Alhidaaya.com
Published on Alhidaaya.com (https://www.alhidaaya.com/sw)

Ukurasa Wa Kwanza > 09D-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: كِتابُ اللِّباسِ وَالزِّينَةِ - Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo الزِّيْنَةُ للمَرْأَةِ المُسْلِمَةِ: Pambo Kwa Mwanamke Wa Kiislamu > 11-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo: Pambo Kwa Mwanamke Wa Kiislamu: Hairuhusiwi Kutumia Mafuta Mazuri, Si Kwa Mume Wala Kwa Mwengine Yeyote Katika Hali Tatu

11-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo: Pambo Kwa Mwanamke Wa Kiislamu: Hairuhusiwi Kutumia Mafuta Mazuri, Si Kwa Mume Wala Kwa Mwengine Yeyote Katika Hali Tatu

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ 

Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo

 

 

الزِّيْنَةُ للمَرْأَةِ المُسْلِمَةِ

Pambo Kwa Mwanamke Wa Kiislamu

 

 

Alhidaaya.com [1]

 

 

 

11-Hairuhusiwi Kutumia Mafuta Mazuri, Si Kwa Mume Wala Kwa Mwengine Yeyote Katika Hali Tatu:

 

Ya kwanza:  Baada ya kuhirimia Hajji au ‘Umrah:

 

Ni kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusiana na aliyehirimia Hajji au ‘Umrah:

 

"وَلاَ تَلْبَسُوا مِنَ الثِّيَابِ شَيْئًا مَسَّهُ الزَّعْفَرَانُ وَلاَ الْوَرْسُ"

 

 “Wala msivae nguo yoyote iliyoingiwa na zafarani wala wars”….  [Al-Bukhaariy.  Takhriyj yake iko kwenye mlango wa Hijja]

 

Hikma ya kuzuiwa mwanamke aliyehirimia, ni kuwa harufu ya mafuta haya ni katika vichangamshi na vichochezi vya jimai ambayo inaharibu ihraam.

 

Ya pili:  Katika eda

 

Mwanamke anakatazwa kutumia mafuta mazuri wakati wa eda ya kufiwa na mumewe.

 

Ya tatu:  Anapotoka nyumbani

 

Na hii ni hata kama atamkusudia mumewe kama tulivyotangulia kugusia hili nyuma kidogo.

 

 

Share [2]
www.alhidaaya.com

Source URL: https://www.alhidaaya.com/sw/node/11651

Links
[1] http://www.alhidaaya.com/
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11651&title=11-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Mavazi%20Na%20Mapambo%3A%20Pambo%20Kwa%20Mwanamke%20Wa%20Kiislamu%3A%20Hairuhusiwi%20Kutumia%20Mafuta%20Mazuri%2C%20Si%20Kwa%20Mume%20Wala%20Kwa%20Mwengine%20Yeyote%20Katika%20Hali%20Tatu