Alhidaaya.com
Published on Alhidaaya.com (https://www.alhidaaya.com/sw)

Ukurasa Wa Kwanza > 09D-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: كِتابُ اللِّباسِ وَالزِّينَةِ - Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo الزِّيْنَةُ للمَرْأَةِ المُسْلِمَةِ: Pambo Kwa Mwanamke Wa Kiislamu > 06-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo: Pambo Kwa Mwanamke Wa Kiislamu: Pambo La Meno

06-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo: Pambo Kwa Mwanamke Wa Kiislamu: Pambo La Meno

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ 

Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo

 

 

الزِّيْنَةُ للمَرْأَةِ المُسْلِمَةِ

Pambo Kwa Mwanamke Wa Kiislamu

 

Alhidaaya.com [1]

 

 

 

06-Pambo La Meno:

 

Uislamu umehimiza kuyatunza meno, na kwa ajili hiyo, umesunisha kutumia mswaki.

 

Abu Hurayrah:  Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

"لَوْلاَ أَنْ أَشُقَّ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ لأَمَرْتُهُمْ بِتَأْخِيرِ الْعِشَاءِ وَبِالسِّوَاكِ عِنْدَ كُلِّ صَلاَةٍ"

‏

“Lau si kuhofia kuwafanyia uzito Waumini, ningeliwaamuru waicheleweshe ‘Ishaa na wapige mswaki wakati wa kila Swalaah”.  [Al-Bukhaariy (887) na Muslim (252) na tamshi ni lake]

 

Ni Haramu Kupasua Mwanya Katika Meno

 

Hii inafanyika kuonyesha kwamba mtu ana umri mdogo au kwamba meno yake ni mazuri.  Kufanya hivi bila kuwa kunahitajika kwa tiba ni haramu, kwa kuwa ni ubadilishaji wa uumbaji wa Allaah na kudanganya. 

 

Rasuli (Swalla Allaah ‘Alayhi wa aalihi wa sallam):

 

"لَعَنَ الْمُتَفَلِّجَاتِ لِلْحُسْنِ، الْمُغَيِّرَاتِ لخَلْقِ اللَّهِ"

 

“Amewalaani wanawake wenye kupasua mwanya wa meno ili waonekane wazuri, hao wanabadilisha uumbaji wa Allaah”.  [Al-Bukhaariy (4886) na Muslim (2125)]

 

Akifanya hivi kwa ajili ya matibabu, basi itaruhusiwa.  Inaruhusiwa vile vile kuyakaza meno kwa dhahabu kama yatahofiwa kutoka, na pia kupandikiza meno na magego.  Haya yote yanaruhusiwa kutokana na dharura.  [Al-Mughniy (3/15,16)]

 

 

 

Share [2]
www.alhidaaya.com

Source URL: https://www.alhidaaya.com/sw/node/11646

Links
[1] http://www.alhidaaya.com/
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11646&title=06-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%3A%20Pambo%20Kwa%20Mwanamke%20Wa%20Kiislamu%3A%20Pambo%20La%20Meno%20