كتاب الزواج
Kitabu Cha Ndoa
الخِطْبَةُ وأَحْكَامُهَا
Posa Na Hukumu Zake
Abu Maalik Kamaal Bin As-Sayyid Saalim
Imetarjumiwa na 'Abdullaah Mu'aawiyah (Abu Baasim)
Alhidaaya.com
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الخِطْبَةُ وأَحْكَامُهَا
Posa Na Hukumu Zake
Alhidaaya.com [3]
01: Taarifu Na Hukmu Yake:
"الخِطْبَةُ" kwa kutia “kasrah” kwenye “khaaun”, ni ombi la kutaka kumwoa mwanamke. Ikiwa ombi litakubaliwa, basi linageuka na kuwa ni ahadi ya ndoa, lakini haimaanishi kwamba ndoa ishafungika, bali mwanamke ataendelea kuwa ni ajnabiyya (mwanamke wa kando) kwa mpeleka posa huyo mpaka pale ndoa itakapofungwa na kuwa ni mkewe.
Hukmu Yake:
Posa si sharti ya kuswihi kwa ndoa. Kama ndoa itafungwa bila kuwepo posa, basi ndoa hiyo ni sahihi, kwa kuwa aghalabu posa inakuwa ni njia ya kufikia kwenye nikaah. Kwa upande wa Jumhuwr ya ‘Ulamaa, posa ni jambo lenye kujuzu kutokana na Kauli Yake Ta’aalaa:
"وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِيمَا عَرَّضْتُم بِهِ مِنْ خِطْبَةِ النِّسَاءِ"
“Wala si dhambi juu yenu katika ambayo mmedokezea ya kuposa wanawake”. [Al-Baqarah: 235]
Ama kwa ‘Ulamaa wa Kishaafi’iy, ni jambo linalopendeza kutokana na alivyofanya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipomposa ‘Aaishah bint Abiy Bakr na Hafswah bint ‘Umar.
Mchakato huu utakwenda ikiwa hakuna kizuizi chochote kwa mwanamke kuolewa. Na kama kipo, basi posa haifai.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الخِطْبَةُ وأَحْكَامُهَا
Posa Na Hukumu Zake
Alhidaaya.com [3]
02: Ni Nani Anayekabidhiwa Posa?
1- Kiasili, posa inapelekwa kwa walii wa mwanamke:
Toka kwa ‘Urwah:
"أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ خَطَبَ عَائِشَةَ إِلَى أَبِي بَكْرٍ، فَقَالَ لَهُ أَبُو بَكْرٍ: إِنَّمَا أَنَا أَخُوكَ، فَقَالَ: أَنْتَ أَخِي فِي دِينِ اللَّهِ وَكِتَابِهِ وَهِىَ لِي حَلاَلٌ"
“Kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimweleza Abu Bakr shauri la kumposa ‘Aaishah. Abu Bakr akamwambia: “Hakika mimi ni nduguyo. Rasuli akamwambia: “Wewe ni ndugu yangu katika Dini ya Allaah na Kitabu Chake, lakini yeye kwangu ni halali”. [Imechakatwa na Al-Bukhaariy (5081)]
2- Mwanamke mkomavu anayejitambua anaweza kupokea posa ya kuchumbiwa yeye mwenyewe au kuikataa:
Ni kwa Hadiyth ya Ummu Salamah:
"لَمَّا مَاتَ أَبُو سَلَمَةَ أَرْسَلَ إِلَىَّ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ حَاطِبَ بْنَ أَبِي بَلْتَعَةَ يَخْطُبُنِي لَهُ فَقُلْتُ: إِنَّ لِي بِنْتًا وَأَنَا غَيُورٌ"
“Alipokufa Abu Salamah, Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimtuma Haatwib bin Abu Balta’ah aniletee posa yake ya kunichumbia mimi. Nikamwambia: Mimi nina binti, na mimi nina wivu sana”. [Hadiyth Swahiyh. Muslim na An-Nasaaiy (6/81)]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الخِطْبَةُ وأَحْكَامُهَا
Posa Na Hukumu Zake
Alhidaaya.com [3]
03: Inajuzu Walii Kumtangazia Bintiye Kwa Watu Anaowaona Kuwa Wana Vigezo Vya Kumwoa:
1- Mzee mwema alimwambia Muwsaa ‘Alayhis salaam:
"قَالَ إِنِّي أُرِيدُ أَنْ أُنكِحَكَ إِحْدَى ابْنَتَيَّ هَاتَيْنِ عَلَىٰ أَن تَأْجُرَنِي ثَمَانِيَ حِجَجٍ"
“Akasema: Mimi nataka nikuozeshe mmojawapo wa binti zangu hawa wawili kwa sharti kuwa unitumikie miaka minane”. [Al-Qaswas: 27]
2- Katika Swahiyh, ni kwamba ‘Umar bin Al-Khattwwaab wakati binti yake Hafswah alipoondokewa na mumewe Khunays bin Hudhaafah As-Sahmiy, alimdokezea kwa ‘Uthmaan, kisha kwa Abu Bakr, na hatimaye Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwoa. [Imechakatwa na Al-Bukhaariy (5122)]
3- Ummu Habiybah alisema:
"يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَنْكِحْ أُخْتِي هَمْنَة بنت أبي سُفْيَان، فَقَالَ: أَوَ تُحِبِّينَ ذَاكَ؟ قَالَتْ: نَعَمْ، لَسْتُ بِمُخْلِيَةٍ بِكَ، وَأَحَبُّ مَنْ شَارَكَنِي فِي خَيْرٍ أُخْتِي. قَالَ: فَإِنَّهَا لاَ تَحِلُّ لِي"
“Ee Rasuli wa Allaah! Mwoe dada yangu Hamnah bint Abiy Sufyaan. Rasuli akamuuliza: Unaridhia hilo? Akasema: Na’am, mimi si mke pekee kwako, nina wake wenza wenzangu, na mtu ambaye ningependa zaidi ashirikiane nami katika kheri hii ni dada yangu. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: Huyo kwangu si halali”. [Hadiyth Swahiyh. Imechakatwa na Al-Bukhaariy (5101) na Muslim (1449)]
4- ‘Aliy bin Abu Twaalib amesema:
"قُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ، مَا لِي أَرَاكَ تَنَوَّقُ فِي قُرَيْشٍ وَتَدَعُنَا؟ قَالَ: عِنْدَكَ شَيْءٌ؟ قُلْتُ: بِنْتُ حَمْزَةَ، قَالَ: هِيَ بِنْتُ أَخِي مِنَ الرَّضَاعَةِ"
