Alhidaaya.com
Published on Alhidaaya.com (https://www.alhidaaya.com/sw)

Ukurasa Wa Kwanza > 09C-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: كِتابُ اللِّباسِ وَالزِّينَةِ وَأَحْكامِ النَّظَر - Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia: أَحْكَامُ النَّظَرِ Hukmu Za Kuangalia

09C-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: كِتابُ اللِّباسِ وَالزِّينَةِ وَأَحْكامِ النَّظَر - Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia: أَحْكَامُ النَّظَرِ Hukmu Za Kuangalia

Swahiyh Fiqh As-Sunnah [1]

 

 

 

 

 

كِتابُ اللِّباسِ وَالزِّينَةِ وَأَحْكامِ النَّظَر

 

 Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia

 

 

 

أَحْكَامُ النَّظَرِ

Hukumu Za Kuangalia 

 

 

Abu Maalik Kamaal Bin As-Sayyid Saalim

 

Imetarjumiwa na 'Abdullaah Mu'aawiyah (Abu Baasim)

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share [2]

01-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia: Hukumu Za Kuangalia: Mwanaume Asiye Maharimu Kumwangalia Mwanamke

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ  وَأَحْكَامُ النَّظَرِ

 

 Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia 

 

  

أَحْكَامُ النَّظَرِ

Hukumu Za Kuangalia 

  

Alhidaaya.com [3] 

 

 

 

01-Mwanaume Asiye Maharimu Kumwangalia Mwanamke:

 

Ni haramu kwa mwanaume kumwangalia mwanamke bila dharura, na Allaah Amewaamuru kuinamisha macho yao chini.

 

1-  Allaah Ta’aalaa Amesema:

 

قُل لِّلْمُؤْمِنِينَ يَغُضُّوا مِنْ أَبْصَارِهِمْ وَيَحْفَظُوا فُرُوجَهُمْ ۚ ذَٰلِكَ أَزْكَىٰ لَهُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ خَبِيرٌ بِمَا يَصْنَعُونَ ﴿٣٠﴾

 

30.  Waambie Waumini wanaume wainamishe macho yao na wahifadhi tupu zao. Hivyo ni utakaso zaidi kwao.  Hakika Allaah Ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika kwa yale wayatendayo.  [An-Nuwr: 30] 

 

 

2-  Ibn ‘Abbaas amesema:

 

"كَانَ الْفَضْلُ بْنُ عَبَّاسٍ رَدِيفَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ، فَجَاءَتْهُ امْرَأَةٌ مِنْ خَثْعَمَ تَسْتَفْتِيهِ ، فَجَعَلَ الْفَضْلُ يَنْظُرُ إِلَيْهَا وَتَنْظُرُ إِلَيْهِ ، فَجَعَلَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَصْرِفُ وَجْهَ الْفَضْلِ إِلَى الشِّقِّ الآخَرِ"

 

“Al-Fadhl bin ‘Abbaas alikuwa amepanda nyuma ya mnyama wa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam), akamjia mwanamke toka Khath-’am kumuuliza fatwa.  Al-Fadhl akaanza kumwangalia mwanamke huyo, na mwanamke naye akawa anamwangalia.  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaugeuza uso wa Fadhl akauelekeza upande mwingine”.  [Al-Bukhaariy (6228) na Muslim (1218)]

 

Kitendo hiki cha Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kinamaanisha kuzuia na kukataza kufanya hivyo kwa mwanaume.

 

3-  Jariyr bin ‘Abdullaah amesema:

 

"سَأَلَتْ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ نَظَرِ الْفُجَاءَةِ ، فَأَمَرَنِي أَنْ أَصْرِفَ بَصَرِي"

 

“Nilimuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu kuangalia kwa ghafla.  Akaniamuru nigeuze jicho langu sehemu nyingine”.   [Muslim (2109), Abu Daawuwd (2148) na At-Tirmidhiy (2776)]

 

4-   Ibn Buraydah toka kwa baba yake amesema:  “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia ‘Aliyy:

 

"يَا عَلِيُّ لاَ تُتْبِعِ النَّظْرَةَ النَّظْرَةَ فَإِنَّ لَكَ الأُولَى وَلَيْسَتْ لَكَ الآخِرَةُ ‏"‏

 

“Ee ‘Aliyy!  Ukiangalia mara moja, usiongeze tena na tena, kwa la kwanza hulaumiwi, lakini jingine hapana”.  [At-Tirmidhiy (2777), Abu Daawuwd (2149), na Ahmad (1377).  Sanad yake ni Hasanun Lighayrih]

 

 

Share [4]

02-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia: Hukumu Za Kuangalia: Mwanaume Anaruhusiwa Kumwangalia Mwanamke Kwa Ajili Ya Maslaha Mazito

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ  وَأَحْكَامُ النَّظَرِ

 

 Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia 

  

أَحْكَامُ النَّظَرِ

Hukumu Za Kuangalia 

  

Alhidaaya.com [3] 

 

 

02-Mwanaume Anaruhusiwa Kumwangalia Mwanamke Kwa Ajili Ya Maslaha Mazito:

 

