كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji
Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
Abu Maalik Kamaal Bin As-Sayyid Saalim
Imetarjumiwa na 'Abdullaah Mu'aawiyah (Abu Baasim)
Alhidaaya.com
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
Taarifu Ya Vyakula
Alhidaaya.com [3]
· Taarifu Ya Vyakula
"الأَطْعِمَةُ" ni wingi wa "طَعَامُ", na katika lugha ni kila kile kinacholiwa, na pia kila kinachotumika kama chakula kutokana na ngano, shayiri na tende. Kinaingia ndani ya taarifu hii kila kinachozalishwa na ardhi kati ya mimea ya mazao na matunda, na pia wanyama wote wanaoliwa, ni sawa wa nchi kavu au wa baharini.
Fuqahaa wanatumia tamko la chakula "الأَطْعِمَةُ" kwa kila kinacholiwa na kila kinachonywewa, ni sawa yakiwa maji au vilevi.
Na maudhui ya vyakula ni anuani inayogusia vilivyo halali kuliwa, vilivyo makruhu, na vilivyoharamishwa.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
Alhidaaya.com [3]
· Asili Ya Vyakula Vyote Ni Halali Mpaka Iwepo Dalili Ya Kuharamisha
1- Allaah Amesema:
"هُوَ الَّذِي خَلَقَ لَكُم مَّا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا"
“Yeye Ndiye Ambaye Amekuumbieni vyote vilivyomo ardhini”. [Al-Baqarah: 29].
2- Amesema tena:
"يَا أَيُّهَا النَّاسُ كُلُوا مِمَّا فِي الْأَرْضِ حَلَالًا طَيِّبًا"
“Enyi watu! Kuleni katika vilivyomo ardhini vya halali, vizuri.” [Al-Baqarah: 168].
3- Na Amesema pia:
"وَكُلُوا وَاشْرَبُوا وَلَا تُسْرِفُوا ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُسْرِفِينَ • قُلْ مَنْ حَرَّمَ زِينَةَ اللَّـهِ الَّتِي أَخْرَجَ لِعِبَادِهِ وَالطَّيِّبَاتِ مِنَ الرِّزْقِ ۚ قُلْ هِيَ لِلَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا خَالِصَةً يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ كَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ"
“Na kuleni na kunyweni na wala msifanye israfu. Hakika Yeye (Allaah) Hapendi wanaofanya israfu • Sema: Nani aliyeharamisha Mapambo ya Allaah ambayo Amewatolea Waja Wake na vilivyo vizuri katika riziki? Sema: Hivyo ni kwa ajili ya wale walioamini katika uhai wa dunia; makhsusi (kwa Waumini) Siku ya Qiyaamah. Hivyo ndivyo Tunavyofasili waziwazi Aayaat kwa watu wanaojua”. [Al-A’araaf: 31, 32].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
Alhidaaya.com [3]
003-Hakiharamishwi Chakula Chochote Ila Kile Tu Alichokiharamisha Allaah Katika Kitabu Chake Au Kupitia Ulimi Wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
1- Allaah Amesema:
"وَمَا لَكُمْ أَلَّا تَأْكُلُوا مِمَّا ذُكِرَ اسْمُ اللَّـهِ عَلَيْهِ وَقَدْ فَصَّلَ لَكُم مَّا حَرَّمَ عَلَيْكُمْ إِلَّا مَا اضْطُرِرْتُمْ إِلَيْهِ ۗ وَإِنَّ كَثِيرًا لَّيُضِلُّونَ بِأَهْوَائِهِم بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِالْمُعْتَدِينَ" ﴿١١٩﴾
“Na mna nini hata msile katika ambavyo limetajwa Jina la Allaah na ilhali Ameshafasilisha waziwazi kwenu yale Aliyokuharamishieni isipokuwa vile mlivyofikwa na dharura navyo. Na hakika wengi wanapotoa (wengine) kwa hawaa zao bila ya elimu. Hakika Rabb wako Yeye Anajua Zaidi wenye kutaadi.” [Al-An’aam: 119].
2- Allaah Ta’aalaa Amesema:
"قُلْ أَرَأَيْتُم مَّا أَنزَلَ اللَّـهُ لَكُم مِّن رِّزْقٍ فَجَعَلْتُم مِّنْهُ حَرَامًا وَحَلَالًا قُلْ آللَّـهُ أَذِنَ لَكُمْ ۖ أَمْ عَلَى اللَّـهِ تَفْتَرُونَ ﴿٥٩﴾ وَمَا ظَنُّ الَّذِينَ يَفْتَرُونَ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَذُو فَضْلٍ عَلَى النَّاسِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَشْكُرُونَ"﴿٦٠﴾
59. Sema: Mnaonaje zile riziki Alizokuteremshieni Allaah, kisha mkazifanya katika hizo ni haramu na halali? Sema: Je, Allaah Amekupeni idhini au mnamtungia (uongo) Allaah? • 60. Na nini dhana ya wale wanaomtungia Allaah uongo Siku ya Qiyaamah? Hakika Allaah bila shaka Ana fadhila (nyingi) juu ya watu, lakini wengi wao hawashukuru”. [Yuwnus: 59, 60].
3- Na Akasema:
"وَلَا تَقُولُوا لِمَا تَصِفُ أَلْسِنَتُكُمُ الْكَذِبَ هَـٰذَا حَلَالٌ وَهَـٰذَا حَرَامٌ لِّتَفْتَرُوا عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ ۚ إِنَّ الَّذِينَ يَفْتَرُونَ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ لَا يُفْلِحُونَ"﴿١١٦﴾
116. “Na wala msiseme kwa ndimi zenu zinazopambia uongo: Hii halali na hii haramu ili mumtungie Allaah uongo. Hakika wale wanaomtungia Allaah uongo hawafaulu”. [An-Nahl: 116].
4- Na Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إِنَّ أَعْظَمَ الْمُسْلِمِينَ فِي الْمُسْلِمِينَ جُرْمًا مَنْ سَأَلَ عَنْ شَىْءٍ لَمْ يُحَرَّمْ عَلَى الْمُسْلِمِينَ فَحُرِّمَ عَلَيْهِمْ مِنْ أَجْلِ مَسْأَلَتِهِ"
“Hakika Muislamu anayewafanyia Waislamu kosa kubwa zaidi, ni yule mwenye kuuliza kitu ambacho hakikuharamishwa kwa Waislamu, halafu wakaharamishiwa kwa sababu ya kuuliza kwake”. [Hadiyth Swahiyh. [Imekharijiwa na Muslim (2358)].
5- Na toka kwa Abu Hurayrah kwamba Nabiy (Swalla Allaah 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"ذَرُونِي مَا تَرَكْتُكُمْ فَإِنَّمَا هَلَكَ مَنْ كَانَ قَبْلَكُمْ بِسُؤَالِهِمْ وَاخْتِلاَفِهِمْ عَلَى أَنْبِيَائِهِمْ فَإِذَا أَمَرْتُكُمْ بِشَىْءٍ فَخُذُوا مِنْهُ مَا اسْتَطَعْتُمْ وَإِذَا نَهَيْتُكُمْ عَنْ شَىْءٍ فَانْتَهُوا"
“Niacheni kama nilivyokuacheni (msiniulize viswali visivyo na umuhimu), kwani hakika waliangamia waliopita kabla yenu kwa sababu ya maswali yao mengi na kwenda kwao kinyume dhidi ya Manabii wao. Hivyo, nikiwaamuruni jambo, basi lifanyeni kiasi cha uwezo wenu, na nikiwakatazeni jambo, basi liacheni”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (7288) na Muslim (1337)].
6- Toka kwa Abud Dardaai ikiwa Marfuw’u:
"مَا أَحَلَّ اللَّهُ فِي كِتَابِهِ فَهُوَ حَلاَلٌ ، وَمَا حَرَّمَ فَهُوَ حَرَامٌ، وَمَا سَكَتَ عَنْهُ فَهُوَ عَافِيَةُ ، فإنً اللهَ لَمْ يَكُنْ نَسِيًّا ، ثُمً تَلاَ هذِهِ الآيَةِ: وَمَا كَانَ رَبُّكَ نَسِيًّا"
“Alilohalalisha Allaah katika Kitabu Chake, basi hilo ni halali, na Aliloharamisha basi hilo ni haramu, na Alilolinyamazia, basi hilo ni msamaha Amekuachilieni, kwani Allaah haiwezekani Akawa Mwenye Kusahau. Kisha Akasoma Aayah hii: “Na Rabb wako Si Mwenye Kusahau kamwe. [Maryam: 64]. [Hadiyth Hasan. Imekharijiwa na Al-Haakim (2/406) na Ad-Daaraqutwniy (2/137). Ina Hadiyth wenza. Angalia Jaami’ul ‘Uluwmi wal Hikam (1/276)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
Alhidaaya.com [3]
004-Je, Mnyama Ambaye Hakutajwa Kwenye Qur-aan Au Hadiyth Za Rasuli, Na Waarabu Wakamwona Mbaya Hafai Kuliwa, Je Litazingatiwa Hilo?
· Je, Mnyama Ambaye Hakutajwa Kwenye Qur-aan Au Hadiyth Za Rasuli, Na Waarabu Wakamwona Mbaya Hafai Kuliwa, Je Litazingatiwa Hilo? [Al-Mughniy (8/585), Ibn ‘Aabidiyna (5/194) na Matwaalibu Ulin Nuhaa (6/311)].
Ikiwa katika Qur-aan au Sunnah hakuna naswi idulishayo uhalali au uharamu wa mnyama fulani, baadhi ya ‘Ulamaa wamesema kwamba itabidi turudi kwa Waarabu. Kama Waarabu watamwona mnyama huyo ni mzuri analika, basi atakuwa halali, na kama watamwona mbaya hafai kuliwa, basi atakuwa ni haramu. Na hii ni kutokana na Neno Lake Ta’aalaa:
"وَيُحِلُّ لَهُمُ الطَّيِّبَاتِ وَيُحَرِّمُ عَلَيْهِمُ الْخَبَائِثَ"
“Na anawahalalishia vilivyo vizuri na anawaharamishia vilivyo vibaya. [Al-A’araaf: 157].
Ibn Qudaamah (Rahimahul Laah) akiizungumzia maana ya Aayah hii amesema:
“Yaani, mnyama ambaye Waarabu wanamwona kuwa mzuri na anafaa kuliwa, basi huyo ni halali, na yule wanayemwona kuwa mbaya hafai kuliwa, basi huyo ni haramu. Na Waarabu ambao kipimo chao cha kumwona mnyama huyu anafaa na kuwa mwingine hafai na ambacho kinazingatiwa, ni watu wa Al-Hijaaz, watu waishio kwenye miji. Kwa kuwa hawa ndio ambao Qur-aan Kariym iliteremka kwao na maneno yake yakaelekezwa kwao pamoja na Sunnah ya Nabiy. Hivyo matamshi yake mengi yanarejea kwenye ada na desturi zao zaidi kuliko watu wengineo”.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
Alhidaaya.com [3]
005- Sababu Ya Kuharamishwa Baadhi Ya Vyakula Na Vinywaji
· Sababu Ya Kuharamishwa Baadhi Ya Vyakula Na Vinywaji
[Al-Mughniy (8/585), Ibn ‘Aabidiyna (5/194) na Matwaalibu Ulin Nuhaa (6/311)].