“Nilimwambia (Rasuli wa Allaah): Ee Rasuli wa Allaah! Mbona umelalia zaidi upande wa Maquraysh na sisi unatusahau! Akauliza: Je, una yeyote? Nikasema: Na’am, binti wa Hamzah. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: Huyo ni binti wa kaka yangu wa kunyonya”. [Hadiyth Swahiyh. Imechakatwa na Muslim (1446) na An-Nasaaiy (6/99)]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الخِطْبَةُ وأَحْكَامُهَا
Posa Na Hukumu Zake
Alhidaaya.com [3]
04: Mwanamke Anaruhusiwa Kisharia Kujinadia Mwenyewe Kwa Mtu Mwema Ili Amwoe:
1- Toka kwa Anas, amesema:
"جَاءَتِ امْرَأَةٌ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ تَعْرِضُ عَلَيْهِ نَفْسَهَا، قَالَتْ: يَا رَسُولَ اللَّهِ أَلَكَ بِي حَاجَةٌ؟ فَقَالَتْ بِنْتُ أَنَسٍ: مَا أَقَلَّ حَيَاءَهَا، وَاسَوْأَتَاهْ وَاسَوْأَتَاهْ. قَالَ أَنَسٌ: هِيَ خَيْرٌ مِنْكِ، رَغِبَتْ فِي النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَعَرَضَتْ عَلَيْهِ نَفْسَهَا"
“Mwanamke mmoja alikuja kwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ili kujitambulisha mwenyewe kwake. Akamwambia: Ee Rasuli wa Allaah! Je, unanihitajia (niwe mkeo)? Binti ya Anas akasema: Kakosa haya kiasi gani mwanamke huyu! Aibu! Aibu! Anas (Radhwiya Allaah ‘anhu) akamwambia: Yeye ni bora kukushinda wewe. Amepata utashi kwa Rasuli na akamweleza bayana dhamira yake”. [Swahiyh. Al-Bukhaariy (5120), An-Nasaaiy (6/78) na Ibn Maajah (2001)]
2- Toka kwa Sahl bin Sa’ad, amesema:
"أَنَّ امْرَأَةً عَرَضَتْ نَفْسَهَا عَلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ لَهُ رَجُلٌ: يَا رَسُولَ اللَّهِ زَوِّجْنِيهَا"
“Kwamba mwanamke mmoja alijielezea mwenyewe kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam). Na hapo mtu mmoja akamwambia: Ee Rasuli wa Allaah! Niozeshe mimi (kama humtaki)”. [Swahiyh. Al-Bukhaariy (5126) na Muslim (1425)]
Hili mwanamke atalifanya kama hakuna fitnah au tatizo lolote. Na kama itakuwepo kama atamweleza mwanaume utashi wake wa kuolewa naye, basi haitojuzu.
"وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ الْفَسَادَ"
“Na Allaah Hapendi ufisadi”. [Al-Baqarah: 205]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الخِطْبَةُ وأَحْكَامُهَا
Posa Na Hukumu Zake
Alhidaaya.com [3]
05: Wanawake Wasiofaa Kuchumbiwa:
1- Wanawake Walioharamishwa kuwaoa milele au kwa muda:
Kwa kuwa posa ni utangulizi wa ndoa, na madhali ndoa imezuilika, basi na posa pia inazuilika. Wanawake walioharamishwa kuwaoa wametajwa nyuma.
Ni vizuri kudokeza hapa kwamba ni halali kumposa mwanamke wa kikafiri (mmajusi na mfano wake) ili mtu amwoe atakaposilimu. [Nihaayatul Muhtaaj]
2- Mwanamke aliye kwenye eda (katika kipindi cha eda tu):
Huyu ingawa anaingia kwenye ujumla wa wanawake walioharamika kuolewa kwa muda -kama ilivyotangulia- ila tu yeye ana ahkaam na changanuo maalumu. Kadhalika, hukmu ya kumchumbia mwenye eda inatofautiana kwa mujibu wa hali yake.
Mwenye Eda Anakuwa Na Hali Tofauti:
(a) Eda ya aliyefiwa na mumewe:
Huyu, mwanaume haruhusiwi kumweleza wazi wazi nia yake ya kumwoa. Kama kumwambia: “Ninataka kukuoa”, au “Eda yako ikimalizika nitakuoa”. Itifaki ya Fuqahaa imeharamisha hili. Pamoja na hivyo, inajuzu kumdokezea hamu ya kumwoa kwa tamshi la kufumbia (lisilo wazi) kama “Huenda nikakutaka”, au “Nani atapata mfano wako?”. Allaah Amesema:
"وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِيمَا عَرَّضْتُم بِهِ مِنْ خِطْبَةِ النِّسَاءِ أَوْ أَكْنَنتُمْ فِي أَنفُسِكُمْ ۚ عَلِمَ اللَّـهُ أَنَّكُمْ سَتَذْكُرُونَهُنَّ وَلَـٰكِن لَّا تُوَاعِدُوهُنَّ سِرًّا إِلَّا أَن تَقُولُوا قَوْلًا مَّعْرُوفًا"
“Wala si dhambi juu yenu katika ambayo mmedokezea ya kuposa wanawake hao au mliyoficha katika nafsi zenu. Allaah Anajua kwamba nyinyi mtawakumbuka lakini msifunge nao ahadi kisiri isipokuwa mseme kauli inayoeleweka kawaida”. [Al-Baqarah: 235]
Sababu ni kuwa ikiwa mwenye nia ya kumwoa mwanamke huyu atamwelezea wazi wazi, basi utashi wake utapata nguvu, na mwanamke huyo anaweza kuongopa kuhusu muda wa kumalizika eda yake.
Sheikh wa Uislamu amesema (32/8): “Na mwenye kufanya hivyo (yaani kumweleza wazi nia ya kumwoa), huyo atastahiki adhabu ya kumkomesha yeye na walio mfano wake. Kadhalika, hatoozeshwa mwanamke huyo kama adhabu kwake”.
Ninasema: “Kati ya picha za kumfumbia, ni ile iliyogusiwa na Ibn ‘Abbaas wakati alipoifasiri Kauli Yake Ta’aalaa:
"وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِيمَا عَرَّضْتُم بِهِ مِنْ خِطْبَةِ النِّسَاءِ"
“Wala si dhambi juu yenu katika ambayo mmedokezea ya kuposa wanawake hao”. [Al-Baqarah: 235]
Akasema: Atasema kumwambia (kwa mfano): “Mimi nataka kuoa, na ningependa zaidi Allaah Anifanyie wepesi kumpata mwanamke mwema”.