Tumeshajua kwamba mwanaume kumwangalia mwanamke -na kinyume chake- ni haramu, kwa kuwa kuangalia ni njia na sababu ya kupelekea kufanyika machafu.  Lakini kuangalia huku kunaruhusiwa endapo kama kuna maslaha mazito.  Na hii ni kutokana na Hadiyth ya ‘Aliyy kuhusiana na kisa cha yeye pamoja na Az-Zubayr na Abu Marthad kutumwa na Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwenda kumwahi mwanamke wa kipagani ambaye alikuwa na barua ya Haatib bin Balta’ah akiipeleka kwa wapagani wa Makkah.  Sehemu ya Hadiyth inasema:

 

"لَقَدْ عَلِمْتُ مَا كَذَبَ رَسُوْلُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ، وَالَّذِي يُحْلَفُ بِهِ لَتُخْرِجِنَّ الْكِتَابَ أَوْ لَأُجَرِّدَنَّكِ ، فَأَهْوَتْ بِيَدِهَا إِلَى حُجْزَتِهَا فَأَخْرَجَتِ الْكِتَابَ "

 

“Kwa hakika ninajua kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakusema uongo.  Basi naapa kwa Yule Ambaye Huapiwa kwa Jina Lake, ima utaitoa barua, au nitakuvua nguo zote.  Akapeleka mkono kwenye fundo la nguo yake, akaitoa barua”.  [Al-Bukhaariy (3081) na Muslim (2494)]

 

Al-Haafidh amesema kwenye Al-Fat-h (11/47):  “Hadiyth inatufunza kwamba inajuzu kuangalia uchi wa mwanamke kwa dharura isiyo na budi”.

 

 

 

Share [5]

03-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia: Hukumu Za Kuangalia: Hali Ambazo Mwanaume Anaruhusiwa Kumwangalia Mwanamke

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ  وَأَحْكَامُ النَّظَرِ

 

 Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia 

  

أَحْكَامُ النَّظَرِ

Hukumu Za Kuangalia 

  

Alhidaaya.com [3] 

 

 

03-Hali Ambazo Mwanaume Anaruhusiwa Kumwangalia Mwanamke:

 

1-  Kuposa:  ‘Ulamaa wamekubaliana wote kwamba ni halali kwa mwanaume kumwangalia mwanamke ambaye anataka kumwoa.  Na hikma ya hilo, ni kumfanya mume mtarajiwa awe na picha kamili ya mkewe mtarajiwa, asije kujuta kama atavamia tu akaoa, kisha akakuta mambo si kama alivyotarajia.  Na kama posa yake itakubaliwa, basi ataoa kwa hamu, shauku na mapenzi.  Mwanaume mwenye busara, haingii kichwa kichwa sehemu yoyote mpaka imbainikie kheri yake na shari yake kabla ya kuingia.

 

2-  Kutibu:  Kimsingi, mwanamke hatibiwi ila na mwanamke mwenzake.  Lakini pamoja na hivyo, hakuna makhitilafiano baina ya ‘Ulamaa juu ya kujuzu mwanaume kumtibu mwanamke na kuangalia sehemu yenye ugonjwa kama italazimika lakini kwa vidhibiti maalum.

 

Sambamba na hilo, mwanamke asiye maharimu anaruhusiwa kumtibu mwanamume katika hali ya dharura. 

 

Ar-Rubayyi’u bin Mu’awwidh amesema: 

 

"كُنَّا نَغْزُو مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ نَسْقِي الْقَوْمَ، وَنَخْدُمُهُمْ، وَنَرُدُّ الْقَتْلَى وَالْجَرْحَى إِلَى الْمَدِينَةِ"

 

“Tulikuwa tunakwenda vitani pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kazi yetu ilikuwa kuwapatia maji wanaume, kuwahudumia, na kuwarejesha Madiynah waliouawa na majeruhi”.  [Swahiyh Al-Bukhaariy (2883)]

 

Lakini pamoja na ruksa hiyo, haifai kutanua na kuachilia katika jambo hili kama tunavyoshuhudia hivi leo.  ‘Ulamaa wametaja vidhibiti vya kuruhusiwa daktari mwanaume kumtibu mwanamke.  Vidhibiti hivyo ni:

 

1-  Kama yuko daktari mwanamke, ni sharti yeye atangulizwe kabla ya daktari wa kiume na hususan ikiwa upimaji na ukaguzi unahusiana na sehemu nyeti za uchi mzito.  Ikiwa hakupatikana daktari mwanamke au ikawa haiwezekani kumwendea, basi hapo itakuwa ni dharura mwanamume kutibu.

 

2-  Daktari awe mwaminifu, asiwe na tuhuma yoyote ya uchafu katika tabia yake wala dini yake.

 

3-  Daktari asivuke mpaka wa kutosheleza dharura katika kuangalia, kupima kugusa na kadhalika.  Ni lazima daktari huyu afunike sehemu zote za mwili wa mgonjwa zisizohitajika kuangaliwa.  Inatosha tu kuangalia sehemu husika ya kutibiwa.

 

4-  Kutibiwa kuwe kunahitajika sana kama kuwa mgonjwa hasa, au awe anakabiliwa na maumivu yasiyovumilika, au awe anahofiwa kudhoofu na kudorora afya.  Ama ikiwa si ugonjwa au hali ya dharura inayohitajia kufanyiwa dawa, basi haijuzu kabisa.  Ni kama mwanamke kwenda kwa daktari wa kiume ili kuboresha afya yake, au kupunguza uzito, au kutengeneza na kurembesha mwili wake.  Haya hayako ndani ya wigo wa haja.

