كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji
Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
العَقِيْقَةُ
‘Aqiyqah (Akika)
Abu Maalik Kamaal Bin As-Sayyid Saalim
Imetarjumiwa na 'Abdullaah Mu'aawiyah (Abu Baasim)
Alhidaaya.com
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
العَقِيْقَةُ
‘Aqiyqah (Akika)
Alhidaaya.com [3]
01-‘Aqiyqah (Akika): Taarifu Yake, Uhalali Wake, Na Hukmu Yake Kisharia:
Asili yake ni neno "العَقُّ" lenye maana ya mpasuko na mkato. Mnyama anayechinjwa huitwa ‘aqiyqah kwa kuwa koo lake hupasuliwa na kukatwa. Pia, unywele unaotoka juu ya kichwa cha mtoto anayezaliwa toka tumboni mwa mama yake huitwa hivyo, ni sawa mtoto wa wanadamu au wa wanyama.
Ama kiistilahi, ni mnyama anayechinjwa kwa mtoto mchanga kwa ajili ya kumshukuru Allaah Ta’aalaa kwa niya na masharti maalum.
· Uhalali Wake Na Hukmu Yake Kisharia:
‘Aqiyqah ni jambo lililoruhusika kisharia kwa mujibu wa kauli ya ‘Ulamaa wote akiwemo Ibn ‘Abbaas, Ibn ‘Umar na ‘Aaishah pamoja na Fuqahaa wa Kitaabi’iyna na Aimmatul Amswaar . Na hii ni kwa dalili hizi zifuatazo:
1- Hadiyth ya Salmaan bin ‘Aamir, amesema: “Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:
"مَعَ الْغُلاَمِ عَقِيقَتُهُ ، فَأَهْرِيقُوا عَنْهُ دَمًا ، وَأَمِيطُوا عَنْهُ الأَذَى "
“Sambamba na kila mtoto (anayezaliwa) pana mnyama wake wa ‘aqiyqah. Basi mwageni damu kwa niaba yake, na mwondosheeni adha”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy ikiwa Mu’allaq, ikiwa imepitishwa (5472), Ahmad ( 4/18), An-Nasaaiy (7/164), Abu Daawuwd (2839) na At-Tirmidhiy (1515)].
2- Hadiyth ya Abu Hurayrah, kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"مَعَ الْغُلَامِ عَقِيقَةٌ ، فَأَهْرِيقُوا عَنْهُ دَمًا ، وَأَمِيْطُوْا عَنهُ الْأَذَى"
“Sambamba na kila mtoto (anayezaliwa) pana mnyama wa ‘aqiyqah. Basi mwageni damu kwa niaba yake, na mwondosheeni adha”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Barraaz (1236) na Al-Haakim (4/238)].
3- Hadiyth ya Samurah bin Jundub, kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"كُلُّ غُلاَمٍ رَهِينَةٌ بِعَقِيقَتِهِ ، تُذْبَحُ عَنْهُ يَوْمَ سَابِعِهِ ، وَيُحْلَقُ ، وَيُسَمَّى"
“Kila mtoto ni rehani kwa mnyama wake wa aqiyqah, huchinjiwa siku yake ya saba, hunyolewa na hupewa jina”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (2838), An Nasaaiy (7/166), At-Tirmidhiy (1522), Ibn Maajah (3165) na wengineo].
4- ‘Aaishah amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"عَنِ اَلْغُلَامِ شَاتَانِ مُكَافِئَتَانِ ، وَعَنْ اَلْجَارِيَةِ شَاةٌ "
“Mtoto wa kiume huchinjiwa kondoo wawili wenye umri sawa, na binti kondoo mmoja”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Ahmad (6/31), At-Tirmidhiy (1513), na Ibn Maajah (3163)].
5- Ibn ‘Abbaas amesema:
"أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَقَّ عَنِ الْحَسَنِ وَالْحُسَيْنِ كَبْشًا كَبْشًا"
“Kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwachinjia (‘aqiyqah) Al-Hasan na Al-Husayn kila mmoja beberu mmoja”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (2841), An-Nasaaiy (7/166) na wengineo. Hadiyth hii ina wenza wengi].