Kwa upembuzi na ufuatiliaji wa karibu wa sababu zilizotolewa na Fuqahaa katika vile walivyovihukumu kuwa ni haramu kuliwa, tunakuta kwamba ni haramu kula chochote, vyovyote iwavyo aina yake, kwa moja ya sababu hizi tano zifuatazo:
1- Kiwe kinasababisha madhara kwa mwili au akili. Allaah Amesema:
"وَلَا تَقْتُلُوا أَنفُسَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِكُمْ رَحِيمًا"
“Wala msijiue. Hakika Allaah Ni Mwenye Kuwarehemuni”. [An-Nisaa: 29].
2- Kiwe kinalewesha, au kinaondosha hisia au kinalaza. Ni haramu kutumia vilevi vyenye kuondosha akili kama pombe na tembo, au mada zote zenye kuondosha hisia na kujitambua kama hashishi, afyuni na mfano wake.
3- Kiwe najisi. Ni haramu kila kilicho najisi au kilichonajisika kwa najisi isiyosameheka.
4- Chenye kuonekana kinyaa na kuhisika kichafu kwa watu wenye maumbile yaliyo salama. Ni kama kinyesi, mkojo, chawa na kiroboto.
5- Kutopata ruksa ya kisharia kama ni mali ya mtu mwingine. Ni haramu mtu kula chakula kisicho chake bila idhini ya mwenyewe au Idhini ya Allaah. Ni kama chakula cha kupora na kuiba, au kilichopatikana kwa njia ya kamari, ukahaba na mfano wa hayo.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
Alhidaaya.com [3]
006-Vyakula Vilivyoharamishwa Na Kitabu Cha Allaah Mfu (01)
Vyakula Vilivyoharamishwa Na Kitabu Cha Allaah Mfu (01)
Allaah Ta’aalaa Amesema:
"حُرِّمَتْ عَلَيْكُمُ الْمَيْتَةُ وَالدَّمُ وَلَحْمُ الْخِنزِيرِ وَمَا أُهِلَّ لِغَيْرِ اللَّـهِ بِهِ وَالْمُنْخَنِقَةُ وَالْمَوْقُوذَةُ وَالْمُتَرَدِّيَةُ وَالنَّطِيحَةُ وَمَا أَكَلَ السَّبُعُ إِلَّا مَا ذَكَّيْتُمْ وَمَا ذُبِحَ عَلَى النُّصُبِ"
03: “Mmeharamishiwa nyamafu, na damu, na nyama ya nguruwe, na kilichotajiwa asiyekuwa Allaah katika kuchinjwa kwake, na (pia) mnyama aliyekufa kwa kukosa hewa au aliyepigwa akafa, au aliyeporomoka toka juu, au aliyepigwa pembe, na aliyeliwa na mnyama mwitu, isipokuwa mliyewahi kumchinja kihalali (kabla ya kufa), na waliochinjwa kwa ajili ya ‘ibaadah ya waabudiwa”. [Al-Maaidah: 03].
Aayah hii imetaja kwa mpangilio baadhi ya vilivyoharamishwa ambavyo ni:
Cha Kwanza:
Mnyama mfu. Naye ni kila mnyama aliyejifia mwenyewe tu bila kuuliwa au kwa chinjo la kisharia. Nao ni:
(a) "الْمُنْخَنِقَةُ". : Ni mnyama aliyenyongwa au kufungiwa sehemu isiyo na hewa akafa.
(b) "الْمَوْقُوْذَةُ" : Ni mnyama aliyepigwa kwa fimbo au mfano wake akafa.
(c) "الْمُتَرَدِّيَةُ" : Ni mnyama aliyeanguka toka sehemu ya juu akafa.
(d) "النَّطِيْحَةُ" : Ni mnyama aliyepigwa pembe na mwenzake akafa kutokana na pigo hilo.
(e) " مَا أَكَلَ السَّبُعُ" : Ni mnyama aliyekufa kwa kujeruhiwa na mnyama mkali na akamla sehemu.
Mnyama yeyote kati ya hawa akiwahiwa kabla hajafa akachinjwa, basi anakuwa ni halali. Ni kwa Neno Lake Ta’aalaa:
"إِلَّا مَا ذَكَّيْتُمْ"
“Isipokuwa mliyewahi kumchinja kihalali (kabla ya kufa)”. [Al-Maaidah: 03].
· Sehemu Ya Mnyama Iliyokatwa Akiwa Hai Inaingia Kwenye Duara La Mfu.
Ni kwa neno la Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"مَا قُطِعَ مِنَ الْبَهِيْمَةِ وَهِيَ حَيَّةٌ فَهُوَ مَيْتَةٌ"
“Kipande (cha nyama) kilichokatwa cha mnyama aliye hai, basi hicho ni mfu”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (2841) na Ibn Maajah (3216)].
Na kwa msingi huu, haifai kula kipande cha kiungo cha mnyama aliye hai.
· Mfu Anayetoka Nje Ya Duara La Uharamu
Kila mtu anajua kwamba ni haramu kula mfu kwa aina zake zote. Lakini Hadiyth ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) imewatoa wafu wawili toka kwenye wigo wa uharamu na kuwaingiza ndani ya duara la uhalali wa kuliwa. Wafu hao ni samaki na nzige. Na hii ni kutokana na Hadiyth iliyopokelewa na Ibn ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) toka kwa Rasuli aliyesema:
"أُحِلَّتْ لَنَا مَيْتَتَانِ وَدَمَانِ: أَمَّا الْمَيْتَتَانِ: فالْحُوْتُ وَالْجَرَادُ ، وَأَمَّا الدَّمَانِ: فَالْكَبِدُ وَالطِّحَالُ"
“Tumehalalishiwa maiti mbili na damu mbili. Ama maiti mbili, ni samaki na nzige. Ama damu mbili, ni ini na wengu”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Ibn Maajah (3314), Ahmad (5690) na wengineo. Angalia As-Swahiyhah (1118). Hadiyth hii ina hukmu ya Raf-‘u].
· Faida Mbili:
Faida Ya Kwanza:
Hukmu Ya Kula Chenye Kuelea Juu Ya Maji Kama Samaki Au Wanyama Wengineo Wa Baharini.
‘Ulamaa wana kauli mbili kuhusu hili:
[Al-Badaai’u (5/35), Al-Muhallaa (7/393), Al-Mughniy (9/35) na Naylul Awtwaar (8/170)].
Kauli Ya Kwanza:
Ni halali kula. Ni madhehebu ya Maalik, Ash-Shaafi’iy, Ahmad, Adh-Dhwaahiriyyah, ‘Atwaa, Mak-huwl, An-Nakh-’iy na Abu Thawr. Ni kauli iliyosimuliwa toka kwa Abu Bakr na Abu Ayyuwb (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa).
Dalili zao ni:
1- Neno Lake Ta’aalaa:
"وَمَا يَسْتَوِي الْبَحْرَانِ هَـٰذَا عَذْبٌ فُرَاتٌ سَائِغٌ شَرَابُهُ وَهَـٰذَا مِلْحٌ أُجَاجٌ ۖ وَمِنْ كُلٍّ تَأْكُلُونَ لَحْمًا طَرِيًّا"
“Na bahari mbili hazilingani sawa; haya ni (maji) matamu ladha yake, yenye kukata kiu, anisi kinywaji chake, na haya ni ya chumvi kali. Na katika kila moja mnakula nyama laini safi”. [Faatwir: 12].
2- Neno Lake Ta’aalaa:
"أُحِلَّ لَكُمْ صَيْدُ الْبَحْرِ وَطَعَامُهُ مَتَاعًا لَّكُمْ وَلِلسَّيَّارَةِ"
“Mmehalalishiwa mawindo ya bahari, na chakula chake ni manufaa kwenu na kwa wasafiri”. [Al-Maaidah: 96].
Ibn ‘Abbaas na wengineo wamesema: “Mawindo yake ni kile mlichokivua, na chakula chake ni kile kilichotupwa nje (ya maji)”.
Aayah hizi mbili kwa ujumla wake zinaashiria uhalali wa mawindo yote ya baharini na vinavyovuliwa toka humo, na Allaah Ta’aalaa Hakukihusisha au kuainisha chochote katika hivi kuwa hiki ni halali na kingine si halali.
"وَمَا كَانَ رَبُّكَ نَسِيًّا"
“Na Rabb wako Si Mwenye Kusahau kamwe”. [Maryam: 64].
3- Ni kutokana na ujumuishi wa kauli yake Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wakati alipoulizwa kuhusu maji ya bahari pale alipojibu akisema:
"هُوَ الطَّهُورُ مَاؤُهُ الْحَلاَلُ مَيْتَتُهُ"
“Bahari maji yake ni twahara, na maiti yake ni halali”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (83), At-Tirmidhiy (69) na An-Nasaaiy (1/176)].
Hii inajumuisha vyote vilivyofia baharini kwa aina zake zote.
4- Kuhusiana na vilivyotolewa nje ya duara la mfu, Ibn ‘Umar (akitumia Hadiyth ya Rasuli) anasema:
" أُحِلَّتْ لَنَا مَيْتَتَانِ …الْحُوْتُ وَالْجَرَادُ "
“Tumehalalishiwa mfu mbili … samaki na nzige.” [Hadiyth Swahiyh. Imetajwa nyuma kidogo].
5- (Kauli ya Ibn ‘Umar) inatiliwa nguvu na Hadiyth ya Jaabir aliyesema:
"أنً الْبَحْرَ قَذَفَ إِلَى السًاحِلِ بِدَابًةٍ ضَخْمَةٍ تُدْعَى العَنْبَرُ ، فَأكَلُوْا مِنْهَا ، وَلَمًا قَدِمُوْا إلَى المدِيْنَةِ سَألُوْا رَسُوْلَ اللهِ صَلًى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلًمَ عَنْهَا ، فَقَالَ: "هُوَ رِزْقٌ أَخْرَجَهُ اللهُ لَكُمْ ، فَهَلْ مَعَكُمْ مِنْ لَحْمِهِ شَيْئًا فَتُطْعِمُوْنَا؟" قَالَ جَابِرٌ: فَأَرْسَلْنَا إِلَى رَسُوْلِ اللهِ صَلًى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلًمَ مِنْهُ فَأَكَلَهُ".
