كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji
Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
الأَشْرِبَةُ
Vinywaji
Abu Maalik Kamaal Bin As-Sayyid Saalim
Imetarjumiwa na 'Abdullaah Mu'aawiyah (Abu Baasim)
Alhidaaya.com
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
الأَشْرِبَةُ
Vinywaji
Alhidaaya.com [3]
01- Vinywaji: Taarifu Yake Na Asili Ya Uhalali Wake:
Vinywaji "الأَشْرِبَةُ" , ni wingi wa "شَرَابُ" kinywaji, na "الشَّرَابُ" ni jina la chochote kinachonywewa kwa aina yake yoyote kiwavyo, ni sawa yawe maji au kinginecho, na kwa hali yoyote kiwavyo, na kila kitu kisichotafunwa, basi husemwa kuwa kinanywewa. [Lisaanul ‘Arab na Mukhtaar As-Swihaah].
· Asili Ya Vinywaji Vyote Ni Halali Ila Vile Vilivyoharamishwa Na Qur-aan Au Hadiyth:
Ni kwa ujumuishi wa dalili zilizotajwa kwenye mlango wa vyakula nyuma zinazothibitisha uasili wa uhalali, lakini pia kwa Hadiyth ya Anas bin Maalik (Radhwiya Allaah ‘anhu):
" لَقَدْ سَقَيْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِهَذَا الْقَدَحِ الشَّرَابَ كُلَّهُ، الْمَاءَ، وَالنَّبِيذَ، وَالْعَسَلَ، وَاللَّبَنَ"
“Kwa hakika nilimnywesha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) vinywaji vyote kwa kikombe hiki; maji, juisi ya zabibu, asali, na maziwa”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (2008) na At-Tirmidhiy katika Ash-Shamaail (1/294)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
الأَشْرِبَةُ
Vinywaji
Alhidaaya.com [3]
002- Vinywaji: Pombe Kwa Aina Zake Zote Ni Haramu
Hili limethibiti katika Qur-aan, Sunnah na Ijmaa. Katika Qur-aan, Allaah Ta’aalaa Anasema:
"يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْخَمْرُ وَالْمَيْسِرُ وَالْأَنصَابُ وَالْأَزْلَامُ رِجْسٌ مِّنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ فَاجْتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿٩٠﴾ إِنَّمَا يُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَن يُوقِعَ بَيْنَكُمُ الْعَدَاوَةَ وَالْبَغْضَاءَ فِي الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ وَيَصُدَّكُمْ عَن ذِكْرِ اللَّـهِ وَعَنِ الصَّلَاةِ ۖ فَهَلْ أَنتُم مُّنتَهُونَ ﴿٩١﴾
“Enyi walioamini! Hakika pombe, kamari, masanamu na kutazamia kwa mishale ya kupigia ramli, ni najisi na chukizo kutokana na kazi ya shaytwaan, basi jiepusheni navyo mpate kufaulu • Hakika shaytwaan anataka kukutilieni baina yenu uadui na bughudha katika pombe na kamari na akuzuieni kumdhukuru Allaah na Swalaah, basi je mtakoma?”. [Al-Maaidah: 90-91].
Uharamisho wa pombe katika Aayaah hizi mbili, umepewa uzito kwa picha kadhaa za usisitizo. Miongoni mwazo ni:
(a) Kutanguliwa Aayah na herufi ya "إِنَّمَا" . Na hii ni herufi ya usisitizo na kulipa jambo uzito.
(b) Allaah Ta’aalaa Ameiweka kundi moja na ibada ya masanamu.
(c) Ameifanya kuwa ni najisi.
(d) Ameifanya kuwa ni kazi ya shaytwaan, na shaytwaan haji isipokuwa na shari tupu.
(e) Ameamuru iepukwe.
(f) Amekufanya kuiepuka ndio mafanikio, hivyo basi, kuinywa hatima yake ni mbaya, lakini pia kunaondosha kheri na baraka zote.
(g) Ametaja matokeo yake mabaya, nayo ni kuzalikana uadui na mizozano kwa wanywaji na wadau wake, mbali na kumzuia mtu asiweze kumdhukuru Allaah na kuchunga nyakati za Swalaah.
(h) Kauli Yake Ta’aalaa: "فَهَلْ أَنتُم مُّنتَهُونَ" basi je mtakoma?.. ni maneno ya nguvu kabisa yaliyofikia ukomo wa mwisho wa kukemea. Ni kama wanaambiwa: Hakika mmesomewa ndani yake madhara yake mbalimbali na namna inavyowazuieni kumdhukuru Allaah, basi je mtaiacha pombe kwa sababu ya madhara haya, au mtaendelea na tabia yenu mliyokuwa nayo, iwe kama hamkuonywa wala kukemewa?!
Ama katika Sunnah, Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"لَعَنَ اللَّهُ الْخَمْرَ، وَشَارِبَهَا، وَسَاقِيَهَا، وَبَائِعَهَا، وَمُبْتَاعَهَا، وَعَاصِرَهَا، وَمُعْتَصِرَهَا، وَحَامِلَهَا، وَالْمَحْمُولَةَ إِلَيْهِ"
“Allaah Ameilaani pombe, mnywaji wake, mhudumu wake, muuzaji wake, mnunuzi wake, mkamuaji wake, mwenye kukamuliwa, mchukuzi wake na mwenye kupelekewa”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (3674), At-Tirmidhiy (1295) na Ibn Maajah (3380)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
الأَشْرِبَةُ
Vinywaji
Alhidaaya.com [3]
003- Vinywaji: Chochote Chenye Kulewesha Ni Pombe:
Jumhuwr ya ‘Ulamaa wakiwemo Watu wa Madiynah na Hijaaz, Ahlul Hadiyth, Mahanbali, na baadhi ya Mashaafi’iy, wanaona kwamba kila kinacholewesha, basi ni pombe kihakika, ni sawa kiwe kimetengenezwa kutokana na zabibu, au tende, au ngano, au shayiri au mada nyinginezo. [Ibn ‘Aabidiyna (5/277), Al-Mudawwanah (6/261), Ad-Dusuwqiy (4/353), Ar-Rawdhwah (10/168) na Al-Mughniy (9/159)].
