كِتابُ اللِّباسِ وَالزِّينَةِ وَأَحْكامِ النَّظَر
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia
لِبَاسُ المَرْأَةِ
Kivazi Cha Mwanamke
Abu Maalik Kamaal Bin As-Sayyid Saalim
Imetarjumiwa na 'Abdullaah Mu'aawiyah (Abu Baasim)
Alhidaaya.com
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتابُ اللِّباسِ وَالزِّينَةِ وَأَحْكامِ النَّظَر
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia
لِبَاسُ المَرْأَةِ
Kivazi Cha Mwanamke
Alhidaaya.com [3]
001-Kivazi Cha Mwanamke Mbele Ya Wanaume Wasio Maharimu
(a) Ni haramu kujishaua kwa kuonyesha uzuri wake na mapambo, na hili limetolewa makamio makali. Allaah Amelikataza hili kwa kusema:
"وَلَا تَبَرَّجْنَ تَبَرُّجَ الْجَاهِلِيَّةِ الْأُولَىٰ"
“Na wala msionyeshe mapambo na uzuri kwa ajinabi mkajishaua kama zama za ujahili”. [Al-Ahzaab: (33)].
Umaymah bint Ruqayqah alikuja kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ili kupeana naye ahadi ya fungamano la Uislamu. Rasuli akamwambia:
"أُبَايِعُكِ على أَنْ لا تُشْرِكِيْ باللهِ شَيْئًا ، ولاَ تَسْرِقِيْ ، ولا تَزْنِيْ ، ولا تَقْتُلِيْ وَلَدَكَ ، ولا تَاْتِي بِبُهْتَانٍ تَفْتَرِيْنَهُ بَيْنَ يَدَيْكِ وَرِجْلَيْكِ ، ولا تَنُوْحِيْ ، ولا تَبَرَّجِيْ تَبَرُّجَ الجَاهِلِيَّةِ الأُوْلَى"
“Ninachukua ahadi ya fungamano kwako kwamba hutomshirikisha Allaah na chochote, wala hutoiba, wala hutozini, wala hutoua watoto wako, wala hutoleta uzushi wowote ukauzua baina ya mikono yako na miguu yako, wala hutoomboleza kijahili, wala hutojishaua mshauo wa ujahili wa kale”. [Musnad Ahmad (2/192) kwa Sanad Hasan].
Naye Abu Hurayrah amehadithia akisema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"صِنْفَانِ مِنْ أَهْلِ النَّارِ لَمْ أَرَهُمَا: قَوْمٌ مَعَهُمْ سِيَاطٌ كَأَذْنَابِ الْبَقَرِ يَضْرِبُونَ بِهَا النَّاسَ ، وَنِسَاءٌ كَاسِيَاتٌ عَارِيَاتٌ مُمِيلَاتٌ مَائِلَاتٌ رُؤُوْسُهُنَّ كَأَسْنِمَةِ الْبُخْتِ الْمَائِلَةِ ، لَا يَدْخُلْنَ الْجَنَّةَ وَلَا يَجِدْنَ رِيحَهَا ، وَإِنَّ رِيحَهَا لَتُوجَدُ مِنْ مَسِيرَةِ كَذَا وَكَذَا"
“Sampuli mbili za watu wa motoni sijaziona bado: Watu wenye mijeledi mithili ya mikia ya ng’ombe wanawapiga nayo watu (bila haki), na wanawake waliovaa lakini kiuhalisia wako uchi, wanawashawishi wenzao kuwa kama wao (au kuwasisimua wanaume), na wanatembea kwa maringo wakipindisha mabega yao, vichwa vyao ni kama nundu za ngamia zilizoinama. Hao hawaingii Peponi na hawatoipata harufu yake, na kwa hakika harufu yake inasikika toka mwendo kadha wa kadha”. [Swahiyh Muslim (2128)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ وَأَحْكَامُ النَّظَرِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia
لِبَاسُ المَرْأَةِ
Kivazi Cha Mwanamke
Alhidaaya.com [3]
002-Masharti Ya Kivazi Cha Mwanamke Wa Kiislamu, Sharti La Kwanza:
Sharti la kwanza:
Kisitiri mwili wake wote, isipokuwa ‘Ulamaa wamekhitilafiana kwa upande wa uso na viganja viwili. Allaah Amesema:
وَقُل لِّلْمُؤْمِنَاتِ يَغْضُضْنَ مِنْ أَبْصَارِهِنَّ وَيَحْفَظْنَ فُرُوجَهُنَّ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا مَا ظَهَرَ مِنْهَا ۖ وَلْيَضْرِبْنَ بِخُمُرِهِنَّ عَلَىٰ جُيُوبِهِنَّ ۖ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا لِبُعُولَتِهِنَّ أَوْ آبَائِهِنَّ أَوْ آبَاءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ أَبْنَائِهِنَّ أَوْ أَبْنَاءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي أَخَوَاتِهِنَّ أَوْ نِسَائِهِنَّ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُنَّ أَوِ التَّابِعِينَ غَيْرِ أُولِي الْإِرْبَةِ مِنَ الرِّجَالِ أَوِ الطِّفْلِ الَّذِينَ لَمْ يَظْهَرُوا عَلَىٰ عَوْرَاتِ النِّسَاءِ ۖ وَلَا يَضْرِبْنَ بِأَرْجُلِهِنَّ لِيُعْلَمَ مَا يُخْفِينَ مِن زِينَتِهِنَّ ۚ وَتُوبُوا إِلَى اللَّـهِ جَمِيعًا أَيُّهَ الْمُؤْمِنُونَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿٣١﴾
31. Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao na wahifadhi tupu zao, na wala wasidhihirishe mapambo yao isipokuwa yale yanayodhihirika. Na waangushe khimaar (shungi) zao mpaka vifuani mwao, na wasidhihirishe mapambo yao isipokuwa kwa waume zao, au baba zao, au baba za waume wao, au wana wao wa kiume, au wana wa kiume wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kiume wa kaka zao, au wana wa kiume wa dada zao, au wanawake wao (wa Kiislamu), au wale iliyowamiliki mikono yao ya kuume, au wafuasi wanaume wasio na matamanio ya jimai miongoni mwa wanaume au watoto ambao hawatambui kitu kuhusu sehemu za siri za wanawake. Na wala wasipige miguu yao yakajulikana yale wanayoyaficha katika mapambo yao. Na tubuni kwa Allaah nyote, enyi Waumini mpate kufaulu. [An-Nuwr: (31)].
Na Amesema tena Ta’aalaa:
يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُل لِّأَزْوَاجِكَ وَبَنَاتِكَ وَنِسَاءِ الْمُؤْمِنِينَ يُدْنِينَ عَلَيْهِنَّ مِن جَلَابِيبِهِنَّ ۚ ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَن يُعْرَفْنَ فَلَا يُؤْذَيْنَ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٥٩﴾
59. Ee Nabiy! Waambie wake zako, na mabinti zako, na wanawake wa Waumini wajiteremshie jilbaab zao. Hivyo kunapeleka karibu zaidi watambulikane (kwa heshima) wasiudhiwe. Na Allaah daima Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu. [Al-Ahzaab: (59)].
Jua kwamba ‘Ulamaa wamekubaliana kwamba ni lazima mwanamke asitiri mwili wake wote, lakini wamekuja wakakhitilafiana kwa vigezo kwa upande wa uso na viganja.
Kundi ambalo linaona kuwa ni lazima asitiri pia uso na viganja lina dalili zifuatazo:
1- Neno Lake Ta’aalaa:
"وَإِذَا سَأَلْتُمُوهُنَّ مَتَاعًا فَاسْأَلُوهُنَّ مِن وَرَاءِ حِجَابٍ"
“Na mnapowauliza wake zake haja, waulizeni nyuma ya pazia”. [Al-Ahzaab: (53)].
Aayah hii iliteremka wakati Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipomwoa Zaynab bint Jahsh. Akaalika watu, wakala, kisha wakatoka wengi wao na wakabakia baadhi wachache ambao walikaa kwa muda mrefu kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Kisha Rasuli akatoka pamoja na Zaynab na kuingia naye (chumbani) mara kadhaa ili watoke. Na hapo ndipo iliposhuka aayah hii, na Rasuli akapiga pazia kati yake na wao. [Sababu hii ya kuteremshwa aayah imekharijiwa na Al-Bukhaariy (4791) na Muslim (1428) kutoka kwa Hadiyth ya Anas, kwa maana yake].
Wanasema kwamba kauli hii inawahusu wanawake wote kwa kuwa wanashirikiana wote katika sababu ya hijabu, nayo ni utwahara wa moyo.
2- Kauli Yake Ta’aalaa:
يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُل لِّأَزْوَاجِكَ وَبَنَاتِكَ وَنِسَاءِ الْمُؤْمِنِينَ يُدْنِينَ عَلَيْهِنَّ مِن جَلَابِيبِهِنَّ ۚ ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَن يُعْرَفْنَ فَلَا يُؤْذَيْنَ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٥٩﴾
“Ee Nabiy! Waambie wake zako, na mabinti zako, na wanawake wa Waumini wajiteremshie jilbaab zao. Hivyo kunapelekea karibu zaidi watambulikane (kwa heshima) wasiudhiwe. Na Allaah daima Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu”. [Al-Ahzaab: (59)].
Wamefasiri “kuteremsha jilbaab” kwenye aayah hii kwa maana ya kufunika uso na kuacha jicho moja tu wazi ili kuonea kwalo.
3- Hadiyth ya Ibn Mas-‘uwd kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"الْمَرْأَةُ عَوْرَةٌ فَإِذَا خَرَجَتِ اسْتَشْرَفَهَا الشَّيْطَانُ"
“Mwanamke ni uchi, na anapotoka nje, basi shetani humpamba (kwenye macho ya wanaume). [At-Tirmidhiy (1173), Ibn Maajah (3/95), na At-Twabaraaniy katika Al-Kabiyr (10115). Ni Hadiyth Swahiyh].
4- Hadiyth ya kuzushiwa Bibi ‘Aaishah zinaa ambapo anaeleza:
"وَكَانَ صَفْوَانُ بْنُ الْمُعَطَّلِ السُّلَمِيُّ مِنْ وَرَاءِ الْجَيْشِ، فَأَصْبَحَ عِنْدَ مَنْزِلِي فَرَأَى سَوَادَ إِنْسَانٍ نَائِمٍ فَأَتَانِي فَعَرَفَنِي حِيْنَ رَآنِي، وَكَانَ يَرَانِي قَبْلَ الْحِجَابِ فَاسْتَيْقَظْتُ بِاسْتِرْجَاعِهِ عَرَفَنِي فَخمَرِتُ وَجْهِي بِجِلْبَابِي .."
