كِتَابُ الْجأمِعِ
Kitabu Cha Mjumuisho
بُلُوغُ الْمَرام
Buluwgh Al-Maraam
كِتَابُ اَلْجَامِعِ
Kitabu Cha Mjumuisho
بَابُ اَلْأَدَبِ
01-Mlango Wa Adabu
1236.
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {حَقُّ اَلْمُسْلِمِ عَلَى اَلْمُسْلِمِ سِتٌّ: إِذَا لَقِيتَهُ فَسَلِّمْ عَلَيْهِ، وَإِذَا دَعَاكَ فَأَجِبْهُ، وَإِذَا اِسْتَنْصَحَكَ فَانْصَحْهُ، وَإِذَا عَطَسَ فَحَمِدَ اَللَّهَ فَسَمِّتْهُ وَإِذَا مَرِضَ فَعُدْهُ، وَإِذَا مَاتَ فَاتْبَعْهُ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Haki ya Muislaam juu ya Muislaam ni sita:[1] unapokutana naye msalimie, anapokualika muitike, anapokutaka nasaha mnasihi, anapopiga chafya na akamhimidi Allaah mrehemu, anapougua mtembelee na akifa msindiize.” [Imetolewa na Muslim]
1237.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {انْظُرُوا إِلَى مَنْ هُوَ أَسْفَلَ مِنْكُمْ، وَلَا تَنْظُرُوا إِلَى مَنْ هُوَ فَوْقَكُمْ، فَهُوَ أَجْدَرُ أَنْ لَا تَزْدَرُوا نِعْمَةَ اَللَّهِ عَلَيْكُمْ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mtazameni ambaye yuko chini yenu[2] wala msimtazame ambaye yuko juu yenu, kwani kufanya hivyo hamtadharau neema za Allaah juu yenu.” [Bukhaariy, Muslim]
1238.
وَعَنْ اَلنَوَّاسِ بْنِ سَمْعَانَ رضى الله عنه قَالَ: سَأَلْتُ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم عَنْ اَلْبِرِّ وَالْإِثْمِ؟ فَقَالَ: {اَلْبِرُّ: حُسْنُ اَلْخُلُقِ، وَالْإِثْمُ: مَا حَاكَ فِي صَدْرِكَ، وَكَرِهْتَ أَنْ يَطَّلِعَ عَلَيْهِ اَلنَّاسُ} أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Anawwaas bin Sam’aan[3] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema nilimuuliza Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ): “Kuhusu wema na dhambi, akasema: “Wema ni tabia njema,[4] na dhambi[5] ni inayotia shaka katika nafsi yako na ukachukia watu kuona.” [Imetolewa na Muslim]
1239.
وَعَنْ اِبْنِ مَسْعُودٍ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {إِذَا كُنْتُمْ ثَلَاثَةً، فَلَا يَتَنَاجَى اِثْنَانِ دُونَ اَلْآخَرِ، حَتَّى تَخْتَلِطُوا بِالنَّاسِ; مِنْ أَجْلِ أَنَّ ذَلِكَ يُحْزِنُهُ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ، وَاللَّفْظُ لِمُسْلِمٍ.
Kutoka kwa Ibn Mas-‘uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mnapokuwa watatu, wawili wasinong’one bila yule mwingine (kusikia)[6] mpaka mchanganyike na watu, kwani hilo litamhuzunisha.” [Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Muslim]
1240.
وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {لَا يُقِيمُ اَلرَّجُلُ اَلرَّجُلَ مِنْ مَجْلِسِهِ، ثُمَّ يَجْلِسُ فِيهِ، وَلَكِنْ تَفَسَّحُوا، وَتَوَسَّعُوا} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mmoja wenu asimsimamishe mtu kwenye kikao chake kisha akaketi yeye,[7] lakini kunjukeni na toeni nafasi.” [Bukhaariy, Muslim]
1241.
وَعَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {إِذَا أَكَلَ أَحَدُكُمْ طَعَامًا، فَلَا يَمْسَحْ يَدَهُ، حَتَّى يَلْعَقَهَا، أَوْ يُلْعِقَهَا} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ.
Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Anapomaliza kula mmoja wenu asipanguse vidole vyake mpaka avirambe au avirambishe.”[8] [Bukhaariy, Muslim]
1242.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {لِيُسَلِّمْ اَلصَّغِيرُ عَلَى اَلْكَبِيرِ، وَالْمَارُّ عَلَى اَلْقَاعِدِ، وَالْقَلِيلُ عَلَى اَلْكَثِيرِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
وَفِي رِوَايَةٍ لِمُسْلِمٍ: {وَالرَّاكِبُ عَلَى اَلْمَاشِي}
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mdogo amsalimie mkubwa, anayetembea amsalimie aliye kaa,[9] na wachache wawasalimie wengi.” [Bukhaariy, Muslim]
Na katika Riwaayah ya Muslim: “…na aliyepanda amsalimie anayetembea.”
1243.
وَعَنْ عَلِيٍّ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {يُجْزِئُ عَنْ اَلْجَمَاعَةِ إِذَا مَرُّوا أَنْ يُسَلِّمَ أَحَدُهُمْ، وَيُجْزِئُ عَنْ اَلْجَمَاعَةِ أَنْ يَرُدَّ أَحَدُهُمْ} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَالْبَيْهَقِيُّ
Kutoka kwa ‘Aliy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Kundi linatoshelezwa kwa mtu mmoja wao kusalimia, na mtu mmoja wao hutosheleza anapojibu salaam.”[10] [Imetolewa na Ahmad na Al-Bayhaqiyy]
1244.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم { لَا تَبْدَؤُوا اَلْيَهُودَ وَالنَّصَارَى بِالسَّلَامِ، وَإِذَا لَقَيْتُمُوهُمْ فِي طَرِيقٍ، فَاضْطَرُّوهُمْ إِلَى أَضْيَقِهِ } أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Msianze kuwasalimia Mayahudi wala Manaswara,[11] munapokutana na mmoja wao njiani msogezeni upande wenye dhiki zaidi.”[12] [Imetolewa na Muslim]
1245.
وَعَنْهُ عَنْ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: {إِذَا عَطَسَ أَحَدُكُمْ فَلْيَقُلْ: اَلْحَمْدُ لِلَّهِ، وَلْيَقُلْ لَهُ أَخُوهُ يَرْحَمُكَ اَللَّهُ، فَإِذَا قَالَ لَهُ: يَرْحَمُكَ اَللَّهُ، فَلْيَقُلْ: يَهْدِيكُمُ اَللَّهُ، وَيُصْلِحُ بَالَكُمْ} أَخْرَجَهُ اَلْبُخَارِيُّ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Akipiga chafya mmoja wenu aseme:
اَلْحَمْدُ لِلَّهِ
Alhamdulillaah[13]
na nduguye au mwenzie amuambie
يَرْحَمُكَ اَللَّهُ
(Allaah Akurehemu).
Atakapomuambia
يَرْحَمُكَ اَللَّهُ
naye amuambie:
يَهْدِيكُمُ اَللَّهُ، وَيُصْلِحُ بَالَكُمْ
(Allaah Awaongeze na Awatengenezee mambo yenu).” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]
1246.
وَعَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {لَا يَشْرَبَنَّ أَحَدٌ مِنْكُمْ قَائِمًا} أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Asinywe mmoja wenu kwa kusimama.”[14] [Imetolewa na Muslim]
1247.
وَعَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {إِذَا اِنْتَعَلَ أَحَدُكُمْ فَلْيَبْدَأْ بِالْيَمِينِ، وَإِذَا نَزَعَ فَلْيَبْدَأْ بِالشِّمَالِ، وَلْتَكُنْ اَلْيُمْنَى أَوَّلَهُمَا تُنْعَلُ، وَآخِرَهُمَا تُنْزَعُ}
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Anapovaa mmoja wenu viatu aanze kulia, na anapovua aanze kushoto. Upande wa kulia uwe wa kwanza kuvaliwa na wa mwisho kuvuliwa.”[15]
1248.
وَعَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {لَا يَمْشِ أَحَدُكُمْ فِي نَعْلٍ وَاحِدَةٍ، وَلْيُنْعِلْهُمَا جَمِيعًا، أَوْ لِيَخْلَعْهُمَا جَمِيعًا} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Asitembee mmoja wenu kwa kiatu kimoja, avae vyote au avue vyote.”[16] [Bukhaariy, Muslim]
1249.
وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {لَا يَنْظُرُ اَللَّهُ إِلَى مَنْ جَرَّ ثَوْبَهُ خُيَلَاءَ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Allaah Hamtazami anayeburuta nguo yake kwa kibri.”[17] [Bukhaariy, Muslim]
1250.
وَعَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: {إِذَا أَكَلَ أَحَدُكُمْ فَلْيَأْكُلْ بِيَمِينِهِ، وَإِذَا شَرِبَ فَلْيَشْرَبْ بِيَمِينِهِ، فَإِنَّ اَلشَّيْطَانَ يَأْكُلُ بِشِمَالِهِ، وَيَشْرَبُ بِشِمَالِهِ} أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Anapokula mmoja wenu ale kwa mkono wa kulia. Na anapokunywa anywe kwa kulia kwake. Kwa hakika shaytwaan hula anapotumia kushoto na hunywa anapokunywa kwa kushoto kwake.”[18] [Imetolewa na Muslim]
1251.
وَعَنْ عَمْرِو بْنِ شُعَيْبٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {كُلْ، وَاشْرَبْ، وَالْبَسْ، وَتَصَدَّقْ فِي غَيْرِ سَرَفٍ، وَلَا مَخِيلَةٍ} أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ، وَأَحْمَدُ، وَعَلَّقَهُ اَلْبُخَارِيُّ
Kutoka kwa ‘Amr bin Shu’ayb kutoka kwa baba yake, naye kutoka kwa babu yake amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Kula, kunywa, vaa na utoe swadaqah bila ya israfu wala kibri.”[19] [Imetolewa na Abuu Daawuwd na Ahmad. Bukhaariy ameitaja kuwa ni Mu’allaq]
[1] Tunajifunza katika Hadiyth hii kuwa kusimamia majukumu haya ni wajibu. Baadhi ya Wanazuoni wanaona kuwa ni Mandub ambayo haitakiwi kuachwa hata mara moja.
[2] Hili ni hamasisho kwa watu kulinganisha hali zao kiuchumi na wale walio chini yao, kwani kufanya hivyo kunajenga iymaan na kuwa na taqwa zaidi katika moyo wa mtu. Mara nyingi kuwaangalia watu walio juu na hadhi kunapelekea katika tamaa, ambayo inapelekea katika hisia ya kutoridhika na husuda na wivu juu yao.
[3] Anawwaas bin Sam’aan bin Khaalid Al-Kilabi Al-‘Amiri alikuwa ni Swahaba katika watu wa Shaam. Inasemekana kuwa baba yake alimtembelea Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) ambaye alimuombea. Alimpa pea za ndara ambazo Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alizipokea.
[4] Tabia njema inahusisha utii kwa Allaah, kutoa swadaqah, kuwatendea watu vizuri, kuwavumilia wanaokukosea, kuhusubiana nao kwa wema, kuimarisha ujamaa na udugu na watu n.k.
[5] Kuna madhambi ya aina mbili: (a) Ni yale makatazo ya kishariy’ah yaliyokuwa wazi. Ni wajibu kwa watu wote kuachana nayo. (b) Ni yale ambayo makatazo yake hayako wazi ila ni mambo ambayo hayapendwi kufanywa, na watu wanayachukia na kuhusu uzito juu yake. Hivyo basi, ni bora kuyaacha.
[6] Hadiyth hii inathibitisha Uislaam kuheshimu hisia za watu. Watu hawatakiwi kufanya vitu vitakavyowaletea watu wengine hisia mbaya.
[7] Hii inathibitisha kuwa ni haki ya mtu aliyekaa katika kikao cha awali kuendelea kukaa pale mwanzo. Haruhusiwi mtu mwingine kukaa sehemu aliyokwisha kaa mwenzake hata kama atakuwa ametoka kidogo basi ni haki yake pale atakaporudi. Au hawezi kumuondoa sehemu aliyekwisha kaa isipokuwa kwa kuomba kusogezana nae apate nafasi.
[8] Sababu ya tukio hili limeelezwa na maneno ya Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ): “Hujui ni sehemu gani katika chakula chako chenye baraka.”
[9] Hadiyth nyingine inaelezea kuwa waliopanda wawasalimie wanaotembea na anayepita amsalimie aliyesimama. Ikiwa kuna watu wawili wanatembea, mmoja inapasa amsalimie mwenzake. Hata hivyo, mbora ni yule anayeanza kutoa salaam. Wanazuoni wamekubaliana kuwa suala hili sio suala la mtu kutaka au kutotaka bali ni suala la lazima.
[10] Kuanza kutoa salaam ni suala la lazima kwa wote na kujibu ni suala la lazima kwa wote. Hata hivyo inatosheleza kama mmoja atasalimia na wengine kujibu.
[11] Wanazuoni wengi wa mwanzo wana rai kuwa Muislaam asitangulie kumsalimia kafiri. Akitoa salaam basi salaam yake ijibiwe. Wanazuoni wengine ni wenye rai kuwa ni ruhusa Waislaam kuanza kuwasalimia makafiri kama si jambo linaloweza kuzuilika.
[12] Kuwabana kwenye njia ya dhiki ni kutowapa heshima yao. Kama sehemu ina zahama basi amruhusu kwanza Muislaam apite kisha afuatie kafiri.
[13] Mtu anatakiwa aendelee kujibu hadi chafya ya tatu (zenye kufuatana). Chafya ikiongezeka zaidi ya hapo hatakiwi kujibu.
[14] Kunywa maji kwa kusimama hakuingii katika makatazo makubwa, bali ni makatazo ya kushauri, ila ikiwa mtu ana sababu za kishariy’ah.
[15] Kimsingi kila jambo zuri linatakiwa lianze kwa upande wa kuume, wakati mambo mengine ni kwa upande wa kushoto. Kwa mfano, kuvaa viatu, kuchana nywele na kuchukua ‘udwuu yote yanatakiwa yaanze kwa upande wa kuume, kuvua viatu, kujisafisha katika sehemu za siri yaanze upande wa kushoto.
[16] Hili vile vile ni katazo la kushauri, silo tatizo kubwa, na huu ndio muono wa Wanazuoni wengi.
[17] Mtu ambaye nguo yake inaburuza chini ya kifundo kwa kusahau au kwa kuwa tumbo lake ni kubwa kiasi cha kuwa hawezi kuzuia nguo yake kuanguka, ni watu wasio husika na hukumu hii. Pamoja na kuwa adhabu inahusisha suala la kibri lakini kuna makatazo ya jumla (bila hata kuhusisha kibri cha mtu) ya kutoruhusu nguo kuwa chini ya vifundo viwili, kulingana na Hadiyth zingine Swahiyh. Hukumu hii inawahusu wanaume peke yao, kwani wanawake wanaelekezwa washushe nguo zao kiasi cha kufunika miguu yao.
[18] Hadiyth hii inasisitiza matumizi ya mkono wa kulia kwa kulia na kunywea, ama makatazo ni kwa ajili ya mkono wa kushoto kufanyia mambo hayo.
[19] Katika Hadiyth hii tunapata maelezo ya ndani zaidi kuhusu aayah ya Qur-aan inayosema:
وَكُلُوا وَاشْرَبُوا وَلَا تُسْرِفُوا
(…na kuleni na kunyweni…) [Al-A’raaf: 31].
Hadiyth hii inasisitiza maadamu ni haraam kufanya matumizi ya kupindukia kwa vitu vilivyokuwa ni halaal kwa mtu, iweje iruhusiwe kwa vitu ambavyo vimekatazwa kabisa. Matumizi haya ya kupindukia katika lugha ya Kiarabu yanaitwa Israaf.
بُلُوغُ الْمَرام
Buluwgh Al-Maraam
كِتَابُ اَلْجَامِعِ
Kitabu Cha Mjumuisho
بَابُ اَلْبِرِّ وَالصِّلَةِ
02-Mlango Wa Wema Na Kuunga Kizazi
1252.
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {مَنْ أَحَبَّ أَنْ يُبْسَطَ عَلَيْهِ فِي رِزْقِهِ، وَأَنْ يُنْسَأَ لَهُ فِي أَثَرِهِ، فَلْيَصِلْ رَحِمَهُ} أَخْرَجَهُ اَلْبُخَارِيُّ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Anayependa kukunjuliwa rizki yake na kurefushwa umri wake na aunge kizazi chake.”[1] [Imetolewa na Al-Bukhaariy]
1253.
وَعَنْ جُبَيْرِ بْنِ مُطْعِمٍ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {لَا يَدْخُلُ اَلْجَنَّةَ قَاطِعٌ} يَعْنِي: قَاطِعَ رَحِمٍ. مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Jubayr bin Mutw’im (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Hataingia Jannah mkataji (yaani mkata udugu).”[2] [Bukhaariy, Muslim]
1254.
