Nisfwu%20Sha%27baan%3F