Dalili zao ni:
1- Kauli ya Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"كُلُّ مُسْكِرٍ حَرَامٌ ، إِنَّ عَلَى اللَّهِ عَهْدًا لِمَنْ يَشْرَبُ الْمُسْكِرَ أَنْ يَسْقِيَهُ مِنْ طِينَةِ الْخَبَالِ . قَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ وَمَا طِينَةُ الْخَبَالِ؟ قَالَ: عَرَقُ أَهْلِ النَّارِ أَوْ عُصَارَةُ أَهْلِ النَّار"
“Kila kinacholewesha ni haramu. Na kwa hakika Allaah Amemwekea ahadi mwenye kunywa chenye kulewesha kwamba Atamnywesha “Twiynatul Khabaal”. Wakauliza ni nini “Twiynatul Khabaal?”. Akasema: Ni jasho la watu wa motoni, au ni usaha wa watu wa motoni. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (2002), An Nasaaiy (8/327) na Ahmad (3/321)].
Na katika tamko la Muslim:
"كُلُّ مُسْكِرٍ خَمْرٌ، وَكُلُّ خَمْرٍ مُسْكِرٍ "
“Chochote chenye kulewesha ni pombe, na pombe yoyote inalewesha”.
2- ‘Umar amesema:
"نَزَلَ تَحْرِيمُ اَلْخَمْرِ وَهِيَ مِنْ خَمْسَةٍ: مِنَ اَلْعِنَبِ ، وَالتَّمْرِ ، وَالْعَسَلِ ، وَالْحِنْطَةِ ، وَالشَّعِيرِ. وَالْخَمْرُ: مَا خَامَرَ اَلْعَقْلَ"
“Kuharamishwa pombe kulishuka ikiwa inatengenezwa kutokana na mali ghafi tano: Zabibu, tende, asali, ngano na shayiri. Na khamr (pombe), ni kile kinachoziba akili”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5581) na Muslim (3032)].
3- Ni kwa kuwa iliposhuka Aayaah ya kuharamisha pombe, Maswahaba – ambao ndio wenye kuielewa vizuri lugha yao- walifahamu kwamba chochote kinachoitwa pombe, basi kinaingia ndani ya marufuku hiyo, na hapo ndipo walipomwaga pombe zote zilizotengenezwa kwa tende kavu (tamr) na “rutwab”, kwa kuwa pombe iliharamishiwa Madiynah, na Madiynah hakukuwa na zabibu. Hawakuwa wakinywa kingine chochote zaidi ya kilichotengenezwa kwa “busr” (tende mbichi) na tende kavu, huku tukizingatia kuwa pombe (khamr) imeitwa hivyo, kwa kuwa inafunika akili, inaipoteza na inaiziba, na hivyo ikahusisha kila chenye kulewesha.
Tunda la mtende lina awamu tano. “Twal-‘u”, “Balah”, “Busr”, “Rutwab”, na hatimaye “Tamr” ambapo huwa limekomaa barabara na kuwa ngumu.
Na Mashaafi’iy wengi, wanafunzi wa Abu Haniyfah na baadhi ya Wamaalik, wanaona kwamba pombe ni ile yenye kulewesha, lakini iwe imetengenezwa kutokana na maji ya zabibu yanapochachuka, ni sawa yawe yametiwa siagi au la.
· Faida Mbili:
Faida ya kwanza: Kama kingi kinalewesha, basi kidogo chake pia ni haramu.
Hili limekubaliwa na Jumhuwr ya ‘Ulamaa wote. Ni kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"كُلُّ مَا أَسْكَرَ حَرَامٌ ، وَمَا أَسْكَرَ الْفَرْقُ فَمِلْءُ الْكَفِّ مِنْهُ حَرَامٌ "
“Kila kinacholewesha ni haramu. Na chochote chenye kulewesha kwa kiasi cha ratili 120, basi hata kwa kiasi cha kujaza kiganja kwacho pia ni haramu”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (3687) na At-Tirmidhiy (1928)].
Faida ya pili: Kila chenye kuondosha akili, basi ni pombe.
Ni kwa neno la ‘Umar: "وَالْخَمْرُ: مَا خَامَرَ اَلْعَقْلَ" Na khamr (pombe), ni kile kinachoziba akili”. [Hadiyth Swahiyh. Imetajwa nyuma kidogo].
Vinavyoingia hapa ni pamoja na hashishi, afyuni, heroin, bangi na mfano wake katika mihadarati. Vyote hivyo ni haramu kwa Ijmaa ya Fuqahaa kwa Hadiyth ya Ummu Salamah:
"أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّمَ نَهَى عَنْ كُلِّ مُسْكِرٍ وَمُفَتِّرٍ "
“Kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kila chenye kulewesha, na kila chenye kupoozesha nguvu za viungo vya mwili”. [Isnaad yake ni dhwa’iyf. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (3686) na Ahmad (6/254)].
Sheikh wa Uislamu amesema: “Hashishi hii kavu ni haramu, nayo inalewesha. Na wanaoitumia ni watu wasiojali maasi wala dhambi, kwa sababu ina handasi na inavuruga akili, na kinywaji kinacholewesha kinafanana nayo katika hilo. Pombe nayo humchemsha mtu akaweza kufanya lolote na kuwa mgomvi, na hashishi hii huleta mpoozo wa viungo vya mwili na udhaifu”.
Kisha akaendelea kusema: “Na mwenye kuihalalisha na akadai kwamba ni halali, basi mtu huyo atatubishwa. Kama atatubu, basi ataachiwa, na akikataa, basi atauliwa kwa kuwa ameritadi. Kwani kila chenye kuidhuru akili, basi hicho ni haramu kwa Ijmaa ya Waislamu”. [Majmuw’ul Fataawaa. Angalia: Ibn ‘Aabidiyna (6/457), Subulus Salaam (4/1322) na Az Zawaajir cha Al-Haythamiy (1/172)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
الأَشْرِبَةُ
Vinywaji
Alhidaaya.com [3]
004- Vinywaji: Kunywa Pombe Kwa Aliyelazimika:
[Al-Muhallaa (7/426), Fat-hul Qadiyr (9/28), Ad-Dusuwqiy (4/353) na Mughnil Muhtaaj]
Kuharamishwa pombe kama tulivyoeleza nyuma, kunakuwa katika hali ya kawaida. Lakini ikiwa katika hali ya kulazimika, hapo mtu ataruhusiwa kunywa pombe lakini kwa mujibu wa vipimo vya kisheria vinavyohalalisha vilivyoharamishwa. Ni kama dharura ya kubanwa na kiu kikali ambapo mtu anahofia kufa (na hana maji), au kukabwa na kitu kooni, au kulazimishwa. Mtu huyo aliyelazimika atakunywa kwa kiasi cha kuondoka tatizo tu. Allaah Ta’aalaa Anasema:
"وَقَدْ فَصَّلَ لَكُم مَّا حَرَّمَ عَلَيْكُمْ إِلَّا مَا اضْطُرِرْتُمْ إِلَيْهِ"
“Na ilhali Ameshafasilisha waziwazi kwenu yale Aliyokuharamishieni isipokuwa vile mlivyofikwa na dharura navyo.” [Al-An’aam: 119].