وَعَنْ اَلْمُغِيرَةِ بْنِ سَعِيدٍ رضى الله عنه عَنْ رَسُولِ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: {إِنَّ اَللَّهَ حَرَّمَ عَلَيْكُمْ عُقُوقَ اَلْأُمَّهَاتِ، وَوَأْدَ اَلْبَنَاتِ، وَمَنْعًا وَهَاتِ، وَكَرِهَ لَكُمْ قِيلَ وَقَالَ، وَكَثْرَةَ اَلسُّؤَالِ وَإِضَاعَةَ اَلْمَالِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Al-Mughiyrah bin Sa’iyd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Hakika Allaah Amewaharamishia kuwaasi mama (zenu), na kuzuia na kukusanya (mali), kuzika mabinti (wakiwa hai). Na Amechukia kwenu: maneno ya uzushi, kuuliza kwingi na kuharibu mali.” [Bukhaariy, Muslim]
1255.
وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا، عَنْ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: {رِضَا اَللَّهِ فِي رِضَا اَلْوَالِدَيْنِ، وَسَخَطُ اَللَّهِ فِي سَخَطِ اَلْوَالِدَيْنِ} أَخْرَجَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ وَالْحَاكِمُ
Kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Radhi ya Allaah iko katika radhi ya wazazi wawili, na hasira za Allaah ziko katika hasira za wazazi wawili.”[3] [Imetolewa na At-Tirmidhiy, na akaisahihisha Ibn Hibbaan na Al-Haakim]
1256.
وَعَنْ أَنَسٍ رضى الله عنه عَنْ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: {وَاَلَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لَا يُؤْمِنُ عَبْدٌ حَتَّى يُحِبَّ لِجَارِهِ أَوْ لِأَخِيهِ مَا يُحِبُّ لِنَفْسِهِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mkononi Mwake, haamini mja yeyote mpaka ampendelee jirani yake au nduguye (Muislamu) analopendelea nafsi yake.”[4] [Bukhaariy, Muslim]
1257.
وَعَنْ اِبْنِ مَسْعُودٍ رضى الله عنه قَالَ سَأَلْتُ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَيُّ اَلذَّنْبِ أَعْظَمُ؟ قَالَ: {أَنْ تَجْعَلَ لِلَّهِ نِدًّا، وَهُوَ خَلَقَكَ. قُلْتُ ثُمَّ أَيُّ؟ قَالَ: ثُمَّ أَنْ تَقْتُلَ وَلَدَكَ خَشْيَةَ أَنْ يَأْكُلَ مَعَكَ. قُلْتُ: ثُمَّ أَيُّ؟ قَالَ: ثُمَّ أَنْ تُزَانِيَ حَلِيلَةَ جَارِكَ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Ibn Mas-‘uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema nilimuuliza Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ): “Ni dhambi gani kubwa zaidi? Akasema: ni kumfanyia Allaah mshirika hali Yeye Amekuumba. Nikasema: kisha ni dhambi gani? Akasema: ni kumuua mwanao kwa kuogopa asije kula pamoja nawe. Nikasema: kisha ni dhambi gani? Akasema: ni kuzini na mke wa jirani yako.”[5] [Bukhaariy, Muslim]
1258.
وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ عَمْرِو بْنِ الْعَاصِ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: {مِنْ اَلْكَبَائِرِ شَتْمُ اَلرَّجُلِ وَالِدَيْهِ. قِيلَ: وَهَلْ يَسُبُّ اَلرَّجُلُ وَالِدَيْهِ؟ قَالَ: نَعَمْ. يَسُبُّ أَبَا اَلرَّجُلِ، فَيَسُبُّ أَبَاهُ، وَيَسُبُّ أُمَّهُ، فَيَسُبُّ أُمَّهُ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Amr bin Al-‘Aasw (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Miongoni mwa madhambi makubwa ni mtu kutukana wazazi wake. Maswahaba wakasema: mtu anaweza kutukana wazazi wake? Akasema: “Ndiyo, atamtukana baba wa mtu naye anamtukana baba yake, na atamtukana mama wa mtu naye atamtukana mama yake.”[6] [Bukhaariy, Muslim]
1259.
وَعَنْ أَبِي أَيُّوبَ رضى الله عنه أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: {لَا يَحِلُّ لِمُسْلِمٍ أَنْ يَهْجُرَ أَخَاهُ فَوْقَ ثَلَاثِ لَيَالٍ يَلْتَقِيَانِ، فَيُعْرِضُ هَذَا، وَيُعْرِضُ هَذَا، وَخَيْرُهُمَا اَلَّذِي يَبْدَأُ بِالسَّلَامِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Abuu Ayyuwb (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Si halaal kwa Muislaam kumhama nduguye zaidi ya siku tatu;[7] anakutana naye, huyu akampa mgongo na huyo akampa mgongo, na mbora kati yao ni yule anayeanza kutoa salaam.” [Bukhaariy, Muslim]
1260.
عَنْ جَابِرٍ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {كُلُّ مَعْرُوفٍ صَدَقَةٌ} أَخْرَجَهُ اَلْبُخَارِيُّ
Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Kila jema ni swadaqah.”[8] [Imetolewa na Al-Bukhaariy]
1261.
وَعَنْ أَبِي ذَرٍّ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {لَا تَحْقِرَنَّ مِنْ اَلْمَعْرُوفِ شَيْئًا، وَلَوْ أَنْ تَلْقَى أَخَاكَ بِوَجْهٍ طَلْقٍ}
Kutoka kwa Abuu Dharri (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Usidharau chochote katika wema[9] hata kama ni kukutana na nduguyo kwa uso mkunjufu.” [Imetolewa na Muslim]
1262.
وَعَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {إِذَا طَبَخْتَ مَرَقَةً، فَأَكْثِرْ مَاءَهَا، وَتَعَاهَدْ جِيرَانَكَ} أَخْرَجَهُمَا مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Abuu Dharri (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Unapopika mchuzi zidisha maji yake na umpe jirani yako.”[10] [Imetolewa na Muslim]
1263.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {مَنْ نَفَّسَ عَنْ مُؤْمِنٍ كُرْبَةً مِنْ كُرَبِ اَلدُّنْيَا، نَفَّسَ اَللَّهُ عَنْهُ كُرْبَةً مِنْ كُرَبِ يَوْمِ اَلْقِيَامَةِ ، وَمَنْ يَسَّرَ عَلَى مُعْسِرٍ، يَسَّرَ اَللَّهُ عَلَيْهِ فِي اَلدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ، وَمَنْ سَتَرَ مُسْلِمًا، سَتَرَهُ اَللَّهُ فِي اَلدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ، وَاَللَّهُ فِي عَوْنِ اَلْعَبْدِ مَا كَانَ اَلْعَبْدُ فِي عَوْنِ أَخِيهِ} أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kumfariji katika dhiki Muumini miongoni mwa dhiki za duniani,[11] Allaah Atamfariji katika dhiki miongoni mwa dhiki za Siku ya Qiyaamah. Mwenye kumrahisishia mwenye uzito, Allaah Atamrahisishia duniani na Aakhirah. Mwenye kumsitiri Muislaam, Allaah Atamsitiri duniani na Aakhirah. Allaah Yumo katika kumsaidia mja madamu mja huyo yumo katika kumsaidia nduguye.” [Imetolewa na Muslim]
1264.
وَعَنْ أَبِي مَسْعُودٍ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {مَنْ دَلَّ عَلَى خَيْرٍ، فَلَهُ مِثْلُ أَجْرِ فَاعِلِهِ} أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Abuu Mas-‘uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kujulisha kheri atapata mfano wa ujira (malipo) wa mwenye kuifanya.” [Imetolewa na Muslim]
1265.
وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: {مِنْ اسْتَعَاذَكُمْ بِاَللَّهِ فَأَعِيذُوهُ، وَمَنْ سَأَلَكُمْ بِاَللَّهِ فَأَعْطُوهُ، وَمَنْ أَتَى إِلَيْكُمْ مَعْرُوفًا فَكَافِئُوهُ، فَإِنْ لَمْ تَجِدُوا، فَادْعُوا لَهُ} أَخْرَجَهُ اَلْبَيْهَقِيُّ.
Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kujilinda kwenu kwa Allaah, basi mlindeni na mwenye kuwaomba kwa Jina la Allaah mpeni, na mwenye kuwatendea wema mlipeni, msipopata cha kumlipa muombeeni du’aa.” [Imetolewa na Al-Bayhaqiy]
[1] Swali linalojitokeza hapa ni kuwa maadamu ya kuwa umri ulishapangwa, iweje wema kwa ndugu na jamaa kutaongeza umri wa mtu? Jibu la swali hili ni kuwa umri wa mtu upo katika elimu ya Allaah, hubaki wala haubadiliki, lakini ule ambao upo katika elimu ya Malaika muhusika wa maisha ya watu unaweza kupungua na kuongezeka vivyo hivyo. Kwa maneno mengine ni kuwa, Malaika wanapewa elimu ya Qadar iliyowekwa na siyo ile ya mwisho na yenyewe kabisa. Kwa mfano, anaambiwa ikiwa mtu fulani anawafanyia wema jamaa zake, atapewa umri wa miaka mia moja, vinginevyo utapunguzwa hadi miaka sitini.
[2] Hiki ni kitisho kikali kwa mwenye kukata udugu. Neno la Kiarabu linalotumika ni Rahm, neno hili linakusanya mahusiano yote na watu ambao ni Mahram na wale wote wenye haki ya kurithi.
[3] Kutomtii mzazi ni katika madhambi makubwa, madamu tu hakukulazimisha kufanya jambo linalopingana na Shariy’ah.
[4] Hadiyth hii inaelezea majukumu makubwa aliyonayo mtu kwa jirani zake.
[5] Hadiyth hii inatupa mafundisho kuwa madhambi makubwa yanatofautiana, kulingana na adhabu zake. Madhambi ya kuzini yanakatazwa kwa ujumla, lakini kulifanya jambo hilo kwa mke wa jirani ni jambo baya zaidi.
[6] Hukmu inayopatikana katika Hadiyth hii ni kuwa jambo lolote ambalo linapelekea katika makatazo linakatazwa vile vile. Hata kama aliyefanya jambo lile hakukusudia kufanya jambo lililokatazwa.
[7] Ikiwa sababu ya jambo hilo ni mambo binafsi, haitakiwi mfarakano huo udumu zaidi ya masiku tatu. Lakini ikiwa jambo hilo linahusiana na jambo la Dini, hakuna makadirio ya muda kwani jambo hilo ni sehemu ya iymaan.
[8] Swadaqah haina maana finyu ya mtu kutoa chochote tu katika mali yake. Bali maana yake ni pana, yaani mtu kufanya tendo lolote zuri na kuacha jambo lolote baya nayo ni Swadaqah.
[9] Bashasha inaweza kuonekana ni jambo dogo machoni mwa watu, jambo hili limepewa nafasi kubwa katika malipo na fadhila zake.
[10] Hukumu hii inakuwa ni ya faradhi ikiwa jirani yako ni mtu maskini. Ikiwa jirani ni tajiri basi hukumu hii inakuwa ni kwa kufadhilisha na kupendezesha zaidi. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Kila Jibriyl anaposhuka kwangu huniusia kuhusu kumfanyia wema jirani kiasi cha kufikiri kuwa huenda jirani akanirithi.”
[11] Mahimizo tunayoyapata hapa ni ule ubora na umuhimu wa kumsaidia Muumini.
بُلُوغُ الْمَرام
Buluwgh Al-Maraam
كِتَابُ اَلْجَامِعِ
Kitabu Cha Mjumuisho
بَابُ اَلزُّهْدِ وَالْوَرَعِ
03-Mlango Wa Kuipa Mgongo Dunia[1]
1266.
عَنْ اَلنُّعْمَانِ بْنِ بَشِيرٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ وَأَهْوَى اَلنُّعْمَانُ بِإِصْبَعَيْهِ إِلَى أُذُنَيْهِ: {إِنَّ اَلْحَلَالَ بَيِّنٌ، وَإِنَّ اَلْحَرَامَ بَيِّنٌ، وَبَيْنَهُمَا مُشْتَبِهَاتٌ، لَا يَعْلَمُهُنَّ كَثِيرٌ مِنْ اَلنَّاسِ، فَمَنِ اتَّقَى اَلشُّبُهَاتِ، فَقَدِ اِسْتَبْرَأَ لِدِينِهِ وَعِرْضِهِ، وَمَنْ وَقَعَ فِي اَلشُّبُهَاتِ وَقَعَ فِي اَلْحَرَامِ، كَالرَّاعِي يَرْعَى حَوْلَ اَلْحِمَى، يُوشِكُ أَنْ يَقَعَ فِيهِ، أَلَا وَإِنَّ لِكُلِّ مَلِكٍ حِمًى، أَلَا وَإِنَّ حِمَى اَللَّهِ مَحَارِمُهُ، أَلَا وَإِنَّ فِي اَلْجَسَدِ مُضْغَةً، إِذَا صَلَحَتْ، صَلَحَ اَلْجَسَدُ كُلُّهُ، وَإِذَا فَسَدَتْ فَسَدَ اَلْجَسَدُ كُلُّهُ، أَلَا وَهِيَ اَلْقَلْبُ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa An-Nu’maan bin Bashiyr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa alimsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema: (Nu’maan akaashiria vidole vyake kwenye masikio yake): “Hakika halaal iko wazi na haraam iko wazi, baina ya mawili hayo kuna mambo yenye utata.[2] Wengi katika watu hawayajui. Basi atakayejiepusha na yenye utata amejiepusha kwa Dini yake na heshima yake. Na ataketumbukia katika yenye utata atatumbukia kwenye haraam. Kama mchunga anayechunga pembeni ya mipaka, ni haraka kulisha humo. Fahamuni! Kila mfalme ana mipaka. Fahamuni! Hakika mipaka ya Allaah ni maharamisho. Zindukeni! Hakika katika mwili kuna kinofu, kinapotengamaa mwili wote unatengamaa. Kinapoaribika mwili wote unaharibika. Fahamuni! Hicho ni moyo.” [Bukhaariy, Muslim]
1267.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {تَعِسَ عَبْدُ اَلدِّينَارِ، وَالدِّرْهَمِ، وَالْقَطِيفَةِ، إِنْ أُعْطِيَ رَضِيَ، وَإِنْ لَمْ يُعْطَ لَمْ يَرْضَ} أَخْرَجَهُ الْبُخَارِيُّ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Ameangamia mtumwa wa dinari na dirhamu, mahameli na khamisa; akipewa huridhika, asipopewa haridhiki.”[3] [Imetolewa na Al-Bukhaariy]
1268.
وَعَنِ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: أَخَذَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم بِمَنْكِبِي، فَقَالَ: {كُنْ فِي اَلدُّنْيَا كَأَنَّكَ غَرِيبٌ، أَوْ عَابِرُ سَبِيلٍ} وَكَانَ اِبْنُ عُمَرَ يَقُولُ: إِذَا أَمْسَيْتَ فَلَا تَنْتَظِرِ اَلصَّبَاحَ، وَإِذَا أَصْبَحْتَ فَلَا تَنْتَظِرِ اَلْمَسَاءَ، وَخُذْ مِنْ صِحَّتِكَ لِسَقَمِك، وَمِنْ حَيَاتِكَ لِمَوْتِكَ. أَخْرَجَهُ اَلْبُخَارِيُّ
Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alishika mabega yangu akaniambia: “Kuwa katika dunia kana kwamba ni mgeni au mpita njia. Ibn ‘Umar alikuwa akisema: ‘Unapochwewa usingoje asubuhi, na unapopambazukiwa usingoje jioni, chukua siha yako kwa ajili ya ugonjwa wako, na uhai wako kwa kifo chako.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]
1269.
وَعَنِ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {مَنْ تَشَبَّهَ بِقَوْمٍ، فَهُوَ مِنْهُمْ} أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ
Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kujifananisha na watu basi yeye ni miongoni mwao.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na akaisahihisha Ibn Hibbaan]
1270.
وَعَنِ اِبْنِ عَبَّاسٍ قَالَ: كُنْتُ خَلْفَ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم يَوْمًا، فَقَالَ: {يَا غُلَامُ! اِحْفَظِ اَللَّهَ يَحْفَظْكَ، اِحْفَظِ اَللَّهَ تَجِدْهُ تُجَاهَكَ، وَإِذَا سَأَلْتَ فَاسْأَلْ اَللَّهَ، وَإِذَا اِسْتَعَنْتَ فَاسْتَعِنْ بِاَللَّهِ} رَوَاهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَقَالَ: حَسَنٌ صَحِيحٌ.
Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema siku moja nilikuwa nyuma ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Ewe kijana! Mhifadhi Allaah [4]Atakuhifadhi. Mhifadhi Allaah utamkuta mbele yako. Unapoomba muombe Allaah. Unapotaka msaada mtake msaada Allaah.” [Imetolewa na At-Tirmidhiy na amesema Hadiyth hii ni Swahiyh Hasan]
1271.
وَعَنْ سَهْلِ بْنِ سَعْدٍ قَالَ: {جَاءَ رَجُلٌ إِلَى اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ: يَا رَسُولَ اَللَّهِ! دُلَّنِي عَلَى عَمَلٍ إِذَا عَمِلْتُهُ أَحَبَّنِي اَللَّهُ، وَأَحَبَّنِي اَلنَّاسُ. فـقَالَ: اِزْهَدْ فِي اَلدُّنْيَا يُحِبُّكَ اَللَّهُ، وَازْهَدْ فِيمَا عِنْدَ اَلنَّاسِ يُحِبُّكَ اَلنَّاسُ} رَوَاهُ اِبْنُ مَاجَه، وَسَنَدُهُ حَسَنٌ
Kutoka kwa Sahl bin Sa’d amesema alikuja mtu kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Nijulishe amali ambayo nikiifanya Allaah Atanipenda na watu pia watanipenda. Akasema: “Chukia dunia Allaah Atakupenda[5] na chukia vilivyo kwa watu, watu watakupenda.” [Imetolewa na Ibn Maajah na isnaad yake ni hasan]
1272.
