Malaika
Imeandaliwa Na 'Abdullaah Mu'aawiyah (Abu Baasim)
Alhidaaya.com
Malaika
Alhidaaya.com [3]
01: Malaika Ni Nani?
Malaika ni viumbe kati ya Viumbe vya Allaah Ta’aalaa. Allaah Amewaumba kutokana na nuru. Ni viumbe waliopewa hishma kubwa, hawamwasi Allaah kwa Anayowaamuru kuyafanya, wanatekeleza yote wanayoamuriwa, na hawana jinsia ya kiume wala ya kike. Hawali, hawanywi, hawaoani, hawachoki, hawahisi tabu, na hakuna ajuaye idadi yao isipokuwa Allaah Ta’aalaa.
Allaah Ta’aalaa Amewawekea kizuizi tusiweze kuwaona, lakini Anaweza kuwafichulia baadhi ya Waja Wake wakaweza kuwaona, na Malaika hawa wana uwezo wa kujiweka katika maumbo tofauti, na wana nguvu kubwa na uwezo wa hali ya juu kabisa wa kugura kutoka sehemu moja hadi nyingine.
Sheikh Ibn ‘Uthaymiyn amesema: “Malaika ni ulimwengu uliofichika kwetu (ghayb), ni viumbe walioumbwa, na wanamwabudu Allaah Ta’aalaa Pekee. Hawana sifa zozote za kimola wala kiungu, na Allaah ‘Azza wa Jalla Amewaumba kutokana na nuru, na Amewapa sifa ya utiifu kamili wa Maamrisho Yake kwao na nguvu ya kuyatekeleza, nao ni wengi mno, na hakuna ajuaye idadi yao isipokuwa Allaah Ta’aalaa”.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
02: Hukmu Ya Kuamini Malaika
Kuamini Malaika ni waajib kwa Muislamu, kwani kuamini uwepo wao ni nguzo kati ya nguzo za Iymaan. Iymaan ya Muislamu haiswihi bila kuamini uwepo wa Malaika. Nguzo za Iymaan kama tujuavyo ni sita: Kumwamini Allaah, kuamini Malaika Wake, kuamini Vitabu Vyake, kuamini Mitume Wake, kuamini Siku ya mwisho, na kuamini Qadar; kheri yake na shari yake. Haya yote ni lazima Muislamu ayaamini ili iymaan yake iwe ni sahihi.
Allaah Amesema:
"آمَنَ الرَّسُولُ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْهِ مِن رَّبِّهِ وَالْمُؤْمِنُونَ ۚ كُلٌّ آمَنَ بِاللَّـهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّن رُّسُلِهِ ۚ وَقَالُوا سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا ۖ غُفْرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ"
“Rasuli ameamini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Rabb wake na Waumini (pia). Wote wamemwamini Allaah, na Malaika Wake, na Vitabu Vyake, na Rusuli Wake. (Nao husema): Hatutofautishi baina ya yeyote kati ya Rusuli Wake. Na wakasema: Tumesikia na tumetii, tunakuomba maghfirah Rabb wetu, na Kwako ndio mahali pa kuishia”. [Al-Baqarah: (285)].
Na yeyote atakayekanusha uwepo wa Malaika, au akawatangazia uadui, au akawatukana, au akawacheza shere, basi huyo amekufuru. Allaah Anasema:
"مَن كَانَ عَدُوًّا لِّلَّـهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَرُسُلِهِ وَجِبْرِيلَ وَمِيكَالَ فَإِنَّ اللَّـهَ عَدُوٌّ لِّلْكَافِرِينَ"
“Yeyote aliyekuwa adui wa Allaah na Malaika Wake, na Rusuli Wake, na Jibriyl, na Miykaala, basi hakika Allaah Ni adui kwa makafiri”. [Al-Baqarah: (98)].
Kadhalika, anakuwa amepotea upotevu wa mbali kabisa. Allaah Ta’aalaa Anasema:
"وَمَن يَكْفُرْ بِاللَّـهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا بَعِيدًا"
“Na atakayemkufuru Allaah na Malaika Wake, na Vitabu Vyake na Rusuli Wake na Siku ya Mwisho, basi kwa yakini amepotoka upotofu wa mbali”. [An-Nisaa: (137)].
Hivyo ni lazima Muislamu aamini uwepo wa Malaika pamoja na nguzo zote za Iymaan, akiacha moja, basi Iymaan yake imebatilika.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
03: Jogoo Ana Uwezo Wa Kumuona Malaika
Kati ya yenye kuthibitisha uwepo wa Malaika, ni Hadiyth ya Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) iliyosimuliwa na Abu Hurayrah isemayo:
"إِذَا سَمِعْتُمْ صِيَاحَ الدِّيَكَةِ فَاسْأَلُوا اللَّهَ مِنْ فَضْلِهِ؛ فَإِنَّهَا رَأَتْ مَلَكاً وَإِذَا سَمِعْتُمْ نَهِيقَ الْحِمَارِ فَتَعَوَّذُوا بِاللَّهِ مِنَ الشَّيطَانِ؛ فَإِنَّهُ رَأَى شَيْطَاناً"
“Mnaposikia jogoo wanawika, basi muombeni Allaah Fadhla Zake, kwani kwa hakika wamemwona Malaika. Na mnaposikia sauti kali ya punda, basi jilindeni kwa Allaah kutokana na shaytwaan, kwani kwa hakika amemwona shaytwaan”. [Al-Bukhaariy (3303) na Muslim (2729)]
Hizo ni sifa ambazo kwazo jogoo na punda wamemzidi mwanadamu wa kuwa na uwezo wa kuona ambavyo mwanadamu hawezi kuviona. Hivyo basi, Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) anatuelekeza kwamba tukimsikia jogoo anawika, basi hapo hapo tumwombe Allaah Fadhla Zake, kwani jogoo kamuona Malaika. Tuseme kwa mfano:
"اللَّهمَّ إنَّا نَسأَلُك مِن فَضلِك"
“Ee Allaah! Hakika sisi tunakuomba Fadhla Zako”.
Kwa kuwa hapo kuna matumaini makubwa ya Malaika huyo kuitikia “Aamiyn” kwa duaa hiyo na kumwombea mtu maghfira, lakini pia kumshuhudilia ikhlaasi yake kwa Allaah. Na hapo duaa zinavaana pamoja na Allaah Anajibu.
Vile vile, tunaposikia punda analia kwa sauti yake kali ya kubughudhi, basi hapo tujilinde kwa Allaah na shaytwaan aliyewekwa mbali na Rahmah za Allaah, kwa kuwa shaytwaan anakuwa yuko eneo hilo. Hivyo tunatakiwa tujilinde kutokana na shari zake na ushawishi wake.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
04: Maana Ya Kuwaamini Malaika
Kuamini Malaika kunakusanya mambo manne:
1- Kuamini kwamba wapo kwa iymaan ya kukata isiyo na chembe ya shaka.
2- Kuamini majina yao kama tunavyoyasikia kama Jibriyl (‘Alayhis Salaam). Ama wale ambao hatuwajui majina, hao tunawaamini wote kiujumla.
3- Kuamini sifa zao tunazozisikia za kimaumbile na za kitabia.
4- Kuamini kazi zao tunazozisikia.
Haafidh Al-Hakamiy akiielezea nguzo ya pili ya iymaan anasema: “Ni kuamini Malaika ambao wao ni Waja wa Allaah waliotukuzwa. Malaika hawa ni mabalozi kati ya Allaah na Mitume Wake (‘Alayhimus Swalaat was Salaam), wametukuka kimaumbile na kitabia, ni wema waliotwaharika kidhati, kisifa, na kivitendo, wanamtii Allaah ‘Azza wa Jalla bila kuasi, nao ni waja kati ya Waja wa Allaah. Allaah Amewaumba kwa nuru kwa ajili ya kumfanyia Yeye ibada, si mabanati wa Allaah ‘Azza wa Jalla wala watoto wa kiume, wala si washirika pamoja Naye, wala hawako sawa Naye. Allaah Yuko mbali kabisa na wanayodai madhalimu, wapingaji na wasioamini uwepo Wake”.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
05: Matunda Ya Kuamini Malaika
Kuna matunda makubwa ya kuamini Malaika. Kati yake ni:
1- Muislamu anapata kujua U’adhwama wa Allaah Ta’alaa, Nguvu Zake, na Ufalme Wake, kwani ukubwa wa kiumbe unatokana na u’adhwama wa Muumbaji wake. Allaah Anasema:
"وَمِنْ آيَاتِهِ خَلْقُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَثَّ فِيهِمَا مِن دَابَّةٍ ۚ وَهُوَ عَلَىٰ جَمْعِهِمْ إِذَا يَشَاءُ قَدِيرٌ"
“Na katika Ishara Zake, ni uumbaji wa mbingu na ardhi, na Aliowatawanya humo kati ya viumbe vinavyotembea, Naye kwa kuwakusanya Atakapo Ni Muweza”. [Ash-Shuwraa: (29)].
Ibn Kathiyr akiifasiri aya hii anasema: “Hii ni pamoja na Malaika, majini, watu na wanyama wengineo, wakiwa wametofautiana maumbo yao, rangi zao, lugha zao, maumbile yao, jinsia zao na aina zao. Na hawa wote, Allaah Ta’aalaa Amewatawanya kwenye majimbo ya mbinguni na ardhini”.
Na Malaika Jibriyl (‘Alayhis Salaam) ana mbawa 600 ambazo zinafunika mashariki yote. Je, Allaah Aliyemuumba Atakuwa vipi?
2- Muislamu anapata kumshukuru Allaah ‘Azza wa Jalla kwa kuwapa wanadamu uangalizi na ulinzi pale Alipowapa baadhi ya Malaika jukumu la kuwalinda, na Malaika wengineo jukumu la kusajili matendo yao na mengineyo katika maslaha yao.
3- Kunamhisisha mtu kwamba Allaah Anamfuatilia, na kwamba Malaika Wake wanasajili matendo yake yote, na hii inakuwa ni chachu kwake ya kuongeza bidii katika ibada na kujiweka mbali na mambo mabaya.
4- Na kwa vile wao hawamwasi Allaah kwa lolote Analowaamuru, na wanafanya yote wanayoamuriwa, kwa hili, Muislamu anajitahidi awaige katika kutekeleza Maamrisho yote ya Allaah Ta’aalaa.
5- Kunamfanya Muislamu kuwa na pupa ya kuwepo mahala ambapo Malaika wanapapenda kama Misikitini, kwenye vikao vya elimu za dini, adhkaar na kadhalika.
Alhidaaya.com [3]
06: Malaika Jibriyl
Allaah ‘Azza wa Jalla Amelitaja jina lake katika aayah tatu kwenye Qur-aan Tukufu.
1- Neno Lake ‘Azza wa Jalla:
"قُلْ مَن كَانَ عَدُوًّا لِّجِبْرِيلَ فَإِنَّهُ نَزَّلَهُ عَلَىٰ قَلْبِكَ بِإِذْنِ اللَّـهِ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ وَهُدًى وَبُشْرَىٰ لِلْمُؤْمِنِينَ "
“Sema: Yeyote aliyekuwa adui wa Jibriyl, basi hakika yeye ameiteremsha Qur-aan katika moyo wako (ee Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم) kwa Idhini ya Allaah inayosadikisha yaliyo kabla yake, na mwongozo na bishara kwa Waumini”. [Al-Baqarah: (97)].
2- Neno Lake Allaah Ta’aalaa:
"مَن كَانَ عَدُوًّا لِّلَّـهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَرُسُلِهِ وَجِبْرِيلَ وَمِيكَالَ فَإِنَّ اللَّـهَ عَدُوٌّ لِّلْكَافِرِينَ"
“Yeyote aliyekuwa adui wa Allaah na Malaika Wake, na Rusuli Wake, na Jibriyl, na Miykaala, basi hakika Allaah Ni adui kwa makafiri”. [Al-Baqarah: (98)].
3- Kauli Yake Ta’aalaa:
"إِنْ تَتُوبَا إِلَى اللَّـهِ فَقَدْ صَغَتْ قُلُوبُكُمَا ۖ وَإِن تَظَاهَرَا عَلَيْهِ فَإِنَّ اللَّـهَ هُوَ مَوْلَاهُ وَجِبْرِيلُ وَصَالِحُ الْمُؤْمِنِينَ ۖ وَالْمَلَائِكَةُ بَعْدَ ذَٰلِكَ ظَهِيرٌ"
“Ikiwa nyinyi wawili mtatubia kwa Allaah basi ni kheri kwenu), kwani kwa hakika nyoyo zenu zimeelemea (kwa yanayomchukiza Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم). Na mkisaidiana dhidi yake, basi hakika Allaah Ndiye Mlinzi Msaidizi wake na Jibriyl na Waumini wema, na zaidi ya hayo, Malaika pia watasaidia”. [At-Tahriym: (04)].
Ama katika Hadiyth:
4- Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaah ‘anhumaa) amesema:
"كَانَ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم أَجْوَدَ النَّاسِ بِالْخَيْرِ، وَكَانَ أَجْوَدَ مَا يَكُونُ فِي شَهْرِ رَمَضَانَ، حَتَّى يَنْسَلِخَ، فَيَأْتِيهِ جِبْرِيلُ، فَيَعْرِضُ عَلَيْهِ الْقُرْآنَ، فَإِذَا لَقِيَهُ جِبْرِيلُ كَانَ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم، أَجْوَدَ بِالْخَيْرِ مِنَ الرِّيحِ الْمُرْسَلَةِ"
“Rasuli wa Allaah alikuwa ni mtoaji zaidi kuliko wote kwa mambo ya kheri, na alikuwa mtoaji kupita mpaka anapokuwa katika Mwezi wa Ramadhaan mpaka unapomalizika, na hapo Jibriyl humjia akamsomesha Qur-aan. Na Jibriyl anapokutana naye, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam), alikuwa ni mtoaji zaidi wa mambo ya kheri kuliko upepo Alioutuma Allaah (kuleta mvua na baraka). [Al-Bukhaariy (06) na Muslim (2308)]
5- Bibi ‘Aaishah amesema:
"كَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا قَامَ مِنَ اللَّيْلِ افْتَتَحَ صَلَاتَهُ فَقَالَ: اللَّهُمَّ رَبَّ جِبْرِيلَ وَمِيكَائِيلَ وَإِسْرَافِيلَ ، فَاطِرَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ، عَالِمَ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ"
“Alikuwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anaposimama usiku, anaifungua swalah yake kwa kusema: “Ee Allaah! Mola wa Jibriyl, Miykaaiyl, na Israafiyl, Muumba wa mbingu na ardhi, Unayejua yaliyofichikana na yenye kuonekana..” [Muslim (628). Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh].
Jibriyl (‘Alayhis Salaam) ndiye Malaika aliyekurubishwa zaidi kwa Allaah kuliko Malaika wengine. Ni Malaika mwenye nguvu kubwa mno. Aliinyanyua miji ya kaumu Luwt kwa ubawa wake, kisha akawapindulia juu chini. Pia ana nguvu za kutekeleza yote anayoamrishwa, hakuna linalomshinda, na Malaika wote wa mbinguni wanamtii kwa yale anayowaamrisha toka kwa Allaah Ta’aalaa.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
07: Malaika Miykaaiyl
Allaah Ta’aalaa Amesema:
"مَنْ كَانَ عَدُوًّا لِّلَّـهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَرُسُلِهِ وَجِبْرِيلَ وَمِيكَالَ فَإِنَّ اللَّـهَ عَدُوٌّ لِّلْكَافِرِينَ"
“Yeyote aliyekuwa adui wa Allaah na Malaika Wake, na Rusuli Wake, na Jibriyl, na Miykaala, basi hakika Allaah Ni adui kwa makafiri”. [Al-Baqarah: 98].
Miykaaiyl ametajwa katika aayaah hii pamoja na Jibriyl (‘Alayhis salaam) kwa kuwa Mayahudi walidai kwamba Jibriyl ni adui yao, lakini Miykaaiyl ni kipenzi chao. Na hapa Allaah Anawajulisha kuwa yeyote kati yao atakayemfanya Jibriyl ni adui, basi amewafanya Malaika wote kuwa maadui. Lakini pia amemfanya Allaah kuwa adui. Na hili ni jambo la hatari kabisa. Muislamu anatakiwa atahadhari sana na itikadi kama hizi.
Malaika Miykaaiyl ndiye anayesimamia suala la mvua na riziki kwa viumbe. Na mbali na kutajwa kwenye aayah hii, pia Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam amemtaja katika duaa yake katika Hadiyth iliyoelezewa na Bibi ‘Aaishah (Radhwiya Allaah ‘anhaa):
"كَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا قَامَ مِنَ اللَّيْلِ افْتَتَحَ صَلَاتَهُ فَقَالَ: اللَّهُمَّ رَبَّ جِبْرِيلَ وَمِيكَائِيلَ وَإِسْرَافِيلَ ، فَاطِرَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ، عَالِمَ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ"
“Alikuwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anaposimama usiku, anaifungua swalah yake kwa kusema: “Ee Allaah! Mola wa Jibriyl, Miykaaiyl, na Israafiyl, Muumba wa mbingu na ardhi, Unayejua yaliyofichikana na yenye kuonekana..” [Muslim (628). Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh].
Malaika
Alhidaaya.com [3]
08: Israafiyl na Maalik
Malaika Israafiyl pia ametajwa kwenye Hadiyth ya Bibi ‘Aaishah:
"كَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا قَامَ مِنَ اللَّيْلِ افْتَتَحَ صَلَاتَهُ فَقَالَ: اللَّهُمَّ رَبَّ جِبْرِيلَ وَمِيكَائِيلَ وَإِسْرَافِيلَ ، فَاطِرَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ، عَالِمَ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ"
“Alikuwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anaposimama usiku, anaifungua swalah yake kwa kusema: “Ee Allaah! Mola wa Jibriyl, Miykaaiyl, na Israafiyl, Muumba wa mbingu na ardhi, Unayejua yaliyofichikana na yenye kuonekana..” [Muslim (628). Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh].
Ibn Al-Qayyim amesema: “Malaika au viongozi wakuu wa Malaika ni watatu: Jibriyl, Miykaaiyl na Israafiyl. Na imetangaa baina ya wanachuoni wengi kwamba Israafiyl ndiye atakayepuliza baragumu Siku ya Qiyaamah. Na baadhi yao wamenukuu ijmaa juu ya hilo, lakini hilo halijathibiti kwa khabari sahihi toka kwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam), au toka kwa Allaah Ta’alaa.
Wengine wamesema pia kuwa Israafiyl ni mmoja kati ya Malaika wanaobeba Arshi ya Allaah, lakini hili pia halikuthibiti kwa khabari sahihi.
Ama Maalik, Allaah Ta’aalaa Amemzungumzia Akisema:
"وَنَادَوْا يَا مَالِكُ لِيَقْضِ عَلَيْنَا رَبُّكَ ۖ قَالَ إِنَّكُم مَّاكِثُونَ"
“Na wataita: Ee Maalik (Mlinzi wa moto)! Na Atumalize Rabb wako tufe. Atasema: Hakika nyinyi ni wenye kubakia kuishi humo”. [Az-Zukhruf: 77].
Maalik ndiye mlinzi na msimamizi wa moto wa Jahannam. Toka kwa Samurah (Radhwiya Allaah ‘anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"رَأَيْتُ اللَّيْلَةَ رَجُلَيْنِ أَتَيَانِي قَالاَ الَّذِي يُوقِدُ النَّارَ مَالِكٌ خَازِنُ النَّارِ، وَأَنَا جِبْرِيلُ، وَهَذَا مِيكَائِيلُ"
“Niliwaona (kwenye njozi) usiku wanaume wawili wamenijia. Mmoja wao akaniambia: Anayewasha moto ni Maalik, naye ndiye mlinzi wa moto, na mimi ni Jibriyl, na huyu ni Miykaaiyl”. [Swahiyh Al-Bukhaariy: (3236)].
Malaika
Alhidaaya.com [3]
09: Munkar Na Nakiyr
Hawa ni Malaika wawili wanaomwadhibu na kumtahini maiti kaburini, na ndio wanaomuuliza Mola wake nani, dini yake ipi, na nani Nabiy wake? Na hii ni kwa Hadiyth ya Abu Hurayrah (Radhwiya Allaah ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إِذَا قُبِرَ الْمَيِّتُ -أوْ قَالَ: أحَدُكُمْ- أَتَاهُ مَلَكَانِ أَسْوَدَانِ أَزْرَقَانِ، يُقَالُ لَأحَدِهِمَا الْمُنْكَرُ وَالآخَرُ النَّكِيرُ، فَيَقُولَانِ: مَا كُنْتَ تَقُولُ في هَذَا الرَّجُلِ؟ فَيَقُولُ مَا كَانَ يَقُولُ: هُوَ عَبْدُ اللَّهِ وَرَسُولُهُ، أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَأنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ، فَيَقُولَانِ: قَدْ كُنَّا نَعْلَمُ أَنَّكَ تَقُولُ هَذَا... وَإِنْ كَانَ مُنَافِقًا قَالَ: سَمِعْتُ النَّاسَ يَقُولُونَ فَقُلْتُ مِثْلَهُ، لَا أَدْرِى، فَيَقُولَانِ: قَدْ كُنَّا نَعْلَمُ أَنَّكَ تَقُولُ ذَلِك"
“Maiti anapotiwa kaburini -au alisema: Mmoja wenu- humjia Malaika wawili weusi wenye macho ya kibuluu. Mmoja wao anaitwa Munkar na mwingine Nakiyr, na watamuuliza: Ulikuwa unasema nini kuhusu mtu huyu? Naye atasema yale aliyokuwa anasema: Yeye ni Mja wa Allaah na Mjumbe Wake. Ninashuhudia kwamba hakuna mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mja Wake na Mjumbe Wake. Malaika watamwambia: Sisi kwa hakika tulikuwa tunajua kwamba wewe utayasema haya. Na kama maiti ni mnafiki, atasema: Nilikuwa nawasikia tu watu wakisema, nami nikasema mfano wake, sijui. Watamwambia: Sisi kwa hakika tulikuwa tunajua kwamba wewe utasema hivyo”. [Imekharijiwa na At-Tirmidhiy (1071) na Ibn Hibaan (3117)].
Imaam Ahmad bin Hanbal amesema: “Muislamu ni lazima aamini kwamba kuna adhabu ya kaburi, na kwamba umma huu utatahiniwa ndani ya kaburi, na utaulizwa kuhusu iymaan na Uislamu, utaulizwa nani Mola wao? Nani Nabiy wao? Na watajiwa na Munkar na Nakiyr kwa ajili hiyo”.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
10: Haaruwta na Maaruwta
Hawa ni Malaika wawili walioteremshwa ardhini kama fitnah na majaribio kwa watu toka kwa Allaah Ta’alaa.
Allaah Ta’aalaa Anasema:
"وَمَا أُنزِلَ عَلَى الْمَلَكَيْنِ بِبَابِلَ هَارُوتَ وَمَارُوتَ ۚ وَمَا يُعَلِّمَانِ مِنْ أَحَدٍ حَتَّىٰ يَقُولَا إِنَّمَا نَحْنُ فِتْنَةٌ فَلَا تَكْفُرْ"
“Na yaliyoteremshwa kwa Malaika wawili katika (mji wa) Baabil; Haaruwta na Maaruwta. Nao wawili hawamfundishi yeyote mpaka waseme: Hakika sisi ni mtihani, basi usikufuru”. [Al-Baqarah: 102]
Waliteremshwa katika mji wa Baabil nchini Iraki, na Allaah Akawapa ruksa ya kuwafundisha watu uchawi kama mtihani kwao, nao walikuwa hawamfundishi mtu ila baada ya kumuusia na kumtahadharisha kwamba asijifundishe fani hiyo, kwani ni ukafiri. Sababu ni kuwa kuwa mtu akishaujua uchawi, bila shaka atakuja kuutumia kudhuru watu bila sababu kutokana na ushawishi wa shaytwaan, au kuutumia katika mambo yasiyo na faida. Hivyo, baadhi ya watu hao walijifundisha fani ya kumtenganisha mtu na mkewe na kuvunja ndoa za watu ambazo Allaah Amejengea ndani yake mapenzi na mahaba kati ya mke na mume.
Na hii ni dalili inayothibitisha kwamba uchawi upo, na wachawi wapo, na kazi yao ni kudhuru watu.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
11: Malakul Mawt (Malaika Wa Kutoa Roho)
Katika baadhi ya aathaar, Malaika mtoa roho (Malakul Mawt) ametajwa kama ‘Izraaiyl, lakini jina hili halijathibitishwa, si katika Qur-aan wala katika Sunnah.
Ibn Kathiyr amesema: “Malakul Mawt jina lake halijatajwa katika Qur-aan wala katika Hadiyth zilizo swahiyh, lakini ametajwa katika baadhi ya aathaar kama ni ‘Izraaiyl, na Allaah Ndiye Ajuaye zaidi”.
Sheikh Bin Baaz (Allaah Amrehemu) aliulizwa kama katika Hadiyth za Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) limethibiti jina la ‘Izraaiyl kama ni Malaika mtoa roho? Naye alijibu akisema: Sijui chochote kilichothibiti kuhusiana na hili, lakini lililotangaa baina ya Wanazuoni ni kuwa jina lake ni ‘Izraaiyl, lakini mimi sijui Hadiyth yoyote iliyo sahihi kwamba jina lake ni hilo, bali limetajwa kwenye aathaar dhaifu ambazo hazifai kuwa ni hoja”.
Ama Al-Albaaniy, yeye kasema: “Malakul Mawt ndio jina lake lililotajwa ndani ya Qur-aan Tukufu. Ama kumuita ‘Izraaiyl kama ilivyotangaa kwa watu, hilo halina asili, bali limechukuliwa toka kwenye Israaiyliyyaat (Hadiyth na riwaayah za kutunga toka kwenye Taurati na Injili”.
‘Abdulrahmaan Al-Barraak amesema: “Jina hili la ‘Izraaiyl ni mashuhuri lakini halikuthibiti, bali majina ya Malaika yaliyothibiti ni Jibriyl, Miykaaiyl, Israafiyl, Maalik mlinzi wa moto, pia Munkar na Nakiyr, nao ni Malaika wawili wanaomuuliza maswali maiti kaburini”.
Malakul Mawt ametajwa katika Kauli Yake Ta’aalaa:
قُلْ يَتَوَفَّاكُم مَّلَكُ الْمَوْتِ الَّذِي وُكِّلَ بِكُمْ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّكُمْ تُرْجَعُونَ
“Sema: Atakufisheni Malaika wa mauti ambaye amewakilishwa kwenu, kisha kwa Rabb wenu mtarejeshwa”. [As-Sajdah: 11].
Malaika
Alhidaaya.com [3]
12: Malaika Mlinzi Wa Pepo
Pia imetangaa kwa wengi kuwa Malaika mwenye jukumu la kusimamia Pepo ni Ridhwaan. Lakini jina hili pia halikuelezwa katika Qur-aan wala katika Hadiyth Swahiyh.
Tume Ya Kudumu Ya Utoaji Fatwaa Ya Saudia iliulizwa: Je, Ridhwaan ni msimamizi wa Pepo? Wapi jina lake limetajwa? Ikajibu ikisema kwamba lililo mashuhuri kwa ‘Ulamaa ni kwamba jina la msimamizi wa Pepo ni Ridhwaan, na jina hili limetajwa kwenye baadhi ya Hadiyth ambazo uthibiti wake una walakini.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
13: Malaika Wameumbwa Kutokana Na Nuru
Toka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaah ‘anhaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"خُلِقَتِ الْمَلاَئِكَةُ مِنْ نُورٍ، وَخُلِقَ الْجَانُّ مِنْ مَارِجٍ مِنْ نَارٍ، وَخُلِقَ آدَمُ مِمَّا وُصِفَ لَكُمْ"
“Malaika wameumbwa kutokana na nuru, na majini wameumbwa kutokana na mwako wa moto, na mwanadamu ameumbwa kutokana na kile mlichoelezewa (na Allaah kwenye Qur-aan)”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim].
Ama wakati wa kuumbwa kwao, hili Allaah Pekee ndilo Alijualo. Lakini lisilo na shaka ni kuwa waliumbwa kabla ya mwanadamu kutokana na Neno Lake Ta’aalaa:
“وَإِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَائِكَةِ إِنِّي جَاعِلٌ فِي الْأَرْضِ خَلِيفَةً ۖ قَالُوا أَتَجْعَلُ فِيهَا مَن يُفْسِدُ فِيهَا وَيَسْفِكُ الدِّمَاءَ وَنَحْنُ نُسَبِّحُ بِحَمْدِكَ وَنُقَدِّسُ لَكَ ۖ قَالَ إِنِّي أَعْلَمُ مَا لَا تَعْلَمُونَ”
“Na pale Rabb wako Alipowaambia Malaika: Hakika Mimi Nitaweka katika ardhi khalifa. Wakasema: Utaweka humo atakayefanya ufisadi humo na kumwaga damu, na hali sisi tunakusabihi kwa Himidi Zako na tunakutukuza kwa Utakatifu Wako? (Allaah) Akasema: Hakika Mimi Nayajua zaidi msiyoyajua”. [Al-Baqarah: 30].
Khalifa hapa ni baba yetu Aadam (‘Alayhis Salaam) kwa mujibu wa kauli ya Ibn Mas-‘uwd na Ibn ‘Abbaas.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
14: Lini Waliumbwa Malaika?
Allaah Pekee Ndiye Ajuaye wakati Alipowaumba. Na jambo lisilo na shaka yoyote ni kwamba Malaika hawa waliumbwa kabla ya kuumbwa baba yetu Aadam (‘alayhis salaam). Na dalili ya hili ni Kauli Yake Ta’aalaa:
"وَإِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَائِكَةِ إِنِّي جَاعِلٌ فِي الْأَرْضِ خَلِيفَةً"
“Na pale Rabb wako Alipowaambia Malaika: Hakika Mimi Nitaweka katika ardhi khalifa”. [Al-Baqarah: 30]
Khalifa anayekusudiwa hapa ni Aadam (‘alayhis salaam) kwa mujibu wa kauli ya Ibn Mas-‘uwd na Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaah ‘anhumaa).
Hivyo basi, Malaika walikuweko kabla ya kuumbwa baba yetu Aadam (‘alayhis Salaam) kwa miaka mingi tu. Wao walitutangulia kuwepo.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
15: Je, Tunaweza Kuwaona Malaika Katika Umbile Lao Halisi?
Haijawahi kuelezwa kwamba kuna yeyote katika umma huu ambaye amewaona Malaika katika umbile lao asilia isipokuwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Yeye alimwona Jibriyl (‘alayhis salaam) mara mbili katika umbile lake asili Alilomuumbia nalo Allaah Ta’aalaa. Mara ya kwanza ni kwa Kauli Yake Ta’aalaa:
"وَلَقَدْ رَآهُ بِالْأُفُقِ الْمُبِينِ"
“Na kwa yakini (Rasuli) alimuona (Jibriyl) katika upeo wa macho ulio bayana”. [At-Takwiyr: 23].
Na ya pili ni:
"وَلَقَدْ رَآهُ نَزْلَةً أُخْرَىٰ ● عِندَ سِدْرَةِ الْمُنتَهَىٰ ● عِندَهَا جَنَّةُ الْمَأْوَىٰ"
“Na kwa yakini amemuona (Jibriyl) katika uteremko mwingine • Kwenye mkunazi wa mpaka wa mwisho kabisa • Karibu yake kuna Jannah ya Al-Ma-waa”. [An-Najm: 13-15].
Ibn Kathiyr amesema: “Neno Lake Ta’aalaa: وَلَقَدْ رَآهُ بِالأُفُقِ الْمُبِينِ lina maana:
Kwa hakika Muhammad alimwona Jibriyl anayemletea Wahyi kutoka kwa Allaah ‘Azza wa Jalla katika umbile lake Alilomuumba nalo Allaah ‘Azza wa Jalla akiwa na mbawa mia sita katika upeo wa macho ulio bayana. Hii ilikuwa ndio mara ya kwanza huko Al-Batwhaa”.
Anaendelea kusema: “Jibriyl alikuwa anamjia Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa sura tofauti. Mara kwa sura ya Dihyat bin Khaliyfah Al-Kalbiy, mara nyingine kwa sura ya bedui, na mara nyingine katika umbile lake asili aliloumbiwa nalo. Ana mbawa mia sita, na kati ya kila mbawa mbili ni kama baina ya mashariki na magharibi. Alimwona katika umbile hili asilia mara mbili; mara alipokuwa anashuka toka mbinguni kuja ardhini, na mara nyingine kwenye mkunazi wa mpaka wa mwisho kabisa Rasuli alipopandishwa mbinguni”.
Bibi ‘Aaishah (Radhwiya Allaah ‘anhaa) alimuuliza Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusiana na Aayah hizi mbili. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia:
"إنما هو جِبريلُ [18]، لم أرَه على صورتِه التي خُلِقَ عليها غيرَ هاتين المرَّتَينِ، رأيتُه مُنهَبِطًا من السَّماءِ، سادًّا عِظَمُ خَلْقِه ما بين السَّماءِ إلى الأرضِ"
“Hakika huyo ni Jibriyl, sikuwahi kumwona katika umbo lake la asili isipokuwa mara hizi mbili. Nilimwona akishuka toka mbinguni huku mwili wake ukiziba sehemu yote baina ya mbingu mpaka ardhini”. [Hadiyth Swahiyh. Muslim (177)]
Naye Bi ‘Aaishah (Radhwiya Allaah ‘anhaa) aliulizwa kuhusu Neno Lake Ta’aalaa:
"ثُمَّ دَنَا فَتَدَلَّىٰ"
“Kisha akakurubia na akashuka”. Akasema:
"إنما ذاك جبريلُ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم، كان يأتيه في صُورةِ الرِّجالِ، وإنَّه أتاه في هذه المرَّةِ في صُورتِه التي هي صورتُه، فسدَّ أُفُقَ السَّماءِ"
“Hakika huyo ni Jibriyl (Swalla Allaah ‘alayhi wa sallam), alikuwa anamjia (Rasuli) katika sura ya mwanaume, na mara hii amemjia katika sura yake ambayo ndiyo ya asili, akaziba upeo wote wa mbingu”. [Hadiyth Swahiyh. Muslim (177)]
Malaika
Alhidaaya.com [3]
16: Mbawa Za Malaika
"الْحَمْدُ لِلَّـهِ فَاطِرِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ جَاعِلِ الْمَلَائِكَةِ رُسُلًا أُولِي أَجْنِحَةٍ مَّثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ ۚ يَزِيدُ فِي الْخَلْقِ مَا يَشَاءُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ"
“AlhamduliLLahi (Himdi Anastahiki Allaah), Muanzilishi wa mbingu na ardhi, Mwenye Kuwafanya Malaika kuwa wajumbe wenye mbawa mbili-mbili, tatu-tatu na nne-nne. Huzidisha katika uumbaji Atakavyo. Hakika Allaah Ni Muweza juu ya kila kitu”. [Faatwir: 01]
Ibn Kathiyr amesema: “Kuna Malaika wenye mbawa mbili mbili, wengine tatu tatu, wengine nne nne, na wengine zaidi ya hapo. Huzitumia kuruka haraka ili kwenda kufikisha yale waliyotumwa na Allaah kuyafikisha au kuyafanya, au kutekeleza jukumu lolote walilokalifishwa”.
‘Abdullaah bin Mas-‘uwd (Radhwiya Allaah ‘anhu) amesema kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwona Jibriyl akiwa na mbawa mia sita”.