“Kwamba bahari ilitema ufukweni samaki mkubwa sana aitwaye anbar, na watu wakamla sehemu. Walipofika Madiynah, walimuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu kumla kwao samaki huyo, na Rasuli akawaambia: “Huyo ni rizki ambayo Allaah Amewatoleeni. Je, mna nyama yake kidogo mkatupa na sisi tukala?” Jaabir anasema: Tukampelekea Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) sehemu ya nyama hiyo naye akaila”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (4362), Muslim (1935) na Ibn Maajah].
Kauli Ya Pili:
Si halali kumla samaki au mnyama wa baharini anayeelea. Ni kauli ya Abu Haniyfah na maswahibu zake. Dalili zao ni:
1- Hadiyth Marfuw’u iliyosimuliwa na Jaabir isemayo:
"مَا أَلْقَاهُ الْبَحْرُ أَوْ جَزَرَ عَنْهُ فَكُلُوْهُ ، وَمَا مَاتَ فِيْهِ فَطَافَ فَلَا تَأْكُلُوْهُ"
“Kilichotemwa na bahari, au ilichokiacha baada ya kupwa, basi kileni, na kilichofia humo kikaelea, basi msikile”. [Hadiyth Dhwa’iyf. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (3815) na Ibn Maajah].
Dalili hii imejibiwa kwa jibu lisemalo kuwa Hadiyth hii ni Dhwa’iyf kwa makubaliano ya wabobezi wa Hadiyth.
2- Baadhi ya aathaar toka kwa Jaabir, ‘Aliy, na Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaah ‘anhum) zinazokataza kula chenye kuelea, na zote ni dhwa’iyf. [Angalia Al-Muhallaa cha Ibn Hazm (7/394)].
Kauli Yenye Nguvu:
Hakuna shaka yoyote kwamba dalili za Jumhuwr ndizo zenye nguvu zaidi. Lakini, ikiwa itathibiti kitiba kwamba samaki anayeelea anakuwa ameharibika na anaweza kuleta madhara kwa mwili na hususan ikiwa umepita muda baada ya kufa, basi hapo, kutomla kutaendana vizuri zaidi na qawaaid za sharia zilizoharamisha vibaya vyenye madhara. Allaah Ndiye Ajuaye zaidi.
Faida Ya Pili:
‘Ulamaa wamekhitilafiana kuhusu kula nzige
[Al-Majmuw’u (9/24), Al-Mughniy (9/315), na Subulus Salaam (4/1390)].
Jamaahiyr ya ‘Ulamaa kati ya watangu wema na waliowafuatia –kinyume na Maalik- wanasema nzige ni halali, ni sawa akiwa amekufa kwa kuwindwa au kwa kujifia tu mwenyewe. Na hii ni kwa dalili zifuatazo:
1- Ni kauli iliyotangulia ya Ibn ‘Umar:
" أُحِلَّتْ لَنَا مَيْتَتَانِ …الْحُوتُ وَالْجَرَادُ "
“Tumehalalishiwa nyamafu mbili … samaki na nzige.”
2- Ni Hadiyth ya ‘Abdullaah bin Abiy Awfaa:
"غَزَوْنَا مَعَ رَسُوْلِ اللهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلًمَ سَبْعَ غَزَوَاتٍ نَأْكُلُ الْجَرَادَ"
“Tulipigana vita saba tukiwa pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) huku tunakula nzige”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5495) na Muslim (1952)].
Maalik (Rahimahul Laah) ameshurutisha kwamba ili nzige awezekanike kuliwa ni kuwa afe kutokana na sababu, nayo ni ima akatwe sehemu ya mwili wake, au achemshwe, au akaangwe akiwa hai au achomwe. Ama akijifia hivi tu mwenyewe, basi hafai kuliwa!!
Kauli ya kwanza ndio yenye nguvu zaidi. Allaah Ndiye Ajuaye zaidi.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
Alhidaaya.com [3]
007- Vilivyoharamishwa Na Kitabu Cha Allaah:
Damu Ya Mnyama Aliyechinjwa (02)
2- Damu Ya Mnyama Aliyechinjwa
Si halali kula au kunywa damu ya mnyama aliyechinjwa. Ni kwa Neno Lake Ta’aalaa:
"حُرِّمَتْ عَلَيْكُمُ الْمَيْتَةُ وَالدَّمُ"
“Mmeharamishiwa nyamafu, na damu”. [Al-Maaidah: 03].
Ama damu kidogo kama ile inayobaki ndani ya mishipa ya mnyama aliyechinjwa ambayo ni vigumu kuepukana nayo, damu hii inasamehewa.
· Damu Iliyo Nje Ya Duara La Uharamu
Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
" أُحِلَّتْ لَنَا مَيْتَتَانِ وَدَمَانِ: ...... وَأَمَّا الدَّمَانِ: فالْكَبِدُ وَالطِّحَالُ "
“Tumehalalishiwa maiti mbili na damu mbili… na ama damu mbili, basi ni ini na wengu. [Hadiyth Swahiyh. Imepita nyuma kidogo].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
Alhidaaya.com [3]
008- Vyakula Vilivyoharamishwa Na Kitabu Cha Allaah (08): Nyama Ya Nguruwe (03)
3- Nyama Ya Nguruwe
Allaah Ta’aalaa Amesema:
"حُرِّمَتْ عَلَيْكُمُ الْمَيْتَةُ وَالدَّمُ وَلَحْمُ الْخِنزِيرِ"
“Mmeharamishiwa nyamafu, na damu, na nyama ya nguruwe”. [Al-Maaidah: 03].
Na Amesema tena ‘Azza wa Jalla:
"قُل لَّا أَجِدُ فِي مَا أُوحِيَ إِلَيَّ مُحَرَّمًا عَلَىٰ طَاعِمٍ يَطْعَمُهُ إِلَّا أَنْ يَكُوْنَ مَيْتَةً أَوْ دَمًا مَّسْفُوْحًا أَوْ لَحْمَ خِنزِيرٍ فَإِنَّهُ رِجْسٌ"
“Sema: Sipati katika yale niliyofunuliwa Wahyi kwangu kilichoharamishwa kwa mlaji kukila isipokuwa kiwe ni nyamafu, au damu inayomwagika, au nyama ya nguruwe, kwani hiyo ni chafu yenye madhara”. [Al-An’aam: 145].
Hakuna makhitilifiano yoyote kati ya ‘Ulamaa kuhusiana na kuharamishwa nguruwe kuanzia nyama yake, shahamu (mafuta) yake na sehemu zake zote. Nyama yake imetajwa mahususi katika Aayah kwa kuwa ndio sehemu kubwa inayoliwa ya mnyama, ama sehemu nyinginezo, hizo ni kama vifuatilizi tu. Kadhalika, imetajwa mahususi ili kuweka wazi ubaya na uharamu wa nyama hii ambayo baadhi ya watu wanaiona kuwa ni nzuri na bora zaidi kuliko nyama nyinginezo zote bila kujali uzito wa katazo la Allaah.
Na kiwakilishi nomino katika Kauli Yake Ta’aalaa:
"أَوْ لَحْمَ خِنزِيْرٍ فَإِنَّهُ رِجْسٌ"
“au nyama ya nguruwe, kwani hiyo ni chafu yenye madhara”, kwa mujibu wa Lugha ya Kiarabu ambayo Qur-aan imeshuka kwayo, kinarejelea kitajwa kilicho karibu zaidi nacho, naye ni nguruwe mwenyewe. Na kwa matamshi haya bayana ya Qur-aan hii, nguruwe kwa kiini chake ni mchafu asiyefaa kuliwa, na yeye wote mzima ni najisi, na najisi ni haramu ambayo ni lazima kuiepuka. Hivyo basi, nguruwe kwa ujumla wake wote ni haramu, haitolewi hata nywele yake au kingine chake chochote kikawa ni halali.
· Faida:
Mwandishi wa Tafsiyrul Manaar (2/98) amesema katika kubainisha hikma ya sharia katika kuharamisha nguruwe:
“Allaah Ameharamisha nyama ya nguruwe kwa kuwa ni chafu isiyo salama, na hii ni kwa vile chakula anachokipenda zaidi nguruwe ni taka, vinyesi na najisi. Nyama hii ina madhara kwenye nchi zote kama ilivyothibiti kwa njia ya majaribio. Kula nyama yake ni katika sababu za kupatwa na minyoo hatari inayoua. Na inasemekana pia kuwa nyama yake ina athari hasi na mbaya kwa tabia takasifu na wivu wa mtu kwa mkewe na banati zake”.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
Alhidaaya.com [3]
009-Vyakula Vilivyoharamishwa Na Kitabu Cha Allaah:
Kilichotajiwa Asiyekuwa Allaah Wakati Wa Kuchinjwa
4- Kilichotajiwa Asiyekuwa Allaah Wakati Wa Kuchinjwa
Ni kwa Neno Lake Ta’aalaa:
"حُرِّمَتْ عَلَيْكُمُ الْمَيْتَةُ وَالدَّمُ وَلَحْمُ الْخِنزِيْرِ وَمَا أُهِلَّ لِغَيْرِ اللَّـهِ بِهِ"
“Mmeharamishiwa nyamafu, na damu, na nyama ya nguruwe, na kilichotajiwa asiyekuwa Allaah katika kuchinjwa kwake”. [Al-Maaidah: 03].
Na Neno Lake ‘Azza wa Jalla:
"وَلَا تَأْكُلُوا مِمَّا لَمْ يُذْكَرِ اسْمُ اللَّـهِ عَلَيْهِ وَإِنَّهُ لَفِسْقٌ"
“Na wala msile katika ambavyo halikutajwa Jina la Allaah (wakati wa kuchinjwa), kwani huo ni ukiukaji wa utiifu kwa Allaah”. [Al-An’aam : 121].
Na kwa ajili hiyo, haifai kula mnyama aliyechinjwa na mshirikina, au mmajusi au aliyeritadi. Ama mnyama aliyechinjwa na Mnaswara au Myahudi, huyo inajuzu kumla madhali haikujulikana kwamba amechinjwa kwa kutajwa Jina lisilo la Allaah. Na hii ni kwa Neno Lake Ta’aalaa:
"وَطَعَامُ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ حِلٌّ لَّكُمْ"
“Na nyama iliyochinjwa na waliopewa Kitabu ni halali kwenu”. [Al-Maaidah: 05].
Faida Mbili:
Ya Kwanza: Nyama Zinazoagizwa Toka Nchi Zisizo Za Kiislam
Ikiwa zinazoagizwa toka nchi zisizo za Kiislamu ni nyama za wanyama wa bahari kama samaki na nyangumi, basi hizo ni halali kula, kwa kuwa hata bila kuchinjwa (chinjo la kisharia) ni halali, ni sawa akiwa aliyewavua ni Muislamu au asiye Muislamu.