Hapa Allaah Ta’aalaa Ameondosha uharamisho wa vya haramu vilivyofasiliwa katika hali ya dharura. Amesema ni vyote (vinahalalika katika hali hiyo), na wala Hakuainisha kimoja nje ya vingine. Hivyo haifai kulifanyia umahususi hili.
Wamaalik wamekataza kunywa pombe ili kuondosha kiu. Wanadai kwamba haiondoshi kiu, bali inaongeza joto na ukavu kooni. Madai yao haya yanajibiwa wakiambiwa kwamba imethibiti kwamba walevi wengi makafiri na watu wasiojali mafundisho ya dini, hawanywi kabisa maji pamoja na kunywa kwao pombe.
Kwa hali yoyote, Aayah hii ni jumuishi kama tulivyosema, na haijuzu kuzuia pombe isinywewe wakati mtu anapohofia kufa kwa kiu. Linalokatazwa ni kuinywa kwa ajili ya kuondosha kiu cha kawaida, na kama si kiu cha kawaida, basi haijuzu kuzuia (ili kuokoa maisha) kama alivyosema Sheikh wa Uislamu. [Angalia: Majmuw’ul Fataawaa (14/471)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
الأَشْرِبَةُ
Vinywaji
Alhidaaya.com [3]
005- Vinywaji: Haijuzu Kumiliki Pombe Wala Kummilikisha Mwingine:
Ni haramu kwa Muislamu kumiliki au kumilikisha pombe kwa sababu yoyote kati ya sababu za umiliki wa kihiari au wa mtu mwenyewe kutaka. Ni kama kuuza, au kununua, au kutunuku na mfano wake. Ni kutokana na neno lake Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"إِنَّ الَّذِي حَرَّمَ شُرْبَهَا حَرَّمَ بَيْعَهَا "
“Hakika Yule Aliyeharamisha kuinywa, Ameharamisha (pia) kuiuza”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (1579), An-Nasaaiy (4664) na Ad-Daaramiy (2103)].
Jaabir kasema: “Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:
"إِنَّ اللَّهَ وَرَسُولَهُ حَرَّمَ بَيْعَ الْخَمْرِ وَالْمَيْتَةِ وَالْخِنْزِيرِ وَالْأَصْنَامِ"
“Hakika Allaah na Rasuli Wake Wameharamisha kuuza pombe, mfu, nguruwe na masanamu”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (2236) na Muslim (1581)].
· Mtu Akiharibu Pombe Ya Mtu, Je, Atalipa?
Fuqahaa wamekubaliana kwamba ikiwa pombe ni mali ya Muislamu, basi atakayeiharibu halipi. Lakini wamekhitalifiana kuhusu aliyeharibu pombe ya asiye Muislamu anayeishi chini ya utawala wa Kiislamu (dhimmiy). Mahanafiy na Wamaalik wamesema atalipa!! Na Mashaafi’iy na Mahanbali wamesema hatalipa, kwa kuwa haina sifa ya kutiwa thamani kama zilivyo najisi nyinginezo.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
الأَشْرِبَةُ
Vinywaji
Alhidaaya.com [3]
006- Vinywaji: Pombe Ikigeuka Siki:
1- Pombe ikigeuka yenyewe kuwa siki bila ya mtu kukusudia kuichechusha, basi siki hiyo, bila makhitilafiano yoyote kati ya Fuqahaa, inakuwa halali kuitumia. Ni kwa Hadiyth ya Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"نِعْمَ الْإِدَامُ الْخَلُّ"
“Kitowezeo bora kabisa ni siki”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (2051), At-Tirmidhiy (1829), An-Nasaaiy (3796) na Abu Daawuwd (3820)].
Ugeukaji wa kuwa siki unajulikana kwa kubadilika ladha ya pombe ambayo ni chungu kuwa na ladha ya tindi kali.
2- Ikiwa pombe itageuzwa siki kwa kutiwa kitu ndani yake kama siki, kitunguu au chumvi, au ikawashiwa moto pembeni yake, kwa hili, ‘Ulamaa wamekhitilafiana katika kauli mbili kuhusu hukmu yake:
[Al-Muhallaa (7/433), Al-Badaai’u (5/114), Al-Qawaaniynul Fiqhiyyah (34), Al-Mughniy (9/145) na Naylul Awtwaar (8/214)].
Kauli ya kwanza:
Haijuzu kuigeuza siki, na siki yenyewe si halali kuitumia. Ni kauli ya ‘Umar bin Al-Khattwaab (Radhwiya Allaah ‘anhu). Pia ni madhehebu ya Shaafi’iy na Hanbali, na riwaayah iliyonukuliwa toka kwa Maalik. Dalili zao ni:
1- Ni kwamba kuigeuza siki ni sawa na kuikumbatia pombe kwa njia ya kujinufaisha, na hii ni kinyume na Amri ya Allaah Aliyetutaka tujiepushe na tujiweke mbali nayo katika Neno Lake:
"فَاجْتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ"
“Basi jiepusheni nayo, mpate kufaulu”. [Al-Maaidah: 90]
2- Hadiyth ya Anas:
"سُئِلَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنِ الْخَمْرِ تُتَّخَذُ خَلاًّ ، فَقَالَ: لاَ "
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliulizwa kuhusu kuitumia pombe ili kutengenezea siki, akasema: Hapana”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (1984) na wengineo].