(b) Eda ya talaka rejea (ya kwanza na ya pili):
Huyu haijuzu kumchumbia posa ya wazi wala ya kufumbia wakati wa eda yake, kwa sababu mumewe bado ana nafasi ya kumrejea. Allaah Ta’aalaa Amemwita mwenye eda ya talaka rejea mke pale Aliposema:
"وَإِذَا طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ فَبَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَلَا تَعْضُلُوهُنَّ أَن يَنكِحْنَ أَزْوَاجَهُنَّ إِذَا تَرَاضَوْا بَيْنَهُم بِالْمَعْرُوفِ"
“Na mtakapowataliki wanawake wakafikia muda wa kumaliza eda yao; basi msiwazuie kuolewa na waume zao (wa awali) ikiwa wameridhiana baina yao kwa mujibu wa ada”. [Al-Baqarah: 232]
Ndoa ya mwanamke huyu bado ipo, na kumchumbia posa isiyo wazi (ya kufumbia) kunazingatiwa kama ni kuharibu mahusiano yake na mumewe. Na kwa vile talaka imemkwaza na kumsababishia taharuki, anaweza kuongopa kuhusu muda wa kumalizika eda yake ili kulipiza kisasi. Haya ndiyo waliyokubaliana Fuqahaa kwa sauti moja.
(c) Mwenye eda ya talaka tatu:
Kwa itifaki ya ‘Ulamaa, haijuzu kumchumbia mwanamke huyu posa ya wazi. Ama posa ya kufumbia, ‘Ulamaa wamekhitalifiana katika kauli mbili:
Kauli ya kwanza: Inajuzu posa ya kufumbia. Ni madhehebu ya Jumhuwr; wanachuoni wa Kimaalik, Kishaafi’y na Kihanbali. Dalili zao ni:
1- Ujumuishi wa Kauli Yake Ta’aalaa:
"وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِيمَا عَرَّضْتُم بِهِ مِنْ خِطْبَةِ النِّسَاءِ"
“Wala si dhambi juu yenu katika ambayo mmedokezea (mmefumbia) ya kuposa wanawake”. [Al-Baqarah: 235]
2- Hadiyth ya Faatwimah bint Qays ambaye mumewe alipompa talaka tatu, Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia:
" اعْتَدِّي عِنْدَ ابْنِ أُمِّ مَكْتُومٍ فَإِنَّهُ رَجُلٌ أَعْمَى تَضَعِينَ ثِيَابَكِ عِنْدَهُ فَإِذَا حَلَلْتِ فَآذِنِينِي"
“Kaa eda yako kwa Ibn Ummi Maktuwm, yeye ni kipofu, utaweza kuvua nguo zako huko kwake, na eda ukimaliza, basi nijulishe”. [Muslim (1480)]
An-Nawawiy kasema: “Hadiyth hii inaonyesha kwamba inajuzu kumposa aliyepewa talaka tatu kwa kauli fumbo, na hili kwetu ni sahihi”.
3- Ni kwamba mwanamke huyu hawezi kurejea tena kwa mumewe, na hali yake hii ni sawa sawa na yule aliyefiwa na mumewe ambaye hawezi tena kurudi. Hawa wote wawili wako duara moja kinyume na mwenye eda ya talaka rejea.
Kauli ya pili: Haijuzu posa ya kufumbia. Ni madhehebu ya ‘Ulamaa wa Kihanafiy. Dalili zao ni:
1- Kwamba Aayah Tukufu inayohalalisha posa ya kufumbia ilikuja kuhusiana na mwenye eda ya kufiwa na mumewe. Hivyo haijuzu kuwahusisha wanawake wengine wenye eda tofauti na hiyo.
2- Mume aliyetaliki anaweza kupata adha kutokana na posa fumbo hii kwa mkewe, na kuzalisha uadui.
Ninasema: “Kauli yenye nguvu ni kwamba inajuzu kumposa kwa kufumbia kutokana na Hadiyth ya Faatwimah bint Qays. Allaah Ndiye Ajuaye zaidi”.
Faida Mbili:
1- Ikiwa mtu atamchumbia mwanamke posa ya wazi wakati wa eda yake kisha akamwoa baada ya kumalizika eda, mtu huyu atapata madhambi lakini ndoa itakuwa ni sahihi. Na kama atamwoa wakati wa eda yake, hapa ndoa itakuwa ni batili.
2- Endapo mtu atamwoa mwanamke wakati wa eda yake, hawa ni lazima watenganishwe, na mwanamke atakamilisha eda ya mume wa kwanza. Kisha atakaa eda ya mume wa pili kama aliwahi kumuingilia, na mahari atapewa kama alikuwa hajui hukumu ya hilo, na kama anajua kwamba haijuzu kuolewa kabla ya eda kwisha, basi kiongozi wa Waislamu ana haki ya kumpa mahari hiyo au kuipeleka Baytul Maal kama adhabu adabishi (ta’aziyr).
Toka kwa Ibn Al-Musayyib na Sulaymaan bin Yasaar:
"أَنَّ طُلَيْحَةَ الأَسَدِيَّةَ، كَانَتْ تَحْتَ رُشَيْدٍ الثَّقَفِيِّ فَطَلَّقَهَا فَنَكَحَتْ فِي عِدَّتِهَا، فَضَرَبَهَا عُمَرُ بْنُ الْخَطَّابِ وَضَرَبَ زَوْجَهَا بِالْمِخْفَقَةِ ضَرَبَاتٍ وَفَرَّقَ بَيْنَهُمَا، ثُمَّ قَالَ عُمَرُ بْنُ الْخَطَّابِ: أَيُّمَا امْرَأَةٍ نَكَحَتْ فِي عِدَّتِهَا فَإِنْ كَانَ زَوْجُهَا الَّذِي تَزَوَّجَهَا لَمْ يَدْخُلْ بِهَا فُرِّقَ بَيْنَهُمَا ثُمَّ اعْتَدَّتْ بَقِيَّةَ عِدَّتِهَا مِنْ زَوْجِهَا الأَوَّلِ ثُمَّ كَانَ الآخَرُ خَاطِبًا مِنَ الْخُطَّابِ، وَإِنْ كَانَ دَخَلَ بِهَا فُرِّقَ بَيْنَهُمَا ثُمَّ اعْتَدَّتْ بَقِيَّةَ عِدَّتِهَا مِنَ الأَوَّلِ ثُمَّ اعْتَدَّتْ مِنَ الآخَرِ ثُمَّ لاَ يَجْتَمِعَانِ أَبَدًا"
“Kwamba Tulayha Al-Asadiyyah, alikuwa mke wa Rushayd Ath-Thaqafiy ambaye alimwacha talaka tatu. Tulayha akaolewa wakati wa kipindi cha eda. ‘Umar bin Al-Khattwwaab akampiga Tulayha, na akamchapa mumewe (mpya) fimbo kadhaa kisha akawaachanisha. Halafu ‘Umar akasema: Mwanamke yeyote atakayeolewa wakati eda yake bado haijamalizika na mumewe akawa hajamuingilia, basi lazima waachanishwe, kisha atamalizia eda ya mume wake wa awali, na mume wa pili atabaki na nafasi ya kuweza kumposa na kumwoa tena. Na kama atakuwa amemuingilia, basi wataachanishwa, kisha atamalizia eda iliyosalia ya mumewe wa awali. Akimaliza hiyo, atakaa eda ya mume wa pili ambaye hatoruhusiwa kumuoa milele”. [Isnaad yake ni Swahiyh. Imechakatwa na Al-Bayhaqiy (7/441) na Abdulrazzaaq (10539)]
Je, Inafaa Mume Wa Pili Kumposa Na Kumwoa Tena Baada Ya Kumaliza Eda Mbili?