Ama zikiwa ni za wanyama wa nchi kavu ambao ni halali kuliwa kama ngamia, ng’ombe, mbuzi, kondoo na ndege, na zikawa zimeagizwa toka nchi ambazo wakazi wake ni wamajusi, au mapagani, au wenye kukanusha kuwepo kwa Allaah kama Wakomunisti, basi nyama hizi hazifai kuliwa.
Na ama zikiagizwa toka nchi ambazo wakazi wake ni Manaswara au Mayahudi (Watu wa Kitabu), basi zinafaa kuliwa lakini kwa masharti mawili:
La kwanza:
Isijulikane kwamba wao walimelitaja jina la asiye Allaah wakati wa kuchinja kama msalaba au masihi na kadhalika.
La pili:
Mnyama achinjwe chinjo la kisharia kwa namna ambayo itakuja kubainishwa mbeleni.
“Katika miaka iliyopita, kwa hakika, ilikuwa tunatosheka kudai nchi hizi zinazosafirisha nyama kwetu kwamba zinachinja kwa mujibu wa sharia ya Kiislamu. Lakini ikaja kugundulika kwa njia mbalimbali kwamba nchi hizi hazichinji chinjo la kisharia, na kwamba muhuri unaotiwa juu ya nyama hizi kuonyesha kwamba zimechinjwa kwa mujibu wa sharia ya Kiislamu, si lolote bali ni utapeli wa kula mali za Waislamu kwa njia haramu. Shehena za kuku walioagizwa toka nje zishawahi kuwasili katika baadhi ya nchi za Kiarabu na kukutwa shingo ya kuku ikiwa nzima na kamili kabisa bila athari yoyote ya chinjo, pamoja na kuandikwa juu yake maneno ya kijadi ya kuwa “Zimechinjwa chinjo la Kiislamu!! Bali hata wamefikia kuzichezea akili za Waislamu kwa kukutwa maboksi ya samaki walioagizwa toka nchi hizo yakiwa yameandikwa juu yake: “Samaki hawa wamechinjwa kwa mujibu wa sharia ya Kiislamu!!” [Al-Fiqhul Waadhwih cha Dk. Muhammad Bakr Ismaa’iyl (2/390 – 395)].
Ya Pili: Jibini Zinazoagizwa Toka Nchi Zisizo Za Kiislamu
[Al-Mufas-swal cha ‘Abdul Kariym Zaydaan (3 / 54-55)]
Ikiwa jibini zinaagizwa toka nchi za Watu wa Kitabu na wao wanazitengeneza kutokana na “rennet” za wanyama ambao ni halali sisi kuwala, basi jibini hizi ni halali kwetu.
Ama ikiwa zinaagizwa toka nchi za wamajusi au wasoshalisti au waabudu masanamu, na wao wanatengeneza jibini hizo kutokana na “rennet” za wanyama wao waliowachinja, basi wanyama hawa kwa upande wa Waislamu ni kama mzoga.
Lakini je, ni halali kula jibini hizi zilizotengenezwa kutokana na “rennet” za mizoga hii?
Sheikh wa Uislamu (Allaah Amrehemu) amesema kuhusiana na jibini za wamajusi zilizotengenezwa kutokana na “rennet” za vichinjwa vyao kwamba kuna kauli mbili za ‘Ulamaa. Kisha akasema: “Lenye kigezo cha nguvu zaidi ni kwamba jibini zao ni halali, na kwamba “rennet” za mfu na maziwa yake ni twahara, kwa vile Maswahaba walipoiteka Iraki walikula jibini za wamajusi, na hili lilikuwa liko wazi limeenea baina yao”. [Majmuw’ul-Fataawaa (21/102 – 103)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
Alhidaaya.com [3]
Vyakula Vilivyoharamishwa Na Kitabu Cha Allaah
Kilichochinjwa Kwa Ajili Ya Asiye Allaah
5- Kilichochinjwa Kwa Ajili Ya Asiye Allaah
Ni kama sanamu, au kiumbe, au kaburi, au maiti kama vile Sayyid Badawiy (Misri) au vinginevyo katika “matwaaghuwtw” (kila kiabudiachwo badala ya Allaah kama watu waliojivika uungu, mashaytwaan na kadhalika).
Na hii ni kwa Neno Lake Ta’aalaa:
"وَمَا ذُبِحَ عَلَى النُّصُبِ"
“Na waliochinjwa kwa ajili ya ‘ibaadah ya waabudiwa”. [Al-Maaidah: 03].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
Alhidaaya.com [3]
011-Vyakula Vilivyoharamishwa Na Hadiyth Za Rasuli
Nyama Ya Punda Wa Mjini
Vilivyoharamishwa Na Hadiyth Za Rasuli
1- Nyama Ya Punda Wa Mjini
Jumhuwr ya ‘Ulamaa wote wameharamisha kula nyama ya punda wa mjini kutokana na Asaaniyd zilizothibiti kwa uwazi kabisa ya kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameharamisha nyama ya punda wa mjini. Kati ya Asaaniyd hizo ni:
1- Hadiyth ya Anas:
"أَنً رَسُوْلَ اللهِ صَلًى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلًمَ أَمَرَ مُنَادِيًا فَنَادَى : إِنَّ اللَّهَ وَرَسُولَهُ يَنْهَيَانِكُمْ عَنْ لُحُومِ الْحُمُرِ الأَهْلِيَّةِ، فَإِنَّهَا رِجْسٌ. فَأُكْفِئَتِ الْقُدُورُ وَإِنَّهَا لَتَفُورُ بِاللَّحْمِ"
“Kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwamuru mwenye kunadi akatangaza: Hakika Allaah na Rasuli Wake wanawakatazeni nyama ya punda wa mjini, kwani nyama yake ni mbaya, si salama. Vyungu vikamwagwa vikiwa vinachemka nyama”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5528) na Muslim (1940)].
2- Hadiyth ya Jaabir bin ‘Abdillaah:
"أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ نَهَى يَوْمَ خَيْبَرَ عَنْ لُحُومِ الْحُمُرِ الْأَهْلِيَّةِ وَأَذِنَ فِي لُحُومِ الْخَيْلِ"
“Kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikataza Siku ya Khaybar nyama ya punda wa mjini, na akaruhusu nyama ya farasi”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (4219) na Muslim (1941)].
Baadhi ya wafuasi wa dhehebu la Maalik –na hii ni kauli yenye nguvu zaidi kwao- wanasema nyama ya punda wa mjini huliwa pamoja na ukaraha wa “tanziyh”, yaani ukaraha au katazo hafifu lisilo na dhambi!!
Na imesimuliwa kuhusiana na Ibn ‘Abbaas na ‘Aaishah kwamba wao walikuwa wakiichukulia kama ilivyo Kauli Yake Ta’aalaa:
"قُل لَّا أَجِدُ فِي مَا أُوحِيَ إِلَيَّ مُحَرَّمًا عَلَىٰ طَاعِمٍ يَطْعَمُهُ إِلَّا أَن يَكُونَ مَيْتَةً"
“Sema: Sipati katika yale niliyofunuliwa Wahyi kwangu kilichoharamishwa kwa mlaji kukila isipokuwa kiwe ni nyamafu”. [Al-An’aam: 145].
Na lililopokelewa kwa njia sahihi toka kwa Ibn ‘Abbaas ni kuwa yeye alisita kuhusiana na Aayah hii na kusema: “Sijui kama Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliikataza kwa sababu punda walikuwa wanawabebea watu mizigo, na hivyo akachukia wabebaji wao kumalizika, au aliharamisha Siku ya Khaybar nyama ya punda wa mjini”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (4227) na Muslim (1939)].
Tukiachilia yote hayo, Ibnu ‘Abdul Barr amesema: “Hakuna makhitalifiano baina ya ‘Ulamaa wa Kiislamu leo kuhusiana na kuharamishwa nyama ya punda”.
Ninasema: “Kuharamishwa kwake kumethibiti uthibitisho usioweza kupingika kutokana na wingi wa upokezi juu ya hili (tawaatur). Uthibitisho huu ni hoja kwa kila mtu, na Allaah Ndiye Ajuaye zaidi”.
Faida Mbili:
Ya Kwanza: Nyama Ya Punda Milia Ni Halali
‘Ulamaa wote wamekubaliana hili. Imethibiti kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikula yeye pamoja na Maswahaba Wake.
Katika Hadiyth ya Abuu Qataadah:
"أنَّهُ كانَ مَعَ قَوْمٍ مُحْرِمِيْنَ – وَهُوَ حَلَّالٌ- فَسَنَحَ لَهُمْ حُمُرٌ وَحْشٌ ، فَحَمَلَ عَلَيْهَا أَبُوْ قَتَادَةِ فَعَقَرَ مِنْهَا أَتَانًا فَأَكَلُوْا مِنْهَا وَقَالُوْا : نَأْكُلُ مِنْ لَحْمِ صَيْدٍ وَنَحْنُ مُحْرِمُوْنَ؟ فَحَمَلُوْا مَا بَقِيَ مِنْ لَحْمِهَا ، فَقَالَ رَسُوْلُ اللهِ صَلًى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلًمَ : "كُلُوا مَا بَقِيَ مِنْ لَحْمِهَا"
“Ni kwamba yeye alikuwa pamoja na watu waliokuwa wamehirimia (Hijja) hali ya kuwa yeye hakuhirimia. Punda milia wakawajia karibu yao, na Abu Qataadah akawawinda na kuwapata, akamchinja jike kati yao kisha wakala sehemu ya nyama yake. Halafu wakajiuliza: Hivi tunakula nyama ya kuwinda na sisi tumehirimia?! Wakabeba nyama iliyobaki, na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawaambia: “Kuleni nyama yake iliyobakia”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (1824) na Muslim (1196)].
Na katika riwaayah, ni kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwauliza:
"هَلْ مَعَكُمْ مِنْهُ شَيْءٌ؟ قَالُوْا: مَعَنَا رِجْلُهُ، قَالَ: فَأَخَذَهَا رَسُوْلُ اللهِ صَلًى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلًمَ فَأَكَلَهَا"
“Je, mna chochote chake kilichosalia? Wakasema: Tuna mguu wake. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akauchukua akaula”.
Ya Pili: Ni Halali Kula Nyama Ya Farasi
[Al-Badaai’u (5/38), Ad-Dusuwqiy (2/117), Al-Majmuw’u (9/5), Al-Mughniy (11/66 pamoja na sharhu), Subulus salaam (4/87) na Naylul Awtwaar (8/125)].
Jumhuwr ya ‘Ulamaa; Mashaafi’iy na Mahanbali, nayo ni kauli ya Maalik pia, pamoja na Jumhuwr ya Maswahaba na Taabi’iyna, hawa msimamo wao ni kuwa ni halali kula nyama ya farasi, ni sawa akiwa farasi wa asili ya Kiarabu au asili nyingine. Dalili zao ni:
1- Hadiyth ya Jaabir:
"نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلًى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلًمَ يَوْمَ خَيْبَرَ عَنْ لُحُومِ الْحُمُرِ الأَهْلِيَّةِ وَأَذِنَ فِي لُحُوْمِ الخَيْلِ"
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikataza Siku ya Khaybar nyama ya punda wa mjini, lakini aliruhusu nyama ya farasi”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (4219) na Muslim (1941)].