Na katika tamshi:
"أَنَّ أَبَا طَلْحَةَ ، سَأَلَ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ أَيْتَامٍ وَرِثُوا خَمْرًا ، قَالَ: "أَهْرِقْهَا" . قَالَ: أَفَلاَ نَجْعَلُهَا خَلاًّ ؟ قَالَ: "لاَ".ٍ
“Kwamba Abu Twalha alimuuliza Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu mayatima waliorithi pombe. Rasuli akamwambia: Imwage. Akamuuliza: Kwa nini basi tusiifanye siki? Akasema: Hapana”. [Imekharijiwa na Abu Daawuwd (3675) na Ahmad (3/119)].
Katazo hili linahukumia haramisho. Lau kama ingelikuweko njia ya kuibadilisha ili iweze kutumika kwa manufaa, basi isingelijuzu kuimwaga, lakini pia Rasuli angeliwaelekeza kwa umahususi jambo hilo la kuibadilisha na hususan wakizingatiwa hao ni mayatima ambao ni haramu mtu kufanya lolote la kudhuru mali yao.
3- Mtu mmoja alimuuliza Ibn ‘Abbaas kuhusu pombe inayotengenezwa kutokana na maji ya zabibu, Ibn ‘Abbaas akamwambia:
"أَهْدَى رَجُلٌ لِرَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ رَاوِيَةَ خَمْرٍ ، فَقَالَ لَهُ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: " أَمَا عَلِمْتَ أَنَّ اللَّهَ حَرَّمَهَا؟" . قَالَ لاَ . فَسَارَّهُ رَجُلٌ إِلَى جَنْبِهِ . فَقَالَ لَهُ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ َ: "بِمَ سَارَرْتَهُ؟" . فَقَالَ: "أَمَرْتُهُ أَنْ يَبِيعَهَا" . فَقَالَ لَهُ رَسُولُ اللَّهِ َ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "إِنَّ الَّذِي حَرَّمَ شُرْبَهَا حَرَّمَ بَيْعَهَا " . فَفَتَحَ الرَّجُلُ الْمَزَادَتَيْنِ حَتَّى ذَهَبَ مَا فِيهِمَا"
“Mtu mmoja alimpa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) zawadi ya kiriba cha pombe. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: Je, hujui kwamba Allaah Ameiharamisha? Akasema hapana. Mtu pembeni yake akamnong’oneza. Rasuli akamuuliza: Umemnong’oneza nini? Akasema: Nimemwamuru aiuze. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: Hakika Yule Aliyeharamisha kuinywa, Ameharamisha (pia) kuiuza”. Mtu yule akayafungulia magudulia mawili mpaka yakabakia matupu”. [Hadiyth Swahiyh. Imetajwa nyuma].
4- ‘Umar (Radhwiya Allaah ‘anhu) alipanda mimbari akasema:
"لا تَأْ كُلْ خَلاًّ مِنْ خَمْرٍ أُفْسِدَتْ ، حَتَّى يَبْدَأَ اللهُ تَعَالَى إِفْسَادَهَا ، وذلِكَ حِيْنَ طَابَ الخَلُّ ، وَلَا بَأْسَ عَلَى امْرِئٍ أَصَابَ خَلاًّ مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ أَنْ يَبْتَاعَهُ ما لَمْ يَعْلَمْ أَنَّهُمْ تَعَمَّدُوا إِفْسَادَهَا"
“Usile siki itokanayo na pombe iliyochachuliwa mpaka Allaah Aichachue (ichachuke yenyewe). Na hakuna ubaya kwa mtu kununua siki kama ataipata kwa Watu wa Kitabu (Ahlul Kitaab) madhali hakujua kwamba waliichachua (pombe yake) kwa makusudi”. [Imekharijiwa na Abu ‘Ubayd katika “Al-Amwaal” (uk. 104)].
Kauli hii imetangaa kwa watu, kwa kuwa ni tangazo la hukmu kwa watu juu ya mimbari, na hakuna yeyote aliyeipinga.
Kauli ya pili:
Inajuzu kuichechusha, na siki yake ni halali kuila. Ni madhehebu ya Hanafiy, kauli yenye nguvu kwa Wamaalik, ni kauli pia ya Abu Muhammad bin Hazm. Dalili zao ni:
1- Kuichechusha ni kuitengeneza ili iweze kufaa na kutumika, na hili linaruhusika kwa kuchukulia qiyaas cha kuisafisha ngozi ya mnyama kwa madawa, na kwa kufanya hivyo ngozi inatwaharika na inafaa kuitumia.
2- Yaliyosimuliwa kwa njia Marfuw’u -kuhusiana na ngozi ya kondoo mfu-:
"إنَّ دِبَاغَهَا يُحِلُّهُ كَمَا يُحِلُّ الخَلُّ الخَمْرَ"
“Hakika kuisafisha kwa madawa kunaihalalisha kama siki inavyohalalisha pombe”. Lakini Hadiyth hii ni Dhwa’iyf, nayo imekharijiwa na Ad-Daaraqutwniy (4/266).
3- Yaliyosimuliwa kwa njia Marfuw’u:
"خَيْرُ خَلِّكُمْ، خَلُّ خَمْرِكُمْ"
“Siki yenu iliyo bora zaidi, ni siki ya pombe yenu”. Hii pia ni Dhwa’iyf. Imekharijiwa na Al-Bayhaqiy katika “Al-Ma-’arifah. Angalia “Naswbur Raayah (4/311).
4- Ni kwa ujumuishi wa neno lake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"نِعْمَ الْإِدَامُ الْخَلُّ"
“Kitowezeo bora kabisa ni siki”. [Hadiyth Swahiyh. Imetajwa nyuma kidogo].
Katika Hadiyth hii, Rasuli hakutofautisha kati ya pombe inayochechuka yenyewe kuwa siki na pombe inayochechushwa.
5- Kwa kuwa kuigeuza kuwa siki kunaondosha sifa inayoifanya isifae, na kuifanya pombe kuwa na sifa ya kufaa, au kukifanya kitu kiwe kinafaa ni jambo linaloruhusika, kwa kuwa kunafanana na kuimwaga pombe.
· Kauli yenye nguvu:
Linaloonekana ni kuwa dalili za kundi la kwanza ndizo zenye nguvu zaidi. Na kwa muktadha huo, ni haramu kuichechusha pombe ili iwe siki. Lakini ikiwa mtu atapewa zawadi siki iliyotengenezwa, basi hakuna ubaya kwake kuitumia, kwa kuwa sifa ya ubovu inakuwa ishaondoka. Lakini pamoja na hivyo, haijuzu kwake kuinunua, kwa kuwa atakuwa anasaidia jambo la dhambi, na Allaah Amesema:
"وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ ۖ وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۖ إِنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ"
“Na shirikianeni katika wema na taqwa, na wala msishirikiane katika dhambi na uadui. Na Mcheni Allaah, hakika Allaah Ni Mkali wa Kuakibu”. [Al-Maaidah: 02].
