Alhidaaya.com
Published on Alhidaaya.com (https://www.alhidaaya.com/sw)

Ukurasa Wa Kwanza > 05-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Kitabu Cha Maamkizi Ya Salaam - كِتابُ السَّلام > 04-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kupendeza Kurudia Salamu kwa Yule Mnayekutana Naye Mara Nyingi kwa Ukaribu wa Kuingia Kisha Kutoka au Ukawatenganisha Wao Mti na Mfano wake

04-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kupendeza Kurudia Salamu kwa Yule Mnayekutana Naye Mara Nyingi kwa Ukaribu wa Kuingia Kisha Kutoka au Ukawatenganisha Wao Mti na Mfano wake

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

 

باب استحباب إعادة السلام عَلَى من تكرر لقاؤه عَلَى قرب بأن دخل ثم خرج

ثُمَّ دخل في الحال ، أَو حال بينهما شجرة ونحوهما

04-Mlango Wa Kupendeza Kurudia Salamu kwa Yule Mnayekutana Naye Mara Nyingi kwa Ukaribu wa Kuingia Kisha Kutoka au Ukawatenganisha Wao Mti na Mfano wake

 

 

Alhidaaya.com [1]

 

 

Hadiyth – 1

عن أَبي هريرة رضي الله عنه في حديثِ المسِيءِ صلاته : أنّه جَاءَ فَصَلَّى ، ثُمَّ جَاءَ إِلَى النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم ، فَسَلَّمَ عَلَيْهِ ، فَرَدَّ عَلَيْهِ السَّلاَمَ ، فَقَالَ : (( ارْجِعْ فَصَلِّ فَإنَّكَ لَمْ تُصَلِّ )) فَرَجَعَ فَصَلَّى ، ثُمَّ جَاءَ فَسَلَّمَ عَلَى النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم ، حَتَّى فَعَلَ ذَلِكَ ثَلاثَ مَرَّاتٍ . متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuhusu yule mtu aliyekosea katika Swalaah yake: ya kwamba alikuja akaswali, kisha akaja kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kumsalimia. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimjibu na kumwambia: "Rudi ukaswali, kwani wewe hujaswali." Yule mtu alirudi kuswali, kisha akaja na kumtolea salamu Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mpaka akafanya hilo mara tatu." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، عن رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إِذَا لَقِيَ أَحَدُكُمْ أخَاهُ فَلْيُسَلِّمْ عَلَيْهِ ، فَإنْ حَالَتْ بَيْنَهُمَا شَجَرَةٌ ، أَوْ جِدَارٌ ، أَوْ حَجَرٌ ، ثُمَّ لَقِيَهُ ، فَلْيُسَلِّمْ عَلَيْهِ )) رواه أَبُو داود .

Na imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anapokutana mmoja wenu na nduguye amsalimie. Baada ya hapo ikiwa watatenganishwa na mti au ukuta au jabali (jiwe), kisha wakakutana tena basi amsalimie tena." [Abu Daawuwd]

 

 

 

Share [2]
www.alhidaaya.com

Source URL: https://www.alhidaaya.com/sw/node/11025

Links
[1] http://www.alhidaaya.com/
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11025&title=04-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kupendeza%20Kurudia%20Salamu%20kwa%20Yule%20Mnayekutana%20Naye%20Mara%20Nyingi%20kwa%20Ukaribu%20wa%20Kuingia%20Kisha%20Kutoka%20au%20Ukawatenganisha%20Wao%20Mti%20na%20Mfano%20wake