Alhidaaya.com
Published on Alhidaaya.com (https://www.alhidaaya.com/sw)

Ukurasa Wa Kwanza > Malaika > 60-Malaika: Nafasi Ya Malaika Kwa Waumini: (08)– Malaika Wanasajili Maneno Mema Wanayotamka Waja

60-Malaika: Nafasi Ya Malaika Kwa Waumini: (08)– Malaika Wanasajili Maneno Mema Wanayotamka Waja

 

Malaika

 

Alhidaaya.com [1]

 

60:   Nafasi Ya Malaika Kwa Waumini  

 

(08)– Malaika Wanasajili Maneno Mema Wanayotamka Waja

 

Imepokelewa toka kwa Rifa’ah bin Raafi Az-Zuraqiy (Radhwiya Allaah ‘anhu):

 

قَالَ كُنَّا يَوْمًا نُصَلِّي وَرَاءَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَلَمَّا رَفَعَ رَأْسَهُ مِنَ الرَّكْعَةِ قَالَ ‏"‏ سَمِعَ اللَّهُ لِمَنْ حَمِدَهُ ‏"‏‏.‏ قَالَ رَجُلٌ وَرَاءَهُ رَبَّنَا وَلَكَ الْحَمْدُ، حَمْدًا كَثِيرًا طَيِّبًا مُبَارَكًا فِيهِ، فَلَمَّا انْصَرَفَ قَالَ ‏"‏ مَنِ الْمُتَكَلِّمُ ‏"‏‏.‏ قَالَ أَنَا‏.‏ قَالَ ‏"‏ رَأَيْتُ بِضْعَةً وَثَلاَثِينَ مَلَكًا يَبْتَدِرُونَهَا، أَيُّهُمْ يَكْتُبُهَا أَوَّلُ ‏"‏‏

 

“Tulikuwa siku moja tunaswali nyuma ya Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na aliponyanyua kichwa chake toka kwenye rukuu alisema:  Sami’a Allaah liman hamidah (Allaah Amemsikia aliyemhimidi).  Mtu mmoja nyuma yake akasema:  Rabbanaa walakal hamdu, hamdan kathiyran mubaarakan fiyh (Ee Mola wetu, ni Yako himdi, himdi nyingi njema iliyo na baraka ndani yake).  Alipomaliza swalah akauliza:  Nani aliyetamka?  Nikasema:  Ni mimi.  Akasema:  Nimewaona Malaika thelathini na kidogo hivi wakilishindania, nani awe wa mwanzo kuliandika kabla ya mwenziye”.  [Swahiyhul Bukhaariy (799)]

 

Hadiyth hii inatufunza fadhla kubwa ya kumhimidi Allaah na kumdhukuru, na pia uhalali kwa maamuma kusoma dhikri kwa sauti kidogo nyuma ya imamu bila kumbughudhi aliye karibu yake.

 

 

Share [2]
www.alhidaaya.com

Source URL: https://www.alhidaaya.com/sw/node/11796

Links
[1] http://www.alhidaaya.com/
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11796&title=60-Malaika%3A%20%20%20Nafasi%20Ya%20Malaika%20Kwa%20Waumini%3A%20%20%20%20%2808%29%E2%80%93%20Malaika%20Wanasajili%20Maneno%20Mema%20Wanayotamka%20Waja