“Swafwaan bin Al-Mu’attwal As-Sulamiy alikuwa nyuma ya jeshi. Akapambaukiwa asubuhi akiwa mbele ya hema langu, akaona weusi wa kivuli cha mtu aliyelala, akanijia, akanitambua aliponiona. Yeye alikuwa ananiona kabla ya kuteremka amri ya kuvaa hijaab, nikaamka kutokana na tamshi lake la kusema “Innaa LiLLaahi wa Innaa ilayhi raaji’uwn” baada ya kunitambua. Nikajifunika uso wangu kwa jilbabu yangu.” [Al-Bukhaariy (4141) na Muslim (2770)].
5- Hadiyth ya Asmaa bint Abiy Bakr:
"كُنَّا نُغَطِّيْ وُجُوْهَنَا مِنَ الرِّجَالِ ، نَمْتَشِطُ قَبْلَ ذلِكَ فِي الإحْرَامِ"
“Tulikuwa tunazifunika nyuso zetu wanaume wasituone, na kabla ya kufanya hivyo, tulikuwa tunachana nywele zetu katika ihraam”. [Mustadrakul Haakim (1/454) kwa Sanad Swahiyh].
Ama kundi la pili la ‘Ulamaa wanaosema kwamba inajuzu kwa mwanamke kuacha wazi uso wake na viganja, na kwamba kuvisitiri viwili hivi ni jambo la sunnah na si waajib, hawa dalili zao ni hizi zifuatazo:
1- Neno Lake Ta’aalaa:
"وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا مَا ظَهَرَ مِنْهَا"
“Na wala wasidhihirishe mapambo yao isipokuwa yale yanayodhihirika”. [An-Nuwr: (31)].
Wamesema “yanayodhihirika” ni uso na viganja. At-Twabariy amekhitari rai hii katika tafsiyr yake (18/84). Lakini pia kuna rai nyingine kuhusiana na hili ambapo baadhi wengine wamesema ni vile vinavyodhihiri bila mwanamke kukusudia, wengine wamesema ni nguo, wengine wanja, pete, bangili na kadhalika.
2- Hadiyth (Dhwa’iyf) ya ‘Aaishah:
"أَنَّ أَسْمَاءَ بِنْتَ أَبِي بَكْرٍ دَخَلَتْ عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَعَلَيْهَا ثِيَاب رقاق فَأَعْرَضَ عَنهُ وَقَالَ: يَا أَسْمَاءُ إِنَّ الْمَرْأَةَ إِذَا بَلَغَتِ الْمَحِيضَ لَنْ يَصْلُحَ أَنْ يُرَى مِنْهَا إِلَّا هَذَا وَهَذَا . وَأَشَارَ إِلَى وَجْهِهِ وَكَفَّيْه"ِ
“Kwamba Asmaa bint Abiy Bakr aliingia kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa amevaa nguo nyepesi. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akageuka asimwone na akamwambia: Ee Asmaa! Mwanamke anapofikia umri wa kutokwa na hedhi, basi haifai aonekane chochote isipokuwa hii na hii, akaashiria uso wake na viganja vyake viwili”. [Hadiyth Dhwa’iyf: Imekharijiwa na Abu Daawuwd (4104), na kwenye sanad yake kuna kasoro nne].
Wametoa dalili kadhaa pia zinazogusia kwamba wanawake wa Kiislamu walikuwa wakifunua nyuso au viganja viwili mbele ya Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) naye hakuwakataza. Kati yake ni:
3- Hadiyth ya Jaabir bin ‘Abdillaah kuhusu Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwatolea mawaidha wanawake siku ya ‘Iyd. Sehemu ya Hadiyth inaeleza:
"فَقَامَتْ امْرَأَةٌ مِنْ سِطَةِ النِّسَاءِ سَفْعَاءُ الْخَدَّيْنِ فَقَالَتْ لِمَ يَا رَسُولَ اللَّه"
“Akasimama mwanamke mmoja aliyesawijika mashavu toka katikati ya wanawake akauliza: Kwa nini ee Rasuli wa Allaah?!” [Muslim (885), An-Nasaaiy (1/233) na Ahmad (3/318)].
Wamesema: Kauli ya Jaabir “aliyesawijika mashavu”, ni dalili kwamba alikuwa hakuyafunika mashavu yake.
4- Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas ambapo Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimpandisha Fadhli bin ‘Abbaas nyuma ya mnyama wake katika Hijjah ya kuaga, na mwanamke akamuuliza Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Sehemu ya Hadiyth inasema:
"...فَأَخَذَ الْفَضْلُ بْنُ عَبَّاسٍ يَلْتَفِتُ إِلَيْهَا وَكَانَتِ امْرَأَةً حَسْنَاءَ ، فَأَخَذَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِذَقْنِ الْفَضْلَ ، فَحَوَّلَ وَجْهَهُ مِنَ الشِّقِّ الآخَرِ"
“…Al-Fadhl bin ‘Abbaas akaanza kugeuka kumwangalia, naye alikuwa mwanamke mrembo wa sura, na Rasuli akakishika kidevu cha Al-Fadhl, akaugeuza uso wake upande mwingine”. [Al-Bukhaariy (6228) na Muslim (1218)].
Katika riwayaah nyingine ya Hadiyth ya ‘Aliyy bin Abiy Twaalib ni kwamba hilo lilikuwa wakati wa kuchinja baada ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kutupia vijiwe Jamarah, kwa maana kwamba swali la mwanamke huyo lilikuwa baada ya tahallul ya ihraam (tahallul ndogo).
Ibn Hazm amesema: “Na lau kama uso ungelikuwa ni uchi unaolazimu kufunikwa, basi Rasuli asingelimruhusu kuufunua mbele ya watu, na badala yake angelimuamrisha auteremshie ushungi toka juu. Na kama uso wake ulikuwa umefunikwa, basi Ibn ‘Abbaas asingelijua kama ni mrembo wa sura au mwenye sura ya kawaida”.
5- Hadiyth ya ‘Aaishah:
"كُنَّ نسَاءُ المؤْمِنَاتِ يَشْهَدْنَ مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الصُّبْحَ مُتَلَفِّعَاتٍ بِمُرُوطِهِنَّ ، ثُمَّ يَنْقَلِبْنَ إِلَى بُيُوْتِهِنَّ حِيْنَ يَقْضِيْنَ الصَّلَاةَ ، لا يَعْرِفُهُنَّ أَحَدٌ مِنَ الْغَلَسِ"
“Wanawake Waumini walikuwa wakihudhuria Swalatul Fajr pamoja na Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wakiwa wamejitanda shungi zao, kisha huondoka haraka kurudi majumbani mwao wakati swalah inapomalizika, hawatambui yeyote sura zao kutokana na kiza”. [Al-Bukhaariy (578) na Muslim (645)].
Wamesema: Tunafahamu hapa kwamba lau si kiza, basi wangelitambulika, na kwa kawaida hutambulikana kutokana na nyuso zikiwa wazi.
6- Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas pale Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipowatolea wanawake mawaidha Siku ya ‘Iyd ambapo aliwahimiza watoe swadaqah. Sehemu ya Hadiyth inasema:
"...وَأَمَرَهُنَّ بِالصَّدَقَةِ ، فَرَأَيْتُهُنَّ يُهْوِينَ إِلَى آذَانِهِنَّ وَحُلُوقِهِنَّ يَدْفَعْنَ إِلَى بِلَالٍ ، ثُمَّ ارْتَفَعَ هُوَ وَبِلَالٌ إِلَى بَيته"
“….na akawaamuru kutoa swadaqah, hapo nikawaona wakipeleka mikono kwenye masikio yao na koo zao (kutoa hereni na mikufu) na kumkabidhi Bilaal, kisha akanyanyuka yeye na Bilaal wakaenda nyumbani kwake”. [Al-Bukhaariy (977), Abu Daawuwd (1143) na An-Nasaaiy (1/227)].
7- Hadiyth ya ‘Aaishah:
"أَنَّ امْرَأَةً أَتَتِ النَّبِيَّ تُبَايِعُهُ، وَلَمْ تَكُنْ مُخْتَضِبَةً، فَلَمْ يُبَايِعْهَا حَتَّى اخْتَضَبَتْ"
“Kwamba mwanamke mmoja alimjia Rasuli wa Allaah kupeana naye ahadi ya fungamano na Uislamu (bay-‘a), mwanamke huyo hakuwa amejipaka hina, na Rasuli hakuchukua ahadi kwake mpaka alipojitia hina”. [Abu Daawuwd (4166) na Al-Bayhaqiy kutoka kwake (7/86). Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh].
Wametoa dalili vile vile kwa jumla ya aathaar zinazoelezea kufanyika matukio ambapo wanawake walikuwa hawafuniki nyuso zao wala viganja vyao baada ya enzi ya Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam). [Angalia kitabu cha “Jilbaabul- Mar-atil Muslimati” cha Al-Albaaniy (uk. 96)].
Na ijulikane kwamba kila kundi katika makundi haya mawili lina hoja pingamizi dhidi ya kila dalili ya kundi jingine, na hapa hatuna nafasi ya kuziweka kwa mapana yake, kwani ni ndefu sana. Lakini unaweza ukaona minakasha hiyo kwa mapana zaidi katika kitabu cha “Al-Hijaab, Adillatul Muwjibiyna” cha Shaykh Mustwafa Al-‘Adawiy, kitabu cha “ ‘Awdatul Hijaab” cha Shaykh Muhammad bin Ismaa’iyl, na kitabu cha “Jilbaabu Al-Mar-atil Muslimati” cha Sheikh Al-Albaaniy.
Na hapa nimeleta makundi mawili pamoja na dalili zao nyingi ili kuonyesha kwamba ‘Ulamaa wamekhitilafiana kwalo tangu zamani na hadi sasa, na kwamba makhitilafiano haya si ya kihasama kiasi cha kulifanya kundi moja kulishadidia kundi jingine na kuliona limepotoka, bali kila kundi linaheshimu hoja za kundi jingine.
Na hapa pia tunachukua nafasi ya kuhadharisha umma na kundi la tatu ambalo Maulamaa wake si lolote si chochote, bali ni wababaishaji tu ambao wanasema kwamba mwanamke kusitiri uso wake ni bid’a na uchupaji mipaka ya dini. Bali ujinga wa baadhi yao umefikia kutunga kitabu ambapo wanasema kwamba kusitiri uso wa mwanamke ni haramu!
Tunamalizia mada hii kwa kuelezea faida hizi:
- ‘Ulamaa kwa pamoja wamekubaliana kwamba ni lazima mwanamke aliye huru asitiri mwili wake wote isipokuwa uso na viganja.
- Kuna makhitilafiano kuhusu uso na viganja kama ilivyoelezwa.