Ama pombe iliyogeuka yenyewe na kuwa siki, hii haina ubaya kuinunua au kuitumia, kama ilivyotangulia. Na Allaah Ndiye Mjuzi zaidi.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
Alhidaaya.com [3]
الأَشْرِبَةُ
Vinywaji
007- Vinywaji: Haijuzu Kutumia Pombe Kama Dawa:
Jumhuwr ya ‘Ulamaa wameharamisha kutumia pombe (au vyote nyenye kulewesha) kama dawa, bali pia wanaona kwamba mwenye kuinywa kama dawa, basi atapewa adhabu ya kisharia (hadd). Uharamisho huu unatiliwa nguvu na haya yafuatayo:
1- Hadiyth ya Twaariq bin Suwayd Al-Ju-’ufiy:
"أَنَّهُ سَأَلَ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنِ الْخَمْرِ ، فَنَهَاهُ أَوْ كَرِهَ أَنْ يَصْنَعَهَا ، فَقَالَ إِنَّمَا أَصْنَعُهَا لِلدَّوَاءِ ، فَقَالَ : إِنَّهُ لَيْسَ بِدَوَاءٍ وَلَكِنَّهُ دَاءٌ"
“Kwamba alimuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu hukmu ya pombe. Rasuli akamkataza, au hakuonyesha kufurahishwa yeye kuitengeneza. Akamwambia: Ninaitengeneza kwa ajili ya dawa tu, na si kwa jinginelo. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: Hiyo si dawa, bali ni ugonjwa”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (1984)].
Sheikh wa Uislamu amesema: “Maneno haya yanayogusia kuzuia kujitibu kwa kutumia pombe, ni jibu kwa aliyeruhusu. Na vingine vilivyoharamishwa ni sawa na pombe kwa qiyaas, kinyume na waliotenganisha kati ya viwili hivi”. [Majmuw’ul Fataawaa (21/568). Angalia “Mukhtaswar Al-Fataawaa Al-Maswriyyah (uk 490)].
Ninasema: “Itakubalika vipi kwa daktari Muislamu anayejua sharia, amwandikie mgonjwa dawa ambayo Rasuli wake ameielezea kama ni ugonjwa!!”
2- Abu Hurayrah amesema:
"نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنِ الدَّوَاءِ الْخَبِيثِ"
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kutumia dawa mbaya hatarishi”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (3870), Ibn Maajah (3459) na Ahmad (2/446)].
3- Toka kwa Abud Dardaai: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إِنَّ اللَّهَ أَنْزَلَ الدَّاءَ وَالدَّوَاءَ ، وَجَعَلَ لِكُلِّ دَاءٍ دَوَاءً ، فَتَدَاوُوا وَلَا تداوَوْا بحرامٍ"
“Hakika Allaah Ameteremsha ugonjwa na dawa, na Ameuwekea kila ugonjwa dawa yake, basi jitibuni kwa dawa, na wala msijitibu kwa kilichoharamishwa”. [Imekharijiwa na Abu Daawuwd (3874) na Al-Bayhaqiy (10/5). Angalia “As-Swahiyhah (1633)].
Hadiyth hizi zinafahamisha kwamba ni haramu kujitibu kwa kutumia madawa yaliyoharamishwa kiujumla, na pombe kimahususi. Lakini kama pataulizwa: Kwa nini isitumike qaaidah ya: “Dharura huhalalisha yaliyokatazwa” الضَّرُوْرِيَّاتُ تُبِيْحُ المحْظُوْرَاتِ" , tunasema: Ni kwa mambo mawili:
La kwanza:
Kujitibu kwa kutumia dawa hakuingii katika mlango wa dharura. Na kwa mujibu wa Jumhuwr ya ‘Ulamaa, kutumia dawa si jambo la wajibu, bali hata Sheikh wa Uislamu amesema: “Sijapata kumjua yeyote katika watangu wema aliyewajibisha kujitibu kwa dawa”.
Linalotilia nguvu maneno haya ni Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas kuhusu mwanamke mweusi aliyekwenda kwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia:
"إِنِّي أُصْرَعُ ، وَإِنِّي أَتَكَشَّفُ ، فَادْعُ اللهَ تَعَالَى لي. قَالَ: إِنْ شِئْتِ صَبَرْتِ وَلَكِ الْجَنَّةُ ، وَإِنْ شِئْتِ دَعَوْتُ اللهَ تَعَالَى أَنْ يُعَافِيَك"
“Mimi nina kifafa, na ninafunukwa nguo (kikinijia), basi niombee kwa Allaah Ta’aalaa. Akasema: Ukitaka, unaweza kusubiri na utaipata Jannah, na ukitaka nitakuombea kwa Allaah Akuponye”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5652) na Muslim (2265)].
Lau kama kuyaondosha maradhi ni jambo la waajib, basi Rasuli asingemchaguza bibi huyo. Na hili pia halipingani na amri ya kutumia dawa kwa ajili ya tiba. Na kuoanisha kati ya haya mawili kunawezekana, tukisema kwamba kuacha kutumia dawa ni bora zaidi ikiwa mtu ataweza kuvumilia na kuwa na subira, lakini kama hawezi kufanya subira juu ya maradhi na ikawa ni dhiki kwake, basi kutumia dawa kutakuwa ni bora zaidi kwa kuwa ubora wa kuacha dawa umeshaondoka kwa kukosa subira. [Ad-Duraariy Al-Mudhiy-at cha Ash-Shawkaaniy (uk. 393)].
La pili:
Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameshaeleza uharamu wa kujitibu kwa kilichoharamishwa kama ilivyotangulia. Na Allaah Ndiye Mjuzi zaidi.