Toka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaah ‘anhu), Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إِذَا قَضَى اللَّهُ فِي السَّمَاءِ أَمْرًا ضَرَبَتِ الْمَلاَئِكَةُ بِأَجْنِحَتِهَا خُضْعَانًا لِقَوْلِهِ كَأَنَّهُ سِلْسِلَةٌ عَلَى صَفْوَانٍ فَإِذَا فُزِّعَ عَنْ قُلُوبِهِمْ قَالُوا مَاذَا قَالَ رَبُّكُمْ قَالُوا الْحَقَّ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْكَبِيرُ"
“Allaah Anapopitisha amri mbinguni, Malaika Hupiga mbawa zao kwa ajili ya kulitii Neno Lake ambalo ni kama sauti ya mnyororo (unaoburutwa) juu ya mwamba. Na fazaiko linapoondoka nyoyoni mwao huuliza: Nini Amesema Mola wenu? (Malaika wabebao ‘Arshi) hujibu: Ni haki, Naye Ni Mwenye ‘Uluwa, Mkubwa wa dhati, vitendo na sifa”. [Hadiyth Swahiyh. Al-Bukhaariy (4800)]
Kwa haya, tunapata kujua kwamba kuna Malaika wenye mbawa mbili mbili, wenye tatu tatu, wenye nne nne na wenye zaidi ya hapo. Jibriyl pekee ameelezewa kuwa anazo mia sita, na wengineo kama wabebao ‘Arshi, Miykaaiyl na Israafiyl hakuna ajuaye isipokuwa Allaah Pekee.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
17: Je, Malaika Wana Sifa Ya Uzuri Wa Sura Na Umbo?
Katika akili za watu, imejengeka taswira ya kuwa Malaika ni viumbe wenye sifa ya uzuri wa sura na maumbo kama Alivyosema Allaah Ta’aalaa kuhusiana na akina mama walioalikwa na Zulaykha wakati walipomwona Yuwsuf (‘Alayhis Salaam):
"فَلَمَّا رَأَيْنَهُ أَكْبَرْنَهُ وَقَطَّعْنَ أَيْدِيَهُنَّ وَقُلْنَ حَاشَ لِلَّـهِ مَا هَـٰذَا بَشَرًا إِنْ هَـٰذَا إِلَّا مَلَكٌ كَرِيمٌ"
“Basi walipomuona (Yuwsuf) walimpa haiba na utukuzo, wakajikatakata mikono yao, na wakasema: Utakasifu ni wa Allaah! Huyu si mtu! Hakuwa huyu ila ni Malaika mtukufu”. [Yuwsuf: 31]
Hii ni dhana njema kwa upande wa viumbe hawa ambao hakuna binadamu yeyote aliopata kuwaona isipokuwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliyemwona Jibriyl (‘alayhis salaam) katika umbile lake la asili akiwa na mbawa mia sita. Na Jibriyl ndiye Malaika aliyeelezewa sifa zake kwenye Qur-aan Tukufu. Allaah Ta’aalaa Anasema:
"عَلَّمَهُ شَدِيدُ الْقُوَىٰ ● ذُو مِرَّةٍ فَاسْتَوَىٰ"
“Amemfunza (Jibriyl) mwenye nguvu shadidi. ● Mwenye muonekano jamili, muruwa na nguvu na kisha akalingamana sawasawa”. [An-Najm: 5-6]
Hizi ndizo sifa za Jibriyl (‘alayhis salaam) kama zilivyoelezewa kwenye Aayaah hii.
Wengine wenye sura nzuri na maumbo ni pamoja na wale wanaomjia muumini mwema wakati anapokufa ambapo humjia wakiwa na nyuso nyeupe. Wengine ni wale watakaowapokea Waislamu wakati wa kuingia Peponi na kadhalika.
Hivyo basi, Malaika kwa mujibu wa majukumu yao, wana maumbile na sura tofauti zikiwemo za kutisha na kuogofya.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
18: Malaika Wenye Sura Na Maumbo Ya Kutisha
(1)- Maalik Mlinzi Na Msimamizi Wa Jahannam
Toka kwa Samurah bin Jundub (Radhwiya Allaah ‘anhu) kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema akihadithia njozi yake:
"فانطَلَقْنا فأَتَينا على رَجُلٍ كَرِيهِ المَرْآةِ، كأكرَهِ ما أنت راءٍ رَجُلًا مَرآةً، وإذا عِنْدَه نارٌ يَحُشُّها ويسعى حَولَها. قال: قُلْتُ لهما: ما هذا؟! قال: قالا لي: انطَلِقِ انطَلِقِ، فانطَلَقْنا... -وفيه-: قالا لي:... وأمَّا الرَّجُلُ الكَريهُ المَرْآةِ، الذي عند النَّارِ يَحُشُّها ويَسْعى حَوْلَها، فإنَّه مالِكٌ خازِنُ جَهَنَّمَ"
“…Tukaondoka, halafu tukamjia mtu mwenye mwonekano mbaya mno, kama vile unavyomwona mtu mwenye sura mbaya mno ambayo hujapata kuiona. Na mtu huyo ana moto anaouchochea na anakwenda akiuzunguka. Nikawauliza: Nani huyu? Wakaniambia: Twende, twende, tukaondoka. (Na Rasuli alipowauliza baadae Malaika hao wawili kuhusu mtu huyo mwenye sura mbaya mno walimwambia): Huyo ni Maalik mlinzi wa Jahannam”. [Hadiyth Swahiyh. Al-Bukhaariy (7047)]
Ibn Rajab amesema: “Maalik ndiye mlinzi wa Jahannam, na ndiye mkuu wa walinzi wa Jahannam. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwona usiku wa Mi’iraji”.
Na mwonekano wake huo mbaya, utakuwa ni nyongeza ya adhabu kwa watu wa motoni. Allaah Atulinde nao.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
19: Malaika Wenye Sura Na Maumbo Ya Kutisha
(2)- Zabaaniyah Wa Jahannam
Allaah Ta’aalaa Anasema:
"يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوا أَنفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَارًا وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ عَلَيْهَا مَلَائِكَةٌ غِلَاظٌ شِدَادٌ لَّا يَعْصُونَ اللَّـهَ مَا أَمَرَهُمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ"
“Enyi walioamini! Jikingeni nafsi zenu pamoja na ahli zenu na moto ambao kuni zake ni watu na mawe. Wanaulinda Malaika washupavu wasio na huruma, wakali, hawamuasi Allaah kwa yale Anayowaamrisha na wanafanya yale wanayoamrishwa”. [At-Tahriym: 06]
Malaika hawa inaonyesha wako chini ya mkuu wao Maalik, kazi yao ni kuwatesa watu wa motoni, kuwadhalilisha na kuwadhibiti.
Ibn Kathiyr akielezea maana ya "شِدَادٌ" amesema: “Wameumbwa kwa maumbile yaliyo kwenye ukomo wa ukali, nguvu na mwonekano wa kukera na kutisha. Hawa ndio “Zabaaniyah”. Tunamwomba Allaah Atulinde tusikutane nao.
As-Sa’adiyy naye kasema akilielezea neno hilo hilo: “Tabia zao ni ngumu mno, wanakemea kwa ukali uliopitiliza, sauti zao zinaogopesha mno, na wanaogopesha mno ukiwaona. Watakuwa wakiwadhalilisha watu wa motoni kwa nguvu walizopewa na Allaah”.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
20: Malaika Wenye Sura Na Maumbo Ya Kutisha
(3)- Munkar Na Nakiyr
Hawa ni Malaika wawili wanaomwadhibu na kumtahini maiti kaburini, na ndio wanaomuuliza Mola wake nani, dini yake ipi, na nani Nabiy wake? Na hii ni kwa Hadiyth ya Abu Hurayrah (Radhwiya Allaah ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إِذَا قُبِرَ الْمَيِّتُ -أوْ قَالَ: أحَدُكُمْ- أَتَاهُ مَلَكَانِ أَسْوَدَانِ أَزْرَقَانِ، يُقَالُ لَأحَدِهِمَا الْمُنْكَرُ وَالآخَرُ النَّكِيرُ، فَيَقُولَانِ: مَا كُنْتَ تَقُولُ في هَذَا الرَّجُلِ؟ فَيَقُولُ مَا كَانَ يَقُولُ: هُوَ عَبْدُ اللَّهِ وَرَسُولُهُ، أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَأنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ، فَيَقُولَانِ: قَدْ كُنَّا نَعْلَمُ أَنَّكَ تَقُولُ هَذَا... وَإِنْ كَانَ مُنَافِقًا قَالَ: سَمِعْتُ النَّاسَ يَقُولُونَ فَقُلْتُ مِثْلَهُ، لَا أَدْرِى، فَيَقُولَانِ: قَدْ كُنَّا نَعْلَمُ أَنَّكَ تَقُولُ ذَلِك"
“Maiti anapotiwa kaburini -au alisema: Mmoja wenu- humjia Malaika wawili weusi wenye macho ya kibuluu. Mmoja wao anaitwa Munkar na mwingine Nakiyr, na watamuuliza: Ulikuwa unasema nini kuhusu mtu huyu? Naye atasema yale aliyokuwa anasema: Yeye ni Mja wa Allaah na Mjumbe Wake. Ninashuhudia kwamba hakuna mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mja Wake na Mjumbe Wake. Malaika watamwambia: Sisi kwa hakika tulikuwa tunajua kwamba wewe utayasema haya. Na kama maiti ni mnafiki, atasema: Nilikuwa nawasikia tu watu wakisema, nami nikasema mfano wake, sijui. Watamwambia: Sisi kwa hakika tulikuwa tunajua kwamba wewe utasema hivyo”. [Imekharijiwa na At-Tirmidhiy (1071) na Ibn Hibaan (3117)].
Kama walivyoelezewa na Hadiyth hii, Malaika hawa Munkar na Nakiyr ambao wanatusubiri tukishazikwa tu, ni weusi wenye macho ya kibuluu. Bila shaka ni mwonekano wa kutisha mno, na hasa tukizingatia kuwa mtu ndio mara yake ya kwanza kukutana nao, akiwa katika mazingira mapya kabisa, na akiwa peke yake baada ya nduguze kuondoka. Ni hali ngumu kwa kweli ambao wengi haiwatikisi hata mshipa wa roho!. Lakini, watakutana nayo tu, na hapo ndipo patakuwa majuto ya kosa lisiloweza kusahihishika!
Ibn Al-‘Arabiy amesema: “Kila anayewaona atasisimkwa vibaya na mwili kutokana na mwonekano wao wa kutisha, sura mbaya na maneno yao makali pamoja na marungu makubwa waliyoyakamata yenye kuzidi kuleta hofu na fazaiko kwa maiti”.
Ibn Al-Malik Ar-Ruwmiy Al-Hanafiy amesema: “Kuja kwao kwa picha hii, ni kuwatia kiwewe makafiri wachanganyikiwe wasiweze kujibu maswali watakayoulizwa”.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
21: Malaika Wenye Sura Na Maumbo Ya Kutisha
(4)- Malaika Wenye Kutoa Roho Ya Kafiri
Al-Baraa bin ‘Aazib (Radhwiya Allaah ‘anhu): “Kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema kuhusiana na kutoka roho:
"وإنَّ العَبدَ الكافِرَ إذا كان في انقِطاعٍ مِنَ الدُّنيا وإقبالٍ مِنَ الآخرةِ، نزل إليه من السَّماءِ مَلائِكةٌ سُودُ الوُجوهِ"
“Na hakika mja kafiri anapokuwa karibu na kuaga dunia na kuikabili aakhirah, humteremkia kutoka mbinguni Malaika wenye nyuso nyeusi”. [Hadiyth Swahiyh. Swahiyhul Jaami’i].
Wanakuja kwa nyuso hizo kuonyesha hasira yao kwa anayekufa. Hiyo ndiyo hatima ya makafiri. Mbali ya kujiwa na nyuso hizo nyeusi, Malaika hao watawapiga nyuso zao na migongo yao katika hali ambayo Rasuli anaambiwa kama angeliona wanavyopigwa, basi angeliona jambo la kutisha mno. Allaah Ta’aalaa Anasema:
"وَلَوْ تَرَىٰ إِذْ يَتَوَفَّى الَّذِينَ كَفَرُوا ۙ الْمَلَائِكَةُ يَضْرِبُونَ وُجُوهَهُمْ وَأَدْبَارَهُمْ وَذُوقُوا عَذَابَ الْحَرِيقِ"
“Na lau ungeliona pale Malaika wanapowafisha wale waliokufuru, wanawapiga nyuso zao na migongo yao na (wanawaambia): Onjeni adhabu iunguzayo”. [Al-Anfaal: 50]
Malaika
Alhidaaya.com [3]
22: Malaika Wana Uwezo Wa Kujigeuza Umbo Jingine Lisilo Lao
Allaah Ta’aalaa Amewapa Malaika uwezo wa kujibadilisha umbo lao la asili na kujiweka kwenye umbo jingine. Jibriyl ‘Alayhis Salaam alipomwendea Bibi Maryam (‘Alayhas Salaam), alijimithilisha katika umbo la binadamu kama inavyoeleza Qur-aan Tukufu:
"فَاتَّخَذَتْ مِن دُونِهِمْ حِجَابًا فَأَرْسَلْنَا إِلَيْهَا رُوحَنَا فَتَمَثَّلَ لَهَا بَشَرًا سَوِيًّا • قَالَتْ إِنِّي أَعُوذُ بِالرَّحْمَـٰنِ مِنكَ إِن كُنتَ تَقِيًّا "
“Akafanya pazia kujitenga nao, Tukampelekea Ruwh Wetu (Jibriyl عليه السلام) akajimithilisha kwake kama bin Aadam timamu ● (Maryam) akasema: Najikinga kwa Ar-Rahmaan usinidhuru, ukiwa ni mwenye taqwa”. [Maryam: 17-18]
Jibriyl alikuwa katika umbo la mwanaume kamili, ndipo Maryam akaogopa asije kumdhuru na hapo akajikinga kwa Allaah Ta’aalaa. Muislamu anapohisi hatari kutoka kwa mtu au kiumbe chochote, basi aharakie kujikinga kwa Allaah na shari yake.
Nabiy Ibraahiym (‘Alayhis Salaam) alijiwa na Malaika wakiwa katika sura ya binadamu, naye hakuwajua kama ni Malaika mpaka alipowatengea nyama na chakula akaona hawala na akaingiwa na hofu, na wao wakajitambulisha kwamba ni Malaika ambao wametumwa kwenda kutekeleza kazi maalum ya kuwaangamiza kaumu Lut waliochupa mipaka. Allaah Anatuambia:
"وَلَقَدْ جَاءَتْ رُسُلُنَا إِبْرَاهِيمَ بِالْبُشْرَىٰ قَالُوا سَلَامًا ۖ قَالَ سَلَامٌ ۖ فَمَا لَبِثَ أَن جَاءَ بِعِجْلٍ حَنِيذٍ • فَلَمَّا رَأَىٰ أَيْدِيَهُمْ لَا تَصِلُ إِلَيْهِ نَكِرَهُمْ وَأَوْجَسَ مِنْهُمْ خِيفَةً ۚ قَالُوا لَا تَخَفْ إِنَّا أُرْسِلْنَا إِلَىٰ قَوْمِ لُوطٍ"
“Na kwa yakini walimjia Ibraahiym Wajumbe Wetu kwa bishara, wakasema: Salaam! (Naye) Akasema: Salaam. Basi hakukawia ila alikuja na ndama aliyebanikwa • Alipoona mikono yao haisogei kumla (ndama) aliwashangaa na ikamuingia khofu kutokana nao. Wakasema: Usiogope! Hakika Sisi Tumetumwa kwa kaumu Luwtw”. [Huwd: 69-70]
Malaika hao baada ya kuondoka kwa Nabiy Ibraahiym (‘Alayhis Salaam), walikwenda kwa Nabiy Lut (‘Alayhis Salaam) kwa umbo lile lile la kibinadamu. Allaah Anatuambia:
"وَلَمَّا جَاءَتْ رُسُلُنَا لُوطًا سِيءَ بِهِمْ وَضَاقَ بِهِمْ ذَرْعًا وَقَالَ هَـٰذَا يَوْمٌ عَصِيبٌ"
“Na Wajumbe Wetu walipomjia Luwtw, alisononeka kwa ajili yao na akawaonea dhiki, akasema: Hii ni siku ngumu mno”. [Huwd: 77]
Mufassiruna wengi wanasema kwamba Malaika hao walipofika kwa Lut, walijiweka katika sura ya vijana wazuri ili kuwajaribu watu hao, nao kwa ujasiri wao wa kiovu wakawataka, na Allaah Akawateremshia mvua ya mawe baada ya mji wao kunyanyuliwa juu kisha ukapinduliwa.
Naye Jibriyl (‘Alayhis Salaam) alikuwa akimjia Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa sura tofauti. Mara humjia kwa sura ya Dihyat bin Khaliyfah Al-Kalbiy, mara nyingine kwa sura ya bedui, na mara mbili katika umbile lake la asili aliloumbiwa nalo akiwa na mbawa mia sita ambapo kati ya kila mbawa mbili ni kama baina ya mashariki na magharibi. Dihyat bin Khaliyfah Al-Kalbiy alikuwa ni miongoni mwa Maswahaba wakubwa na alikuwa na sura nzuri mno.
Malaika hawa walikuwa wakija kwa umbo la kibinadamu ili waweze kuonekana. Mwanadamu hana uwezo wa kumwona Malaika katika umbile lake la asili kutokana na udhaifu wake wa kuweza kukabiliana na hilo isipokuwa wale tu ambao Allaah Amewapa nguvu ya kuliweza hilo kama Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
Maswahaba walibahatika kumwona Jibriyl (‘Alayhis Salaam) katika umbo la kibinadamu kama inavyoeleza Hadiyth ya ‘Umar:
“Wakati tukiwa tumekaa siku moja pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa sallam), mara ghafla akatutokezea mtu aliyevaa nguo nyeupe mno, nywele zake nyeusi mno, haonekani na athari yoyote ya safari, na hakuna yeyote kati yetu anayemjua. Akaja na kukaa mbele ya Rasuli na akaegemeza magoti yake kwenye magoti ya Rasuli, na akaweka viganja vyake juu ya mapaja yake, kisha akasema: Ee Muhammad! Nieleze kuhusu Uislamu. …………”
Baada ya kumuuliza Rasuli kuhusu Uislamu, iymaan, ihsaan, qiyaamah na alama zake aliondoka, na Rasuli akawajulisha Maswahaba kwamba huyo alikuwa ni Jibriyl ambaye alikuja kwa ajili ya kuwafundisha dini yao kupitia maswali aliyomuuliza yeye.
Kadhalika, katika kisa cha mtu aliyeua watu 99, mtu huyo alipokuwa anahama kwenda sehemu nyingine baada ya kutubia, mauti yalimjia katikati ya njia ya kati ya kule alikotoka na kule anakoelekea. Malaika wa rahmah wakavutana na Malaika wa adhabu kuhusu nani anayestahiki kumchukua kati yao. Hapo akawajia Malaika katika umbo la kibinadamu akawaambia: Pimeni masafa ya kuanzia hapa alikofia baina ya kule anakoelekea na kule alikotoka. Kama kule anakoelekea pamebakia kidogo, basi Malaika wa rahmah wamchukue.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
23: Malaika Hawana Sifa Ya Jinsia Ya Kiume Wala Ya Kike
Mapagani wa Kiarabu walifanya makosa makubwa walipodai kwamba Malaika ni wanawake na ni mabanati wa Allaah kama Anavyosema Allaah Ta’aalaa:
"وَجَعَلُوا الْمَلَائِكَةَ الَّذِينَ هُمْ عِبَادُ الرَّحْمَـٰنِ إِنَاثًا ۚ أَشَهِدُوا خَلْقَهُمْ ۚ سَتُكْتَبُ شَهَادَتُهُمْ وَيُسْأَلُونَ"
“Na wakawafanya Malaika ambao ni Waja wa Ar-Rahmaan kuwa ni wa kike. Je, kwani wameshuhudia uumbaji wao? Utaandikwa ushahidi wao, na wataulizwa”. [Az-Zukhruf: 19]
Na Anasema tena:
"أَصْطَفَى الْبَنَاتِ عَلَى الْبَنِينَ ● مَا لَكُمْ كَيْفَ تَحْكُمُونَ"
“Je, Amekhitari mabanati kuliko wana wa kiume? ● Mna nini! Vipi mnahukumu?” [Az-Zukhruf: 153-154]
Hilo ni kosa kubwa kabisa walilolifanya mapagani hao, kwa kuwa hawana dalili inayothibitisha madai yao hayo ambayo yamekwisha andikwa, na Siku ya Qiyaamah watakuja kuulizwa walete dalili na hawatakuwa nayo. Hii ndiyo hatari ya mtu kudai jambo lolote bila ya kuwa na dalili nalo, ajue kwamba atakuja atakwe ushahidi wake Siku ya Qiyaamah.
Hivyo basi kuwasifu Malaika kwa jinsia ya kike ni ukafiri, na pia ni ukadhibishaji wa Qur-aan Tukufu. Ama kuelezewa kuwa wana jinsia au maumbile ya kiume, jambo hilo halikuja kwa uwazi katika Qur-aan wala katika Sunnah.
Sa’iyd bin Al-Musayyib amesema: “Malaika “Alayhimus Salaam si wanaume wala wanawake, hawazaani, na hawali wala hawanywi”.
Ibn Hajar amesema: “Malaika si wanaume wala wanawake”.
Na ‘Aliy Al-Qaariy amesema: “Malaika ni waja watakatifu, hawamtangulii Allaah kwa neno, bali maagizo Yake wanayatekeleza, wamelindwa na makosa na hawamwasi Allaah, na wametakaswa na sifa ya kuwa wanaume au wanawake”.
Ama kuwasifu kwa jinsia ya kiume, Allaah Ametumia vitenzi vya kiume katika Aayah zote zinazohusiana nao, ingawa katika baadhi Ametumia vinavyoashiria uke kama neno مُعَقِّبَاتٌ katika Kauli Yake:
"لَهُ مُعَقِّبَاتٌ مِّن بَيْنِ يَدَيْهِ وَمِنْ خَلْفِهِ يَحْفَظُونَهُ مِنْ أَمْرِ اللَّـهِ"
“Ana Malaika wanaofuatana kwa zamu mbele yake na nyuma yake wanamhifadhi kwa Amri ya Allaah”. [Ar-Ra’ad: 13]
Hili limefafanuliwa kitaaluma na Mufassiruna waliobobea lugha.
Jibriyl (‘alayhis-salaam) alikuwa akimjia Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa umbo la mwanaume kwa sura ya Dihyat Al-Kalbiy, au bedui, na hata aliwajia Maswahaba kwa picha hiyo hiyo wakati walipokuwa wamekaa na Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Na pia alikuja kwa umbo hilo hilo wakati wa vita vya Badr, na hata Malaika walioteremka kuwasaidia Waumini kwenye vita. Na hata kwa Bi Maryam, Jibriyl alimwendea kwa umbo la mwanaume.
Makusudio ni kwamba wanawajia wanadamu kama Mitume kwa sura ya mwanaume na si ya mwanamke, na hao Malaika wanasifiwa kwa sifa za kiume na si kwa sifa za kike, na hii haimaanishi kwamba ni wanaume katika maumbo yao ya asili. Pamoja na yote hayo, hakuna yeyote ajuaye namna walivyoumbwa, sifa ya maumbile yao na uhakika wa kuumbwa kwao isipokuwa Allaah Ta’aalaa. Yeye Pekee Ndiye Ajuaye undani na uchambuzi wa yote.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
24: Malaika Hawali, Hawanywi, Hawaoani Wala Hawazai
Allaah Anasema:
’فَرَاغَ إِلَىٰ أَهْلِهِ فَجَاءَ بِعِجْلٍ سَمِينٍ ● فَقَرَّبَهُ إِلَيْهِمْ قَالَ أَلَا تَأْكُلُونَ ● فَأَوْجَسَ مِنْهُمْ خِيفَةً ۖ قَالُوا لَا تَخَفْ ۖ وَبَشَّرُوهُ بِغُلَامٍ عَلِيمٍ"
“Akaondoka bila kuhisiwa kuelekea kwa ahli yake, akaleta ndama aliyenona • Akawakurubishia pale walipo, akasema: Mbona hamli? ● Akawaogopa ndani ya nafsi yake. Wakasema: Usikhofu! Na wakambashiria ghulamu mjuzi”. [Adh-Dhaariyaat: 26-28]
Hawa ni Malaika waliokwenda kwa Nabiy Ibraahiym (‘alayhis Salaam) katika umbile la kibinadamu kama wageni wake. Naye haraka akawatayarishia ndama aliyenona. Alipokuwa tayari, aliwatengea na kuwakaribisha lakini hawakula, na hapo akaingiwa na hofu, lakini walijitambulisha kwamba wao ni Malaika, na Malaika hawali, wala hawanywi. Malaika hawa walikuwa wametumwa kwenda kwa Nabiy Lut (‘Alayhis Salaam) ili kuwaangamiza kaumu yake.
Ibn Kathiyr amesema: “Malaika hawana habari na chakula, hawakitamani wala hawakili”.
As-Safaaraaniy amesema: “Ulamaa wahakiki wamefikia itifaki ya kwamba Malaika hawali, wala hawanywi, wala hawazaani, na wala hawana matamanio ya kimwili. Hii ni kwa vile wao wanamsabbih Allaah usiku na mchana na wala hawachoki kama Anavyosema Allaah Ta’aalaa:
"يُسَبِّحُونَ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ لَا يَفْتُرُون"
“Wanamsabbih Allaah usiku na mchana na wala hawachoki”. [Al-Anbiyaa: 24]
Hawasiti hata dakika moja kumsabbih Allaah. Ikiwa hii ndiyo sifa yao, basi haiwezekani wakawa wanakula, au kunywa, au kujamii.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
25: Malaika Hawachoki Wala Hawahisi Tabu
Malaika wanamwabudu Allaah na kutii Amri Zake bila kuchoka wala kuhisi uzito, hawapati mchoko au kuhisi tabu kama anavyohisi mwanadamu. Allaah Ta’aalaa Anasema:
"فَإِنِ اسْتَكْبَرُوا فَالَّذِينَ عِندَ رَبِّكَ يُسَبِّحُونَ لَهُ بِاللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَهُمْ لَا يَسْأَمُونَ"
“Lakini wakitakabari, basi wale (Malaika) walio kwa Rabb wako wanamsabbih usiku na mchana, nao hawachoki”. [Fusswilat: 38]
As-Sa’adiyy akielezea sifa za Malaika amesema: “Allaah Amewasifu kwa sifa zilizokamilika, nao wana nguvu kamili za kumwabudu Allaah na utashi mkubwa kabisa wa kufanya hilo. Wanamsabbih Allaah usiku na mchana na wala hawachoki, hawana kibri cha kukataa kumwabudu, bali wanaliona hilo kuwa ni katika neema kubwa kwao, hawamwasi Allaah kwa Alilowaamrisha na wanafanya wanayoamuriwa”.
As-Suyuwtwiy amesema: “Niliulizwa zamani kuhusu Malaika, je wanalala?” Nikajibu kwamba sikuona nukuu yoyote inayogusia hilo, lakini inavyoonyesha ni kuwa hawalali kutokana na Kauli Yake Ta’aalaa:
"يُسَبِحُونَ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ لَا يَفْتُرُونَ"
“Wanamsabbih usiku na mchana, nao hawachoki”.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
26: Makazi Ya Malaika
Makazi na mashukio ya Malaika ni mbinguni. Bibi ‘Aaishah (Radhwiya Allaah ‘anhaa) alimsikia Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:
"إنَّ المَلَائِكَةَ تَنْزِلُ في العَنَانِ: وهو السَّحَابُ، فَتَذْكُرُ الأمْرَ قُضِيَ في السَّمَاءِ، فَتَسْتَرِقُ الشَّيَاطِينُ السَّمْعَ فَتَسْمَعُهُ، فَتُوحِيهِ إلى الكُهَّانِ، فَيَكْذِبُونَ معهَا مِئَةَ كَذْبَةٍ مِن عِندِ أنْفُسِهِمْ"
“Hakika Malaika hushuka kwenye anga za karibu wakaelezana jambo lililopitishwa mbinguni. Mashetani hudukua wakapata kusikiliza wanayoyasema, halafu huja kuwapasha habari makuhani na kuongeza kwenye habari moja uongo 100 kutoka kwao”. [Al-Bukhaariy: (3210)]
Abu Hurayrah: “Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إذا قالَ أحَدُكُمْ: آمِينَ، وقالتِ المَلائِكَةُ في السَّماءِ: آمِينَ، فَوافَقَتْ إحْداهُما الأُخْرَى غُفِرَ له ما تَقَدَّمَ مِن ذَنْبِهِ"
“Akisema mmoja wenu aamiyn, na Malaika mbinguni wakasema aamiyn, na aamiyn zote mbili zikakutana, basi husamehewa dhambi zake zilizotangulia”. [Hadiyth Swahiyh: Al-Bukhaariy (781) na Muslim (410)]
Ibn Kathiyr amesema: “Hakuna mahala popote katika mbingu saba isipokuwa wako Malaika. Kati yao wako walio simama daima, wako walio rukuu daima, na wako wenye kusujudu daima, na wako wengine wa aina nyingine ambao Allaah Pekee Ndiye Anaowajua”.
As-Suyuwtwiy amesema: “Mbingu ndio makazi yao na mahala pao kama yalivyo mabustani mazuri kwa upande wa ardhi”.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
27: Idadi Ya Malaika
Idadi ya Malaika ni kubwa mno na hakuna ajuaye idadi hiyo isipokuwa Allaah Ta’aalaa. Allaah Ta’aalaa Anasema:
"وَمَا يَعْلَمُ جُنُودَ رَبِّكَ إِلَّا هُوَ ۚ وَمَا هِيَ إِلَّا ذِكْرَىٰ لِلْبَشَرِ"
“Na hakuna ajuaye majeshi ya Rabb wako isipokuwa Yeye Pekee. Na haya si chochote isipokuwa ni ukumbusho kwa binaadamu”. [Al-Muddath-thir: 31]
Kila aliyebaleghe anao Malaika wawili wa kusajili matendo yake mema na mabaya, mbali na wale wanaomlinda mtu asipatikane na dhara lolote ambalo Allaah Hakumwandikia. Isitoshe, kuna wale wanaozunguka huku na kule kutafuta vikao vya kiilmu vya Waumini na kuvihudhuria, na wengineo wengi tu.
Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimuuliza Jibriyl (‘alayhis salaam) kuhusu Al-Bayt Al-Ma’amuwr. Jibriyl akamwambia:
"هَذَا الْبَيْتُ الْمَعْمُورُ يَدْخُلُهُ كُلَّ يَوْمٍ سَبْعُونَ أَلْفَ مَلَكٍ إِذَا خَرَجُوا مِنْهُ لَمْ يَعُودُوا فِيهِ آخِرُ مَا عَلَيْهِمْ"
“Al-Bayt Al-Ma’amuwr hii, wanaswali ndani yake kila siku Malaika elfu 70, na wanapotoka hawarudi tena”. [Al-Bukhaariy (3207) na Muslim (164)]
Ikiwa kila siku wanaingia kwa idadi hiyo na hawarudi tena baada ya kutoka, watakuwa ni kiasi gani toka wameanza kuingia hadi Qiyaamah!
Katika yanayoonyesha wingi wao, ni yale yaliyosimuliwa na ‘Abdullaah bin Mas-‘uwd (Radhwiya Allaah ‘anhu) toka kwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"يُؤْتَى بجهَنَّمَ يَوْمَئذٍ لَهَا سَبْعُوْنَ ألفَ زِمامٍ، مَعَ كُلِّ زِمَامٍ سَبْعُوْنَ ألفَ مَلَكٍ يجرُّونَها"
“Italetwa Siku hiyo Jahannam ikiwa na hatamu elfu sabini, kila hatamu imekamatwa na Malaika elfu 70 wanaikokota”. [Muslim (2842)]
Kwa hesabu ya haraka haraka, idadi ya Malaika hao itakuwa ni bilioni 4 milioni 900, yaani 70,000 X 70,000 = 4,900,000,000. Hao pengine kazi yao ni hiyo tu kwa siku hiyo ya Qiyaamah.
Ibn Taymiyyah amesema: “Hakuna awezaye kukokotoa idadi ya Malaika isipokuwa Allaah Pekee. Aayaat za Qur-aan na Hadiyth za Rasuli zinazozungumzia majukumu wanayoyasimamia Malaika kwa mwanadamu, zinaonyesha namna walivyo wengi. Kuna Malaika mwenye jukumu la tone la uzazi, Malaika wawili wa kuandika matendo ya kila mwanadamu, Malaika wa kumlinda, Qarinu wa Kimalaika wa kumwongoza na kumwelekeza, na wengineo na wengineo.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
28: Je, Malaika Wanakufa?
‘Aqiydah ya Ahlus Sunnat wal Jama’a inaeleza kwamba Allaah ‘Azza wa Jalla Ameandika mauti kwa viumbe vyote hai, na Yeye Pekee Ndiye Atakayebakia. Na juu ya msingi huu, wanaamini kwamba Malaika inajuzu kwao kupatwa na umauti, na Allaah Ana uwezo wa hilo. Allaah Anasema:
"كُلُّ مَنْ عَلَيْهَا فَانٍ ● وَيَبْقَىٰ وَجْهُ رَبِّكَ ذُو الْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ"
“Kila aliyekuwa juu yake ni mwenye kutoweka ● Na utabakia Wajihi wa Rabb wako Mwenye Ujalali na Ukarimu”. [Ar-Rahmaan: 26-27]
Ibn Kathiyr amesema: “Allaah Anaeleza hapa kwamba wakazi wote wa ardhi wataondoka na watakufa wote, na pia vile vile wakazi wa mbinguni isipokuwa wale tu ambao Allaah Atataka wabakie. Na hatobaki yeyote isipokuwa Wajihi Wake Mtukufu, kwa kuwa Rabbi Aliyetukuka Hafi, bali Yeye Ndiye Aliye Hai Ambaye Hafi milele.