- Wenye kusema kwamba si lazima kusitiri uso, wanaona kwamba ni bora kusitiriwa na hususan katika zama za fitnah.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ وَأَحْكَامُ النَّظَرِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia
لِبَاسُ المَرْأَةِ
Kivazi Cha Mwanamke
Alhidaaya.com [3]
003-Masharti Ya Kivazi Cha Mwanamke Wa Kiislamu, Sharti La Pili:
Sharti la pili:
Vazi lenyewe lisiwe ni pambo. Ni kwa Neno Lake Ta’aalaa:
"وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا مَا ظَهَرَ مِنْهَا"
“Na wala wasidhihirishe mapambo yao isipokuwa yale yanayodhihirika”. [An-Nuwr: 31].
Hii kwa ujumuishi wake, ni pamoja na nguo ya juu ikiwa ina mapambo yenye kuvuta macho ya wanaume.
Na kwa neno lake Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"ثَلاَثَةٌ لاَ تَسْأَلْ عَنْهُمْ: رَجُلٌ فَارَقَ الْجَمَاعَةَ وَعَصَى إِمَامَهُ فَمَاتَ عَاصِيًا ، وَأَمَةٌ أَوْ عَبْدٌ أَبِقَ مِنْ سَيِّدِهِ فَمَاتَ ، وَامْرَأَةٌ غَابَ عَنْهَا زَوْجُهَا ، قدْ كَفَاهَا مَؤُونَةَ الدُّنْيَا فَتَبَرَّجَتْ بَعْدَهُ، فَلاَ تَسْأَلْ عَنْهُمْ"
“Watatu, usiwaulizie (adhabu inayowasubiri): Ni mtu aliyetengana na umoja (wa nduguze Waislamu), akamwasi kiongozi wake na akafa akiwa mwasi, na kijakazi au mtumwa aliyetoroka kisha akafa, na mwanamke ambaye mumewe yuko mbali naye nailhali amemtosheleza mahitaji yake yote ya maisha, kisha akajishaua nyuma yake. Hao usiwaulizie”. [Fat-hul Bayaan (7/274)].
Makusudio ya kuamrishwa kuvaa jilbabu ni kuficha pambo la mwanamke, hivyo haiwezekani kiakili jilbabu lenyewe liwe ni pambo.
Angalizo:
Baadhi ya wanawake wanaowajibika kidini, wanadhani kwamba vazi lolote lisilo jeusi, basi linakuwa ni pambo. Dhana hii ni kosa kwa sababu mbili:
Ya kwanza: Kwa neno lake Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
طِيبُ الْمَرْأَة ما ظَهَرَ لَوْنُهُ وَخَفِيَ رِيْحُهُ"
“Mafuta mazuri kwa mwanamke ni yale ambayo rangi yake inaonekana lakini harufu yake haisikiki.” [Hadiyth Hasan Bitwuruqih. Imekharijiwa na At-Tirmidhiy (2788) na Abu Daawuwd (2174)].
Ya pili: Wanawake Maswahaba walizoeleka kuvaa nguo za rangi zisizo nyeusi. Yafuatayo yanathibitisha hili:
1- Hadiyth ya ‘Ikrimah:
"أَنَّ رِفَاعَةَ، طَلَّقَ امْرَأَتَهُ، فَتَزَوَّجَهَا عَبْدُ الرَّحْمَنِ بْنُ الزَّبِيرِ، قَالَتْ عَائِشَةُ وَعَلَيْهَا خِمَارٌ أَخْضَرُ. فَشَكَتْ إِلَيْهَا، وَأَرَتْهَا خُضْرَةً بِجِلْدِهَا، فَلَمَّا جَاءَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَتْ عَائِشَةُ: مَا رَأَيْتُ مِثْلَ مَا يَلْقَى الْمُؤْمِنَاتُ، لَجِلْدُهَا أَشَدُّ خُضْرَةً مِنْ ثَوْبِهَا"
“Kwamba ‘Rifa’at alimpa talaka mkewe na ‘Abdulrahmaan bin Az-Zubayr akamwoa. Bi ‘Aaishah anaeleza kwamba bi huyo alikuja kwake akiwa na mtandio wa kijani, akamshtakia na kumwonyesha alama za kijani kwenye ngozi yake (kutokana na kipigo). Na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuja, ‘Aaishah alimwambia: Sijapata kuona mfano wa mateso yanayowapata Waumini wanawake, ngozi yake imekuwa kijani kuliko mtandio wake”. [Al-Bukhaariy (5825)].
2- Hadiyth ya Ummu Khaalid bint Khaalid:
"أُتِيَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِثِيَابٍ فِيهَا خَمِيصَةٌ سَوْدَاءُ صَغِيرَةٌ ، فَقَالَ: مَنْ تَرَوْنَ نَكْسُو هَذِهِ؟ فَسَكَتَ الْقَوْمُ ، قَالَ: ائْتُونِي بِأُمِّ خَالِدٍ. فَأُتِيَ بِهَا تُحْمَلُ فَأَخَذَ الْخَمِيصَةَ بِيَدِهِ فَأَلْبَسَهَا وَقَالَ: أَبْلِي وَأَخْلِقِي ". وَكَانَ فِيهَا عَلَمٌ أَخْضَرُ أَوْ أَصْفَرُ فَقَالَ: يَا أُمَّ خَالِدٍ هَذَا سَنَاهْ، وَسَنَاهْ بِالْحَبَشِيَّةِ حَسَنٌ"
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliletewa nguo likiwemo vazi dogo jeusi la khamiyswa, halafu akasema: Mnaona tumvishe nani hili? Watu wakanyamaza. Akasema: Basi nileteeni Ummu Khaalid. Akaletewa akiwa amebebwa, akalichukua vazi akamvisha kwa mkono wake, kisha akamwombea du’aa akimwambia: Ulivae na uishi nalo muda mrefu lichakae hadi ulishone. Na vazi lilikuwa na mistari kijani au njano. Halafu akamwambia: Ee Ummu Khaalid! Hili ni “sanah”, na “sanah” kwa Kihabeshi ni zuri, (yaani ni vazi zuri limekupendeza)”. [Al-Bukhaariy (5823)].
3- Al-Qaasim kasema:
"أَنَّ عَائِشَةَ كَانَتْ تَلْبَسُ الثِّيَابَ الْمُعَصْفَرَةَ وَهِيَ مُحْرِمَةٌ"
“ ’Aaishah alikuwa anavaa nguo ya rangi ya kinjano akiwa amehirimia”. [Ibn Abiy Shaybah (8/372) kwa Sanad Swahiyh].
Ninasema:
1- Ilivyo ni kwamba nguo ambayo yenyewe ni pambo, ni ile iliyofumwa kwa rangi mbalimbali, au yenye nakshi za rangi ya dhahabu au silva, inayovuta macho ya akina baba na kuyazimua.
2- Vazi jeusi ndilo bora zaidi kwa wanawake na lenye sitara zaidi, nalo ndilo vazi la wake wa Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kama alivyoeleza Bibi ‘Aaishah kwenye Hadiyth kuhusiana na yeye kuonwa na Swafwaan ambapo anasema:
"فَرَأَى سَوَادَ إِنْسَانٍ نَائِمٍ"
“Akaona weusi wa kiwiliwili cha mtu aliyelala”.
Na pia Hadiyth nyingine ya ‘Aaishah kuhusu kutoka kwa wanawake wa Ki-Answaar, anasema:
"كَأَنَّ عَلى رُؤُوسِهِنَّ الغِرْبِانُ"
“Kana kwamba kuna kunguru juu ya vichwa vyao”. [Swahiyh Muslim (2128)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ وَأَحْكَامُ النَّظَرِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia
لِبَاسُ المَرْأَةِ
Kivazi Cha Mwanamke
Alhidaaya.com [3]
004-Masharti Ya Kivazi Cha Mwanamke Wa Kiislamu, Sharti La Tatu Na La Nne:
Sharti la tatu:
Nguo iwe nzito isiyoonyesha rangi ya ngozi ya mwili. Hii ni kwa Hadiyth iliyotangulia ya Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"صِنْفَانِ مِنْ أَهْلِ النَّارِ لَمْ أَرَهُمَا: قَوْمٌ مَعَهُمْ سِيَاطٌ كَأَذْنَابِ الْبَقَرِ يَضْرِبُونَ بِهَا النَّاسَ ، وَنِسَاءٌ كَاسِيَاتٌ عَارِيَاتٌ مُمِيلَاتٌ مَائِلَاتٌ رُؤُوْسُهُنَّ كَأَسْنِمَةِ الْبُخْتِ الْمَائِلَةِ ، لَا يَدْخُلْنَ الْجَنَّةَ وَلَا يَجِدْنَ رِيحَهَا ، وَإِنَّ رِيحَهَا لَتُوجَدُ مِنْ مَسِيرَةِ كَذَا وَكَذَا"
“Sampuli mbili za watu wa motoni sijaziona bado: Watu wenye mijeledi mithili ya mikia ya ng’ombe wanawapiga nayo watu (bila haki), na wanawake waliovaa lakini kiuhalisia wako uchi, wanawashawishi wenzao kuwa kama wao (au kuwasisimua wanaume), na wanatembea kwa maringo wakipindisha mabega yao, vichwa vyao ni kama nundu za ngamia zilizoinama. Hao hawaingii Peponi na hawatoipata harufu yake, na kwa hakika harufu yake inasikika toka mwendo kadha wa kadha”. [Swahiyh Muslim (2128)].
Wanaokusudiwa hapa ni wanawake wanaovaa nguo nyepesi zinazoonyesha mwili badala ya kuusitiri, au nguo fupi, au zenye kubana mwili, wao kwa jina wamevaa, lakini kiuhalisia wako uchi.
Sharti la nne:
Nguo iwe pana, isiwe inabana ikaonyesha mikatiko ya mwili wake.
Usaamah bin Zayd anahadithia:
"كَسَانِي رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قُبْطِيَّةً كَثِيفَةً كَانَتْ مِمَّا أَهْدَاهَا دِحْيَةُ الْكَلْبِيُّ، فَكَسَوْتُهَا امْرَأَتِي، فَقَالَ لِي رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: " مَا لَكَ لَمْ تَلْبَسِ الْقُبْطِيَّةَ؟ " قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللهِ، كَسَوْتُهَا امْرَأَتِي. فَقَالَ لِي رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: (مُرْهَا فَلْتَجْعَلْ تَحْتَهَا غِلَالَةً، إِنِّي أَخَافُ أَنْ تَصِفَ حَجْمَ عِظَامِهَا"
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alinivalisha “qubtwiyyah” zito ambalo alikuwa amepewa zawadi na Dihyatul Kalbiyy, nami nikamvisha mke wangu. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliponiona akaniambia: Vipi? Mbona hukuvaa “qubtwiyyah”? Nikamwambia: Ee Rasuli wa Allaah, nimemvalisha mke wangu. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaniambia: Mwamuru avalie ndani yake nguo nyingine, kwani nahofia “qubtwiyyah” litaonyesha mifupa yake ilivyo”. [Ahmad (5/205) kwa Sanad Layyin. Ina Hadiyth mwenza kwa Abu Daawuwd (4116) ambayo kwayo inafanywa Hadiyth Hasan].
