A-Majina Ya Swahaba: Maana, Wasifu Wao Kwa Mukhtasari
Alhidaaya.com [2]
‘Abbaad Bin Bishr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ)
Jina Lake: ‘Abbaad Bin Bishr
(Al-Answaariyy)
عبّاد بن بشر
Maana Yake: Mwenye kumwabudu Allaah (عَزَّ وَجَلَّ) mno.
Wasifu Wake:
‘Abbaad bin Bishr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) akijulikana kwa taqwa yake na ‘ibaadah zake, elimu yake na ushujaa vitani.
’Abbaad bin Bishr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alipofika umri wa miaka kumi na nane kwa mara ya kwanza alipomsikia Musw’ab bin Umayr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) akisoma Qur-aan alisisimkwa sana. Qur-aan ilikua na sehemu maalumu katika moyo wa ‘Abbaad.
Alikua mashuhuri sana kwa usomaji wa Qur-aan mpaka ikampelekea kutambulika na Swahaba wengineo (رَضِيَ الْلَّهُ عَنْهُمْ) kwani alijulikana kama ni rafiki wa Qur-aan.
‘Aaishah (رَضِيَ الْلَّهُ عَنْهَا) kuna wakati alisema “Kuna watu watatu miongoni mwa ma Answaar hakuna ambaye atawazidi kwa ubora wa fadhila kama Sa’ad bin Mu’aadh Usayd ibn Khudayr na ‘Abbaad bin Bishr.
Kufariki Kwake:
A-Majina Ya Swahaba: Maana, Wasifu Wao Kwa Mukhtasari
‘Abdur-Rahmaan Bin ‘Awf (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ)
Alhidaaya.com [5]
Jina Lake: ‘Abdur-Rahmaan Bin ‘Awf
(Al-Qurayshiyy)
عبد الرّحمن بن عوف
Maana Yake: ‘Abdur-Rahmaan – Mja wa Mwingi wa Rahmah
Wasifu Wake:
Katika zama za ujahiliya, jina lake ‘Abdur-Rahman bin ‘Awf lilikuwa ‘Abdul-K’abah. Kisha Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimpa kwa jina jipya na kumwita ‘Abdur-Rahman.
Ni Swahaba aliyeshuhudia vita vote alivopigana Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Alisimama imara na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) katika vita va Uhud.
‘Abdur-Rahmaan bin ‘Awf (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) katika Swahaba kumi waliobashiriwa Jannah.
Alikua ni mfano bora na mfuasi wa kweli wa Uislamu ambaye alitoa mali yake kwa wingi katika jihaad fiy SabiliLlaah ikawa ni sababu ya kufikia radhi za Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى)
Kufariki Kwake:
‘Abdur-Rahmaan bin ‘Awf (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 75, na aliswaliwa Swalaah ya Janaazah na ‘Uthmaan bin ‘Affaan (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ).
A-Majina Ya Swahaba: Maana, Wasifu Wao Kwa Mukhtasari
Abu ‘Ubaydah 'Aamir Bin Al-Jarraah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ)
Alhidaaya.com [5]
Jina Lake:‘ Abu ‘Ubayadah ‘Aamir bin Al-Jarraah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ)
(Al-Qurayshiyy)
أبو عبيدة عامر بن الجرّاح
Maana Yake: ‘Ubaydah ni Mja au Mtumishi wa Allaah
Wasifu Wake:
Abu ‘Ubaydah Bin Al-Jarraah ni Swahaba aliyejulikana kuwa ni hakimu mwaminifu.
Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimpa jukumu la kuliongoza jeshi lililokwenda kumsaidia ‘Amru bin Al-‘Aasw (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) katika vita vilivyojulikana kwa jina la 'Dhaatus Salaasil'. Katika vita hivyo alipewa uongozi wa jeshi ambalo ndani yake alikuwemo Abu Bakr na ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا).
Abu ‘Ubaydah Bin Al-Jarraah ni Swahaba ambaye Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) alisema kuhusu yake: "Hakika kila umma una mwaminifu wake, na mwaminifu wa Umma huu ni Abu ‘Ubaydah ‘Aamir bin Al-Jarraah."
Abu ‘Ubaydah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alikuwa mwenye uso mkunjufu, mwembamba, mrefu, na jicho hutulia na kufurahi kila linapomuona. Alikuwa mpole mwenye huruma.