Ibn Taymiyah aliulizwa: Je viumbe vyote wakiwemo Malaika watakufa? Akajibu: “Ambalo watu wengi wanaliamini ni kwamba viumbe wote wanakufa na hata Malaika. Waislamu, Mayahudi na Manaswara wanakubaliana uwezekano wa hilo na uwezo wa Allaah wa kulitenda. Allaah Ana uwezo wa kuwafisha kisha kuwahuisha kama Alivyo na uwezo wa kuwafisha wanadamu na majini kisha Akawahuisha tena. Allaah Ta’aalaa Amesema:
"وَهُوَ الَّذِي يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ وَهُوَ أَهْوَنُ عَلَيْهِ"
“Naye Ndiye Anayeanzisha uumbaji, kisha Anaurudisha, nayo ni sahali mno Kwake”. [Ar-Ruwm: 27]
As Suyuwtwiy amesema: “Niliulizwa: Je, Malaika watakufa kwa mpulizo wa kwanza wa baragumu, na watafufuka kwa mpulizo wa pili? Nikajibu: Ndio”.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
29: Malaika Ni Waja Wa Allaah Na Hawana Sifa Za Kiola
Malaika ni waja wa Allaah na hawana sifa zozote za kimola au kiungu, nao wanamwogopa Allaah ukweli wa kumwogopa. Allaah Ta’alaa Anasema:
"مَا كَانَ لِبَشَرٍ أَن يُؤْتِيَهُ اللَّـهُ الْكِتَابَ وَالْحُكْمَ وَالنُّبُوَّةَ ثُمَّ يَقُولَ لِلنَّاسِ كُونُوا عِبَادًا لِّي مِن دُونِ اللَّـهِ وَلَـٰكِن كُونُوا رَبَّانِيِّينَ بِمَا كُنتُمْ تُعَلِّمُونَ الْكِتَابَ وَبِمَا كُنتُمْ تَدْرُسُونَ ● وَلَا يَأْمُرَكُمْ أَن تَتَّخِذُوا الْمَلَائِكَةَ وَالنَّبِيِّينَ أَرْبَابًا ۗ أَيَأْمُرُكُم بِالْكُفْرِ بَعْدَ إِذْ أَنتُم مُّسْلِمُونَ"
“Ni mustahili kwa mtu kwamba Allaah Amempa Kitabu na Al-Hukma na Unabii kisha aje awaambie watu: Kuweni wenye kuniabudu mimi badala ya Allaah, bali (atawaambia): Kuweni Wanachuoni waswalihina kwa yale mliyokuwa mkiyafundisha ya Kitabu na kwa yale mliyokuwa mkiyadurusu. ● Na wala hakuamuruni kuwachukua Malaika na Manabii kuwafanya miola. Je, anakuamrisheni ukafiri baada ya nyinyi kuwa mmejisalimisha kwa Allaah?” [Aal ‘Imraan: 79-80]
Hapa Allaah Ta’aalaa Anabainisha kwamba kuwafanya Malaika na Mitume waola ni kufru. Na yeyote atakayewafanya Malaika au Mitume hivyo, akawaomba wamletee manufaa au wamwondoshee madhara, au wamsamehe dhambi zake, au waongoe moyo wake au wamsaidie kumletea faraja kwa misukosuko inayomkabili, basi mtu huyo ni kafiri kwa itifaki ya Waislamu.
Allaah Ta’alaa Anasema:
"وَقَالُوا اتَّخَذَ الرَّحْمَـٰنُ وَلَدًا ۗ سُبْحَانَهُ ۚ بَلْ عِبَادٌ مُّكْرَمُونَ ● لَا يَسْبِقُونَهُ بِالْقَوْلِ وَهُم بِأَمْرِهِ يَعْمَلُونَ ● يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَلَا يَشْفَعُونَ إِلَّا لِمَنِ ارْتَضَىٰ وَهُم مِّنْ خَشْيَتِهِ مُشْفِقُونَ ● وَمَن يَقُلْ مِنْهُمْ إِنِّي إِلَـٰهٌ مِّن دُونِهِ فَذَٰلِكَ نَجْزِيهِ جَهَنَّمَ ۚ كَذَٰلِكَ نَجْزِي الظَّالِمِينَ"
“Na wakasema: Ar-Rahmaan Amejifanyia mwana! Subhaanah! Utakasifu ni Wake! Bali (hao) ni waja waliokirimiwa ● Hawamtangulii (Allaah) kwa kauli, nao kwa Amri Yake wanatenda ● Anajua yale yaliyoko mbele yao, na yale yaliyoko nyuma yao, na wala hawataomba shafaa’ah (yeyote) isipokuwa kwa yule ambaye (Allaah) Amemridhia, nao kutokana na kumkhofu, ni wenye khofu na kutahadhari ● Na yeyote yule miongoni mwao atakayesema: Mimi ni mwabudiwa badala Yake, basi huyo Tutamlipa Jahannam. Hivyo ndivyo Tunavyolipa madhalimu”. [Al-Anbiyaa: 26-29]
As- Sa’adiy amesema: “Allaah Ta’aalaa Anatueleza katika Aayaat hizi kuhusu sifa za Malaika. Anatuambia kwamba Malaika ni waja waliokirimiwa, na wao wanaendeshwa kama walivyo viumbe wote. Lakini pia ni viumbe waliotakaswa kutokana na machafu, wamefikia ukomo wa mwisho wa kumheshimu Allaah, nao wanatekeleza Maamrisho Yake yote. Hawasemi jambo lolote bila ya amri toka kwa Allaah na hawawezi kufanya lolote kwa utashi wao bila maelekezo toka kwa Allaah Ta’alaa”.
Hivyo basi, Malaika hawa ni sehemu ya viumbe wa Allaah walio chini ya mamlaka Yake. Hawana uwezo wa kufanya lolote ila lile tu walilowezeshwa na Allaah Ta’aalaa.
Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaah ‘anhumaa) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia Jibriyl:
"أَلاَ تَزُورُنَا أَكْثَرَ مِمَّا تَزُورُنَا؟ قَالَ: فَنَزَلَتْ: وَمَا نَتَنَزَّلُ إِلاَّ بِأَمْرِ رَبِّكَ لَهُ مَا بَيْنَ أَيْدِينَا وَمَا خَلْفَنَا"
“Mbona hututembelei zaidi ya unavyotutembelea? Hapo ikashuka Kauli Yake Taalaa:
“Na (sisi Malaika) hatuteremki ila kwa Amri ya Rabb wako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Ni Yake Yeye yaliyoko mbele yetu, na yaliyoko nyuma yetu". [Al-Bukhaariy (3218) na Muslim (3158)]
Malaika
Alhidaaya.com [3]
30: Aina Za Ibada Ambazo Malaika Wanazifanya
(1)- Kumsabbih Allaah
Allaah Ta’alaa Amesema:
"وَإِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَائِكَةِ إِنِّي جَاعِلٌ فِي الْأَرْضِ خَلِيفَةً ۖ قَالُوا أَتَجْعَلُ فِيهَا مَن يُفْسِدُ فِيهَا وَيَسْفِكُ الدِّمَاءَ وَنَحْنُ نُسَبِّحُ بِحَمْدِكَ وَنُقَدِّسُ لَكَ ۖ قَالَ إِنِّي أَعْلَمُ مَا لَا تَعْلَمُونَ"
“Na pale Rabb wako Alipowaambia Malaika: Hakika Mimi Nitaweka katika ardhi khalifa. Wakasema: Utaweka humo atakayefanya ufisadi humo na kumwaga damu, na hali sisi tunakusabihi kwa Himidi Zako na tunakutukuza kwa Utakatifu Wako? (Allaah) Akasema: Hakika Mimi Nayajua zaidi msiyoyajua". [Al-Baqarah: 30]
Na Anasema tena Akiwazungumzia Malaika wabebao ‘Arshi Yake:
"الَّذِينَ يَحْمِلُونَ الْعَرْشَ وَمَنْ حَوْلَهُ يُسَبِّحُونَ بِحَمْدِ رَبِّهِمْ وَيُؤْمِنُونَ بِهِ"
“(Malaika) ambao wanabeba ‘Arsh na walio pembezoni mwake, wanasabbih na kumhimidi Rabbi wao”. [Ghaafir: 07]
Malaika wote kiujumla wanamsabbih. Allaah Ta’aalaa Anasema:
"تَكَادُ السَّمَاوَاتُ يَتَفَطَّرْنَ مِن فَوْقِهِنَّ ۚ وَالْمَلَائِكَةُ يُسَبِّحُونَ بِحَمْدِ رَبِّهِمْ وَيَسْتَغْفِرُونَ لِمَن فِي الْأَرْضِ ۗ أَلَا إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ"
“Zinakaribia mbingu kuraruka moja juu ya nyingine, na ilhali Malaika wanasabbih na kumhimidi Rabb wao, na wanawaombea maghfirah walioko ardhini. Tanabahi! Hakika Allaah Ndiye Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu. [Ash-Shuwraa: 05]
Kumsabbih kwao Allaah ni jambo la kudumu, halisimami. Allaah ‘Azza wa Jalla Anasema:
"يُسَبِّحُونَ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ لَا يَفْتُرُونَ"
“Wanasabihi usiku na mchana, hawaishiwi nguvu”. [Al-Anbiyaa: 20]
As-Sa’adiy amesema: “Malaika wamezamia katika kumwabudu Allaah na kumsabbih katika wakati wao wote, hawana wakati wa faragha wala wa kupita bure, wako katika sifa hii pamoja na wingi wao. Na hii inabainisha Uadhwama wa Allaah, Utukufu wa Mamlaka Yake, ukamilifu wa Elimu Yake na Hikma Yake, na haya yanawajibisha asiabudiwe mwingine yoyote zaidi Yake”.
Abu Dharri (Radhwiya Allaah ‘anhu) amesema: “Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliulizwa: Ni maneno yepi yaliyo bora zaidi? Akasema:
"مَا اصْطَفَى اللَّهُ لِمَلاَئِكَتِهِ أَوْ لِعِبَادِهِ سُبْحَانَ اللَّهِ وَبِحَمْدِهِ " .
“Ni yale ambayo Allaah Amewachagulia Malaika Wake au Waja Wake, nayo ni: Subhaana Allaah wa bihamdihi. [Muslim (2731)]
Hadiyth hii inatukumbusha kwamba dhikri ya tasbiyh ndiyo iliyochaguliwa na Allaah kwa Malaika na sisi pamoja na vitu vyote Alivyoviumba Allaah ambavyo vyote hivyo vinamsabbih. Usije wewe ukawa nje ya duara hili. Allaah Anasema:
"تُسَبِّحُ لَهُ السَّمَاوَاتُ السَّبْعُ وَالْأَرْضُ وَمَن فِيهِنَّ ۚ وَإِن مِّن شَيْءٍ إِلَّا يُسَبِّحُ بِحَمْدِهِ وَلَـٰكِن لَّا تَفْقَهُونَ تَسْبِيحَهُمْ ۗ إِنَّهُ كَانَ حَلِيمًا غَفُورًا"
“Zinamsabihi mbingu saba na ardhi na waliomo humo. Na hakuna kitu chochote isipokuwa kinasabihi na kumhimidi Yeye, lakini hamzifahamu tasbiyh zao. Hakika Yeye Ni Mvumilivu, Mwingi wa Kughufuria”. [Al-Israa: 44]
Malaika
Alhidaaya.com [3]
31: Aina Za Ibada Ambazo Malaika Wanazifanya
(2)- Kupanga Safu Zilizonyooka Kwa Ajili Ya Ibada
Allaah Ta’aalaa Anasema Akiizungumzia kauli ya Malaika Wake:
"وَإِنَّا لَنَحْنُ الصَّافُّونَ"
“Na hakika sisi bila shaka ni wenye kujipanga safu safu (kwa ‘ibaadah)”. [As-Swaaffaat: 165]
Malaika hawa hujipanga safu huko mbinguni, safu zilizonyooka barabara, baadhi yao pembeni ya wengine kwa ajili ya kumwabudu Allaah ikiwa ni pamoja na swalah na ibada nyinginezo.
Toka kwa Jaabir bin Samurah (Radhwiya Allaah ‘anhu) kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
" أَلاَ تَصُفُّونَ كَمَا تَصُفُّ الْمَلاَئِكَةُ عِنْدَ رَبِّهِمْ؟ قَالُوا: وَكَيْفَ تَصُفُّ الْمَلاَئِكَةُ عِنْدَ رَبِّهِمْ؟ قَالَ: يُتِمُّونَ الصَّفَّ الأَوَّلَ ثُمَّ يَتَرَاصُّونَ فِي الصَّفِّ"
“Kwa nini msipange safu kama wanavyopanga safu Malaika kwa Mola wao? Tukasema: Ee Rasuli wa Allaah, vipi Malaika wanapanga safu kwa Mola wao? Akasema: Wanakamilisha safu baada ya safu, na wanajipanga vizuri bila kuacha pengo katika safu”. [Swahiyh Ibn Maajah (818)]
Kunyoosha safu kunakuwa ndio ukamilifu na utimilifu wa swalaah kwa Waislamu wanaposwali kama alivyoamuru Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Jambo hili pia ni katika mambo bora tuliyohusishwa nayo sisi Umma wa Muhammad (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anasema:
"فُضِّلْنَا عَلَى النَّاسِ بِثَلَاثٍ جُعِلَتْ صُفُوفُنَا كَصُفُوفِ الْمَلَائِكَةِ وَجُعِلَتْ لَنَا الْأَرْضُ كلهَا مَسْجِدا وَجعلت تربَتهَا لنا طَهُورًا إِذَا لَمْ نَجِدِ الْمَاء"َ
“Tumefanywa bora kuliko umma zilizotangulia kwa mambo matatu: Safu zetu zimefanywa kama safu za Malaika, na ardhi yote imefanywa kwetu kuwa sehemu ya kuswalia, na mchanga wake umefanywa kitwaharishio chetu tukikosa maji”. [Muslim (526)]
Malaika
Alhidaaya.com [3]
32: Aina Za Ibada Ambazo Malaika Wanazifanya
(3)- Kutufu Al-Baytul Ma’amuwr
Nyumba hii Allaah Ameiapia Aliposema:
"وَالْبَيْتِ الْمَعْمُورِ"
“Na Naapa kwa Nyumba yenye kuamiriwa nyakati zote (na Malaika)”. [At-Tuwr: 04]
Al-Baghawiy amesema: “Nyumba hii iko katika mbingu ya saba na imeitwa hivi kutokana na wingi wa Malaika wanaoikusudia. Iko mkabala na Al-Ka’abah kiwima, na utukuzo wake mbinguni ni sawa na utukuzo wa Al-Ka’abah hapa ardhini, na kila siku wanaingia humo Malaika elfu 70 kwa ajili ya kutufu na kuswali humo, kisha hawarudi tena humo milele”.
Imepokelewa toka kwa Maalik bin Swa-‘aswa-’ah kuhusiana na kisa cha Israa kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"رُفِعَ لِيَ الْبَيْتُ الْمَعْمُورُ فَقُلْتُ: يَا جِبْرِيلُ مَا هَذَا؟ قَالَ: هَذَا الْبَيْتُ الْمَعْمُورُ يَدْخُلُهُ كُلَّ يَوْمٍ سَبْعُونَ أَلْفَ مَلَكٍ إِذَا خَرَجُوا مِنْهُ لَمْ يَعُودُوا فِيهِ آخِرُ مَا عَلَيْهِمْ"
“Nilinyanyuliwa Al-Baytul Al-Ma-‘amuwr nikasema: Ee Jibriyl, nini hii? Akasema: Hii ni Al-Baytul Ma-‘amuwr, kila siku wanaingia ndani yake Malaika elfu sabini, na wakitoka humo hawarudi tena hadi wa mwisho wao”.
Imepokelewa pia toka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaah ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akizungumzia kisa cha Israa amesema:
"ففُتِح لنا فإذا أنا بإبراهيمَ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم مُسنِدًا ظَهْرَه إلى البيتِ المعمورِ، وإذا هو يدخُلُه كلَّ يومٍ سبعون ألْفَ مَلَكٍ لا يعودون إليه"
“Tukafunguliwa (mbingu), na hapo nikamkuta Ibraahiym (‘Alayhis Salaam) akiwa ameegemeza mgongo wake kwenye Al-Baytul Ma’amuwr ambayo wanaingia humo kila siku Malaika elfu sabini na hawarudi tena humo”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Ahmad (14082), Ibn Abiy Shaybah katika Al-Muswannaf (17883) na Abu Ya’alaa (3373)]
Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimkuta Nabiy Ibraahiym (‘alayhis salaam) katika hali hiyo kwa kuwa yeye ndiye aliyeijenga Al-Ka’abah ya hapa ardhini, na hayo ndiyo malipo yake, kwani malipo ni kwa mujibu wa matendo.
As-Sam-’aaniy amesema: “Kauli maarufu ni kwamba hiyo ni Nyumba iliyoko mbinguni. Limesemwa hili na Ibn ‘Abbaas na Mufassiruna wote, pia limehadithiwa toka kwa ‘Aliyy bin Abiy Twaalib (Radhwiya Allaah ‘anhu)”.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
33: Aina Za Ibada Ambazo Malaika Wanazifanya
(4)- Kumwogopa Allaah
Malaika wanamwogopa na kumkhofu sana Allaah, wao wanamjua Allaah vyema na wanamwadhimisha mno. Allaah Akiwazungumzia Anasema:
"يَخَافُونَ رَبَّهُم مِّن فَوْقِهِمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ"
“Wanamkhofu Rabb wao Aliye juu yao, na wanafanya yale wanayoamrishwa”. [An-Nahl: 50]
Anasema tena:
"يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَلَا يَشْفَعُونَ إِلَّا لِمَنِ ارْتَضَىٰ وَهُم مِّنْ خَشْيَتِهِ مُشْفِقُونَ"
“Anajua yale yaliyoko mbele yao, na yale yaliyoko nyuma yao, na wala hawataomba shafaa’ah (yeyote) isipokuwa kwa yule ambaye (Allaah) Amemridhia, nao kutokana na kumkhofu, ni wenye khofu na kutahadhari”. [Al-Anbiyaa: 28]
Anasema pia:
"وَلَا تَنفَعُ الشَّفَاعَةُ عِندَهُ إِلَّا لِمَنْ أَذِنَ لَهُ ۚ حَتَّىٰ إِذَا فُزِّعَ عَن قُلُوبِهِمْ قَالُوا مَاذَا قَالَ رَبُّكُمْ ۖ قَالُوا الْحَقَّ ۖ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْكَبِيرُ"
“Na wala haitofaa shafaa’ah (uombezi) mbele Yake isipokuwa kwa yule Aliyempa idhini. Mpaka litakapoondolewa fazaiko nyoyoni mwao husema: Amesema nini Rabb wenu? Watasema: Ya haki, Naye Ni Mwenye ‘Uluwa, Mkubwa wa dhati, vitendo na sifa”. [Sabaa: 23]
Ibn Kathiyr amesema: “Hili pia ni daraja la juu kabisa katika uadhwama, nayo ni kwamba Allaah Ta’aalaa Anapotamka wahyi, Malaika husikia Maneno Yake na hupatwa na mshtuko mkubwa unaofuatiwa na mfano wa kifo kutokana na kumwogopa Allaah”. Tamko hili limesemwa vile vile na Ibn Mas-‘uwd, Masruwq na wengineo.
Toka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaah ‘anhu): Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إِذَا قَضَى اللَّهُ فِي السَّمَاءِ أَمْرًا ضَرَبَتِ الْمَلاَئِكَةُ بِأَجْنِحَتِهَا خُضْعَانًا لِقَوْلِهِ كَأَنَّهُ سِلْسِلَةٌ عَلَى صَفْوَانٍ فَإِذَا فُزِّعَ عَنْ قُلُوبِهِمْ قَالُوا مَاذَا قَالَ رَبُّكُمْ قَالُوا الْحَقَّ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْكَبِيرُ"
“Allaah Anapopitisha amri mbinguni, Malaika Hupiga mbawa zao kwa ajili ya kulitii Neno Lake ambalo ni kama sauti ya mnyororo (unaoburutwa) juu ya mwamba. Na fazaiko linapoondoka nyoyoni mwao huuliza: Nini Amesema Mola wenu? (Malaika wabebao ‘Arshi) hujibu: Ni haki, Naye Ni Mwenye ‘Uluwa, Mkubwa wa dhati, vitendo na sifa”. [Hadiyth Swahiyh. Al-Bukhaariy (4800)].
Malaika
Alhidaaya.com [3]
34: Malaika Wana Sifa Ya Kuona Haya
Malaika wana hisia ya kuona haya. Hadiyth hii ya ‘Aaishah (Radhwiya Allaah ‘anhaa) inathibitisha:
"أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ جَالِسًا كَاشِفًا عَنْ فَخِذِهِ ، فَاسْتَأْذَنَ أَبُو بَكْرٍ فَأَذِنَ لَهُ وَهُوَ عَلَى حَالِهِ ، ثُمَّ اسْتَأْذَنَ عُمَرُفَأَذِنَ لَهُ وَهُوَ عَلَى حَالِهِ ، ثُمَّ اسْتَأْذَنَ عُثْمَانُ فَجَلَسَ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم وَسَوَّى ثِيَابَهُ ، فَلَمَّا خَرَجَ قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللهِ، دَخَلَ أَبُو بَكْرٍ فَلَمْ تَهَشَّ وَلَمْ تُبَالِهِ، ثُمَّ دَخَلَ عُمَرُ فَلَمْ تَهَشَّ وَلَمْ تُبَالِهِ، ثُمَّ دَخَلَ عُثْمَانُ فَجَلَسْتَ وَسَوَّيْتَ ثِيَابَكَ؟ قَالَ: أَلاَ أَسْتَحِي مِنْ رَجُلٍ تَسْتَحِي مِنْهُ الْمَلاَئِكَةُ؟"
“Kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa ameketi huku akiwa amelifunua paja lake. Abu Bakr akapiga hodi, akamruhusu kuingia akiwa hivyo hivyo (akazungumza naye halafu akatoka). Kisha ‘Umar naye akapiga hodi, akamruhusu kuingia akiwa hivyo hivyo (akazungumza naye kisha akatoka). Halafu ‘Uthmaan akapiga hodi, na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaketi sawa, akaiweka vizuri nguo yake. Alipoondoka nilimuuliza: Ee Rasuli wa Allaah! Abu Bakr ameingia, ukabaki ulivyokuwa wala hukujali, kisha ‘Umar akaingia, ukabaki hivyo hivyo, lakini ‘Uthmaan alipoingia, uliketi sawa na kuiweka vizuri nguo yako. Akasema: “Iwaje nisimwonee haya mtu ambaye Malaika wanamwonea haya?!” [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (2401)].
Malaika
Alhidaaya.com [3]
35: Malaika Ni Wajuzi Wa Kutekeleza Kazi Zao
Malaika wana elimu na ujuzi wa mambo mbalimbali kwa mujibu wa kazi wanazokalifishwa na Allaah Ta’alaa. Allaah Ta’aalaa Anasema:
وَعَلَّمَ آدَمَ الْأَسْمَاءَ كُلَّهَا ثُمَّ عَرَضَهُمْ عَلَى الْمَلَائِكَةِ فَقَالَ أَنبِئُونِي بِأَسْمَاءِ هَـٰؤُلَاءِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ● قَالُوا سُبْحَانَكَ لَا عِلْمَ لَنَا إِلَّا مَا عَلَّمْتَنَا ۖ إِنَّكَ أَنتَ الْعَلِيمُ الْحَكِيمُ"
“Na Akamfunza Aadam majina yote (ya kila kitu), kisha Akavionesha mbele ya Malaika; Akasema: Niambieni majina ya hivi mkiwa ni wakweli ● Wakasema: Utakasifu ni Wako, hatuna elimu isipokuwa Uliyotufunza, hakika Wewe Ni Mjuzi wa yote, Mwenye hikmah wa yote”. [Al-Baqarah: 31-32]
Allaah Ta’aalaa Amewafunulia baadhi ya Malaika Wake elimu ambayo wanaihitaji katika majukumu Aliyowabebesha kama Malaika wanaosajili matendo ya binadamu. Malaika hawa ni lazima wayajue matendo yote mema na mabaya yanayomhusu mwanadamu pamoja na vipimo vyake, matamshi yao, mienendo yao na kadhalika. Ni lazima pia wajue lugha ili waweze kupambanua kati ya mema wanayoyasema watu au mabaya. Allaah Ta’alaa Anasema:
"وَإِنَّ عَلَيْكُمْ لَحَافِظِينَ ● كِرَامًا كَاتِبِينَ ● يَعْلَمُونَ مَا تَفْعَلُونَ"
“Na hakika juu yenu bila shaka kuna wenye kuhifadhi (na kuchunga) ● Watukufu wanaoandika (amali). Wanajua yale myafanyayo”. [Al-Infitwaar: 10-12]
Malakul Mawt (Malaika wa kutoa roho) anajua wakati, saa, dakika, sekunde ya kuitoa roho ya kiumbe na mahala pa kufia kiumbe hicho. Kadhalika, ana utaalamu wa kibobezi wa kuitoa roho ya kafiri na roho ya Muislamu, kwani kuna tofauti kati ya roho mbili hizi, pamoja na viumbe vinginevyo. Allaah Ta’aalaa Anatuambia:
"قُلْ يَتَوَفَّاكُم مَّلَكُ الْمَوْتِ الَّذِي وُكِّلَ بِكُمْ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّكُمْ تُرْجَعُونَ"
“Sema: Atakufisheni Malaika wa mauti ambaye amewakilishwa kwenu, kisha kwa Rabb wenu mtarejeshwa”. [As-Sajdah: 11]
Malaika
Alhidaaya.com [3]
36: Malaika Wanazungumza
Allaah Ta’alaa Amesema:
"وَإِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَائِكَةِ إِنِّي جَاعِلٌ فِي الْأَرْضِ خَلِيفَةً ۖ قَالُوا أَتَجْعَلُ فِيهَا مَن يُفْسِدُ فِيهَا وَيَسْفِكُ الدِّمَاءَ وَنَحْنُ نُسَبِّحُ بِحَمْدِكَ وَنُقَدِّسُ لَكَ ۖ قَالَ إِنِّي أَعْلَمُ مَا لَا تَعْلَمُونَ ● وَعَلَّمَ آدَمَ الْأَسْمَاءَ كُلَّهَا ثُمَّ عَرَضَهُمْ عَلَى الْمَلَائِكَةِ فَقَالَ أَنبِئُونِي بِأَسْمَاءِ هَـٰؤُلَاءِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ● قَالُوا سُبْحَانَكَ لَا عِلْمَ لَنَا إِلَّا مَا عَلَّمْتَنَا ۖ إِنَّكَ أَنتَ الْعَلِيمُ الْحَكِيمُ"
“Na pindi Rabb wako Alipowaambia Malaika: Hakika Mimi Nitaweka katika ardhi khalifa. Wakasema: Utaweka humo atakayefanya ufisadi humo na kumwaga damu, na hali sisi tunakusabihi kwa Himidi Zako na tunakutukuza kwa Utakatifu Wako? (Allaah) Akasema: Hakika Mimi Nayajua zaidi msiyoyajua ● Na Akamfunza Aadam majina yote (ya kila kitu), kisha Akavionesha mbele ya Malaika; Akasema: Niambieni majina ya hivi mkiwa ni wakweli ● Wakasema: Utakasifu ni Wako hatuna elimu isipokuwa Uliyotufunza; hakika Wewe Ni Mjuzi wa yote, Mwenye hikmah wa yote”. [Al-Baqarah: 30-32]
Hapa, Malaika hawa walikuwa wanazungumza na Allaah Ta’alaa. Malaika hawa pia wanazungumza wao kwa wao, na Allaah Pekee Ndiye Ajuaye lugha yao hiyo. Allaah Ta’aalaa Anatuambia tena:
"حَتَّىٰ إِذَا فُزِّعَ عَن قُلُوبِهِمْ قَالُوا مَاذَا قَالَ رَبُّكُمْ ۖ قَالُوا الْحَقَّ ۖ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْكَبِيرُ"
“Mpaka litakapoondolewa fazaiko nyoyoni mwao watasema (Malaika): Amesema nini Rabb wenu? Watasema: Ya haki, Naye Ni Mwenye ‘Uluwa, Mkubwa wa dhati, vitendo na sifa”. [As-Sajdah: 23]
Ibn ‘Uthaymiyn amesema: “Aayah hii inatuthibitishia kwamba Malaika wanazungumza, wanafahamu na wana akili. Tunaona kwenye aayah hii baadhi wanauliza wengine kuhusu maneno Aliyoyasema Allaah, na wengine wanajibu kuwa Amesema haki. Hii ni kinyume na wale wanaodai kwamba Malaika hawana sifa hiyo, na kwa madai yao hayo itakuwa na maana kwamba sisi tumepokea sharia ya dini na mengineyo kutoka kwa viumbe wasio na akili. Na hii bila shaka ni kuitia dosari sharia, na jambo lisiloingia akilini”.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
37: Malaika Wamejipanga Vizuri Katika Mambo Yao Yote
Malaika wanatekeleza majukumu yao wakiwa wamejipanga vyema. Malaika hawa watakuja Siku ya Qiyaamah wakiwa wamejipanga safu kwa safu zilizonyooka barabara. Allaah Ta’aalaa Anatuambia:
"وَجَاءَ رَبُّكَ وَالْمَلَكُ صَفًّا صَفًّا"
“Na Atakapokuja Rabb wako pamoja na Malaika walio safusafu”. [Al-Fajr: 22]
Wanapofanya ibada, pia vile vile hunyoosha safu zao bila kuacha hata mwanya kidogo. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
" أَلاَ تَصُفُّونَ كَمَا تَصُفُّ الْمَلاَئِكَةُ عِنْدَ رَبِّهِمْ؟ قَالُوا: وَكَيْفَ تَصُفُّ الْمَلاَئِكَةُ عِنْدَ رَبِّهِمْ؟ قَالَ: يُتِمُّونَ الصَّفَّ الأَوَّلَ ثُمَّ يَتَرَاصُّونَ فِي الصَّفِّ"
“Kwa nini msipange safu kama wanavyopanga safu Malaika kwa Mola wao? Tukasema: Ee Rasuli wa Allaah, vipi Malaika wanapanga safu kwa Mola wao? Akasema: Wanakamilisha safu baada ya safu, na wanajipanga vizuri bila kuacha pengo katika safu”. [Swahiyh Ibn Maajah (818)]
Na Siku ya Qiyaamah, Jibriyl (‘alayhis salaam) pamoja na Malaika wengine watasimama mbele ya Allaah kwa unyenyekevu na heshima ya hali ya juu kabisa wakiwa katika safu zilizonyooka barabara. Allaah Ta’aalaa Anasema:
"يَوْمَ يَقُومُ الرُّوحُ وَالْمَلَائِكَةُ صَفًّاۖ لَّا يَتَكَلَّمُونَ إِلَّا مَنْ أَذِنَ لَهُ الرَّحْمَـٰنُ وَقَالَ صَوَابًا"
“Siku atakayosimama Ruwh (Jibriyl) na Malaika safusafu. Hatozungumza isipokuwa yule ambaye Ar-Rahmaan Amempa idhini na atasema yaliyo sahihi”. [‘Amma: 38]
Mbali ya hivyo, Malaika wako makini sana katika utendaji wao wa kazi na katika kutekeleza maagizo ya Allaah Subhaanahu wa Ta’aalaa. Toka kwa Anas (Radhwiya Allaah ‘anhu):
"آتِي بَابَ الْجَنَّةِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَأَسْتَفْتِحُ، فَيَقُولُ الْخَازِنُ : مَنْ أَنْتَ؟ فَأَقُولُ مُحَمَّدٌ . فَيَقُولُ : بِكَ أُمِرْتُ لاَ أَفْتَحُ لأَحَدٍ قَبْلَكَ"
“Nitaujia mlango wa Pepo kisha nitabisha. Mlinzi wake atauliza: Ni nani wewe? Nitajibu: Muhammad. Atasema: Ni kwako tu nimeamuriwa, simfungulii yeyote kabla yako”. [Muslim: 197]
Malaika
Alhidaaya.co [3]m
38: Kazi Za Malaika
(1)- Jibriyl (‘alayhis salaam): Kumteremshia Qur-aan Tukufu Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
Huyu anajulikana kama “Ar Ruwhul Amiyn” au “Ruwhul Qudus”. Allaah Ta’alaa Anasema:
"وَإِنَّهُ لَتَنزِيلُ رَبِّ الْعَالَمِينَ ● نَزَلَ بِهِ الرُّوحُ الْأَمِينُ ● عَلَىٰ قَلْبِكَ لِتَكُونَ مِنَ الْمُنذِرِينَ ● بِلِسَانٍ عَرَبِيٍّ مُّبِينٍ"
“Na hakika hii (Qur-aan) ni Uteremsho wa Rabb wa walimwengu ● Ameiteremsha Ar-Ruwh (Jibriyl) mwaminifu ● Juu ya moyo wako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) ili uwe miongoni mwa waonyaji.● Kwa lugha ya Kiarabu bayana”. [Ash-Shu’araa: 192-195]
"قُلْ نَزَّلَهُ رُوحُ الْقُدُسِ مِن رَّبِّكَ بِالْحَقِّ لِيُثَبِّتَ الَّذِينَ آمَنُوا وَهُدًى وَبُشْرَىٰ لِلْمُسْلِمِينَ"
“Sema: Ameiteremsha Ruwhul-Qudus (Jibriyl) kutoka kwa Rabb wako kwa haki ili iwathibitishe wale walioamini, na ni mwongozo na bishara kwa Waislamu”. [An-Nahl: 102)]
Ibn ‘Atwiyyah amesema: “Allaah Ta’aalaa Amemwamuru Mtume Wake aeleze kwamba Qur-aan hii kwa aayaat zake zenye kufuta na zenye kufutwa, kwa hakika Aliyeiteremsha ni Jibriyl (‘Alayhis Salaam), naye ndiye Ruwhul Qudus, na hakuna mvutano wowote kuhusu hili”.
Na Allaah Ta’alaa Ameendelea kusema:
"إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ ●عَلَّمَهُ شَدِيدُ الْقُوَىٰ ● ذُو مِرَّةٍ فَاسْتَوَىٰ"
“Hayo si chochote isipokuwa ni Wahy unaofunuliwa ● Amemfunza (Jibriyl) mwenye nguvu shadidi ● Mwenye muonekano jamili, muruwa na nguvu na kisha akalingamana sawasawa”. [An-Najm: 4-6]
Na Anasema tena:
"إِنَّهُ لَقَوْلُ رَسُولٍ كَرِيمٍ ● ذِي قُوَّةٍ عِندَ ذِي الْعَرْشِ مَكِينٍ ● مُّطَاعٍ ثَمَّ أَمِينٍ"
“Hakika hii (Qur-aan) bila shaka ni kauli (ameifikisha) Mjumbe mtukufu (Jibriyl) ● Mwenye nguvu na cheo kitukufu kwa (Allaah) Anayemiliki ‘Arsh ● Anayetiiwa (na Malaika), mwaminifu huko (mbinguni)”. [At-Takwiyr: 19-21]
Ibn Al-Qayyim amesema: “Allaah Subhaanahu wa Ta’alaa Amemsifu kwa sifa njema kabisa mja Wake Jibriyl katika Qur-aan. Amemweleza kama ni Mjumbe Wake, anaheshimika heshima kubwa Kwake, ana nguvu na hadhi kubwa mbele Yake, anatiiwa na kusikilizwa huko mbinguni, na yeye ndiye mbeba dhamana ya wahyi”.
Ibn Kathiyr naye kasema: “Neno Lake: “Ni kauli ya Mjumbe Mtukufu (Jibriyl)” lina maana: Hakika Qur-aan hii imefikishwa na Mjumbe mwenye heshima kubwa, naye ni Malaika mwenye umbo zuri na mwonekano wa kupendeza, na Malaika huyu ni Jibriyl (‘alayhis salaam).
Hizi ndizo baadhi ya sifa za Malaika Jibriyl (‘alayhis salaam) kama Alivyosifiwa na Allaah Ta’aalaa pamoja na jukumu lake la kumteremshia Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Qur-aan Tukufu. Na hapa kuna Jibriyl Mtukufu anayeiteremsha Qur-aan, kuna Rasuli Mtukufu (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na Qur-aan Tukufu. Ni utukufu juu ya utukufu.
Mbali na kumteremshia Rasuli Qur-aan, Jibriyl (‘alayhis salaam) alikuwa akiteremka kuja kwa Rasuli kwa ajili ya kujibu maswali ya waulizaji, kumsomesha Rasuli Qur-aan na hususan katika Mwezi wa Ramadhaan, na mengineyo.
Toka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaah ‘anhu) kwamba:
"سَمِعَ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ سَلاَمٍ، بِقُدُومِ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَهْوَ فِي أَرْضٍ يَخْتَرِفُ، فَأَتَى النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ إِنِّي سَائِلُكَ عَنْ ثَلاَثٍ لاَ يَعْلَمُهُنَّ إِلاَّ نَبِيٌّ فَمَا أَوَّلُ أَشْرَاطِ السَّاعَةِ وَمَا أَوَّلُ طَعَامِ أَهْلِ الْجَنَّةِ وَمَا يَنْزِعُ الْوَلَدُ إِلَى أَبِيهِ أَوْ إِلَى أُمِّهِ قَالَ " أَخْبَرَنِي بِهِنَّ جِبْرِيلُ آنِفًا".