2- Hadiyth ya Asmaa bint Abiy Bakr:
"نَحَرْنَا عَلَى عَهْدِ رَسُولِ اَللَّهِ صَلًى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلًمَ فَرَساً فَأَكَلْنَاهُ وَنَحْنُ بِالمدِيْنَةِ"
“Tulichinja farasi enzi ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) tukamla, nasi tuko Madiynah”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5510) na Muslim (1196)].
Lakini Mahanafiy, ikiwa pia ni kauli ya pili ya Wamaalik, nayo pia ni kauli ya Ibn ‘Abbaas, wao wanaona kwamba kuna ukaraha au uharamisho wa kula nyama ya farasi. Hoja yao ni:
1- Kauli Yake Ta’aalaa:
"وَالْخَيْلَ وَالْبِغَالَ وَالْحَمِيرَ لِتَرْكَبُوهَا وَزِينَةً"
“Na farasi, na baghala, na punda, ili muwapande na wawe mapambo”. [An-Nahl: 08].
Wanasema: Kufupisha manufaa yake katika kupandwa na kuwa mapambo tu, kunadulisha kwamba wanyama hawa si wa kuliwa, kwani lau kama wangelikuwa ni wa kuliwa, basi Allaah Angelisema:
"وَمِنْهَا تَأْكُلُونَ"
“Na miongoni mwao mnawala”.
Hoja hii inajibiwa hivi: Kwamba Aayah hii ilishuka Makkah kwa makubaliano ya Mufassiruna wote, na ruksa ya kula ilikuja baada ya Hijrah. Isitoshe, Aayah haigusii katazo la kula huku zikiwepo Ahaadiyth zilizo wazi kabisa katika kuhalalisha.
2- Yanayohadithiwa toka kwa Khaalid bin Al Waliyd (Radhwiya Allaah ‘anhu):
"أَنَّ النَّبِيَ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ نَهَى عَنْ أَكْلِ لُحُومِ الْخَيْلِ وَالبِغَالِ وَالحَمِيرِ ، وَكُلِّ ذِيْ نَابٍ مِنَ السِبَاعِ ، وَكُلِّ ذِيْ مِخْلَبٍ مِنَ الطَّيْر"ِ
“Kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikataza kula nyama ya farasi, baghala na punda, na kila mnyama mwenye meno katika wanyama wakali, na kila mwenye kucha katika ndege”. [Hadiyth hii ni Dhwa’iyf, haitolewi hoja kwayo, nayo imekharijiwa na An Nasaaiy (4332), Abu Daawuwd (3790), Ibn Maajah (3198) na Ahmad (16214)].
Lililo sahihi ni kauli ya Jumhuwr isemayo kuwa kula farasi ni halali. Allaah Ndiye Ajuaye zaidi.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
Alhidaaya.com [3]
012-Vyakula Vilivyoharamishwa Na Hadiyth Za Rasuli
Kila Mnyama Mkali Mwenye Kucha
2- Kila Mnyama Mkali Mwenye Kucha
Mnyama yeyote mwenye meno anayoulia kwayo kiwindwa, ni sawa akiwa mnyama mkali kama simba, mbwa mwitu, chui, chita na kadhalika, au mnyama wa kienyeji anayeishi na watu kama mbwa na paka, hawa wote si halali kuliwa kwa mujibu wa kauli ya Jumhuwr. Na hii ni kwa dalili zifuatazo:
1- Hadiyth ya Abu Hurayrah:
"كُلُّ ذِي نَابٍ مِنَ السِّباعِ فأَكْلُهُ حَرَامٌ"
“Kila mnyama mkali mwenye meno, kumla ni haramu. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (1933)].
2- Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas:
"نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلًى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلًمَ عَنْ ُ َكُلِّ ذِيْ نَابٍ مِنَ السِّبَاعِ، وَعَنْ كُلِّ ذِيْ مِخْلَبٍ مِنَ الطَّيْرِ"
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kila mwenye meno katika wanyama wakali, na kila mwenye kucha katika ndege”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (1934), Abu Daawuwd (3785) na An Nasaaiy (7/206)].
3- Toka kwa Abu Az Zubayr:
"سَأَلْتُ جَابِرًا عَنْ ثَمَنِ الْكَلْبِ، وَالسِّنَّوْرِ. قَالَ: زَجَرَ النَّبِيُّ صَلًى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلًمَ عَنْ ذَلِكَ"
“Nilimuuliza Jaabir kuhusu bei ya mbwa na paka. Akasema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kuhusu hilo”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (1569)].
Imethibiti vile vile toka kwa Ibn ‘Abbaas kwamba Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إِنً اللهَ إِذَا حَرًمَ عَلَى قَوْمٍ أَكْلَ شَيْءٍ حَرًمَ عَلَيْهِمْ ثَمَنَهُ"
“Hakika Allaah Anapowaharamishia watu kula kitu, Huwaharamishia pia thamani yake (kukiuza au kukinunua)”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (3488) na wengineo. Ina Hadiyth mwenza kwenye Swahiyh Mbili].
Faida:
Sungura Ni Halali Kuliwa
Ni halali kula sungura kwa mujibu wa rai ya Jumhuwr. Ni kwa Hadiyth ya Anas aliyesema:
"أَنْفَجْنَا أَرْنَبًا فَسَعَى الْقَوْمُ فَلَغَبُوا، فَأَخَذْتُهَا وجِئْتُ بِهَا إِلَى أَبِي طَلْحَةَ فَذَبَحَهَا، فَبَعَثَ بِوَرِكِهَا أَوْ قَالَ بِفَخِذِهَا إِلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَقَبِلَهُ"
“Mara moja tulimchokonoa sungura (toka ndani ya shimo lake akatoka), watu wakamfukuza na hatimaye wakachoka hoi. (Mimi nilimkimbiza mpaka nikamkamata), nikamchukua na kwenda naye kwa Abu Twalha, akamchinja, na akapeleka paja lake kwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na Rasuli akalipokea”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al Bukhaariy (2572) na Muslim (1953)].
Na kwa vile sungura pia ni katika wanyama wanaopendeka, hawana meno ya kujeruhi, na hakuna matini yoyote inayogusia kuharamishwa kwake. [Al-Badaai’u (5/39), As Swaawiy (1/322), Nihaayatul Muhtaaj (8/143), Al-Mughniy (11/81) pamoja na Ash Sharhul Kabiyr, na Al Muhallaa (7/432)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
Alhidaaya.com [3]
Vyakula Vilivyoharamishwa Na Hadiyth Za Rasuli
Kila Ndege Mwenye Kucha (Ndege Wawindaji Wenye Kujeruhi Na Kuua)
3- Kila Ndege Mwenye Kucha (Ndege Wawindaji Wenye Kujeruhi Na Kuua)
Ni kama kozi, kipanga, mwewe, na mfano wao. Ni kwa Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas iliyotangulia:
"أَنَّ النَّبِيَ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ نَهَى عَنْ كُلِّ ذِيْ مِخْلَبٍ مِنَ الطَّيْرِ"
“Kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kila ndege mwenye makucha”. [Hadiyth Swahiyh. Imetajwa nyuma kidogo].
Muradi wa makucha hapa ni yale anayowindia, kwa kuwa ni maarufu kwa Waarabu kwamba hawamuiti “Mwenye Makucha” kwao isipokuwa yule mwenye kuwinda kwa kutumia makucha yake tu. Ama jogoo, njiwa na ndege wengineo wasiowinda kwa kutumia makucha, hao hawaitwi “Wenye Makucha” katika Lugha ya Kiarabu, kwa kuwa makucha yao ni ya kujishikilia uzani wa mwili na kuchakuria, na si kwa kuwindia au kuulia.
Jumhuwr ya ‘Ulamaa - kinyume na Maalik!! – wamesema ni haramu kila ndege mwenye makucha (ya kuwindia, kujeruhia na kuulia).
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
Alhidaaya.com [3]
Vyakula Vilivyoharamishwa Na Hadiyth Za Rasuli
014-Al-Jallaalah: (الْجَلَّالَةُ)
4- Al-Jallaalah: (الْجَلَّالَةُ)
Hawa ni wanyama wanaokula najisi – au sehemu kubwa ya majani wanayokula au malisho au chakula ni najisi – ni sawa wakiwa ni ngamia, ng’ombe, mbuzi, kondoo, kuku na kadhalika. Wanyama hawa si halali nyama zao wala maziwa yao.
Hii ni kauli ya Ahmad – katika moja ya riwaayah mbili – kutokana na Hadiyth ya Ibn ‘Umar:
"نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ أَكْلِ الْجَلَّالَةِ وَأَلْبَانِهَا"
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kula mnyama mwenye kula najisi pamoja na maziwa yake”. [Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (3767), At-Tirmidhiy (1883) na Ibn Maajah (3189)].
Lakini Ash-Shaafi’iy amekamata mwelekeo wa kusema kwamba ni makruhu na wala si haramu kula (nyama ya mnyama huyu au kunywa maziwa yake). Na hii ni riwaayah nyingine toka kwa Ahmad.
· Ni Wakati Gani Inakuwa Halali Kumla Mnyama Anayekula Najisi?
Mnyama huyu kama atafungiwa siku tatu (ili asije kula vyakula najisi) na akalishwa malisho twahara safi, basi itahalalika kumchinja, kula nyama yake na kunywa maziwa yake.
Imeripotiwa kuhusiana na Ibn ‘Umar kwamba:
"كَانَ يَحْبِسُ الدًجَاجَةَ الْجَلاًلَةَ ثَلَاثًا"
“Alikuwa anamfungia kuku mla najisi siku tatu”. [Isnaad yake ni Swahiyh. Imekharijiwa na Ibn Abiy Shaybah (4660 – 8847). Angalia Al-Irwaa (2504)].
Imenukuliwa pia toka kwa Imaam Ahmad (Rahimahul Laah) akisema kwamba atafungiwa siku tatu, ni sawa akiwa ndege au mnyama. Na pia katika riwaayah aliyonukuliwa amesema: “Kuku atafungiwa siku tatu, na ngamia, ng’ombe na mfano wao, watazuiliwa siku 40”.
Alaa kulli haal, tunasema kuwa “Al Jallaalah” anahalalika kwa kumfungia na kumlisha chakula safi twahara kwa makubaliano ya ‘Ulamaa wote, lakini wamekhitalifiana muda wa kumfungia.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
Alhidaaya.com [3]
Vyakula Vilivyoharamishwa Na Hadiyth Za Rasuli
Mnyama Ambaye Rasuli Kaamuru Kumuua Si Halali Kuliwa
05- Mnyama Ambaye Rasuli Kaamuru Kumuua Si Halali Kuliwa
Ni kama panya, nge, kunguru, mwewe, mbwa anayeng’ata watu ovyo, mjusi wa viambaza na nyoka.