Katika Hadiyth hii, ‘Umar amezuia asimwoe tena milele. Maalik, Al-Layth na Al-Awzaaiy wamesema hivyo hivyo. Ama ‘Aliyy bin Abiy Twaalib, yeye amejuzisha. Toka kwa ‘Atwaa: “Kwamba ‘Aliyy aliletewa kesi kama hiyo akawaachanisha, halafu akamwamuru mwanamke amalizie eda yake ya kwanza, kisha akae eda nyingine ya kando ya wa mume wa pili, na ikimalizika basi atakuwa mwenyewe na hiari; akitaka ataolewa na asipotaka basi”. [Ni Dhwa’iyf, ina Hadiyth wenza. Imechakatwa na Ash-Shaafi’iy katika Al-Ummu (5/233), Al-Bayhaqiy (10/441) na Abdulrazzaaq (10532)]
Jumhuwr wameiunga mkono kauli hii ya ‘Aliyy ambayo ndiyo yenye nguvu kwa kuwa ndio asili mbali na kwamba hukmu ya ‘Umar haina dalili. Inawezekana alihukumu hivyo kama ni adhabu adabishi (ta’aziyr).
(d) Eda inayotokana na nikaha batili au iliyovunjwa:
Ni kama eda ya li’aan (mume kuikataa mimba kwa kumshuhudilia Allaah) au kuritadi, au kwa mwenye kuangalia kama tumboni kuna kitu baada ya kuzini, au aliyeachishwa kutokana na kasoro, au mume kukosa nguvu za kiume na mfano wa hayo. Jumhuwr ya ‘Ulamaa wamesema kwamba inajuzu kumchumbia kwa kufumbia kutokana na ujumuishi wa aayah tukufu, na kwa kuchukulia qiyas cha mwenye talaka tatu, na kwa vile pia mamlaka ya mume yanakuwa hayako tena.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الخِطْبَةُ وأَحْكَامُهَا
Posa Na Hukumu Zake
Alhidaaya.com [3]
06: Kumchumbia Mwanamke Ambaye Amekwishachumbiwa Na Muislamu:
Mwanaume Muislamu akimchumbia mwanamke, basi si halali kwa mwanaume mwingine kumposa.
1- Abu Hurayrah: Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"ولَا يَخْطُبُ الرَّجُلُ عَلَى خِطْبَةِ أَخِيهِ حَتَّى يَنْكِحَ أَو يَتْرُكَ"
“Na mtu asipose juu ya posa ya nduguye mpaka aoe au aachilie”. [Swahiyh. Al-Bukhaariy (5143) na Muslim (1413)]
2- Ibn ‘Umar (Radhwiya Allaah ‘anhu):
"نَهَى النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنْ يَبِيعَ بَعْضُكُمْ عَلَى بَيْعِ بَعْضٍ، وَلاَ يَخْطُبَ الرَّجُلُ عَلَى خِطْبَةِ أَخِيهِ، حَتَّى يَتْرُكَ الْخَاطِبُ قَبْلَهُ، أَوْ يَأْذَنَ لَهُ الْخَاطِبُ"
“Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kuuziana kitu ambacho kimekwishauzwa, au mtu kuposa juu ya posa ya nduguye mpaka mposaji aliyetangulia avunje posa au mposaji amruhusu”. [Swahiyh. Al-Bukhaariy (5142) na Muslim (1412)]
3- ‘Uqbah bin ‘Aamir: Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"الْمُؤْمِنُ أَخُو الْمُؤْمِنِ فَلاَ يَحِلُّ لِلْمُؤْمِنِ أَنْ يَبْتَاعَ عَلَى بَيْعِ أَخِيهِ وَلاَ يَخْطُبَ عَلَى خِطْبَةِ أَخِيهِ حَتَّى يَذَرَ"
“Muumini ni ndugu ya muumini, hivyo basi, haifai muumini kununua kitu alichokwisha nunua nduguye, au kuposa juu ya posa ya nduguye mpaka aiachie posa”. [Swahiyh. Muslim (1414)]
Jumhuwr ya ‘Ulamaa wanasema kwamba katazo hili linabeba sifa ya uharamu kwa sababu kufanya hivi kunasababisha madhara kwa mhusika, kunajenga uadui, chuki, na adha, lakini pia ni uchupiaji wa mipaka ya haki ya Muislamu.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الخِطْبَةُ وأَحْكَامُهَا
Posa Na Hukumu Zake
Alhidaaya.com [3]
07: Ni Upi Mpaka Wa Posa Ambayo Ni Haramu Kuiposea?
‘Ulamaa kwa sauti moja wameharamisha posa juu ya posa ya Muislamu ikiwa mposaji amejibiwa jibu la wazi la kukubaliwa posa yake, lakini pia awe hajatoa idhini kwa mwingine kuposa, na posa awe hajaiachilia, isitoshe mposaji wa pili ajue kwamba kuna mposaji aliyemtangulia ambaye posa yake imekubaliwa.
‘Ulamaa wa Kihanbali hawakushurutisha kukubaliwa posa kwa tamko wazi kuwe ndio kigezo cha kuharamisha posa juu ya posa ya mwingine. Wamesema hata kukubaliwa kwa fumbo ni kigezo cha cha kuharamisha posa juu ya posa ya mwingine. Huenda wamefarijika na Hadiyth isemayo:
"وَإِذْنُهَا صُمَاتُهَا"
“Kunyamaza kwake ndio kukubali kwake”. [Hadiyth Swahiyh]
Hivyo kunyamaza kwake kunakuwa ni dalili ya kukubali kwake!
Ama ‘Ulamaa wa Kishaafi’iy, Kihanafiy na Kimaalik, wao wanaona kwamba kujibiwa mposaji kwa jibu la fumbo hakuharamishi mwingine kuposa juu ya posa yake. Wameitolea dalili hoja yao hiyo kwa Hadiyth ya Faatwimah bint Qays wakati alipomweleza Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba Abu Jahm na Mu’aawiyah wamemposa, na Rasuli akamwamuru aolewe na Usaamah. Wanasema kwamba Rasuli hakukemea kwa nini wachumbie posa juu ya posa, bali yeye mwenyewe akamposea kwa Usaamah.