 

 

Share [6]

04-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia: Hukumu Za Kuangalia: Mwanamke Anaweza Kuangaliwa na Hakimu Na Shahidi Na Katika Miamala

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ  وَأَحْكَامُ النَّظَرِ

 

 Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia 

  

أَحْكَامُ النَّظَرِ

Hukumu Za Kuangalia 

  

Alhidaaya.com [3] 

 

                                                                       

04-Mwanamke Anaweza Kuangaliwa na Hakimu Na Shahidi Na Katika Miamala:

 

Hakimu na shahidi kumwangalia mwanamke ni katika hali zinazovuliwa kwa dharura.  Na hii ni pale anapoitwa mwanaume kumtolea mwanamke ushahidi wa kumtoa kwenye tuhuma au kumthibitishia.   Au hakimu akiwa mwanaume itabidi amtazame ili atoe hukumu ya adhabu likithibiti kosa kama atakiri au kumwachia,  au kwa mashuhuda kutoa ushahidi wa kwamba wanamjua na kadhalika.  Hii ni kwa vile katika kesi ni lazima mwanamke atazamwe ili hukumu iwe ya haki.  Mambo ya dharura huhalalisha yaliyo marufuku. 

 

Na ikiwa shahidi atamtambua akiwa na niqab, basi si lazima afunue, kwa kuwa dharura hukadiriwa kwa kiasi chake.

 

Kumwangalia Kwa Ajili Ya Muamala Kama Kuuza Au Kununua:

 

Fuqahaa wanasema kwamba inajuzu mwanaume kumwangalia mwanamke kwa ajili ya muamala kama biashara na kadhalika.  Mwanaume akifanya biashara na mwanamke kwa kununua kutoka kwake au kumuuzia, ni lazima amwangalie na amjue vizuri -lakini kwa kadiri ya haja- ili kudhamini haki yake ya malipo au thamani ya bidhaa au haki nyingine yoyote inayohusiana na biashara kati yao.  

 

An-Nawawiy amesema:  “Inajuzu kwa mwanaume kuangalia uso wa mwanamke ajnabiya wakati wa kutoa ushahidi, na wakati wa kuuza au kununua kutoka kwake.  Na yeye anaruhusiwa vile vile kuangalia uso wa mwanaume”.  [Al-Majmuw’u (16/139)].

 

 

Share [7]

05-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia: Hukumu Za Kuangalia: Mwanaume Kubisha Hodi Ili Kuingia Kwa Maharimu Zake

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ  وَأَحْكَامُ النَّظَرِ

 

 Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia 

  

أَحْكَامُ النَّظَرِ

Hukumu Za Kuangalia 

  

Alhidaaya.com [3] 

 

 

05-Mwanaume Kubisha Hodi Ili Kuingia Kwa Maharimu Zake:

 

Nyuma pamekwisha ainishwa uchi wa mwanamke mbele ya maharimu zake, na kwamba mwanamke haamuriwi kujifunika mbele ya maharimu hawa.  Lakini pamoja na hivyo, haitakikani mwanamume aingie kwa maharimu zake bila kuwabishia, kwani anaweza kuingia bila hodi akawakuta katika hali isiyofurahisha, kama kuwa uchi na mfano wa hivyo.

 

‘Alqamah amesema:  “Mtu mmoja alikwenda kwa ‘Abdullaah bin Mas-‘uwd akamwambia: 

 

"أأَسْتَأْذِنُ عَلَى أُمِّيْ؟ قَالَ: مَا عَلَى كُلِّ أَحْيَانِهَا تُحِبُّ أَنْ تَرَاهَا"

 

“Je, nipige hodi kuingia kwa mama yangu?  Akamwambia:  Si katika nyakati zake zote anapenda umwone”.  [Al-Bukhaariy katika Al-Adab Al-Mufrad (1059) kwa Sanad Swahiyh]

 

‘Atwaa amesema:  “Nilimuuliza Ibn ‘Abbaas:  

 

"أَسْتَأْذِنُ عَلَى أُخْتَىّْ؟  فَفَالَ: نَعَمْ فَقُلْتُ: أُخْتَانِ في حِجْرِيْ وأَنا أُمَوِّنُهُمَا وأُنْفِقُ عَلَيْهِمَا، أَسْتَأْذِنُ عَلَيْهِمَا؟ قَالَ: نَعَمْ، أَتُحِبُّ أَنْ تَرَاهُمَا عرْيَانَتَيْنِ؟!"