Al-Hasan na Daawuwd wanaona kwamba ‘aqiyqah ni waajib kutokana na amri zilizomo ndani ya baadhi ya Hadiyth hizi. Lakini Jumhuwr ya ‘Ulamaa wanaona kwamba ‘aqiyqah ni jambo lililosuniwa. Na hii ni kwa Hadiyth hii ya Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"مَنْ وُلِدَ لَهُ وَلَدٌ فَأَحَبَّ أَنْ يَنْسُكَ عَنْ وَلَدِهِ فَلْيَفْعَلْ"
“Mwenye kuruzukiwa mtoto na akapenda kumfanyia swadaqah mtoto wake huyo, basi afanye”. Wameifanya Hadiyth hii kuwa imeondosha na kufuta amri zilizomo kwenye Hadiyth zilizotangulia.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
العَقِيْقَةُ
‘Aqiyqah (Akika)
Alhidaaya.com [3]
02-‘Aqiyqah (Akika): Ni Nani Anayepaswa Kuchinja ‘Aqiyqah?
[Subulus Salaam (4/1429) na Al-Mawsuw’ah (30/277)]
Anayetakiwa kuchinja ‘aqiyqah ni baba mtu– au mtu anayewajibikiwa na matumizi ya mtoto- , atamnunua kwa pesa yake na si kwa pesa ya kichanga kilichozaliwa, na mtu mwingine haruhusiwi kufanya hilo ila kwa idhini yake.
Kusema hivi hakukinzani na kitendo cha Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) cha kuwachinjia ‘aqiyqah wajukuu zake Al-Hasan na Al-Husayn. Hii ni kwa kuwepo uwezekaniko wa kwamba yeye Rasuli alikuwa ameyabeba masurufu yao na si wazazi wao, lakini pia kwa kuwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ana haki zaidi kwa Waumini kuliko nafsi zao.
Mashaafi’iy wameshurutisha kwa mwenye kubeba jukumu hilo kuwa awe ni mwenye kujiweza kipesa, awe anaweza kulifanya hilo, na liwe ni la ziada katika mahitaji yake na mahitaji ya wale aliowajibikiwa kuwakimu.
Ama Mahanbali, wao wameeleza kwamba imesuniwa kwa baba kuchinja hata kama hali yake ni ngumu, na anaweza kukopa kama ataweza kulipa. Imaam Ahmad amesema: “Kama hana cha kuchinja, basi akope, nami nataraji Allaah Atampa cha kulipa, kwa kuwa amehuisha Sunnah ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam)”.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
العَقِيْقَةُ
‘Aqiyqah (Akika)
Alhidaaya.com [3]
03-‘Aqiyqah (Akika): Mnyama Anayetosheleza Kwa ‘Aqiyqah:
Tumeitaja Hadiyth ya Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) isemayo:
"عَنِ اَلْغُلَامِ شَاتَانِ مُكَافِئَتَانِ ، وَعَنِ اَلْجَارِيَةِ شَاةٌ "
“Mtoto wa kiume achinjiwe kondoo wawili wenye umri sawa, na binti kondoo mmoja”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Ahmad (6/31), At-Tirmidhiy (1513), Ibn Maajah (3163)].
Kwa mujibu wa Hadiyth hii, wa kiume ni kondoo wawili, na wa kike ni kondoo mmoja. Ni kauli ya Wanachuoni wengi akiwemo Ibn ‘Abbaas na ‘Aaishah. Pia ni kauli ya Ash-Shaafi’iy, Ahmad, Is-haaq na Abu Thawr. [Al-Mughniy (9/363) na Al-Mawsuw’ah (30/279)].