“Qubtwiyyah” ni vazi la zamani la Kimisri.
Kwa dada zetu wa Kiislamu katika zama zetu za leo, tunapenda kuwaambia kwamba haitoshi ukasitiri tu nywele zako na shingo yako, kisha bila kujali baada ya hapo, ukavaa nguo za kubana na fupi zisizovuka nusu muundi. Na jueni kwamba haitoshi kuvaa soksi kwenye miundi miwili iliyo wazi. Jilazimisheni kuwa na pupa ya kukamilisha sitara kama Alivyoamuru Allaah Ta’aalaa na kuwaiga pia wanawake wenzenu waliohamia mwanzo Madiynah (Muhaajiraat) wakati ilipoteremka amri ya kuteremsha shungi zao. Hapo hapo walipasua mitandio yao wakajifunika nayo. Na sisi hatuwatakeni mpasue nguo zenu zozote, bali tunawatakeni mrefushe nguo zenu na mzitanue ili ziwe ni kivazi chenye kusitiri mwili wote ambao Allaah Amewaamuru kuusitiri. [Ni maneno ya Al-‘Allaamah Al-Albaaniy kuhusu jilibabu].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ وَأَحْكَامُ النَّظَرِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia
لِبَاسُ المَرْأَةِ
Kivazi Cha Mwanamke
Alhidaaya.com [3]
005-Masharti Ya Kivazi Cha Mwanamke Wa Kiislamu, Sharti La Tano Na La Sita:
Sharti la tano:
Nguo isiwe imefukizwa au imepuliziwa manukato. Abu Muwsaa Al-Ash-‘ariyy amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"أَيُّمَا امْرَأَةٍ اسْتَعْطَرَتْ فَمَرَّتْ عَلَى قَوْمٍ لِيَجِدُوا مِنْ رِيحِهَا فَهِيَ زَانِيَةٌ"
“Mwanamke yeyote aliyejifukiza manukato, halafu akapita karibu na wanaume ili waipate harufu yake, basi ni mzinifu”. [An-Nasaaiy (2/283), Abu Daawuwd (4173), At-Tirmidhiy (2786) na wengineo kwa Sanad Hasan].
Sababu ya kukataza hilo iko wazi, nayo ni kuwa tabia hiyo inachochea na kuchemsha matamanio ya kimwili ya wanaume. Na ‘Ulamaa wameingiza mambo mengine ndani ya hili na kuyafanya kuwa sawa nalo kama vile kuvaa vipambo vinavyoonekana, mavazi ya kuvutia, mapambo ya kifahari na kuchanganyika na wanaume. [Fat-hul Baariy (2/279)].
Al-Haythamiy ameeleza kwenye “Az-Zawaajir” (2/37) kwamba mwanamke akitoka nyumbani kwake akiwa amejitia manukato na kujipamba, basi hilo ni katika madhambi makubwa, hata kama ametoka kwa ruksa ya mumewe.
Sharti la sita:
Nguo yake isifanane na nguo za kiume. Ibn ‘Abbaas amesema:
"لَعَنَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الْمُتَشَبِّهِينَ مِنَ الرِّجَالِ بالنِّسَاءِ، وَالْمُتَشَبِّهَاتِ من النِّسَاءِ بِالرِّجَالِ"
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amewalaani wanaume wanaojifananisha na wanawake, na wanawake wanaojifananisha na wanaume”. [Al-Bukhaariy (5885), At-Tirmidhiy (2784), Abu Daawuwd (4097) na Ibn Maajah (1904)].
Maana ni kwamba haijuzu wanaume kujifananisha na wanawake katika mavazi na mapambo ambayo yanawahusu wanawake na kinyume chake.
Na Abu Hurayrah amesimulia:
"لَعَنَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الرَّجُلَ يَلْبَسُ لِبْسَةَ الْمَرْأَةِ وَالْمَرْأَةَ تَلْبَسُ لِبْسَةَ الرَّجُلِ"
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amemlaani mwanaume anayevaa mavazi ya kike, na mwanamke anayevaa mavazi ya kiume”. [Abu Daawuwd (4098) na Hamad (2/325) kwa Sanad Swahiyh].
Faida:
Kidhibiti katika kukataza Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kila jinsia kujifananisha na nyingine, hakirejei tu katika kile wanachojichagulia wanaume na wanawake, au wanavyovitamani na wanavyovizoea, bali kinarejea kwa kila kinachowafaa wanaume na kinachowafaa wanawake. Kinachowafaa wanawake ni lazima kinasibiane na kile walichoamrishwa katika kujisitiri na kujifunika bila kuonekana yasiyofaa kuonekana na ajinabi. Na kwa msingi huu, tutaona kwamba sharia ina makusudio mawili. La kwanza ni kuweka tofauti kati ya mwanaume na mwanamke, na la pili ni kusitiriwa mwanamke, na yote mawili ni lazima yapatikane.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ وَأَحْكَامُ النَّظَرِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia
لِبَاسُ المَرْأَةِ
Kivazi Cha Mwanamke
Alhidaaya.com [3]
006- Masharti Ya Kivazi Cha Mwanamke Wa Kiislamu, Sharti La Saba Na La Nane:
Sharti la saba:
Isifanane na nguo za wanawake wa kikafiri. Hii ni kwa mujibu wa yaliyopitishwa na sharia ya Kiislamu kwamba haifai kwa Waislamu -wanaume kwa wanawake- kujifananisha na makafiri, ni sawa katika ibada zao, au sikukuu zao, au mavazi yao yanayowahusu wao.
Kuna matini nyingi zinazoelezea nukta hii. Kwa yanayohusiana na nguo, ni Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Amri aliyesema:
"رَأَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَلَىَّ ثَوْبَيْنِ مُعَصْفَرَيْنِ فَقَالَ: "إِنَّ هَذِهِ مِنْ ثِيَابِ الْكُفَّارِ فَلاَ تَلْبَسْهَا"
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliniona nimevaa nguo mbili za rangi ya zafarani. Akaniambia: Hakika hizi ni katika nguo za makafiri, usizivae”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (2077)].
Mbali ya Hadiyth hii, ziko nyingine nyingi tele. Na makusudio hapa ni kutaka ijulikane kuwa haifai kwa mwanamke wa Kiislamu avae nguo ifananayo na nguo za wanawake wa kikafiri, kwa kuwa kushirikiana katika jambo la dhahiri, kunazalisha mvaano na muundano kati ya wafananao, na hatima yake ni kukubaliana tabia na matendo, na hili kiuhalisia liko. [Kwa maudhui hii, pitia kitabu cha “Iqtidhwaau As-Swiraat Al-Mustaqiym” cha Ibn Taymiyyah. Kitabu hiki hakina mfano wake].
Sharti la nane:
Lisiwe ni vazi la umashuhuri (la kipekee tofauti na mengineyo). Ni kwa Hadiyth ya Ibn ‘Umar:
"مَنْ لَبِسَ ثَوْبَ شُهْرَةٍ فيٍ الدُّنْيَا أَلْبَسَهُ اللَّهُ ثَوْبَ مَذَلَّةٍ يَوْمَ الْقِيَامَةِ، ثُمَّ أَلْهَبَ فِيْهِ نَارًا"
“Mwenye kuvaa nguo ya umashuhuri duniani, Allaah Atamvisha nguo ya udhalili Siku ya Qiyaamah, kisha Atamwashia ndani yake moto”. [Abu Daawuwd (4029) na Ibn Maajah (3607) kwa Sanad Hasan Lighayrih].
Nguo ya umashuhuri ni nguo yoyote ambayo mtu anataka apate umashuhuri kwayo kwa watu, ni sawa ikiwa nguo yenyewe ni ya thamani kubwa anaivaa ili kujifaharisha nayo, au iwe ni ya thamani duni ili kuonyesha zuhd (kutoijali dunia) na riyaa.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ وَأَحْكَامُ النَّظَرِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia
لِبَاسُ المَرْأَةِ
Kivazi Cha Mwanamke
Alhidaaya.com [3]
007- Mwanamke Anaruhusiwa Kuvaa Hariri:
Jua dada yangu Muislamu kwamba wanawake wanaruhusiwa kuvaa hariri lakini wanaume hawaruhusiwi kutokana na neno lake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"حُرِّمَ لِبَاسُ الْحَرِيرِ وَالذَّهَبِ عَلَى ذُكُورِ أُمَّتِي وَأُحِلَّ لإِنَاثِهِمْ"
“Kuvaa hariri na dhahabu kumeharamishwa kwa wanaume wa umati wangu, lakini kumehalalishwa kwa wanawake wao”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (4057), At-Tirmidhiy (1720), An-Nasaaiy (8/160) na Ibn Maajah (3595)].
‘Aliyy amesema:
"كَسَانِي اَلنَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ حُلَّةً سِيَرَاءَ، فَخَرَجْتُ فِيهَا، فَرَأَيْتُ اَلْغَضَبَ فِي وَجْهِهِ، فَشَقَقْتُهَا بَيْنَ نِسَائِي"
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alinivisha vazi la “siyraa”, nami nikatoka nalo nje nimelivaa, nikaona ghadhabu kwenye uso wake, nikalipasua, nikaligawa kati ya wake (wa jamaa) zangu”. [Al-Bukhaariy (5840) na Muslim (2071)].
Ametoa dalili kwa maneno haya kwamba inajuzu kwa mwanamke kuvaa hariri safi asili kwa kujengea kwamba vazi la “siyraa” halishonwi ila kwa hariri safi. [Fat-hul Baariy (1/300)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ وَأَحْكَامُ النَّظَرِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia
لِبَاسُ المَرْأَةِ
Kivazi Cha Mwanamke
Alhidaaya.com [3]
008-Sehemu Ya Nguo Ya Mwanamke Inayoburuza Chini:
Ummu Salamah:
"قُلْتُ لِرَسُولِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ حِينَ ذُكِرَ الإِزَارُ: فَالْمَرْأَةُ يَا رَسُولَ اللَّهِ؟ قَالَ: تُرْخِيهِ شِبْرًا، قُلْتُ: إِذًا يَنْكَشِفُ عَنْهَا، قَالَ: فَذِرَاعًا لاَ تَزِيدُ عَلَيْهِ"
“Nilimwambia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wakati ilipotajwa izari (ifike wapi kwa mwanaume): Na vipi kuhusu mwanamke ee Rasuli wa Allaah? Akasema: Ateremshe shubiri. Nikasema: Ikiwa hivyo, basi miguu (kwato) itaonekana (wakitembea). Akasema: Basi iwe dhiraa, na isizidi zaidi ya hapo”. [Abu Daawuwd (4117), na Maalik katika Al-Muwattwa (1700) kwa Sanad Swahiyh].