Na ili posa iwe haramu juu ya posa nyingine, ‘Ulamaa wa Kimaalik wameshurutisha ridhaa ya mwanamke aliyeposwa au walii wake, na mposaji asiwe mtu asiyejali madhambi.
Ninasema: “Ninaloona mimi ni kuwa kwa kule tu Muislamu kupeleka posa kwa mwanamke, kunaifanya posa ya mwingine kuwa haramu kama atajua kuna posa iliyomtangulia. Haitojuzu kupeleka posa wakati huo isipokuwa tu kama atajua kwamba mposaji wa awali amekataliwa, au ameruhusu mwingine apose, au akafuta posa yake. Haya ni madhehebu ya Abu Muhammad bin Hazm, na chaguo la Ash-Shawkaaniy (Allaah Awarehemu wote). Msimamo huu unatiliwa nguvu na Hadiyth ya Ibn ‘Umar kuhusiana na kisa cha ‘Umar bin Al-Khattwaab kumnadia binti yake Hafswah kwa ‘Uthmaan na Abu Bakr, na kisha Abu Bakr kuja kumweleza ‘Umar (Radhwiya Allaah ‘anhumaa) akimwambia: “Hakika hakuna kilichonizuia kukujibu kuhusiana na uliyonidokezea (kuhusu Hafswah) isipokuwa tu mimi nilikwisha jua kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amemtaja. Nisingeliweza kutoboa siri ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Na lau Rasuli asingelimwoa, basi mimi ningelimkubali”. [Hadiyth Swahiyh. Al-Bukhaariy (5145)]
Na hapa tunaona kwamba Abu Bakr kwa kule tu kujua kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ana nia ya kumposa Hafswah, hakuthubutu kumposa au hata kumjibu baba yake ‘Umar, akasubiri Rasuli kama atatimiza azma yake au la. Basi itakuwaje kwa yule ambaye ameshawasilisha posa yake? Na vipi kwa ambaye posa yake isharidhiwa na kukubaliwa?
Ama Hadiyth ya Faatwimah bint Qays, Hadiyth hii haikinzani na Hadiyth nyingine Swahiyh zinazokataza posa juu ya posa. Kwa kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwelekeza baada ya kumshauri huku maamuzi yakiwa bado mkononi mwake.
Na kama itaulizwa: Kwani Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakujua kwamba bibi huyu (Faatwimah) ameposwa na zaidi ya mtu mmoja? Na vipi alimkubalia baada ya kukataza mtu kuposa juu ya posa ya nduguye?
Swali hili linajibiwa hivi: Kuna uwezekano wa kuwa mposaji wa pili alimposa bila kujua kwamba kuna mposaji wa kwanza aliyemtangulia, au posa mbili zilikuja wakati mmoja au muda unaokaribiana. Kadhalika, inawezekana yeye mwenyewe alimkataa mposaji au walii wake, lakini tu yeye akataka ushauri wa Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusiana na kila aliyemposa.
Tunakumbushia hapa tena kwamba hikma ya kukataza posa juu ya posa, ni kuepusha chuki, mipasuko na uadui kati ya ndugu Waislamu. Ni vizuri kuepukana na hili isipokuwa tu kama mposaji wa awali ataruhusu, au ataiachia posa, au akakataliwa na mwanamke au walii wake, hapo hakuna tatizo. Allaah Ndiye Mjuzi wa yote.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الخِطْبَةُ وأَحْكَامُهَا
Posa Na Hukumu Zake
Alhidaaya.com [3]
08: Ikiwa Mtu Ataposa Juu Ya Posa Ya Mwingine Kisha Akamwoa Mwanamke, Je, Itaswihi Ndoa?
Tumeshasema kwamba mtu kuposa juu ya posa ya nduguye ni haramu. Sasa ikiwa mposaji wa pili atamwoa mwanamke badala ya mposaji wa kwanza, hapa ‘Ulamaa wana kauli mbili:
Kauli ya kwanza:
Ndoa hii ni batili, ni lazima waachanishwe. Ni chaguo la Sheikh wa Uislamu ambaye amesema kwamba katazo linaonyesha kuwa kilichokatazwa madhara yake ni makubwa kuliko maslaha yake.
Kauli ya pili:
Ndoa ni sahihi, lakini mwoaji huyo anakuwa ni mwasi na anapata madhambi. Haya ni madhehebu ya Jumhuwr. Wanasema kwamba hakuna mafungamano kati ya uharamu wa posa juu ya posa na kuswihi kwa ndoa ya mposaji wa pili, na kwamba posa si sehemu ya ‘aqdi ya ndoa, na ndoa inaswihi hata bila posa. Isitoshe, kosa la mposaji huyo wa pili linabaki pale pale hata kama hakufunga ndoa.
Ninasema: “Kauli ya Jumhuwr ina nguvu zaidi”.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الخِطْبَةُ وأَحْكَامُهَا
Posa Na Hukumu Zake
Alhidaaya.com [3]
09: Posa Juu Ya Posa Ya Kafiri:
Picha ya suala hili iko hivi: “Dhimmiy” (kafiri anayeishi chini ya himaya ya Dola ya Kiislamu) ameposa mwanamke wa Kinaswara au Kiyahudi na posa ikakubaliwa, kisha akaja Muislamu akaposa mwanamke huyo huyo. Au mposaji ni taarikus swalaah, naye anazingatiwa kafiri na ‘Ulamaa wanaoona kwamba asiyeswali ni kafiri. ‘Ulamaa wana kauli mbili katika hali kama hii:
Kauli ya kwanza:
Inajuzu kuposa juu ya posa. Ni kauli ya Ahmad, Al-Awzaaiy, Ibn Al-Mundhir na Al-Khattwaabiy. Dalili zao ni:
1- Kauli ya Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"الْمُؤْمِنُ أَخُو الْمُؤْمِنِ فَلاَ يَحِلُّ لِلْمُؤْمِنِ أَنْ يَبْتَاعَ عَلَى بَيْعِ أَخِيهِ وَلاَ يَخْطُبَ عَلَى خِطْبَةِ أَخِيهِ حَتَّى يَذَرَ"
“Muumini ni ndugu ya muumini, hivyo basi, haifai muumini kununua kitu alichokwisha nunua nduguye, au kuposa juu ya posa ya nduguye mpaka aiachie posa”. [Swahiyh. Muslim (1414)]
Allaah Ta’aalaa Ameukata udugu kati ya kafiri na Muislamu, hivyo katazo ni kati ya Muislamu na nduguye Muislamu.
2- Uhalali ndio asili katika mambo yote mpaka lije katazo. Na katazo la kuposa juu ya posa nyingine limekuja likiwa limefungamanishwa na Muislamu tu, na mengineyo yanabakia hivyo hivyo katika uhalali wake.