· Angalizo:
Sindano ya ganzi (nusu kaputi) na mfano wake ambayo huondosha akili – kama haikupatikana ya kuchukua nafasi yake-, basi itajuzu kuitumia wakati wa dharura isiyoepukika katika shughuli za upasuaji. [Al-Muntaqaa cha Al-Baajiy (3/149), Mughnil Muhtaaj (4/187), Kashful Qinaa’i (96), Al-Muhallaa (7/508) na Naylul Awtwaar (81/211)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
الأَشْرِبَةُ
Vinywaji
Alhidaaya.com [3]
008- Vinywaji: Hukmu Ya Vinywaji Viwili Vilivyochanganywa:
Haijuzu kuchanganya vitu viwili vinavyolowekeka ndani ya maji kama “busr” na “rutwab”, au “tamr” (tende kavu) na zabibu kavu, hata kama havitakuwa na ukali. Ni kwa Hadiyth ya Abu Qataadah aliyesema:
"نَهَى النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنْ يُجْمَعَ بَيْنَ التَّمْرِ وَالزَّهْوِ، وَالتَّمْرِ وَالزَّبِيبِ، وَلْيُنْبَذْ كُلُّ وَاحِدٍ مِنْهُمَا عَلَى حِدَةٍ"
“Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kuchanganya kati ya tende mbivu na mbichi, na tende mbivu na zabibu kavu. Kila kimoja cha viwili kitayarishwe kivyake”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5173) na Muslim (1987)].
“Rutwab” ni awamu na nne ya tunda la mtende kabla ya kukomaa na kuwa “tamr”.
Jaabir bin ‘Abdullaah:
"َأَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ نَهَى أَنْ يُخْلَطَ الزَّبِيبُ وَالتَّمْرُ ، والْبُسْرُ وَالتَّمْرُ "
“Kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kuchanganya zabibu kavu pamoja na tende kavu (tamr mbivu), na “busr” pamoja na tende kavu (mbivu)”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (1986)].
“Busr” ni tunda na mtende kati ya “Balah” na “Rutwab”.
Mantiki ya kukataza mchanganyo huo ni kwamba nguvu ya kulewesha huzalikana haraka sana kabla ya kutaghayuri, na hapo mnywaji atadhani kwamba kinywaji hakileweshi, hali ya kuwa kinalewesha. Kwa ajili hiyo, Rasuli amekataza hilo ili kuziba njia ya kuingia humo.
Maalik ameharamisha mchanganyo huo wa vitu viwili hata kama hauleweshi. Pia ni kauli ya Ash-Shaafi’iy, Ahmad, Is-haaq na Ibn Hazm ambaye amehusisha hilo na aina zilizotajwa tu pasi na nyinginezo.
Ama Jumhuwr, wao wanasema kwamba ni makruhu madhali kinywaji hakijafikia nguvu ya kulewesha, lakini kama kitafikia nguvu hiyo, basi hapo kinakuwa ni haramu. Na Mahanbali wameiawilisha kauli ya Ahmad (Rahimahul Laah) isemayo: “Michanganyo miwili ni haramu” kuwa kwa maana ya: “Kinywaji kikiwa kikali na chenye nguvu ya kulewesha”.
Ama Abu Haniyfah, yeye anaona kwamba hakuna ubaya wowote wa kunywa mchanganyo wa vitu viwili madhali haukufikia nguvu ya kulewesha, kwa kuwa kila kimoja kinayeyuka chenyewe, na kwa hivyo si makruhu. Maneno yake yametolewa dalili na yaliyosimuliwa toka kwa Hadiyth Dhwa’iyf ya ‘Aaishah aliyesema:
"كُنَّا نَنْبِذُ لِرَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي سِقَاءٍ ، فَنَأْخُذُ قَبْضَةً مِنْ تَمْرٍ أَوْ قَبْضَةً مِنْ زَبِيبٍ فَنَطْرَحُهَا فِيهِ ، ثُمَّ نَصُبُّ عَلَيْهِ الْمَاءَ فَنَنْبِذُهُ غُدْوَةً فَيَشْرَبُهُ عَشِيَّةً ، وَنَنْبِذُهُ عَشِيَّةً فَيَشْرَبُهُ غُدْوَةً"
“Tulikuwa tukimtengenezea Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kinywaji cha zabibu (au tende) katika kiriba cha ngozi. Tunachukua teko moja la tende mbivu au teko moja la zabibu kavu tukalitupia humo, kisha tunamiminia maji. Tunatengeneza hivyo asubuhi mapema, na yeye akanywa jioni, au tunatengeneza hivyo jioni, na yeye akanywa asubuhi”. Hadiyth hii ni Dhwa’iyf, imekharijiwa na Ibn Maajah (3398), na haifai kutolewa hoja.
Ninasema: “Katazo linahukumia uharamisho madhali hakuna kauli nyingine ya kuondosha uharamisho huo. Halafu, kila mtu anajua kwamba ukiwemo ulewesho, basi kinywaji ni haramu, ni sawa kikiwa kimetengenezwa kutokana na mchanganyo wa vitu viwili, au kitu kimoja peke yake”.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
الأَشْرِبَةُ
Vinywaji
Alhidaaya.com [3]
009- Vinywaji: Nabidh "النَّبِيْذُ" Itokanayo Na Aina Moja:
[Al-Mudawwanah (6/263), Rawdhwat At-Twaalibiyna (10/168), Al-Mughniy na Fat-hul Baariy (10/57)].
"النَّبِيْذُ" (Nabiydh), ni tende kavu (tamr) au zabibu kavu au mfano wa viwili hivi ambavyo hulowekwa ndani ya maji mpaka maji hayo yakageuka tamu na kupata ladha ya vitu hivyo, kisha hunywewa. Maji hayo (juisi) yanakuwa halali kunywewa ikiwa muda wa kulowekwa ni mfupi au mdogo kiasi cha kutokuwa makali au ya kulewesha.
Ama muda wa kulowekwa, Mahanbali wamesema ni siku moja na usiku wake. Ama Wamaalik na Mashaafi’iy, wao muda hawakuuzingatia, wanachoangalia ni kinywaji kufikia nguvu ya kulewesha au la. Nami ninasema kwamba hili ndilo linalokubalika zaidi. Kijakazi wa Kihabeshi amesema:
"كُنْتُ أَنْبِذُ للنَّبِيِّ فِيْ سِقَاءٍ مِنَ اللَّيْلِ وَأُوْكِيْهِ وَأُعَلِّقُهُ، فَإِذَا أَصْبَحَ شَرِبَ مِنْهُ"
“Nilikuwa nikimtengenezea Rasuli juisi ya (tende au zabibu kavu) kwenye kiriba cha ngozi kuanzia usiku, nikakifunga mdomo wake na kukitundika, na kunapopambazuka anainywa”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (2005)].