1- Toka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaah ‘anhaa) toka kwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"خَمْسٌ فَوَاسِقُ يُقْتَلْنَ فِي الْحَرَمِ الْفَأْرَةُ وَالْعَقْرَبُ وَالْحُدَيَّا وَالْغُرَابُ وَالْكَلْبُ الْعَقُورُ "
“(Wanyama) watano wabaya huuliwa katika Al-Haram: Panya, nge, mwewe (kengewa), kunguru na mbwa anayeuma watu ovyo”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (3314) na Muslim (1198)].
2- Toka kwa Sa-‘ad bin Abiy Waqqaasw (Radhwiya Allaah ‘anhu) amesema:
"أَمَرَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلًمَ بِقَتْلِ الْوَزَغِ وَسَمَّاهُ فُوَيْسِقًا"
“Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameamuru kumuua mjusi wa viambaza (mjusi kafiri), na akamwita kuwa ni kijinyama kidogo hatari”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (2238). Ina Hadiyth mwenza kwa Al-Bukhaariy toka Hadiyth ya Ummu Shurayk].
3- Toka kwa ‘Abdullaah bin Mas-‘uwd (Radhwiya Allaah ‘anhumaa) amesema:
" كُنَّا مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلًمَ فِي غَارٍ وَقَدْ أُنْزِلَتْ عَلَيْهِ : ( وَالْمُرْسَلاَتِ عُرْفًا) . فَنَحْنُ نَأْخُذُهَا مِنْ فِيهِ رَطْبَةً إِذْ خَرَجَتْ عَلَيْنَا حَيَّةٌ فَقَالَ : " اقْتُلُوهَا " ، فَابْتَدَرْنَاهَا لِنَقْتُلَهَا فَسَبَقَتْنَا ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلًمَ : "وَقَاهَا اللَّهُ شَرَّكُمْ كَمَا وَقَاكُمْ شَرَّهَا" .
“Tulikuwa pamoja na Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika pango akiwa ameshateremshiwa (Wal Mursalaat ‘Urfan). Na wakati tukiwa tunaisikiliza (suwrah) toka mdomoni mwake ikiwa bado mbichi mpya, mara ghafla akatutokezea nyoka mkubwa, na Rasuli hapo hapo akatuambia: “Muueni”. Tukakimbizana haraka tuwahi kumuua lakini akawahi kutukimbia. Na Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa sallam) akasema: Allaah Amemlinda na shari yenu kama Alivyowalindeni nyinyi na shari yake”.
Na kwa vile pia viumbe hawa ni khabithi wanaowafanya watu wenye maumbile salama kuchefukwa na roho.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
Alhidaaya.com [3]
Vyakula Vilivyoharamishwa Na Hadiyth Za Rasuli
016-Mnyama Ambaye Allaah Au Rasuli Wamekataza Kumuua Si Halali Kuliwa
06- Mnyama Ambaye Allaah Au Rasuli Wamekataza Kumuua Si Halali Kuliwa
Ni kama sisimizi, nyuki, hud-hud, tiva (shrikes) na chura.
1- Toka kwa Ibn ‘Abbaas amesema:
"نَهَى رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلًمَ عَنْ قَتْلِ أَرْبَعِ مِنْ اَلدَّوَابِّ : اَلنَّمْلَةُ، وَالنَّحْلَةُ، وَالْهُدْهُدُ، وَالصُّرَدُ"
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kuua viumbe wanne: Sisimizi, nyuki, hud-hud na tiva (shirkes)”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na An-Nasaaiy (5/189), Ahmad (6/83) na wengineo].
2- Toka kwa ‘Abdul Rahmaan bin ‘Uthmaan amesema:
"ذَكَرَ طَبِيبٌ عِنْدَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلًمَ دَوَاءً، وذَكَرَ الضِّفْدَعً يَجْعَلُ فِيْهِ، فَنَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلًمَ عَنْ قَتْلِ الضِّفْدَع"
“Tabibu (daktari) alitaja mbele ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) dawa, na akaeleza kwamba dawa hiyo anaitengeneza kutokana na chura. Na hapo Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akakataza kuua chura”. [Hadiyth Hasan. Imekharijiwa na Ahmad (15197), Ad-Daaramiy (1998) na Ibn Maajah (3223)].
Ash-Shawkaaniy amepinga amri ya kuua kitu au kukataza kukiua, iwe ndio katika sababu za kuharamisha kukila. Akasema: “Allaah Ambaye Ndiye Mwekaji sharia, Hakutueleza chochote kinachofidisha kuharamisha kukila kile ambacho Ameamuru kukiua, au kilichokatazwa kukiua mpaka iwe amri na katazo ni dalili juu ya hilo. Hivyo hakuna kigezo chochote cha kulifanya hilo kuwa ni chimbuko kati ya machimbuko ya kuharamisha. Bali ikiwa kilichoamriwa kuuawa au kilichokatazwa kuuawa ni katika vinavyoingia ndani ya duara la vichafu, basi uharamisho wake unakuwa kwa Aayah Tukufu. Na kama si katika hivyo, basi kitakuwa ni halali kwa kutegemea msingi wa uasili wa uhalali kama ilivyogusiwa nyuma, na kuwepo dalili kuu juu ya hayo”. [Naylul Awtwaar (8)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
Alhidaaya.com [3]
017-Vilivyoharamishwa Ni Halali Wakati Wa Dharura
· Vilivyoharamishwa Ni Halali Wakati Wa Dharura
Waislamu wote kwa pamoja wanakubaliana kuwa inafaa kula mfu na mfano wake kwa yeyote aliyelazimika. Allaah ‘Azza wa Jalla Amepataja mahala patano ndani ya Qur-aan Tukufu ambapo mwenye kulazimika anaweza kula vilivyoharamishwa.
1- Allaah Amesema - baada ya kutaja kuharamisha maiti na mfano wake -:
"فَمَنِ اضْطُرَّ غَيْرَ بَاغٍ وَلَا عَادٍ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ"
“Lakini aliyefikwa na dharura (akala) bila ya kutamani wala kupindukia mipaka, basi si dhambi juu yake. Hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu. [Al-Baqarah: 173].
2- Amesema tena - baada ya kutaja kuharamisha maiti na mfano wake -:
"فَمَنِ اضْطُرَّ فِي مَخْمَصَةٍ غَيْرَ مُتَجَانِفٍ لِّإِثْمٍ ۙ فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ"
“Basi atakayelazimika katika njaa kali bila kulalia kwenye dhambi (akala vilivyoharamishwa), basi hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu”. [Al-Maaidah: 03].
3- Na Akasema tena - baada ya kuvitaja -:
"فَمَنِ اضْطُرَّ غَيْرَ بَاغٍ وَلَا عَادٍ فَإِنَّ رَبَّكَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ"
“Lakini atakayefikwa na dharura bila ya kutamani wala kuvuka mipaka, basi hakika Rabb wako Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu”. [Al-An’aam: 145].
4- Amesema pia:
"وَمَا لَكُمْ أَلَّا تَأْكُلُوا مِمَّا ذُكِرَ اسْمُ اللَّـهِ عَلَيْهِ وَقَدْ فَصَّلَ لَكُم مَّا حَرَّمَ عَلَيْكُمْ إِلَّا مَا اضْطُرِرْتُمْ إِلَيْهِ"
“Na mna nini hata msile katika ambavyo limetajwa Jina la Allaah na ilhali Ameshafasilisha waziwazi kwenu yale Aliyokuharamishieni isipokuwa vile mlivyofikwa na dharura navyo”. [Al-An’aam: 119].
5- Amesema vile vile:
"فَمَنِ اضْطُرَّ غَيْرَ بَاغٍ وَلَا عَادٍ فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ"
“Basi atakayefikwa na dharura bila ya kutamani wala kuvuka mipaka, basi hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu”. [An-Nahl: 115].
· Mpaka Wa Dharura Unaoruhusu Kilichoharamishwa
Maana ya dharura katika Aayah hizi Tukufu, na mpaka wa dharura wenye kuruhusu kula mfu na vingine vilivyoharamishwa, ni hofu ya kuhiliki. [Ahkaamul Qur-aan cha Al-Jas-Swaasw (1/150) na Adh-waaul Bayaan (1/64-95)].
· Makusudio Ya Kuhalalisha (Kuruhusu) Kilichoharamishwa
Mafuqahaa wamekhitalifiana kuhusiana na makusudio ya kuhalalisha mfu na mfano wake katika kauli mbili:
Ya Kwanza:
Makusudio ni kuwa inajuzu kula au kutokula. Ni kauli ya baadhi ya Wamaalik, Mashaafi-‘iy, na Mahanbali. Ni kwa uwazi wa Kauli Yake Ta’aalaa:
"فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ"
“Basi si dhambi juu yake”. [Al-Baqarah: 173].
Ya Pili:
Makusudio ni kuwa ni waajib kula kwa aliyekurubia kufa. Ni madhehebu ya Jumhuwr kutokana na Neno Lake Ta’aalaa:
"وَلَا تُلْقُوا بِأَيْدِيكُمْ إِلَى التَّهْلُكَةِ"
“Wala msijitupe katika maangamizi kwa mikono yenu”. [Al-Baqarah: 195].
Wamesema: Na hakuna shaka kuwa yule anayewacha kula mfu na mfano wake mpaka akafa, basi huyo anazingatiwa kuwa amejiua na amejitupa mwenyewe kwenye maangamizi. Kwa kuwa kujizuia kula ni kitendo kinachonasibishwa kwa mtu mwenyewe.
Ama Neno Lake Ta’aalaa فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ, hili halipingani na kauli ya kusema ni waajib, kwa kuwa kukanusha dhambi kwa kula ni suala jumuishi, linakusanya hali ya kujuzu na hali ya ulazima.
· Masharti Ya Kuruhusika Kula Mfu Kwa Aliyedharurika
Fuqahaa wameweka masharti ya mtu kuruhusika kula mfu au mfano wake katika vilivyoharamishwa. Wamekubaliana katika baadhi ya masharti na wamekhitalifiana katika baadhi nyingine. Kati ya waliyokubaliana kwayo ni:
1- Asipate kabisa chakula cha halali japo tonge moja. Kama atalipata, basi ni lazima alile kwanza, na kama halikumtosha, hapo basi kilichoharamishwa kitahalalika kwake.
2- Asiwe amekurubia kufa kwa hali ambayo hata akila chakula hakitomfaa tena. Ikiwa ataishilia katika hali hii, basi hapo kilichoharamishwa hakitohalalika tena kwake.
3- Asipate chakula cha halali cha Muislamu au Dhimmiy. Kuna ufafanuzi wa Fuqahaa kuhusiana na sharti hii.