“Kwamba Abdullaah bin Salaam alisikia kwamba Rasuli wa Allaah ((Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) yuko njiani anakuja Madiynah, na yeye alikuwa shambani kwake akivuna matunda. Akamwendea Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) (baada ya kuwasili) akamwambia: Nitakuuliza maswali matatu ambayo hajui majibu yake yeyote isipokuwa Nabiy. Ni ipi alama ya kwanza ya Qiyaamah? Ni kipi chakula cha kwanza cha watu wa Peponi? Kipi kinachosababisha mtoto kufanana na baba yake au mama yake? Rasuli akamwambia: Jibriyl amenieleza majibu ya hayo muda si mrefu uliopita”. [Al-Bukhaariy: (3329)]
Abu Dharri Al-Ghiffaariy (Radhwiya Allaah ‘anhu):
" أَتَانِي جِبْرِيلُ - عَلَيْهِ السَّلاَمُ - فَبَشَّرَنِي أَنَّهُ مَنْ مَاتَ مِنْ أُمَّتِكَ لاَ يُشْرِكُ بِاللَّهِ شَيْئًا دَخَلَ الْجَنَّةَ. قُلْتُ: وَإِنْ زَنَى وَإِنْ سَرَقَ . قَالَ : وَإِنْ زَنَى وَإِنْ سَرَقَ"
Kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Jibrily alinijia na kunipa habari ya kufurahisha kwamba yeyote katika umma wako atakayekufa hali ya kuwa hamshirikishi Allaah na chochote ataingia Peponi. Nikamuuliza: Na hata kama ameiba, na hata kama amezini!. Akasema: Hata kama ameiba, hata kama amezini”. [Al-Bukhaariy (1237) na Muslim (94)]
Malaika
Alhidaaya.com [3]
39: Kazi Za Malaika:
(2)- Miykaaiyl (‘alayhis salaam): Anasimamia Mawingu Ya Kuleta Mvua Na Mimea:
‘Ulamaa wengi wameeleza kwamba Malaika aliyepewa jukumu la kuendesha mawingu ya mvua na kuyapeleka pale ambapo Allaah Anamwamuru, ni Miykaaiyl (‘alayhis salaam). Wamesema hivyo kwa kutegemea Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Abbaas (Radhwiya Allaah ‘anhumaa) aliyesema:
"أقبلَتْ يهودُ إلى رَسولِ اللهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم فقالوا: يا أبا القاسِمِ، إنَّا نسألُك عن خمسةِ أشياءَ، فإن أنبَأْتَنا بهِنَّ عرَفْنا أنَّك نبيٌّ واتَّبَعْناك، فأخَذ عليهم ما أخَذ إسرائيلُ على بَنِيه؛ إذ قالوا: اللهُ عَلَى مَا نَقُولُ وَكِيلٌ، قال: هاتوا، قالوا:... ليس من نبيٍّ إلَّا له مَلَكٌ يأتيه بالخبَرِ، فأخبِرْنا مَن صاحِبُك؟ قال: جبريلُ [18] عليه السَّلامُ، قالوا: جِبريلُ [18]! ذاك الذي يَنزِلُ بالحَرْبِ والقِتالِ والعَذابِ، عَدُوُّنا! لو قُلتَ: ميكائيلُ [43] الذي يَنزِلُ بالرَّحمةِ والنَّباتِ والقَطرِ، لكان! فأنزل اللهُ عزَّ وجلَّ: مَنْ كَانَ عَدُوًّا لِجِبْرِيلَ [18]..."
“Mayahudi walikwenda kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wakamwambia: Ee Abal Qaasim! Sisi tutakuuliza mambo matano, kama utatujibu, basi tutajua kwamba wewe kweli ni Mtume, na sisi tutakuamini. Rasuli akachukua kutoka kwao ahadi ile ile ambayo Israaiyl aliichukua toka kwa wanawe, nao wakasema: Allaah Ni Mdhamini kwa haya tunayoyasema. Akawaambia: Yaleteni. Wakasema: Hakuna Nabiy yeyote isipokuwa ana Malaika ambaye anamletea habari. Hebu tueleze, ni nani Malaika wako? Akasema: Ni Jibriyl (‘alayhis salaam). Wakasema: Huyo ndiye yule anayeteremsha vita, mapigano na adhabu, huyu ni adui yetu. Lau ungelisema Miykaaiyl ambaye anateremsha rahmah, mimea na mvua, basi lingetimu jambo letu. Na hapo Allaah Akateremsha:
"قُلْ مَن كَانَ عَدُوًّا لِّجِبْرِيلَ فَإِنَّهُ نَزَّلَهُ عَلَىٰ قَلْبِكَ بِإِذْنِ اللَّـهِ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ وَهُدًى وَبُشْرَىٰ لِلْمُؤْمِنِينَ"
“Sema: Yeyote aliyekuwa adui wa Jibriyl, basi hakika yeye ameiteremsha Qur-aan katika moyo wako (ee Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم) kwa Idhini ya Allaah inayosadikisha yaliyo kabla yake, na mwongozo na bishara kwa Waumini”. [Hadiyth Swahiyh. Ahmad (2483) na An-Nasaaiy (9072 katika As-Sunan Al-Kubraa. Ipo pia katika As-Silsilat As-Swahiyhah 4/191]
Ibn Al-Qayyim amesema: “Jibriyl ndiye mwenye dhamana ya kuteremsha wahyi ambao ndio uhai kwa nyoyo na roho, na Miykaaiyl ndiye mwenye dhamana ya mvua ambayo ndio uhai kwa ardhi, mimea na wanyama”.
Ibn Baaz naye kasema: “Miykaaiyl kapewa jukumu la kusimamia maji na mvua”.
Na Ibn ‘Uthaymiyn kasema: “Tunaamini kwamba Malaika wana kazi walizobebeshwa, na kati yao ni Miykaaiyl ambaye anasimamia mvua na mimea”.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
40: Kazi Za Malaika
(3)- Atakayepuliza Baragumu Siku Ya Qiyaamah
Allaah Ta’aalaa Amesema:
"وَنُفِخَ فِي الصُّورِ فَصَعِقَ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَمَن فِي الْأَرْضِ إِلَّا مَن شَاءَ اللَّـهُ ۖ ثُمَّ نُفِخَ فِيهِ أُخْرَىٰ فَإِذَا هُمْ قِيَامٌ يَنظُرُونَ"
Toka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaah ‘anhu):
"ما طرَفَ صاحبُ الصورِ مُذْ وُكِّلَ بِهِ مُسْتَعِدًّا ينظُرُ نحْوَ العرشِ مخافَةَ أنْ يَؤْمَرَ قبْلَ أنْ يَرْتَدَّ إليْهِ طَرْفُهُ، كَأَنَّ عَيْنَيْهِ كَوْكَبَانِ دُرِّيَّانِ"
“Kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: (Malaika) mwenye kulikamata baragumu hajawahi kupepesa jicho lake tokea pale alipokabidhiwa baragumu hilo, amekaa tayari wakati wote akiwa amelielekeza jicho lake upande wa ‘Arshi kwa kuhofia kupewa amri (ya kulipuliza) kabla jicho lake halijapepesa, macho yake ni kama nyota mbili zenye mwanga mkali”. [Imekharijiwa na Abu Ash-Shaykh katika Al-‘Adhwamah (391) na Al-Haakim (8676). Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh katika Silsilatu Al-Ahaadiythi As-Swahiyha (1078)]
Hali hii ilimfanya Rasuli (Swalla Acllaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kukosa raha kabisa ya ladha ya maisha kutokana na kitisho cha jambo hilo hadi kuwaeleza Maswahaba wake ili nao wapate picha ya uhalisia huo. Anasema Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"كَيْفَ أَنْعَمُ وَقَدِ الْتَقَمَ صَاحِبُ الْقَرْنِ الْقَرْنَ وَحَنَى جَبْهَتَهُ وَأَصْغَى سَمْعَهُ يَنْتَظِرُ أَنْ يُؤْمَرَ أَنْ يَنْفُخَ فَيَنْفُخَ " . قَالَ الْمُسْلِمُونَ: فَكَيْفَ نَقُولُ يَا رَسُولَ اللَّهِ؟ قَالَ: قُولُوا حَسْبُنَا اللَّهُ وَنِعْمَ الْوَكِيلُ تَوَكَّلْنَا عَلَى اللَّهِ رَبِّنَا "
“Vipi nitakuwa na utulivu wa maisha wakati ambapo mwenye baragumu ashalitia baragumu kinywani, ameinamisha paji lake na amelitega vizuri sikio lake akisubiri apewe amri ya kulipuliza akalipuliza?! Maswahaba wakamuuliza: Tuseme vipi ee Rasuli wa Allaah? Akawaambia: Semeni: Allaah Anatutosha, Naye Ndiye Mtegemewa bora kabisa, Tumetawakkal kwa Allaah, Mola wetu”. [Hadiyth Swahiyh katika Swahiyh At-Tirmidhiy (3243)]
Hadiyth hii inatuonyesha ni namna gani Malaika huyu alivyojiandaa kusubiri amri toka kwa Allaah ya kulipuliza baragumu la kwanza kisha la pili. Maswahaba walipoipata picha hii, wakamuuliza Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) nini waseme ili Allaah Awapitishe salama na kizaazaa hicho cha siku hiyo, naye akawaambia nini cha kusema.
Kiufupi, jina la Malaika huyu ambaye amelishikilia baragumu halikutajwa katika Qur-aan wala Sunnah. Lakini baadhi ya ‘Ulamaa wamenukulu ‘Ijmaa ya kwamba Malaika ambaye atapuliza baragumu Siku ya Qiyaamah ni Israafiyl.
Hadiyth hii inatufunza yafuatayo:
1- Rasuli pamoja na utukufu wake wa daraja, anaiogopa Siku hiyo ya Qiyaamah litakapopulizwa baragumu. Hili liwe chachu kwetu kuiogopa zaidi Siku hiyo kwa kushikamana barabara na matendo mema na kujiepusha na mabaya.
2- Neno: "حَسْبُنَا اللهُ ونعمَ الوَكِيْلُ" lina fadhila kubwa, nalo pia ni katika viokozi vya mfazaiko wa Qiyaamah. Muislamu ajitahidi kulitamka nyakati zote ili aweze kusalimika na misukosuko ya dunia na kizaazaa cha kesho akhera.
3- Baragumu liko pamoja na Malaika ambaye amelishikilia tayari kulipuliza akipewa amri, na kwamba Qiyaamah kipo karibu kutokana na utayari wa Malaika huyo.
4- Namna ambavyo Malaika wanamwogopa Allaah Mtukufu na wanavyomtii kinyume na sisi ambao hatumpi Allaah heshima Anayostahiki.
5- Nguvu kubwa aliyopewa Malaika huyo ya kuweza kupuliza baragumu hilo likavifanya viumbe vyote vya ardhini na mbinguni kufa. Je, Huyo Aliyempa nguvu hizo, Nguvu Zake zikoje?!
Malaika
Alhidaaya.com [3]
41: Kazi Za Malaika
(4)- Malaika Wabebao ‘Arshi
Allaah Ta’aalaa Anasema:
"الَّذِينَ يَحْمِلُونَ الْعَرْشَ وَمَنْ حَوْلَهُ يُسَبِّحُونَ بِحَمْدِ رَبِّهِمْ وَيُؤْمِنُونَ بِهِ وَيَسْتَغْفِرُونَ لِلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا وَسِعْتَ كُلَّ شَيْءٍ رَّحْمَةً وَعِلْمًا فَاغْفِرْ لِلَّذِينَ تَابُوا وَاتَّبَعُوا سَبِيلَكَ وَقِهِمْ عَذَابَ الْجَحِيمِ"
“(Malaika) ambao wanabeba ‘Arsh na walio pembezoni mwake, wanasabbih na kumhimidi Rabbi wao, na wanamwamini, na wanawaombea maghfirah wale walioamini (wakisema): Rabb wetu! Umekienea kila kitu kwa rahmah na ujuzi, basi Waghufurie wale waliotubu, na wakafuata njia Yako, na Wakinge na adhabu ya moto uwakao vikali mno”. [Ghaafir: 07]
Malaika hao mbali na kubeba ‘Arshi, Allaah Amewapa kazi nyingine ya kutuombea maghfirah kwa Allaah, Allaah Atukinge na adhabu ya Moto, Allaah Atuingize Pepo za kudumu pamoja na wazazi wetu, wake zetu na dhuria zetu walo wema na Atukinge na maovu na misukosuko ya Siku ya Qiyaamah. Allaah Anasema:
"رَبَّنَا وَأَدْخِلْهُمْ جَنَّاتِ عَدْنٍ الَّتِي وَعَدتَّهُمْ وَمَن صَلَحَ مِنْ آبَائِهِمْ وَأَزْوَاجِهِمْ وَذُرِّيَّاتِهِمْ ۚ إِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ • "وَقِهِمُ السَّيِّئَاتِ ۚ وَمَن تَقِ السَّيِّئَاتِ يَوْمَئِذٍ فَقَدْ رَحِمْتَهُ ۚ وَذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ"
“Rabb wetu! Waingize Jannaat za kudumu milele ambazo Umewaahidi, pamoja na waliotengenea miongoni mwa baba zao, na wake zao, na dhuria wao. Hakika Wewe Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote ● Na Wakinge na maovu, kwani Unayemkinga na maovu Siku hiyo, basi kwa yakini Umemrehemu. Na huko ndiko kufuzu adhimu”. [Ghaafir: 8-9]
Amesema tena:
"وَالْمَلَكُ عَلَىٰ أَرْجَائِهَا ۚ وَيَحْمِلُ عَرْشَ رَبِّكَ فَوْقَهُمْ يَوْمَئِذٍ ثَمَانِيَةٌ"
“Na Malaika watakuwa pembezoni mwake, na watabeba ‘Arsh ya Rabb wako juu yao siku hiyo (Malaika) wanane”. [Al-Haaqqah: 17]
Toka kwa Jaabir (Radhwiya Allaah ‘anhumaa) kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"أُذِنَ لِي أَنْ أُحَدِّثَ عَنْ مَلَكٍ مِنْ مَلاَئِكَةِ اللَّهِ مِنْ حَمَلَةِ الْعَرْشِ إِنَّ مَا بَيْنَ شَحْمَةِ أُذُنِهِ إِلَى عَاتِقِهِ مَسِيرَةُ سَبْعِمِائَةِ عَامٍ"
“Nimepewa ruksa nimzungumzie Malaika miongoni mwa Malaika wa Allaah Ta’aalaa katika wanaobeba ‘Arshi. Kati ya ndewe ya sikio lake hadi kwenye bega lake ni mwendo wa miaka 700”. [Imekharijiwa na Abu Daawuwd (4727), na tamshi ni lake, At-Twabaraaniy (4421), na Al-Bayhaqiy (846). Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh katika Swahiyh Sunan Abiy Daawuwd (4727)]
Mwendo huo ni wa spidi ya farasi au ndege kama walivyosema baadhi ya ‘Ulamaa. Ikiwa kutoka kwenye ndewe ya sikio hadi kwenye bega ni safari ya miaka 700, je kiwiliwili chake kizima toka juu hadi chini utakuwa ni mwendo wa miaka mingapi?! Ukubwa huu hawezi kiumbe yoyote kuujua isipokuwa Muumbaji Mwenyewe Allaah Aliyetukuka. Hao pengine ndio viumbe wa pili kwa ukubwa baada ya ‘Arshi ya Allaah Ta’aalaa. Sasa Aliyewaumba hao, Atakuwaje? Tumwogopeni sana Allaah.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
42: Kazi Za Malaika
(5)- Malaika Wa Milima
Bibi ‘Aaishah (Radhwiya Allaah ‘anhaa) alimuuliza Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:
"هَلْ أَتَى عَلَيْكَ يَوْمٌ كَانَ أَشَدَّ مِنْ يَوْمِ أُحُدٍ؟ قَالَ: لَقَدْ لَقِيتُ مِنْ قَوْمِكِ مَا لَقِيتُ، وَكَانَ أَشَدُّ مَا لَقِيتُ مِنْهُمْ يَوْمَ الْعَقَبَةِ، إِذْ عَرَضْتُ نَفْسِي عَلَى ابْنِ عَبْدِ يَالِيلَ بْنِ عَبْدِ كُلاَلٍ، فَلَمْ يُجِبْنِي إِلَى مَا أَرَدْتُ، فَانْطَلَقْتُ وَأَنَا مَهْمُومٌ عَلَى وَجْهِي، فَلَمْ أَسْتَفِقْ إِلاَّ وَأَنَا بِقَرْنِ الثَّعَالِبِ، فَرَفَعْتُ رَأْسِي، فَإِذَا أَنَا بِسَحَابَةٍ قَدْ أَظَلَّتْنِي، فَنَظَرْتُ فَإِذَا فِيهَا جِبْرِيلُ فَنَادَانِي فَقَالَ إِنَّ اللَّهَ قَدْ سَمِعَ قَوْلَ قَوْمِكَ لَكَ وَمَا رَدُّوا عَلَيْكَ، وَقَدْ بَعَثَ إِلَيْكَ مَلَكَ الْجِبَالِ لِتَأْمُرَهُ بِمَا شِئْتَ فِيهِمْ، فَنَادَانِي مَلَكُ الْجِبَالِ، فَسَلَّمَ عَلَىَّ ثُمَّ قَالَ يَا مُحَمَّدُ، فَقَالَ ذَلِكَ فِيمَا شِئْتَ، إِنْ شِئْتَ أَنْ أُطْبِقَ عَلَيْهِمِ الأَخْشَبَيْنِ، فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم بَلْ أَرْجُو أَنْ يُخْرِجَ اللَّهُ مِنْ أَصْلاَبِهِمْ مَنْ يَعْبُدُ اللَّهَ وَحْدَهُ لاَ يُشْرِكُ بِهِ شَيْئًا".
“Ee Rasuli wa Allaah! Je uliwahi kukutana na siku ngumu zaidi kuliko Siku ya Vita vya Uhud? Rasuli akasema: Hakika nimepata mateso mengi na adha nyingi sana toka kwa watu wako (Maquraysh). Lakini siku ngumu zaidi niliyopambana nayo toka kwao ilikuwa siku ya ‘Aqabah. Ni pale nilipojitambulisha kwa Ibn ‘Abdi Yaaliyla bin ‘Abdi Kulaal lakini hakunijibu matakwa yangu. Nikaondoka na huzuni kubwa mno, na sikuzindukana ila baada ya kufika Qarn Ath-Tha’aalib. Nikanyanyua kichwa changu na kushtukizwa kuona wingu limenifunika kwa kivuli chake. Nikaliangalia na tahamaki nikamwona Jibriyl ndani yake. Akaniita na kuniambia: Hakika Allaah ‘Azza wa Jalla Amesikia waliyokwambia watu wako, na majibu waliyokupa, na Yeye Amekutumia Malaika wa milima ili umwamuru lolote ulitakalo. Malaika wa milima akaniita na kunisalimia, kisha akasema: Ee Muhammad! Hakika Allaah Amesikia maneno waliyokwambia watu wako, na mimi ndiye Malaika wa milima, na Mola wako Amenituma kwako ili uniamuru lolote utakalo kwa watu hao. Ukitaka nitawafudikiza kwa milima miwili, basi nitawafudikiza. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: Bali ninatumai Allaah Atatoa toka kwenye migongo yao watakaomwabudu Allaah Peke Yake na hawatamshirikisha na chochote”. [Swahiyhul Bukhaariy (3231)]
Siku hii ni pale Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipoelekea Taif kulingania Uislamu baada ya kufariki ami yake Abu Twaalib na mkewe Bi Khadiyjah. Akaelekea moja kwa moja kwa viongozi watatu wa kabila la Thaqiyf lakini hakuna hata mmoja kati yao aliyeitikia wito wake wa kuingia katika Uislamu au hata kumpa ahadi yoyote au usalama. Akakuta mambo ambayo hakuyatarajia kabisa ya kuchezwa shere, kukanushwa, kupingwa na kuzuiwa asifanye lolote kuhusu Uislamu. Lakini pia wakamsumbua na wakawatuma watoto na vijana wahuni, wakampopoa kwa mawe mpaka akatota damu hadi miguuni. Akatoka Taif kurudi Makkah akiwa amegubikwa ghamu na huzuni kubwa kutokana na uzito wa hayo yaliyomkuta mpaka alipofika Qarn Ath-Tha’aalib, ndipo hapo alipozindukana. Haya ndiyo yaliyomkuta Rasuli katika kuifikisha Dini kwetu, lakini sisi hatuioni thamani yake!
Ibn ‘Uthaymiyn amesema: “Tunaamini kwamba Malaika wana kazi walizopewa, na miongoni mwao ni Malaika wa milima”.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
43: Kazi Za Malaika
(6)- Malaika Wa Tumbo La Uzazi
Anas bin Maalik: “Kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إِنَّ اللَّهَ ـ عَزَّ وَجَلَّ ـ وَكَّلَ بِالرَّحِمِ مَلَكًا يَقُولُ يَا رَبِّ نُطْفَةٌ، يَا رَبِّ عَلَقَةٌ، يَا رَبِّ مُضْغَةٌ. فَإِذَا أَرَادَ أَنْ يَقْضِيَ خَلْقَهُ قَالَ أَذَكَرٌ أَمْ أُنْثَى شَقِيٌّ أَمْ سَعِيدٌ فَمَا الرِّزْقُ وَالأَجَلُ فَيُكْتَبُ فِي بَطْنِ أُمِّهِ "
“Hakika Allaah ‘Azza wa Jalla Amempa jukumu Malaika kushughulika na tumbo la uzazi. Anasema: Ee Mola wangu, ni tone la uzazi (niandike?). Ee Mola wangu, ni pande la damu (niandike?). Ee Mola wangu, ni pande la nyama (niandike?). Na Allaah Anapotaka kukamilisha umbo lake (kuwa binadamu kamili na kupuliziwa roho) Malaika huuliza: Je, ni wa kiume (niandike) au wa kike? Je, ni mwovu (niandike) au mwema? Ni kiasi gani riziki yake (nyingi au kidogo niandike)? Je, ataishi muda gani (umri mrefu niandike au mfupi)? Na hapo huyaandika hayo kitoto kikiwa bado ndani ya tumbo la uzazi la mama”. [Swahiyhul Bukhaariy (318)]
Rekodi ya mwanadamu kuhusiana na maisha yake yote imeanza kuandikwa akiwa bado ndani ya tumbo la mama na Malaika. Akiwa tone la mbegu ya uzazi, halafu pande la damu, kisha pande la nyama, hayo yote yanasajiliwa na Malaika mwenye kazi hiyo. Likiingia tone la uzazi, anamuuliza Allaah: Hili tone la uzazi limeingia, je niandike? Likibadilika na kuwa pande la damu anauliza hivyo hivyo na kuandika hadi pande la nyama. Halafu yanaendelea mabadiliko, awamu kwa awamu, hadi anazaliwa mtoto kamili. Huu ndio ukweli usiopingika. Na kwa mujibu wa Hadiyth hii, inaonyesha Malaika wanaofanya kazi hii ni wengi sana, kwa kuwa idadi ya mimba za wanadamu zinazotunga kila wakati ni nyingi mno. Nao huendelea kufuatilia hatua kwa hatua ukuaji wa mimba mpaka mtoto anapozaliwa. Kisha huyu huyu mwanadamu, anakuja kuwa na kibri, anamwasi Mola wake bila kujali na anajisahau kule alikotoka!
Malaika
Alhidaaya.com [3]
44: Kazi Za Malaika
(7)- Malaika Wa Kumlinda Mwanadamu Na Hatari
Malaika wenye kazi ya kumlinda mtu akiwa mjini kwake au safarini, akiwa macho au usingizini, na katika hali zake zote wanajulikana kama “Al-Mu’aqqibaatu”. Allaah Ta’aalaa Anatuambia:
"لَهُ مُعَقِّبَاتٌ مِّن بَيْنِ يَدَيْهِ وَمِنْ خَلْفِهِ يَحْفَظُونَهُ مِنْ أَمْرِ اللَّـهِ"
“Ana Malaika wanaofuatana kwa zamu mbele yake na nyuma yake wanamhifadhi kwa Amri ya Allaah”. [Ar-Ra’ad: 11]
Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaah ‘anhumaa) amesema kuhusiana na Malaika hawa: “Hawa ni malaika wanaomlinda mwanadamu kutoka mbele yake na nyuma yake, na inapokuja Qadari ya Allaah, huachana naye”.
Malaika hawa kama inavyoashiria aayah, humlinda mwanadamu kwa zamu, wanakamata hawa doria ya kumlinda, na muda wao unapomalizika wengine wa kuchukua nafasi yao wanakuja na kadhalika. Ni huduma ya ulinzi wa bure Aliyotuwekea Allaah Mtukufu. Wanatulinda kutokana na tusivyoviona kama majini, mashetani, wachawi, virusi, vimelea na kadhalika. Hivi visivyoonekana inakuwa mtu haiwezekaniki kujilinda navyo kama virusi vya maradhi ya kuambukiza na kadhalika, na Allaah Anatulinda navyo kupitia Malaika hawa. Kadhalika, wanatulinda na tunavyoviona. Hivi tunaweza kuvikwepa, lakini wakati mwingine vinatutokea ghafla na mtu anajikuta ameokoka navyo kwa njia ya ajabu. Hapa Malaika hawa wanakuwa wamefanya kazi yao, isipokuwa kwa lile tu ambalo mtu kaandikiwa.
Mujaahid kasema: “Hakuna mtu yeyote isipokuwa ana Malaika mwenye jukumu juu yake la kumlinda akiwa macho au usingizini kutokana na majini, wanadamu na vijinyama na wadudu hatari”.
Na Allaah Amesema tena:
"وَهُوَ الْقَاهِرُ فَوْقَ عِبَادِهِ ۖ وَيُرْسِلُ عَلَيْكُمْ حَفَظَةً حَتَّىٰ إِذَا جَاءَ أَحَدَكُمُ الْمَوْتُ تَوَفَّتْهُ رُسُلُنَا وَهُمْ لَا يُفَرِّطُونَ"
“Naye Ndiye Aliyedhibiti vyote chini ya Mamlaka Yake, Aliye juu ya Waja Wake. Na Anakutumieni Malaika wachungaji wadhibiti, hata yanapomfikia mmoja wenu mauti, Wajumbe Wetu humfisha, nao hawafanyi taksiri. [Al-An’aam: 61]
Ash-Shawkaaniy amesema: “Maana ya aayah hii ni kwamba Allaah Anatutumia Malaika wanaotulinda kutokana na maafa mbalimbali na kulinda matendo yetu pia”.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
45: Kazi Za Malaika
(8)- Malaika Wa Kusajili Amali Za Kheri Na Shari Za Binadamu
Ibn Abiy Zamaniyna amesema: “Ahlus Sunnah wanaamini uwepo wa Malaika wenye kusajili amali za mwanadamu; za kheri na za shari”.
Baadhi ya Waislamu wanafahamu kwamba katika Malaika hawa wawili, yuko Raqiyb anayekaa kuliani, na ‘Atiyd anayekuwa kushotoni. Hii ni kosa, kwa kuwa haya si majina yao, bali hizi ni sifa zao. “Raqiyb” ina maana ya mchungaji aliye macho wakati wote, na ‘Atiyd” ina maana ya aliye tayari bila kuchelewa kuandika lolote analolitamka mwanadamu au analolifanya. Hivyo kila mmoja wa Malaika hawa ana sifa hizi mbili za uchungaji na uandishi.
Allaah Ta’aalaa Anasema:
"إِذْ يَتَلَقَّى الْمُتَلَقِّيَانِ عَنِ الْيَمِينِ وَعَنِ الشِّمَالِ قَعِيدٌ ● مَّا يَلْفِظُ مِن قَوْلٍ إِلَّا لَدَيْهِ رَقِيبٌ عَتِيدٌ"
“Pale wanapopokea wapokeaji wawili (Malaika) wanaokaa kuliani na kushotoni • Hatamki kauli yeyote isipokuwa anaye mchungaji aliye tayari (kurekodi)”. [Qaaf: 17-18]
Malaika hawa wana ujuzi kamili wa kazi yao; wanamjua vyema mwanadamu, wanajua matendo yake na kauli zake zote, ya siri yake na ya dhahiri yake.
Allaah Ta’aalaa Amesema:
"وَإِنَّ عَلَيْكُمْ لَحَافِظِينَ ● كِرَامًا كَاتِبِينَ ● يَعْلَمُونَ مَا تَفْعَلُونَ"
“Na hakika juu yenu bila shaka kuna wenye kuhifadhi (na kuchunga) ● Watukufu wanaoandika (amali) ● Wanajua yale myafanyayo”. [Al-Infitwaar: 10-12]
Na Anasema tena Allaah ‘Azza wa Jalla:
"أَمْ يَحْسَبُونَ أَنَّا لَا نَسْمَعُ سِرَّهُمْ وَنَجْوَاهُم ۚ بَلَىٰ وَرُسُلُنَا لَدَيْهِمْ يَكْتُبُونَ"
“Au wanadhania kwamba Sisi Hatusikii siri zao na minong’ono yao? Sivyo! (Tunasikia!) Na Wajumbe Wetu wako kwao wanaandika”. [Az-Zukhruf: 80]
As-Sa’adiy amesema kuhusiana na aayah hii: “Hivi wao kwa ujinga wao na dhulma zao wanadhani kwamba Sisi Hatusikii siri zao ambazo hawakuzizungumza zikasikika?! Bali Sisi Tunajua hata siri zilizomo ndani ya nyoyo zao na yote wanayonong’onezana kwa siri. Na wao wanadhani kwamba haya yote yanapita tu hivi hivi! La hasha! Malaika Wetu wako nao na wanaandika yao yote ya siri na dhahiri, na yote yatahifadhiwa mpaka watakapohudhurishwa Siku ya Qiyaamah, yote waliyoyafanya na waliyoyatamka yatahudhurishwa, na Allaah Hatomdhulumu yeyote”.
Al-Baghawiy kasema kuhusiana na aayah hii: “Malaika wawili wenye kazi ya kusajili matendo ya mwanadamu wanapokea matendo yote anayoyafanya mwanadamu na maneno yote anayoyatamka, wanayahifadhi na wanayaandika. Malaika mmoja yuko kulia, na huyu anaandika matendo yote mema na maneno yote mema, na mwingine yuko kushoto, na huyu anaandika matendo yote mabaya na maneno yote mabaya, na kila mmoja wao yuko tayari wakati wote kufuatia matendo na kusikiliza maneno, na hawambanduki mtu hata dakika moja. Chochote unachokitamka, basi uko nao, na chochote ukifanyacho, basi unao”.
Abu Hurayrah (Radhwiya Allaah ‘anhu) amesema: “Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إِذَا هَمَّ عَبْدِي بِسَيِّئَةٍ فَلاَ تَكْتُبُوهَا عَلَيْهِ فَإِنْ عَمِلَهَا فَاكْتُبُوهَا سَيِّئَةً وَإِذَا هَمَّ بِحَسَنَةٍ فَلَمْ يَعْمَلْهَا فَاكْتُبُوهَا حَسَنَةً فَإِنْ عَمِلَهَا فَاكْتُبُوهَا عَشْرًا"
“Allaah ‘Azza wa Jalla Amesema (kuwaambia Malaika): Mja wangu akidhamiria kufanya jambo baya, basi msimwandikie, na kama atalifanya, basi mwandikieni baya moja. Na akidhamiria kufanya jambo jema na asilifanye, basi mwandikieni jema moja, na kama atalifanya, basi mwandikieni mema kumi”. [Al-Bukhaariy (7501) na Muslim (128)]
Na amesema tena Abu Hurayrah: “Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"قَالَتِ الْمَلاَئِكَةُ: رَبِّ ذَاكَ عَبْدُكَ يُرِيدُ أَنْ يَعْمَلَ سَيِّئَةً - وَهُوَ أَبْصَرُ بِهِ – فَقَالَ: ارْقُبُوهُ، فَإِنْ عَمِلَهَا فَاكْتُبُوهَا لَهُ بِمِثْلِهَا . وَإِنْ تَرَكَهَا فَاكْتُبُوهَا لَهُ حَسَنَةً، إِنَّمَا تَرَكَهَا مِنْ جَرَّاىَ"
“Malaika husema: Ee Rabbi wetu! Yule Mja Wako anataka kufanya baya -na Allaah Anamwona zaidi-, Allaah Huwaambia: Mfuatilieni, kama atalifanya, basi mwandikieni mfano wake, na kama ataliacha, basi mwandikieni jema moja, kwani hakika ameliacha kwa ajili Yangu”. [Al-Bukhaariy (42) na Muslim (129)]
Malaika
Alhidaaya.com [3]
46: Kazi Za Malaika
(9)- Malaika Wanaozunguka Kwenye Njia Na Barabara Kutafuta Majaalis Za Dhikr
Malaika hawa hawana kazi nyingine isipokuwa kuzunguka huku na kule kuwatafuta watu waliokaa pamoja kwa ajili ya kumdhukuru Allaah. Wakiwapata, huwazunguka kwa mbawa zao, huwaombea maghfira na husikiliza adhkaar zao.
Abu Hurayrah amesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إِنَّ لِلَّهِ مَلاَئِكَةً يَطُوفُونَ فِي الطُّرُقِ، يَلْتَمِسُونَ أَهْلَ الذِّكْرِ، فَإِذَا وَجَدُوا قَوْمًا يَذْكُرُونَ اللَّهَ تَنَادَوْا هَلُمُّوا إِلَى حَاجَتِكُمْ. قَالَ: فَيَحُفُّونَهُمْ بِأَجْنِحَتِهِمْ إِلَى السَّمَاءِ الدُّنْيَا. قَالَ: فَيَسْأَلُهُمْ رَبُّهُمْ وَهُوَ أَعْلَمُ مِنْهُمْ: مَا يَقُولُ عِبَادِي؟ قَالُوا: يَقُولُونَ يُسَبِّحُونَكَ، وَيُكَبِّرُونَكَ، وَيَحْمَدُونَكَ وَيُمَجِّدُونَكَ. قَالَ: فَيَقُولُ هَلْ رَأَوْنِي؟ قَالَ: فَيَقُولُونَ لاَ وَاللَّهِ مَا رَأَوْكَ. قَالَ: فَيَقُولُ وَكَيْفَ لَوْ رَأَوْنِي؟ قَالَ: يَقُولُونَ لَوْ رَأَوْكَ كَانُوا أَشَدَّ لَكَ عِبَادَةً، وَأَشَدَّ لَكَ تَمْجِيدًا، وَأَكْثَرَ لَكَ تَسْبِيحًا. قَالَ: يَقُولُ فَمَا يَسْأَلُونِي قَالَ يَسْأَلُونَكَ الْجَنَّةَ. قَالَ: يَقُولُ وَهَلْ رَأَوْهَا؟ قَالَ: يَقُولُونَ لاَ وَاللَّهِ يَا رَبِّ مَا رَأَوْهَا. قَالَ: يَقُولُ فَكَيْفَ لَوْ أَنَّهُمْ رَأَوْهَا؟ قَالَ: يَقُولُونَ لَوْ أَنَّهُمْ رَأَوْهَا كَانُوا أَشَدَّ عَلَيْهَا حِرْصًا، وَأَشَدَّ لَهَا طَلَبًا، وَأَعْظَمَ فِيهَا رَغْبَةً. قَالَ: فَمِمَّ يَتَعَوَّذُونَ؟ قَالَ: يَقُولُونَ مِنَ النَّارِ. قَالَ: يَقُولُ وَهَلْ رَأَوْهَا؟ قَالَ: يَقُولُونَ لاَ وَاللَّهِ مَا رَأَوْهَا. قَالَ: يَقُولُ فَكَيْفَ لَوْ رَأَوْهَا؟ قَالَ: يَقُولُونَ لَوْ رَأَوْهَا كَانُوا أَشَدَّ مِنْهَا فِرَارًا، وَأَشَدَّ لَهَا مَخَافَةً. قَالَ: فَيَقُولُ فَأُشْهِدُكُمْ أَنِّي قَدْ غَفَرْتُ لَهُمْ. قَالَ: يَقُولُ مَلَكٌ مِنَ الْمَلاَئِكَةِ فِيهِمْ فُلاَنٌ لَيْسَ مِنْهُمْ إِنَّمَا جَاءَ لِحَاجَةٍ. قَالَ: هُمُ الْجُلَسَاءُ لاَ يَشْقَى بِهِمْ جَلِيسُهُمْ ".