وَعَنْ سَعْدِ بْنِ أَبِي وَقَّاصٍ رضى الله عنه قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: {إِنَّ اَللَّهَ يُحِبُّ اَلْعَبْدَ اَلتَّقِيَّ، اَلْغَنِيَّ، اَلْخَفِيَّ} أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Sa’d bin Abiy Waqqaasw (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema nilimsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema: “Hakika Allaah Anampenda mja mwenye Taqwa mwenye kujitosha na mwenye kujificha.”[6] [Imetolewa na Muslim]
1273.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {مِنْ حُسْنِ إِسْلَامِ اَلْمَرْءِ، تَرْكُهُ مَا لَا يَعْنِيهِ} رَوَاهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَقَالَ حَسَنٌ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Katika uzuri wa Uislaam wa mtu ni kuacha lisilomhusu.”[7] [Imetolewa na At-Tirmidhiy na akasema ni Hadiyth hii ni Hasan]
1274.
وَعَنْ اَلْمِقْدَامِ بْنِ مَعْدِيكَرِبَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {مَا مَلَأَ ابْنُ آدَمَ وِعَاءً شَرًّا مِنْ بَطْنٍ} أَخْرَجَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ وَحَسَّنَهُ
Kutoka kwa Al-Miqdaam bin Ma’d Yakrib (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwana Aadam hakujaza chombo chenye shari zaidi kuliko tumbo lake.”[8] [Imetolewa na At-Tirmidhiy na akasema kuwa Hadiyth hii ni Hasan]
1275.
وَعَنْ أَنَسٍ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {كُلُّ بَنِي آدَمَ خَطَّاءٌ، وَخَيْرُ اَلْخَطَّائِينَ اَلتَّوَّابُونَ} أَخْرَجَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَابْنُ مَاجَهْ، وَسَنَدُهُ قَوِيٌّ
Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Kila mwana Aadam ni mkosaji na bora wa wakosaji ni wanayetubia.”[9] [Imetolewa na At-Tirmidhiy na Ibn Maajah, na Isnaad yake ina nguvu]
1276.
وَعَنْ أَنَسٍ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {اَلصَّمْتُ حِكْمَةٌ، وَقَلِيلٌ فَاعِلُهُ} أَخْرَجَهُ اَلْبَيْهَقِيُّ فِي " اَلشُّعَبِ" بِسَنَدٍ ضَعِيفٍ وَصَحَّحَ أَنَّهُ مَوْقُوفٌ مِنْ قَوْلِ لُقْمَانَ اَلْحَكِيمِ
Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Kunyamaza ni hekima,[10] na ni wachache wafanyaji wake.” [Imetolewa na Al-Bayhaqiy katika Kitabu ‘Ash-Shu’ab’ kwa Iisnaad dhaifu. Na imeswihi kuwa ni Mawquwf ni kauli ya Luqmaan mwenye hekima]
[1] Neno la Kiarabu linalotumika hapa ni الْوَرَعِ yenye maana ya kujitenga na mambo yenye shaka mtu asije angukia kwenye haraam.
[2] Hadiyth hii inatufungamanisha na hukmu muhimu za Kiislaam. Mushtabihaat ni yale mambo ambayo yana utata, yapo baina ya halaal na haraam. Wanazuoni wametofautiana kuhusu makatazo yake. Kuharibika kwa kiungo kimoja mwilini kunatokana na kuharibika kwa moyo wa mtu. Kwa sababu moyo wa mtu ndiyo unaongoza matendo ya mtu. Ikiwa mfalme amepotoka kimaadili basi uwezekano wa raia zake kupotoka vile vile ni mkubwa. Vivyo hivyo, ikiwa mfalme ni mwenye Taqwa raia zake watakuwa mfano wake.
[3] Hili linarejea kwa mtu mwenye tamaa. Akiendelea kufurahia neema za ulimwengu huu, atakuwa na furaha naye atamridhisha Allaah. Ikiwa ni kinyume chake hatopata vitu hivi basi hatofurahi kwa alichopewa na Allaah, na hatojiridhia vile vile.
[4] Kumhifadhi Allaah ni kufahamu mafundisho ya Allaah na kukatazika na makatazo yake. Kuwa ni mtu uliyehifadhiwa na Allaah ni kuwa Allaah Atakulipa malipo mazuri siku ya Qiyaamah na utapata jazaa na kusahau tabu za duniani. Hadiyth hii inaingiza hisia za Tawhiyd katika mioyo ya waja na ya kuwa hakuna kinachoweza kukudhuru kama Allaah Hakutaka.
[5] Njia sahihi na pekee ya mtu kujikurubisha na Allaah ni kujitenga na dunia hii, na kuweka iymaan ya juu kwa Allaah na kuachana na tamaa ya yaliyokuwa kwa watu.
[6] Allaah Anapompenda mja wake Humtakia mema, Humuongoza katika haki. Mwenye Taqwa ni yule ambaye anatekeleza maamrisho ya Allaah na kukatazika na makatazo yake. Tajiri ni yule aiyekuwa tajiri katika moyo wake na anamshkuru Allaah kwa kila alichopewa. Khafiyy ni yule mtu asiye mnafiki na wala hajioneshi, hujishughulisha tu na ‘ibaadah ya Allaah.
[7] Ikiwa mtu ana hakika kuwa Allaah Anamuona kwa kile anachofanya na kusema na ni mwenye elimu ya hilo, mtu huyo atakuwa ni mwepesi kujizuia na kuzungumza vibaya au na mazungumzo yasiyo na faida yoyote.
[8] Hadiyth hii inaelezea kuwa kuelekea katika kuzidisha jambo hakufai. Suala la chakula ni muhimu lakini himizo tunalopata hapa ni jinsi gani lilivyobeba shari ya mwana Aadam.
[9] Hadiyth hii imethibitisha kuwa wana Aaadam wote ni wakosaji isipokuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Allaah Hachukii sana kwa yule anayefanya dhambi, bali Anamfurahia zaidi yule anayeomba maghfirah na tawbah. Imepokewa na Abuu Hurayrah katika Swahiyh Muslim ikiwa wana Aadam wote watamuasi Allaah kisha wasiombe maghfirah kwake baada ya madhambi yale, Allaah Ataungamiza ulimwengu huu na kuubadilisha na watu wengine watakaotubu na kumuomba Allaah maghfirah baada ya kuyafanya madhambi.
[10] Hadiyth nyingi zimepokelewa zikionesha umuhimu wa mtu kunyamaza kama hana zuri la kusema. Hadiyth mojawapo inaelezea kuwa ikiwa hakuna cha kuzungumza bora kukaa kimya.
بُلُوغُ الْمَرام
Buluwgh Al-Maraam
كِتَابُ اَلْجَامِعِ
Kitabu Cha Mjumuisho
بَابُ اَلرَّهَبِ مِنْ مَسَاوِئِ اَلْأَخْلَاقِ
04-Mlango Wa Onyo Dhidi Ya Akhlaaq (Tabia) Mbaya
1277.
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {إِيَّاكُمْ وَالْحَسَدَ، فَإِنَّ اَلْحَسَدَ يَأْكُلُ اَلْحَسَنَاتِ، كَمَا تَأْكُلُ اَلنَّارُ اَلْحَطَبَ} أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ
وَلِابْنِ مَاجَهْ: مِنْ حَدِيثِ أَنَسٍ نَحْوُهُ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Tahadharini na hasadi,[1] hakika hasadi hula mema kama vile moto unavyokula kuni.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd. Ibn Maajah aliripoti mfano wa Hadiyth hii kutoka katika Hadiyth za Anas]
1278.
وَعَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {لَيْسَ اَلشَّدِيدُ بِالصُّرَعَةِ، إِنَّمَا اَلشَّدِيدُ اَلَّذِي يَمْلِكُ نَفْسَهُ عِنْدَ اَلْغَضَبِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Si mwenye nguvu mwenye kushinda mieleka, bali mwenye nguvu ni anaemiliki nafsi yake wakati wa ghadhabu.”[2] [Bukhaariy, Muslim]
1279.
وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {اَلظُّلْمُ ظُلُمَاتٌ يَوْمَ اَلْقِيَامَةِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Dhulma[3] ni giza Siku ya Qiyaama.” [Bukhaariy, Muslim]
1280.
وَعَنْ جَابِرٍ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ : {اِتَّقُوا اَلظُّلْمَ، فَإِنَّ اَلظُّلْمَ ظُلُمَاتٌ يَوْمَ اَلْقِيَامَةِ، وَاتَّقُوا اَلشُّحَّ ، فَإِنَّهُ أَهْلَكَ مَنْ كَانَ قَبْلَكُمْ} أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ.
Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Ogopeni dhulma, hakika kudhulumu ni giza Siku ya Qiyaamah, na ogopeni ubakhili, hakika ubakhili uliangamiza waliokuwa kabla yenu.” [Imetolewa na Muslim]
1281.
وَعَنْ مَحْمُودِ بْنِ لَبِيدٍ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {إِنَّ أَخْوَفَ مَا أَخَافُ عَلَيْكُمْ اَلشِّرْكُ اَلْأَصْغَرُ: اَلرِّيَاءُ} أَخْرَجَهُ أَحْمَدُ بِسَنَدٍ حَسَنٍ
Kutoka kwa Mahmuwd bin Labiyd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Kwa hakika jambo ninalowahofia zaidi ni shirki ndogo (nayo ni) riyaa.”[4] [Imetolewa na Ahmad kwa Isnaad hasan]
1282.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {آيَةُ اَلْمُنَافِقِ ثَلَاثٌ: إِذَا حَدَّثَ كَذَبَ، وَإِذَا وَعَدَ أَخْلَفَ، وَإِذَا ائْتُمِنَ خَانَ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Alama za mnafiki ni tatu:[5] akizungumza anaongopa, akitoa ahadi anakhalifu na akiaminiwa anakhini.” [Bukhaariy, Muslim]
1283.
وَعَنْ اِبْنِ مَسْعُودٍ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {سِبَابُ اَلْمُسْلِمِ فُسُوقٌ، وَقِتَالُهُ كُفْرٌ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Ibn Mas-‘uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Kumtukana Muislaam ni ufasiki na kupigana naye ni ukafiri.”[6] [Bukhaariy, Muslim]
1284.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {إِيَّاكُمْ وَالظَّنَّ، فَإِنَّ اَلظَّنَّ أَكْذَبُ اَلْحَدِيثِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Tahadharini kudhania,[7] hakika dhana ni mazungumzo ya uongo.” [Bukhaariy, Muslim]
1285.
وَعَنْ مَعْقِلِ بْنِ يَسَارٍ رضى الله عنه قَالَ سَمِعْتُ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: {مَا مِنْ عَبْدِ يَسْتَرْعِيهِ اَللَّهُ رَعِيَّةً، يَمُوتُ يَوْمَ يَمُوتُ، وَهُوَ غَاشٌّ لِرَعِيَّتِهِ، إِلَّا حَرَّمَ اَللَّهُ عَلَيْهِ اَلْجَنَّةَ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Ma’qil bin Yasaar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema nilimsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema: “Hakuna mja yeyote Allaah Amempa kuwaongoza raia, siku ya kufa akafa ilihali ni mwenye kughushi raia zake isipokuwa Allaah Atamharamishia Jannah.”[8] [Bukhaariy, Muslim]
1286.
وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {اَللَّهُمَّ مَنْ وَلِيَ مِنْ أَمْرِ أُمَّتِي شَيْئًا، فَشَقَّ عَلَيْهِ، فَاشْقُقْ عَلَيْهِ} أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Ee Allaah! Atakayesimamia jambo katika mambo ya ummah wangu na akawafanyia uzito, basi Nawe Mfanyie uzito.” [Imetolewa na Muslim]
1287.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {إِذَا قَاتَلَ أَحَدُكُمْ، فَلْيَتَجَنَّبِ اَلْوَجْهَ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Anapopigana mmoja wenu na ajiepushe (kulenga) uso.”[9] [Bukhaariy, Muslim]
1288.
وَعَنْهُ أَنَّ رَجُلاً قَالَ: {يَا رَسُولَ اَللَّهِ! أَوْصِنِي. فَقَالَ: لَا تَغْضَبْ، فَرَدَّدَ مِرَارًا. قَالَ: لَا تَغْضَبْ} أَخْرَجَهُ اَلْبُخَارِيُّ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa mtu mmoja alimuambia Ee Rasuli wa Allaah! Niusie: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akamuambia: “Usighadhibike.”[10] Akarudia mara nyingi (Nabiy) akasema: “Usighadhibike.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]
1289.
وَعَنْ خَوْلَةَ اَلْأَنْصَارِيَّةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {إِنَّ رِجَالاً يتخوَّضون فِي مَالِ اَللَّهِ بِغَيْرِ حَقٍّ، فَلَهُمْ اَلنَّارُ يَوْمَ اَلْقِيَامَةِ} أَخْرَجَهُ اَلْبُخَارِيُّ
Kutoka kwa Khawlah Al-Answaariy[11] (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Hakika watu wanaotumia mali ya Allaah[12] bila haki wana moto Siku ya Qiyaamah.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]
1290.
وَعَنْ أَبِي ذَرٍّ رضى الله عنه عَنْ اَلنَّبِيِّ صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِيمَا يَرْوِي عَنْ رَبِّهِ قَالَ: {يَا عِبَادِي! إِنِّي حَرَّمْتُ اَلظُّلْمَ عَلَى نَفْسِي، وَجَعَلْتُهُ بَيْنَكُمْ مُحَرَّمًا، فَلَا تَظَّالَمُوا} أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Abuu Dharri (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) katika anayoyapokea kutoka kwa Rabb wake, amesema: “Enyi waja Wangu, Hakika Mimi Nimejiharamishia dhulma katika Nafsi yangu na Nimeijaalia haraam miongoni mwenu; kwa hivyo msidhulumiane.” [Imetolewa na Muslim]
1291.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: {أَتَدْرُونَ مَا اَلْغِيبَةُ؟ قَالُوا: اَللَّهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ قَالَ: ذِكْرُكَ أَخَاكَ بِمَا يَكْرَهُ. قِيلَ: أَرَأَيْتَ إِنْ كَانَ فِي أَخِي مَا أَقُولُ؟ قَالَ: إِنْ كَانَ فِيهِ مَا تَقُولُ فَقَدْ اِغْتَبْتَهُ، وَإِنْ لَمْ يَكُنْ فَقَدْ بَهَتَّهُ} أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mnajua nini Ghiybah (kusengenya)? Wakasema Allaah na Rasuli wake Wanajua. Akasema: ‘ni kumtaja nduguyo kwa analochukia’ ikasemwa: unaonaje iwapo kwa ndugu yangu yapo nisemayo? Akasema: “Ikiwa analo usemalo umemsengenya[13] na ikiwa hana ulisemalo umemzulia.” [Imetolewa na Muslim]
1292.
وَعَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {لَا تَحَاسَدُوا وَلَا تَنَاجَشُوا، وَلَا تَبَاغَضُوا، وَلَا تَدَابَرُوا، وَلَا يَبِعْ بَعْضُكُمْ عَلَى بَيْعِ بَعْضٍ، وَكُونُوا عِبَادَ اَللَّهِ إِخْوَانًا، اَلْمُسْلِمُ أَخُو اَلْمُسْلِمِ، لَا يَظْلِمُهُ، وَلَا يَخْذُلُهُ، وَلَا يَحْقِرُهُ، اَلتَّقْوَى هَا هُنَا، وَيُشِيرُ إِلَى صَدْرِهِ ثَلَاثَ مِرَارٍ، بِحَسْبِ اِمْرِئٍ مِنْ اَلشَّرِّ أَنْ يَحْقِرَ أَخَاهُ اَلْمُسْلِمَ، كُلُّ اَلْمُسْلِمِ عَلَى اَلْمُسْلِمِ حَرَامٌ، دَمُهُ، وَمَالُهُ، وَعِرْضُهُ} أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Msihusudiane wala msipandishiane bei, wala msichukiane, wala msikatane. Wala baadhi yenu asiuze kwa mauzo ya nduguye; nyote kuweni waja wa Allaah hali ya kuwa ni ndugu. Muislaam ni ndugu wa Muislaam; hamdhulumu wala hamdharau wa hamtelekezi. Taqwa ipo hapa.” Akaashiria mara tatu kifuani mwake. “Yatosha mtu kutenda shari atakapomdharau nduguye Muislaam. Kila Muislaam juu ya Muislaam mwenzie ni haraam: damu yake, mali yake na heshima yake.”[14] [Imetolewa na Muslim]
1293.