Hadiyth hii inathibitisha kwamba wanawake wako nje ya duara la makamio yanayowahusu wanaume wenye kuburura nguo. ‘Ulamaa kwa sauti moja wanasema kwamba inajuzu mwanamke kuteremsha nguo yake chini ya vifundo viwili vya miguu.
Ingia kwenye tovuti upate kujua urefu halisi wa dhiraa na shubiri.
Faida:
Ni kutokea wapi inapimwa shubiri ambayo mwanamke anaiteremsha nguo yake?
Shubiri hupimwa toka nusu ya muundi kama ilivyonukuliwa katika Kitabu cha ‘Awnul Ma’abuwd (11/174). Na kwa ajili hiyo, Ummu Salamah akasema kwamba kwato za miguu yao zitaonekana, na hapo Rasuli akawaruhusu kuteremsha dhiraa. Na makusudio hapa, ni kumzindua mwanamke ajue mambo mawili. La kwanza, ni kuwa ni wajibu kwake afunike kwato zake mbili kwa nguo yake, na pili ni kwamba inajuzu kuiteremsha nguo yake kwa kiasi cha kutozidi dhiraa kama tulivyotangulia kusema.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ وَأَحْكَامُ النَّظَرِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia
لِبَاسُ المَرْأَةِ
Kivazi Cha Mwanamke
Alhidaaya.com [3]
009- Kivazi Cha Mwanamke: Mwanamke Kuvaa Suruali:
Suruali ni mtihani mbaya zaidi uliowakumba wanawake wengi (Allaah Awahidi). Ingawa suruali zao zinasitiri uchi, lakini wakati huo huo zinakuwa zikitoa umbile la mwanamke kwa picha ya kuchemsha matamanio ya wanaume na hususan zinapokuwa na rangi tofauti, miundo na aina. Na dada zetu wa Kiislamu, bila shaka mmeshajua kwamba miongoni mwa shuruti za hijabu ya kisharia ni isiwe nguo yenye kubana mwili kiasi cha kuonyesha maungo ya kuvutia ya mwili. Imekuwa suruali kwa sasa ndio yenye uchochezi na fitnah zaidi kuliko nguo fupi, ima kwa kuwa kwake inabana sana, au kwa kuwa sawa na rangi ya ngozi ya mwili kiasi cha kuonekana kama hakuvaa kitu. Huu ni uovu mbaya ulioenea, na kwa ajili hiyo, haifai mwanamke kuvaa suruali isipokuwa kama atamvalia mumewe lakini kwa sharti kwamba isifanane na ya wanaume, na wala asitoke nayo mbele ya maharimu zake wala watu ajinabi. Pamoja na hayo yote, hakuna ubaya akivaa suruali ndani ya abaya linalomsitiri, kwani itamsitiri asionekane mwili na hususan wakati anapopanda gari na mfano wake. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi.
Je, Mwanamke Anaruhusiwa Kuvaa Viatu Vya Visigino Virefu?
Ibn Mas-‘uwd amesema:
"كَانَ الرِّجَالُ وَالنِّسَاءُ في بَنِيْ إِسْرَائِيْلَ يُصَلُّونَ جَمِيْعًا، فَكَانَتِ المَرْأَةُ لَهَا الخَلِيْلُ تَلْبَسُ القَالِبَيْنِ تَطُوْلُ بِهِمَا لِخَلِيْلِهَا، فَأُلْقِيَ عَلَيْهِنَّ الحَيْضُ". فَكَانَ ابنُ مَسْعُودِ يَقُوْلُ: "أَخْرِجُوهُنَّ حَيْثُ أَخْرَجَهُنَّ اللهُ"
“Wanaume na wanawake wa Kinabiy Israaiyl walikuwa wanaswali wote kwa pamoja. Akawa mwanamke mwenye mpenzi wake anavaa viatu vya mbao vya soli ndefu vinavyomfanya aonekane mrefu kwa mpenzi wake. Na kwa sababu hiyo, wakateremshiwa hedhi.” Na akawa Ibn Mas-‘uwd anasema: “Wawekeni nyuma pale ambapo Allaah Amewaweka”. [Muswannafu ‘Abdulrazzaaq (5115) na Sanad yake ni Swahiyh].
Linaloonekana kuhusiana na visigino virefu ni kwamba ikiwa mwanamke atavaa ili achomoze kwa wanaume na wanaume wapate kumwona, basi itakuwa ni haramu, kwa kuwa viatu hivyo vya visigino virefu katika hali hii, vitakuwa ndiyo sababu ya uharibifu na uenezaji wa maasia. [Jaami’u Ahkaamin Nisaa (4/434)].
Ninasema: “Kuongezea na haya, kuvaa viatu vya visigino virefu kunaufanya mwendo wa mwanamke na miondoko yake kuwa yenye kuvutia macho ya wanaume, mbali na sauti yake ambayo pia inawababaisha. Na kwa msingi huu, mwanamke hatakiwi avae viatu hivi anapotoka nyumbani kwake”.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ وَأَحْكَامُ النَّظَرِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia
لِبَاسُ المَرْأَةِ
Kivazi Cha Mwanamke
Alhidaaya.com [3]
010- Kivazi Cha Mwanamke Mbele Ya Maharimu Zake:
Kabla hatujaelezea sehemu ya mwili ambayo inajuzu kwa mwanamke kuiwacha wazi mbele ya maharimu zake, ingelipendeza kwanza tumjue mahram ni nani.
Mahram ni kila mwanaume ambaye ni haramu kwake kumwoa mwanamke uharamu wa milele kutokana na kuwepo sababu halali ya kuzuia hilo. Mahram huyu, anaruhusiwa kumwangalia mwanamke huyu, kukaa naye peke yake na kusafiri pamoja naye. Tukisema “Uharamu wa milele”, tunamtoa nje ya duara hili dada ya mke, shangazi yake, khalati yake na mfano wao, kwani hawa uharamu wao ni wa muda. [Sharhu Muslim cha An-Nawawiy (3/484)].
Allaah Ta’aalaa Anasema:
"وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا لِبُعُولَتِهِنَّ أَوْ آبَائِهِنّ"
“Na wasidhihirishe mapambo yao isipokuwa kwa waume zao, au baba zao”. [An-Nuwr: 31].
Aayah hii inaruhusu maharimu kuangalia sehemu za mapambo ya mwanamke, kwa kuwa dharura inalazimisha kuchanganyika, kuweko maingiliano, mapishano na matangamano ambayo huwafanya waonane mara nyingi na waangaliane kutokana na ukaraba. Isitoshe, fitnah baina yao iko mbali.
Katika aayah hii, Allaah Ta’aalaa Ameanza na waume kisha maharimu wengineo. Maharimu hawa kiujumla ni hawa wafuatao:
1- Baba na pia mababu, ni sawa wa upande wa baba au wa mama.
2- Baba wa mke (baba mkwe).
3- Watoto wao wa kiume na watoto wa kiume wa waume zao. Hapa wanaingia pia wajukuu na kwenda chini.
4- Makaka zake (ndugu zake wa kiume), ni sawa wawe wa tumbo moja baba na mama, au kwa baba tu, au kwa mama tu, na hata wakienda chini.
5- Watoto wa kiume wa kaka au wa dada, kwa kuwa hawa ni makaka, wote ni ndugu.
6- Maami (baba wadogo) na wajomba, hawa ni maharimu ingawa hawakutajwa katika Aayaah tukufu. Jumhuwr ya ‘Ulamaa wanasema kuwa hukmu ya hawa ni sawa na maharimu wengineo, na ushahidi wake ni Hadiyth ya ‘Aaishah:
"أَنَّ أَفْلَحَ أَخَا أَبِي الْقُعَيْسِ، جَاءَ يَسْتَأْذِنُ عَلَيْهَا وَهُوَ عَمُّهَا مِنَ الرَّضَاعَةِ بَعْدَ أَنْ أُنْزِلَ الْحِجَابُ قَالَتْ فَأَبَيْتُ أَنْ آذَنَ لَهُ فَلَمَّا جَاءَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَخْبَرْتُهُ بِالَّذِي صَنَعْتُ فَأَمَرَنِي أَنْ آذَنَ لَهُ عَلَىَّ"
“Kwamba kaka wa Aflah Al-Qu’ays ambaye ni ami yake kwa kunyonya, alikuja na kumbishia hodi baada ya kushuka Aayaah ya hijab ya kuwaamuru wake za Nabiy kuweka pazia wasionwe na wanaume. ‘Aaishah anasema: Nilikataa kumfungulia mlango. Na alipokuja Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) nilimweleza jambo nililolifanya, naye akaniamuru nimfungulie mlango akija”. [Al-Bukhaariy (5103) na Muslim (1445)].
7- Maharimu wa kunyonya, na hawa pia hawakutajwa kwenye Aayah. ‘Ulamaa pia wamekubaliana kuwa hawa ni kama maharimu wengineo, na hii ni kwa Hadiyth ya ‘Aaishah iliyotajwa hapo juu.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ وَأَحْكَامُ النَّظَرِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia
لِبَاسُ المَرْأَةِ
Kivazi Cha Mwanamke
Alhidaaya.com [3]
011-Ni Kiasi Gani Cha Mwili Wake Ambacho Mwanamke Anaweza Kukiachilia Mbele Ya Maharimu Wake?
‘Ulamaa wana kauli mbili mashuhuri kuhusiana na hili:
Ya kwanza: Maharimu wanaruhusiwa kuangalia mwili wote wa mwanamke isipokuwa sehemu iliyo kati ya kitovu na magoti. Hii ni kauli ya madhehebu ya Jumhuwr. Dalili ni:
1- Neno lake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"..وَإِذَا أَنْكَحَ أَحَدُكُمْ عَبْدَهُ أَوْ أَجِيْرَهُ فَلَا يَنْظُرَنَّ مِنْ عَوْرَتِهِ، فَإِنَّ مَا أَسْفَلَ مِنْ سُرَّتِهِ إِلَى رُكْبَتَيْهِ من عَوْرَتِهِ"
“Na anapomwozesha mmoja wenu mtumwa wake au mtumishi wake, basi asiangalie sehemu yoyote ya uchi wake, kwa kuwa sehemu iliyo chini ya kitovu chake hadi kwenye magoti yake ni uchi wake”. [Ahmad (2/187) na Abu Daawuwd (495) kwa Sanad Hasan].