“Hakika Allaah Ana Malaika wanaozunguka majiani kuwatafuta watu wa dhikri. Wanapowapata watu wanaomdhukuru Allaah huitana wakisema: Haya njooni kwenye lile mlitafutalo. Na hapo huwazungushia mbawa zao hadi kwenye mbingu ya dunia. Halafu Mola wao Huwauliza nailhali Yeye Anajua zaidi kuliko wao: Waja Wangu wanasema nini? Malaika hujibu wakisema: Wanakutakasa, wanakukabirisha, wanakuhimidi na wanakutukuza. Allaah Huwauliza: Je, wameniona? Malaika hujibu: Hapana, tunaapa kwa Jina Lako. Allaah Huwaambia: Ingekuwaje kama wangeniona? Hujibu: Kama wangelikuona, basi wangelikuabudu kwa nguvu zaidi, wangelikutukuza na kukuhimidi zaidi, na wangelikutakasa kwa wingi zaidi. Allaah Huwauliza tena: Wananiomba nini? Husema: Wanakuomba Jannah. Huwauliza: Je, wameiona? Wanajibu: Hapana wa-Allaah, ee Mola wetu, hawajaiona. Huwaambia: Itakuwa vipi lau wangelioona? Hujibu: Kama wangeliiona, basi wangelikuwa na pupa nayo zaidi, wangekuwa na haja nayo zaidi, na utashi mkubwa nayo zaidi. Huwauliza: Ni kitu gani wanajilinda nacho? Hujibu: Wanajilinda na moto. Huwauliza: Je, wameuona? Hujibu: Hapana wa-Allaah, ee Mola wetu, hawajauona. Huwauliza: Ingekuwa vipi lau wangeliuona? Hujibu: Wangeliuona, basi wangeliukimbia kwa nguvu zao zote na wangeliuogopa zaidi. Huwaambia: Basi Nakushuhudilieni kwamba Mimi Nimewasamehe. Malaika mmoja atasema: Yuko fulani, si katika wao, yeye amekuja tu kwa haja nyingine. Allaah Atamwambia: Wote hao ni wa majilisi moja, anayekaa nao hataadhibiwa”. [Swahiyhul Bukhaariy (6408)]
Abu Hurayrah amesema tena: Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"مَا اجْتَمَعَ قَوْمٌ فِي بَيْتٍ مِنْ بُيُوتِ اللَّهِ تَعَالَى يَتْلُونَ كِتَابَ اللَّهِ وَيَتَدَارَسُونَهُ بَيْنَهُمْ إِلاَّ نَزَلَتْ عَلَيْهِمُ السَّكِينَةُ وَغَشِيَتْهُمُ الرَّحْمَةُ وَحَفَّتْهُمُ الْمَلاَئِكَةُ وَذَكَرَهُمُ اللَّهُ فِيمَنْ عِنْدَهُ " .
“Hawakusanyiki watu katika Nyumba yoyote katika Nyumba za Allaah ili kusoma na kufundishana Kitabu cha Allaah, isipokuwa huwateremkia utulivu, rahmah huwafunika, Malaika huwazunguka, na Allaah Huwataja kwa wale walio Kwake”. [Muslim (2699)]
Ibn ‘Uthaymiyn amesema: “Miongoni mwa faida za Hadiyth hii ni kwamba Allaah Anawatumikisha Malaika Wake kwa ajili ya mwanadamu, na hapa Waumini hawa wanaosoma Kitabu cha Allaah, wanapata utukuzo na hishma kubwa ya kuzungukwa na Malaika hao”.
Bila shaka hali kama hii haimruhusu shaytwaan kukurubia.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
47: Kazi Za Malaika
(10)- Malaika Wenye Kuizuru Al-Baytul Ma’amuwr
Nyumba hii Allaah Ameiapia Aliposema:
"وَالْبَيْتِ الْمَعْمُورِ"
“Na Naapa kwa Nyumba yenye kuamiriwa nyakati zote (na Malaika)”. [At-Tuwr: 04]
Al-Baghawiy amesema: “Nyumba hii iko katika mbingu ya saba na imeitwa hivi kutokana na wingi wa Malaika wanaoikusudia. Iko mkabala na Al-Ka’abah kiwima, na utukuzo wake mbinguni ni sawa na utukuzo wa Al-Ka’abah hapa ardhini, na kila siku wanaingia humo Malaika elfu 70 kwa ajili ya kutufu na kuswali humo, kisha hawarudi tena humo milele”.
Imepokelewa toka kwa Maalik bin Swa-‘aswa-’ah kuhusiana na kisa cha Israa kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"رُفِعَ لِيَ الْبَيْتُ الْمَعْمُورُ فَقُلْتُ: يَا جِبْرِيلُ مَا هَذَا؟ قَالَ: هَذَا الْبَيْتُ الْمَعْمُورُ يَدْخُلُهُ كُلَّ يَوْمٍ سَبْعُونَ أَلْفَ مَلَكٍ إِذَا خَرَجُوا مِنْهُ لَمْ يَعُودُوا فِيهِ آخِرُ مَا عَلَيْهِمْ"
“Nilinyanyuliwa Al-Baytul Al-Ma-‘amuwr nikasema: Ee Jibriyl, nini hii? Akasema: Hii ni Al-Baytul Ma-‘amuwr, kila siku wanaingia ndani yake Malaika elfu sabini, na wakitoka humo hawarudi tena hadi wa mwisho wao”.
Imepokelewa pia toka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaah ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akizungumzia kisa cha Israa amesema:
"ففُتِح لنا فإذا أنا بإبراهيمَ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم مُسنِدًا ظَهْرَه إلى البيتِ المعمورِ، وإذا هو يدخُلُه كلَّ يومٍ سبعون ألْفَ مَلَكٍ لا يعودون إليه"
“Tukafunguliwa (mbingu), na hapo nikamkuta Ibraahiym (‘Alayhis Salaam) akiwa ameegemeza mgongo wake kwenye Al-Baytul Ma’amuwr ambayo wanaingia humo kila siku Malaika elfu sabini na hawarudi tena humo”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Ahmad (14082), Ibn Abiy Shaybah katika Al-Muswannaf (17883) na Abu Ya’alaa (3373)]
Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimkuta Nabiy Ibraahiym (‘alayhis salaam) katika hali hiyo kwa kuwa yeye ndiye aliyeijenga Al-Ka’abah ya hapa ardhini, na hayo ndiyo malipo yake, kwani malipo ni kwa mujibu wa matendo.
As-Sam-’aaniy amesema: Kauli maarufu ni kwamba hiyo ni Nyumba iliyoko mbinguni. Limesemwa hili na Ibn ‘Abbaas na Mufassiruna wote, pia limehadithiwa toka kwa ‘Aliyy bin Abiy Twaalib (Radhwiya Allaah ‘anhu).
An-Nawawiy amesema: “Hii ni dalili kubwa ya kuonyesha idadi kubwa mno ya Malaika rehmah na amani ziwe juu yao”.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
48: Kazi Za Malaika
(11)- Malaika Mwenye Kutoa Roho
Katika baadhi ya aathaar, Malaika mtoa roho (Malakul Mawt) ametajwa kama ‘Izraaiyl, lakini jina hili halijathibitishwa, si katika Qur-aan wala katika Sunnah.
Ibn Kathiyr amesema: “Ama Malakul Mawt, yeye jina lake halijatajwa katika Qur-aan wala katika Hadiyth zilizo swahiyh, lakini ametajwa katika baadhi ya aathaar kama ni ‘Izraaiyl, na Allaah Ndiye Ajuaye zaidi”.
Sheikh Bin Baaz (Allaah Amrehemu) aliulizwa kama katika Hadiyth za Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) limethibiti jina la ‘Izraaiyl kama ni Malaika mtoa roho? Naye alijibu akisema: Sijui chochote kilichothibiti kuhusiana na hili, lakini lililotangaa baina ya Wanazuoni ni kuwa jina lake ni ‘Izraaiyl, lakini mimi sijui Hadiyth yoyote iliyo sahihi kwamba jina lake ni hilo, bali limetajwa kwenye aathaar dhaifu ambazo hazifai kuwa ni hoja”.
Ama Al-Albaaniy, yeye kasema: “Malakul Mawt ndio jina lake lililotajwa ndani ya Qur-aan Tukufu. Ama kumuita ‘Izraaiyl kama ilivyotangaa kwa watu, hilo halina asili, bali limechukuliwa toka kwenye Israaiyliyyaat (Hadiyth na riwaayah za kutunga toka kwenye Taurati na Injili”.
‘Abdulrahmaan Al-Barraak amesema: “Jina hili la ‘Izraaiyl ni mashuhuri lakini halikuthibiti, bali majina ya Malaika yaliyothibiti ni Jibriyl, Miykaaiyl, Israafiyl, Maalik mlinzi wa moto, pia Munkar na Nakiyr, nao ni Malaika wawili wanaomuuliza maswali maiti kaburini”.
Malakul Mawt ametajwa katika Kauli Yake Ta’aalaa:
قُلْ يَتَوَفَّاكُم مَّلَكُ الْمَوْتِ الَّذِي وُكِّلَ بِكُمْ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّكُمْ تُرْجَعُونَ
“Sema: Atakufisheni Malaika wa mauti ambaye amewakilishwa kwenu, kisha kwa Rabb wenu mtarejeshwa”. [As-Sajdah: 11].
Malaika huyu ana wasaidizi wake. Hebu fikiria, katika kipindi cha saa 24 au dakika kadhaa, ni watu wangapi wanakufa duniani kote? Hivyo ni lazima awe na wasaidizi wake. Allaah Ta’aalaa Anasema:
"حَتَّىٰ إِذَا جَاءَ أَحَدَكُمُ الْمَوْتُ تَوَفَّتْهُ رُسُلُنَا وَهُمْ لَا يُفَرِّطُونَ • ثُمَّ رُدُّوا إِلَى اللَّـهِ مَوْلَاهُمُ الْحَقِّ ۚ أَلَا لَهُ الْحُكْمُ وَهُوَ أَسْرَعُ الْحَاسِبِينَ"
“Hata yanapomfikia mmoja wenu mauti, Wajumbe Wetu (Malaika) humfisha, nao hawafanyi taksiri • Kisha watarudishwa (wote waliofishwa) kwa Allaah Rabb wao wa haki. Tanabahi! Hukumu ni Yake Pekee; Naye ni Ni Mwepesi zaidi kuliko wote wanaohisabu. [Al-An’aam: 61-62]
Malaika hawa hupokea amri toka kwa Malakul mawt ya kutoa roho ya mtu ambaye muda wake umefika, na utoaji huo unanasibishwa kwa Malakul Mawt kana kwamba yeye ndiye aliyetekeleza zoezi hilo moja kwa moja. Ni kama vile mkuu wa jeshi anapoamuru askari wake kufanya operesheni fulani, yeye hashiriki, lakini zoezi hilo linanasibishwa kwake.
Na katika Az-Zumar, Allaah Amelinasibisha zoezi hili Kwake Yeye Mwenyewe Aliposema:
"اللَّـهُ يَتَوَفَّى الْأَنفُسَ حِينَ مَوْتِهَا"
“Allaah Huzichukua roho wakati wa kufa kwake”. [Az-Zumar: 42]
Na hapa hakuna ukinzani kati ya Aayaah, kwa kuwa hakuna yeyote anayekufa isipokuwa kwa kupenda Kwake Allaah. Malaika hao wasingeweza kufanya kazi hiyo bila Yeye ‘Azza wa Jalla kutaka, na Yeye Ndiye pia Aliyeupanga muda wa kuishi wa kila kiumbe, hivyo basi mambo yote yananasibishwa Kwake.
Nafsi au roho kabla haijatoka, mtu hujiwa na Malaika wa rahmah wenye sanda na mafuta mazuri ya Peponi kama ni mwema. Baada tu ya Malakul Mawt kuitoa roho yake, Malaika hao huichukua hapo kwa papo, wakaikafini na kisha wakaondoka nayo kwenda nayo juu. Roho yake itakafiniwa na Malaika hao, na mwili wake utaoshwa, utakafiniwa, utaswaliwa na utazikwa na nduguze Waislamu.
Ama kafiri, roho yake itavikwa vile vile sanda ya motoni na kuwa na harufu mbaya ya kuchukiza mno. Roho ikitoka tu, itadakwa na Malaika wa adhabu, na hapo safari ya mateso inaanza. Hadiyth hii ya Al-Baraa bin ‘Aazib inathibitisha haya. Amesema:
"خرَجْنا مع النَّبيِّ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم في جِنازةِ رَجُلٍ من الأنصارِ، فانتَهَينا إلى القبرِ ولَمَّا يُلحَدْ، فجلس رسولُ الله صلَّى اللهُ عليه وسلَّم، وجلَسْنا حولَه كأنَّ على رُؤوسِنا الطيرَ، وفي يَدِه عودٌ يَنكُتُ في الأرضِ، فرفع رأسَه، فقال: استعيذوا باللهِ من عذابِ القَبرِ، مَرَّتينِ أو ثلاثًا، ثمَّ قال: إنَّ العبْدَ المؤمِنَ إذا كانَ في انْقِطاعٍ مِنَ الدُّنْيا، وإقْبالٍ مِنَ الآخِرَةِ، نزَلَ إليه مَلائكةٌ مِنَ السَّماءِ بِيضُ الوُجوهِ، كَأنَّ وُجوهَهُمُ الشَّمْسُ، معَهُم كَفَنٌ مِن أَكْفانِ الجَنَّةِ، وحَنُوطٌ مِن حَنُوطِ الجَنَّةِ، حتَّى يَجْلِسوا مِنه مَدَّ البَصَرِ، ثمَّ يَجيءُ مَلَكُ المَوْتِ علَيه السَّلامُ، حتَّى يَجْلِسَ عندَ رَأْسِه، فيَقُولُ: أَيَّتُها النَّفْسُ الطَّيِّبَةُ، اخْرُجي إِلى مَغْفرةٍ مِنَ اللهِ ورِضْوانٍ. فتَخْرُجُ تَسِيلُ كَما تَسِيلُ القَطْرةُ مِن فِي السِّقَاءِ، فيَأْخُذُها، فإذا أخَذَها لم يَدَعُوها في يَدِه طَرْفةَ عينٍ حتَّى يَأخُذوها، فيَجْعَلوها في ذَلِك الكَفَنِ، وفي ذَلِك الحَنُوطِ، ويَخْرُجُ مِنها كَأَطْيبِ نَفْحةِ مِسْكٍ وُجِدَت على وَجْهِ الْأَرْضِ. فيَصْعَدونَ بِها"
“Tulitoka kwenda kumzika mwanaume wa Kianswaar pamoja na Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Tulipofika kaburini, mwanandani ulikuwa bado unachimbwa. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akakaa, nasi tukakaa pembezoni mwake kimya kana kwamba kuna ndege juu ya vichwa vyetu. Rasuli alikuwa na kijiti mkononi mwake na akawa anakigonga gonja chini (kama vile mtu mwenye ghamu), kisha akanyanyua kichwa chake akasema: Jilindeni kwa Allaah na adhabu ya kaburi, alisema mara mbili au tatu halafu akaendelea kusema: Mja muumini akiwa katika hali ya kuondoka duniani na kuelekea aakhirah, Malaika wenye nyuso nyeupe mithili ya jua humteremkia toka mbinguni wakiwa na sanda kati ya sanda za Peponi pamoja na mafuta katika mafuta mazuri ya Peponi, na hukaa upeo wa macho toka pale alipo. Kisha Malakul Mawt (‘Alayhis Salaam) huja na kukaa mbele ya kichwa chake na kumwambia: Ee nafsi njema, toka uende kwenye maghfira ya Allaah na radhi Zake. Roho hiyo itatoka ikichuruzika kama tone la maji linavyochuruzika toka chomboni, na Malakul Mawt huichukua, na anapoichukua haibaki kwenye mkono wake muda wa pepeso la jicho ila huchukuliwa na Malaika (wa rahmah) ambao wanaiweka kwenye sanda hiyo na kwenye mafuta hayo. Kisha roho hiyo hutoka kwake harufu mzuri mno kama mnuso wa mafuta ya miski ambayo hakuna mfano wake juu ya uso wa ardhi, halafu hupanda nayo juu”. [Hadiyth Swahiyh. Swahiyhul Jaami’i (1676)]
Malaika
Alhidaaya.com [3]
49: Kazi Za Malaika
(12)- Malaika Wanaowasaili Maiti Kaburini
Malaika hawa ni wawili na wanajulikana kama Munkar na Nakiyr. Ni weusi wenye macho kibuluu, na humjia maiti ili kumuuliza baadhi ya maswali baada ya kuzikwa. Ndio maana Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametuamuru tumwombee maghfira ndugu yetu tuliyemzika ili asaa dua zetu zikamsaidia katika kukabiliana na mtihani huo mgumu na mazingira hayo ya kutisha anayokabiliana nayo kwa mara ya kwanza kabisa. Huo ni miongoni mwa mitihani ya mwanzo inayotukabili ya aakhirah baada ya kupitia mitihani mingine ya hapa duniani. Maswali wanayomuuliza maiti si magumu, ni ya kawaida tu, lakini yanaweza kuwa magumu kwa Muislamu mwenye kumwasi Allaah, na kama ni kafiri au mushrik, basi hatoweza kujibu lolote. Amali njema za mja na kumcha Allaah ndiyo silaha zitakazomwezesha kuyajibu maswali hayo, na Allaah Ndiye Atakayempa uthabiti kama Anavyotuambia:
"يُثَبِّتُ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا بِالْقَوْلِ الثَّابِتِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ ۖ وَيُضِلُّ اللَّـهُ الظَّالِمِينَ ۚ وَيَفْعَلُ اللَّـهُ مَا يَشَاءُ"
“Allaah Huwathibitisha wale walioamini kwa kauli thabiti katika uhai wa dunia na Aakhirah. Na Allaah Huwaacha kupotoka madhalimu. Na Allaah Anafanya Atakavyo”. [Ibraahiym: 27]
Katika Hadiyth iliyopokelewa na Anas bin Maalik (Radhwiya Allaah ‘anhu), Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إنَّ العَبْدَ إذَا وُضِعَ في قَبْرِهِ وتَوَلَّى عنْه أصْحَابُهُ، وإنَّه لَيَسْمَعُ قَرْعَ نِعَالِهِمْ، أتَاهُ مَلَكَانِ فيُقْعِدَانِهِ، فَيَقُولَانِ: ما كُنْتَ تَقُولُ في هذا الرَّجُلِ؛ لِمُحَمَّدٍ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم، فأمَّا المُؤْمِنُ، فيَقولُ: أشْهَدُ أنَّه عبدُ اللَّهِ ورَسولُهُ، فيُقَالُ له: انْظُرْ إلى مَقْعَدِكَ مِنَ النَّارِ قدْ أبْدَلَكَ اللَّهُ به مَقْعَدًا مِنَ الجَنَّةِ، فَيَرَاهُما جَمِيعًا، وَأمَّا المُنَافِقُ والكَافِرُ فيُقَالُ له: ما كُنْتَ تَقُولُ في هذا الرَّجُلِ؟ فيَقولُ: لا أدْرِي، كُنْتُ أقُولُ ما يقولُ النَّاسُ، فيُقَالُ: لا دَرَيْتَ ولَا تَلَيْتَ، ويُضْرَبُ بمَطَارِقَ مِن حَدِيدٍ ضَرْبَةً، فَيَصِيحُ صَيْحَةً يَسْمَعُهَا مَن يَلِيهِ غيرَ الثَّقَلَيْنِ"
“Mja anapowekwa katika kaburi lake na watu wake wakaondoka, na kwa hakika husikia mchakato wa viatu vyao, humjia Malaika wawili wakamkalisha, kisha humuuliza: Ulikuwa unasema nini kuhusu mtu huyu? Yaani Muhammad (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Akiwa maiti ni Muumini atasema: Ninashuhudia kwamba yeye ni Mja wa Allaah na Mtume Wake. Na hapo ataambiwa: Angalia kwenye makazi yako motoni, Allaah Amekubadilishia kwayo kuwa makazi ya Peponi, naye atayaona makazi yote mawili. Ama mnafiki na kafiri, yeye pia ataulizwa: Ulikuwa unasema nini kuhusu mtu huyu? Atasema: Sijui, nilikuwa nasema yale wayasemayo watu. Ataambiwa: Hukujua wala hukusoma. Kisha atapigwa nyundo ya chuma pigo moja kali (kati ya masikio yake mawili), na atapiga ukelele watakaousikia viumbe wote walio karibu yake isipokuwa majini na wanadamu”. [Swahiyhul Jaami’i (1675)]
Hadiyth hii imegusia swali moja tu kumhusu Mtume (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam), lakini Hadiyth nyingine zinasema ataulizwa: Nani Mola wako? Ipi dini yako? Nani Nabiy wako?
Namwomba Allaah ‘Azza wa Jalla Atupe uthabiti tuweze kuyajibu maswali haya sawasawa, na tupite salama kwenye mtihani huo mgumu.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
50: Kazi Za Malaika
(13)- Malaika Wasimamizi Na Walinzi Wa Pepo
Allaah Ta’aalaa Amesema:
"وَسِيقَ الَّذِينَ اتَّقَوْا رَبَّهُمْ إِلَى الْجَنَّةِ زُمَرًا ۖ حَتَّىٰ إِذَا جَاءُوهَا وَفُتِحَتْ أَبْوَابُهَا وَقَالَ لَهُمْ خَزَنَتُهَا سَلَامٌ عَلَيْكُمْ طِبْتُمْ فَادْخُلُوهَا خَالِدِينَ"
“Na wataongozwa wale waliomcha Rabb wao kuelekea Jannah makundi-makundi, mpaka watakapoifikia na milango yake ishafunguliwa, na walinzi wake watawaambia: Salaamun ‘Alaykum! Amani iwe juu yenu, furahini na iingieni, mdumu milele. [Az-Zumar: 73]
Aayaah hii na aayah ya 71 ya Suwrah hii, ni dalili kwamba Pepo na Moto zina milango inayofungwa na kufunguliwa, na kila moja ina walinzi na wasimamizi wake.
Katika Hadiyth ya Anas, Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"آتي بابَ الجَنَّةِ يَومَ القِيامَةِ فأسْتفْتِحُ، فيَقولُ الخازِنُ: مَن أنْتَ؟ فأقُولُ: مُحَمَّدٌ، فيَقولُ: بكَ أُمِرْتُ لا أفْتَحُ لأحَدٍ قَبْلَكَ"
“Nitauendea mlango wa Pepo Siku ya Qiyaamah na kubisha. Mlinzi wake atauliza: Nani wewe? Nitamjibu: Muhammad. Atasema: Ni wewe tu nimeamrishwa kufungua, simfungulii yeyote kabla yako”. [Swahiyh Muslim: 197]
Hadiyth hii ni dalili pia kwamba Malaika wako makini sana katika kazi na majukumu yao.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
51: Kazi Za Malaika
(14)- Malaika Walinzi Na Malaika Wa Adhabu Wa Moto (Zabaaniyah)
Malaika mlinzi mkuu wa moto wa Jahannam ni Maalik. Allaah Ta’aalaa Anasema:
"وَنَادَوْا يَا مَالِكُ لِيَقْضِ عَلَيْنَا رَبُّكَ ۖ قَالَ إِنَّكُم مَّاكِثُونَ"
“Na wataita: Ee Maalik! (Mlinzi wa moto) Na Atumalize tufe Rabb wako. Atasema: Hakika nyinyi ni wenye kubakia kuishi humo”. [Az-Zukhruf: 77]
Huyu ana wasaidizi wake wanaojulikana kama Zabaaniyah. Hawa ni Malaika wa adhabu kwa watu wa motoni. Wana nguvu za kupindukia, wana maumbo na sauti za kutisha na kukera mno, na ni wakali mno. Allaah ‘Azza wa Jalla Amewataja katika Suwrat Al-‘Alaq Aliposema:
"سَنَدْعُ الزَّبَانِيَةَ"
“Nasi Tutawaita Az-Zabaaniyah (Malaika wa adhabu)”.
Malaika hawa watawapokea watu watakaoingia motoni. Sijui yatakuwa mapokezi ya aina gani ya kupokewa na Malaika kama hao! Bila shaka ni adhabu juu ya adhabu. Hapa duniani tunaona namna askari wanavyowapokea baadhi ya watu wanaoshukiwa tu kwa kosa vituoni au mahabusu kwa mateke na vipigo. Hali itakuwaje kwa hao watakaoswagwa kupelekwa motoni na Malaika hao! Allaah ‘Azza wa Jalla Anatuambia:
"وَسِيقَ الَّذِينَ كَفَرُوا إِلَىٰ جَهَنَّمَ زُمَرًا ۖ حَتَّىٰ إِذَا جَاءُوهَا فُتِحَتْ أَبْوَابُهَا وَقَالَ لَهُمْ خَزَنَتُهَا أَلَمْ يَأْتِكُمْ رُسُلٌ مِّنكُمْ يَتْلُونَ عَلَيْكُمْ آيَاتِ رَبِّكُمْ وَيُنذِرُونَكُمْ لِقَاءَ يَوْمِكُمْ هَـٰذَا ۚ قَالُوا بَلَىٰ وَلَـٰكِنْ حَقَّتْ كَلِمَةُ الْعَذَابِ عَلَى الْكَافِرِينَ"
“Na wataswagwa wale waliokufuru kuelekea Jahannam makundi-makundi, mpaka watakapoifikia, itafunguliwa milango yake, na walinzi wake watawaambia: Je, hawajakufikieni Rusuli miongoni mwenu, wakikusomeeni Aayaat za Rabb wenu, na wakikuonyeni kukutana na Siku yenu hii? Watasema: Ndio! Lakini neno la adhabu limethibiti juu ya makafiri”. [Az-Zumar: 71]
Juu ya moto wa Jahannam watakuwepo Malaika 19. Na hawa ni mbali na hao wengineo. Allaah Anatuambia:
"عَلَيْهَا تِسْعَةَ عَشَرَ"
“Juu yake wako (walinzi) kumi na tisa”. [Al-Muddath-thir: 30]
Namwomba Allaah ‘Azza wa Jalla Atuepushe tusije kuonana na viumbe hawa.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
52: Kazi Za Malaika
(15)- Malaika Wenye Kuwasaidia Manabii Na Mitume Na Kuwaangamiza Makafiri
Dalili toka kwenye Qur-aan na Hadiyth za Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) zinaonyeha kwamba Jibriyl (‘alayhis Salaam) alikuwa na jukumu la kuwasaidia, kuwatia nguvu na kuwanusuru Manabii na Mitume (‘alayhimus Salaam), lakini pia kupigana na maadui zao na kuwaangamiza. Allaah Ta’aalaa Anasema:
"وَإِن تَظَاهَرَا عَلَيْهِ فَإِنَّ اللَّـهَ هُوَ مَوْلَاهُ وَجِبْرِيلُ وَصَالِحُ الْمُؤْمِنِينَ ۖ وَالْمَلَائِكَةُ بَعْدَ ذَٰلِكَ ظَهِيرٌ"
“Na mkisaidiana dhidi yake, basi hakika Allaah Ndiye Mlinzi Msaidizi wake na Jibriyl na Waumini wema, na zaidi ya hayo, Malaika pia watasaidia”. [At-Tahriym: 04]
Allaah, Jibriyl, Waumini wema pamoja na Malaika, wote wanamsaidia Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Ikiwa hawa wote wako pamoja naye, basi ni nani ataweza kumdhuru?! Na hii ni fadhila kubwa na sharafu adhimu kwa Bwana wa Mitume Muhammad (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Aliyopewa na Mola wake.
Malaika huyu Jibriyl (‘Alayhis Salaam), Allaah Ta’aalaa Amemwelezea kama ni mwenye nguvu nyingi. Amesema:
"عَلَّمَهُ شَدِيدُ الْقُوَىٰ"
“Amemfunza (Jibriyl) mwenye nguvu shadidi”. [An-Najm: 05]
Yaani, aliyemfundisha Muhammad (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Qur-aan ni Jibriyl (‘alayhis Salaam) mwenye nguvu shadidi.
Inasimuliwa kwamba Malaika huyu Jibriyl, alin’goa miji au vijiji vya kaumu Lut, halafu akavipandisha hadi juu mbinguni, kisha akavipindua juu chini, vikaporomoka hadi chini ardhini. Allaah Anasema:
"وَالْمُؤْتَفِكَةَ أَهْوَىٰ"
“Na miji iliyopinduliwa, Ameiporomosha mbali mbali”. [An-Najm: 53]
Ibn Jariyr akiizungumzia aayah hii anasema kwamba hiyo ni miji ya Sodom na Gomorrah ya kaumu Lut, Allaah Aliiporomosha, Akamwamrisha Jibriyl (‘alayhis salaam) ainyanyue toka ardhi ya saba kwa ubawa wake hadi juu mbinguni, kisha aiporomoshe toka huko ikiwa chini juu.
Lakini pia, aliwapigia ukelele mmoja tu watu wa Thamud wakabaki majumbani mwao wameanguka kifudifudi (wamekufa).
Muhammad bin Ka’ab Al-Quradhiy amesema: “Jibriyl (‘alayhis salaam) alitumwa kwenda kwenye miji iliyopinduliwa ya kaumu Lut. Akaibeba kwa ubawa wake, halafu akapanda nayo juu kiasi cha hata wakazi wa mbinguni wakaweza kusikia sauti za mbwa wao wakibweka na sauti za kuku wao wakilia kwa hofu. Kisha Allaah Akaiandamizia kwa mawe kama Anavyosema:
"فَلَمَّا جَاءَ أَمْرُنَا جَعَلْنَا عَالِيَهَا سَافِلَهَا وَأَمْطَرْنَا عَلَيْهَا حِجَارَةً مِّن سِجِّيلٍ مَّنضُودٍ"
“Basi ilipokuja Amri Yetu, Tuliupindua (mji wao) juu chini, na Tukauteremshia mvua ya mawe ya udongo mgumu uliookwa yenye kuandamana”. Allaah Akaiangamiza pamoja na walio pembezoni mwa miji hii ambayo ilikuwa ni mitano”
Na wakati Allaah Ta’aalaa Alipomwokoa Muwsaa (‘alayhis salaam) pamoja na watu wake aliokuwa nao, na Akamwangamiza adui yao Firauni pamoja na askari na wafuasi wake, Jibriyl (‘alayhis salaam) alikuwepo hapo akisaidia. Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaah ‘anhumaa amesema: “Jibriyl alikuwa akishindilia tope la mchanga kwenye kinywa cha Firauni akihofia asije kutamka: “Laa Ilaah Illa Allaah”.
Kadhalika, Jibriyl (‘alayhis salaam) alimtia nguvu Nabiy ‘Iysaa (‘alayhis salaam) kama Anavyosema Allaah:
"وَأَيَّدْنَاهُ بِرُوحِ الْقُدُسِ"
“Na Tukamtia nguvu kwa Ruwhil-Qudus (Jibriyl (عليه السلام. [Al-Baqarah: 87]
Vile vile, Rasuli (Swalla Allaah (‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwombea Hassaan bin Thaabit (Radhwiya Allaah ‘anhu) kwamba Allaah Ta’aalaa Amtie nguvu kupitia Jibriyl katika kumtetea yeye kwa mashairi dhidi ya matusi ya Maquraysh.
Bibi ‘Aaishah amesema:
"كان ينافِحُ عن رَسولِ اللهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم"
“Alikuwa akimtetea Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) (kwa mashairi yake). [Muslim: (2490)]
Isitoshe, Allaah Ta’aalaa Alimtia nguvu Nabiy Wake Muhammad (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa pamoja na Waumini kupitia Jibriyl (‘alayhis salaam) katika baadhi ya vita.
Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaah ‘anhumaa) amesema kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema Siku ya Badr:
.
"هذا جِبريلُ [18] آخِذٌ برأسِ فَرَسِه، عليه أداةُ الحَربِ"
“Huyu ni Jibriyl, amekamata kichwa cha farasi wake, amevalia zana za kivita”. [Swahiyh Al-Bukhaariy: (3995)]
Hapa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwazindusha Maswahaba wake uwepo wa Jibriyl katika uwanja wa vita ili kuwapa ukakamavu na uimara zaidi, lakini pia kuwatuliza nyoyo.
Kadhalika, katika Vita vya Makundi, Siku ya Khandaq, Jibriyl pia aliwasaidia Waumini. Bibi ‘Aaishah amesema:
"فَلَمَّا رَجَعَ رَسولُ اللهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم مِنَ الخَنْدَقِ وَضَعَ السِّلَاحَ، فَاغْتَسَلَ، فأتَاهُ جِبْرِيلُ [18] وَهو يَنْفُضُ رَأْسَهُ مِنَ الغُبَارِ، فَقالَ: وَضَعْتَ السِّلَاحَ؟ وَاللَّهِ ما وَضَعْنَاهُ، اخْرُجْ إليهِم، فَقالَ رَسولُ اللهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم: فأيْنَ؟ فأشَارَ إلى بَنِي قُرَيْظَةَ، فَقَاتَلَهُمْ رَسولُ اللهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم، فَنَزَلُوا علَى حُكْمِ رَسولِ اللهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم، فَرَدَّ رَسولُ اللهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم الحُكْمَ فيهم إلى سَعْدٍ"
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliporejea toka Vita vya Khandaq, aliirejesha silaha yake mahala pake, kisha akaoga. Jibriyl akamjia huku akikun’guta vumbi kichwa chake. Akamuuliza: Umeweka silaha chini? Naapa kwa Allaah, sisi bado hatujaweka silaha chini, toka uwafuate. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamuuliza: Wapi? Akamwashiria kwenda kwa Baniy Quraydhwah. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akapambana nao mpaka wakasalimu amri kuwa chini ya utawala wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Halafu Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaurejeshea utawala kwa Sa’ad awaongoze”. [Al-Bukhaariy (4122) na Muslim (1769)]
Isitoshe, Malaika wa milima pia alikuja kumsaidia Rasuli kama angetaka baada ya kupopolewa mawe na watu wa Taif alipokwenda kuwalingania dini na kuomba hifadhi yao.
