Alhidaaya.com
Published on Alhidaaya.com (https://www.alhidaaya.com/sw)

Ukurasa Wa Kwanza > 06-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Kitabu Cha Kumzuru Mgonjwa, Jeneza... - كتاب عيادة المريض وتشييع الميت والصلاة عليه وحضور دفنه > 06-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kuruhusiwa Mgonjwa Kusema: Ninaumwa au Ninaumwa Sana, Lakini ni Karaha Kusema Hivyo kwa Kukata Tamaa

06-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kuruhusiwa Mgonjwa Kusema: Ninaumwa au Ninaumwa Sana, Lakini ni Karaha Kusema Hivyo kwa Kukata Tamaa

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب جواز قول المريض : أنَا وجع ، أَوْ شديد الوجع

أَوْ مَوْعُوكٌ أَوْ وارأساه ونحو ذلك . وبيان أنَّه لا كراهة في ذلك

إِذَا لَمْ يكن عَلَى سبيل التسخط وإظهار الجزع

06-Mlango Wa Kuruhusiwa Mgonjwa Kusema: Ninaumwa au Ninaumwa Sana, Lakini ni Karaha Kusema Hivyo kwa Kukata Tamaa

 

Alhidaaya.com [1]

 

 

Hadiyth – 1

عن ابن مسعود رضي الله عنه ، قَالَ : دَخَلْتُ عَلَى النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم وَهُوَ يُوعَكُ ، فَمَسسْتُهُ ، فَقلتُ : إنَّكَ لَتُوعَكُ وَعَكاً شَديداً ، فَقَالَ : (( أجَلْ ، إنِّي أُوعَكُ كَمَا يُوعَكُ رَجُلانِ مِنْكُمْ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba, nilimzuru Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wakati alipokuwa na homa, nikamwambia: "Ee Rasuli wa Allaah! Hakika wewe una homa kali." Akasema: "Ndio, mimi huumwa kwa maumivu yaliyo sawa na watu wawili miongoni mwenu." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 2

وعن سعدِ بن أَبي وقاصٍ رضي الله عنه ، قَالَ : جَاءني رسولُ الله صلى الله عليه وسلم يَعُودُنِي مِنْ وَجَعٍ اشْتَدَّ بِي ، فقلتُ: بَلَغَ بِي مَا تَرَى ، وَأنَا ذُو مَالٍ ، وَلاَ يَرِثُنِي إِلاَّ ابْنَتِي .. وذَكر الحديث . متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Sa'd bin Waqqaas amesema kwamba: "Alikuja kunizuru mimi Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) nikiwa mgonjwa sana." Nikamwambia: "Ee Rasuli wa Allaah! Umenifikia mimi ugonjwa huu kama unavyoniona na mimi ni tajiri na hakuna anayenirithi isipokuwa binti yangu mmoja"... Na akaitaja Hadiyth. [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 3

وعن القاسم بن محمد، قَالَ : قالت عائشةُ رضي الله عنها : وَارَأسَاهُ ! فَقَالَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم : (( بَلْ أنَا ، وَارَأسَاهُ ! )) ... وذكر الحديث . رواه البخاري .

Na imepokewa kutoka kwa Al-Qaasim bin Muhammad kwamba 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) alisema: "Ah, kichwa changu." Hapo Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Bali, ni kichwa changu"... Na akaitaja Hadiyth. [Al-Bukhaariy]

 

 

 

Share [2]
www.alhidaaya.com

Source URL: https://www.alhidaaya.com/sw/node/11054

Links
[1] http://www.alhidaaya.com/
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11054&title=06-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kuruhusiwa%20Mgonjwa%20Kusema%3A%20Ninaumwa%20au%20Ninaumwa%20Sana%2C%20Lakini%20ni%20Karaha%20Kusema%20Hivyo%20kwa%20Kukata%20Tamaa