Baadhi ya ‘Ulamaa akiwemo Ibn ‘Umar wamesema kuwa inatosheleza kondoo mmoja kwa mtoto wa kiume na kondoo mmoja kwa mtoto wa kike. Dalili yao ni Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas:
"أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَقَّ عَنِ الْحَسَنِ وَالْحُسَيْنِ كَبْشًا كَبْشًا"
“Kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwachinjia (‘aqiyqah) Al-Hasan na Al-Husayn kila mmoja beberu mmoja”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (2841), An-Nasaaiy (7/166) na wengineo. Hadiyth hii ina wenza wengi].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
العَقِيْقَةُ
‘Aqiyqah (Akika)
Alhidaaya.com [3]
04-‘Aqiyqah (Akika): Je, Mnyama Mwingine Anaweza Kutosheleza Badala Ya Kondoo Au Mbuzi?
Ibn Mulaykah amesema:
"نُفِسَ لِعَبْدِ الرَّحْمنِ بن أَبِيْ بَكْرِ غُلَامٌ ، فَقِيْلَ لِعَائِشَةَ: يا أُمِّ المُؤْمِنِيْنَ ، عُقِّيْ عَنْهُ جَزُوْرًا ، فَقَالَتْ: مَعَاذَ اللهِ ، وَلكِن مَا قَالَ رَسُوْلُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: شَاتَانِ مُكَافِئَتَانِ"
“’Abdurrahmaan bin Abi Bakr aliruzukiwa mtoto wa kiume. ‘Aaishah akaambiwa: Ee Mama wa Waumini! Mfanyie ‘aqiyqah ya ngamia. Akasema: Najilinda kwa Allaah, lakini (nitachinja) kwa mujibu wa alivyosema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam): Kondoo wawili wenye umri sawa”. [Hadiyth Swahiyh. Imetajwa nyuma kidogo].
Na kundi la baadhi ya ‘Ulamaa wamesema kwamba achio la kutoainisha aina ya mnyama katika kauli yake Rasuli فَأَهْرِيقُوا عَنْهُ دَمًا “Basi mwageni damu kwa niaba yake”, linaainishwa na kauli yake nyingine:
"عَنِ اَلْغُلَامِ شَاتَانِ مُكَافِئَتَانِ ، وَعَنْ اَلْجَارِيَةِ شَاةٌ "
“Mtoto wa kiume huchinjiwa kondoo wawili wenye umri sawa, na binti kondoo mmoja”. Na kwa muktadha huu, ‘aqiyqah haijuzu ila kwa kondoo au mbuzi tu.
Na mnyama anayechinjwa ni lazima asiwe na kasoro yoyote inayozuia chinjo hili la kiibada. Lakini Ibn Hazm amesema kwenye kitabu chake cha Al-Muhallaa: “Anatosheleza katika ‘aqiyqah mnyama mwenye kasoro, ni sawa kasoro zinazojuzisha kwa mnyama wa udhwhiyah, au zile zisizojuzisha, lakini aliyekamilisha vigezo ni bora zaidi”.
Ninasema: “Linatosha Neno Lake Ta’aalaa:
"وَلَا تَيَمَّمُوا الْخَبِيثَ مِنْهُ تُنفِقُونَ"
“Na wala msikusudie vibaya kutoka humo mkavitoa”. [Al-Baqarah: 267]
Na kauli yake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"إِنَّ اللَّهَ طَيِّبٌ لَا يَقْبَلُ إِلَّا طَيِّبًا"
“Hakika Allaah Ni Mzuri na Hakubali isipokuwa kilicho kizuri tu”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (1015) na wengineo].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
العَقِيْقَةُ
‘Aqiyqah (Akika)
Alhidaaya.com [3]
05-‘Aqiyqah (Akika): Miongoni Mwa Hukumu Za ‘Aqiyqah:
1- Wakati Wake:
Ni Sunnah mtoto achinjiwe siku yake ya saba ya kuzaliwa. Ni kwa Hadiyth ya Samurah bin Jundub: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"الغُلاَمُ رَهِينَةٌ بِعَقِيقَتِهِ ، تُذْبَحُ عَنْهُ يَوْمَ سَابِعِهِ ، وَيُحْلَقُ ، وَيُسَمَّى"
“Mtoto ni rehani kwa mnyama wake wa aqiyqah, huchinjiwa siku yake ya saba, hunyolewa, na hupewa jina”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (2838), An Nasaaiy (7/166), At-Tirmidhiy (1522), Ibn Maajah (3165) na wengineo].
