Alhidaaya.com
Published on Alhidaaya.com (https://www.alhidaaya.com/sw)

Ukurasa Wa Kwanza > 08-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Kitabu Cha Fadhila Mbalimbali - كِتابُ الْفَضائِل > 44-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Amri kwa Mfungaji Kuhifadhi Ulimi Wake na Viungo Vyake kwa Kwenda Kinyume na Matusi na Mfano Wake

44-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Amri kwa Mfungaji Kuhifadhi Ulimi Wake na Viungo Vyake kwa Kwenda Kinyume na Matusi na Mfano Wake

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب أمر الصائم بحفظ لسانه وجوارحه

عن المخالفات والمشاتمة ونحوها

44-Mlango Wa Amri kwa Mfungaji Kuhifadhi Ulimi Wake na Viungo Vyake kwa Kwenda Kinyume na Matusi na Mfano Wake

 

Alhidaaya.com [1]

 

Hadiyth – 1

عن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قَالَ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( إِذَا كَانَ يَوْمُ صَوْمِ أَحَدِكُمْ ، فَلاَ يَرْفُثْ وَلاَ يَصْخَبْ ، فَإنْ سَابَّهُ أحَدٌ أَوْ قَاتَلَهُ ، فَلْيَقُلْ : إنِّي صَائِمٌ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Ikiwa mmoja wenu amefunga basi asiseme maneno machafu na wala asifanye zogo, kama yeyote (katika watu) ikatokea kumtukana au kupigana naye na aseme, 'Mimi nimefunga'." [Al-Bukhaariy, Muslim, Maalik, Abu Daawuwd na An-Nasaaiy]

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قَالَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ لَمْ يَدَعْ قَوْلَ الزُّورِ وَالعَمَلَ بِهِ فَلَيْسَ للهِ حَاجَةٌ في أنْ يَدَعَ طَعَامَهُ وَشَرَابَهُ )) رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Yeyote ambaye hataacha maneno ya uwongo na matendo machafu, Allaah hana haja kuacha kwake chakula na kinywaji." [Al-Bukhaariy].

 

 

Share [2]
www.alhidaaya.com

Source URL: https://www.alhidaaya.com/sw/node/11224

Links
[1] http://www.alhidaaya.com/
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11224&title=44-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Amri%20kwa%20Mfungaji%20Kuhifadhi%20Ulimi%20Wake%20na%20Viungo%20Vyake%20kwa%20Kwenda%20Kinyume%20na%20Matusi%20na%20Mfano%20Wake