Hadiyth hii ingawa inawahusu wanaume ila ni kwamba wanawake ni ndugu moja na wanaume.
2- Hadiyth ya Abuu Salamah:
"دَخَلْتُ أَنَا وَأَخُو عَائِشَةَ عَلَى عَائِشَةَ فَسَأَلَهَا أَخُوهَا عَنْ غُسْلِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَدَعَتْ بِإِنَاءٍ نَحْوًا مِنْ صَاعٍ، فَاغْتَسَلَتْ وَأَفَاضَتْ عَلَى رَأْسِهَا، وَبَيْنَنَا وَبَيْنَهَا حِجَابٌ"
“Niliingia mimi pamoja na kaka yake ‘Aaishah kwa ‘Aaishah. Kaka yake akamuuliza namna Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anavyofanya ghuslu (ya janaba). Akaagiza aletewe maji kwenye chombo cha kiasi cha pishi, akaoga na kisha akajimiminia juu ya kichwa chake huku kikiweko kizuizi kati yetu na yeye”. [Al-Bukhaariy (251) na Muslim (320)].
Al-Qaadhiy ‘Ayyaadh amesema: “Inavyoonekana ni kwamba wawili hao waliona anavyofanya kwenye kichwa chake na sehemu ya juu ya mwili wake inayoruhusika kuonwa na mahram, kwa kuwa Bibi ‘Aaishah ni khalati ya Abu Salamah kwa kunyonya. Bibi ‘Aaishah alisitiri sehemu ya chini ya mwili wake ambayo si halali kwa mahram kuiona”.
Kauli ya pili: Maharimu wanaruhusiwa kuangalia sehemu ambayo kikawaida inakuwa wazi kwa mwanamke kama viungo vya wudhuu. [Sunan Al-Bayhaqiy (9417), Al-Inswaaf (8/20), Al-Mughniy (6/554) na Al-Majmuw’u (16/140)].
Ibn ‘Umar amesema:
"كَانَ الرِّجَالُ وَالنِّسَاءُ يَتَوَضَّئُونَ فِي زَمَانِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ جَمِيعًا"
“Wanaume na wanawake walikuwa wakitawadha wote kwa pamoja enzi ya Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam”. [Al-Bukhaariy (193), Abu Daawuwd (79), An-Nasaaiy (1/57) na Ibn Maajah (381)].
Na hili linachukulika kama linawahusu wake na maharimu. Na kwa muktadha huu, kuna dalili ya kujuzu mwanamume kuangalia sehemu za kutiwa maji ya wudhuu ya maharimu zake na kinyume chake. Allaah Ndiye Mjuzi zaidi.
Maangalizo:
1- Kwa mujibu wa maelezo yaliyotangulia, ruksa ya maharimu kumwangalia mwanamke inashurutishwa kwamba kuangalia kwenyewe kusiwe kwa njia ya matamanio, au kuhisi utamu, au burudiko. Ikiwa haya yatakuwepo, basi hakuna shaka kwamba itakuwa hairuhusiwi.
2- Baadhi ya ‘Ulamaa wametofautisha baina ya baadhi ya maharimu kingazi kwa ambayo mwanamke anaweza kuyaonyesha kwa mujibu wa yaliyomo ndani ya nafsi za watu. Hakuna shaka yoyote kwamba sehemu ya mwili ambayo mwanamke anaiacha wazi mbele ya baba yake au kaka yake, haiwi sawa mbele ya mtoto wa kiume wa mumewe, kwani huyu inabidi kuweko hadhari na sitara zaidi. Hivyo, ngazi za sehemu ya kuonekana ya mwili wake zinatofautiana. Kwa baba yake, atawacha wazi sehemu ambazo haruhusiwi kuziacha wazi mbele ya mtoto wa kiume wa mume wake. Haya yamesemwa na Al-Qurtubiy. [Yameelezwa haya pia na Sheikh wetu katika kitabu cha Jaami’u Ahkaamin Nisaa (4/504), kisha akasema: “Haya yanakubalika kwa upande wa mwono, lakini yanahitaji dalili ya kuyathibitisha”].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ وَأَحْكَامُ النَّظَرِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia
لِبَاسُ المَرْأَةِ
Kivazi Cha Mwanamke
Alhidaaya.com [3]
012-Mahram Anaruhusiwa Kumgusa Mwanamke Na Kumbusu Ikiwa Si Kwa Matamanio
Katika Hadiyth ya ‘Aaishah kuhusiana na yeye kumkasirikia ‘Abdullaah bin Az-Zubayr ambaye ni mtoto wa dada yake Asmaa, akaweka nadhiri kwamba hatomsemesha, na kisha ‘Abdullaah bin Az-Zubayr kumwomba na kumsihi aseme naye. (Na hii ni baada ya kupangwa namna ya kuwasuluhisha. Mpango ulipokuwa tayari, ‘Abdullaah bin Az-Zubayr alikwenda kwa ‘Aaishah pamoja na watu wawili, wakagonga mlango na) ‘Aaishah akasema:
"ادْخُلُوا كُلُّكُمْ -ولا تَعْلَمُ أّنَّ مَعَهُمَا ابنُ الزُّبَيْرِ- فَلَمَّا دّخَلُوا دَخَلَ ابن الزُّبِيْرِ الحِجَابَ فَاعْتَنَقَ عَائِشَةَ وطَفِقَ يُنِاشِدُهَا ويَبْكِيْ..."
“Ingieni nyote -naye hajui kwamba wako pamoja na ‘Abdullaah bin Az-Zubayr-. Walipoingia, ‘Abdullaah bin Az-Zubayr akaingia ndani ya pazia, akamkumbatia ‘Aaishah, na akaanza kumsihi na kumwomba (aachane na msimamo wake) huku analia. [Al-Bukhaariy (6073)].
Na pia ‘Aaishah amesema:
"..كَانَتْ إِذَا دَخَلَتْ عَلَيْهِ قَامَ إِلَيْهَا النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ، فَأَخَذَ بِيَدِهَا وَقَبَّلَهَا وَأَجْلَسَهَا فِي مَجْلِسِهِ، وَكَانَ إِذَا دَخَلَ عَلَيْهَا قَامَتْ إِلَيْهِ فَأَخَذَتْ بِيَدِهِ، فَقَبَّلَتْهُ، وَأَجْلَسَتْهُ فِي مَجْلِسِهَا"
“Alikuwa (Faatwimah) anapoingia, Rasuli humsimamia, akaukamata mkono wake, akambusu na kumkalisha sehemu yake anakoketi. Naye (Faatwimah) kwa upande wake, Rasuli anapoingia kwake, humsimamia, akaukamata mkono wake, akambusu na akamkalisha sehemu yake anakoketi”. [Abu Daawuwd (5217), At-Tirmidhiy (3872) na Al-Haakim (4/272). Ni Hadiyth Swahiyh].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ وَأَحْكَامُ النَّظَرِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia
لِبَاسُ المَرْأَةِ
Kivazi Cha Mwanamke
Alhidaaya.com [3]
013-Inajuzu Mwanamke Kupakiwa Nyuma Ya Mwanaume Ambaye Ni Maharimu Wake:
Ni kwa Hadiyth ya Anas ambaye amesema:
"كُنَّا مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مَقْفَلَهُ مِنْ عُسْفَانَ، وَرَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَلَى رَاحِلَتِهِ، وَقَدْ أَرْدَفَ صَفِيَّةَ بِنْتَ حُيَىٍّ، فَعَثَرَتْ نَاقَتُهُ فَصُرِعَا جَمِيعًا"
“Tulikuwa tunarudi pamoja na Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) toka ‘Usfaan. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa amempanda ngamia wake na amempakia nyuma yake (mkewe) Swafiyyah bint Huyay. Na mara ghafla ngamia wake akajikwaa na wote wawili wakaanguka chini. [Al-Bukhaariy (3085) na Muslim (1345)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ وَأَحْكَامُ النَّظَرِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia
لِبَاسُ المَرْأَةِ
Kivazi Cha Mwanamke
Alhidaaya.com [3]
014- Kivazi Cha Mwanamke Mbele Ya Wanawake Wenzake
Allaah Mtukufu Anasema:
"وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا مَا ظَهَرَ مِنْهَا ۖ وَلْيَضْرِبْنَ بِخُمُرِهِنَّ عَلَىٰ جُيُوبِهِنَّ ۖ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا لِبُعُولَتِهِنَّ أَوْ آبَائِهِنَّ أَوْ آبَاءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ أَبْنَائِهِنَّ أَوْ أَبْنَاءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي أَخَوَاتِهِنَّ أَوْ نِسَائِهِنَّ"
“Na wala wasidhihirishe mapambo yao isipokuwa yale yanayodhihirika. Na waangushe khimaar (shungi) zao mpaka vifuani mwao, na wasidhihirishe mapambo yao isipokuwa kwa waume zao, au baba zao, au baba za waume wao, au wana wao wa kiume, au wana wa kiume wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kiume wa kaka zao, au wana wa kiume wa dada zao, au wanawake wenzao (wa Kiislamu)”. [An-Nuwr: 31]
Ibn Kathiyr amesema (3/284): Neno Lake “Au wanawake wenzao”, ina maana adhihirishe pambo lake pia kwa wanawake wenzake wa Kiislamu.
Na uchi wa mwanamke ambao ni lazima ausitiri kwa mwanamke mwenzake, ni uchi ule ule wa mwanaume kwa mwanaume mwenzake ambao ni kutoka kitovu hadi magoti. [Al-Mughniy (6/562)].
Haijuzu mwanamke kuangalia sehemu ya kati ya kitovu na magoti ya mwanamke mwenzake kama wanavyofanya hivyo wanawake wengi wa Kiislamu. Ibn Al-Jawziy amesema: “Wanawake wengi wasiofahamu, hawajali kuachia wazi uchi wao au sehemu ya uchi mbele ya mama, au dada, au bint huku wakisema kwamba hawa ni watu wa karibu. Basi na ajue kila mwanamke kwamba akifikisha miaka saba, haruhusiwi mama yake, wala dada yake wala binti yake kuangalia uchi wake”. [Ahkaamun Nisaa cha Ibn Al-Jawziy (uk. 76)].