Bibi ‘Aaishah (Radhwiya Allaah ‘anhaa) alimuuliza Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:
"هَلْ أَتَى عَلَيْكَ يَوْمٌ كَانَ أَشَدَّ مِنْ يَوْمِ أُحُدٍ؟ قَالَ: لَقَدْ لَقِيتُ مِنْ قَوْمِكِ مَا لَقِيتُ، وَكَانَ أَشَدُّ مَا لَقِيتُ مِنْهُمْ يَوْمَ الْعَقَبَةِ، إِذْ عَرَضْتُ نَفْسِي عَلَى ابْنِ عَبْدِ يَالِيلَ بْنِ عَبْدِ كُلاَلٍ، فَلَمْ يُجِبْنِي إِلَى مَا أَرَدْتُ، فَانْطَلَقْتُ وَأَنَا مَهْمُومٌ عَلَى وَجْهِي، فَلَمْ أَسْتَفِقْ إِلاَّ وَأَنَا بِقَرْنِ الثَّعَالِبِ، فَرَفَعْتُ رَأْسِي، فَإِذَا أَنَا بِسَحَابَةٍ قَدْ أَظَلَّتْنِي، فَنَظَرْتُ فَإِذَا فِيهَا جِبْرِيلُ فَنَادَانِي فَقَالَ إِنَّ اللَّهَ قَدْ سَمِعَ قَوْلَ قَوْمِكَ لَكَ وَمَا رَدُّوا عَلَيْكَ، وَقَدْ بَعَثَ إِلَيْكَ مَلَكَ الْجِبَالِ لِتَأْمُرَهُ بِمَا شِئْتَ فِيهِمْ، فَنَادَانِي مَلَكُ الْجِبَالِ، فَسَلَّمَ عَلَىَّ ثُمَّ قَالَ يَا مُحَمَّدُ، فَقَالَ ذَلِكَ فِيمَا شِئْتَ، إِنْ شِئْتَ أَنْ أُطْبِقَ عَلَيْهِمِ الأَخْشَبَيْنِ، فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم بَلْ أَرْجُو أَنْ يُخْرِجَ اللَّهُ مِنْ أَصْلاَبِهِمْ مَنْ يَعْبُدُ اللَّهَ وَحْدَهُ لاَ يُشْرِكُ بِهِ شَيْئًا".
“Ee Rasuli wa Allaah! Je uliwahi kukutana na siku ngumu zaidi kuliko Siku ya Vita vya Uhud? Rasuli akasema: Hakika nimepata mateso mengi na adha nyingi sana toka kwa watu wako (Maquraysh). Lakini siku ngumu zaidi niliyopambana nayo toka kwao ilikuwa siku ya ‘Aqabah. Ni pale nilipojitambulisha kwa Ibn ‘Abdi Yaaliyla bin ‘Abdi Kulaal lakini hakunijibu matakwa yangu. Nikaondoka na huzuni kubwa mno, na sikuzindukana ila baada ya kufika Qarn Ath-Tha’aalib. Nikanyanyua kichwa changu na kushtukizwa kuona wingu limenifunika kwa kivuli chake. Nikaliangalia na tahamaki nikamwona Jibriyl ndani yake. Akaniita na kuniambia: Hakika Allaah ‘Azza wa Jalla Amesikia waliyokwambia watu wako, na majibu waliyokupa, na Yeye Amekutumia Malaika wa milima ili umwamuru lolote ulitakalo. Malaika wa milima akaniita na kunisalimia, kisha akasema: Ee Muhammad! Hakika Allaah Amesikia maneno waliyokwambia watu wako, na mimi ndiye Malaika wa milima, na Mola wako Amenituma kwako ili uniamuru lolote utakalo kwa watu hao. Ukitaka nitawafudikiza kwa milima miwili, basi nitawafudikiza. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: Bali ninatumai Allaah Atatoa toka kwenye migongo yao watakaomwabudu Allaah Peke Yake na hawatamshirikisha na chochote”. [Swahiyhul Bukhaariy (3231)]
Mwisho, tunauliza: Kuna hikma gani ya Malaika kupigana pamoja na Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wakati tunajua kwamba Jibriyl ana uwezo wa kuwaangamiza makafiri wote kwa unyoya mmoja tu wa ubawa wake?!
Jibu nakuachia mpenzi msomaji ulitafute mwenyewe.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
53: Nafasi Ya Malaika Kwa Waumini
(01)- Malaika Wanawapenda Waumini
Allaah Ta’aalaa kama Alivyo na sifa ya kupenda, pia vile vile Amewapa Malaika Wake sifa ya kuwapenda Waumini. Katika Hadiyth ya Abu Hurayrah (Radhwiya Allaah ‘anhu), Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إِنَّ اللَّهَ تَبَارَكَ وَتَعَالَى إِذَا أَحَبَّ عَبْدًا نَادَى جِبْرِيلَ: إِنَّ اللَّهَ قَدْ أَحَبَّ فُلاَنًا فَأَحِبَّهُ فَيُحِبُّهُ جِبْرِيلُ، ثُمَّ يُنَادِي جِبْرِيلُ فِي السَّمَاءِ: إِنَّ اللَّهَ قَدْ أَحَبَّ فُلاَنًا فَأَحِبُّوهُ، فَيُحِبُّهُ أَهْلُ السَّمَاءِ، وَيُوضَعُ لَهُ الْقَبُولُ فِي أَهْلِ الأَرْضِ"
“Allaah Anapompenda mja, Humnadia Jibriyl: Hakika Allaah Anampenda fulani, basi na wewe mpende, na yeye Jibriyl humpenda mtu huyo. Halafu naye Jibriyl huwanadia wakazi wa mbinguni (Malaika): Hakika Allaah Anampenda fulani, basi na nyinyi mpendeni, na wakazi hao wa mbinguni humpenda. Kisha huandikiwa maridhio kwa wakazi wa ardhi”. [Swahiyh Muslim (2637)]
Maridhio yanayokusudiwa hapa ni mapenzi ya watu kwake, yaani nyoyo zao zitajazwa mapenzi ya kumpenda yeye. Na watakaompenda ni Waumini, wachaMungu, si kila mmoja.
Bila shaka, kwa mfano, mwanamke akijua kwamba mume wake anampenda na anamtaja kwa jina kwa watu wake, ni furaha ilioje inayoingia ndani ya moyo wake! Na wewe ndugu yangu mtukufu! Unapojua kwamba mkuu wa nchi, au waziri, au mheshimiwa yeyote, au bosi wako amekupenda na akakutaja mbele ya baraza lake, je, furaha yako inakuwaje? Basi hali itakuwa vipi ikiwa Allaah Mola wa mbingu na ardhi Ndiye Aliyekupenda, na Akalitaja jina lako kwa Jibriyl, na kisha Jibriyl naye akawajuza Malaika wote wa mbinguni, na akawatajia jina lako, ukawa umejulikana kote huko, na akawataka nao wakupende, ni hadhi na furaha ilioje hiyo?!
Basi hongera kwa wale ambao Allaah ‘Azza wa Jalla Amewapenda, na Akawaamrisha Malaika Wake wampende, na akaandikiwa kupendwa na watu wa ardhi. Na hawa ni wachaji na watenda mema wenye kupita juu ya njia Yake iliyonyooka.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
54: Nafasi Ya Malaika Kwa Waumini
(02)– Malaika Wanawatia Nguvu Waumini Na Kuwaelekeza
Jibriyl (‘alayhis salaam) alimtia nguvu Nabiy ‘Iysaa (‘alayhis salaam) katika jukumu la kuwafikishia Baniy Israaiyl Dini ya Allaah. Allaah Anasema:
"وَآتَيْنَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ الْبَيِّنَاتِ وَأَيَّدْنَاهُ بِرُوحِ الْقُدُسِ"
“Na Tukampa ‘Iysaa mwana wa Maryam hoja bayana na Tukamtia nguvu kwa Ruwhil-Qudus (Jibriyl (عليه السلام”. [Al-Baqarah: 87]
Mufassiruna wengi wamesema kwamba “Ruwhul Qudus” ni Jibriyl (‘alayhis salaam).
Toka kwa Hassaan bin Thaabit (Radhwiya Allaah ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia:
"يا حَسَّانُ، أجِبْ عن رسولِ اللهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم، اللهُمَّ أيِّدْه برُوحِ القُدُسِ"
“Ee Hassaan! Mtetee (kwa mashairi) Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) . Ee Allaah! Mtie nguvu kwa Ruwhul Qudus”. [Swahiyhul Bukhaariy (3212]
Ibn Hubayrah amesema: “Hadiyth hii ni dalili kwamba Allaah Anaweza kumtia nguvu mshairi kupitia kwa Jibriyl (‘alayhis salaam) kwa kumlinda na shetani asije kupenyeza maneno yasiyofaa kwenye ulimi wake.
Toka kwa Abu Hurayrah: Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"لأطوفَنَّ الليلةَ بمائةِ امرأةٍ، تَلِدُ كُلُّ امرأةٍ غُلامًا يقاتِلُ في سَبيلِ اللهِ. فقال له الملَكُ: قُلْ: إن شاء اللهُ، فلم يقُلْ، ونَسِيَ، فأطاف بهِنَّ، ولم تلِدْ إلَّا امرأةٌ منهنَّ نِصفَ إنسانٍ. قال النَّبيُّ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم: لو قال: إن شاء اللهُ، لم يحنَثْ، وكان أرجى لحاجَتِه"
“Kwamba Sulaymaan (‘alayhis salaam) alisema: (Naapa kwa Allaah) nitawazungukia (nitawaingilia) wanawake 100, na kila mwanamke atazaa kijana atakayepigana katika Njia ya Allaah. Malaika akamwambia: Sema In Shaa Allaah. Hakusema (kwa ulimi) na akasahau. Akawazungukia, na hakuna aliyezaa kati yao isipokuwa mmoja tu aliyezaa nusu mtu”. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: Kama angelisema In Shaa Allaah, basi tarajio lake lisingepita tupu, na neno hilo lingempa matumaini zaidi ya haja yake”. [Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (3424) na Muslim (1654)]
Hapa tunaona namna Malaika alivyomkumbusha na kumwelekeza Nabiy Sulaymaan (‘alayhis salaam) atamke neno hilo. Neno hilo alilisemea moyoni akalitegemeza kwa Allaah, lakini hakulitamka ulimini, kwani haiwezekani Nabiy kama yeye kughafilika na jambo kama hilo. Na matokeo yake yakawa ndiyo hayo, hakuna aliyezaa isipokuwa huyo mmoja tu aliyezaa nusu mtu. Hiyo pia ni katika mitihani ya Allaah kwa Waja Wake na mafunzo kwao.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
55: Nafasi Ya Malaika Kwa Waumini
(03)– Malaika Wanawaombea Dua Waumini
Allaah Ta’aalaa Ametueleza kwamba Malaika Wake wanamswalia Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) pale Aliposema:
"إِنَّ اللَّـهَ وَمَلَائِكَتَهُ يُصَلُّونَ عَلَى النَّبِيِّ"
”Hakika Allaah na Malaika Wake Wanamswalia Nabiy”. [Al-Ahzaab: 56]
Ametueleza tena kwamba Malaika hao wanawaswalia Waumini pia Aliposema:
"هُوَ الَّذِي يُصَلِّي عَلَيْكُمْ وَمَلَائِكَتُهُ لِيُخْرِجَكُم مِّنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ ۚ وَكَانَ بِالْمُؤْمِنِينَ رَحِيمًا"
“Yeye (Allaah) Ndiye Anakurehemuni, na Malaika Wake (wanakuombeeni maghfirah na rahmah) ili Akutoeni kutoka katika viza kuingia katika Nuru. Naye daima Ni Mwenye Kurehemu Waumini”. [Al-Ahzaab: 43]
Maana ya Allaah kuwaswalia Waja Wake ni kuwasifia na kuwataja vyema kwa Malaika Wake. Ama Malaika kuwaswalia waja, ni kuwaombea rahmah na maghfirah, na hili lina athari njema kwa Waumini ambapo kama inavyoeleza aayah hii, ni kwamba linapelekea Waumini kutolewa kwenye giza la ukafiri na kuingizwa kwenye nuru ya iymaan.
As-Sa’adiy amesema: “Kati ya Rehma Zake na Upole Wake kwa Waumini, Allaah Amejaalia Yeye kuwasifia kwa Malaika Wake, na Malaika hao kuwaombea maghfira na rahmah kuwa ni sababu ya kuwatoa toka kwenye giza za madhambi na ujinga kwenda kwenye nuru ya iymaan, elimu, utendaji mwema wa amali, na kuwezeshwa kwa yanayomridhisha Allaah. Hii ni moja kati ya neema kubwa kabisa ambazo Allaah Amewaneemesha kwazo Waja Wake watiifu ambazo zinawazindusha wazishukuru na wakithirishe kumdhukuru Allaah Aliyewatunuku.
Yafuatayo ni miongoni mwa mambo ambayo yatakuingiza ndani ya wigo wa kuombewa maghfirah na Malaika.
1- Kusubiri swala ya jamaa msikitini na kukaa baada ya kumalizika swala. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anasema:
"إِنَّ الْمَلاَئِكَةَ تُصَلِّي عَلَى أَحَدِكُمْ مَا دَامَ فِي مُصَلاَّهُ الَّذِي صَلَّى فِيهِ مَا لَمْ يُحْدِثِ : اللَّهُمَّ اغْفِرْ لَهُ، اللَّهُمَّ ارْحَمْهُ"
“Hakika Malaika wanamwombea mmoja wenu madhali amebakia sehemu yake aliyoswalia na kuwa hajatengukwa na wudhuu wake. (Wanasema): Ee Allaah, Mghufurie, ee Allaah Mrehemu”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (659) na Muslim (649)]
Mwanamke anaweza kuipata fadhila hii kama atakuwa na sehemu yake mahsusi ya kuswalia nyumbani kwake.
2- Kuswali safu ya kwanza.
Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anasema:
"إِنَّ اللَّهَ وَمَلَائِكَتَهُ يُصَلُّونَ عَلَى الصَّفِّ الْأَوَّلِ"
“Hakika Allaah na Malaika Wake Huwaswalia wanaoswali safu ya kwanza”. [Hadiyth Swahiyh. Swahiyh Ibn Maajah]
Kuwaswalia hapa kuna maana ya kwamba, kwa upande wa Allaah ni kuwasifu na kuwarehemu, na kwa Malaika ni kuwaombea maghfirah.
3- Kutafuta ‘ilmu.
Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anasema:
"مَنْ سَلَكَ طَرِيقًا يَطْلُبُ فِيهِ عِلْمًا سَلَكَ اللَّهُ بِهِ طَرِيقًا مِنْ طُرُقِ الْجَنَّةِ وَإِنَّ الْمَلاَئِكَةَ لَتَضَعُ أَجْنِحَتَهَا رِضًا لِطَالِبِ الْعِلْمِ وَإِنَّ الْعَالِمَ لَيَسْتَغْفِرُ لَهُ مَنْ فِي السَّمَوَاتِ وَمَنْ فِي الأَرْضِ وَالْحِيتَانُ فِي جَوْفِ الْمَاء"
“Mwenye kupita njia kwa lengo la kutafuta ‘ilmu, basi Allaah Atampitisha kwayo njia katika njia za Peponi. Na kwa hakika Malaika hushusha mbawa zao kuonyesha kufurahishwa kwao na mwanafunzi mtafutaji ‘ilmu. Na kwa hakika (pia), aliyeelimika, huombewa maghfirah na walioko mbinguni na walioko ardhini, na (hata) samaki walioko ndani ya kina cha maji”. [Sunan Abu Daawuwd].
Angalia hapa, si tu kwamba anapewa hishma kubwa na Malaika ya kushushiwa mbawa zao, bali hata viumbe vyote vilivyoko mbinguni kati ya Malaika wengineo wakiwemo wale wabebao ‘Arshi ya Allaah, pamoja na viumbe vinginevyo tusivyovijua huko, mbali na viumbe vyote vilivyoko ardhini hata vile tunavyovidharau kama nzi, panya, chawa na kadhalika, isitoshe na vyote vilivyoko ardhini, -vyote hivyo kwa wingi wote huo wa idadi isiyoweza kukokotoleka- vinamwombea maghfirah mwanafunzi anayetafuta ‘ilmu. Na ‘ilmu inayolengwa hapa ni ‘ilmu ya dini, kwani hiyo ndiyo itakayomwongoza Muislamu katika ‘aqiydah safi, atajua vyema mambo yote ya ‘ibaadah kuanzia twahara, swala, zakah, funga, hijja na mengineyo yote kuhusu kusoma Qur-aan kama inavyotakikana, Hadiyth za Rasuli na kadhalika. Haya ndiyo yatakayomfanya kuishi kwa amani hapa duniani na kesho aakhirah.
4- Kufundisha watu mambo ya kheri.
Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anasema:
"إِنَّ اللَّهَ وَمَلاَئِكَتَهُ وَأَهْلَ السَّمَوَاتِ وَالأَرْضِ حَتَّى النَّمْلَةَ فِي جُحْرِهَا وَحَتَّى الْحُوتَ لَيُصَلُّونَ عَلَى مُعَلِّمِ النَّاسِ الْخَيْرَ"
“Hakika Allaah na Malaika Wake, pamoja na wakazi wa mbingu na ardhi, hata mdudu chungu katika shimo lake, na hata samaki, wanamwombea mwenye kuwafundisha watu mambo ya kheri”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na At-Tirmidhiy (2685) na At-Twabaraaniy (8/278)]
Mwalimu wa mambo ya kheri anayekusudiwa hapa ni Mwanachuoni, kwani yeye huwafundisha watu Maamrisho ya Allaah na kuwaonyesha Makatazo Yake ili wayaepuke, na mambo mengineyo yatakayowafaa katika dunia yao na aakhirah yao.
Ni wangapi kati yao wameshafariki zamani, lakini elimu zao hadi leo zinaendelea kuwanufaisha Waislamu. Na hii ina maana kuwa bado nao wanaendelea kuombewa na wote waliotajwa katika Hadiyth hii ingawa wako makaburini!
Lakini pia, hata yeyote anayesambaza elimu ya dini kwa njia ya mitandao kama tunavyoona vijana wetu hivi leo, basi wanaingia ndani ya duara la wigo huu, kuanzia wanaotarjumi, wanao-edit, wanaosambaza na kadhalika. Allaah Awalipe wote jazaa njema.
5- Kumswalia Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam)
Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"مَا مِنْ مُسْلِمٍ يُصَلِّي عَلَىَّ إِلاَّ صَلَّتْ عَلَيْهِ الْمَلاَئِكَةُ مَا صَلَّى عَلَىَّ فَلْيُقِلَّ الْعَبْدُ مِنْ ذَلِكَ أَوْ لِيُكْثِرْ"
“Hakuna Muislamu yeyote anayeniswalia isipokuwa Malaika nao humswalia madhali anaendelea kuniswalia. Basi na mja afanye uchache kwa hilo, au akithirishe”. [Hadiyth Hasan. Ibn Maajah]
6- Kumzuru mgonjwa
Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anasema:
"مَا مِنْ رَجُلٍ يَعُودُ مَرِيضًا مُمْسِيًا إِلاَّ خَرَجَ مَعَهُ سَبْعُونَ أَلْفَ مَلَكٍ يَسْتَغْفِرُونَ لَهُ حَتَّى يُصْبِحَ وَكَانَ لَهُ خَرِيفٌ فِي الْجَنَّةِ وَمَنْ أَتَاهُ مُصْبِحًا خَرَجَ مَعَهُ سَبْعُونَ أَلْفَ مَلَكٍ يَسْتَغْفِرُونَ لَهُ حَتَّى يُمْسِيَ وَكَانَ لَهُ خَرِيفٌ فِي الْجَنَّةِ"
“Hakuna mtu yeyote anayemzuru mgonjwa wakati wa jioni, isipokuwa hutoka pamoja naye Malaika elfu sabini wanaomwombea maghfira mpaka apambaukiwe asubuhi, na atapata pia bustani iliyosheheni matunda Peponi. Na atakayemwendea asubuhi, hutoka pamoja naye Malaika elfu sabini wanaomwombea maghfira mpaka jioni, na atapata bustani iliyosheheni matunda Peponi”. [Hadiyth Hasan. Swahiyh Abu Daawuwd]
7- Wanaokula daku
Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anasema:
"إنَّ اللهَ وَمَلائِكَتَهُ يُصَلُّوْنَ عَلَى المُتَسَحِّرِيْنَ"
“Hakika Allaah na Malaika Wake wanawaswalia wenye kula daku”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Ibn Hibaan (3467)]
Kuswaliwa na Allaah kuwasifu na kuwarehemu, na Malaika ni kuombewa maghfirah kwa Allaah.
Daku ni barakah. Si lazima kula mlo kamili wa shibe, bali inatosha hata kwa funda la maji ili kupata kusifiwa na Allaah na kuombewa maghfirah na Malaika Wake.
Alhidaaya.com [3]
56: Nafasi Ya Malaika Kwa Waumini
(04)– Malaika Wanaitikia “Aamiyn” Kwa Dua Za Waumini
Malaika huitikia “aamiyn” kwa du’aa wanazoomba Waumini. Na kwa kuitikia huku, du’aa inakuwa karibu zaidi kujibiwa kwa Idhni ya Allaah Ta’aalaa.
Katika Hadiyth iliyopokelewa na Abud Dardaai (Radhwiya Allaah ‘anhu), Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"دعوةُ الْمُسْلِمِ لِأَخِيهِ بِظَهْرِ الْغَيْبِ مُسْتَجَابَةٌ عِنْدَ رَأْسِهِ مَلَكٌ مُوَكَّلٌ كُلَّمَا دَعَا لِأَخِيهِ بِخَيْرٍ قَالَ الْمَلَكُ الْمُوَكَّلُ بِهِ: آمِينَ وَلَكَ بِمِثْلٍ"
“Du’aa ya siri ya mtu Muislamu kwa nduguye ni yenye kujibiwa. Huwepo Malaika mteuliwa kwenye kichwa chake, kila anapomwombea nduguye kheri, Malaika huyu mteuliwa kwa ajili yake husema: “Aamiyn”, na wewe upate kama hilo”. [Hadiyth Swahiyh. Imesimuliwa na Muslim]
Toka kwa Ummu Salamah: “Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إِذَا حَضَرْتُمُ الْمَرِيضَ أَو الْمَيِّت فَقولُوا خيرا فَإِن الْمَلَائِكَةَ يُؤَمِّنُونَ عَلَى مَا تَقُولُونَ"
“Mkiwepo kwa mgonjwa au maiti, basi waombeeni kheri, kwani Malaika huitikia “aamiyn” kwa mnaloliomba”. [Hadiyth Swahiyh. Muslim (919)]
“Aamiyn maana yake ni: “Ee Allaah, Itikia”.
Abul ‘Abbaas Al-Qurtubiy kasema: “Ulamaa wetu wanapendelea watu watakaokuwepo karibu na mtu wakati anapokaribia kufariki, wawe ni watu wema na watu wa kheri ili wapate kumkumbusha, na wamwombee yeye pamoja na ndugu na jamaa zake wahusika yaliyo ya kheri, kwani hapo itakutana du’aa yao na itikio la “aamiyn” la Malaika, na hivyo basi maiti pamoja na ndugu na jamaa zake hufaidika”.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
57: Nafasi Ya Malaika Kwa Waumini
(05)– Malaika Wanawaombea Maghfirah Waumini
Allaah Ta’aalaa Anatueleza katika Qur-aan Tukufu kwamba Malaika Wake wanawaombea maghfirah walioko ardhini Akituambia:
"تَكَادُ السَّمَاوَاتُ يَتَفَطَّرْنَ مِن فَوْقِهِنَّ ۚ وَالْمَلَائِكَةُ يُسَبِّحُونَ بِحَمْدِ رَبِّهِمْ وَيَسْتَغْفِرُونَ لِمَن فِي الْأَرْضِ ۗ أَلَا إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ"
“Zinakaribia mbingu kuraruka moja juu ya nyingine, na Malaika wanasabbih na kumhimidi Rabb wao, na wanawaombea maghfirah walioko ardhini. Tanabahi! Hakika Allaah Ndiye Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu”. [Ash-Shuwraa: 05]
Wanaoombewa bila shaka ni Waumini walioko kwenye njia iliyonyooka ambayo inamridhisha Allaah, na si watu wote. Hii ni katika Fadhla kubwa za Allaah kwetu ikiwa tutashikamana na Maamrisho Yake na kujiepusha na Makatazo Yake. Inakuwa ni zawadi kwetu kwa kuwajibika huko.
Malaika wenye kufanya hivyo ni wale wenye kubeba ‘Arshi ya Allaah Ta’aalaa kama Anavyotuambia:
"الَّذِينَ يَحْمِلُونَ الْعَرْشَ وَمَنْ حَوْلَهُ يُسَبِّحُونَ بِحَمْدِ رَبِّهِمْ وَيُؤْمِنُونَ بِهِ وَيَسْتَغْفِرُونَ لِلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا وَسِعْتَ كُلَّ شَيْءٍ رَّحْمَةً وَعِلْمًا فَاغْفِرْ لِلَّذِينَ تَابُوا وَاتَّبَعُوا سَبِيلَكَ وَقِهِمْ عَذَابَ الْجَحِيمِ"
“(Malaika) ambao wanabeba ‘Arsh na walio pembezoni mwake, wanasabbih na kumhimidi Rabbi wao, na wanamwamini, na wanawaombea maghfirah wale walioamini (wakisema): Rabb wetu! Umekienea kila kitu kwa rahmah na ujuzi, basi Waghufurie wale waliotubu, na wakafuata njia Yako, na Wakinge na adhabu ya moto uwakao vikali mno”. [Ghaafir: 07]
Baadhi ya Mufassiruna wamesema kwamba si wanaobeba ‘Arshi tu, bali ni Malaika wote.
Al-Qurtubiy amesema: “Yahyaa bin Mu’aadh Ar-Raaziy aliwaambia wenzake kuhusiana na aayah hii: Ifahamuni vyema, kwani hakuna kinga duniani kote yenye kutumainiwa zaidi kuliko aayah hii. Hakika Malaika mmoja tu, lau atamwomba Allaah Awaghufurie Waumini wote, basi Atawaghufiria. Basi hali ikoje ikiwa Malaika wote pamoja na wabebao ‘Arshi wanawaombea maghfirah Waumini?!”
Naye Khalaf bin Hishaam Al-Bazzaaz Al-Qaariy amesema: “Nilikuwa namsomea Saliym bin ‘Iysaa. Nilipofika:
وَيَسْتَغْفِرُونَ لِلَّذِينَ آمَنُوا
“Na wanawaombea maghfirah wale walioamini” alilia, kisha akasema: Ee Khalaf! Ni utukuzo ulioje wa Muislamu kwa Allaah! Yuko amelala kitandani mwake na huku Malaika Wake wanamwombea maghfirah!”
Na Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anasema:
"إِنَّ الْمَلاَئِكَةَ تُصَلِّي عَلَى أَحَدِكُمْ مَا دَامَ فِي مُصَلاَّهُ الَّذِي صَلَّى فِيهِ مَا لَمْ يُحْدِثِ : اللَّهُمَّ اغْفِرْ لَهُ، اللَّهُمَّ ارْحَمْهُ"
“Hakika Malaika wanamwombea mmoja wenu madhali amebakia sehemu yake aliyoswalia na kuwa hajatengukwa na wudhuu wake. (Wanasema): Ee Allaah Mghufurie, ee Allaah Mrehemu”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (659) na Muslim (649)]
Malaika
Alhidaaya.com [3]
58: Nafasi Ya Malaika Kwa Waumini
(06)– Malaika Wanahudhuria Vikao Vya Ki’ilmu, Halaqah Za Dhikri, Na Huwafunika Wahusika Kwa Mbawa Zao
Abu Hurayrah amesema: Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إِنَّ لِلَّهِ مَلاَئِكَةً يَطُوفُونَ فِي الطُّرُقِ، يَلْتَمِسُونَ أَهْلَ الذِّكْرِ، فَإِذَا وَجَدُوا قَوْمًا يَذْكُرُونَ اللَّهَ تَنَادَوْا هَلُمُّوا إِلَى حَاجَتِكُمْ. قَالَ: فَيَحُفُّونَهُمْ بِأَجْنِحَتِهِمْ إِلَى السَّمَاءِ الدُّنْيَا"
“Hakika Allaah Ana Malaika wanaozunguka majiani kuwatafuta watu wa dhikri. Wanapowapata watu wanaomdhukuru Allaah huitana wakisema: Haya njooni kwenye lile mlitafutalo. Na hapo huwazungushia mbawa zao hadi kwenye mbingu ya dunia”. [Swahiyhul Bukhaariy (6408)]
Abu Hurayrah amesema tena: Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"مَا اجْتَمَعَ قَوْمٌ فِي بَيْتٍ مِنْ بُيُوتِ اللَّهِ تَعَالَى يَتْلُونَ كِتَابَ اللَّهِ وَيَتَدَارَسُونَهُ بَيْنَهُمْ إِلاَّ نَزَلَتْ عَلَيْهِمُ السَّكِينَةُ وَغَشِيَتْهُمُ الرَّحْمَةُ وَحَفَّتْهُمُ الْمَلاَئِكَةُ وَذَكَرَهُمُ اللَّهُ فِيمَنْ عِنْدَهُ ".
“Hawakusanyiki watu katika Nyumba yoyote katika Nyumba za Allaah ili kusoma na kufundishana Kitabu cha Allaah, isipokuwa huwateremkia utulivu, rahmah huwafunika, Malaika huwazunguka, na Allaah Huwataja kwa wale walio Kwake (Malaika)”. [Muslim (2699)]
Amali njema ndio sababu ya Malaika kuwa karibu na Waumini. Na lau kama Waumini wangeendelea kuwa katika hali ya juu kabisa ya utakasifu wa kiroho, basi wangelifikia ngazi ya kuweza kuwaona Malaika, kusalimiana nao na kupeana nao mikono. Imepokelewa toka kwa Handhwalah Al-Usaydiy kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"الَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لَوْ تَدُومُونَ عَلَى مَا تَكُونُونَ عِنْدِي وَفِي الذِّكْرِ لَصَافَحَتْكُمُ الْمَلَائِكَةُ عَلَى فُرُشِكُمْ وَفِي طُرُقِكُمْ وَلَكِنْ يَا حَنْظَلَةُ سَاعَةٌ وَسَاعَةٌ"
“Naapa kwa Yule Ambaye Nafsi yangu iko Mkononi Mwake, lau mtadumu na hali mnayokuwa nayo wakati mnapokuwa kwangu na katika kumdhukuru Allaah, basi Malaika wangeliwapeni mikono mkiwa vitandani mwenu na majiani mwenu. Lakini, ee Handhwalah, kuna saa (ya kusabilia moyo wako wote kwa Allaah) na kuna saa (ya kushughulikia mambo ya dunia yako)”. [Muslim: 43]
Malaika
Alhidaaya.com [3]
59: Nafasi Ya Malaika Kwa Waumini
(07)– Malaika Wanasajili Majina Ya Wenye Kuhudhuria Swalah Ya Ijumaa
Malaika wanahudhuria Misikitini Siku ya Ijumaa na kusimama kwenye milango yake ili kuwasajili wanaoingia mmoja baada ya mwingine.
Abu Hurayrah: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إِذَا كَانَ يَوْمُ الْجُمُعَةِ وَقَفَتِ الْمَلَائِكَةُ عَلَى بَابِ الْمَسْجِدِ يَكْتُبُونَ الْأَوَّلَ فَالْأَوَّلَ"
“Inapokuwa Siku ya Ijumaa, Malaika husimama kwenye milango ya Msikiti na kuwasajili (wanaoingia) mmoja baada ya mwingine”. [Al-Bukhaariy na Muslim]
Toka kwa Abu Hurayrah: Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
إِذَا كَانَ يَوْمُ الْجُمُعَةِ، وَقَفَتِ الْمَلاَئِكَةُ عَلَى باب الْمَسْجِدِ يَكْتُبُونَ الأَوَّلَ فَالأَوَّلَ، فَإِذَا خَرَجَ الإِمَامُ طَوَوْا صُحُفَهُمْ، وَيَسْتَمِعُونَ الذِّكْرَ"
“Inapokuwa Siku ya Ijumaa, Malaika husimama kwenye mlango wa Msikiti na kusajili (wanaoingia) mmoja baada ya mwingine. Na khatibu anapochomoza, huyakunja madaftari yao na kusikiliza khutba (na yaliyomo humo katika utajo wa Allaah)”. [Al-Bukhaariy (881) na Muslim (850)]
Rasuli (Swalla Allaah ‘;alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"مَنِ اغْتَسَلَ يَوْمَ الْجُمْعَةِ غُسْلَ الْجَنَابَةِ، ثُمَّ رَاحَ فِي السَّاعَةِ الأُوْلَى فَكَأَنَّمَا قَرَّبَ بَدَنَةً، وَمَنْ رَاحَ فِي السَّاعَةِ الثَّانِيَةِ، فَكَأَنَّمَا قَرَّبَ بَقَرَةً، وَمَنْ رَاحَ فِي السَّاعَةِ الثَّالِثَةِ، فَكَأَنَّمَا قَرَّبَ كَبْشًا أَقْرَنَ، وَمَنْ رَاحَ فِي السَّاعَةِ الرَّابِعَةِ فَكَأَنَّمَا قَرَّبَ دَجَاجَةً، وَمَنْ رَاحَ فِي السَّاعَةِ الْخَامِسَةِ فَكَأَنَّمَا قَرَّبَ بَيْضَةً، فَإِذَا خَرَجَ الإِمَامُ حَضَرَتِ الْمَلاَئِكَةُ يَسْتَمِعُونَ الذِّكْرَ "
“Mwenye kuoga kikamilifu siku ya Ijumaa kama anavyofanya katika ghuslu ya janaba, kisha akaenda (Msikitini) katika saa la mwanzo, basi anakuwa kama ametoa swadaqah ngamia, na mwenye kwenda saa la pili, anakuwa kama ametoa swadaqah ng’ombe, na mwenye kwenda saa la tatu, anakuwa kama ametoa swadaqah kondoo dume mwenye pembe, na mwenye kwenda saa la nne, anakuwa kama ametoa swadaqah kuku, na mwenye kwenda saa la tano, anakuwa kama ametoa swadaqah yai. Na Imamu anapotokeza (akapanda mimbari), Malaika huingia na kuketi kusikiliza utajo”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (881) na Muslim (850)]
An-Nawawiy amesema: “Malaika hawa si wale wenye kumlinda mtu, bali hawa ni maalum kwa kusajili wanaohudhuria Swalaatul Jum’ah”.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
60: Nafasi Ya Malaika Kwa Waumini
(08)– Malaika Wanasajili Maneno Mema Wanayotamka Waja
Imepokelewa toka kwa Rifa’ah bin Raafi Az-Zuraqiy (Radhwiya Allaah ‘anhu):
قَالَ كُنَّا يَوْمًا نُصَلِّي وَرَاءَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَلَمَّا رَفَعَ رَأْسَهُ مِنَ الرَّكْعَةِ قَالَ " سَمِعَ اللَّهُ لِمَنْ حَمِدَهُ ". قَالَ رَجُلٌ وَرَاءَهُ رَبَّنَا وَلَكَ الْحَمْدُ، حَمْدًا كَثِيرًا طَيِّبًا مُبَارَكًا فِيهِ، فَلَمَّا انْصَرَفَ قَالَ " مَنِ الْمُتَكَلِّمُ ". قَالَ أَنَا. قَالَ " رَأَيْتُ بِضْعَةً وَثَلاَثِينَ مَلَكًا يَبْتَدِرُونَهَا، أَيُّهُمْ يَكْتُبُهَا أَوَّلُ "
“Tulikuwa siku moja tunaswali nyuma ya Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na aliponyanyua kichwa chake toka kwenye rukuu alisema: Sami’a Allaah liman hamidah (Allaah Amemsikia aliyemhimidi). Mtu mmoja nyuma yake akasema: Rabbanaa walakal hamdu, hamdan kathiyran mubaarakan fiyh (Ee Mola wetu, ni Yako himdi, himdi nyingi njema iliyo na baraka ndani yake). Alipomaliza swalah akauliza: Nani aliyetamka? Nikasema: Ni mimi. Akasema: Nimewaona Malaika thelathini na kidogo hivi wakilishindania, nani awe wa mwanzo kuliandika kabla ya mwenziye”. [Swahiyhul Bukhaariy (799)]
Hadiyth hii inatufunza fadhla kubwa ya kumhimidi Allaah na kumdhukuru, na pia uhalali kwa maamuma kusoma dhikri kwa sauti kidogo nyuma ya imamu bila kumbughudhi aliye karibu yake.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
61: Nafasi Ya Malaika Kwa Waumini
(09)– Malaika Wanapokezana Zamu Usiku Na Mchana Kuwafuatilia Waumini
Kuna Malaika wanaozunguka kwenye njia na barabara kutafuta vikao vya dhikri. Kuna wengineo wanaohudhuria Swalah za Ijumaa na Swalah za jamaa kwa zamu; kundi moja linakuja na jingine linaondoka. Kadhalika, Malaika hawa hukusanyika pamoja katika Swalah ya Alfajiri na Swalah ya Alasiri.