 

“Je, nipige hodi kuingia kwa dada zangu?  Akasema:  Na’am.  Nikamwambia:  Hao ni dada zangu wawili ninawalea, na mimi ndiye ninawakimu kimaisha na kuwapa masurufu, vipi niwabishie?!  Akasema:  Na’am.  Je, utapenda kuwaona wakiwa uchi?!  Kisha akasoma:

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لِيَسْتَأْذِنكُمُ الَّذِينَ مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ وَالَّذِينَ لَمْ يَبْلُغُوا الْحُلُمَ مِنكُمْ ثَلَاثَ مَرَّاتٍ ۚ مِّن قَبْلِ صَلَاةِ الْفَجْرِ وَحِينَ تَضَعُونَ ثِيَابَكُم مِّنَ الظَّهِيرَةِ وَمِن بَعْدِ صَلَاةِ الْعِشَاءِ ۚ ثَلَاثُ عَوْرَاتٍ لَّكُمْ ۚ

 

“Enyi walioamini!  Wakuombeni idhini wale iliyowamiliki mikono yenu ya kuume, na wale wasiofikia umri wa kubaleghe miongoni mwenu mara tatu: kabla ya Swalaah ya alfajiri na wakati mnapovua nguo zenu adhuhuri (kulala) na baada ya Swalaah ya ‘Ishaa.  Nyakati tatu za faragha kwenu”.  [Al-Bukhaariy katika Al-Adab Al-Mufrad (1063) kwa Sanad Swahiyh]

 

 

 

Share [8]

06-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia: Hukumu Za Kuangalia: Ni Haramu Kwa Mwanaume Kukaa Pweke na Mwanamke Asiye Maharimu Yake (Ajnabiyyah)

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ  وَأَحْكَامُ النَّظَرِ

 

 Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia 

  

أَحْكَامُ النَّظَرِ

Hukumu Za Kuangalia 

  

Alhidaaya.com [3] 

 

 

06-Ni Haramu Kwa Mwanaume Kukaa Pweke na Mwanamke Asiye Maharimu Yake (Ajnabiyyah):

 

 

Ibn ‘Abbaas:  “Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: 

 

"لاَ يَخْلُوَنَّ رَجُلٌ بِامْرَأَةٍ إِلاَّ وَمَعَهَا ذُو مَحْرَمٍ ‏"‏

 

“Mwanaume kamwe asibaki pweke na mwanamke ila akiwa pamoja naye mahram yake”. ‏ [Al-Bukhaariy 3006) na Muslim (1341]

 

Na Rasuli anasema tena:

 

"لَا يَخْلُوَنَّ رَجُلٌ بِامْرَأَةٍ، فَإِنَّ الشَّيْطَانَ ثَالثُهُمَا"

 

“Kamwe asibaki mwanaume pweke na mwanamke, kwani shaytwan atakuwa ni wa tatu wao”.  [Ahmad katika Al-Musnad (1/18) kwa Sanad Swahiyh]

 

Na ikiwa wanaume wawili au watatu ambao wanaaminika na uwezekano wa wao kula njama ya kufanya machafu uko mbali, basi wanaruhusiwa kuingia kwa mwanamke mmoja.  Na hii ni kwa Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Amri:

 

 "أَنَّ نَفَرًا مِنْ بَنِي هَاشِمٍ دَخَلُوا عَلَى أَسْمَاءَ بِنْتِ عُمَيْسٍ فَدَخَلَ أَبُو بَكْرٍ الصِّدِّيقُ وَهِيَ تَحْتَهُ يَوْمَئِذٍ  فَكَرِهَ ذَلِكَ ، فَذَكَرَ ذَلِكَ لِرَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَقَالَ: لَمْ أَرَ إِلاَّ خَيْرًا ‏.‏ فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ‏"‏إِنَّ اللَّهَ قَدْ بَرَّأَهَا مِنْ ذَلِكَ"‏ ‏.‏ ثُمَّ قَامَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَلَى الْمِنْبَرِ فَقَالَ: ‏"‏لاَ يَدْخُلَنَّ رَجُلٌ بَعْدَ يَوْمِي هَذَا عَلَى مُغِيبَةٍ إِلاَّ وَمَعَهُ رَجُلٌ أَوِ اثْنَانِ" 

 

“Watu kadhaa wa ukoo wa Bani Hashim waliingia kwa Asmaa bint ‘Umays.  Abu Bakr As-Swiddiyq akaingia -na Asmaa ashakuwa mkewe wakati huo- na jambo hilo halikumfurahisha.  Akaenda kumweleza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) lakini alimwambia:  Sikuona ila kheri (simtuhumu ubaya wala siwatuhumu).  Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia:  Hakika Allaah Amemtakasa na hilo.  Kisha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasimama juu ya mimbari akasema:  Asiingie mwanaume yeyote baada ya siku hii kwa mwanamke ambaye mumewe hayuko ila awe pamoja naye mwanaume mwingine au wawili”.  [Swahiyh Muslim (2173)]

 

Vile vile, mwanaume anaruhusiwa kumzuru mwanamke mgonjwa kama ipo dhamana ya kutokuweko fitnah.   Na hii ni kwa Hadiyth ya Jaabir bin ‘Abdillaah aliyesema:

 

"أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ دَخَلَ عَلَى أُمِّ السَّائِبِ فَقَالَ: ‏"‏مَا لَكِ يَا أُمَّ السَّائِبِ، تُزَفْزِفِينَ"‏‏.‏ قَالَتِ: الْحُمَّى لاَ بَارَكَ اللَّهُ فِيهَا.‏ فَقَالَ: ‏"‏لاَ تَسُبِّي الْحُمَّى فَإِنَّهَا تُذْهِبُ خَطَايَا بَنِي آدَمَ كَمَا يُذْهِبُ الْكِيرُ خَبَثَ الْحَدِيدِ "‏

 

“Kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliingia kwa Ummu As-Saaib na kumwambia:  Una nini Ummu As-Saaib?  Naona unatetema.  Akasema:  Ni homa, Allaah Asiibariki.  Rasuli akamwambia:  Usiitukane homa, kwani homa inaondosha madhambi ya mwanadamu kama moto wa mfua chuma unavyosafisha uchafu wa chuma”.   