Ninasema: “Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"لَا يَنْظُرُ الرَّجُلُ إِلَى عَوْرَةِ الرَّجُلِ وَلَا الْمَرْأَةُ إِلَى عَوْرَةِ الْمَرْأَةِ ، وَلَا يُفْضِي الرَّجُلُ إِلَى الرَّجُلِ فِي ثَوْبٍ وَاحِدٍ وَلَا تُفْضِي الْمَرْأَةُ إِلَى الْمَرْأَةِ فِي ثَوْبٍ وَاحِدٍ "
“Mwanaume haruhusiwi kuangalia uchi wa mwanaume mwenzake, wala mwanamke kuangalia uchi wa mwanamke mwenzake. Na mwanaume asigusane ngozi kwa ngozi na mwanaume mwenzake ndani ya nguo moja, na mwanamke pia asigusane ngozi kwa ngozi na mwanamke mwenzake ndani ya nguo moja”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (338), At-Tirmidhiy (2793) na Abu Daawuwd (4018)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ وَأَحْكَامُ النَّظَرِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia
لِبَاسُ المَرْأَةِ
Kivazi Cha Mwanamke
Alhidaaya.com [3]
015-Je, Mwanamke Wa Kiislamu Anaruhusiwa Kuonyesha Mapambo Yake Kwa Mwanamke Kafiri?
Kundi la baadhi ya ‘Ulamaa wanaona kwamba haijuzu kwa mwanamke kuonyesha mapambo yake kwa wanawake wasio wa Kiislamu ili wasije kwenda kuelezea na kusifu waliyoyaona kwa waume zao. Na hii ni kwa Neno Lake Ta’aalaa: أَوْ نِسَائِهِنَّ “au wanawake wenzao” ambao ni wanawake wa Kiislamu. Na kwa hivyo, wanatoka nje ya duara hili wanawake wa kipagani ikiwa ni pamoja na wanaoishi chini ya ulinzi wa dola ya Kiislamu (dhimmiyyaat) na wengineo.
Ama ‘Ulamaa wengineo, hao wanaona kwamba hilo linajuzu, na kwamba hakuna tofauti kati ya mwanamke wa Kiislamu na mwanamke wa kidhimmiyat katika kumwangalia mwanamke mwenzake. Dalili yao wanasema kwamba wanawake makafiri wa Kiyahudi walikuwa wakiingia kwa wake za Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na wala hawakuwa wanajifunika, na hawakuamrishwa pia kujifunika. Bibi ‘Aaishah amesema:
"أَنَّ يَهُودِيَّةً دَخَلَتْ عَلَيْهَا فَذَكَرَتْ عَذَابَ الْقَبْرِ فَقَالَتْ لَهَا أَعَاذَكِ اللَّهُ مِنْ عَذَابِ الْقَبْرِ ، فَسَأَلَتْ عَائِشَةُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ عَذَابِ الْقَبْرِ فَقَالَ: نَعَمْ عَذَابُ الْقَبْر ، قَالَت عَائِشَة رَضِي الله عَنْهَا: فَمَا رَأَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بعد صلى صَلَاة إِلَّا تَعَوَّذَ مِنْ عَذَابِ الْقَبْر"
“Kwamba mwanamke mmoja wa Kiyahudi alimtembelea na akamwelezea adhabu ya kaburi, halafu akamwambia (akimwombea): Allaah Akulinde na adhabu ya kaburi. ‘Aaishah baadaye akaja kumuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu adhabu ya kaburi, naye akamjibu: Na’am, adhabu ya kaburi iko. ‘Aaishah anaendelea kusema: Sikumwona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) baada ya Swalaah yoyote anayoiswali, isipokuwa anajilinda kwa Allaah na adhabu ya kaburi”. [Al-Bukhaariy (1372) na Muslim (903)].
Asmaa amesema:
"إِنَّ أُمِّي قَدِمَتْ عَلَىَّ وَهِىَ رَاغِبَةٌ ، فَسَأَلْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ : أَفَأَصِلُهَا؟ قَالَ: نَعَمْ "
“Mama yangu alikuja kunitembelea naye amekakasika na Uislamu, nikamuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam): Je, niendelee kutangamana naye kwa wema? Akasema: Na’am”. [Al-Bukhaariy (2620) na Muslim (1003)].
Ninasema: “Ikiwa mwanamke wa Kiyahudi au Kinaswara atashukiwa kwamba anamweleza mumewe anayoyaona kwa mwanamke wa Kiislamu, basi mwanamke wa Kiislamu ajizuie kuonyesha mapambo yake kwake. Allaah Ndiye Ajuaye zaidi”.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ وَأَحْكَامُ النَّظَرِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia
لِبَاسُ المَرْأَةِ
Kivazi Cha Mwanamke
Alhidaaya.com [3]
016-Kivazi Cha Mwanamke Mbele Ya Mtumwa Wake:
‘Ulamaa wengi wanaona kwamba mtumwa anayemilikiwa na mwanamke anakuwa ni kama mahramu yake, anaweza kumwangalia yale anayoyaangalia mahramu. Dalili yao ni Kauli Yake Ta’aalaa:
"وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا مَا ظَهَرَ مِنْهَا ۖ وَلْيَضْرِبْنَ بِخُمُرِهِنَّ عَلَىٰ جُيُوبِهِنَّ ۖ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا لِبُعُولَتِهِنَّ أَوْ آبَائِهِنَّ أَوْ آبَاءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ أَبْنَائِهِنَّ أَوْ أَبْنَاءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي أَخَوَاتِهِنَّ أَوْ نِسَائِهِنَّ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُنَّ"
“Na wala wasidhihirishe mapambo yao isipokuwa yale yanayodhihirika. Na waangushe khimaar (shungi) zao mpaka vifuani mwao, na wasidhihirishe mapambo yao isipokuwa kwa waume zao, au baba zao, au baba za waume wao, au wana wao wa kiume, au wana wa kiume wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kiume wa kaka zao, au wana wa kiume wa dada zao, au wanawake wao (wa Kiislamu), au wale iliyowamiliki mikono yao ya kuume”. [An-Nuwr: 31].
Wamesema: Kauli Yake أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُنَّ “au wale iliyowamiliki mikono yao ya kuume”, inawahusu watumwa wa kiume na vijakazi, na haiwezekani kauli hii ikawahusu vijakazi, kwa kuwa hilo limetajwa kabla ya hapo katika Kauli Yake Ta’aalaa أَوْ نِسَائِهِنَّ “au wanawake wenzao”. [Al-Mabsuwtw (10/157)].
Na pia Hadiyth ya Anas:
"أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَتَى فَاطِمَةَ بِعَبْدٍ قَدْ وَهَبَهُ لَهَا، قَالَ: وَعَلَى فَاطِمَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا ثَوْبٌ، إِذَا قَنَّعَتْ بِهِ رَأْسَهَا لَمْ يَبْلُغْ رِجْلَيْهَا، وَإِذَا غَطَّتْ بِهِ رِجْلَيْهَا لَمْ يَبْلُغْ رَأْسَهَا، فَلَمَّا رَأَى النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مَا تَلْقَى قَالَ: إِنَّهُ لَيْسَ عَلَيْكِ بَأْسٌ إِنَّمَا هُوَ أَبُوكِ وَغُلاَمُكِ "
“Kwamba Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimletea Faatwimah mtumwa ambaye alikuwa amemzawadia, na Faatwimah amevaa nguo ambayo akijifunika kichwa chake haifiki chini ikafunika miguu, na akijifunika nayo miguu, basi haifiki kichwani. Rasuli alipoona Faatwimah anavyohangaika alimwambia: Usitaabike, hakuna neno, ni mimi hapa baba yako na mtumwa wako”. [Abu Daawuwd (4106) na Al-Bayhaqiy (7/95). Ni Hadiyth Hasan].
Sheikh wa Uislamu amerajihisha kujuzu mtumwa kumwangalia bibi anayemmiliki kwa ajili ya haja, kwa kuwa bibi huyu anahitaji kuzungumza na mtumwa wake zaidi ya anavyohitajia kuonwa na shuhuda, au mwenye kufanya naye miamala au anayemsemesha. Na hawa kama wanaruhusiwa kumwangalia, basi mtumwa wake ana haki zaidi ya kumwangalia. [Majmuw’ul Fataawaa (16/141)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ وَأَحْكَامُ النَّظَرِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia
لِبَاسُ المَرْأَةِ
Kivazi Cha Mwanamke
Alhidaaya.com [3]
017-Kivazi Cha Mwanamke Kwa Wanaume Wasio Na Matamanio Ya Wanawake:
Allaah Amesema:
"أَوِ التَّابِعِينَ غَيْرِ أُولِي الْإِرْبَةِ مِنَ الرِّجَالِ"
“Au wafuasi wanaume wasio na matamanio ya jimai miongoni mwa wanaume”. [An-Nuwr: 31].
Hawa ni wale wasio na matamanio ya kingono kwa wanawake kutokana na utu uzima uliopevuka, au ukhanithi, au kufa kabisa nguvu za kiume. Watu kama hawa wanaruhusika kumwangalia mwanamke kwa haja ya dharura tu ili kuepusha usumbufu, lakini ikiwa itagundulika kwamba khanithi kwa mfano anadadisi mambo ya akina mama na kuyaeleza kwa watu nje, basi huyo atazuiliwa kuingia kwa wanawake na kuwaangalia.
Ummu Salamah amesema:
"أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ عِنْدَهَا وَفِي الْبَيْتِ مُخَنَّثٌ ، فَقَالَ المُخَنَّثٌ لِعَبْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي أُمَيَّةَ أَخِي أُمِّ سَلَمَةَ: يَا عَبْدَ اللَّهِ إِنْ فَتَحَ اللَّهُ لَكُمْ غَدًا الطَّائِفَ فَإِنِّي أَدُلُّكَ عَلَى ابْنَةِ غَيْلَانَ فَإِنَّهَا تُقْبِلُ بِأَرْبَعٍ وَتُدْبِرُ بِثَمَانٍ ، فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: لَا يَدْخُلَنَّ هَذا عَلَيْكُم"
“Kwamba Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa nyumbani kwake na ndani ya nyumba yuko khanithi. Khanithi yule akamwambia kaka wa Ummu Salamah ‘Abdullaah bin Abiy Umayyah: Ee ‘Abdullaah! Allaah Akiwafungulieni Twaif kesho mkaiteka, basi nitakupeleka umuone binti wa Ghaylaan. Akikuelekea, utaona mikunjano minne ya tumbo lake (kutokana na unene), na akikupa mgongo, utaona minane. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema hapo hapo: Msimruhusu huyu kuingia tena hapa”. [Al-Bukhaariy (5235) na Muslim (2180)].
Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipomsikia anamsifia binti wa Ghaylaan, alijua kwamba huyo anafahamu na kufuatilia mambo ya wanawake, na moja kwa moja akaamuru asiruhusiwe kuingia kwake.