3- Tamshi la katazo linamhusu Muislamu tu na kumwambatisha nalo mwingine kunaswihi ikiwa ni mfano wake. “Dhimmiy” si kama Muislamu, na hadhi yake si sawa na hadhi ya Muislamu, na kwa ajili hiyo, haikuwa ni wajibu kuwaitikia mwaliko wao wa walima au mfano wake.
Kauli ya pili:
Ni haramu kuposa juu ya posa ya kafiri. Ni kauli ya Jumhuwr. Wanasema kwamba hilo linasababisha adha kwa mposaji wa awali.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الخِطْبَةُ وأَحْكَامُهَا
Posa Na Hukumu Zake
Alhidaaya.com [3]
10: Kuulizwa Kuhusu Mposa Na Mposwa Na Kutaja Kasoro Zao:
Mtu akiulizwa na kushauriwa kuhusu mposaji au mposwa, ni lazima aseme ukweli hata ikibidi kutaja mabaya na kasoro zake, na hii haingii kwenye duara la kusengenya kuliko haramishwa ikiwa makusudio yake ni kunasihi na kuhadharisha, na si kumchafua mhusika. Ni kama Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alivyomwambia Faatwimah bint Qays wakati alipomtaka ushauri wake:
""أَمَّا أَبُو جَهْمِ فَرَجُلٌ لا يَضَعُ عَصَاهُ عَنْ عَاتِقِهِ، وَأَمَّا مُعَاوِيَةُ فَصُعْلُوكٌ لاَ مَالَ لَه"
“Ama Abu Jahm, yeye ni mtu ambaye hashushi fimbo yake begani (yaani anapiga sana, au anasafiri sana). ُ Ama Mu’aawiya, huyo ni masikini hohehahe, hana chochote”. [Muslim (1480), An-Nasaaiy (3245) na Abu Daawuwd (2284)]
Na akasema tena:
"إِنَّ الدِّينَ النَّصِيحَةُ"
“Hakika dini (haswa) ni kunasihiana”. [Hadiyth Swahiyh]
Mahala pa kutaja mabaya ni pale tu inapohitajika, ama isipohitajika, basi haifai kuyataja.
Na kama atatakwa ajieleze yeye mwenyewe, basi ni lazima aweke wazi kasoro zake kama vile: “Mimi ni bahili sana”, au “Tabia yangu ni ngumu sana” na mfano wa hivyo. Na kama kuna baadhi ya maasia anayafanya, basi ni lazima atubie haraka na asiyataje. Na kama atawaambia: “Mimi siwafai” bila kueleza sababu za kutofaa, itatosha.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الخِطْبَةُ وأَحْكَامُهَا
Posa Na Hukumu Zake
Alhidaaya.com [3]
11: Istikhaarah Kwa Ajili Ya Posa:
Inapendeza kwa mposaji na mposwa kuswali swalaatul istikhaarah kwa ajili ya jambo la ndoa. Kila mmoja ataswali kumhusu mwenzake, wakati mwafaka wa ndoa na mfano wa hayo. Katika mlango wa swalah, swalatul istikhaarah imeelezewa kimapana pamoja na baadhi ya adabu zake. Imesuniwa kuomba duaa ya istikhaarah kwa ikhlaas, kuikithirisha na kuihimizia. Na hakuna ubaya kuiswali zaidi ya mara moja, kwa kuwa ni du’aa.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الخِطْبَةُ وأَحْكَامُهَا
Posa Na Hukumu Zake
Alhidaaya.com [3]
12: Inajuzu Mtu Kuwa Mshenga:
Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwombea Mughiyth kwa Bariyrah ili akubali kuolewa naye. Bariyrah akamuuliza Rasuli kama hiyo ni amri au la, na Rasuli akamwambia ni ombi tu, na si amri. Bariyrah akamwambia: Simtaki”.
Ibn ‘Umar alikuwa anapoiwasilisha posa ya mtu kwa wahusika anasema:
"الحَمْدُ للهِ وصَلَّى اللهُ عَلَى مُحَمَّدٍ، إنَّ فُلَانًا خَطَبَ إِلَيْكُمْ فُلَاَنةً، إنْ أنكَحْتُمُوهُ فَالْحمْدُ للهِ، وإن ردَدْتُمُوهُ فَسُبْحَانَ اللهِ"
“Himdi Anastahiki Allaah. Allaah Ampe rahmah Muhammad. Hakika fulani ameleta posa kwenu ya fulani, na ikiwa mtamwozesha, basi Himdi Anastahiki Allaah, na kama mtamrejesha, basi Utakasifu ni wa Allaah”. [Isnaad yake ni swahiyh. Imechakatwa na Al-Bayhaqiy (7/181)]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الخِطْبَةُ وأَحْكَامُهَا
Posa Na Hukumu Zake
Alhidaaya.com [3]
13: Je, Mwanaume Anaruhusiwa Kumwangalia Kikaguzi Mwanamke Aliyekusudia Kumposa?:
Jumhuwr ya Wanazuoni wamekubaliana kwamba mwanaume anayekusudia kumwoa mwanamke anaruhusiwa kisharia kumwangalia. Na asili ya hili ni:
1- Neno Lake Ta’aalaa:
"لَّا يَحِلُّ لَكَ النِّسَاءُ مِن بَعْدُ وَلَا أَن تَبَدَّلَ بِهِنَّ مِنْ أَزْوَاجٍ وَلَوْ أَعْجَبَكَ حُسْنُهُنَّ"
“Si halali kwako wanawake wengine baada ya hao na wala kuwabadilisha kwa wake wengine japo kama uzuri wao umekupendeza”. [Al-Ahzaab: 52]
Uzuri hauwezi kujulikana ila kwa kumwangalia.