Toka kwa Abu Hurayrah: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"يَتَعَاقَبُونَ فِيكُمْ مَلاَئِكَةٌ بِاللَّيْلِ وَمَلاَئِكَةٌ بِالنَّهَارِ وَيَجْتَمِعُونَ فِي صَلاَةِ الْفَجْرِ وَصَلاَةِ الْعَصْرِ ثُمَّ يَعْرُجُ الَّذِينَ بَاتُوا فِيكُمْ فَيَسْأَلُهُمْ رَبُّهُمْ وَهُوَ أَعْلَمُ بِهِمْ كَيْفَ تَرَكْتُمْ عِبَادِي فَيَقُولُونَ تَرَكْنَاهُمْ وَهُمْ يُصَلُّونَ وَأَتَيْنَاهُمْ وَهُمْ يُصَلُّونَ"
Wanaandamana kwa zamu kwenu Malaika usiku na Malaika mchana, na wote hao wanajumuika katika Swalah ya Alfajiri na Swalah ya Alasiri, kisha wale waliokesha kwenu hupanda na Mola wao Huwauliza ilhali Yeye Anajua zaidi hali yao: Vipi mmewaacha Waja Wangu? Malaika hujibu: Tumewaacha wakiwa wanaswali, na tumewajia wakiwa wanaswali”. [Al-Bukhaariy (7486) na Muslim (632)]
Huenda Malaika hawa ndio wale wanaopandisha amali za waja kwa Allaah Ta’alaa. Toka kwa Abu Muwsaa Al-Ash’ariyy:
"قَامَ فِينَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِخَمْسِ كَلِمَاتٍ فَقَالَ: "إِنَّ اللَّهَ عز وَجل لَا يَنَامُ وَلَا يَنْبَغِي لَهُ أَنْ يَنَامَ يَخْفِضُ الْقِسْطَ وَيَرْفَعُهُ يُرْفَعُ إِلَيْهِ عَمَلُ اللَّيْلِ قَبْلَ عَمَلِ النَّهَارِ وَعَمَلُ النَّهَارِ قَبْلَ عَمَلِ اللَّيْل"
Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisimama baina yetu na kutuambia maneno matano: Hakika Allaah ‘Azza wa Jalla Halali na haiwezekaniki Akalala, Anaishusha mizani na Anaipandisha, hupandishwa Kwake amali za usiku kabla ya amali za mchana, na amali za mchana kabla ya amali za usiku”. [Muslim: (179)]
Allaah Ta’aalaa Ameipa utukuzo mkubwa Swalah ya Alfajiri. Ametueleza kwamba Malaika Wake wanaihudhuria Swalah hii Aliposema:
"أَقِمِ الصَّلَاةَ لِدُلُوكِ الشَّمْسِ إِلَىٰ غَسَقِ اللَّيْلِ وَقُرْآنَ الْفَجْرِ ۖ إِنَّ قُرْآنَ الْفَجْرِ كَانَ مَشْهُودًا"
“Simamisha Swalaah jua linapopinduka hadi kiza cha usiku na Qur-aan ya (Swalaah ya) Alfajiri. Hakika Qur-aan ya Alfajiri ni yenye kushuhudiwa”. [Al-Israa: 78]
Ibn Jariyr amesema: “Qur-aan inayosomwa katika Swalah ya Alfajiri inakuwa ni yenye kushuhudiwa. Wanaishuhudia Malaika wa usiku na Malaika wa mchana”.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
62: Nafasi Ya Malaika Kwa Waumini
(10)– Malaika Wanateremka Wakati Muumini Anasoma Qur-aan
Hali hii inatokea pale Muumini anapoisoma Qur-aan kwa ikhlaas na tartiyl makini, anapohudhurisha moyo wake, anapoizingatia ipasavyo, na anapokuwa mnyenyekevu kwayo.
Toka kwa Al-Baraa bin ‘Aazib (Radhwiya Allaah ‘anhu):
"قَرَأَ رَجُلٌ الْكَهْفَ وَفِي الدَّارِ دَابَّةٌ، فَجَعَلَتْ تَنْفِرُ فَنَظَرَ فَإِذَا ضَبَابَةٌ أَوْ سَحَابَةٌ قَدْ غَشِيَتْهُ، قَالَ: فَذَكَرَ ذَلِكَ لِلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ: اقْرَأْ فُلاَنُ، فَإِنَّهَا السَّكِينَةُ تَنَزَّلَتْ عِنْدَ الْقُرْآنِ أَوْ تَنَزَّلَتْ لِلْقُرْآنِ"
“Mtu mmoja alisoma Al-Kahf, na nyumbani kwake alikuwepo farasi, farasi akaanza kuchacharika. Mtu yule akaangalia, na ghafla akaona wingu limemfunika. Kisha akaenda kumweleza Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Rasuli akamwambia: Laiti ungeendelea kusoma, kwa kuwa hao walikuwa ni Malaika waliojawa utulivu, nao huteremka kwa kuandamana wakati Qur-aan inasomwa, au wanateremka kwa ajili ya Qur-aan.” [Swahiyh Muslim: (795)].
Abul ‘Abbaas Al-Qurtubiy amesema: “Neno السكينةُ katika Hadiyth, ni jina la Malaika, na wameitwa hivyo kutokana na utulivu wao wa hali ya juu wa kukiheshimu kisomo pamoja na Qur-aan yenyewe”.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
63: Nafasi Ya Malaika Kwa Waumini
(11)– Malaika Wanamfikishia Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Salamu Toka Kwa Umma Wake Baada Ya Yeye Kufariki
Kumswalia na kumsalimia Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni jambo lenye fadhla kubwa sana. Kati ya fadhla hizo, ni kwamba anayemsalimia Rasuli, basi salamu yake inamfikia moja kwa moja kaburini kwake, na salamu hiyo inafikishwa na Malaika maalum wenye kazi hiyo. Na hii ni katika mambo ya ghayb ambayo inabidi kama Waislamu tuyaamini.
Toka kwa ‘Abdullaah bin Mas-‘uwd (Radhwiya Allaah ‘anhu): Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إِنَّ لِلَّهِ مَلاَئِكَةً سَيَّاحِينَ فِي الْأَرْضِ يُبَلِّغُونِي مِنْ أُمَّتِي السَّلاَمَ"
“Hakika Allaah Ana Malaika Wake wanaozunguka ardhini, wananifikishia salamu toka kwa umma wangu”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na An-Nasaaiy (1282) na Ahmad (3666)]
Hadiyth hii inatuhimiza tukithirishe kumswalia na kumsalimia Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na inatubainishia namna Allaah Alivyomtukuza Nabiy Wake na kuienzi hadhi yake. Pia, inabainisha muujiza kati ya miujiza yake (Swalla Allaah ‘alayhi wa sallam).
Basi na tukithirishe kumswalia na kumsalimia Nabiy wetu (Swalla Allaah ‘alayhi wa sallam), na hii ni kwa faida yetu wenyewe.
Alhidaaya.com [3]
64: Nafasi Ya Malaika Kwa Waumini
(12)– Malaika Wanawapa Habari Njema Waumini
Malaika huwapa Waumini habari njema itokayo kwa Allaah Ta’alaa. Allaah Ta’alaa Anasema:
"إِنَّ الَّذِينَ قَالُوا رَبُّنَا اللَّـهُ ثُمَّ اسْتَقَامُوا تَتَنَزَّلُ عَلَيْهِمُ الْمَلَائِكَةُ أَلَّا تَخَافُوا وَلَا تَحْزَنُوا وَأَبْشِرُوا بِالْجَنَّةِ الَّتِي كُنتُمْ تُوعَدُونَ"
“Hakika wale waliosema: Rabb wetu ni Allaah, kisha wakathibiti imara, Malaika huwateremkia (kuwaambia): Msikhofu, na wala msihuzunike, na pokeeni bishara njema ya Jannah ambayo mlikuwa mkiahidiwa”. [Fus-swilat: 30]
As-Sam’aaniy amesema: “Maneno haya huambiwa mtu wakati wa kufa, au wakati wa kufufuliwa”.
Abul ‘Aaliyah Ar-Riyaahiy amesema: “Muumini atapewa habari ya furaha katika mahala patatu: Wakati anaingia kaburini, wakati wa kufufuliwa, na wakati anaingia Peponi”.
Na katika baadhi ya Tafaasiyr, Mufassiruna wamesema: “Mja akifufuliwa, watampokea Malaika wawili ambao walikuwa wanaandika amali zake na watamwambia: Usiogope wala usihuzunike, bali pokea habari ya furaha ya kupata Pepo ambayo ulikuwa umeahidiwa, na wala yasikuogopeshe unayoyaona, hayo wamekusudiwa kwayo wengine”.
Hapa duniani, Malaika walimpa habari njema Nabiy Ibraahiym (‘alayhis salaam) ya kupata watoto wema. Allaah Anatuambia:
"فَأَوْجَسَ مِنْهُمْ خِيفَةً ۖ قَالُوا لَا تَخَفْ ۖ وَبَشَّرُوهُ بِغُلَامٍ عَلِيمٍ"
“Akawaogopa ndani ya nafsi yake. Wakasema: Usikhofu! Na wakambashiria ghulamu mjuzi”. [Adh-Dhaariyaat: 28]
Walimpa Zakariyaa pia habari njema ya kumpata Yahyaa (‘alayhimas salaam). Allaah Anatuambia:
"فَنَادَتْهُ الْمَلَائِكَةُ وَهُوَ قَائِمٌ يُصَلِّي فِي الْمِحْرَابِ أَنَّ اللَّـهَ يُبَشِّرُكَ بِيَحْيَىٰ مُصَدِّقًا بِكَلِمَةٍ مِّنَ اللَّـهِ وَسَيِّدًا وَحَصُورًا وَنَبِيًّا مِّنَ الصَّالِحِينَ "
“Malaika akamwita (Zakariyyaa) naye akiwa amesimama anaswali katika chumba chake cha ‘ibaadah wakamwambia: Hakika Allaah Anakubashiria Yahyaa atakayesadikisha Neno (la Kun!) kutoka kwa Allaah. Atakuwa mtu wa kuheshimika, mtawa anayejitenga mbali na matamanio, na Nabiy miongoni mwa Swalihina”. [Aal-‘Imraan: 39]
Habari hizi njema wanazotoa Malaika haziishilii kwa Manabii na Mitume tu, bali hata Waumini wengineo wanaweza kubashiriwa na Malaika. Katika Hadiyth ya Abu Hurayrah, Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"أَنَّ رَجُلاً زَارَ أَخًا لَهُ فِي قَرْيَةٍ أُخْرَى، فَأَرْصَدَ اللَّهُ لَهُ عَلَى مَدْرَجَتِهِ مَلَكًا، فَلَمَّا أَتَى عَلَيْهِ قَالَ: أَيْنَ تُرِيدُ؟ قَالَ: أُرِيدُ أَخًا لِي فِي هَذِهِ الْقَرْيَةِ. قَالَ: هَلْ لَكَ عَلَيْهِ مِنْ نِعْمَةٍ تَرُبُّهَا؟ قَالَ: لاَ، غَيْرَ أَنِّي أَحْبَبْتُهُ فِي اللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ . قَالَ: فَإِنِّي رَسُولُ اللَّهِ إِلَيْكَ بِأَنَّ اللَّهَ قَدْ أَحَبَّكَ كَمَا أَحْبَبْتَهُ فِيهِ"
“Kwamba mtu mmoja alimtembelea nduguye aliyekuwa mji mwingine. Allaah Akamwekea njiani Malaika amngojee. Alipofika pale aliko Malaika, Malaika alimuuliza: Unakwenda wapi? Akamwambia: Nimekusudia kuja kumwona ndugu yangu katika mji huu. Akamuuliza: Je, kuna maslahi yoyote kutoka kwake ambayo unayalinda? Akasema hapana, hakuna chochote isipokuwa mimi nimempenda tu kwa ajili ya Allaah ‘Azza wa Jalla. Akamwambia: Basi mimi ni Mjumbe wa Allaah kwako, Amenituma nikueleze kwamba Allaah Amekupenda kama wewe ulivyompenda (nduguyo) kwa ajili Yake” . [Swahiyh Muslim (2567)]
Hadiyth hii inatufundisha:
1- Fadhila ya Waislamu kupendana kwa ajili ya Allaah na si kwa jingine lolote.
2- Kupendana na kutembeleana kwa ajili ya Allaah ni moja kati ya amali bora kabisa, na hasa ikiwa ziara bila ya maslahi yoyote ya kidunia.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
65: Nafasi Ya Malaika Kwa Waumini
(13)– Malaika Wanapigana Pamoja Na Waumini Na Wanawaimarisha Na Kuwatia Nguvu Vitani
Allaah Ta’aalaa Amesema kuhusiana na watu wa Badri:
"إِذْ يُوحِي رَبُّكَ إِلَى الْمَلَائِكَةِ أَنِّي مَعَكُمْ فَثَبِّتُوا الَّذِينَ آمَنُوا ۚ سَأُلْقِي فِي قُلُوبِ الَّذِينَ كَفَرُوا الرُّعْبَ فَاضْرِبُوا فَوْقَ الْأَعْنَاقِ وَاضْرِبُوا مِنْهُمْ كُلَّ بَنَانٍ"
“Pale Rabb wako Alipowatia ilhamu Malaika (kuwaambia): Hakika Mimi Niko pamoja nanyi; basi wathibitisheni wale walioamini. Nitatia kizaazaa katika nyoyo za waliokufuru. Basi wapigeni juu ya shingo na wapigeni kila kiungo (au ncha za vidole). [Al-Anfaal: 12]
As-Sa’adiy akiifasiri aayah hii anasema: “Allaah Ta’aalaa Aliwafunulia Malaika Wake kwa kuwaambia: Hakika Mimi Niko pamoja nanyi kwa kuwapa msaada, nusra na kuwatieni nguvu, hivyo basi, wapeni uimara wale walioamini, yaani, tupieni katika nyoyo zao ushujaa wa kupambana na maadui zao, na wajazeni utashi wa kupigana Jihaad na kupupia fadhila zake”.
Allaah Ta’aalaa Ameelezea hikmah ya usaidizi huu wa Malaika kwa Waumini pale Aliposema:
"وَمَا جَعَلَهُ اللَّـهُ إِلَّا بُشْرَىٰ وَلِتَطْمَئِنَّ بِهِ قُلُوبُكُمْ ۚ وَمَا النَّصْرُ إِلَّا مِنْ عِندِ اللَّـهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ"
“Na Allaah Hakujaalia haya isipokuwa ni bishara, na ili zitumainike nyoyo zenu kwayo. Na hakuna nusura isipokuwa kutoka kwa Allaah. Hakika Allaah Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote. [Al-Anfaal: 10]
Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaah ‘anhumaa) amesema kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema Siku ya Badr:
"هذا جِبريلُ [18] آخِذٌ برأسِ فَرَسِه، عليه أداةُ الحَربِ"
“Huyu ni Jibriyl, amekamata kichwa cha farasi wake, amevalia zana za kivita”. [Swahiyh Al-Bukhaariy: (3995)]
Hapa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwazindusha Maswahaba wake juu ya uwepo wa Jibriyl katika uwanja wa vita ili kuwapa ukakamavu, uimara na morali zaidi, lakini pia kuwatuliza nyoyo.
Katika Vita vya Badr, baadhi ya Maswahaba walisikia kishindo cha pigo la Malaika kwa kafiri. Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaah ‘anhumaa) amesema:
"بَيْنَمَا رَجُلٌ مِنَ الْمُسْلِمِينَ يَوْمَئِذٍ يَشْتَدُّ فِي أَثَرِ رَجُلٍ مِنَ الْمُشْرِكِينَ أَمَامَهُ، إِذْ سَمِعَ ضَرْبَةً بِالسَّوْطِ فَوْقَهُ وَصَوْتَ الْفَارِسِ يَقُولُ: أَقْدِمْ حَيْزُومُ . فَنَظَرَ إِلَى الْمُشْرِكِ أَمَامَهُ فَخَرَّ مُسْتَلْقِيًا فَنَظَرَ إِلَيْهِ فَإِذَا هُوَ قَدْ خُطِمَ أَنْفُهُ وَشُقَّ وَجْهُهُ كَضَرْبَةِ السَّوْطِ فَاخْضَرَّ ذَلِكَ أَجْمَعُ . فَجَاءَ الأَنْصَارِيُّ فَحَدَّثَ بِذَلِكَ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ " صَدَقْتَ ذَلِكَ مِنْ مَدَدِ السَّمَاءِ الثَّالِثَةِ "
“Katika siku hiyo, wakati Muislamu alipokuwa anamkimbiza mpagani aliyekuwa anakimbia mbele yake, ghafla alisikia sauti ya pigo la mjeledi juu yake na sauti ya mpanda farasi akisema: Ongeza mbio Khayzuwm. Akamwangalia mpagani akamwona anaanguka chali mbele yake, na alipomkagua vizuri, aliona pua ina kovu na uso wake umepasuliwa kama vile amepigwa na mjeledi, huku mwili wake wote ukiwa umegeuka kijani. M-Answaariy huyo alikwenda na kulielezea tukio kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na Rasuli akamwambia: Umesema kweli, huyo alikuwa (Malaika wa) msaada toka mbingu ya tatu”. [Swahiyh Muslim: (1763)]
Khayzuwm ni jina la farasi wa Malaika huyo.
Kadhalika, katika Vita vya Makundi, Siku ya Khandaq, Jibriyl pia aliwasaidia Waumini. Bibi ‘Aaishah amesema:
"فَلَمَّا رَجَعَ رَسولُ اللهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم مِنَ الخَنْدَقِ وَضَعَ السِّلَاحَ، فَاغْتَسَلَ، فأتَاهُ جِبْرِيلُ [18] وَهو يَنْفُضُ رَأْسَهُ مِنَ الغُبَارِ، فَقالَ: وَضَعْتَ السِّلَاحَ؟ وَاللَّهِ ما وَضَعْنَاهُ، اخْرُجْ إليهِم، فَقالَ رَسولُ اللهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم: فأيْنَ؟ فأشَارَ إلى بَنِي قُرَيْظَةَ، فَقَاتَلَهُمْ رَسولُ اللهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم، فَنَزَلُوا علَى حُكْمِ رَسولِ اللهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم، فَرَدَّ رَسولُ اللهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم الحُكْمَ فيهم إلى سَعْدٍ"
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliporejea toka Vita vya Khandaq, aliirejesha silaha yake mahala pake, kisha akaoga. Jibriyl akamjia huku akikun’guta vumbi kichwa chake. Akamuuliza: Umeweka silaha chini? Naapa kwa Allaah, sisi bado hatujaweka silaha chini, toka uwafuate. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamuuliza: Wapi? Akamwashiria kwenda kwa Baniy Quraydhwah. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akapambana nao mpaka wakasalimu amri kuwa chini ya utawala wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Halafu Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaurejeshea utawala kwa Sa’ad awaongoze”. [Al-Bukhaariy (4122) na Muslim (1769)]
Haya yote yanaonyesha kwamba Malaika huandamana na wanaopigana katika Njia ya Allaah, na huwasaidia madhali watakuwa ni wenye kufuata Maagizo ya Allaah na Rasuli Wake, na kama watakwenda kinyume nayo, basi hapo hufarikiana na kuachana nao.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
66: Nafasi Ya Malaika Kwa Waumini
(14)– Malaika Wanamlinda Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Dhidi Ya Maadui Zake
Malaika hubeba jukumu la kumlinda Rasuli wa Allaah na Rusuli wengineo kutokana na njama za maadui na makafiri. Abu Hurayrah amesema:
"قَالَ أَبُو جَهْلٍ: هَلْ يُعَفِّرُ مُحَمَّدٌ وَجْهَهُ بَيْنَ أَظْهُرِكُمْ؟ قَالَ: فَقِيلَ نَعَمْ . فَقَالَ: وَاللاَّتِ وَالْعُزَّى لَئِنْ رَأَيْتُهُ يَفْعَلُ ذَلِكَ لأَطَأَنَّ عَلَى رَقَبَتِهِ أَوْ لأُعَفِّرَنَّ وَجْهَهُ فِي التُّرَابِ، قَالَ: فَأَتَى رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَهُوَ يُصَلِّي زَعَمَ لِيَطَأَ عَلَى رَقَبَتِهِ، قَالَ: فَمَا فَجِئَهُمْ مِنْهُ إِلاَّ وَهُوَ يَنْكِصُ عَلَى عَقِبَيْهِ وَيَتَّقِي بِيَدَيْهِ - قَالَ - فَقِيلَ لَهُ مَا لَكَ فَقَالَ إِنَّ بَيْنِي وَبَيْنَهُ لَخَنْدَقًا مِنْ نَارٍ وَهَوْلاً وَأَجْنِحَةً . فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " لَوْ دَنَا مِنِّي لاَخْتَطَفَتْهُ الْمَلاَئِكَةُ عُضْوًا عُضْوًا " .
“Abu Jahl aliuliza wenzake: Je, (mnamwona) Muhammad akiuweka uso wake mchangani na nyinyi mnamtazama? Akaambiwa na’am. Akasema: Naapa kwa Al-Laati na Al-‘Uzzaa, lau nitamwona anafanya hivyo, basi nitaikanyaga shingo yake na kuigaragazisha mchangani. Na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuwa anaswali, alimwendea ili aikanyage shingo yake (atakaposujudu). Hapo wenzake walishtukizwa kumwona anarudi kinyume nyume (kwa hofu) huku anazuilia (kitu) kwa mikono yake. Wakamuuliza: Una nini? Mbona hivyo? Akasema: Hakika kuna shimo refu la moto kati yangu mimi na yeye, na kuna kitu cha kutisha pamoja na mbawa. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: Lau angenikurubia, basi Malaika wangemnyofoa kiungo kimoja kimoja”. [Swahiyh Muslim: (2797)]
Malaika
Alhidaaya.com [3]
67: Nafasi Ya Malaika Kwa Waumini
(15)– Wanahudhuria Mazishi Ya Baadhi Ya Watu Wema
Alipokufa Swahaba mtukufu Sa’ad bin Mu’aadh, Malaika wapatao elfu sabini walishuhudia mazishi yake. Toka kwa Ibn ‘Umar: Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema kuhusu Sa’ad bin Mu’aadh (Radhwiya Allaah ‘anhu) wakati alipokufa:
"هَذَا الَّذِي تَحَرَّكَ لَهُ الْعَرْشُ وَفُتِحَتْ لَهُ أَبْوَابُ السَّمَاءِ وَشَهِدَهُ سَبْعُونَ أَلْفًا مِنْ الْمَلَائِكَةِ ، لَقَدْ ضُمَّ ضَمَّةً ثُمَّ فُرِّجَ عَنْهُ"
“Huyu ndiye ambaye ‘Arshi ilitikisika kwa ajili yake, milango ya mbingu ikafunguliwa kwa ajili yake, na Malaika elfu 70 walishuhudia mazishi yake, huyu (aliyefanyiwa yote haya) amebanwa akabanika, kisha akaachiliwa”. [Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh katika “Swahiyh An-Nasaaiy”].
Malaika
Alhidaaya.com [3]
68: Nafasi Ya Malaika Kwa Waumini
(16)– Wanamfunika Aliyekufa Kishahidi Kwa Mbawa Zao
Imepokelewa toka kwa Jaabir (Radhwiya Allaah ‘anhu) akisema:
"جيءَ بِأَبِي إِلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَقَدْ مُثِّلَ بِهِ وَوُضِعَ بَيْنَ يَدَيْهِ، فَذَهَبْتُ أَكْشِفُ عَنْ وَجْهِهِ، فَنَهَانِي قَوْمِي، فَسَمِعَ صَوْتَ صَائِحَةٍ فَقِيلَ ابْنَةُ عَمْرٍو، أَوْ أُخْتُ عَمْرٍو. فَقَالَ: " لِمَ تَبْكِي أَوْ لاَ تَبْكِي، مَا زَالَتِ الْمَلاَئِكَةُ تُظِلُّهُ بِأَجْنِحَتِهَا"
“(Maiti ya) baba yangu ililetwa kwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hali ya kuwa imefanyiwa ukatili na ikawekwa mbele yake. Nikajaribu kuikaribia ili niufunue uso wake lakini jamaa zangu walinikataza. Rasuli akasikia sauti ya mwanamke ambaye ima ni binti ya ‘Amri au dada ya ‘Amri akilia kwa sauti ya kuomboleza, akauliza: Kwa nini analia (au usilie)? Malaika bado wanaendelea kumwekea kivuli kwa mbawa zao”. [Swahiyh Al-Bukhaariy (2816)]
Abul ‘Abbaas Al-Qurtwubiy amesema: “Kitendo hicho cha Malaika cha kumfunika kwa mbawa zao, kinamaanisha kwamba wanamkusanyikia na kusongana kwa shahidi huyo ili wapate kukutana naye na kupanda juu pamoja na roho yake takatifu, lakini pia kumpa bishara njema kwa yanayomsubiri mbele ya Allaah kati ya mambo mazuri na daraja za juu kabisa”.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
69: Nafasi Ya Malaika Kwa Waumini
(17)– Malaika Waliokuja Na Kasha Lenye Utulivu Ndani Yake
Allaah Ta’aalaa Anasema:
"وَقَالَ لَهُمْ نَبِيُّهُمْ إِنَّ آيَةَ مُلْكِهِ أَن يَأْتِيَكُمُ التَّابُوتُ فِيهِ سَكِينَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَبَقِيَّةٌ مِّمَّا تَرَكَ آلُ مُوسَىٰ وَآلُ هَارُونَ تَحْمِلُهُ الْمَلَائِكَةُ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لَّكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ "
“Nabiy wao akawaambia: Hakika ishara ya ufalme wake ni kwamba litakujieni kasha ndani yake mna kituliza nyoyo kutoka kwa Rabb wenu na mabaki katika yale waliyoacha watu wa Muwsaa na watu wa Haaruwn, watalibeba Malaika. Hakika katika hayo mna ishara kwenu mkiwa ni Waumini”. [Al-Baqarah: 248]
As- Sa‘adiy amesema: “Nabiy wao aliwaelezea vile vile muujiza wa kihisia ambao wataushuhudia. Muujiza huu ni kuletwa kasha ambalo walilipoteza muda mrefu uliopita ambapo ndanimwe kuna utulivu wa kuzipooza nyoyo na akili zao, lakini pia kuna mabaki katika yale waliyoacha watu wa Muwsaa na watu wa Haaruwn. Malaika wakaja nalo wakiwa wamelibeba na wao wanaliona wazi wazi”.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
70: Nafasi Ya Malaika Kwa Waumini
(18)– Malaika Watailinda Makkah Na Madiynah Kutokana Na Dajjaal
Al-Masiyh Ad Dajjaal atakapodhihiri, ataingia miji yote isipokuwa Makkah na Madiynah kwa kuwa itakuwa inalindwa na Malaika.
Katika kisa cha Tamiym Ad Daariyy (Radhwiya Allaah ‘anhu) alichokihadithia kwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema: “Dajjaal alisema: Hakika mimi ni Al-Masiyh Ad-Dajjaal, na muda umekaribia niruhusiwe kutoka. Nikitoka nitatembea dunia yote, siachi mji wowote isipokuwa nitatuwa hapo katika muda wa siku 40, ila Makkah na Madiynah. Miji yote hiyo miwili ni marufuku kabisa kwangu. Kila nitakavyojaribu kuingia kwenye mji mmoja kati ya hiyo miwili, atanikabili Malaika mwenye upanga uliochomolewa anizuie kuingia, na katika kila kona na njia ya miji hiyo kutakuwa na Malaika wanalinda. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akagonga mimbari kwa fimbo yake na kusema: Huu ni Twaybah, huu ni Twaybah, huu ni Twaybah”. [Swahiyh Muslim: 2942]
Twaybah ni Madiynah.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
71: Nafasi Ya Malaika Kwa Waumini
(19)– Malaika Wanawateremshia Makafiri Adhabu
Kama tunavyosoma katika Qur-aan Tukufu, Allaah Ta’aalaa Aliwaangamiza watu ambao waliwakadhibisha Mitume wao, na kazi ya kuwaangamiza ilikuwa inafanywa na Malaika katika baadhi ya nyakati. Mfano kaumu Lut, Allaah Ta’alaa Anatuambia:
"فَلَمَّا جَاءَ أَمْرُنَا جَعَلْنَا عَالِيَهَا سَافِلَهَا وَأَمْطَرْنَا عَلَيْهَا حِجَارَةً مِّن سِجِّيلٍ مَّنضُودٍ"
“Basi ilipokuja Amri Yetu, Tuliupindua (mji wao) juu chini, na Tukauteremshia mvua mfululizo ya mawe ya udongo mgumu uliookwa”. [Hud: 82]
Jibriyl ‘Alayhis Salaam ndiye aliyefanya kazi hii.
Wakati wa kutoka roho kwa makafiri, Malaika pia hufanya kazi ya kuwaadhibu. Allaah Anatuambia:
"وَلَوْ تَرَىٰ إِذِ الظَّالِمُونَ فِي غَمَرَاتِ الْمَوْتِ وَالْمَلَائِكَةُ بَاسِطُو أَيْدِيهِمْ أَخْرِجُوا أَنفُسَكُمُ ۖ الْيَوْمَ تُجْزَوْنَ عَذَابَ الْهُونِ بِمَا كُنتُمْ تَقُولُونَ عَلَى اللَّـهِ غَيْرَ الْحَقِّ وَكُنتُمْ عَنْ آيَاتِهِ تَسْتَكْبِرُونَ"
"Na lau ungeliona madhalimu pale wakiwa katika mateso makali ya mauti (ungeona jambo la kutisha sana), na Malaika wamenyosha mikono yao (wakiwaambia): Toeni nafsi zenu! Leo mnalipwa adhabu ya kudhalilisha kwa yale mliyokuwa mkiyasema juu ya Allaah pasi na haki, na mlikuwa mkitakabari msizifuate Aayaat Zake”. [Al-An’aam: 93]
Halafu kaburini, kuna Malaika wawili Munkar na Nakiyr. Hawa watawatahini wafu na kuwauliza maswali, na atakayeshindwa kujibu, basi ole wake.
Kisha Siku ya Qiyaamah, Malaika watawaswaga watu wa motoni na kuwakabidhi kwa walinzi wa moto ambao watawaadhibu na kuwatesa ndani ya moto wa Jahannam. Allaah Atulinde nao.
Malaika
Alhidaaya.com [3]
72: Nafasi Ya Malaika Kwa Waumini
(20)– Malaika Wanawalaani Makafiri na Baadhi Ya Watu Mafasiki
Allaah Ta’aalaa Anatuambia:
"إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَمَاتُوا وَهُمْ كُفَّارٌ أُولَـٰئِكَ عَلَيْهِمْ لَعْنَةُ اللَّـهِ وَالْمَلَائِكَةِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ "
“Hakika wale waliokufuru na wakafa hali ya kuwa ni makafiri, hao iko juu yao Laana ya Allaah na Malaika na watu wote”. [Al-Baqarah: 161]
Malaika hawalaani makafiri tu, bali pia wanawalaani Waislamu ambao wamefanya madhambi maalum. Kati ya watu hao ni:
1- Mwenye kuficha haki:
Allaah Ta’aalaa Amesema:
"إِنَّ الَّذِينَ يَكْتُمُونَ مَا أَنزَلْنَا مِنَ الْبَيِّنَاتِ وَالْهُدَىٰ مِن بَعْدِ مَا بَيَّنَّاهُ لِلنَّاسِ فِي الْكِتَابِ ۙ أُولَـٰئِكَ يَلْعَنُهُمُ اللَّـهُ وَيَلْعَنُهُمُ اللَّاعِنُونَ "
“Hakika wale wanaoficha yale Tuliyoyateremsha katika hoja bayana na mwongozo baada ya kuwa Tumeyabainisha kwa watu katika Kitabu, hao Anawalaani Allaah na wanalaaniwa na kila mwenye kulaani”. [Al-Baqarah: 159]
Ibn Al-Jawziy amesema: “Kuna kauli nne kuhusiana na wenye kumlaani mtu huyu:
Ya kwanza: Ni wanyama wa ardhini. Ya pili: Ni Waumini. Ya tatu: Ni Malaika na Waumini. Ya nne: Ni majini, wanadamu na wanyama wote”.
Ama As-Sa’adiy, yeye kasema: “Ni viumbe wote wanamlaani, laana toka viumbe wote inawateremkia. Kwa kuwa watu hawa lengo lao kuu ni kudanganya watu, kuharibu dini yao na kuwaweka mbali na Rahma ya Allaah. Hivyo wanalipwa kwa mujibu wa matendo yao”.
Kama ambavyo mtu mwenye kuwafundisha watu kheri, Allaah pamoja na Malaika Wake Humsalia mtu huyo, hadi samaki ndani ya maji, kwa kuwa mtu huyo lengo lake kuu ni maslaha ya viumbe, kuwatengenezea dini yao, na kuwakurubisha kwenye Rehma za Allaah. Hivyo naye analipwa kwa mujibu wa lengo na juhudi zake hizo.
2- Mwanamke asiyemwitikia mumewe kwa tendo la ndoa:
Abu Hurayrah amesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إِذَا دَعَا الرَّجُلُ امْرَأَتَهُ إِلَى فِرَاشِهِ فَأَبَتْ فَبَاتَ غَضْبَانَ لَعَنَتْهَا الْمَلَائِكَةُ حَتَّى تُصْبِحَ"
“Mume akimwita mkewe kitandani halafu akakataa, na mume akalala hali ya kuwa amemkasirikia, basi Malaika watamlaani hadi kupambazuke”. [Al-Bukhaariy na Muslim]
Malaika humlaani kwa sababu mwanamke ameamuriwa amtii mumewe kwenye jambo lolote lisilo la maasia isipokuwa kama kuna udhuru. Na hedhi si udhuru wa kumkatalia, kwa kuwa mume ana haki ya kumchezea sehemu zote za mwili isipokuwa utupu. Na hukmu ya mchana ni hivyo hivyo, watamlaani mpaka jua lichwe.
Ibn ‘Uthaymiyn amesema: “Laana ya Malaika ina maana kwamba wanamwombea laana mwanamke huyu, na laana ni kuwekwa mbali na Rahma ya Allaah”.