Ibn ‘Abbaas amesema:
"كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يُنْتَبَذُ لَهُ أَوَّلَ اللَّيْلِ فَيَشْرَبُهُ إِذَا أَصْبَحَ يَوْمَهُ ذَلِكَ ، وَاللَّيْلَةَ الَّتِي تَجِيءُ ، وَالْغَدَ ، وَاللَّيْلَةَ الأُخْرَى ، وَالْغَدَ إِلَى الْعَصْرِ، فَإِنْ بَقِيَ شَىْءٌ سَقَاهُ الْخَادِمَ ، أَوْ أَمَرَ بِهِ فَصُبَّ"
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akilowekewa zabibu kavu (au tende kavu) mwanzoni mwa usiku, kisha hunywa maji yake tamu inapopambazuka siku yake yote na usiku wake ujao, na kesho pamoja na usiku wake, na siku inayofuatia hadi alasiri. Kama kitabakia chochote, basi humpa mtumishi wake anywe, au huamuru yakamwagwa”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (2004)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
الأَشْرِبَةُ
Vinywaji
Alhidaaya.com [3]
010- Vinywaji: Kuvuta Sigara:
Sigara (tumbaku) ilipoingia mwanzoni mwa karne ya 11 Hijria, na baadhi ya watu wakaanza kuitumia, Fuqahaa walikhitalifiana kuhusiana na hukmu yake. Kuna waliosema kuwa ni haramu, wengine wakasema ni makruhu, na wengine wakasema ni halali.
Lakini kiufupi, tunasema kwamba sigara ni haramu, kwa kuwa sababu zote za kuiharamisha zipo na za kutosha. Sababu zenyewe ni:
1- Inasababisha viungo kuchoka na mwili kupooza. Na Rasuli amekataza kutumia kitu kama hicho.
"أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّمَ نَهَى عَنْ كُلِّ مُسْكِرٍ وَمُفَتِّرٍ "
“Kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kila chenye kulewesha, na kila chenye kupoozesha nguvu za viungo vya mwili”. [Isnaad yake ni dhwa’iyf. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (3686) na Ahmad (6/254)].
2- Sigara ni katika vitu vichafu na hususan tunapokuta kwamba tumbaku yake ni lazima iloweshwe kwa pombe kiwandani katika mchakato wa kuitengeneza. Kwa picha hii, mtu mwenye akili zake hawezi kuona kwamba sigara ni katika vitu vizuri. Allaah Ta’aalaa Anasema:
"وَيُحَرِّمُ عَلَيْهِمُ الْخَبَائِثَ"
“Na Anawaharamishia vilivyo vibaya”. [Al-A’araaf: 157].
3- Madhara ya sigara kwa mwili wa mwanadamu yameshaonekana kutokana na mada za sumu zilizomo ndani yake kama nicotine, lami na nyinginezo ambazo husababisha saratani ya mapafu na koo. Na Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"لاَ ضَرَرَ وَلاَ ضِرَارَ"
“Ni marufuku kujidhuru au kusababishiana madhara”. [Hadiyth Hasan].
4- Ni israfu na upotezaji wa mali. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameeleza kuchukizwa kwake na suala la utumiaji vibaya wa mali.
"كَرِهَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِضَاعَةَ الْمَالِ "
“Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anachukizwa na ufujaji wa mali”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (477) na Muslim (1715)].
Hakuna tofauti katika ufujaji kati ya kutupa mali baharini au kuichoma moto.
· Faida:
Jarida la “La Vest” la tiba lilichapisha makala kuhusu uvutaji sigara. Makala hiyo inasema: “Utafiti wa kisasa uliofanywa nchini Marekani, umefikia matokeo yale yale waliyoyafikia wataalamu nchini Uingereza. Ni kwamba akina mama wanaovuta sigara wana hatari ya kufikia mapema mno umri wa kukatikiwa na hedhi, na majaribio waliyofanyiwa wanawake 3500 nchini Marekani walio katika umri wa kati (kuanzia miaka 40 kwenda juu), yamethibitisha pia matokeo hayo.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
الأَشْرِبَةُ
Vinywaji
Alhidaaya.com [3]
011- Vinywaji: Taratibu Njema Za Kunywa:
1- Kupiga Bismil Laah kabla ya kunywa.
2- Kunywa kwa mkono wa kulia. Dalili kuhusu hili imetajwa katika adabu njema za kula.
3- Mtu anywe hali ya kuwa ameketi, lakini pia inajuzu kunywa kwa kusimama. Abu Hurayrah: Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"لَا يَشْرَبَنَّ أَحَدٌ مِنْكُمْ قَائِمًا ، فَمَنْ نَسِيَ مِنْكُمْ فَلْيَسْتَقِئْ"
“Asinywe kabisa mmoja wenu akiwa amesimama. Na atakayesahau kati yenu, basi ajitapishe”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (3775)].
Katazo hili linachukuliwa kama la kimakruhu na si la uharamisho. Kwani imethibiti toka kwa Ibn ‘Abbaas:
"أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ شَرِبَ مِنْ زَمْزَمَ مِنْ دَلْوٍ مِنْهَا وَهُوَ قَائِمٌ "
“Kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikunywa kwenye Zamzam kwa kutumia ndoo ya hapo akiwa amesimama”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5617) na Muslim (2027)].
4- Anywe kwa mapigo matatu, apumue kati ya kila pigo nje ya chombo.
Kwani Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapokunywa, anapumua mara mbili au tatu kwa kukitenga kinywa chake na gilasi huku akisema:
"إِنَّهُ أرْوَى وَأَبْرَأُ وَأَمْرَأُ"
“Hakika hivi kunakata haraka zaidi kiu, kunaleta afya zaidi, na kuna manufaa makubwa zaidi”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5631) na Muslim (3782), na tamko ni lake].
5- Asipumulie ndani ya chombo au kupulizia humo.
Abu Qataadah: “Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إِذَا شَرِبَ أَحَدُكُمْ ، فَلَا يَتَنَفَّسْ فِي اَلْإِنَاءِ "
“Anapokunywa mmoja wenu, basi asipumulie ndani ya kikombe”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (153) na Muslim (267)].