 

 

Share [9]

07-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia: Hukumu Za Kuangalia: Mwanamke Kuwaangalia Wanaume Wasio Maharimu Wake

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ  وَأَحْكَامُ النَّظَرِ

 

 Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia 

  

أَحْكَامُ النَّظَرِ

Hukumu Za Kuangalia 

  

Alhidaaya.com [3] 

 

 

07-Mwanamke Kuwaangalia Wanaume Wasio Maharimu Wake:

 

Kwa mujibu wa itifaki ya ‘Ulamaa, ni haramu kwa mwanamke kuangalia uso wa mwanaume asiye maharimu kwa matamanio.  Na ikiwa bila matamanio na hakuna hofu ya fitnah, basi itajuzu.  Sehemu zinazoruhusiwa kuangaliwa kwa kauli yenye nguvu ni zile zisizo kati ya kitovu na magoti ikiwa hakuna hofu ya fitnah.  Hili linatiliwa nguvu na:

 

-   Hadiyth ya ‘Aaishah: 

 

"رَأَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَوْمًا عَلَى بَاب حُجْرَتِي، وَالْحَبَشَةُ يَلْعَبُونَ فِي الْمَسْجِدِ وَرَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَسْتُرُنِي بِرِدَائِهِ، أَنْظُرُ إِلَى لَعِبِهِمْ"‏

 

“Nilimwona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) siku hiyo kwenye mlango wa chumba changu huku Wahabeshi wakicheza ndani ya Msikiti  (kwa mikuki), Rasuli wa Allaah akanifunika kwa ridaa yake ili niweze kuwaangalia wanavyocheza”.  [Al-Bukhaariy (455) na Muslim (892)].

 

Hadiyth iko wazi kwamba mwanamke anaruhusiwa kumwangalia mwanaume.

 

-  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipomwambia Faatwimah binti Qays:

 

" فَاذْهَبِي إِلَى ابْنِ أُمِّ مَكْتُومٍ فَكُونِي عِنْدَهُ فَإِنَّهُ رَجُلٌ أَعْمَى تَضَعِينَ ثِيَابَكِ عِنْدَهُ"

 

“Basi nenda kwa Ibn Ummi Maktuwm uishi kwake, yeye ni kipofu, utaweza kuvua nguo zako huko (naye hawezi kukuona)”.   [Swahiyh Muslim (1480)]

 

Hii ni dalili kwamba mwanamke anaruhusiwa kumwangalia mwanaume sehemu ambazo mwanaume haruhusiwi kumwangalia mwanamke.  Ama uchi, hilo haliruhusiwi.  [Al-Jaami’u Liahkaamil Qur-aan cha Al-Qurtwubiy (12/228)].

 

Kwa muktadha huu, dalili hizi mbili zinakuwa mahsusi kwa Kauli Yake Ta’aalaa:

 

"وَقُل لِّلْمُؤْمِنَاتِ يَغْضُضْنَ مِنْ أَبْصَارِهِنَّ"

 

“Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao”.  [An-Nuwr: 31].

 

Lakini hata hivyo, mwanamke kuruhusiwa kumwangalia mwanaume kunashurutishwa kuwe bila matamanio, kusalimike na fitnah na iweko haja.  Na hili halimaanishi kwamba anaruhusiwa kuchanganyika na wanaume ajaanib (wasio maharimu), kuangaliana nao uso kwa uso na kuzungumza nao bila uwepo wa haja.  Allaah Ndiye Ajuaye zaidi.

 

 

Share [10]

08-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia: Hukumu Za Kuangalia: Mwanamke Anaruhusiwa Kumtembelea Mwanaume Mgonjwa Kwa Sharti Ajisitiri Na Pasiwepo Fitnah

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ  وَأَحْكَامُ النَّظَرِ

 

 Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia 

 

 

أَحْكَامُ النَّظَرِ

Hukumu Za Kuangalia 

 

  

Alhidaaya.com [3] 

 

 

08-Mwanamke Anaruhusiwa Kumtembelea Mwanaume Mgonjwa Kwa Sharti Ajisitiri Na Pasiwepo Fitnah:

 

‘Aaishah:

 

"لَمَّا قَدِمَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الْمَدِينَةَ وُعِكَ أَبُو بَكْرٍ وَبِلاَلٌ ، فَدَخَلْتُ عَلَيْهِمَا فَقُلْتُ: يَا أَبَتِ كَيْفَ تَجِدُكَ؟ وَيَا بِلاَلُ كَيْفَ تَجِدُك؟َ"

 

“Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuja Madiynah, Abu Bakr na Bilaal walipigwa na homa.  Nikaingia waliko nikasema:  Ee baba yangu kipenzi! Vipi hali yako? Wajisikiaje? Na ee Bilaal! Vipi hali yako? Wajisikiaje?....”[Al-Bukhaariy (3926) na Muslim (1376), na tamshi ni la Al-Bukhaariy].