‘Abdullaah bin ‘Umar bin Al Khattwaab (رَضِيَ اللهُ عَنْهما) alisema juu yake: "Watatu katika ma-Quraysh walikuwa wenye nyuso kunjufu, mwenendo na tabia njema, wingi wa hayaa, na hawasemi uongo wanapozungumza na wala hawakukadhibishi unapozungumza nao; Abu Bakr Asw-Swiddiyq, ‘Uthmaan bin ‘Affaan na Abu ‘Ubaydah bin Al-Jarraah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمْ)."
Kufariki Kwake:
Abu ‘Ubaydah 'Aamir Bin Al-Jarraah alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 58 kwa ugonjwa wa tauni uliojulikana kwa jina la ‘Twa’uwn Amuwaas’ kutokana na jina la mji wa Amuwaas (Jordan) ulioshambuliwa na maradhi hayo. Na hii ilikuwa katika mwaka wa kumi na nane (18), na wengine wakasema kuwa amefariki katika mwaka wa kumi na saba (17) Hijriyyah.
A-Majina Ya Swahaba: Maana, Wasifu Wao Kwa Mukhtasari
Abu Bakr Asw-Swiddiyq (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ)
Alhidaaya.com [5]
Jina Lake: Abu Bakr Asw-Swiddiyq
(Al-Qurayshiyy)
ابو بكر الصّدّيق
Maana Yake: Abu ni baba na Bakr ni ngamia mchanga (mtoto).
Wasifu Wake:
Jina halisi la Abu Bakr ni ‘Abdullaah ibn Abi Quhaafah.
Abu Bakr alijulikana kama Asw-Swiddiyq (msema kweli). Heshima yake ilikua kubwa sana baina ya ma-Quraysh.
Abu Bakr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alikua mtu mwenye elimu kubwa ya kuhifadhi nasaba za makabila na mataifa ya kiarabu.
Abu Bakr aliishi kama mfanya biashara hapo Makkah. Inasemekana kwamba alitoa mali nyingi fiy SabiliLlaah (njia ya Allaah) kuliko yeyote mwengine.
Abu Bakr ni Swahaba wa kwanza aliyebashiriwa Jannah.
Alizaliwa miaka miwili baada ya kuzaliwa Nabiy Muhammad (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ).
Upendo wa Abu Bakr kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) ulikuwa mkubwa sana kiasi kwamba alikuwa tayari kutoa maisha yake kwa ajili ya kumlinda na kumfariji Nabiy Muhammad (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ).
Alikua Swahaba mnyenyekevu na mkarimu ambaye aliaminiwa na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) katika kila kitu kwa kiwango ambacho aliitwa As-Swiddiyq na Nabiy Muhammad (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ).
Utu wake mkubwa na utumishi wake kwa Uislamu na Waislamu ulimpatia upendo na heshima ya Waislamu wote, alichaguliwa na Waislamu wote kama Khalifa wa kwanza baada ya kifo cha Nabiy Muhammad (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ).
Kufariki Kwake:
Abu Bakr Asw-Swiddiyq (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alifariki akiwa na umri wa miaka 63 mwaka wa 13 wa Hijri.
A-Majina Ya Swahaba: Maana, Wasifu Wao Kwa Mukhtasari
‘Abdullaah Bin ‘Amr Ibn Al-‘Aasw (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ)
Alhidaaya.com [5]
Jina Lake: ‘Abdullaah bin ‘Amr Ibn Al-‘Aasw
(Al-Qurayshiyy)
عبد الله بن عمر بن العاص
Maana Yake: Mja wa Allaah.
Wasifu Wake:
‘Abdullah ibn ‘Amr ibn Al-‘Aasw (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alikuwa ni mtoto wa Swahaba mashuhuri ‘Amr ibn Al-‘Aasw (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ). Alikusanya Hadiyth nyingi za Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم).