وَعَنْ قُطْبَةَ بْنِ مَالِكٍ رضى الله عنه قَالَ: كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: {اَللَّهُمَّ جَنِّبْنِي مُنْكَرَاتِ اَلْأَخْلَاقِ، وَالْأَعْمَالِ، وَالْأَهْوَاءِ، وَالْأَدْوَاءِ} أَخْرَجَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ وَاللَّفْظِ لَهُ
Kutoka kwa Qutwbah bin Maalik[15] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema:
اَللَّهُمَّ جَنِّبْنِي مُنْكَرَاتِ اَلْأَخْلَاقِ، وَالْأَعْمَالِ، وَالْأَهْوَاءِ، وَالْأَدْوَاءِ
“Ee Allaah! Niepushe na akhlaaq (tabia) mbaya, na amali mbaya, na matamanio na magonjwa.” [Imetolewa na At-Tirmidhiy na akaisahihisha Al-Haakim
1294.
وَعَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {لَا تُمَارِ أَخَاكَ، وَلَا تُمَازِحْهُ، وَلَا تَعِدْهُ مَوْعِدًا فَتُخْلِفَهُ} أَخْرَجَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ بِسَنَدٍ فِيهِ ضَعْفٌ
Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Usishindane na nduguyo, wala usimfanyie mzaha, wala usimuahidi ahadi na ukamkhalifu.” [Imetolewa na At-Tirmidhiy kwa isnaad dhaifu]
1295.
وَعَنْ أَبِي سَعِيدٍ اَلْخُدْرِيِّ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {خَصْلَتَانِ لَا يَجْتَمِعَانِ فِي مُؤْمِنٍ: اَلْبُخْلُ، وَسُوءُ اَلْخُلُقِ} أَخْرَجَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَفِي سَنَدِهِ ضَعْفٌ
Kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mambo mawili hayakutani kwa Muumini: ubakhili na khulqa (tabia) mbaya.” [Imetolewa na At-Tirmidhiy na katika isnaad yake kuna udhaifu]
1296.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ : {اَلْمُسْتَبَّانِ مَا قَالَا، فَعَلَى اَلْبَادِئِ، مَا لَمْ يَعْتَدِ اَلْمَظْلُومُ} أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Wawili wenye kutukanana wana dhambi (kiasi wanavyosema), aliyeanza ni mwenye dhambi nyingi zaidi madamu aliyedhulumiwa hajavuka mpaka (katika kujibu).”[16] [Imetolewa na Muslim]
1297.
وَعَنْ أَبِي صِرْمَةَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {مَنْ ضَارَّ مُسْلِمًا ضَارَّهُ اَللَّهُ، وَمَنْ شَاقَّ مُسَلِّمًا شَقَّ اَللَّهُ عَلَيْهِ} أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ وَاَلتِّرْمِذِيُّ وَحَسَّنَهُ
Kutoka kwa Abuu Swirmah[17] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kumdhuru Muislaam, Allaah Atamdhuru,[18] na mwenye kumsumbua Muislaam Allaah Atamsumbua.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na At-Tirmidhiy na kwa isnaad Hasan]
1298.
وَعَنْ أَبِي اَلدَّرْدَاءِ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {إِنَّ اَللَّهَ يُبْغِضُ اَلْفَاحِشَ اَلْبَذِيءَ} أَخْرَجَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَصَحَّحَهُ
وَلَهُ مِنْ حَدِيثِ اِبْنِ مَسْعُودٍ رَفَعَهُ: {لَيْسَ اَلْمُؤْمِنُ بِالطَّعَّانِ، وَلَا اَللَّعَّانُ، وَلَا اَلْفَاحِشَ، وَلَا اَلْبَذِيءَ} وَحَسَّنَهُ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ، وَرَجَّحَ اَلدَّارَقُطْنِيُّ وَقْفَهُ
Kutoka kwa Abuu Ad-Dardaa[19] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Hakika Allaah Anamchukia muovu, mwenye maneno mabaya.” [Imetolewa na At-Tirmidhiy na akaisahihisha]
Pia amepokea kutoka katika Hadiyth ya Ibn Mas-‘uwd marfuw’: “Muumini si mtukanaji, wala si mlaanifu,[20] wala mchafu, wala si mwenye maneno mabaya.” [Na amesema ni Hasan na akaisahihisha Al-Haakim. Ad-Daaraqutwniy ameitilia nguvu kuwa ni Marfuw’]
1299.
وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {لَا تَسُبُّوا اَلْأَمْوَاتَ، فَإِنَّهُمْ قَدْ أَفْضَوْا إِلَى مَا قَدَّمُوا} أَخْرَجَهُ اَلْبُخَارِيُّ
Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Msishutumu wafu,[21] hakika wao wameshayaendea waliyoyatanguliza.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]
1300.
وَعَنْ حُذَيْفَةَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {لَا يَدْخُلُ اَلْجَنَّةَ قَتَّاتٌ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Hudhayfah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mchonganishi hataingia Jannah.”[22] [Bukhaariy, Muslim]
1301.
وَعَنْ أَنَسٍ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {مَنْ كَفَّ غَضَبَهُ، كَفَّ اَللَّهُ عَنْهُ عَذَابَهُ} أَخْرَجَهُ اَلطَّبَرَانِيُّ فِي " اَلْأَوْسَطِ"
وَلَهُ شَاهِدٌ: مِنْ حَدِيثِ اِبْنِ عُمَرَ عِنْدَ اِبْنِ أَبِي اَلدُّنْيَا
Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kuzuwia ghadhabu zake, Allaah Atamzuilia adhabu Yake.” [Imetolewa na Atw-twabaraaniy katika kitabu cha ‘Al-Awsatw’. Nayo ina Ushahidi wa Hadiyth ya ‘Abdullaah ibn ‘Umar kwa Ibn Abuu Ad-Dunyaa]
1302.
وَعَنْ أَبِي بَكْرٍ اَلصِّدِّيقِ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {لَا يَدْخُلُ اَلْجَنَّةَ خِبٌّ، وَلَا بَخِيلٌ، وَلَا سَيِّئُ اَلْمَلَكَةِ} أَخْرَجَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَفَرَّقَهُ حَدِيثَيْنِ، وَفِي إِسْنَادِهِ ضَعْفٌ
Kutoka kwa Abuu Bakr Asw-Swiddiyq (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Haingii Jannah mwenye hadaa wala bakhili wala mbaya wa kumiliki.” [Imetolewa na At-Tirmidhiy na ameigawa katika Hadiyth mbili, na katika isnaad yake kuna udhaifu]
1303.
وَعَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {مَنْ تَسَمَّعَ حَدِيثَ قَوْمٍ، وَهُمْ لَهُ كَارِهُونَ، صُبَّ فِي أُذُنَيْهِ اَلْآنُكُ يَوْمَ اَلْقِيَامَةِ} يَعْنِي: اَلرَّصَاصَ. أَخْرَجَهُ اَلْبُخَارِيُّ
Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Anayesikiliza mazungumzo ya watu na ilihali wenyewe wanachukia siku ya Qiyaamah atamiminiwa risasi masikioni mwake.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]
1304.
وَعَنْ أَنَسٍ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {طُوبَى لِمَنْ شَغَلَهُ عَيْبَهُ عَنْ عُيُوبِ اَلنَّاسِ} أَخْرَجَهُ اَلْبَزَّارُ بِإِسْنَادٍ حَسَنٍ
Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Furaha ni ya ambaye aibu zake zimemshughulisha, akaachana na aibu za watu.” [Imetolewa na Al-Bazzaar kwa isnaad Hasan]
1305.
وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {مَنْ تَعَاظَمَ فِي نَفْسِهِ، وَاخْتَالَ فِي مِشْيَتِهِ، لَقِيَ اَللَّهَ وَهُوَ عَلَيْهِ غَضْبَانُ} أَخْرَجَهُ اَلْحَاكِمُ وَرِجَالُهُ ثِقَاتٌ
Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kujikweza nafsini mwake, akaringa katika kutembea kwake, atakutana na Allaah ilihali Amemghadhibikia.”[23] [Imetolewa na Al-Haakim na wapokezi wake ni Madhubuti]
1306.
وَعَنْ سَهْلِ بْنِ سَعْدٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {اَلْعَجَلَةُ مِنَ اَلشَّيْطَانِ} أَخْرَجَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَقَالَ: حَسَنٌ
Kutoka kwa Sahl bin Sa’d (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Haraka inatokana na shaytwaan.” [Imetolewa na At-Tirmidhiy na amesema ni Hasan]
1307.
وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: {اَلشُّؤْمُ: سُوءُ اَلْخُلُقِ} أَخْرَجَهُ أَحْمَدُ وَفِي إِسْنَادِهِ ضَعْفٌ
Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Ukorofi ni khulqa (tabia) mbaya.”[24] [Imetolewa na Ahmad na katika isnaad yake kuna udhaifu]
1308.
وَعَنْ أَبِي اَلدَّرْدَاءِ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {إِنَّ اَللَّعَّانِينَ لَا يَكُونُونَ شُفَعَاءَ، وَلَا شُهَدَاءَ يَوْمَ اَلْقِيَامَةِ} أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Abuu Ad-Dardaa (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Wenye kulaani hawawi waombezi wala Mashahidi Siku ya Qiyaamah.” [Imetolewa na Muslim]
1309.
وَعَنْ مُعَاذِ بْنِ جَبَلٍ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {مَنْ عَيَّرَ أَخَاهُ بِذَنْبٍ، لَمْ يَمُتْ حَتَّى يَعْمَلَهُ} أَخْرَجَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ وَحَسَّنَهُ، وَسَنَدُهُ مُنْقَطِعٌ
Kutoka kwa Mu’aadh bin Jabal (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kumuaibisha nduguye kwa dhambi hatakufa hadi aifanye.”[25] [Imetolewa na At-Tirmidhiy na amesema ni Hasan na isnaad yake imekatika]
1310.
وَعَنْ بَهْزِ بْنِ حَكِيمٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ: قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {وَيْلٌ لِلَّذِي يُحَدِّثُ، فَيَكْذِبُ ; لِيَضْحَكَ بِهِ اَلْقَوْمُ، وَيْلٌ لَهُ، ثُمَّ وَيْلٌ لَهُ} أَخْرَجَهُ اَلثَّلَاثَةُ، وَإِسْنَادُهُ قَوِيٌّ
Kutoka kwa Bahz bin Hakiym kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Ole wake anayezungumza akadanganya ili kuwachekesha watu.[26] Ole wake! Kisha ole wake!” [Imetolewa na Ath-Thalaathah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd) na isnaad yake ina nguvu]
1311.
وَعَنْ أَنَسٍ رضى الله عنه عَنْ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: {كَفَّارَةٌ مَنْ اِغْتَبْتَهُ أَنْ تَسْتَغْفِرَ لَهُ} رَوَاهُ اَلْحَارِثُ بْنُ أَبِي أُسَامَةَ بِسَنَدٍ ضَعِيفٍ
Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Kafara ya uliyemsengenya ni kumuombea maghfirah.”[27] [Imetolewa na Al-Haarith bin Abuu Usaamah kwa isnaad dhaifu]
1312.
وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {أَبْغَضُ اَلرِّجَالِ إِلَى اَللَّهِ اَلْأَلَدُّ اَلْخَصِمُ} أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mtu anayechukiwa kabisa na Allaah ni katili mwingi wa ugomvi.” [Imetolewa na Muslim]
[1] Katika lugha ya kiarabu ‘Hasad’ (husuda na wivu) hurejea kwa mtu anayemuonea wivu mwenzake na kuhusudu alichokuwa nacho na kutamani neema ile imuondokee na ije kwake. Jambo hili limekatazwa. Ikiwa mtu anatamani apate kitu fulani lakini hataki vile vile kimuondokee mwenzake, jambo hili linaitwa ‘Hiqd’. Hisia hii inahitajika katika mambo ya kidini.
[2] Hili linathibitisha umuhimu wa kusamehe, na kutopendelea kulipa kisasi haswa unapoghadhibishwa na jambo. Watu wanatakiwa wajifunze namna ya kujizuia na ghadhabu au hasira kwani hasira hasara. Mambo yanayoweza kuzuia hasira ni: Kujikinga na Allaah dhidi ya shaytwaan kwa kusema:
أَعـوذُ بِاللهِ مِنَ الشَّيْـطانِ الرَّجيـم
Na kuchukua wudhuu na kukaa chini kama utakuwa umesimama na kulala kama utakuwa umekaa.
[3] Dhulma, maana yake ni kuweka kitu sehemu isiyokuwa yake, au kuficha ukweli ili usitokeze. Katika Siku ya Hukmu (Qiyaamah) itaonekana na rangi yake itakuwa ni nyeusi. Hadiyth hii inatufundisha kuwa dhulma ni kitu kibaya na ni haraam ikiwa kwa mtu, katika heshima au utajiri wake.
[4] Riyaa ni kujionyesha. Ni pale mja anapofanya tendo lolote la ki ‘ibaadah kama la kuacha makatazo na kutekeleza maamrisho, lakini mtu anafanya hivyo ili watu wamuone kuwa ni mtiifu, hivyo anaridhisha watu badala ya kumridhisha Allaah. Au anaweza kufanya tendo la ‘ibaadah kwa malengo ya kidunia. Riyaa ina namna mbili: Ya kwanza ni kutenda jambo la ‘ibaadah, na kulionyesha kwa watu. Ya pili ni kufanya ‘ibaadah ambayo watu hawajui kisha anawajulisha watu kuwa kafanya. Aina hii ya riyaa inaitwa ‘Sum’ah’ na ile ya kwanza ndio riyaa yenyewe. Zote hazitakiwi.
[5] Unafiki ni aina mbili: a) Unafiki wa matendo na b) Unafiki katika Iymaan. Unafiki wa matendo umeshatajwa katika Hadiyth hii. Unafiki wa Iymaan pindi anapoficha ukafiri na kudhihirisha Uislaam. Unafiki wa Iymaan ni mbaya na hatari zaidi kuliko ukafiri wenyewe. Unafiki wa kimatendo ni moja ya madhambi makubwa ambao unaweza kusamehewa.
[6] ‘Fisq’ ni mtu kuangukia katika kumuasi Allaah. Kwa mfano, Allaah Amekataza Muislaam kutumia maneno machafu, na kuwa mtu anamuasi Allaah kwa kumuita nduguye majina mabaya, mtu huyo anakuwa ‘Faasiq’ (mwenye dhambi). Lakini ikiwa mtu huyo huyo au mwingine akaamua kupigana na mwenzake ambaye ni Muislaam, katika Hadiyth hii mtu huyo ni ‘Kufr’ (kufanya jambo la ukafiri). Ikiwa mambo haya mawili hayamhusu mtu mmoja basi neno hili litakuwa limetumika kama fumbo, yaani kufanya jambo la kikafiri.
[7] Dhana (kufikiria kitu kisichokuwepo). Limeelezwa kama ni mazungumzo ya uongo na Wanazuoni na ni uzushi na ni moja kati ya madhambi makubwa.
[8] Hali hii ya ‘Ghasb’, kunyanga’nya ni katika madhambi makubwa, kwani ni jambo linaloweza kumzuia kuingia Jannah. Watawala wanatakiwa wawahukumu watu kwa uadilifu. Inaonya kuwa adhabu kali zinawakabili watawala dhalimu.
[9] Hadiyth hii inaonyesha makatazo ya kupiga uso, hata kama ni adhabu ya makosa ya mtu. Hata wanyama wasipigwe usoni.
[10] Hadiyth hii ni mfano halisi wa wema ambao unataka uonyeshwe katika maisha haya ya duniani. Hili linatokana na ukweli kuwa mtu anayeepushwa na khulqa (tabia) njema ya huruma na kuwa na khulqa ya hasira kwa upande mmoja na upande wa pili khulqa ile ya hasira huwakera watu wengine. Hali hii ni mbaya kwani inamuathiri yule mtu mwenyewe na inawaathiri waliomzunguka.
[11] Khawlah, binti wa Thamir Al-Answaariy akiitwa Umm Muhammad na baba yake akiitwa Qays bin Qahad. Alikuwa katika Banuu Maalik bin An-Najjaar, aliolewa na Hamza bin ‘Abdil-Mutwalib, mumewe alipouwawa katika Uhud aliolewa na An-Nu’maan bin Al-‘Ajlaan Al-Answaariy Az-Zuraqi.
[12] Hadiyth hii ni dalili kuwa hata watawala wanaweza kutumia mali za ‘Baytul Maal’ vibaya, hili ni katika madhambi makubwa.
[13] Hadiyth hii imetajwa na Maswahaba wengi, na imepokelewa katika njia nyingi. Kuna makubaliano ya Wanazuoni kuwa kusengenya ni haraam.
[14] Tunajifunza katika Hadiyth hii Muislaam hatakiwi kuwa na kinyongo kwa Muislaam mwenzake.
[15] Alikuwa ni Swahaba kutoka kwa Banuu Tha’laba bin Sa’d bin Dhubyaan, alikuwa pia akiitwa Adh-Dhubyaan. Alikuwa ni mkazi wa Kufa mji uliopo ‘Iraq, baadhi ya Hadiyth zake zilipokewa na mpwawe Ziyaad bin ‘Alaqa.
[16] Hadiyth hii inabainisha mambo mawili: a) Suala la kulipa ubaya uliyofanyiwa na mwingine, ni suala linarohusiwa, b) suala la dhambi litamuhusu yule aliyeanzisha hali ile, maadamu yule wa pili hajavuka mipaka kwa kufanya uadui. Pamoja na yote hayo lililo bora zaidi ni kumsamehe aliyefanya makosa.