Kama siku ya saba itapita, basi iwe siku ya kumi na nne, na hii nayo ikipita, basi iwe siku ya ishirini na moja. Wameyasema haya Mahanbali na Is-haaq. Kadhalika, limesimuliwa hili toka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaah ‘anhaa).
Wengine wamesema kuwa ikiwa atachinjiwa kabla ya siku saba au baada yake, basi itatosheleza, kwa kuwa makusudio yanapatikana.
Nao Mashaafi’iy kwa upande wao, wanasema kwamba ‘aqiyqah haipiti kwa kuichelewesha, lakini imestahabiwa kuwa isicheleweshwe zaidi ya umri wa kubaleghe. Kama itacheleweshwa mpaka akabaleghe, basi hukumu yake itadondoka kwa baba wa mtoto, naye mtoto atakuwa na khiyari ya kujichinjia mwenyewe. [Al-Mughniy (9/364) na Al-Mawsuw’ah (30/278)].
2- Kuchinja Mnyama Ni Bora Zaidi Kuliko Kutoa Thamani Yake:
Kwa kuwa tendo la kuchinja na kumwagika damu ndilo linalokusudiwa, kwani tendo hilo ni ‘ibaadah iliyofungamanishwa pamoja na Swalaah kama Alivyosema Allaah Ta’aalaa:
"فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ"
“Basi swali kwa ajili ya Rabb wako na chinja”. [Al-Kawthar: 02].
Isitoshe, kuchinja ni mwongozo wa Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam), lakini pia ni Sunnah yake ambayo hatutakiwi tujiengue nayo.
3- Haiswihi Kushirikiana Mnyama Mmoja Katika ‘Aqiyqah:
Mnyama mmoja hatoshelezi isipokuwa kwa mtu mmoja tu. Ni kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"مَعَ الْغُلاَمِ عَقِيقَتُهُ ، فَأَهْرِيقُوا عَنْهُ دَمًا ، وَأَمِيطُوا عَنْهُ الأَذَى"
”Sambamba na kila mtoto (anayezaliwa), pana mnyama wake wa ‘aqiyqah. Basi mwageni damu kwa niaba yake, na mwondosheeni adha”. [Hadiyth Swahiyh. Imetajwa nyuma].
Na kauli yake nyingine:
"كُلُّ غُلاَمٍ رَهِينَةٌ بِعَقِيقَتِهِ ، تُذْبَحُ عَنْهُ يَوْمَ سَابِعِهِ ، وَيُحْلَقُ ، وَيُسَمَّى"
“Kila mtoto ni rehani kwa mnyama wake wa ‘aqiyqah, huchinjiwa siku yake ya saba, hunyolewa, na hupewa jina”. [Hadiyth Swahiyh. Imetajwa nyuma kidogo].
Kwa mujibu wa Hadiyth hizi, ni kuwa kila mtoto achinjiwe mnyama wake anayemhusu yeye tu, na hakuna ruhusa yoyote iliyowekwa ya kushirikiana watu mnyama mmoja kama ilivyo kwenye wanyama wa kuchinja kwenye Hijja au udhwhiyah.
4- Hakuna Hadiyth Yoyote Swahiyh Inayozuia Kuvunja Mifupa Ya Mnyama Wa ‘Aqiyqah:
Hakuna pia hata ukaraha wa hilo, hakuna lolote lililothibiti kutoka kwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam), wala hata amri ya kumtuma mwanaume aende kwa mkunga (kupeleka nyama).