· Zindushi Mbili:
1- Hairuhusiwi kuvuka kiasi cha kuokoa maisha yake au kumwondoshea madhara. Hili ndilo Aliloliashiria Allaah ‘Azza wa Jalla: غَيْرَ بَاغٍ وَلَا عَادٍ (Bila ya kutamani wala kuvuka mipaka).
2- Kilichoharamishwa kwa kuwa kinamuua mwanadamu kama sumu, hicho hakiruhusiwi kwa aliyedharurika, kwa kuwa kukila ni kuharakisha mauti na kuiua nafsi, na hili ni katika madhambi makubwa, nalo limekubaliwa na wote.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
Alhidaaya.com [3]
018-Adabu Za Kula: Kupiga “Bismil Laahi” Kabla Ya Kula
Adabu Za Kula
Huu ni mjumuiko wa adabu za kisharia katika kula ambazo inatakikana tuzizingatie, kwani ndani yake kuna uhuisho wa Sunnah ya Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Kadhalika, ndani yake kuna kumfukuza, kumweka mbali na kumzuia shaytwaan ambaye anakuwa na shime ya kushirikiana na Muislamu katika chakula chake, kinywaji chake, mavazi yake na malazi yake ili aweze kumpoteza na kuutawala moyo wake, akili yake na viungo vyake. Vilevile, ndani yake kuna ufanikishaji wa maslaha ya kidini, kiuchumi na kijamii.
Kati ya adabu hizi ni:
1- Kupiga “Bismil Laahi” Kabla Ya Kula:
Toka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaah ‘anhaa) amesema: “Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إِذَا أَكَلَ أَحَدُكُمْ طَعَاماً فَلْيَقُلْ بِسْمِ اللَّهِ، فَإِنْ نَسِيَ فِي أَوَّلِهِ فَلْيَقُلْ بسْمِ اللَّهِ فِي أَوَّلِهِ وَآخِرِهِ"
“Anapokula mmoja wenu chakula chochote, basi aseme Bismil Laah. Akisahau mwanzoni (kisha akakumbuka) basi aseme: Bismil Laahi, katika mwanzo wake na mwisho wake”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (3767), At Tirmidhiy (1858) na Ahmad (6/143)].
Na toka kwa Hudhayfah kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إِنَّ الشَّيْطَانَ يَسْتَحِلُّ الطَّعَامَ أَنْ لَا يُذْكَرَ اسْمُ اللهِ عَلَيْهِ"
“Hakika shaytwaan kinakuwa halali kwake chakula ambacho hakikutajiwa Jina la Allaah.” [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (2017) na Ahmad (5/383)].
Na Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia pia ‘Amri bin Abiy Salamah:
"يَا غُلَامُ ! سَمِّ اَللَّهَ ، وَكُلْ بِيَمِيْنِكَ ، وَكُلْ مِمَّا يَلِيْكَ"
“Ee kijana mdogo! Mtaje Allaah, kula na mkono wako wa kulia, na kula kilicho mbele yako”. [Hadiyth Swahiyh].
Na ikiwa atasahau kusema “Bismil Laah” wakati anapoanza kula:
Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) –akilizungumzia hili-amesema:
"مَنْ نَسِيَ أَنْ يَذْكُرَ اللَّهَ عَزَّ وَجَلَّ فِي أَوَّلِ طَعَامِهِ فَلْيَقُلْ حِيْنَ يَذْكُرُ : بِسْمِ اللَّهِ أَوَّلَهُ وَآخِرَهُ، فَإِنَّهُ يَسْتَقْبِلُ طَعَامًا جَدِيْدًا، أَوْ يَمْتَنِعُ الخَبِيْثُ مِمَّا كَانَ يُصِيْبُ مِنْهُ".
“Anayesahau kulitaja Jina la Allaah ‘Azza wa Jalla mwanzoni anapokula, basi aseme anapokumbuka: “Bismil Laah, mwanzo wake na mwisho wake”, kwani (kwa kusema hivyo) atakianza upya chakula chake, au khabithi (shaytwaan) ataiachia sehemu ya chakula aliyokuwa anaipata”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Ibn As-Sunniy katika kitabu chake “Amalul Yawm wal Laylah (461) kwa Sanad Swahiyh. Ina Hadiyth mwenza toka kwa ‘Aaishah, nayo imetajwa nyuma].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
Alhidaaya.com [3]
Adabu Za Kula
019-Kula Kwa Mkono Wa Kulia
Na Kutomega Chakula Kilicho Mbele Ya Mwingine
2-3- Kula Kwa Mkono Wa Kulia, Na Kutomega Chakula Kilicho Mbele Ya Mwingine Kama Wanakula Sahani Moja
Toka kwa ‘Abdullaah bin ‘Umar kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إذَا أَكَلَ أَحَدُكُمْ فَلْيَأْكُلْ بِيَمِيْنِهِ، وَإِذَا شَرِبَ فَلْيَشْرَبْ بِيَمِيْنِهِ، فَإِنَّ اَلشَّيْطَانَ يَأْكُلُ بِشِمَالِهِ، وَيَشْرَبُ بِشِمَالِهِ".
“Anapokula mmoja wenu, basi na ale kwa mkono wake wa kuume, na anapokunywa, basi na anywe kwa mkono wake wa kuume, na sababu ni kuwa shaytwaan anakula kwa mkono wake wa kushoto, na anakunywa kwa mkono wake wa kushoto”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (2020), At-Tirmidhiy (1800) na Abu Daawuwd (3776)].
Na toka kwa ‘Amr bin Abiy Salamah, amesema:
"كُنْتُ غُلاَماً فِي حِجْرِ رَسُوْلِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلًمَ ، وَكَانَتْ يَدِيْ تَطِيْشُ في الصَّحْفَةِ، فَقَالَ لِيْ رَسُوْلُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلًمَ : يَا غُلاَمُ ! سَمِّ اَللَّهَ ، وَكُلْ بِيَمِيْنِكَ ، وَكُلْ مِمَّا يَلِيْكَ"، فَمَا زَالَتْ تِلْكَ طِعْمَتِي بَعْدُ".
“Nilikuwa kijana mdogo nikilelewa na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na mkono wangu ulikuwa ukitembea huku na kule kwenye sinia. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaniambia: “Ee kijana mdogo! Sema “Bismil Laah” , kula na mkono wako wa kuume, na kula kile kilicho mbele yako”. Na baada ya hapo, ukawa huo ndio ulaji wangu siku zote. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5376) na Muslim (2022)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
Alhidaaya.com [3]
Adabu Za Kula
020-Kula Toka Pembezoni Mwa Chakula Na Si Kutoka Katikati Yake
4- Kula Toka Pembezoni Mwa Chakula Na Si Kutoka Katikati Yake
Toka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaah ‘anhumaa) toka kwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"الْبَرَكَة تَنْزِلُ فِيْ وَسَطِ الطَّعَامِ ، فَكُلُوا مِنْ حَافَتَيْهِ ، وَلاَ تَأْكُلُوا مِنْ وَسَطِهِ"
“Baraka inateremka katikati ya chakula, basi kuleni toka pambizo zake, na msile toka katikati yake”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (3772), Ibn Maajah (3277) na Ahmad (1/343-345)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
Alhidaaya.com [3]
Adabu Za Kula
021-Mtu Asile Huku Ameegemea
5- Mtu Asile Huku Ameegemea
Ni kwa Hadiyth ya Abu Juhayfah, amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"أَمَّا أَنَا، فَلا آكُلُ مُتَّكِئًا"
“Mimi kwa upande wangu, sili huku nimeegemea kitu”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5398) na At-Tirmidhiy katika Ash-Shamaail (64)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
Alhidaaya.com [3]
Adabu Za Kula
022-Asikitie Doa Chakula Au Kukisema Vibaya Kama Hakukipenda
6- Asikitie Doa Chakula Au Kukisema Vibaya Kama Hakukipenda
Toka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaah ‘anhu) amesema:
"مَا عَابَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلًمَ طَعَامًا قَطُّ ، إِن اشْتَهَاهُ أَكَلَهُ ، وَإِنْ كَرِهَهُ تَرَكَهُ"
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakukitia doa kamwe chakula. Akikitamani hukila, na kama hakukipenda hukiacha”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5409) na Muslim (2064)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
Alhidaaya.com [3]
Adabu Za Kula
023-Watu Wale Kwa Pamoja Na Mtu Asile Peke Yake
7- Watu Wale Kwa Pamoja Na Mtu Asile Peke Yake
Kwa kuwa mikono mingi kwenye chakula hukiongezea baraka kama alivyosema Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"طَعَامُ الاِثْنَيْنِ كَافِي الثَّلاَثَةِ وَطَعَامُ الثَّلاَثَةِ كَافِي الأَرْبَعَةِ"
“Chakula cha wawili huwatosha watatu, na chakula cha watatu huwatosha wanne”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5392) na Muslim (2058)].
Imesimuliwa kwamba Maswahaba wa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) walisema:
"يَا رَسُوْلَ اللهِ ، إِنَّا نَأْكُلُ وَلاَ نَشْبَعُ ، فَقَالَ : فَلَعَلَّكُمْ تَفْتَرِقُوْنَ؟ قَالُوْا نَعَمْ ، قَالَ : فَاحْتَمِعُوْا عَلَى طَعَامِكُمْ ، وَذْكُرُوا اسْمَ الله ، يُبَارِكْ لَكُمْ فِيْهِ"
“Ee Rasuli wa Allaah! Mbona sisi tunakula na wala hatushibi?! Rasuli akawaambia: Huenda nyinyi mnakula kila mmoja kivyake. Wakasema: Ni kweli. Akasema: Basi jumuikeni pamoja katika chakula chenu, na litajeni Jina la Allaah, na Yeye Atawabarikieni ndani yake”. Hadiyth hii ni Dhwa’iyf.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
Alhidaaya.com [3]
Adabu Za Kula
024-Kulila Tonge –Likianguka- Baada Ya Kulipangusa Uchafu
8- Kulila Tonge –Likianguka- Baada Ya Kulipangusa Uchafu
Toka kwa Jaabir amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إِذَا وَقَعَتْ لُقْمَةُ أَحَدِكُمْ فَلْيَأْخُذْهَا ، فَلْيُمِطْ مَا كَانَ بِهَا مِنَ الأَذَى وَلْيَأْكُلْهَا ، وَلاَ يَدَعْهَا لِلشَّيْطَانِ"
“Likianguka tonge la mmoja wenu basi aliokote, kisha alipanguse uchafu uliolipata na alile, na wala asiliache kwa shaytwaan.” [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (2033)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
Alhidaaya.com [3]
Adabu Za Kula
025-Kulamba Vidole Na Sahani Kabla Ya Kuosha Mkono Au Kuupangusa
9- Kulamba Vidole Na Sahani Kabla Ya Kuosha Mkono Au Kuupangusa
Toka kwa Jaabir:
"أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَمَرَ بِلَعْقِ الْأَصَابِعِ وَالصَّفْحَةِ ، وَقَالَ : "إِنَّكُمْ لَا تَدْرُونَ: فِي أَيَّهِ الْبَرَكَةُ؟ ".
Kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameamuru kulamba vidole na sahani kwa kusema: “Hakika nyinyi hamjui wapi ilipo baraka yake”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (2033)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
Alhidaaya.com [3]
Adabu Za Kula
026- Kumhimidi Allaah Na Kuomba Du’aa Baada Ya Kumaliza Kula
10 -11 – Kumhimidi Allaah Na Kuomba Du’aa Baada Ya Kumaliza Kula
Toka kwa Anas, amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إِنَّ اللَّهَ تَعَالَى لَيَرْضَى عَنِ العَبْدِ أَنْ يَأْكُلَ الأكْلَةَ فَيَحْمَدُهُ عَلَيْهِ أَوْ يَشْرَبَ الشَّرْبَةَ فَيَحْمَدَهُ عَلَيْهَا"
“Hakika Allaah Humridhia kwa yakini mja anayekula mlo mmoja tu (au tonge moja tu) akamshukuru Allaah kwa mlo huo, au anayekunywa mara moja tu (au funda moja tu) akamshukuru Allaah kwa unywaji huo”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (2724) na At-Tirmidhiy (1816)].
Matamshi mengi ya himdi na du’aa yamethibiti toka kwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) baada ya kumaliza kula. Kati yake ni:
1- "الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي كَفَانَا وَأَرْوَانَا، غَيْرَ مَكْفِيٍّ، وَلاَ مَكْفُورٍ"
“Himdi Anastahiki Allaah Ambaye Ametutosheleza mahitajio yetu na Akatuondoshea kiu, hazilipiki (Fadhila Zake) wala hazikanushiki. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5459)].
2- "الْحَمْـدُ للهِ حَمْـداً كَثـيراً طَيِّـباً مُبـارَكاً فِيْهِ، غَيْرَ مَكْفِيٍّ وَلا مُوَدَّعٍ وَلا مُسْتَغْـنىً عَنْـهُ رَبَّـنا"
“Himdi Anastahiki Allaah, himdi zilizo nyingi, zilizo njema na zilizojaa baraka tele ndani yake, haziwezi kulipika, wala kuachwa, wala kutohitajiwa tena, ee Rabbi wetu”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5458), Abu Daawuwd (3849), Ibn Maajah (3284 na Ahmad (5/256)].
3- "الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِيْ أَطْعَمَ وَسَقَى وَسَوَّغَهُ وَجَعَلَ لَهُ مَخْرَجًا"
“Himdi Anastahiki Allaah Ambaye Amelisha, Amenywesha, Akakifanya (chakula) kuwa chepesi kuingia mwilini, na Akakiwekea njia ya kutoka mwilini.” [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (3851) na Ibn As-Sunniy].
4- "اللّهُمَّ أَطْعَمْتَ وَسَقَيْتَ وَأَغْنَيْتَ وَأَقْنَيْتَ وَهَدَيْتَ وَأَحْيَيْتَ ، فَلَكَ الحَمْدُ عَلَى مَا أَعْطَيْتَ"
“Ee Allaah! Umelisha, Umenywesha, Umetosheleza, Umekinaisha, Umeongoa, na Umehuisha. Basi ni Yako Himdi kwa yote Uliyotoa”. [Hadiyth Hasan. Imekharijiwa na Ahmad katika “Al-Musnad” nambari 1600].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
Alhidaaya.com [3]
Adabu Za Kula
027-Kumwombea Du’aa Aliyeandaa Au Kualika Chakula
12- Kumwombea Du’aa Aliyeandaa Au Kualika Chakula. Kati ya du’aa zilizothibiti kwa hilo ni:
"أَفْطَـرَ عِنْدَكُمُ الصَّـائِمُوْنَ ، وَأَكَلَ طَعَامَـكُمُ الأبْـرَارُ ، وَصَلَّـتْ عَلَـيْكُمُ الملائِكَـةُ"
“Wamefungua kwenu waliofunga, na wamekula chakula chenu watu wema, na Malaika wamewaombeeni rahmah”. [Hadiyth Swahiyh kwa wenza wake. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (3854), Ibn Maajah (1747) na wengineo].
"اللّهُـمَّ بارِكْ لَهُمْ فيما رَزَقْـتَهُم، وَاغْفِـرْ لَهُـمْ وَارْحَمْهُمْ"
“Ee Allaah! Wabarikie katika Ulivyowaruzuku, Waghufirie na Warehemu”.
[Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (3805), At-Tirmidhiy (3500) na Abu Daawuwd (3241)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
Alhidaaya.com [3]
Adabu Za Kula
028-Kuosha Mkono Ili Kuondosha Harufu Ya Chakula
13- Kuosha Mkono Ili Kuondosha Harufu Ya Chakula
Toka kwa Abu Hurayrah, amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إِذَا بَاتَ أَحَدُكُمْ وَفِيْ يَدِهِ غَمَرٌ فَأَصَابَهُ شَيْءٌ ، فَلَا يَلُومَنَّ إِلَّا نَفْسَهُ"
“Ikiwa mmoja wenu atalala na hali ana uchafu mkononi mwake, halafu akapatwa na lolote, basi asilaumu chochote ila ajilaumu yeye mwenyewe.” [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na At-Tirmidhiy (1860), Abu Daawuwd (3852), Ibn Maajah (3297) na Ahmad (8175)].
…………………
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/284
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11159&title=08-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20%20%D9%83%D9%90%D8%AA%D9%8E%D8%A7%D8%A8%D9%8F%20%D8%A7%D9%84%D8%A3%D9%8E%D8%B7%D9%92%D8%B9%D9%90%D9%85%D9%8E%D8%A9%D9%90%20%D9%88%D9%8E%D8%A7%D9%84%D8%A3%D9%8E%D8%B4%D9%92%D8%B1%D9%90%D8%A8%D8%A9%20-%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%20
[3] http://www.alhidaaya.com/
[4] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11160&title=001-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20Taarifu%20Ya%20Vyakula
[5] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11161&title=002-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20Asili%20Ya%20Vyakula%20Vyote%20Ni%20Halali%20Mpaka%20Iwepo%20Dalili%20Ya%20Kuharamisha%20
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11162&title=003-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20Hakiharamishwi%20Chakula%20Chochote%20Ila%20Kile%20Tu%20Alichokiharamisha%20Allaah%20Katika%20Kitabu%20Chake%20Au%20Kupitia%20Ulimi%20Wa%20Nabiy%20%28%D8%B5%D9%84%D9%89%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%20%D8%B9%D9%84%D9%8A%D9%87%20%D9%88%D8%A2%D9%84%D9%87%20%D9%88%D8%B3%D9%84%D9%85%29%20%20%20
[7] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11163&title=004-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20Mnyama%20Ambaye%20Hakutajwa%20Kwenye%20Qur-aan%20Au%20Hadiyth%20Za%20Rasuli%2C%20Na%20Waarabu%20Wakamwona%20Mbaya%20Hafai%20Kuliwa%2C%20Je%20Litazingatiwa%20Hilo%3F%20
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11164&title=005-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20Sababu%20Ya%20Kuharamishwa%20Baadhi%20Ya%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%20%20
[9] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11165&title=006-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20Vyakula%20Vilivyoharamishwa%20Na%20Kitabu%20Cha%20Allaah%3A%20Mfu%20
[10] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11166&title=007-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20Damu%20Ya%20Mnyama%20Aliyechinjwa%20
[11] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11167&title=008-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20Nyama%20Ya%20Nguruwe%20%20
[12] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11168&title=009-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3AKilichotajiwa%20Asiyekuwa%20Allaah%20Wakati%20Wa%20Kuchinjwa%20
[13] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11169&title=010-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20Kilichochinjwa%20Kwa%20Ajili%20Ya%20Asiye%20Allaah%20%20
[14] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11170&title=011-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20Nyama%20Ya%20Punda%20Wa%20Mjini
[15] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11171&title=012-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20Kila%20Mnyama%20Mkali%20Mwenye%20Kucha
[16] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11172&title=013-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20Kila%20Ndege%20Mwenye%20Kucha
[17] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11173&title=014-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20Al-Jallaalah%3A%20%28%D8%A7%D9%84%D9%92%D8%AC%D9%8E%D9%84%D9%91%D9%8E%D8%A7%D9%84%D9%8E%D8%A9%D9%8F%29
[18] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11174&title=015-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20Mnyama%20Ambaye%20Rasuli%20Kaamuru%20Kumuua%20Si%20Halali%20Kuliwa
[19] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11175&title=016-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20Mnyama%20Ambaye%20Allaah%20Au%20Rasuli%20Wamekataza%20Kumuua%20Si%20Halali%20Kuliwa
[20] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11176&title=017-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20Vilivyoharamishwa%20Ni%20Halali%20Wakati%20Wa%20Dharura
[21] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11177&title=018-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20Adabu%20Za%20Kula%3A%20Kupiga%20%E2%80%9CBismil%20Laahi%E2%80%9D%20Kabla%20Ya%20Kula%20%20
[22] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11178&title=019-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3AKula%20Kwa%20Mkono%20Wa%20Kulia%2C%20Na%20Kutomega%20Chakula%20Kilicho%20Mbele%20Ya%20Mwingine
[23] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11179&title=020-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20Kula%20Toka%20Pembezoni%20Mwa%20Chakula%20Na%20Si%20Kutoka%20Katikati%20Yake
[24] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11180&title=021-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20Mtu%20Asile%20Huku%20Ameegemea
[25] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11181&title=022-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20Asikitie%20Doa%20Chakula%20Au%20Kukisema%20Vibaya%20Kama%20Hakukipenda
[26] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11182&title=023-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20Watu%20Wale%20Kwa%20Pamoja%20Na%20Mtu%20Asile%20Peke%20Yake%20
[27] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11183&title=024-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20Kulila%20Tonge%20Likianguka%20Baada%20Ya%20Kulipangusa%20Uchafu%20
[28] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11184&title=025-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3AKulamba%20Vidole%20Na%20Sahani%20Kabla%20Ya%20Kuosha%20Mkono%20Au%20Kuupangusa
[29] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11185&title=026-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20Kumhimidi%20Allaah%20Na%20Kuomba%20Du%E2%80%99aa%20Baada%20Ya%20Kumaliza%20Kula
[30] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11186&title=027-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20Kumwombea%20Du%E2%80%99aa%20Aliyeandaa%20Au%20Kualika%20Chakula
[31] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11187&title=028-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20Kuosha%20Mkono%20Ili%20Kuondosha%20Harufu%20%20Ya%20Chakula%20%20%20