[17] Huyu ni Maalik bin Qays au Qays bin Maalik, alikuwa ni Swahaba kutoka katika kabila la Maazin. Alishiriki vita vya Badr na vita vingine vilivyofuatia na amepokea baadhi ya Hadiyth.
[18] Hadiyth hii inaonyesha kumdhuru Muislaam kwa jambo lolote lile hata kama litaonekana ni dogo kiasi gani hairuhusiwi.
[19] Jina halisi la Abuu Ad-Dardaa lilikuwa ni ‘Uwaymir bin Zayd au Ibn ‘Aamir au Ibn Maalik bin ‘Abdillaah bin Qays. Alikuwa ni Answaar wa kabila la Khazraj. Alikuwa ni Swahaba aliyejinyima raha na anasa za kidunia. Alisilimu katika siku ya vita vya Badr na alishiriki vita vya Uhud. ‘Umar alimhusisha katika watu waliyoshiriki Badr. Alikuwa ni katika watu walioikusanya Qur-aan na alifanywa kuwa ni Qaadhi wa Damascus. Ana fadhila nyingi. Amesikika akisema: “Umaarufu na riyaa ya saa moja inaweza kusababisha huzuni ya muda mrefu.” Alifariki 32 Hijriyyah.
[20] Hadiyth hii inatuelekeza kuwa si katika khulqa (tabia) ya Muumini kuwaita nduguze majina mabaya au kuwalaani. Hata hivyo inaruhusiwa kumtukana na kumlaani yule aliyelaaniwa na Allaah na Rasuli wake. Au kutaja kwa ujumla laana ya Allaah kwa makafiri. Watu wenye kufanya mambo mabaya na machafu. Vinginevyo si halaal kumlaani mtu kwa kumtaja jina lake.
[21] Hapa tunajifunza kuwa hairuhusiwi kabisa kuwaita waliokufa kwa majina mabaya, kuwasema vibaya. Hili linahusu kwa Waislaam hususan na hata kwa makafiri ambao wana udugu na baadhi ya Waislaam kwani kuwatusi au kuwasema vibaya kutawasikitisha ndugu zao Waislaam.
[22] Hafiydh Mundhir anaona kuwa makubaliano ya Wanazuoni wa Ummah huu ni kuwa mchochezi au mchukua maneno hapa na kuyapeleka kule ili kuleta utesi baina ya watu amefanya jambo la haraam na baya sana na linahesabiwa kuwa ni katika madhambi makubwa.
[23] Maelezo tunayopata kwenye Hadiyth hii ni makemeo kuhusu kibri na ni katika madhambi makubwa. Imepokewa na At-Tirmidhiy kuwa: “Mwenye sehemu ndogo ya kibri katika nafsi yake hatoingia Jannah.”
[24] Shari anazopata mwana Aadam ni kutokana na khulqa (tabia) zake mbaya. Hadiyth hii inaonyesha kuwa khulqa nzuri au mbaya za mtu zinatokana na chaguo lake binafsi.
[25] Tunajua kuwa kutaja maovu ya mtu ni dhambi. Ni vibaya sana kutaja udhaifu wa mtu na matatizo yake mbele za watu, ili kumuumbua au kumuaibisha. Hadiyth hii inatuhimiza kuwa mtu asitaje madhambi ya fulani eti kwa sababu naye amekashifiwa.
[26] Kusema uongo hata ikiwa ni kwa utani tu ili watu wacheke ni katika makatazo makubwa na ni sifa mojawapo ya unafiki. Uongo ambao haumnufaishi mtu hapa duniani na hata huko Aakhirah hauna maana na ni uongo mbaya sana. Kusikiliza uongo vile vile ni jambo lisilokubalika, aidha mtu azungumze ubaya wake au aondoke kwenye kikao hicho.
[27] Tawbah ya kusengenya ni: ikiwa mtu atamsengenya mtu mwingine ni bora amuombe msamaha. Kama hatompata mtu mwenyewe basi amuombee du’aa kwa Allaah Amghufurie madhambi yake.
بُلُوغُ الْمَرام
Buluwgh Al-Maraam
كِتَابُ اَلْجَامِعِ
Kitabu Cha Mjumuisho
بَابُ اَلتَّرْغِيبِ فِي مَكَارِمِ اَلْأَخْلَاقِ
05-Mlango wa Mahimizo Ya Akhlaaq (Tabia) Njema
1313.
عَنِ اِبْنِ مَسْعُودٍ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {عَلَيْكُمْ بِالصِّدْقِ، فَإِنَّ اَلصِّدْقَ يَهْدِي إِلَى اَلْبِرِّ، وَإِنَّ اَلْبِرَّ يَهْدِي إِلَى اَلْجَنَّةِ، وَمَا يَزَالُ اَلرَّجُلُ يَصْدُقُ، وَيَتَحَرَّى اَلصِّدْقَ، حَتَّى يُكْتَبَ عِنْدَ اَللَّهِ صِدِّيقًا، وَإِيَّاكُمْ وَالْكَذِبَ، فَإِنَّ اَلْكَذِبَ يَهْدِي إِلَى اَلْفُجُورِ، وَإِنَّ اَلْفُجُورَ يَهْدِي إِلَى اَلنَّارِ، وَمَا يَزَالُ اَلرَّجُلُ يَكْذِبُ، وَيَتَحَرَّى اَلْكَذِبَ، حَتَّى يُكْتَبَ عِنْدَ اَللَّهِ كَذَّابًا} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Ibn Mas-‘uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Shikamaneni na ukweli. Hakika ukweli unaongoza kwenye wema na wema unaongoza Jannah. Mtu hataacha kusema kweli na anachagua ukweli mpaka aandikwe mbele ya Allaah kuwa ni mkweli. Nawatahadharisheni na uongo. Hakika uongo huongoza kwenye uovu, na uovu huongoza motoni. Mtu hataacha kudanganya na anaendelea kudanganya mpaka aandikwe mbele ya Allaah kuwa ni mdanganyifu.” [Bukhaariy, Muslim]
1314.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: {إِيَّاكُمْ وَالظَّنَّ، فَإِنَّ اَلظَّنَّ أَكْذَبُ اَلْحَدِيثِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Tahadharini na dhana, hakika dhana ni mazungumzo ya uongo.” [Bukhaariy, Muslim]
1315.
وَعَنْ أَبِي سَعِيدٍ اَلْخُدْرِيِّ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {إِيَّاكُمْ وَالْجُلُوسَ بِالطُّرُقَاتِ. قَالُوا: يَا رَسُولَ اَللَّهِ! مَا لَنَا بُدٌّ مِنْ مَجَالِسِنَا، نَتَحَدَّثُ فِيهَا. قَالَ " فَأَمَّا إِذَا أَبَيْتُمْ، فَأَعْطُوا اَلطَّرِيقَ حَقَّهُ. قَالُوا: وَمَا حَقُّهُ؟قَالَ:" غَضُّ اَلْبَصَرِ، وَكَفُّ اَلْأَذَى، وَرَدُّ اَلسَّلَامِ، وَالْأَمْرُ بِالْمَعْرُوفِ، وَالنَّهْيُ عَنْ اَلْمُنْكَرِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Tahadharini kukaa njiani.[1] Wakasema: Ee Rasuli wa Allaah! Hatuna budi na vikao vyetu. Akasema: “Iwapo mtakataa isipokuwa kukaa basi ipeni njia haki yake. Wakasema: Ni ipi haki ya njia? Akasema: ni kuinamisha macho (kutotazama yalio haramishwa), kuondoa udhia, kurudisha salaam, kuamrisha mema na kukataza mabaya.” [Bukhaariy, Muslim]
1316.
وَعَنْ مُعَاوِيَةَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {مَنْ يُرِدِ اَللَّهُ بِهِ خَيْرًا، يُفَقِّهْهُ فِي اَلدِّينِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Mu’aawiyah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Anayemtakia Allaah kheri Humjaalia ufaqihi (‘ilmu ya kina) katika Dini.”[2] [Bukhaariy, Muslim]
1317.
وَعَنْ أَبِي اَلدَّرْدَاءِ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {مَا مِنْ شَيْءٍ فِي اَلْمِيزَانِ أَثْقَلُ مِنْ حُسْنِ اَلْخُلُقِ} أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ، وَاَلتِّرْمِذِيُّ وَصَحَّحَهُ
Kutoka kwa Abuu Ad-Dardaa (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Hakuna jambo zito katika mizani ya Muumini Siku ya Qiyaamah kama khulqa (tabia) njema.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na At-Tirmidhiy na akaisahihisha]
1318.
وَعَنِ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {اَلْحَيَاءُ مِنْ اَلْإِيمَانِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Hayaa ni katika iymaan.”[3] [Bukhaariy, Muslim]
1319.
وَعَنْ أَبِي مَسْعُودٍ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {إِنَّ مِمَّا أَدْرَكَ اَلنَّاسُ مِنْ كَلَامِ اَلنُّبُوَّةِ اَلْأُولَى: إِذَا لَمْ تَسْتَحِ، فَاصْنَعْ مَا شِئْتَ} أَخْرَجَهُ اَلْبُخَارِيُّ
Kutoka kwa Abuu Mas-‘uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Hakika miongoni mwa waliyopata watu kutoka katika mafundisho ya Manabiy wa mwanzo ni: usipostahi fanya utakalo.”[4] [Imetolewa na Al-Bukhaariy]
1320.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {اَلْمُؤْمِنُ اَلْقَوِيُّ خَيْرٌ وَأَحَبُّ إِلَى اَللَّهِ مِنْ اَلْمُؤْمِنِ اَلضَّعِيفِ، وَفِي كُلٍّ خَيْرٌ، اِحْرِصْ عَلَى مَا يَنْفَعُكَ، وَاسْتَعِنْ بِاَللَّهِ، وَلَا تَعْجَزْ، وَإِنْ أَصَابَكَ شَيْءٌ فَلَا تَقُلْ: لَوْ أَنِّي فَعَلْتُ كَانَ كَذَا وَكَذَا، وَلَكِنْ قُلْ: قَدَّرَ اَللَّهُ وَمَا شَاءَ فَعَلَ; فَإِنَّ لَوْ تَفْتَحُ عَمَلَ اَلشَّيْطَانِ} أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Muumini mwenye nguvu ni bora na anapendeza mno kwa Allaah[5] kuliko Muumini dhaifu, na katika wote (hao) muna kheri. Jali linalokunufaisha na muombe Allaah msaada wala usichoke. Utakapopatwa na jambo usiseme ‘Lau ningalifanya kadha wa kadha’ isipokuwa sema:
قَدَّرَ اَللَّهُ وَمَا شَاءَ فَعَلَ
‘Allaah Amekadiria, na Atakalo huwa’
kwani neno ‘lau’ hufungua amali ya shaytwaan.” [Imetolewa na Muslim]
1321.
وَعَنْ عِيَاضِ بْنِ حِمَارٍ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {إِنَّ اَللَّهَ أَوْحَى إِلَيَّ أَنْ تَوَاضَعُوا، حَتَّى لَا يَبْغِيَ أَحَدٌ عَلَى أَحَدٍ، وَلَا يَفْخَرَ أَحَدٌ عَلَى أَحَدٍ} أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa ‘Iyaadw bin Himaar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Hakika Allaah Amenifunulia Wahy kwamba nyenyekeeni ili yeyote asimdhulumu yeyote wala yeyote asijifakhiri juu ya yeyote.”[6] [Imetolewa na Muslim]
1322.
وَعَنْ أَبِي اَلدَّرْدَاءِ رضى الله عنه عَنْ اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: {مَنْ رَدَّ عَنْ عِرْضِ أَخِيهِ بِالْغَيْبِ، رَدَّ اَللَّهُ عَنْ وَجْهِهِ اَلنَّارَ يَوْمَ اَلْقِيَامَةِ} أَخْرَجَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَحَسَّنَهُ
وَلِأَحْمَدَ، مِنْ حَدِيثِ أَسْمَاءَ بِنْتِ يَزِيدَ نَحْوُهُ
Kutoka kwa Abuu Ad-Dardaa (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Atakayerudisha heshima ya nduguye asiyekuwepo,[7] Allaah Ataepusha uso wake dhidi ya moto siku ya Qiyaamah.” [Imetolewa na At-Tirmidhiy na amesema ni Hasan. Ahmad ana Hadiyth inayofanana kutoka kwa Asmaa[8] bint Yaziyd]
1323.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {مَا نَقَصَتْ صَدَقَةٌ مِنْ مَالٍ، وَمَا زَادَ اَللَّهُ عَبْدًا بِعَفْوٍ إِلَّا عِزًّا، وَمَا تَوَاضَعَ أَحَدٌ لِلَّهِ إِلَّا رَفَعَهُ} أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Swadaqah haijapunguza mali, Allaah Hamzidishii mja kwa msamaha ila utukufu, na hanyenyekei yeyote kwa ajili ya Allaah isipokuwa Allaah (عز وجل) Atamuinua.”[9] [Imetolewa na Muslim]
1324.
وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ سَلَّامٍ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {يَا أَيُّهَا اَلنَّاسُ! أَفْشُوا اَلسَّلَام، وَصِلُوا اَلْأَرْحَامَ، وَأَطْعِمُوا اَلطَّعَامَ، وَصَلُّوا بِاللَّيْلِ وَالنَّاسُ نِيَامٌ، تَدْخُلُوا اَلْجَنَّةَ بِسَلَامٍ} أَخْرَجَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ وَصَحَّحَهُ
Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Salaam (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Enyi watu! Enezeni salaam, na lisheni chakula, na ungeni kizazi na mswali (usiku) hali ya watu wamelala, mtaingia Jannah kwa amani.” [Imetolewa na At-Tirmidhiy na akaisahihisha]
1325.
وَعَنْ تَمِيمٍ الدَّارِيِّ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ صلى الله عليه وسلم {اَلدِّينُ اَلنَّصِيحَةُ " ثَلَاثًا. قُلْنَا: لِمَنْ يَا رَسُولَ اَللَّهِ؟ قَالَ:" لِلَّهِ وَلِكِتَابِهِ وَلِرَسُولِهِ وَلِأَئِمَّةِ اَلْمُسْلِمِينَ وَعَامَّتِهِمْ} أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Tamiym Ad-Daariy[10] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Dini ni nasaha.[11] Amesema mara tatu. Tukasema: ‘kwa nani Ee Rasuli wa Allaah! Akasema: “Hiyo ni kwa ajili ya Allaah, na Kitabu Chake, Rasuli Wake, viongozi wa Waislaam na watu wote.” [Imetolewa na Muslim]
1326.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {أَكْثَرُ مَا يُدْخِلُ اَلْجَنَّةَ تَقْوى اَللَّهِ وَحُسْنُ اَلْخُلُقِ} أَخْرَجَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mengi yanayowaingiza watu Jannah ni kuwa na taqwa Allaah[12] na khulqa (tabia) njema.” [Imetolewa na At-Tirmidhiy na akaisahihisha Al-Haakim]
1327.
وَعَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {إِنَّكُمْ لَا تَسَعُونَ اَلنَّاسَ بِأَمْوَالِكُمْ، وَلَكِنْ لِيَسَعْهُمْ بَسْطُ اَلْوَجْهِ، وَحُسْنُ اَلْخُلُقِ} أَخْرَجَهُ أَبُو يَعْلَى، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Nyinyi hamuwezi kuwatosheleza watu kwa mali zenu, lakini iwatoshe wao kutoka kwenu uchangamfu wa uso na khulqa (tabia) njema.” [Imetolewa na Abuu Ya’laa na akaisahihisha Al-Haakim]
1328.
وَعَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {اَلْمُؤْمِنُ مِرْآةُ اَلْمُؤْمِنِ} أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ بِإِسْنَادٍ حَسَنٍ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Muumini ni kioo[13] cha ndugu yake Muumini.” [Imetolewa na Abuu Daawud kwa isnaad Hasan]
1329.
وَعَنِ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {اَلْمُؤْمِنُ اَلَّذِي يُخَالِطُ اَلنَّاسَ، وَيَصْبِرُ عَلَى أَذَاهُمْ خَيْرٌ مِنْ اَلَّذِي لَا يُخَالِطُ اَلنَّاسَ وَلَا يَصْبِرُ عَلَى أَذَاهُمْ} أَخْرَجَهُ اِبْنُ مَاجَهْ بِإِسْنَادٍ حَسَنٍ، وَهُوَ عِنْدَ اَلتِّرْمِذِيِّ: إِلَّا أَنَّهُ لَمْ يُسَمِّ اَلصِّحَابِيَّ
Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Muumini anayetangamana na watu na anasubiri maudhi yao, ni bora kuliko Muumini asiyetangamana na watu wala hasubiri maudhi yao.” [Imetolewa na Ibn Maajah kwa Isnaad Hasan nayo iko kwa At-Tirmidhiy lakini hakutaja Swahaba]
1330.
وَعَنِ اِبْنِ مَسْعُودٍ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {اَللَّهُمَّ كَمَا أَحْسَنْتَ خَلْقِي، فَحَسِّنْ خُلُقِي} رَوَاهُ أَحْمَدُ وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّان َ
Kutoka kwa Ibn Mas-‘uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema:
اَللَّهُمَّ كَمَا أَحْسَنْتَ خَلْقِي، فَحَسِّنْ خُلُقِي
“Ee Allaah! Kama Ulivyofanya umbo langu kuwa bora nitengenezee tabia yangu.” [Imetolewa na Ahmad na akaisahihisha Ibn Hibbaan]
[1] Majukumu matano ya kuketi njiani yametajwa hapa. Kadhalika kuna mengine yaliyotajwa kama vile kumuelekeza mpita njia na kumjibu mwenye kupiga chafya n.k. majukumu haya yanafikia kumi na nne. katika lugha ya Kiarabu غَضُّ اَلْبَصَرِ ina maana kuinamisha macho chini na kutowaangalia wanawake, na mengine yaliyoharamishwa.