Ibn ‘Abbaas:
"أّنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ نَهَى أَنْ يُتَنَفَّسَ فِي الْإِنَاءِ أَوْ يُنْفَخَ فِيهِ"
“Kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kupumuliwa ndani ya kikombe au kupuliziwa humo”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (3728), At-Tirmidhiy (1889) na Ibn Maajah (3429)].
6- Asinywe mtu kwa mdomo wa kiriba au gilasi na mfano wake
Abu Hurayrah:
"أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ نَهَى أَنْ يُشْرَبَ مِنْ فَمِ السِّقَاءِ"
“Kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza maji kunywewa moja kwa moja toka mdomo wa kiriba cha kunywea maji”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5627)].
Sababu ya katazo hili ni kuwa maji hububujika na kumiminika kwa mara moja kooni, na hii huleta ugonjwa wa ini na kusababisha madhara kwa tumbo. [Ar-Rawdhwat An-Naddiyyah (2/210)].
7- Kuanza kumpa maji aliye kulia kisha anayefuatia kulia
Anas bin Maalik:
"أَنَّ رَسُوْلَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أُتِيَ بِلَبَنٍ قَدْ شِيبَ بِمَاءٍ ، وَعَنْ يَمِينِهِ أَعْرَابِيٌّ ، وَعَنْ يَسَارِهِ أَبُو بَكْرٍ ، فَشَرِبَ ثُمَّ أَعْطَى الأَعْرَابِيَّ ، وَقَالَ: الأَيْمَنَ فَالأَيْمَنَ"
“Kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliletewa maziwa yaliyochangaywa na maji, kulia kwake alikuweko bedui, na kushoto kwake Abu Bakr. (Rasuli) akayanywa, kisha akampa bedui, na akasema: (Mpeni) wa kulia kwanza, kisha anayemfuatia wa kulia”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (2352) na Muslim (2029)].
Sahl bin Sa’ad:
"أُتِيَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِقَدَحٍ فَشَرِبَ مِنْهُ، وَعَنْ يَمِينِهِ غُلاَمٌ أَصْغَرُ الْقَوْمِ، وَالأَشْيَاخُ عَنْ يَسَارِهِ فَقَالَ: "يَا غُلاَمُ أَتَأْذَنُ لِي أَنْ أُعْطِيَهُ الأَشْيَاخَ؟ ". قَالَ: مَا كُنْتُ لأُوثِرَ بِفَضْلِي مِنْكَ أَحَدًا يَا رَسُولَ اللَّهِ. فَأَعْطَاهُ إِيَّاهُ"
“Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliletewa gilasi ya maziwa akanywa kidogo. Kuliani kwake alikuweko kijana mdogo kuliko wote waliokuweko, na kushotoni mwake wazee. Akamuuliza (kijana mdogo): Ee kijana! Je, utaniruhusu niwape wazee kwanza? Akajibu: Siwezi kabisa kumpendelea yeyote ufadhilisho wako kwangu ee Rasuli wa Allaah. Rasuli akampa maziwa”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (2351) na Muslim (2030)].
8- Anayewanywesha watu awe wa mwisho kunywa
Ni kwa Hadiyth ya Abu Qataadah, kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"سَاقِي الْقَوْمِ آخِرُهُمْ شُرْبًا"
“Ahudumiaye watu maji, awe wa mwisho kunywa”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (681)].
9- Kumhimidi Allaah baada ya kumaliza kunywa
Ni kwa neno la Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"إِنَّ اللَّهَ تَعَالَى لَيَرْضَى عنِ العبدِ أَنْ يَشْرَبَ الشَّرْبَةَ فَيَحْمَدَهُ عَلَيْهَا"
“Hakika Allaah Ta’aalaa kwa yakini, Humfurahikia mja anayekunywa mara moja tu (au funda moja tu) akamshukuru Yeye kwa unywaji huo”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (2734) na At-Tirmidhiy (1816)].
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/284
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11452&title=08E-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20%D9%83%D9%90%D8%AA%D9%8E%D8%A7%D8%A8%D9%8F%20%D8%A7%D9%84%D8%A3%D9%8E%D8%B7%D9%92%D8%B9%D9%90%D9%85%D9%8E%D8%A9%D9%90%20%D9%88%D9%8E%D8%A7%D9%84%D8%A3%D9%8E%D8%B4%D9%92%D8%B1%D9%90%D8%A8%D8%A9%D9%90%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20%D8%A7%D9%84%D8%A3%D9%8E%D8%B4%D9%92%D8%B1%D9%90%D8%A8%D9%8E%D8%A9%D9%8F%20-%20Vinywaji
[3] http://www.alhidaaya.com/
[4] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11454&title=01-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20%28Vinywaji%29%20Taarifu%20Yake%20Na%20Asili%20Ya%20Uhalali%20Wake
[5] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11455&title=02-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20%28Vinywaji%29%20Pombe%20Kwa%20Aina%20Zake%20Zote%20Ni%20Haramu
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11456&title=03-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20%28Vinywaji%29%20Chochote%20Chenye%20Kulewesha%20Ni%20Pombe
[7] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11457&title=04-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20%28Vinywaji%29%20Kunywa%20Pombe%20Kwa%20Aliyelazimika
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11458&title=05-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20%28Vinywaji%29%20Haijuzu%20Kumiliki%20Pombe%20Wala%20Kummilikisha%20Mwingine
[9] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11459&title=06-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20%28Vinywaji%29%20Pombe%20Ikigeuka%20Siki
[10] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11460&title=07-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20%28Vinywaji%29%20Haijuzu%20Kutumia%20Pombe%20Kama%20Dawa
[11] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11461&title=08-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20%28Vinywaji%29%20Hukmu%20Ya%20Vinywaji%20Viwili%20Vilivyochanganywa
[12] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11462&title=09-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20%28Vinywaji%29%20Nabidh%20%22%D8%A7%D9%84%D9%86%D9%91%D9%8E%D8%A8%D9%90%D9%8A%D9%92%D8%B0%D9%8F%22%20Itokanayo%20Na%20Aina%20Moja
[13] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11463&title=10-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20%28Vinywaji%29%20Kuvuta%20Sigara
[14] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11464&title=11-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Vyakula%20Na%20Vinywaji%3A%20%28Vinywaji%29%20Taratibu%20Njema%20Za%20Kunywa