 

Vile vile, mwanamke anaruhusiwa kumtibu mwanaume kama kuna dharura.  Ni kwa Hadiyth iliyotangulia ya Ar-Rubayyi’u bin Mu’awwidh aliyesema: 

 

"كُنَّا نَغْزُو مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ نَسْقِي الْقَوْمَ، وَنُدَاوِيْ الْجَرْحَى وَنَرُدُّ القَتْلَى إِلَى الْمَدِينَةِ"

 

“Tulikuwa tunakwenda vitani pamoja na Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na tulikuwa tunawapatia maji wanaume, tunawatibu majeruhi, na tunawarejesha waliouawa Madiynah”.  [Swahiyh Al-Bukhaariy (2883)]

 

Lakini sharti ya hili ni kutopatikana mwanaume anayeweza kutoa huduma hii ya matibabu.  Allaah Ndiye Ajuaye zaidi.

 

 

 

Share [11]

09-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia: Hukumu Za Kuangalia: Mwanamke Haruhusiwi Kupeana Mkono Na Mwanaume Ajinabi (Asiye Maharimu)

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ  وَأَحْكَامُ النَّظَرِ

 

 Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia 

 

  

أَحْكَامُ النَّظَرِ

Hukumu Za Kuangalia 

  

Alhidaaya.com [3] 

 

 

 

09-Mwanamke Haruhusiwi Kupeana Mkono Na Mwanaume Ajinabi (Asiye Maharimu):

 

Ni kwa Hadiyth ya Mu’aql bin Yasaar:

 

"لأَنْ يُطْعَنَ فِي رَأْسِ أَحَدِكُمْ بِمِخْيَطٍ مِنْ حَدِيْدٍ خَيْرٌ لَهُ مِنْ أَنْ يَمَسَّ امْرَأَةً لا تَحِلُّ لَهُ"

 

“Kupondwa mmoja wenu kwa sindano la chuma, ni nafuu zaidi kuliko kumgusa mwanamke ambaye si halali kwake”.  [At-Twabaraaniy katika Al-Kabiyr (20/211) kwa Sanad Hasan.  Angalia As-Silsilat As-Swahiyhah].

 

Kadhalika, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakuwa akiwapa mkono wanawake, na wala hakuchukua kwao ahadi ila kwa maneno tu.

 

‘Aaishah anasema: 

 

"أَنَّ رَسُولَ الله صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ يَقُولُ للمَرْأَةِ المُبَايِعَةِ: "قَدْ بَايَعْتُكِ كَلَامًا"

 

“Kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akimwambia mwanamke anayechukua kutoka kwake ahadi:  “Nimechukua ahadi toka kwako kwa maneno”. 

 

Pia anasema tena: 

 

وَاللَّهِ مَا مَسَّتْ يَدُهُ يَدَ امْرَأَةٍ قَطُّ فِي الْمُبَايَعَةِ، وَمَا بَايَعَهُنَّ إِلاَّ بِقَوْلِهِ‏:"قَدْ بَا يَعْتُكِ عَلى ذلِكَ"

 

“Wa-Allaah, mkono wake haujagusa kamwe mkono wa mwanamke katika kupeana nao ahadi.  Hakupeana nao ahadi ila kwa kuwaambia:  “Nimechukua ahadi kwako juu ya hilo”.   [Swahiyhul Bukhaariy (2713)].

 

Na katika riwaayah, Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwaambia:

 

"إِنِّيْ لَا أُصَافِحُ النِّسَاءَ ...."

 

 “Mimi sipeani mikono na wanawake”.  [Muwattwaa Maalik (1842), Ahmad (6/357), At-Tirmidhiy (1597), An-Nasaaiy (4181) na Ibn Maajah (2874)].

 

 

Share [12]

10-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia: Hukumu Za Kuangalia: Inaruhusiwa Mwanamke Kumsalimia Mwanaume Na Kinyume Chake Lakini Bila Kupeana Mikono

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ  وَأَحْكَامُ النَّظَرِ

 

 Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia 

  

 

أَحْكَامُ النَّظَرِ

Hukumu Za Kuangalia 

  

Alhidaaya.com [3] 

 

 

 

10-Inaruhusiwa Mwanamke Kumsalimia Mwanaume Na Kinyume Chake Lakini Bila Kupeana Mikono:

 

Ummu Haani:

 

"ذَهَبْتُ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَامَ الْفَتْحِ فَوَجَدْتُهُ يَغْتَسِلُ، وَفَاطِمَةُ ابْنَتُهُ تَسْتُرُهُ فَسَلَّمْتُ عَلَيْهِ" ‏

 

“Nilikwenda kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mwaka ule Makkah ilipokombolewa.  Nikamkuta anaoga na binti yake Faatwimah amemwekea pazia, nikamsalimia”.  [Al-Bukhaariy (3171) na Muslim (336)].

 

Hadiyth inatufunza kwamba mwanamke anaweza kumsalimia mwanaume bila kupeana mkono, lakini kama mazingira ya fitnah hayapo. 

 

Na pia mwanaume anaruhusiwa kumsalimia mwanamke bila kupeana mkono.  Asmaa bint Yaziyd amesema:

 

" أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مَرَّ فِي المَسْجِدِ يومًا، وعُصْبَةٌ منَ النِّسَاءِ قُعُوْدٌ، فَأَلْوَى بِيَدِهِ بالتسليم‏‏‏"

 

“Kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipita siku moja Msikitini na kundi la wanawake likiwa limekaa humo.  Akawasalimia na kuwaashiria kwa mkono wake”.  [At-Tirmidhiy (2697), Abu Daawuwd (5204), Ibn Maajah (3701)].