Angalizo:
Jumhuwr ya ‘Ulamaa wamekubaliana kwamba mwanaume aliyehasiwa au aliyekatwa uume, ni haramu kwao kuwaangalia wanawake, kwa kuwa kiungo ingawa hakifanyi kazi au hakipo, lakini matamanio ya wanaume yanabakia kwenye nyoyo zao. [Angalia Al-Mabsuwtw (10/158) na Al-Majmuw’u (16/140)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ وَأَحْكَامُ النَّظَرِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia
لِبَاسُ المَرْأَةِ
Kivazi Cha Mwanamke
Alhidaaya.com [3]
018-Kuonyesha Mapambo Kwa Watoto Ambao Hawafahamu Chochote Kuhusu Mambo Ya Wanawake Wala Uchi Wao:
Allaah Amesema:
"أَوِ الطِّفْلِ الَّذِينَ لَمْ يَظْهَرُوا عَلَىٰ عَوْرَاتِ النِّسَاءِ"
“Au watoto ambao hawatambui kitu kuhusu sehemu za siri za wanawake”. [An-Nuwr: 31].
Ibn Kathiyr amesema: “Yaani, kutokana na umri wao mdogo, hawafahamu hali za wanawake na nyuchi zao, au maneno yao ya siri za ndani. Ikiwa mtoto ni mdogo hafahamu chochote katika hayo, basi hakuna ubaya kuingia kwa wanawake. Lakini kama ni barobaro au anakaribia ubarobaro kiasi ambacho anaweza kuyajua hayo na kuyatambua, au anaweza kutofautisha kati ya mwanamke mbaya na mrembo, basi asiruhusiwe kuingia kwa wanawake”.
Yanayoashiria hayo ni Hadiyth ya Jaabir:
"أَنَّ أُمَّ سَلَمَةَ اسْتَأْذَنَتْ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي الْحِجَامَةِ ، فَأَمَرَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَبَا طَيْبَةَ أَنْ يَحْجُمَهَا، قَالَ: حَسِبْتُ أَنَّهُ قَالَ: كَانَ أَخَاهَا مِنَ الرَّضَاعَةِ أَو غُلَامًا لم يَحْتَلِمْ."
“Kwamba Ummu Salamah alimwomba ruhusa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) afanye hijama. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwamuru Abu Twaybah amuumike. Anasema: Nadhani kama alisema: Alikuwa ni kaka yake wa kunyonya au kijana mdogo ambaye hajabaleghe”. [Muslim (2206), Abu Daawuwd (4105) na Ibn Maajah (3480)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ وَأَحْكَامُ النَّظَرِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia
لِبَاسُ المَرْأَةِ
Kivazi Cha Mwanamke
Alhidaaya.com [3]
019-Kivazi Cha Mwanamke Na Mapambo Yake Kwa Mumewe:
Kauli ya Jumhuwr inasema: “Mke na mume wana haki ya kuangaliana wenyewe kwa wenyewe mwili mzima bila ukakasi wowote, ni sawa iwe kwa matamanio au bila matamanio, iwe kwenye sehemu nyeti au penginepo popote”. Baadhi ya yanayoashiria hili ni:
1- Kauli Yake Ta’aalaa:
"وَالَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ • إِلَّا عَلَىٰ أَزْوَاجِهِمْ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِين"َ
“Na ambao wanahifadhi tupu zao • Isipokuwa kwa wake zao, au wale iliyowamiliki mikono yao ya kuume, basi hao si wenye kulaumiwa”. [Al-Ma’aarij: 29, 30].
Aayah hii inaonyesha kwamba yaliyo juu ya kuangalia ambayo ni kugusa na kuvaana kimwili, ni halali kwao. Na kwa vile mume ameruhusiwa kustarehe na utupu wa mkewe, basi kwa ustahikivu zaidi, anaruhusiwa kuuangalia na kuugusa kama sehemu nyinginezo zote za mwili. [Al-Mabsutw (10/148) na Al-Muhallaa (10/33)].
2- ‘Aaishah amesema:
"كُنْتُ أَغْتَسِلُ أَنَا وَالنَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مِنْ إِنَاءٍ وَاحِدٍ مِنْ قَدَحٍ يُقَالُ لَهُ الْفَرَقُ"
“Nilikuwa mimi naoga pamoja na Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwenye chombo kimoja kiitwacho “Al-Faraq”. [Al-Bukhaariy (250) na Muslim (319)].
Na hii ni dalili ya kujuzu mwanaume kuangalia uchi wa mkewe na mkewe kuangalia wake. [Fat-hul Baariy (1/364)].
3- Toka kwa Bahz bin Hakiym, toka kwa baba yake toka kwa babu yake, amesema:
"يَا رَسُولَ اللَّهِ ، عَوْرَاتُنَا مَا نَأْتِي مِنْهَا وَمَا نَذَرُ؟ قَالَ: "احْفَظْ عَوْرَتَكَ إِلاَّ مِنْ زَوْجَتِكَ أَوْ مِمَّا مَلَكَتْ يَمِينُكَ"
“Ee Rasuli wa Allaah! Kuhusu nyuchi zetu, ni zipi ambazo tunaweza kuzifunika, na ni zipi ambazo tunaweza kuziachia? Akasema: Uhifadhi uchi wako isipokuwa kwa mkewe au watumwa wako”. [Hadiyth Hasan. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (7/40), At-Tirmidhiy (2769) na Ibn Maajah (1920)].
Kiufupi, hakuna mpaka wa uchi kati ya mke na mume. Mwanamke anaruhusiwa kuvaa chochote atakacho kwa mumewe, kuvua chochote atakacho, na kujipamba kwa mumewe kwa aina zote za mapambo yanayoruhusiwa kisharia ambayo yatakuja kuzungumziwa milango ya mbeleni In Shaa Allaah.
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/284
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11512&title=09B-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20%D9%83%D9%90%D8%AA%D8%A7%D8%A8%D9%8F%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%91%D9%90%D8%A8%D8%A7%D8%B3%D9%90%20%D9%88%D9%8E%D8%A7%D9%84%D8%B2%D9%91%D9%90%D9%8A%D9%86%D9%8E%D8%A9%D9%90%20%D9%88%D9%8E%D8%A3%D9%8E%D8%AD%D9%92%D9%83%D8%A7%D9%85%D9%90%20%D8%A7%D9%84%D9%86%D9%91%D9%8E%D8%B8%D9%8E%D8%B1%20-%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20%20%D9%84%D9%90%D8%A8%D9%8E%D8%A7%D8%B3%D9%8F%20%D8%A7%D9%84%D9%85%D9%8E%D8%B1%D9%92%D8%A3%D9%8E%D8%A9%D9%90%20%20Kivazi%20Cha%20Mwanamke
[3] http://www.alhidaaya.com/
[4] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11513&title=01-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Kivazi%20Cha%20Mwanamke%3A%20Kivazi%20Cha%20Mwanamke%20Mbele%20Ya%20Wanaume%20Wasio%20Maharimu
[5] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11514&title=02-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Kivazi%20Cha%20Mwanamke%3A%20Masharti%20Ya%20Kivazi%20Cha%20Mwanamke%20Wa%20Kiislamu%2C%20Sharti%20La%20Kwanza
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11515&title=03-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Kivazi%20Cha%20Mwanamke%3A%20Masharti%20Ya%20Kivazi%20Cha%20Mwanamke%20Wa%20Kiislamu%2C%20Sharti%20La%20Pili
[7] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11516&title=04-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Kivazi%20Cha%20Mwanamke%3A%20Masharti%20Ya%20Kivazi%20Cha%20Mwanamke%20Wa%20Kiislamu%2C%20Sharti%20La%20Tatu%20Na%20La%20Nne
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11517&title=05-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Kivazi%20Cha%20Mwanamke%3A%20Masharti%20Ya%20Kivazi%20Cha%20Mwanamke%20Wa%20Kiislamu%2C%20Sharti%20La%20Tano%20Na%20La%20Sita%20
[9] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11518&title=06-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Kivazi%20Cha%20Mwanamke%3A%20Masharti%20Ya%20Kivazi%20Cha%20Mwanamke%20Wa%20Kiislamu%2C%20Sharti%20La%20Saba%20Na%20La%20Nane%20
[10] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11519&title=07-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Kivazi%20Cha%20Mwanamke%3A%20Mwanamke%20Anaruhusiwa%20Kuvaa%20Hariri
[11] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11520&title=08-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Kivazi%20Cha%20Mwanamke%3A%20Sehemu%20Ya%20Nguo%20Ya%20Mwanamke%20Inayoburuza%20Chini%20
[12] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11521&title=09-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Kivazi%20Cha%20Mwanamke%3A%20Mwanamke%20Kuvaa%20Suruali
[13] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11522&title=10-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Kivazi%20Cha%20Mwanamke%3A%20Kivazi%20Cha%20Mwanamke%20Mbele%20Ya%20Maharimu%20Zake%20
[14] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11523&title=11-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Kivazi%20Cha%20Mwanamke%3A%20Ni%20Kiasi%20Gani%20Cha%20Mwili%20Wake%20Ambacho%20Mwanamke%20Anaweza%20Kukiachilia%20Mbele%20Ya%20Maharimu%20Wake%3F%20
[15] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11524&title=12-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Kivazi%20Cha%20Mwanamke%3A%20Mahram%20Anaruhusiwa%20Kumgusa%20Mwanamke%20Na%20Kumbusu%20Ikiwa%20Si%20Kwa%20Matamanio%20
[16] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11525&title=13-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Kivazi%20Cha%20Mwanamke%3A%20Inajuzu%20Mwanamke%20Kupakiwa%20Nyuma%20Ya%20Mwanaume%20Ambaye%20Ni%20Maharimu%20Wake%20
[17] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11526&title=14-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Kivazi%20Cha%20Mwanamke%3A%20Kivazi%20Cha%20Mwanamke%20Mbele%20Ya%20Wanawake%20Wenzake
[18] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11527&title=15-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Kivazi%20Cha%20Mwanamke%3A%20Je%2C%20Mwanamke%20Wa%20Kiislamu%20Anaruhusiwa%20Kuonyesha%20Mapambo%20Yake%20Kwa%20Mwanamke%20Kafiri%3F%20
[19] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11528&title=16-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Kivazi%20Cha%20Mwanamke%3AKivazi%20Cha%20Mwanamke%20Mbele%20Ya%20Mtumwa%20Wake%20
[20] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11529&title=17-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Kivazi%20Cha%20Mwanamke%3A%20Kivazi%20Cha%20Mwanamke%20Kwa%20Wanaume%20Wasio%20Na%20Matamanio%20Ya%20Wanawake
[21] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11530&title=18-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Kivazi%20Cha%20Mwanamke%3A%20Kuonyesha%20Mapambo%20Kwa%20Watoto%20Ambao%20Hawafahamu%20Chochote%20Kuhusu%20Mambo%20Ya%20Wanawake%20Wala%20Uchi%20Wao%20
[22] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11531&title=19-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Kivazi%20Cha%20Mwanamke%3A%20Kivazi%20Cha%20Mwanamke%20Na%20Mapambo%20Yake%20Kwa%20Mumewe