3- Mwenye kumnyooshea nduguye kipande cha chuma (au silaha):
Abu Hurayrah amesema: "Abul Qaasim (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"مَنْ أَشَارَ إِلَى أَخِيهِ بِحَدِيدَةٍ فَإِنَّ الْمَلَائِكَةَ تَلْعَنُهُ حَتَّى يَضَعَهَا وَإِنْ كَانَ أخاهُ لأبيهِ وَأُمِّهِ"
“Atakayemnyooshea nduguye chuma (au silaha), Malaika watakuwa ni wenye kumlaani mpaka aiweke chini, hata kama ni nduguye wa baba na mama mmoja”. [Swahiyh Muslim: 2616]
Kunyooshea huku ni sawa kuwe kwa utani au kukusudia kikweli.
4- Mwenye kuzusha au kufanya lolote baya Madiynah:
Abu Hurayrah amesimulia:
"الْمَدِينَةُ حَرَمٌ، فَمَنْ أَحْدَثَ فِيهَا حَدَثًا أَوْ آوَى مُحْدِثًا فَعَلَيْهِ لَعْنَةُ اللَّهِ وَالْمَلاَئِكَةِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ، لاَ يُقْبَلُ مِنْهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عَدْلٌ وَلاَ صَرْفٌ"
“Madiynah ni takatifu yenye marufuku maalum. Basi yeyote atakayezusha humo lisilo katika dini, au akampa hifadhi mzushaji, basi zimpate laana za Allaah, Malaika na watu wote. Hatokubaliwa Siku ya Qiyaamah fidia wala toba”. [Al-Bukhaariy na Muslim].
Malaika
Alhidaaya.com [3]
73: Wanachopaswa Waumini Kukitenda Kwa Ajili Ya Malaika
(01)- Kujiepusha Na Kila Jambo Linalowaudhi Au Kuwakera
Waumini wanatakiwa kujiepusha na kila jambo ambalo linawakera au kuwaudhi Malaika. Jambo kubwa linalowakera zaidi ni ukafiri, shirki, madhambi na maasia. Na kwa ajili hiyo, Malaika hawaingii nyumba ambazo ndanimwe kuna watu wanaomwasi Allaah, au nyumba ambazo ndanimwe kuna Anayoyachukia Allaah kama masanamu na picha. Vile vile, hawamkurubii mtu aliyevaana na maasia kama mlevi, mraibu na kadhalika.
Toka kwa Abu Twalha Al-Answaariyy (Radhwiya Allaah ‘anhu): “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"لا تَدْخُلُ الْمَلاَئِكَةُ بَيْتًا فِيهِ كَلْبٌ وَلاَ صُورَةٌ "
“Malaika (wa rahmah na baraka) hawaingii nyumba yoyote ambamo ndani yake kuna mbwa au picha”. [Sunan An Nasaaiy (5347)]
Toka kwa ‘Abdullah bin ‘Abbaas (Radhwiya Allaah ‘anhumaa):
"ثَلَاثٌ لَا تَقْرَبُهُمُ الْمَلَائِكَةُ: جِيفَةُ الْكَافِرِ، وَالْمُتَضَمِّخُ بِالْخَلُوقِ، وَالْجُنُبُ إِلَّا أَن يتَوَضَّأ"
“Malaika (wa rahma) hawawakurubii watatu: Mzoga wa kafiri, aliyejisiriba khaluwq, na mwenye janaba mpaka atawadhe”. [Swahiyh At-Targhiyb: 174]
“Khaluwq” ni aina ya manukato yenye rangi, hutengenezwa kutokana na zafarani na mada nyinginezo.
Kadhalika, Malaika hawawakurubii watu wenye kengele. Abu Hurayrah amesema: (Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"لَا تَصْحَبُ الْمَلَائِكَةُ رُفْقَةً فِيهَا كَلْبٌ وَلَا جَرَسٌ"
“Malaika hawaandamani na wasafiri wenye mbwa au kengele”. [Mishkaat Al-Maswaabiyh: (3894)]
Jingine linalowakera na kuwaudhi Malaika ni kila chenye kuwaudhi na kuwakera wanadamu kama harufu mbaya, uvundo, uchafu na kadhalika.
Toka kwa Jaabir (Radhwiya Allaah ‘anhu): “Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"مَنْ أَكَلَ الْبَصَلَ وَالثُّومَ وَالْكُرَّاثَ فَلاَ يَقْرَبَنَّ مَسْجِدَنَا، فَإِنَّ الْمَلاَئِكَةَ تَتَأَذَّى مِمَّا يَتَأَذَّى مِنْهُ بَنُو آدَمَ "
“Aliyekula kitunguu maji, au kitunguu thawm, au kitunguu majani, basi akae mbali kabisa na Msikiti wetu, kwa kuwa Malaika wanakereka na yale yanayowakera watu”. [Muslim 564]
Kadhalika, Muislamu anaposwali, asiteme upande wake wa kulia. Hilo Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amelikataza. Kwa kuwa mtu anaposwali, Malaika husimama upande wake wa kulia.
Toka kwa Abu Hurayrah: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إِذَا قَامَ أَحَدُكُمْ إِلَى الصَّلَاةِ فَلَا يَبْصُقْ أَمَامَهُ فَإِنَّمَا يُنَاجِي اللَّهَ مَا دَامَ فِي مُصَلَّاهُ، وَلَا عَنْ يَمِينِهِ فَإِنَّ عَنْ يَمِينِهِ مَلَكًا، وَلْيَبْصُقْ عَنْ يَسَارِهِ أَوْ تَحْتَ قَدَمِهِ فَيَدْفِنُهَا"
“Anaposimama mmoja wenu kuswali, basi asiteme mbele yake, kwa sababu anakuwa ni mwenye kusemezana na Allaah madhali yuko sehemu yake anayoswalia. Na pia asiteme kuliani mwake, kwani kuliani mwake yuko Malaika. Ateme kushotoni mwake, au chini ya mguu wake, halafu afukie. [Al-Bukhaariy na Muslim]
Malaika
Alhidaaya.com [3]
74: Wanachopaswa Waumini Kukitenda Kwa Ajili Ya Malaika
(02)- Kuwapenda Wote Bila Kubagua
Muislamu anatakiwa awapende Malaika wote kwa daraja sawa, asipambanue kati ya Malaika na Malaika, wote hao ni Waja wa Allaah. Mayahudi wamedai kwamba kuna baadhi ya Malaika ambao ni vipenzi kwao na wengine ni maadui kwao. Wamedai kwamba Jibriyl (‘alayhis salaam) ni adui yao, na Miykaaiyl ni kipenzi chao. Allaah Amewajibu madai yao haya Akisema:
"قُلْ مَن كَانَ عَدُوًّا لِّجِبْرِيلَ فَإِنَّهُ نَزَّلَهُ عَلَىٰ قَلْبِكَ بِإِذْنِ اللَّـهِ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ وَهُدًى وَبُشْرَىٰ لِلْمُؤْمِنِينَ ● مَن كَانَ عَدُوًّا لِّلَّـهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَرُسُلِهِ وَجِبْرِيلَ وَمِيكَالَ فَإِنَّ اللَّـهَ عَدُوٌّ لِّلْكَافِرِينَ "
“Sema: Yeyote aliyekuwa adui wa Jibriyl, basi hakika yeye ameiteremsha Qur-aan katika moyo wako (ee Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم) kwa Idhini ya Allaah inayosadikisha yaliyo kabla yake, na mwongozo na bishara kwa Waumini. ●. Yeyote aliyekuwa adui wa Allaah na Malaika Wake, na Rusuli Wake, na Jibriyl, na Miykaala, basi hakika Allaah Ni adui kwa makafiri”. [Al-Baqarah: 97-98]
Malaika
Alhidaaya.com [3]
75: Malaika Wanazidiana Kwa Daraja
Malaika wanazidiana kwa ubora. Baadhi yao ni wabora kuliko wengineo, na walio bora zaidi ni wale waliokurubishwa kwa Allaah Ta’aalaa kama Anavyosema Allaah:
"لَّن يَسْتَنكِفَ الْمَسِيحُ أَن يَكُونَ عَبْدًا لِّلَّـهِ وَلَا الْمَلَائِكَةُ الْمُقَرَّبُونَ ۚ وَمَن يَسْتَنكِفْ عَنْ عِبَادَتِهِ وَيَسْتَكْبِرْ فَسَيَحْشُرُهُمْ إِلَيْهِ جَمِيعًا "
“Al-Masiyh kamwe hatojiona bora aje akatae kuwa ni mja kwa Allaah, wala Malaika waliokurubishwa. Na atakayejiona bora akakataa Kumwabudu (Allaah) na akatakabari, basi Atawakusanya wote Kwake”. [An-Nisaa: 173]
Aayah hii inaonyesha kwamba tabaka za Malaika zinatofautiana kwa ngazi na ubora, na wanaoongoza ni pamoja na Jibriyl, Miykaaiyl, Israafiyl na wabebaji ‘Arshi ya Allaah.
Na Malaika aliye juu na mbora kuliko wote ni Jibriyl ‘Alayhis Salaam. Yeye ni Mjumbe kati ya Allaah na Mitume Wake ambapo alikuwa akiwateremshia Wahyi kutoka kwa Allaah ili nao wawafikishie watu wao.
Allaah Ta’aalaa Amemwita kwa majina matukufu na kumsifu kwa sifa njema kabisa. Amemwita “Ruwhul Qudus” Aliposema:
"قُلْ نَزَّلَهُ رُوحُ الْقُدُسِ مِن رَّبِّكَ بِالْحَقِّ لِيُثَبِّتَ الَّذِينَ آمَنُوا وَهُدًى وَبُشْرَىٰ لِلْمُسْلِمِينَ"
“Sema: Ameiteremsha Ruwhul-Qudus (Jibriyl) kutoka kwa Rabb wako kwa haki ili iwathibitishe wale walioamini, na ni mwongozo na bishara kwa Waislamu”. [An-Nahl: 102]
Pia Amemwita “Ruwhul Amiyn”:
"نَزَلَ بِهِ الرُّوحُ الْأَمِينُ "
“Ameiteremsha Ar-Ruwh (Jibriyl) mwaminifu”. [Ash-Shu’araa: 193]
Isitoshe, Allaah Ta’aalaa Amemwelezea kama ni mjumbe mtukufu, mwenye nguvu, mwenye hadhi maalum Kwake Allaah, anatiiwa na Malaika, lakini pia ni mwaminifu. Allaah Anasema:
"إِنَّهُ لَقَوْلُ رَسُولٍ كَرِيمٍ ● ذِي قُوَّةٍ عِندَ ذِي الْعَرْشِ مَكِينٍ ● مُّطَاعٍ ثَمَّ أَمِينٍ"
“Hakika hii (Qur-aan) bila shaka ni kauli ya Mjumbe mtukufu (Jibriyl) ● Mwenye nguvu na cheo kitukufu kwa (Allaah) Anayemiliki ‘Arsh ● Anayetiiwa (na Malaika), mwaminifu huko (mbinguni). [At-Takwiyr: 19-21]
Ama Miykaaiyl na Israafiyl, hawa pia ni katika Malaika wenye hadhi kwa Allaah, kwani wametajwa mara kadhaa katika Qur-aan pamoja na Jibriyl ‘Alayhis Salaam. Kadhalika, Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiwataja katika dua ya ufunguzi wa Swalah zake za usiku. Bibi ‘Aaishah (Radhwiya Allaah ‘anhaa amesema:
"كَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا قَامَ مِنَ اللَّيْلِ افْتَتَحَ صَلَاتَهُ فَقَالَ: اللَّهُمَّ رَبَّ جِبْرِيلَ وَمِيكَائِيلَ وَإِسْرَافِيلَ ، فَاطِرَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ، عَالِمَ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ"
“Alikuwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anaposimama usiku, anaifungua swalah yake kwa kusema: “Ee Allaah! Mola wa Jibriyl, Miykaaiyl, na Israafiyl, Muumba wa mbingu na ardhi, Unayejua yaliyofichikana na yenye kuonekana..” [Muslim (628). Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh].
Malaika
Alhidaaya.com [3]
76: Kuzidiana Ubora Kati Ya Malaika Na Wanadamu
‘Ulamaa wametofautiana kuhusiana na suala hili katika kauli kadhaa.
Kauli ya kwanza: Ni ya Jumhuwr Ahlis Sunnat wal Jama’ah. Inasema kwamba Manabii na watu wema wamewazidi Malaika kwa ubora kutokana na dalili nyingi. Miongoni mwa dalili hizo ni:
1- Kauli Yake Ta’aalaa:
"وَلَقَدِ اخْتَرْنَاهُمْ عَلَىٰ عِلْمٍ عَلَى الْعَالَمِينَ"
“Na kwa yakini Tuliwakhitari (wana wa Israaiyl) kwa elimu kuliko walimwengu wowote”. [Ad-Dukhaan: 32]
2- Kauli Yake Ta’aalaa:
"إِنَّ اللَّـهَ اصْطَفَىٰ آدَمَ وَنُوحًا وَآلَ إِبْرَاهِيمَ وَآلَ عِمْرَانَ عَلَى الْعَالَمِينَ "
“Hakika Allaah Amemkhitari Aadam na Nuwh na kizazi cha Ibraahiym na kizazi cha ‘Imraan juu ya walimwengu”. [Aal-‘Imraan: 33]
Ibn Taymiyah ametofautiana na kundi hili kwa kusema: “Neno "العَالَمِيْنَ" linaweza kuja kwa maana ya aina zote za viumbe kama katika "الحَمْدُ للهِ رَبِّ العَالَمِيْنَ" . Pia linaweza kuja kwa maana ya wanadamu tu kama katika aayah:
"أَتَأْتُونَ الذُّكْرَانَ مِنَ الْعَالَمِينَ "
“Je, mnawaendea wanaume miongoni mwa walimwengu?" [Ash-Shu’araa: 165]
Au:
"وَلُوطًا إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِ أَتَأْتُونَ الْفَاحِشَةَ مَا سَبَقَكُم بِهَا مِنْ أَحَدٍ مِّنَ الْعَالَمِينَ"
“Na (Tulimtuma) Luwtw, alipowaambia kaumu yake: Je, mnafanya uchafu (wa liwati) ambao hajakutangulieni nao yeyote katika walimwengu?” [Al-A’araaf: 80]
Na inavyojulikana ni kwamba walikuwa hawawaingilii wanyama au majini au viumbe vingine, isipokuwa wanaume wenzao.
Kadhalika, "العَالَمِيْنَ" linaweza kuja kwa maana ya watu walioishi zama moja. Ni kama katika Neno Lake Ta’aalaa:
"وَلَقَدِ اخْتَرْنَاهُمْ عَلَىٰ عِلْمٍ عَلَى الْعَالَمِينَ"
“Na kwa yakini Tuliwakhitari (wana wa Israaiyl) kwa elimu kuliko walimwengu wowote”. [Ad-Dukhaan: 32]
Kwa msingi huu, "العَالَمِيْنَ" inaweza kubeba maana ya aina zote za viumbe, au wanadamu tu. Ni jina linalowahusu viumbe wote ambao kupitia kwao Allaah Anajulikana, nao ndio dalili ya uwepo Wake na hususan kwa watambuzi kama Malaika. Na kwa muktadha huu, ni lazima jina libebe maana ya ujumla isipokuwa kama itakuja dalili ya kulihusisha na kiumbe fulani pasi na wengineo.
Kauli ya pili: Ni ya Ibn Hazm na wengineo. Wanasema kwamba Malaika wamewazidi wanadamu katika hali zote. Dalili zao ni:
1- Kauli Yake Ta’aalaa:
"وَلَقَدْ كَرَّمْنَا بَنِي آدَمَ وَحَمَلْنَاهُمْ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ وَرَزَقْنَاهُم مِّنَ الطَّيِّبَاتِ وَفَضَّلْنَاهُمْ عَلَىٰ كَثِيرٍ مِّمَّنْ خَلَقْنَا تَفْضِيلًا"
“Na kwa yakini Tumewakirimu wana wa Aadam, na Tukawabeba katika nchi kavu na baharini, na Tukawaruzuku katika vizuri na Tukawafadhilisha juu ya wengi miongoni mwa Tuliowaumba kwa ufadhilisho mkubwa”. [Al-Israa: 70]
Ibn Hazm amesema kuhusu aayah hii: “Allaah Amemfadhilisha mwanadamu juu ya viumbe wengi Aliowaumba lakini si juu ya viumbe wote. Hakuna shaka yoyote kwamba wanadamu ni bora kuliko majini, wanyama na viumbe visivyo na roho, lakini kiumbe pekee anayetolewa nje ya duara hilo ni Malaika ambao Allaah Amewafadhilisha juu ya mwanadamu”.
2- Kauli Yake Ta’aalaa:
"لَّن يَسْتَنكِفَ الْمَسِيحُ أَن يَكُونَ عَبْدًا لِّلَّـهِ وَلَا الْمَلَائِكَةُ الْمُقَرَّبُونَ ۚ وَمَن يَسْتَنكِفْ عَنْ عِبَادَتِهِ وَيَسْتَكْبِرْ فَسَيَحْشُرُهُمْ إِلَيْهِ جَمِيعًا "
“Al-Masiyh kamwe hatojiona bora aje akatae kuwa ni mja kwa Allaah, wala Malaika waliokurubishwa. Na atakayejiona bora akakataa Kumwabudu (Allaah) na akatakabari, basi Atawakusanya wote Kwake. [An-Nisaa: 172]
Ibn Hazm kasema pia kuhusu aayah hii: “Neno Lake Ta’aalaa baada ya kumtaja Al-Masiyh: “Wala Malaika waliokurubishwa”, ni kielelezo wazi kuhusu daraja kubwa waliyonayo Malaika ya ukaribu wao kwa Allaah Mtukufu”.
3- Al-Hadiyth Al-Qudsiy:
Imesimuliwa na Abu Hurayrah: “Kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"يَقُولُ اللَّهُ تَعَالَى: أَنَا عِنْدَ ظَنِّ عَبْدِي بِي، وَأَنَا مَعَهُ إِذَا ذَكَرَنِي، فَإِنْ ذَكَرَنِي فِي نَفْسِهِ ذَكَرْتُهُ فِي نَفْسِي، وَإِنْ ذَكَرَنِي فِي مَلَأٍ ذَكَرْتُهُ فِي مَلَأٍ خير مِنْهُم"
“Allaah Ta’aalaa Anasema: Mimi Niko kwa mujibu wa dhana ya Mja Wangu anavyonidhania, na Mimi Ninakuwa pamoja naye anaponidhukuru. Akinidhukuru ndani ya nafsi yake, Mimi Nitamdhukuru ndani ya Nafsi Yangu, na Akinidhukuru katika hadhira, Mimi Nitamdhukuru katika hadhira iliyo bora zaidi kuliko hiyo”. [Swahiyhul Bukhaariy: 7405]
Ibn Battwaal amesema: “Hadithi hii ni uthibitisho kwamba Malaika ni bora kuliko wanadamu, na hii ndiyo kauli ya jopo la ‘Ulamaa”.
Kauli ya tatu: ‘Ulamaa wa kundi hili wameamua kukaa kimya kuhusiana na suala hili. Wameamua kutosema ni nani mbora kati ya wawili hawa. Wametosheka kusema tu kwamba lililo wajibu kwetu ni kuamini Malaika na Manabii, na si kuamini kundi lipi lililo bora kuliko jingine, na kama hili lingekuwa ni wajibu, basi lingegusiwa na Qur-aan au Sunnah”.
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/246
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11727&title=Malaika
[3] http://www.alhidaaya.com/
[4] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11728&title=01-Malaika%3A%20Malaika%20Ni%20Nani%3F
[5] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11729&title=02-Malaika%3A%20Hukmu%20Ya%20Kuamini%20Malaika
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11737&title=03-Malaika%3A%20Jogoo%20Ana%20Uwezo%20Wa%20Kumwona%20Malaika
[7] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11738&title=04-Malaika%3A%20Maana%20Ya%20Kuwaamini%20Malaika
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11739&title=05-Malaika%3A%20Matunda%20Ya%20Kuamini%20Malaika
[9] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11740&title=06-Malaika%3A%20Malaika%20Jibriyl
[10] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11741&title=07-Malaika%3A%20Malaika%20Miykaaiyl
[11] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11742&title=08-Malaika%3A%20Israafiyl%20na%20Maalik
[12] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11743&title=09-Malaika%3A%20Munkar%20Na%20Nakiyr
[13] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11744&title=10-Malaika%3A%20Haaruwta%20na%20Maaruwta
[14] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11745&title=11-Malaika%3A%20Malakul%20Mawt%20%28Malaika%20Wa%20Kutoa%20Roho%29
[15] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11746&title=12-Malaika%3A%20Malaika%20Mlinzi%20Wa%20Pepo%20
[16] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11747&title=13-Malaika%3A%20Malaika%20Wameumbwa%20Kutokana%20Na%20Nuru
[17] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11748&title=14-Malaika%3A%20Lini%20Waliumbwa%20Malaika%3F
[18] https://dorar.net/aqeeda/1075
[19] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11749&title=15-Malaika%3A%20%20Je%2C%20Tunaweza%20Kuwaona%20Malaika%20Katika%20Umbile%20Lao%20Halisi%3F
[20] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11750&title=16-Malaika%3A%20%20Mbawa%20Za%20Malaika
[21] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11751&title=17-Malaika%3A%20%20Je%2C%20Malaika%20Wana%20Sifa%20Ya%20Uzuri%20Wa%20Sura%20Na%20Umbo%3F
[22] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11752&title=18-Malaika%3A%20%20Malaika%20Wenye%20Sura%20Na%20Maumbo%20Ya%20Kutisha%3A%20%281%29-%20%20Maalik%20Mlinzi%20Na%20Msimamizi%20Wa%20Jahannam
[23] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11753&title=19-Malaika%3A%20%20Malaika%20Wenye%20Sura%20Na%20Maumbo%20Ya%20Kutisha%3A%20%282%29-%20%20Zabaaniyah%20Wa%20Jahannam
[24] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11754&title=20-Malaika%3A%20%20Malaika%20Wenye%20Sura%20Na%20Maumbo%20Ya%20Kutisha%3A%20%283%29-%20%20Munkar%20Na%20Nakiyr
[25] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11755&title=21-Malaika%3A%20%20Malaika%20Wenye%20Sura%20Na%20Maumbo%20Ya%20Kutisha%3A%20%20%284%29-%20%20Malaika%20Wenye%20Kutoa%20Roho%20Ya%20Kafiri
[26] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11756&title=22-Malaika%3A%20%20Malaika%20Wana%20Uwezo%20Wa%20Kujigeuza%20Umbo%20Jingine%20Lisilo%20Lao
[27] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11757&title=23-Malaika%3A%20%20Malaika%20Hawana%20Sifa%20Ya%20Jinsia%20Ya%20Kiume%20Wala%20Ya%20Kike
[28] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11758&title=24-Malaika%3A%20%20Malaika%20Hawali%2C%20Hawanywi%2C%20Hawaoani%20Wala%20Hawazai
[29] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11759&title=25-Malaika%3A%20%20Malaika%20Hawachoki%20Wala%20Hawahisi%20Tabu
[30] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11760&title=26-Malaika%3A%20%20Makazi%20Ya%20Malaika
[31] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11761&title=27-Malaika%3A%20%20Idadi%20Ya%20Malaika
[32] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11762&title=28-Malaika%3A%20%20Je%2C%20Malaika%20Wanakufa%3F
[33] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11763&title=29-Malaika%3A%20%20Malaika%20Ni%20Waja%20Wa%20Allaah%20Na%20Hawana%20Sifa%20Za%20Kiola
[34] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11764&title=30-Malaika%3A%20%20Aina%20Za%20Ibada%20Ambazo%20Malaika%20Wanazifanya%3A%20%281%29-%20Kumsabbih%20Allaah
[35] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11765&title=31-Malaika%3A%20%20Aina%20Za%20Ibada%20Ambazo%20Malaika%20Wanazifanya%3A%20%20%282%29-%20Kupanga%20Safu%20Zilizonyooka%20Kwa%20Ajili%20Ya%20Ibada
[36] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11766&title=32-Malaika%3A%20%20Aina%20Za%20Ibada%20Ambazo%20Malaika%20Wanazifanya%3A%20%20%283%29-%20Kutufu%20Al-Baytul%20Ma%E2%80%99amuwr
[37] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11767&title=33-Malaika%3A%20%20Aina%20Za%20Ibada%20Ambazo%20Malaika%20Wanazifanya%3A%20%20%284%29-%20Kumwogopa%20Allaah
[38] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11768&title=34-Malaika%3A%20%20Malaika%20Wana%20Sifa%20Ya%20Kuona%20Haya
[39] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11769&title=35-Malaika%3A%20%20Malaika%20Ni%20Wajuzi%20Wa%20Kutekeleza%20Kazi%20Zao
[40] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11770&title=36-Malaika%3A%20%20Malaika%20Wanazungumza
[41] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11771&title=37-Malaika%3A%20%20Malaika%20Wamejipanga%20Vizuri%20Katika%20Mambo%20Yao%20Yote
[42] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11772&title=38-Malaika%3A%20%20%20Kazi%20Za%20Malaika%3A%20%20%281%29-%20Jibriyl%20%28%E2%80%98alayhis%20salaam%29%3A%20Kumteremshia%20Qur-aan%20Tukufu%20Nabiy%20%28Swalla%20Allaah%20%E2%80%98alayhi%20wa%20aalihi%20wa%20sallam%29.
[43] https://dorar.net/aqeeda/1077
[44] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11773&title=39-Malaika%3A%20%20%20Kazi%20Za%20Malaika%3A%20%20%282%29-%20Miykaaiyl%20%28%E2%80%98alayhis%20salaam%29%3A%20%20Anasimamia%20Mawingu%20Ya%20Kuleta%20Mvua%20Na%20Mimea
[45] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11774&title=40-Malaika%3A%20%20%20Kazi%20Za%20Malaika%3A%20%20%283%29-%20Atakayepuliza%20Baragumu%20Siku%20Ya%20Qiyaamah
[46] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11775&title=41-Malaika%3A%20%20%20Kazi%20Za%20Malaika%3A%20%20%284%29-%20Malaika%20Wabebao%20%E2%80%98Arshi
[47] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11776&title=42-Malaika%3A%20%20%20Kazi%20Za%20Malaika%3A%20%20%20%20%285%29-%20Malaika%20Wa%20Milima
[48] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11777&title=43-Malaika%3A%20%20%20Kazi%20Za%20Malaika%3A%20%20%20%20%286%29-%20Malaika%20Wa%20Tumbo%20La%20Uzazi
[49] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11778&title=44-Malaika%3A%20%20%20Kazi%20Za%20Malaika%3A%20%20%20%20%287%29-%20Malaika%20Wa%20Kumlinda%20Mwanadamu%20Na%20Hatari
[50] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11779&title=45-Malaika%3A%20%20%20Kazi%20Za%20Malaika%3A%20%20%20%20%288%29-%20Malaika%20Wa%20Kusajili%20Amali%20Za%20Kheri%20Na%20Shari%20Za%20Binadamu
[51] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11782&title=46-Malaika%3A%20%20%20Kazi%20Za%20Malaika%3A%20%289%29-%20Malaika%20Wanaozunguka%20Kwenye%20Njia%20Na%20Barabara%20Kutafuta%20Majaalis%20Za%20Dhikr
[52] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11783&title=47-Malaika%3A%20%20%20Kazi%20Za%20Malaika%3A%20%2810%29-%20Malaika%20Wenye%20Kuizuru%20Al-Baytul%20Ma%E2%80%99amuwr
[53] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11784&title=48-Malaika%3A%20%20%20Kazi%20Za%20Malaika%3A%20%20%2811%29-%20Malaika%20Mwenye%20Kutoa%20Roho
[54] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11785&title=49-Malaika%3A%20%20%20Kazi%20Za%20Malaika%3A%20%20%2812%29-%20Malaika%20Wanaowasaili%20Maiti%20Kaburini
[55] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11786&title=50-Malaika%3A%20%20%20Kazi%20Za%20Malaika%3A%20%20%2813%29-%20Malaika%20Wasimamizi%20Na%20Walinzi%20Wa%20Pepo
[56] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11787&title=51-Malaika%3A%20%20%20Kazi%20Za%20Malaika%3A%20%20%2814%29-%20Malaika%20Walinzi%20Na%20Malaika%20Wa%20Adhabu%20Wa%20Moto%20%28Zabaaniyah%29
[57] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11788&title=52-Malaika%3A%20%20%20Kazi%20Za%20Malaika%3A%20%20%2815%29-%20Malaika%20Wenye%20Kuwasaidia%20Manabii%20Na%20Mitume%20Na%20Kuwaangamiza%20Makafiri
[58] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11789&title=53-Malaika%3A%20%20%20Nafasi%20Ya%20Malaika%20Kwa%20Waumini%3A%20%20%2801%29-%20%20Malaika%20Wanawapenda%20Waumini
[59] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11790&title=54-Malaika%3A%20%20%20Nafasi%20Ya%20Malaika%20Kwa%20Waumini%3A%20%20%20%20%2802%29%E2%80%93%20Malaika%20Wanawatia%20Nguvu%20Waumini%20Na%20Kuwaelekeza
[60] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11791&title=55-Malaika%3A%20%20%20Nafasi%20Ya%20Malaika%20Kwa%20Waumini%3A%20%20%20%20%2803%29%E2%80%93%20Malaika%20Wanawaombea%20Dua%20Waumini
[61] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11792&title=56-Malaika%3A%20%20%20Nafasi%20Ya%20Malaika%20Kwa%20Waumini%3A%20%20%20%20%2804%29%E2%80%93%20Malaika%20Wanaitikia%20%E2%80%9CAamiyn%E2%80%9D%20Kwa%20Dua%20Za%20Waumini
[62] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11793&title=57-Malaika%3A%20%20%20Nafasi%20Ya%20Malaika%20Kwa%20Waumini%3A%20%20%20%20%2805%29%E2%80%93%20Malaika%20Wanawaombea%20Maghfirah%20Waumini
[63] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11794&title=58-Malaika%3A%20%20%20Nafasi%20Ya%20Malaika%20Kwa%20Waumini%3A%20%20%20%20%2806%29%E2%80%93%20Malaika%20Wanahudhuria%20Vikao%20Vya%20Ki%E2%80%99ilmu%2C%20Halaqah%20Za%20Dhikri%2C%20Na%20Huwafunika%20Wahusika%20Kwa%20Mbawa%20Zao
[64] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11795&title=59-Malaika%3A%20%20%20Nafasi%20Ya%20Malaika%20Kwa%20Waumini%3A%20%20%20%20%2807%29%E2%80%93%20Malaika%20Wanasajili%20Majina%20Ya%20Wenye%20Kuhudhuria%20Swalah%20Ya%20Ijumaa
[65] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11796&title=60-Malaika%3A%20%20%20Nafasi%20Ya%20Malaika%20Kwa%20Waumini%3A%20%20%20%20%2808%29%E2%80%93%20Malaika%20Wanasajili%20Maneno%20Mema%20Wanayotamka%20Waja
[66] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11797&title=61-Malaika%3A%20%20%20Nafasi%20Ya%20Malaika%20Kwa%20Waumini%3A%20%20%20%20%2809%29%E2%80%93%20Malaika%20Wanapokezana%20Zamu%20Usiku%20Na%20Mchana%20Kuwafuatilia%20Waumini
[67] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11798&title=62-Malaika%3A%20%20%20Nafasi%20Ya%20Malaika%20Kwa%20Waumini%3A%20%20%20%20%2810%29%E2%80%93%20Malaika%20Wanateremka%20Wakati%20Muumini%20Anasoma%20Qur-aan
[68] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11799&title=63-Malaika%3A%20%20%20Nafasi%20Ya%20Malaika%20Kwa%20Waumini%3A%20%20%20%20%2811%29%E2%80%93%20Malaika%20Wanamfikishia%20Rasuli%20%28Swalla%20Allaah%20%E2%80%98alayhi%20wa%20aalihi%20wa%20sallam%29%20Salamu%20Toka%20Kwa%20Umma%20Wake%20Baada%20Ya%20Yeye%20Kufariki
[69] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11800&title=64-Malaika%3A%20%20%20Nafasi%20Ya%20Malaika%20Kwa%20Waumini%3A%20%20%20%20%2812%29%E2%80%93%20Malaika%20Wanawapa%20Habari%20Njema%20Waumini
[70] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11801&title=65-Malaika%3A%20%20%20Nafasi%20Ya%20Malaika%20Kwa%20Waumini%3A%20%20%20%20%2813%29%E2%80%93%20Malaika%20Wanapigana%20Pamoja%20Na%20Waumini%20Na%20Wanawaimarisha%20Na%20Kuwatia%20Nguvu%20Vitani
[71] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11802&title=66-Malaika%3A%20%20%20Nafasi%20Ya%20Malaika%20Kwa%20Waumini%3A%20%20%20%20%2814%29%E2%80%93%20Malaika%20Wanamlinda%20Rasuli%20%28Swalla%20Allaah%20%E2%80%98alayhi%20wa%20aalihi%20wa%20sallam%29%20Dhidi%20Ya%20Maadui%20Zake
[72] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11803&title=67-Malaika%3A%20%20%20Nafasi%20Ya%20Malaika%20Kwa%20Waumini%3A%20%20%20%20%2815%29%E2%80%93%20Wanahudhuria%20Mazishi%20Ya%20Baadhi%20Ya%20Watu%20Wema
[73] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11804&title=68-Malaika%3A%20%20%20Nafasi%20Ya%20Malaika%20Kwa%20Waumini%3A%20%20%20%20%2816%29%E2%80%93%20Wanamfunika%20Aliyekufa%20Kishahidi%20Kwa%20Mbawa%20Zao
[74] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11805&title=69-Malaika%3A%20%20%20Nafasi%20Ya%20Malaika%20Kwa%20Waumini%3A%20%20%20%20%2817%29%E2%80%93%20Malaika%20Waliokuja%20Na%20Kasha%20Lenye%20Utulivu%20Ndani%20Yake
[75] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11806&title=70-Malaika%3A%20%20%20Nafasi%20Ya%20Malaika%20Kwa%20Waumini%3A%20%20%20%20%2818%29%E2%80%93%20Malaika%20Watailinda%20Makkah%20Na%20Madiynah%20Kutokana%20Na%20Dajjaal
[76] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11807&title=71-Malaika%3A%20%20%20Nafasi%20Ya%20Malaika%20Kwa%20Waumini%3A%20%20%20%20%2819%29%E2%80%93%20Malaika%20Wanawateremshia%20Makafiri%20Adhabu
[77] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11808&title=72-Malaika%3A%20%20%20Nafasi%20Ya%20Malaika%20Kwa%20Waumini%3A%20%20%20%20%2820%29%E2%80%93%20Malaika%20Wanawalaani%20Makafiri%20na%20Baadhi%20Ya%20Watu%20Mafasiki
[78] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11809&title=73-Malaika%3A%20%20%20Wanachopaswa%20Waumini%20Kukitenda%20Kwa%20Ajili%20Ya%20Malaika%3A%20%20%20%20%2801%29-%20Kujiepusha%20Na%20Kila%20Jambo%20Linalowaudhi%20Au%20Kuwakera
[79] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11810&title=74-Malaika%3A%20%20%20Wanachopaswa%20Waumini%20Kukitenda%20Kwa%20Ajili%20Ya%20Malaika%3A%20%20%20%20%2802%29-%20Kuwapenda%20Wote%20Bila%20Kubagua
[80] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11811&title=75-Malaika%3A%20%20%20Malaika%20Wanazidiana%20Kwa%20Daraja
[81] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11812&title=76-Malaika%3A%20%20%20Kuzidiana%20Ubora%20Kati%20Ya%20Malaika%20Na%20Wanadamu