 

 

Share [13]

11-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia: Hukumu Za Kuangalia: Mwanamke Anaweza Kumsemesha Mwanaume Kama Fitnah Haipo Na Kwa Vidhibiti Vya Kisheria

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ  وَأَحْكَامُ النَّظَرِ

 

 Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia 

  

 

أَحْكَامُ النَّظَرِ

Hukumu Za Kuangalia 

  

Alhidaaya.com [3] 

 

 

11-Mwanamke Anaweza Kumsemesha Mwanaume Kama Fitnah Haipo Na Kwa Vidhibiti Vya Kisheria:

 

Kumsemesha huku kunatakikana kuwe kunatokana na dharura na haja pamoja na kuwajibika na vidhibiti vya kisharia.  Asilegeze maneno, akayalainisha, akayalaza.  Na hii ni kwa Kauli Yake Ta’aalaa:

 

“فَلَا تَخْضَعْنَ بِالْقَوْلِ فَيَطْمَعَ الَّذِي فِي قَلْبِهِ مَرَضٌ وَقُلْنَ قَوْلًا مَّعْرُوفًا”

 

“Basi msilegeze kauli asije akaingiwa tamaa ambaye moyoni mwake mna maradhi, na semeni kauli inayokubalika”.  [Al-Ahzaab: 32].

 

Na jingine linalodulisha kuruhusika hilo ni Neno Lake Ta’aalaa:

 

"وَإِذَا سَأَلْتُمُوهُنَّ مَتَاعًا فَاسْأَلُوهُنَّ مِن وَرَاءِ حِجَابٍ"

 

“Na mnapowauliza wake zake haja, waulizeni nyuma ya pazia”.  [Al-Ahzaab: 53].

 

Na Neno Lake Ta’aalaa kuhusu Nabiy Muwsaa ‘alayhis Salaam kuwasemesha wanawake wawili wa Madyana:

 

"وَوَجَدَ مِن دُونِهِمُ امْرَأَتَيْنِ تَذُودَانِ ۖ قَالَ مَا خَطْبُكُمَا ۖ قَالَتَا لَا نَسْقِي حَتَّىٰ يُصْدِرَ الرِّعَاءُ ۖ وَأَبُونَا شَيْخٌ كَبِيرٌ  • فَسَقَىٰ لَهُمَا ثُمَّ تَوَلَّىٰ إِلَى الظِّلِّ فَقَالَ رَبِّ إِنِّي لِمَا أَنزَلْتَ إِلَيَّ مِنْ خَيْرٍ فَقِيرٌ • فَجَاءَتْهُ إِحْدَاهُمَا تَمْشِي عَلَى اسْتِحْيَاءٍ قَالَتْ إِنَّ أَبِي يَدْعُوكَ لِيَجْزِيَكَ أَجْرَ مَا سَقَيْتَ لَنَا"

 

“Na akakuta kando yake wanawake wawili wanawazuia (wanyama wao). Akasema:  Mna nini?  Wakasema:  Hatunyweshi mpaka waondoke wachungaji, na baba yetu ni mtu mzima sana  •  Basi akawanyweshea, kisha akageuka kwenda kivulini, akasema:  Rabb wangu!  Hakika mimi ni mhitajia wa kheri yoyote Utakayoniteremshia  •  Basi akamjia mmoja kati ya wanawake wawili akitembea kwa kuona hayaa, akasema:  Baba yangu anakwita ili akulipe ujira wa kutunyweshea”.  [Al-Qaswas: 23-25]

 

Maudhui hii ina Hadiyth nyingi tu.  Kati yake ni ya Anas:

 

"لَمَّا ثَقُلَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ جَعَلَ يَتَغَشَّاهُ الكَرْبُ، فَقَالَتْ فَاطِمَةُ عَلَيْهَا السَّلاَمُ: وَاكَرْبَ أَبَاهُ‏.‏ فَقَالَ لَهَا: "‏لَيْسَ عَلَى أَبِيكِ كَرْبٌ بَعْدَ الْيَوْمِ ‏"‏‏.‏‏ فَلَمَّا دُفِنَ قَالَتْ فَاطِمَةُ عَلَيْهَا السَّلاَمُ : يَا أَنَسُ، أَطَابَتْ أَنْفُسُكُمْ أَنْ تَحْثُوا عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ التُّرَابَ"

 

“Maradhi yalipomzidia Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam), ghamu kubwa ilianza kumtamalaki.  Faatwimah (‘alayhas Salaam) akasema:   Dhiki na tabu iliyoje kwa baba yangu!  Akamwambia:  Ghamu na dhiki hatoipata tena baba yako baada ya leo.  Alipozikwa, Faatwimah (‘alayhas Salaam) alimwambia Anas:  Ee Anas!  Je mlijisikia vizuri kummiminia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mchanga!”.  [Swahiyhul Bukhaariy (4462)].