‘Abdullaah alijitolea kwa bidii kuhudumia Dini ya Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى) kupita kiasi mpaka alilazimishwa na baba yake kuoa. Usiku wa Nikaah yake alimuomba mke wake (biharusi) ruhusa ili aswali rakaa mbili. Kutokana na khushuu ya Swalaah yake, akajisahau aliendelea na Swalaah mpaka Adhaan ya Alfajiri. Siku ya pili alikaa na mke wake ilipofika usiku alimwomba tena ruhusa mke wake aende akaswali rakaa mbili. Akapitiza tena mpaka Adhaan ya Alfajiri. Alirudia tena hivo hivo siku ya tatu. ‘Amr ibn Al-‘Aasw alienda kumtembelea mke wa mwanae na kumuulizia mwanae ‘Abdullaah. Yule mke alimweleza kuhusu ‘Abdullaah na ‘ibaadah zake. Yule baba alimchukua mwanae na kumpeleka kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) ili amkumbushe haki za wengine na haki za miili yetu. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) alimweleza ‘Abdullaah kwamba aswali usiku na pia awe analala, afunge (Swiyaam) siku chache na aache siku zingine, aupe mwili wake mwili haki, ampe mke wake haki, na hata wageni wake awape haki zao.
Kufariki Kwake:
‘Abdullaah bin ‘Amr ibn Al-‘Aasw (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alifariki Misr na alizikwa kwenye nyumba yake ndogo mwaka 65AH. Hakuzikwa kwenye makaburi alizikwa nyumbani kwasababu ya mfarakano wa jeshi dhidi ya Marwaan.
A-Majina Ya Swahaba: Maana, Wasifu Wao Kwa Mukhtasari
‘Abdullaah bin Mas’uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ)
Alhidaaya.com [5]
Jina lake:
‘Abdullaah bin Mas’uwd
(Al-Qurayshiyy)
عبد الله ابن مسعود
Maana Yake: Mja wa Allaah
Wasifu Wake:
‘Abdullaah bin Mas’uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alitoka kwenye mazingira ya kimaskini.
Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akimpenda sana na akipenda sana usomaji wake wa Qur-aan.
Ni Swahaba wa kwanza aliyesimama mbele ya ma-Quraysh bila uwoga na kusoma Qur-aan kwa sauti kubwa.
‘Abdullaah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alikua ni mtunzaji siri za Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ).
Na ni Swahaba ambaye daiman alikua akimbebea Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) viatu vyake.
Alikua ni Swahaba mwembamba na mwenye miguu membamba sana. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alisema kuwa miguu ya ‘Abdullaah itakuwa mizito katika Miyzaan Siku ya Qiyaamah kuliko Jabal Uhud.
‘Abdullaah (رضي الله عنه) alikua ni hakimu wa Kufa na pia muweka hazina katika ukhalifa wa ‘Umar na mwanzo wa ukhalifa wa ‘Uthmaan, kisha akahamia Madiynah.
Kufariki Kwake:
‘Abdullaah bin Mas-‘uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alifariki Madiynah mwaka 32AH alipofika umri wa miaka 70 na alizikwa Al-Baaqiy.
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/233
[2] http://www.alhidaaya.com/sw/
[3] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10938&title=A-Majina%20Ya%20Swahaba%3A%20Maana%2C%20Wasifu%20Wao%20Kwa%20Mukhtasari
[4] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10939&title=A-Majina%20Ya%20Swahaba%3A%20Maana%2C%20Wasifu%20Wao%20Kwa%20Mukhtasari%3A%20%27Abbaad%20Bin%20Bishr%20
[5] http://www.alhidaaya.com
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10944&title=A-Majina%20Ya%20Swahaba%3A%20Maana%2C%20Wasifu%20Wao%20Kwa%20Mukhtasari%3A%20%27Abdur-Rahmaan%20bin%20%27Awf
[7] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10943&title=A-Majina%20Ya%20Swahaba%3A%20Maana%2C%20Wasifu%20Wao%20Kwa%20Mukhtasari%3A%20%27Abu%20%27Ubaydah%20Bin%20Aamir%20Al-Jarraah
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10942&title=A-Majina%20Ya%20Swahaba%3A%20Maana%2C%20Wasifu%20Wao%20Kwa%20Mukhtasari%3A%20Abu%20Bakr%20Asw-Swiddiyq
[9] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10940&title=A-Majina%20Ya%20Swahaba%3A%20Maana%2C%20Wasifu%20Wao%20Kwa%20Mukhtasari%3A%20%E2%80%98Abdullaah%20Bin%20%E2%80%98Amr%20Ibn%20Al-%E2%80%98Aasw%20
[10] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10941&title=A-Majina%20Ya%20Swahaba%3A%20Maana%2C%20Wasifu%20Wao%20Kwa%20Mukhtasari%3A%20%E2%80%98Abdullaah%20bin%20Mas%E2%80%99uwd