2- Hadiyth ya Abu Hurayrah aliyesema:
"كُنْتُ عِنْدَ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَأَتَاهُ رَجُلٌ فَأَخْبَرَه أَنَّه تَزَوَّجَ امْرَأَةً من الأَنْصَارِ، فَقَالَ له رَسُوْلُ الله: أَنَظَرْتَ إِلَيْهَا؟ قَالَ: لا، قَالَ: اذْهَبْ فَانْظُرْ إِلَيْهَا فَإِنَّ فِي أَعْيُنِ الْأَنْصَارِ شَيْئًا"
“Nilikuwa kwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam), kisha mtu mmoja akamjia na kumweleza kwamba amemwoa mwanamke wa Kianswaar. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamuuliza: Je, umemwangalia? Akasema: Hapana. Akamwambia: Nenda ukamwangalie, kwani hakika katika macho ya Answaar kuna ila fulani”. [Hadiyth Swahiyh. Muslim (1424) na An-Nasaaiy (6/69)]
3- Hadiyth ya Jaabir aliyesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:
“إذا خَطَبَ أحدُكمُ المرأةَ فَقَدرَ أَنْ يَرَى مِنْهَا بَعْضَ ما يَدْعُوهُ إِلَيْهَا فَلِيَفْعَلْ"
“Mmoja wenu akimposa mwanamke na akaweza kumwona baadhi ya sehemu zitakazomshawishi amwoe, basi na afanye”. [Hadiyth Hasan. Abu Daawuwd (2082), Ahmad (3/360), Al-Haakim (2/165) na Al-Bayhaqiy (7/84)]
4- Hadiyth ya Sahl bin Sa’ad:
"أَنَّ امْرَأَةً جَاءَتْ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَقَالَتْ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، جِئْتُ لأَهَبَ نَفْسِي لَكَ. فَنَظَرَ إِلَيْهَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَصَعَّدَ النَّظَرَ إِلَيْهَا وَصَوَّبَهُ ثُمَّ طَأْطَأَ رَأْسَهُ"
“Kwamba mwanamke mmoja alikuja kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: Ee Rasuli wa Allaah! Nimekuja ili kujitoa mwenyewe kwako (unioe bila mahari). Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamtazama, kisha akamwangalia juu hadi chini halafu akainamisha kichwa chake chini”. [Swahiyh. Al-Bukhaariy (5126) na Muslim (1425)]
5- Hadiyth ya ‘Aaishah aliyesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliniambia:
"أُرِيْتُكِ فِي الْمَنَامِ يَجِيءُ بِكِ الْمَلَكُ فِي سَرَقَةٍ مِنْ حَرِيرٍ، فَقَالَ لِي: هَذِهِ امْرَأَتُكَ. فَكَشَفْتُ عَنْ وَجْهِكِ الثَّوْبَ، فَإِذَا أَنْتِ هِيَ فَقُلْتُ: إِنْ يَكُ هَذَا مِنْ عِنْدِ اللَّهِ يُمْضِهِ".
“Nilionyeshwa wewe kwenye njozi (kabla ya kukuoa). Nilimwona Malaika anakuleta ndani ya kitambaa cha hariri akaniambia: Huyu ni mkeo, nami nikakufunua uso, tahamaki nikakuona ni wewe. Nikasema: Ikiwa hili linatoka kwa Allaah, basi Atalipitisha”. [Hadiyth Swahiyh. Al-Bukhaariy (5125) na Muslim]
6- Al-Mughiyrah bin Shu’ubah alimchumbia mwanamke, na Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia:
"انْظُرْ إِلَيْهَا فَإِنَّهُ أَحْرَى أَنْ يُؤْدَمَ بَيْنَكُمَا "
“Mwangalie, kwani hakika hilo lina nguvu kuleta zaidi matangamano mema kati yenu wawili”. [Al-Albaaniy kasema ni swahiyh. Imechakatwa na At-Tirmidhiy (3087), na iko katika Swahiyh At-Tirmidhiy (934). Ad-Daaraqutwniy ameitia kasoro, lakini hata hivyo ina Hadiyth wenza]
Hikma ya kumwangalia mwanamke wa kumposa ni mtu kujiridhisha mwenyewe kutakakomsukuma kumwoa, na hili bila shaka litakwenda kudumisha maisha ya ndoa kati ya wawili hao. Na hali inaweza kuwa kinyume ikiwa hakumwona hadi ndoa ikafungwa. Anaweza mwanaume kushtukizwa na asiyoyapenda, na matokeo yake ni maisha ya ukorofi.
Ninasema: “Hukmu ya mtu kumwangalia mwanamke aliyemposa kwa Wanachuoni inazungukia kati ya kuwa ni mubaah na kuwa jambo lenye kupendeza ambalo liko karibu zaidi na dalili zilizopita. Hakuna yeyote aliyesema kwamba ni lazima kumwangalia -kwa mujibu wa ninavyojua- mbali na kuwa si sharti ya kuswihi kwa ndoa. Kwa ajili hiyo, Sheikh wa Uislamu amesema: “Ndoa inaswihi hata kama hakumwona”.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الخِطْبَةُ وأَحْكَامُهَا
Posa Na Hukumu Zake
Alhidaaya.com [3]
14: Mipaka Ya Kumwangalia:
Inajuzu kumwangalia uso na vitanga viwili vya mikono. Ni kauli isiyo na mvutano kati ya ‘Ulamaa waliojuzisha hili. Lakini walichokhitilafiana ni sehemu ambazo inajuzu kuziangalia zaidi ya uso na vitanga. Katika hili, kuna kauli nne:
Kauli ya kwanza:
Haangaliwi isipokuwa uso na mikono tu. Ni kauli ya Jumhuwr wanaosema kwamba uso ndio sehemu inayoonyesha uzuri na ujamala wa mwanamke, na vitanga ndivyo vinavyoashiria urutuba wa mwili wake. Lakini pia, viungo hivi viwili ndivyo ambavyo kikawaida huonekana, na hivyo basi, kuonekana vingine zaidi yake hairuhusiwi.
Kauli ya pili:
Ni halali kumwangalia viungo ambavyo aghlabu huonekana kama shingo, mikono miwili na miguu miwili. Hii ni kauli ya Mahanbali. Dalili yao wanasema kwamba wakati Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliporuhusu mwanamke kuangaliwa bila yeye kujua, ina maana aliruhusu kumwangalia zile sehemu ambazo kikawaida huonekana. Isitoshe, kwa vile sharia imeruhusu mwanamke huyo atazamwe, hapo mwanaume ana ruhusa ya kumwangalia sawa na wanavyomwangalia maharimu zake.
Kauli ya tatu:
Anaruhusika kumwangalia sehemu yoyote aitakayo isipokuwa utupu. Haya ni madhehebu ya Al-Awzaaiy.
Kauli ya nne:
Anaruhusika kumwangalia mwili wote. Ni madhehebu ya Daawuwd, Ibn Hazm na riwaayah ya tatu toka kwa Ahmad. Ni kwa ubayana wa neno la Rasuli:
"انْظُرْ إِلَيْهَا"
“Mwangalie”.
Ninasema: “Lenye nguvu ambalo nafsi inatulia kwalo ni kwamba mtu anapokwenda kumposa mwanamke, basi mwanamke huyo atamwonyesha uso wake na viganja viwili kama walivyosema Jumhuwr. Ama ikiwa mposaji huyo atajificha, basi atamwangalia sehemu zile ambazo zitamvutia na kumfanya amwoe. Hatakikani kumtaka amfunulie mwili wake zaidi ya uso na viganja. Lakini pamoja na hayo, ana haki ya kuulizia viungo vingine zaidi ya hivyo viwili kutoka kwa mama ya mwanamke au dada yake, au akajificha ili kuona hayo ayatakayo ya ziada. Allaah Ndiye Ajuaye zaidi”.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الخِطْبَةُ وأَحْكَامُهَا
Posa Na Hukumu Zake
Alhidaaya.com [3]
15: Je, Ni Sharti Mwanamke Anayeposwa Atakwe Idhini Ya Kuangaliwa Na Ajue Hilo?