5- Kichanga Hakigusishwi Chochote Katika Damu Ya Mnyama:
Hili ni katika ada na desturi za kijahilia ambalo Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alilikataza, na akalibadili hilo kwa kumnyoa kichwa, na kutoa swadaqah ya fedha kwa uzito wa nywele zake. Al-Buraydah (Radhwiya Allaah ‘anhu amesema:
"كُنَّا فِي الْجَاهِلَيَّةِ إِذَا وُلِدَ لِأَحَدِنَا غُلَامٌ ، ذَبَحَ شاةً وَلَطَّخَ رَأْسَهُ بِدَمِهِ ، فَلَمَّا جَاءَ الْإِسْلَامُ كُنَّا نَذْبَحُ الشَّاةَ يَوْمَ السَّابِعِ ، وَنَحْلِقُ رَأْسَهُ ، وَنُلَطِّخُهُ بِزَعْفَرَانٍ"
“Tulikuwa wakati wa ujahilia, anaporuzukiwa mmoja wetu mtoto, anachinja kondoo na kukipaka kichwa chake (mtoto) damu yake (kondoo). Na Uislamu ulipokuja, tukawa tunachinja kondoo siku ya saba (ya kuzaliwa mtoto), tunanyoa kichwa chake, na tunakipaka zafarani”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (2843), At-twahhaawiy (1/460) na Al-Haakim (4/238)].
‘Aaishah (katika Hadiyth ya ‘aqiyqah) amesema:
"وَكَانَ أَهْلُ الجَاهِلِيَّةِ يَجْعَلُوْنَ قُطْنَةً فِي دَمِ العَقِيْقَةِ ، وَيَجْعَلُوْنَهُ عَلَى رَأْسِ الصَّبِي ، فَأَمَرَ رَسُوْلُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنْ يُجْعَلَ مَكَانَ الدَّمِ خَلُوْقًا"
“Watu wa enzi ya ujahilia, walikuwa wakichovya pamba kwenye damu ya mnyama wa ‘aqiyqah, kisha huipaka juu ya kichwa cha mtoto. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaja kuamuru liwekwe nukato lolote zuri mahala pa damu (kichwani)”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Ibn Hibaan (1057) na Al-Bayhaqiy (9/303)].
6- Inapendeza Kuipika Nyama Badala Ya Kuitoa Mbichi:
Sababu ya hili ni kuwaondoshea masikini na majirani gharama za kupika. Na hii ni nyongeza ya ihsani kwao sambamba na kuishukuru zaidi neema hii, mbali na kuwa kielelezo cha tabia njema na utoaji.
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/284
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11438&title=08D-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20%D9%83%D9%90%D8%AA%D9%8E%D8%A7%D8%A8%D9%8F%20%D8%A7%D9%84%D8%A3%D9%8E%D8%B7%D9%92%D8%B9%D9%90%D9%85%D9%8E%D8%A9%D9%90%20%D9%88%D9%8E%D8%A7%D9%84%D8%A3%D9%8E%D8%B4%D9%92%D8%B1%D9%90%D8%A8%D8%A9%D9%90%20%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20%D8%A7%D9%84%D8%B9%D9%8E%D9%82%D9%90%D9%8A%D9%92%D9%82%D9%8E%D8%A9%D9%8F%20-%20%27Aqiyqah
[3] http://www.alhidaaya.com/
[4] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11439&title=01-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20Vinywaji%3A%20%20Taarifu%20Yake%2C%20Uhalali%20Wake%2C%20Na%20Hukmu%20Yake%20Kisharia%20
[5] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11440&title=02-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20%E2%80%98Aqiyqah%20%28Akika%29%3A%20Ni%20Nani%20Anayepaswa%20Kuchinja%20%E2%80%98Aqiyqah%3F
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11441&title=03-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3AAqiyqah%20%28Akika%29%3A%20Mnyama%20Anayetosheleza%20Kwa%20%E2%80%98Aqiyqah
[7] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11442&title=04-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%E2%80%98Aqiyqah%20%28Akika%29%3A%20Je%2C%20Mnyama%20Mwingine%20Anaweza%20Kutosheleza%20Badala%20Ya%20Kondoo%20Au%20Mbuzi%3F
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11443&title=05-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%E2%80%98Aqiyqah%20%28Akika%29%3A%20Miongoni%20Mwa%20Hukumu%20Za%20%E2%80%98Aqiyqah