[2] Elimu ya halaal na haraam katika Shariy’ah inaitwa Fiqh. Maelezo haya yanaonesha utukufu na ukubwa wa somo hili muhimu. Kilichoelezwa hapa ni elimu ya Qur-aan na Sunnah ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), siyo mijadala ya kifalsafa yaliyopo katika masomo ya Shariy’ah leo hii, ambayo hayawezi kufahamika na akili ya mtu wa kawaida.
[3] Hadiyth hii inaonyesha kuwa kutojikweza kwa mtu na hayaa ni katika mambo yanayomsaidia na kutofanya madhambi, au kushindwa kutekeleza haki za wengine, kwa hakika hili linamfanya afikirie jina lake katika jamii lau baadhi ya madhambi yake yatadhihirika. Katika lugha nyingine, khulqa (tabia) njema na mtu kuwa na hayaa yanamfanya kutokariri mambo mabaya. Kwa hakika hayaa ni msingi wa khulqa (tabia) njema na ni sehemu katika iymaan ya mja.
[4] Pamoja na kuwa Shariy’ah za Rasuli waliyopita zimetenguliwa, suala la staha, ambalo ni moja ya taratibu zilizopita haikufutwa. Staha ni kigingi kinachomsaidia mtu katika kujizuia na kufanya mambo yoyote ayatakayo.
[5] Nini maana ya Muumini mwenye nguvu? Hii haimaanishi nguvu za kiwili wili. Badili yake inatujulisha utashi wa mtu kwa anayoyafanya katika mambo mema na kutaraji thawabu na malipo huko Aakhirah.
[6] Katika Hadiyth hii tunaona kuwa dhulma, kibr ni khulqa (tabia) zisizopendeza kwa mtu. Katika Hadiyth mojawapo inaelezwa kuwa dhulma ni katika mabaya zaidi ambayo mtu anaadhibiwa kwayo zaidi hapa duniani na huko Aakhirah. Hata hivyo kiini cha tatizo hili ni mtu kujikweza na kujiona.
[7] Ikiwa mtu atamsengenya mtu, anayesikia ni lazima amkataze anayesengenya, na kama inawezekana mtu aeleze mazuri yake badala ya mabaya yake.
[8] Huyu ni Asmaa binti wa Yaziyd bin As-Sakan Al-Ash-haliya. Alikuwa ni msemaji wa wanawake. Alishiriki katika vita vya Yarmuk na peke yake aliuwa watu tisa siku ile akiwa na upondo.
[9] Sifa tatu zilizotajwa katika Hadiyth hii zinaitwa kuwa ni ‘Misingi ya khulqa (tabia) njema’. Ambayo inafundisha usamehevu na unyenyekevu.
[10] Huyu ni Abuu Ruqaiyah, Tamiym bin Aws bin Kharija Ad-Dar. Alisilimu mwaka wa tisa Hijriyyah. Aliishi Baytul-Maqdis (Jerusalem). Ibn Siriyn anasema kuwa: “Alikusanya Qur-aan na alikuwa akiisoma kwa usiku mmoja.” Alifariki mwaka wa 40 Hijriyyah.
[11] Hadiyth hii ni kiini cha msingi wa Dini hii. Ni Hadiyth inayohitaji maelezo marefu, ingawaje hapa si penyewe kwa hilo. Nasaha kwa Allaah ni mtu kuwa na iymaan kwa Allaah, asimshirikishe na chochote na afuate mafundisho yake. Nasaha katika kitabu cha Allaah ni kuamini kuwa ni maneno ya Allaah, kuchukuwa kulichokatazwa na kukatazika nalo na kulifanyia kazi lililoamrishwa, kusoma kwa umakini na kufahamu maana yake na kufanya kazi. Nasaha kwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) ni kukiri Unabii wake na kufuata Sunnah zake. Ama nasaha kwa watawala Waislaam ni kuwasaidia katika yaliyo ya haki, kufuata amri zao, kuwakumbusha na mahitaji ya raia zake, kuwashauri katika wema na kuwaheshimu na kuwahamasisha kuendelea kufanya uadilifu. Na mwisho ni nasaha kwa Waislaam wote nayo ni kuwaelezea maslahi yao katika maisha yao hapa duniani na kesho Aakhirah, kuwalinda na uharibifu wowote au madhara yoyote, kuwaamrisha mema na kuwakataza maovu.
[12] Khulqa (tabia) njema hapa inahusisha: kutengamana na watu kwa wema, kutowafanyia ubaya, na kutabasamu kila unapokutana nao. Neno la Kiarabu تَقْوى linasimama kwa maana ya kufuata yaliyoamrishwa na kuacha yaliyokatazwa.
[13] Mtu anajifunza kuonekana kwake iwe ni uzuri au ubaya pindi anapojiangalia katika kioo. Vivyo hivyo, Muislaam ndio kioo cha Muislaam mwenzake na anatakiwa ajifunze kutoka kwa mwenzake kwa khulqa (tabia) alizonazo ili apendeze kwa Allaah na kwa watu baada ya kuondokana na khulqa yake mbaya.
بُلُوغُ الْمَرام
Buluwgh Al-Maraam
كِتَابُ اَلْجَامِعِ
Kitabu Cha Mjumuisho
بَابُ اَلذِّكْرِ وَالدُّعَاءِ
06-Mlango Wa Adhkaar Na Du’aa
1331.
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {يَقُولُ اَللَّهُ تَعَالَى: أَنَا مَعَ عَبْدِي مَا ذَكَرَنِي، وَتَحَرَّكَتْ بِي شَفَتَاهُ} أَخْرَجَهُ ابْنُ مَاجَهْ، وَصَحَّحَهُ ابْنُ حِبَّانَ، وَذَكَرَهُ اَلْبُخَارِيُّ تَعْلِيقًا
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Allaah (تعالى) Anasema: “Mimi Niko katika dhana ya mja wangu[1] anaponitaja na midomo yake inatikisika kwa sababu Yangu.” [Imetolewa na Ibn Maajah na akaisahihisha Ibn Hibbaan. Al-Bukhaariy ameitaja kuwa ni Mu’allaq]
1332.
وَعَنْ مُعَاذِ بْنِ جَبَلٍ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {مَا عَمِلَ ابْنُ آدَمَ عَمَلاً أَنْجَى لَهُ مِنْ عَذَابِ اَللَّهِ مِنْ ذِكْرِ اَللَّهِ} أَخْرَجَهُ ابْنُ أَبِي شَيْبَةَ، وَالطَّبَرَانِيُّ بِإِسْنَادٍ حَسَنٍ
Kutoka kwa Mu’aadh bin Jabal (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwana Aadam hajatenda amali yenye kumuokoa zaidi na adhabu ya Allaah kuliko kumdhukuru Allaah.” [Imetolewa na Ibn Abuu Shaybah na Atw-Twabaraaniy kwa isnaad nzuri]
1333.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {مَا جَلَسَ قَوْمٌ مَجْلِسًا، يَذْكُرُونَ اَللَّهَ إِلَّا حَفَّتْ بِهِمُ الْمَلَائِكَةُ، وَغَشِيَتْهُمُ الرَّحْمَةُ، وَذَكَرَهُمُ اللَّهُ فِيمَنْ عِنْدَهُ} أَخْرَجَهُ مُسْلِم ٌ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Watu hawakai wakamdhukuru Allaah isipokuwa Malaika Huwazunguka,[2] na rahmah huwaenea na utulivu huwateremkia, na Allaah Huwataja kwa walioko Kwake.” [Imetolewa na Muslim]
1334.
وَعَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {مَا قَعَدَ قَوْمٌ مَقْعَدًا لَمْ يَذْكُرُوا اَللَّهَ، وَلَمْ يُصَلُّوا عَلَى اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم إِلَّا كَانَ عَلَيْهِمْ حَسْرَةً يَوْمَ اَلْقِيَامَةِ} أَخْرَجَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَقَالَ: "حَسَنٌ"
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Watu hawakai kikao chochote na ikatokea hawamdhukuru Allaah katika kikao hicho wala hawamswalii Nabiy[3] (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) isipokuwa kitakuwa ni majuto kwao Siku ya Qiyaamah.” [Imetolewa na At-Tirmidhiy na amesema Hadiyth hii ni Hasan]
1335.
وَعَنْ أَبِي أَيُّوبَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {مَنْ قَالَ: لَا إِلَهَ إِلَّا اَللَّهُ، وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ عَشْرَ مَرَّاتٍ، كَانَ كَمَنْ أَعْتَقَ أَرْبَعَةَ أَنْفُسٍ مِنْ وَلَدِ إِسْمَاعِيلَ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Abuu Ayyuwb (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Atakayesema
لَا إِلَهَ إِلَّا اَللَّهُ، وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ
Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, peke yake hana mshirika
Ni kama mwenye kuacha huru nafsi nne katika wana wa Ismaa’iyl.”[4] [Bukhaariy, Muslim]
1336.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {مَنْ قَالَ: سُبْحَانَ اَللَّهِ وَبِحَمْدِهِ مِائَةَ مَرَّةٍ حُطَّتْ خَطَايَاهُ، وَإِنْ كَانَتْ مِثْلَ زَبَدِ اَلْبَحْرِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Atakayesema:
سُبْحَانَ اَللَّهِ وَبِحَمْدِهِ
Kutakasika ni kwa Allaah na Kuhimidiwa ni Kwak
e
Mara mia kwa siku atafutiwa dhambi zake hata kama ni mfano wa povu la bahari.” [Bukhaariy, Muslim]
1337.
وَعَنْ جُوَيْرِيَةَ بِنْتِ اَلْحَارِثِ قَالَتْ: قَالَ لِي رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {لَقَدْ قُلْتُ بَعْدَكِ أَرْبَعَ كَلِمَاتٍ، لَوْ وُزِنَتْ بِمَا قُلْتِ مُنْذُ اَلْيَوْمِ لَوَزَنَتْهُنَّ: سُبْحَانَ اَللَّهِ وَبِحَمْدِهِ، عَدَدَ خَلْقِهِ، وَرِضَا نَفْسِهِ، وَزِنَةَ عَرْشِهِ، وَمِدَادَ كَلِمَاتِهِ} أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Juwayriyah bint Al-Haarith[5] (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliniambia: “Nimesema maneno manne baada yako lau yangelinganishwa na uliosema tangu leo, ya kwangu yangeyashinda:[6]
سُبْحَانَ اَللَّهِ وَبِحَمْدِهِ، عَدَدَ خَلْقِهِ، وَرِضَا نَفْسِهِ، وَزِنَةَ عَرْشِهِ، وَمِدَادَ كَلِمَاتِهِ
Kutakasika ni kwa Allaah, na kuhimidiwa ni Kwake, kwa idadi ya viumbe Vyake na radhi ya nafsi Yake na uzito wa ‘Arshi Yake na wingi wa (kuandikia) maneno Yake.” [Imetolewa na Muslim]
1338.
وَعَنْ أَبِي سَعِيدٍ اَلْخُدْرِيِّ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {اَلْبَاقِيَاتُ اَلصَّالِحَاتُ: لَا إِلَهَ إِلَّا اَللَّهُ، وَسُبْحَانَ اَللَّهِ، وَاَللَّهُ أَكْبَرُ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ، وَلَا حَوْلَ وَلَا قُوَّةَ إِلَّا بِاَللَّهِ} أَخْرَجَهُ النَّسَائِيُّ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ، وَالْحَاكِمُ
Kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Amali njema yenye kubakia:[7]
لَا إِلَهَ إِلَّا اَللَّهُ، وَسُبْحَانَ اَللَّهِ، وَاَللَّهُ أَكْبَرُ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ، وَلَا حَوْلَ وَلَا قُوَّةَ إِلَّا بِاَللَّهِ
Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, na Kutakasika ni kwa Allaah, na Allaah ni Mkubwa, na sifa njema ni za Allaah na hapana uwezo wala nguvu ila vyote vinatokana na Allaah.”
[Imetolewa na An-Nasaaiy na akaisahihisha Ibn Hibbaan na Al-Haakim]
1339.
وَعَنْ سَمُرَةَ بْنِ جُنْدُبٍ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {أَحَبُّ اَلْكَلَامِ إِلَى اَللَّهِ أَرْبَعٌ، لَا يَضُرُّكَ بِأَيِّهِنَّ بَدَأْتَ: سُبْحَانَ اَللَّهِ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ، وَلَا إِلَهَ إِلَّا اَللَّهُ، وَاَللَّهُ أَكْبَرُ} أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Samurah bin Jundub (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Maneno yapendwayo mno kwa Allaah ni manne hakitakudhuru lolote utakaloanza
سُبْحَانَ اَللَّهِ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ، وَلَا إِلَهَ إِلَّا اَللَّهُ، وَاَللَّهُ أَكْبَرُ
Kutakasika ni kwa Allaah, sifa njema ni za Allaah, Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, Allaah ni Mkubwa.” [Imetolewa na Muslim]
1340.
وَعَنْ أَبِي مُوسَى اَلْأَشْعَرِيِّ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ لِي رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {يَا عَبْدَ اَللَّهِ بْنَ قَيْسٍ! أَلَّا أَدُلُّكَ عَلَى كَنْزٍ مِنْ كُنُوزِ اَلْجَنَّةِ؟ لَا حَوْلَ وَلَا قُوَّةَ إِلَّا بِاَللَّهِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْه ِ
زَادَ النَّسَائِيُّ: {وَلَا مَلْجَأَ مِنَ اللَّهِ إِلَّا إِلَيْهِ}
Kutoka kwa Abuu Muwsaa Al-Ash’ariyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Ee Abdullaah bin Qays! Nikujulishe hazina za Jannah?[8]
لَا حَوْلَ وَلَا قُوَّةَ إِلَّا بِاَللَّهِ
Hapana uwezo wala nguvu ila vyote vinatokana na Allaah.” [Bukhaariy, Muslim]
An-Nasaaiy ameongezea:
لَا مَلْجَأَ مِنَ اللَّهِ إِلَّا إِلَيْهِ
Hakuna pa kukimbilia ila ni kwake (Allaah).”
1341.
وَعَنِ النُّعْمَانِ بْنِ بَشِيرٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: {إِنَّ اَلدُّعَاءَ هُوَ اَلْعِبَادَةُ} رَوَاهُ اَلْأَرْبَعَةُ، وَصَحَّحَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ
وَلَهُ مِنْ حَدِيثِ أَنَسٍ بِلَفْظِ: {اَلدُّعَاءُ مُخُّ اَلْعِبَادَةِ}
وَلَهُ مِنْ حَدِيثِ أَبِي هُرَيْرَةَ رَفَعَهُ: {لَيْسَ شَيْءٌ أَكْرَمَ عَلَى اَللَّهِ مِنَ الدُّعَاءِ} وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ، وَالْحَاكِمُ
Kutoka kwa An-Nu’maan bin Bashiyr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Hakika du’aa ndio ‘ibaadah.”[9] [Imetolewa na Al-Arba’ah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah) na akaisahihisha At-Tirmidhiy]
Naye amepokea kutoka katika Hadiyth ya Anas kwa tamshi: “Du’aa ni ubongo wa ‘ibaadah.”
Vile vile amepokea katika Hadiyth ya Abuu Hurayrah Marfuw’: “Hakuna kitu kilicho kitukufu kwa Allaah kuliko du’aa.” Na akaisahihisha Ibn Hibbaan na Al-Haakim
1342.
وَعَنْ أَنَسٍ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {اَلدُّعَاءُ بَيْنَ اَلْأَذَانِ وَالْإِقَامَةِ لَا يُرَدُّ} أَخْرَجَهُ النَّسَائِيُّ، وَغَيْرُهُ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ، وَغَيْرُهُ
Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Du’aa baina ya Adhaan na Iqaamah hairudishwi.”[10] [Imetolewa na An-Nasaaiy na wengine na akaisahihisha Ibn Hibbaan na wengine]
1343.
وَعَنْ سَلْمَانَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {إِنَّ رَبَّكُمْ حَيِيٌّ كَرِيمٌ، يَسْتَحِي مِنْ عَبْدِهِ إِذَا رَفَعَ إِلَيْهِ يَدَيْهِ أَنْ يَرُدَّهُمَا صِفَرًا} أَخْرَجَهُ اَلْأَرْبَعَةُ إِلَّا النَّسَائِيَّ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ
Kutoka kwa Salmaan (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Hakika Rabb Wenu ni mwenye hayaa Mkarimu Anamstahi mja Wake anapoinua mikono yake Kwake kuirudisha patupu.”[11] [Imetolewa na Al-Arba’ah (At-Tirmidhiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah) isipokuwa An-Nasaaiy na akaisahihisha Al-Haakim]
1344.
