Alhidaaya.com
Published on Alhidaaya.com (https://www.alhidaaya.com/sw)

Ukurasa Wa Kwanza > 07-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: كِتابُ الأيمان وَالنُّذور - Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri > 013-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri: Mwenye Kusema: وَايْمُ اللَّهِ “Waiymul Laah”

013-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri: Mwenye Kusema: وَايْمُ اللَّهِ “Waiymul Laah”

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الأَيْمَانِ وَالنُّذُوْرِ

 

Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri

 

013- Mwenye Kusema: وَايْمُ اللَّهِ “Waiymul Laah”

 

Alhidaaya.com [1]

 

 

 

Yamini inafungika kwa kusema hivyo.  Hili limethibiti toka kwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam).  Katika Hadiyth ya ‘Aaishah, Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

" وَايْمُ اللَّهِ، لَوْ أَنَّ فَاطِمَةَ بِنْتَ مُحَمَّدٍ سَرَقَتْ لَقَطَعَ مُحَمَّدٌ يَدَهَا" 

 

“Naapa kwa Allaah, lau Faatwimah bint Muhammad angeiba, basi Muhammad angeukata mkono wake”.  [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (6788) na Muslim (1688)].

 

Na katika Hadiyth ya Abu Hurayrah toka kwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) -kuhusu kisa cha Nabiy Sulaymaan (‘Alayhis Salaam) ambapo aliapa kuwa atawazungukia wakeze 90 [usiku mmoja na kila mmoja atamzalia mtoto mpanda farasi atakayepigana Jihaad]-, Rasuli anasema:

 

"وَايْمُ الَّذِي نَفْسُ مُحَمَّدٍ بِيَدِهِ لَوْ قَالَ إِنْ شَاءَ اللَّهُ،‏ لَجَاهَدُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ فُرْسَانًا أَجْمَعُونَ "

 

“Naapa kwa Ambaye nafsi ya Muhammad iko Mkononi Mwake, lau angesema: In Shaa Allaah, basi wangelipigana Jihaad katika Njia ya Allaah wakiwa wote wapanda farasi”.  [Hadiyth Swahiyhy.  Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (6639) na Muslim (1654)].

 

Asili ya " وَايْمُ اللَّهِ " ni  " أَيْمٌنُ الله" aymunul Laah, nalo ni jina linalotumika kwa kiapo kwa maana ya “Yamini ya Allaah”.

                                               

 

 

 

Share [2]
www.alhidaaya.com

Source URL: https://www.alhidaaya.com/sw/node/11269

Links
[1] http://www.alhidaaya.com/sw/
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11269&title=013-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Viapo%20Na%20Nadhiri%3A%20Mwenye%20Kusema%3A%20%D9%88%D9%8E%D8%A7%D9%8A%D9%92%D9%85%D9%8F%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%91%D9%8E%D9%87%D9%90%20%E2%80%9CWaiymul%20Laah%E2%80%9D