 

 

 

Share [14]

12-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia: Hukumu Za Kuangalia: Kuzungumza Na Mwanaume Kwa Simu Kwa Haja

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ  وَأَحْكَامُ النَّظَرِ

 

 Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia 

  

 

أَحْكَامُ النَّظَرِ

Hukumu Za Kuangalia 

  

Alhidaaya.com [3] 

 

12-Kuzungumza Na Mwanaume Kwa Simu Kwa Haja:

 

Mwanamke anaruhusiwa kuzungumza na mwanaume ajinabi kwa simu ya kawaida, mobile na kadhalika kutokana na haja, lakini hilo ni lazima lifungamanishwe na vidhibiti vya kisharia.  Ama ikiwa simu hiyo itaibua kati yao mazingira yanayofanana na hali ya wao kuwa wawili peke yao ambayo inaweza kuwapeleka kwenye mazungumzo yatakayowakokota kwenye uchafu wa zinaa, basi kuacha hilo ni lazima.  Na hii ni kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam: 

 

"لَا يَخْلُوَنَّ رَجُلٌ بِامْرَأَةٍ، فَإِنَّ الشَّيْطَانَ ثَالثُهُمَا"

 

“Kamwe asibaki mwanaume pweke na mwanamke, kwani shaytwan atakuwa ni wa tatu wao”.  [Ahmad katika Al-Musnad (1/18) kwa Sanad Swahiyh]

 

 

 

Share [15]
www.alhidaaya.com

Source URL: https://www.alhidaaya.com/sw/node/11624

Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/284
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11624&title=09C-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20%D9%83%D9%90%D8%AA%D8%A7%D8%A8%D9%8F%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%91%D9%90%D8%A8%D8%A7%D8%B3%D9%90%20%D9%88%D9%8E%D8%A7%D9%84%D8%B2%D9%91%D9%90%D9%8A%D9%86%D9%8E%D8%A9%D9%90%20%D9%88%D9%8E%D8%A3%D9%8E%D8%AD%D9%92%D9%83%D8%A7%D9%85%D9%90%20%D8%A7%D9%84%D9%86%D9%91%D9%8E%D8%B8%D9%8E%D8%B1%20-%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20%20%D8%A3%D9%8E%D8%AD%D9%92%D9%83%D9%8E%D8%A7%D9%85%D9%8F%20%D8%A7%D9%84%D9%86%D9%91%D9%8E%D8%B8%D9%8E%D8%B1%D9%90%20Hukmu%20Za%20Kuangalia
[3] http://www.alhidaaya.com/
[4] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11625&title=01-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Hukumu%20Za%20Kuangalia%3A%20Mwanaume%20Asiye%20Maharimu%20Kumwangalia%20Mwanamke
[5] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11626&title=02-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Hukumu%20Za%20Kuangalia%3A%20Mwanaume%20Anaruhusiwa%20Kumwangalia%20Mwanamke%20Kwa%20Ajili%20Ya%20Maslaha%20Mazito
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11627&title=03-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Hukumu%20Za%20Kuangalia%3A%20Hali%20Ambazo%20Mwanaume%20Anaruhusiwa%20Kumwangalia%20Mwanamke%20%20
[7] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11628&title=04-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Hukumu%20Za%20Kuangalia%3A%20Mwanamke%20Anaweza%20Kuangaliwa%20na%20Hakimu%20Na%20Shahidi%20Na%20Katika%20Miamala%20
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11629&title=05-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Hukumu%20Za%20Kuangalia%3A%20Mwanaume%20Kubisha%20Hodi%20Ili%20Kuingia%20Kwa%20Maharimu%20Zake%20
[9] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11630&title=06-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Hukumu%20Za%20Kuangalia%3A%20Ni%20Haramu%20Kwa%20Mwanaume%20Kukaa%20Pweke%20na%20Mwanamke%20Asiye%20Maharimu%20Yake%20%28Ajnabiyyah%29%20
[10] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11631&title=07-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Hukumu%20Za%20Kuangalia%3A%20Mwanamke%20Kuwaangalia%20Wanaume%20Wasio%20Maharimu%20Wake
[11] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11632&title=08-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Hukumu%20Za%20Kuangalia%3A%20Mwanamke%20Anaruhusiwa%20Kumtembelea%20Mwanaume%20Mgonjwa%20Kwa%20Sharti%20Ajisitiri%20Na%20Pasiwepo%20Fitnah%20
[12] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11633&title=09-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Hukumu%20Za%20Kuangalia%3A%20Mwanamke%20Haruhusiwi%20Kupeana%20Mkono%20Na%20Mwanaume%20Ajinabi%20%28Asiye%20Maharimu%29%20
[13] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11634&title=10-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Hukumu%20Za%20Kuangalia%3A%20Inaruhusiwa%20Mwanamke%20Kumsalimia%20Mwanaume%20Na%20Kinyume%20Chake%20Lakini%20Bila%20Kupeana%20Mikono%20
[14] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11635&title=11-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Hukumu%20Za%20Kuangalia%3A%20Mwanamke%20Anaweza%20Kumsemesha%20Mwanaume%20Kama%20Fitnah%20Haipo%20Na%20Kwa%20Vidhibiti%20Vya%20Kisheria%20
[15] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11636&title=12-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%20Na%20Hukmu%20Za%20Kuangalia%3A%20Hukumu%20Za%20Kuangalia%3A%20Kuzungumza%20Na%20Mwanaume%20Kwa%20Simu%20Kwa%20Haja%20