وَعَنْ عُمَرَ رضى الله عنه قَالَ: {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم إِذَا مَدَّ يَدَيْهِ فِي اَلدُّعَاءِ، لَمْ يَرُدَّهُمَا، حَتَّى يَمْسَحَ بِهِمَا وَجْهَهُ} أَخْرَجَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ
وَلَهُ شَوَاهِدُ مِنْهَا: حَدِيثُ اِبْنِ عَبَّاسٍ: عَنْ أَبِي دَاوُدَ وَمَجْمُوعُهَا يَقْتَضِي أَنَّهُ حَدِيثٌ حَسَنٌ
Kutoka kwa ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ): “Alikua anaponyoosha mikono yake katika du’aa hairudishi hadi aipangusie uso wake.”[12] [Imetolewa na At-Tirmidhiy]
Nayo ina ushahidi mwingi ikiwemo Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) iliyoko kwa Abuu Daawuwd na wengineo. Jumla ya ushahidi wote unapelekea kuwa hii ni Hadiyth Hasan.
1345.
وَعَنِ ابْنِ مَسْعُودٍ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {إِنَّ أَوْلَى اَلنَّاسِ بِي يَوْمَ اَلْقِيَامَةِ، أَكْثَرُهُمْ عَلَيَّ صَلَاةً} أَخْرَجَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ
Kutoka kwa Ibn Mas-‘uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Atakayekuwa karibu zaidi nami siku ya Qiyaamah ni yule anayeniswalia kwa wingi zaidi.”[13] [Imetolewa na At-Tirmidhiy na akaisahihisha Ibn Hibbaan]
1346.
وَعَنْ شَدَّادِ بْنِ أَوْسٍ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {سَيِّدُ اَلِاسْتِغْفَارِ، أَنْ يَقُولَ اَلْعَبْدُ: اَللَّهُمَّ أَنْتَ رَبِّي، لَا إِلَهَ إِلَّا أَنْتَ، خَلَقْتَنِي، وَأَنَا عَبْدُكَ، وَأَنَا عَلَى عَهْدِكَ وَوَعْدِكَ مَا اِسْتَطَعْتُ، أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا صَنَعْتُ، أَبُوءُ لَكَ بِنِعْمَتِكَ عَلَيَّ، وَأَبُوءُ لَكَ بِذَنْبِي، فَاغْفِرْ لِي; فَإِنَّهُ لَا يَغْفِرُ اَلذُّنُوبَ إِلَّا أَنْتَ} أَخْرَجَهُ اَلْبُخَارِيُّ
Kutoka kwa Shaddaad bin Aws (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Bwana wa Istighfaar[14] ni mja kusema:
اَللَّهُمَّ أَنْتَ رَبِّي، لَا إِلَهَ إِلَّا أَنْتَ، خَلَقْتَنِي، وَأَنَا عَبْدُكَ، وَأَنَا عَلَى عَهْدِكَ وَوَعْدِكَ مَا اِسْتَطَعْتُ، أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا صَنَعْتُ، أَبُوءُ لَكَ بِنِعْمَتِكَ عَلَيَّ، وَأَبُوءُ لَكَ بِذَنْبِي، فَاغْفِرْ لِي; فَإِنَّهُ لَا يَغْفِرُ اَلذُّنُوبَ إِلَّا أَنْتَ
Ee Allaah, Wewe ni Rabb wangu, hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe, umeniumba mimi na mimi ni mja Wako, nami niko juu ya ahadi Yako, na agano Lako, kiasi cha uwezo wangu, najikinga Kwako kutokana na shari ya nilichokifanya, nakiri Kwako kwa kunineemesha, na nakiri kwa madhambi yangu, basi nakuomba unighufurie kwani hakuna wa kughufuria madhambi ila Wewe.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]
1347.
وَعَنِ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {لَمْ يَكُنْ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَدَعُ هَؤُلَاءِ اَلْكَلِمَاتِ حِينَ يُمْسِي وَحِينَ يُصْبِحُ: اَللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ اَلْعَافِيَةَ فِي دِينِي، وَدُنْيَايَ، وَأَهْلِي، وَمَالِي، اَللَّهُمَّ اسْتُرْ عَوْرَاتِي، وَآمِنْ رَوْعَاتِي، وَاحْفَظْنِي مِنْ بَيْنِ يَدَيَّ، وَمِنْ خَلْفِي، وَعَنْ يَمِينِي، وَعَنْ شِمَالِي، وَمِنْ فَوْقِي، وَأَعُوذُ بِعَظَمَتِكَ أَنْ أُغْتَالَ مِنْ تَحْتِي} أَخْرَجَهُ النَّسَائِيُّ، وَابْنُ مَاجَهْ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ
Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) hakuwa anaacha maneno haya anapochwewa[15] na anapopambazuka:
اَللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ اَلْعَافِيَةَ فِي دِينِي، وَدُنْيَايَ، وَأَهْلِي، وَمَالِي، اَللَّهُمَّ اسْتُرْ عَوْرَاتِي، وَآمِنْ رَوْعَاتِي، وَاحْفَظْنِي مِنْ بَيْنِ يَدَيَّ، وَمِنْ خَلْفِي، وَعَنْ يَمِينِي، وَعَنْ شِمَالِي، وَمِنْ فَوْقِي، وَأَعُوذُ بِعَظَمَتِكَ أَنْ أُغْتَالَ مِنْ تَحْتِي
“Ee Allaah, hakika nakuomba msamaha na Al’-Aafiyah (hifadhi, amani, salama) duniani na Aakhirah, na ahli wangu, na mali yangu. Ee Allaah nisitiri aibu zangu na nitulize khofu yangu. Ee Allaah, nihifadhi mbele yangu, na nyuma yangu, na kulia kwangu, na kushoto kwangu, na juu yangu, na najikinga kwa Uadhimu Wako kwa kutekwa chini yangu.”
[Imetolewa na An-Nasaaiy na Ibn Maajah na akaisahihisha Al-Haakim]
1348.
وَعَنِ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: {اَللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ زَوَالِ نِعْمَتِكَ، وَتَحَوُّلِ عَافِيَتِكَ، وَفَجْأَةِ نِقْمَتِكَ، وَجَمِيعِ سَخَطِكَ } أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akisema:
اَللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ زَوَالِ نِعْمَتِكَ، وَتَحَوُّلِ عَافِيَتِكَ، وَفَجْأَةِ نِقْمَتِكَ، وَجَمِيعِ سَخَطِكَ
“Ee Allaah! Najilinda Kwako kutokana na kuondoka neema Zako,[16] kubadilika uzima wangu, na adhabu yako ya ghafla, najilinda Kwako kutokana na hasira Zako zote.” [Imetolewa na Muslim]
1349.
وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: { كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: اَللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ غَلَبَةِ اَلدَّيْنِ، وَغَلَبَةِ اَلْعَدُوِّ، وَشَمَاتَةِ اَلْأَعْدَاءِ} رَوَاهُ النَّسَائِيُّ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ
Kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akisema:
اَللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ غَلَبَةِ اَلدَّيْنِ، وَغَلَبَةِ اَلْعَدُوِّ، وَشَمَاتَةِ اَلْأَعْدَاءِ
“Ee Allaah! Najilinda Kwako kushindwa na madeni, kushindwa na adui[17] na kuchekwa na maadui.” [Imetolewa na An-Nasaaiy na akaisahihisha Al-Haakim]
1350.
وَعَنْ بُرَيْدَةَ رضى الله عنه قَالَ: {سَمِعَ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم رَجُلاً يَقُولُ: اَللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ بِأَنِّي أَشْهَدُ أَنَّكَ أَنْتَ اَللَّهُ لَا إِلَهَ إِلَّا أَنْتَ، اَلْأَحَدُ اَلصَّمَدُ، اَلَّذِي لَمْ يَلِدْ، وَلَمْ يُولَدْ، وَلَمْ يَكُنْ لَهُ كُفُوًا أَحَدٌ. فَقَالَ" لَقَدْ سَأَلَ اَللَّهُ بِاسْمِهِ اَلَّذِي إِذَا سُئِلَ بِهِ أَعْطَى، وَإِذَا دُعِيَ بِهِ أَجَابَ} أَخْرَجَهُ اَلْأَرْبَعَةُ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ
Kutoka kwa Buraydah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimsikia mtu anaomba:
اَللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ بِأَنِّي أَشْهَدُ أَنَّكَ أَنْتَ اَللَّهُ لَا إِلَهَ إِلَّا أَنْتَ، اَلْأَحَدُ اَلصَّمَدُ، اَلَّذِي لَمْ يَلِدْ، وَلَمْ يُولَدْ، وَلَمْ يَكُنْ لَهُ كُفُوًا أَحَدٌ
“Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba kuwa mimi nashuhudia kuwa Wewe ni Allaah, hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe, Wewe Peke Yako, Mkusudiwa wa yote, Ambaye Hakuzaa wala Hakuzaliwa na wala hakuna mfano Wake chochote.”
Akasema Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ): Kwa hakika amemuomba Allaah kwa Jina lake ambalo Akiombwa nalo Hutoa[18] na Akiombwa kwalo Hujibu.” [Imetolewa na Al-Arba’ah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah) na akaisahihisha Ibn Hibbaan]
1351.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ: {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم إِذَا أَصْبَحَ، يَقُولُ: اَللَّهُمَّ بِكَ أَصْبَحْنَا، وَبِكَ أَمْسَيْنَا، وَبِكَ نَحْيَا، وَبِكَ نَمُوتُ، وَإِلَيْكَ اَلنُّشُورُ} وَإِذَا أَمْسَى قَالَ مِثْلَ ذَلِكَ ; إِلَّا أَنَّهُ قَالَ: {وَإِلَيْكَ اَلْمَصِيرُ} أَخْرَجَهُ اَلْأَرْبَعَةُ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa anapopambazuka anasema:
اَللَّهُمَّ بِكَ أَصْبَحْنَا، وَبِكَ أَمْسَيْنَا، وَبِكَ نَحْيَا، وَبِكَ نَمُوتُ، وَإِلَيْكَ اَلنُّشُورُ
“Ee Allaah! Kwako tumepambazuka na Kwako tunakuchwa, Kwako tunaishi, na Kwako tutakufa,[19] na Kwako tutafufuliwa.”
Na anapofikia jioni akisema vivo hivyo isipokuwa mwisho husema
وَإِلَيْكَ اَلْمَصِيرُ
Na marejeo ya mwisho ni Kwako.
[Imetolewa na Al-Arba’ah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah)]
1352.
وَعَنْ أَنَسٍ رضى الله عنه قَالَ: {كَانَ أَكْثَرُ دُعَاءِ رَسُولِ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم رَبَّنَا آتِنَا فِي اَلدُّنْيَا حَسَنَةً، وَفِي اَلْآخِرَةِ حَسَنَةً، وَقِنَا عَذَابَ اَلنَّارِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Du’aa ya Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliyokuwa akikithiri mno kuisoma ilikuwa ni:
رَبَّنَا آتِنَا فِي اَلدُّنْيَا حَسَنَةً، وَفِي اَلْآخِرَةِ حَسَنَةً، وَقِنَا عَذَابَ اَلنَّارِ
Ee Rabb! Tupe mema duniani na (Tupe) mema Aakhirah[20] na Utukinge na adhabu ya moto.”[21] [Bukhaariy, Muslim]
1353.
وَعَنْ أَبِي مُوسَى اَلْأَشْعَرِيِّ رضى الله عنه قَالَ: {كَانَ اَلنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم يَدْعُو: اَللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي خَطِيئَتِي، وَجَهْلِي، وَإِسْرَافِي فِي أَمْرِي، وَمَا أَنْتَ أَعْلَمُ بِهِ مِنِّي، اَللَّهُمَّ اِغْفِرْ لِي جِدِّي، وَهَزْلِي، وَخَطَئِي، وَعَمْدِي، وَكُلُّ ذَلِكَ عِنْدِي، اَللَّهُمَّ اِغْفِرْ لِي مَا قَدَّمْتُ، وَمَا أَخَّرْتُ، وَمَا أَسْرَرْتُ، وَمَا أَعْلَنْتُ، وَمَا أَنْتَ أَعْلَمُ بِهِ مِنِّي، أَنْتَ اَلْمُقَدِّمُ وَالْمُؤَخِّرُ، وَأَنْتَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Abuu Muwsaa Al-Ash’ariyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa anaomba du’aa hii:
اَللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي خَطِيئَتِي، وَجَهْلِي، وَإِسْرَافِي فِي أَمْرِي، وَمَا أَنْتَ أَعْلَمُ بِهِ مِنِّي، اَللَّهُمَّ اِغْفِرْ لِي جِدِّي، وَهَزْلِي، وَخَطَئِي، وَعَمْدِي، وَكُلُّ ذَلِكَ عِنْدِي، اَللَّهُمَّ اِغْفِرْ لِي مَا قَدَّمْتُ، وَمَا أَخَّرْتُ، وَمَا أَسْرَرْتُ، وَمَا أَعْلَنْتُ، وَمَا أَنْتَ أَعْلَمُ بِهِ مِنِّي، أَنْتَ اَلْمُقَدِّمُ وَالْمُؤَخِّرُ، وَأَنْتَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ
“Ee Allaah! Nighufurie makosa yangu, ujahili (ujinga) wangu, na israaf (upindukaji mipaka) katika mambo yangu, Unayoyajua Wewe kutoka kwangu. Ee Allaah! Nighufurie niliyoyafanya kwa kudhamiria, na niliyoyafanya kwa kukosea, na makosa yangu yote. Ee Allaah! Nighufurie niliyoyatanguliza na niliyoyachelewesha, na niliyoyaficha, na niliyoyadhihirisha, na ambayo Wewe Unayajua kuliko mimi, Wewe ni Mwenye kutanguliza, na Wewe ni mwenye kuchelewesha. Wewe ni Muweza juu ya kila kitu.” [Bukhaariy, Muslim]
1354.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ: {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: اَللَّهُمَّ أَصْلِحْ لِي دِينِي اَلَّذِي هُوَ عِصْمَةُ أَمْرِي، وَأَصْلِحْ لِي دُنْيَايَ اَلَّتِي فِيهَا مَعَاشِي، وَأَصْلِحْ لِي آخِرَتِي اَلَّتِي إِلَيْهَا مَعَادِي، وَاجْعَلْ اَلْحَيَاةَ زِيَادَةً لِي فِي كُلِّ خَيْرٍ، وَاجْعَلْ اَلْمَوْتَ رَاحَةً لِي مِنْ كُلِّ شَرٍّ} أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akisema:
اَللَّهُمَّ أَصْلِحْ لِي دِينِي اَلَّذِي هُوَ عِصْمَةُ أَمْرِي، وَأَصْلِحْ لِي دُنْيَايَ اَلَّتِي فِيهَا مَعَاشِي، وَأَصْلِحْ لِي آخِرَتِي اَلَّتِي إِلَيْهَا مَعَادِي، وَاجْعَلْ اَلْحَيَاةَ زِيَادَةً لِي فِي كُلِّ خَيْرٍ، وَاجْعَلْ اَلْمَوْتَ رَاحَةً لِي مِنْ كُلِّ شَرٍّ
“Ee Allaah! Nitengenezee Dini yangu ambayo ndio hifadhi ya mambo yangu, na Nitengenezee dunia yangu ambayo ndani yake ni maisha yangu. Na nitengenezee Aakhirah yangu ambayo ndio marejeo kwangu. Yafanye maisha ni ziada kwangu katika kila kheri, na mauti ni raha yangu kutokana na kila shari.”[22] [Imetolewa na Muslim]
1355.
وَعَنْ أَنَسٍ رضى الله عنه قَالَ: {كَانَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ:" اَللَّهُمَّ اِنْفَعْنِي بِمَا عَلَّمْتَنِي، وَعَلِّمْنِي مَا يَنْفَعُنِي، وَارْزُقْنِي عِلْمًا يَنْفَعُنِي} رَوَاهُ النَّسَائِيُّ، وَالْحَاكِمُ
وَلِلتِّرْمِذِيِّ: مِنْ حَدِيثِ أَبِي هُرَيْرَةَ نَحْوُهُ، وَقَالَ فِي آخِرِهِ: {وَزِدْنِي عِلْمًا، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ عَلَى كُلِّ حَالٍ، وَأَعُوذُ بِاَللَّهِ مِنْ حَالِ أَهْلِ اَلنَّارِ} وَإِسْنَادُهُ حَسَنٌ
Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akisema:
اَللَّهُمَّ اِنْفَعْنِي بِمَا عَلَّمْتَنِي، وَعَلِّمْنِي مَا يَنْفَعُنِي، وَارْزُقْنِي عِلْمًا يَنْفَعُنِي
“Ee Allaah! Ninufaishe kwa Ulichonifundisha, Unifundishe kitakachonifaa na Uniruzuku elimu itakayoninufaisha.”[23] [Imetolewa na An-Nasaaiy na Al-Haakim]
At-Tirmidhiy amepokea kutoka katika Hadiyth ya Abuu Hurayrah mfano wake mwisho wake akasema:
وَزِدْنِي عِلْمًا، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ عَلَى كُلِّ حَالٍ، وَأَعُوذُ بِاَللَّهِ مِنْ حَالِ أَهْلِ اَلنَّارِ
“Na Unizidishie elimu. Kuhimidiwa ni kwa Allaah kwa hali zote, na najilinda kwa Allaah kwa hali ya watu wa motoni.” [Isnaad yake ni Hasan]
1356.
وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم عَلَّمَهَا هَذَا اَلدُّعَاءَ: {اَللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ مِنَ الْخَيْرِ كُلِّهِ، عَاجِلِهِ وَآجِلِهِ، مَا عَلِمْتُ مِنْهُ وَمَا لَمْ أَعْلَمْ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنَ الشَّرِّ كُلِّهِ، عَاجِلِهِ وَآجِلِهِ، مَا عَلِمْتُ مِنْهُ وَمَا لَمْ أَعْلَمْ، اَللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ مِنْ خَيْرِ مَا سَأَلَكَ عَبْدُكَ وَنَبِيُّكَ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا عَاذَ بِهِ عَبْدُكَ وَنَبِيُّكَ، اَللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ اَلْجَنَّةَ، وَمَا قَرَّبَ إِلَيْهَا مِنْ قَوْلٍ أَوْ عَمَلٍ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنَ النَّارِ، وَمَا قَرَّبَ مِنْهَا مِنْ قَوْلٍ أَوْ عَمَلٍ، وَأَسْأَلُكَ أَنْ تَجْعَلَ كُلَّ قَضَاءٍ قَضَيْتَهُ لِي خَيْرًا} أَخْرَجَهُ اِبْنُ مَاجَهْ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ، وَالْحَاكِمُ
Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimfundisha du’aa hii:
اَللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ مِنَ الْخَيْرِ كُلِّهِ، عَاجِلِهِ وَآجِلِهِ، مَا عَلِمْتُ مِنْهُ وَمَا لَمْ أَعْلَمْ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنَ الشَّرِّ كُلِّهِ، عَاجِلِهِ وَآجِلِهِ، مَا عَلِمْتُ مِنْهُ وَمَا لَمْ أَعْلَمْ، اَللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ مِنْ خَيْرِ مَا سَأَلَكَ عَبْدُكَ وَنَبِيُّكَ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا عَاذَ بِهِ عَبْدُكَ وَنَبِيُّكَ، اَللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ اَلْجَنَّةَ، وَمَا قَرَّبَ إِلَيْهَا مِنْ قَوْلٍ أَوْ عَمَلٍ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنَ النَّارِ، وَمَا قَرَّبَ مِنْهَا مِنْ قَوْلٍ أَوْ عَمَلٍ، وَأَسْأَلُكَ أَنْ تَجْعَلَ كُلَّ قَضَاءٍ قَضَيْتَهُ لِي خَيْرًا
“Ee Allaah! Nakuomba kheri zote za dunia na Aakhirah, ninazozijua na nisizozijua. Najilinda Kwako na shari zote za dunia na Aakhirah, ninazozijua humo na nisizozijua. Ee Allaah! Nakuomba kheri aliyokuomba mja Wako na Nabiy Wako, na najilinda Kwako na shari aliyokuomba mja Wako na Nabiy Wako. Ee Allaah! Nakuomba Jannah na kinachokaribisha Jannah kwa kauli au kitendo, na najilinda Kwako na moto na kinachokaribisha motoni kwa kauli au kitendo. Nakuomba Ufanye kila hukumu Uliyohukumu kwangu iwe ya kheri.” [Imetolewa na Ibn Maajah na akaisahihisha Ibn Hibbaan na Al-Haakim]
1357.
وَأَخْرَجَ اَلشَّيْخَانِ عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {كَلِمَتَانِ حَبِيبَتَانِ إِلَى اَلرَّحْمَنِ، خَفِيفَتَانِ عَلَى اَللِّسَانِ، ثَقِيلَتَانِ فِي اَلْمِيزَانِ، سُبْحَانَ اَللَّهِ وَبِحَمْدِهِ ، سُبْحَانَ اَللَّهِ اَلْعَظِيمِ}
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Kuna maneno mawili yanapendwa mno na Ar-Rahmaan, mepesi katika ulimi, mazito katika mizani:
سُبْحَانَ اَللَّهِ وَبِحَمْدِهِ ، سُبْحَانَ اَللَّهِ اَلْعَظِيمِ
Kutakasika ni kwa Allaah na Kuhimidiwa ni Kwake, Kutakasika ni kwa Allaah Mtukufu.”[24] [Bukhaariy, Muslim]
[1] Katika Hadiyth hii Allaah (عز وجل) Anatangaza kuwa yu Pamoja na mja Wake si kwa kiwiliwili chake bali kwa elimu yake na kwa uweza Wake. Allaah Yupo katika ‘Arshi Yake.
[2] Tunajifunza kupitia Hadiyth hii tukufu kuwa Malaika wanavizungukia vikao vya kumdhukuru Allaah na huenezwa rahmah za Allaah ndani yake. Allaah (عز وجل) Anaweza kukumbukwa kupitia vikao hivi, kwa kumuomba Yeye tu na kusoma Qur-aan.
[3] Hadiyth nyingine inasema hivi: “Atawaadhibu, na Akipenda Atawasamehe.” Maneno haya ya kumdhukuru Allaah na kumswalia Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) ni ya lazima kufanywa.
[4] Hadiyth hii na Hadiyth za mfano huu, zenye maneno ya kuwa atakayefanya hivi na vile, atapata malipo haya na yale na kughufuriwa madhambi yake. Kuna rai tofauti kwa Wanazuoni kwa maana haswa ya Hadiyth hizi. Baadhi wanaona kuwa malipo yatalipwa kwa yule atakayefanya matendo yale siku zote, wakati Wanazuoni wengine hawahusishi sharti hili. Wanaona kuwa atakayefanya jambo lile la kulipwa ni vizuri ajizuie na madhambi makubwa kwanza. Hii ina maana ya kuwa matendo yale mazuri yatafuta madhambi madogo tu na sio makubwa. Wanazuoni wengine wanaona kuwa hayaingiliani kuwa ni madhambi madogo na makubwa, bali ni suala tu la malipo ayapatayo mtu. Baadhi ya Wanazuoni wana muono kuwa madhambi madogo yanaghufuriwa na kufutika kwa mambo mema ayafanyayo mtu, ama madhambi makubwa kifutio chake ni kutubia na kuomba maghfirah wa Allaah.
[5] Juwayriyah: Huyu ni Ummul-Mu’uminiyn, alikuwa katika mateka wa vita vya Al-Murais. Alikuwa ni katika fungu la hisa la Thaabit bin Qays bin Shammas, ambaye alikubaliana naye kumuuzia uhuru wake. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimlipa na akamuoa. Baada ya hapo Swahaba wakawaacha huru jamaa za Juwayriyah wakisema: “Hizi ni Shariy’ah za Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ).” Alikuwa ni mwanamke mwenye msaada mkubwa kwa watu wake. Alifariki mwaka 56 Hijriyyah.
[6] Maelezo ni kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliondoka na kumuacha Juwayriyah akiendelea na ‘ibaadah. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliporudi katika ‘ibaadah wakati wa Dhwuhaa alimuona Juwayriya akiendelea na ‘ibaadah. Wakati huo Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akamtajia maneno yale.
[7] Maelezo mengi yanaonesha kuwa malipo ya matendo yote ya utiifu kwa Allaah na kufanya wema, yatabakia katika amali za aliyefanya matendo hayo. Miongoni mwa hayo ni maneno haya manne yaliyotajwa katika Hadiyth hii.
[8] Ina maana ya kuwa malipo ya kusema maneno haya ni makubwa, malipo yenyewe Allaah Ameyahifadhi Jannah. Kama zilivyo hazina zozote zenye thamani kubwa zinahifadhiwa katika sehemu yenye usalama.
[9] Du’aa ni sehemu ya ‘ibaadah. Kadhalika inaweza kuwa na maana kuwa Du’aa katika aayah ya Allaah:
وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ ۚ إِنَّ الَّذِينَ يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِي سَيَدْخُلُونَ جَهَنَّمَ دَاخِرِينَ﴿٦٠﴾
“Na Rabb wenu Amesema: Niombeni, Nitakuitikieni. Hakika wale wanaotakabari katika kuniabudu wataingia Jahanam wadhalilike” [Al Ghaafir: 60] ina maana ‘Niabudu nami Nitajibu du’aa zako…’
[10] Tunabainishiwa hapa kuwa kuna baadhi ya muda du’aa zinajibiwa, kama vile katikati ya usiku na baada ya Swalaah ya fardhi. Watu walimuuliza Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) ni nini cha kuomba katikati ya Adhana na Iqaamah. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliwaambia wamuombe Allaah al-‘aafiyah (afya na salama) katika maisha yao ya kila siku na Iymaan yao katika kuyaendea mambo yao ya Dini.
[11] Katika Hadiyth hii tunajifunza kuwa ni Sunnah kunyanyua mikono wakati wa kuomba du’aa
[12] Kutokana na mapokezi ya Hadiyth hii ni kuwa baada ya kumaliza du’aa ni vizuri kupangusa uso kwa matumbo ya mkono.
[13] Kwa hakika kumswalia Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) ni du’aa kwa Allaah ya kumuombea rahmah Nabiy wake (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) katika kongamano la Malaika, na ni tendo kubwa la ki’ibaadah. Baada ya du’aa tukufu ya
لاَ إله الاَّ الله
inafuatiwa na ‘ibaadah ya kumuombea Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) wetu na kumswalia.
[14] Du’aa hii imeitwa kuwa ni bwana wa Istighfaar (kuomba maghfirah). Ina hisia kubwa ya mja kujidhalilisha kwa Bwana wake apate kile anachokiomba.
[15] Al-‘Aafiyah ni neno linalojumuisha Allaah (عزّ وجلّ) kumjaalia mja Wake salama na kumpa amani, na kumlinda na maradhi, balaa, majanga, madhara, misukosuko, na kila aina za shari za wanaadam na majini na kubakia salama katika Dini yake na Aakhirah yake. Katika Dini ni ile hali ya kuacha madhambi na bid’ah, au kupuuzia majukumu ya mtu ya Dini au kuyaacha moja kwa moja. Al-‘Aafiyah kwa familia ni kutokupata maradhi, na mahitaji makubwa ya matamanio ya dunia. Al-‘Aafiyah katika utajiri na mali ni mtu kuokolewa na yanayoangamiza. Katika Hadiyth hii na du’aa Allaah Anatulinda na majanga yote yanayotokana na kukosa Al-‘Aafiyah. Tukizingatia kuwa mwana Aadam amezungukwa na maadui wake wengi kutokana na mashaytwaan wa kibin Aadam na mashaytwaan wa kijini, mwana Aadam ni kama kondoo katikati ya mbwa mwitu; kama hana ulinzi kutoka kwa Allaah, hawezi kujilinda yeye mwenyewe.
[16] Neema za Allaah zinaondoshwa na madhambi ya mtu. Kwa maneno mengine, kama kwamba maneno yaliyo katika du’aa hii ni kama kumuomba Allaah Atukinge na ubaya wa matendo yetu. Kwa hakika haya ni maneno tunayofundishwa na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) na sio ya kuwa yeye ndie aliyekuwa muhitaji zaidi kwani hakuwa na dhambi.
[17] Kuzidiwa na madeni na ile hali ya kuwa mtu anashindwa tena kuyalipa madeni yale na hali hii huondoa hata nia ya kulipa deni lenyewe. Kwa hakika mwenye niyyah halisi ya kulipa deni lake Allaah Atamsahilishia njia ya kulilipa na kumpa nguvu ya kulipa kama ilivyotajwa katika Hadiyth. Ama kushindwa na maadui ni ile hali ya mtu kushindwa kujitetea au kulipa kisasi cha uadui uliofanywa.
[18] Katika lugha ya Kiarabu kuomba ina maana ya kuomba jambo fulani makhsusi, wakati du’aa ni ya jumla jamala (kuomba chochote). Vile vile kumuomba Allaah kitu, inatakiwa kutumiwa maneno yale yale yaliyokuja katika Hadiyth ambayo yatapata hadhi zaidi ya kujibiwa au kukubaliwa.
[19] Inasemwa, ‘Kulala ni nusu ya mauti’. Kutokana na uhusiano uliyopo wa maneno haya. Muda wowote mtu anapolala, ni kama anarejesha roho yake katika asili yake. Vivyo hivyo, neno la Kiarabu اَلْمَصِيرُ (mwisho wa kitu) limetumika katika Hadiyth hii (mwisho wako) kwa yule anayejitayarisha kulala. Mfano huo huo, mtu anapoamka, kama kwamba anarejesha uhai baada ya kifo. Katika lugha ya Kiarabu اَلنُّشُورُ (ufufuo) umetumika katika Hadiyth hii kwa maana ya (ufufuo wako) kwa yule ambaye anaamka kutoka usingizini.
[20] حَسَنَةً Mema ya maisha haya yanahusisha vitu vizuri vyema kama vile: mwenza wa maisha (mke/mume), Taqwah, watoto wema, utajiri na kujitosha, matumizi mazuri ya elimu ya mtu, n.k. mema ya Aakhirah ni mja kuingia Jannah, na mengine mfano wake kama vile kuwa mbali na wasiwasi, hesabu ya mtu kuwa nyepesi na kuokolewa na moto. Hadiyth iliyopokelewa na Abuu Hurayrah kwamba mtu anamuomba Allaah na anajikinga na moto mara saba, nao moto unamuomba Allaah kwa kusema: ‘Mja wako fulani anaomba ulinzi wako dhidi yangu, hivyo mpe ulinzi wako.’
[21] Al-Baqarah aayah ya 201
[22] Katika du’aa hii, uzuri wa maisha yote mawili ni yenye kutafutwa. Haina maana kuwa mtu aombee kifo chake. Bali matamanio aina gani ya kifo ikibidi yawe, ambayo ayatampa mja malazi na makazi mazuri baada ya hapo kutokana na kila jambo la shari kabla ya kufa katika maisha haya na baada yake (kaburini).
[23] Hadiyth hii inatufungua macho kuwa tuombe elimu yenye manufaa, na tuombe kwa Allaah na tujikinge na elimu isiyokuwa na manufaa. Elimu isiyokuwa na manufaa n ile isiyokuwa na manufaa na wewe katika Aakhirah yako.
[24] Imaam Al-Bukhaariy alihitimisha Swahiyh Al-Bukhaariy kwa kutaja Hadiyth hii. Kwa kufuata mfano wake waandishi wengi na wakusanyaji wengi wamemaliza Hadiyth kwa Hadiyth hii. Hadiyth hii inathibitisha kuwepo kwa Miyzaan (kipimo cha kupima matendo ya siku ya hukumu) kama yalivyotajwa kwa uwazi katika Qur-aan. Kuna mgongano wa rai miongoni mwa Wanazuoni katika upimaji wa matendo ya watu. Baadhi ya Wanazuoni wana muono kuwa hata ile rekodi ya matendo ya watu itapimwa, kama ilivyothibitishwa na Hadiyth ya “Bitaqa” iliyoripotiwa na Ahmad, Tirmidhiy, Ibn Maajah na wengineo. (Silsilah Ahadiyth Asw-Swahiyhah 1/212 namba 135). Wanazuoni wengine wana rai kwamba kila tendo lina maana yake, kwa maana kila tendo litapimwa kivyake, kama ilivyothibitishwa na Hadiyth ya mwisho katika Buluwgh Al-Maraam (namba 1358). Hadiyth hii inatuelezea upana wa rahmah ya Allaah, kuwa anatoa malipo makubwa sana kwa matendo madogo sana, na watu kusamehewa kwa makosa yao mara kwa mara.
Ee Allaah! Al-Ghafuwr na Ar-Rahiym, Muokoe mja wako katika asiyoyaona na Mkubalie Tawbah yake kwa huruma yako. Aamiyn, Ee Allaah! Mhifadhi wa dunia na Aakhirah. Ee Allaah! Msamehe madhambi ya mwandishi wa kitabu hiki Aamiyn.
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/277
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10266&title=16-Buluwgh%20Al-Maraam%3A%20Kitabu%20Cha%20Mjumuisho%20-%20%D9%83%D9%90%D8%AA%D9%8E%D8%A7%D8%A8%D9%8F%20%D8%A7%D9%8E%D9%84%D9%92%D8%AC%D9%8E%D8%A7%D9%85%D9%90%D8%B9%D9%90
[3] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10267&title=01-Buluwgh%20Al-Maraam%3A%20Kitabu%20Cha%20Mjumuisho%3A%20Mlango%20Wa%20Adabu
[4] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10268&title=02-Buluwgh%20Al-Maraam%3A%20Kitabu%20Cha%20Mjumuisho%3A%20Mlango%20Wa%20Wema%20Na%20Kuunga%20Kizazi
[5] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10269&title=03-Buluwgh%20Al-Maraam%3A%20Kitabu%20Cha%20Mjumuisho%3A%20Mlango%20Wa%20Kuipa%20Mgongo%20Dunia
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10280&title=04-Buluwgh%20Al-Maraam%3A%20Kitabu%20Cha%20Mjumuisho%3A%20Mlango%20Wa%20Onyo%20Dhidi%20Ya%20Akhlaaq%20%28Tabia%29%20Mbaya
[7] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10432&title=05-Buluwgh%20Al-Maraam%3A%20Kitabu%20Cha%20Mjumuisho%3A%20Mlango%20Wa%20Mahimizo%20Ya%20Akhlaaq%20%28Tabia%29%20Njema
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10433&title=06-Buluwgh%20Al-Maraam%3A%20Kitabu%20Cha%20Mjumuisho%3A%20Mlango%20Wa%20Adhkaar%20Na%20Du%E2%80%99aa