Jumhuwr ya ‘Ulamaa wanasema kwamba si sharti mwanamke ajue au atakwe idhini yeye au walii wake, inatosha tu kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameruhusu hilo. Ni kama ilivyo kwenye Hadiyth ya Jaabir iliyotangulia kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إِذَا خَطَبَ أَحَدُكُمُ الْمَرْأَةَ فَإِنِ اسْتَطَاعَ أَنْ يَنْظُرَ إِلَى مَا يَدْعُوهُ إِلَى نِكَاحِهَا فَلْيَفْعَلْ". قَالَ: فَخَطَبْتُ جَارِيَةً فَكُنْتُ أَتَخَبَّأُ لَهَا حَتَّى رَأَيْتُ مِنْهَا مَا دَعَانِي إِلَى نِكَاحِهَا وَتَزَوُّجِهَا فَتَزَوَّجْتُهَا"
“Akimposa mmoja wenu mwanamke na akaweza kumwangalia pale ambapo patamshawishi kumwoa, basi na afanye. Akasema: Nikamposa msichana, na nikawa najificha kumwangalia, mpaka nikaona kilichonivuta kumwoa, na nikamwoa”. [Hadiyth Hasan. Abu Daawuwd (2082), Ahmad (3/360), Al-Haakim (2/165) na Al-Bayhaqiy (7/84)]
Kadhalika, imesimuliwa kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إِذَا خَطَبَ أَحَدُكُمُ امْرَأَةً فلا جُنَاحَ عَلَيْهِ أَنْ يَنْظُرَ إِلَيْهَا إِذَا كَانَ إِنَّمَا يَنْظُرُ إِلَيْهَا لِخِطْبَتِهَا وإِنْ كَانَتْ لا تَعْلَمُ"
“Akiposa mmoja wenu mwanamke, basi hakuna ubaya kama atamwangalia, lakini kuwe kumwangalia huko ni kwa ajili ya kumwoa tu na si vinginevyo, hata kama mwenyewe hajui”.
Bali hata baadhi ya Fuqahaa wamesema kwamba mwanamke kutojua kwamba anaangaliwa inakuwa ni bora zaidi, kwa kuwa akijua, anaweza kujitengeneza akaonekana kinyume na alivyo na mwanamume akahadaika na uzuri bandia.
Lakini wanachuoni wa Kimaalik wanaona kwamba ni lazima mwanamke ajulishwe au walii wake ili kuziba mwanya kwa mafasiki kuweza kuangalia wanawake kwa malengo yao mengine wakidai kwamba wao ni waposaji.
Ninasema: “Kauli ya Jumhuwr iko karibu zaidi na maneno ya Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Halafu, ikiwa mwanaume ataweza kumwangalia kabla ya kumposa, itakuwa vyema zaidi, kwa kuwa posa yake inaweza kukataliwa, na hapo akaumia na kujeruhika kisaikolojia”.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الخِطْبَةُ وأَحْكَامُهَا
Posa Na Hukumu Zake
Alhidaaya.com [3]
16: Je, Mwanaume Anaruhusiwa Kumwangalia Kwa Matamanio Au Kwa Hisia Ya Ladha?
Ili kumwangalia mwanamke kuruhusike, ‘Ulamaa wa Kihanbali wameshurutisha kuwepo usalama wa fitnah. Hivyo basi kumwangalia mwanamke kwa hisia ya ladha na matamanio ni haramu.
Ama Jumhuwr, wao hawajashurutisha hilo, bali wanasema kwamba mwanamume anaruhusika kumwangalia kwa lengo la kumwoa hata kama atahofia kumtamani au kuwepo fitnah kutokana na mambo mawili:
1- Kwamba Hadiyth zilizogusia uhalali wa kumwangalia mwanamke kwa ajili ya kumwoa, hazikuainisha kumwangalia kwa kumtamani au bila kumtamani, bali zimeuachia mlango wazi.
2- Maslaha yanayopatikana kwa hilo ni makubwa zaidi kuliko madhara.
Kumwangalia Mchumba Zaidi Ya Mara Moja:
Mposaji ana haki ya kumwangalia anayemposa kwa zaidi ya mara moja ili kutaamuli mazuri zaidi aliyonayo na kupata picha wazi zaidi ya alivyo, ili asije kujuta baada ya kumwoa. Anaweza kufanya hivyo hata bila ya idhini. Lengo mara nyingi halipatikani kwa mtizamo wa mara moja. Lakini pamoja na hivyo, anatakikana ajidhibiti vizuri kwa kiasi cha haja ya kumwezesha kupata uhakika tosha wa kumkubali. Ikiwa mara moja au zaidi itatosha kujikinaisha na kujiridhisha, basi zaidi ya hapo ni haramu, na mwanamke huyo atarudi kuwa ajnabiyya (mwanamke wa kando) kwake mpaka atakapofunga naye ndoa.
Ninasema: “Kwa muktadha huu, haitakikani mwanaume kukutana mara kwa mara na mchumba wake kama inavyofanyika siku hizi. Utamwona mvulana anamtembelea mchumba wake takriban kila siku, anakaa naye masaa mengi na kumwangalia juu chini, wakati ambapo mara za mwanzo alikwisha mkagua vyema na akaridhishwa naye. Haya ayafanyayo hayana maana nyingine zaidi ya kujipumbaza kwa uzuri wa mwanamke huyo jambo ambalo ni haramu, kwa kuwa msichana huyo bado ni ajnabiyya kwake (mwanamke wa kando)”.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الخِطْبَةُ وأَحْكَامُهَا
Posa Na Hukumu Zake
Alhidaaya.com [3]
17: Kama Mwanaume Hajapendezwa Na Mwanamke, Nini Afanye?
Kama mwanaume atamwangalia mwanamke na asimpendeze, basi analotakiwa ni kunyamaza. Haifai kutangazia chochote cha kumchafua mwanamke au familia yake. Yale ambayo hayakumpendeza yeye yanaweza yakamfurahisha mwingine. Ni vizuri pia asiseme kwamba hamtaki, hilo linaumiza, anyamaze tu.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الخِطْبَةُ وأَحْكَامُهَا
Posa Na Hukumu Zake
Alhidaaya.com [3]
18: Je, Inatosha Kuangalia Picha Ya Mchumba?
Mposaji anaruhusiwa kuangalia picha ya mchumba wake ni sawa ikiwa ni ya fotografu au video. Hizi zinaingia kwenye ujumuishi wa dalili zenye kuhimiza kumwangalia sehemu zitakazomshawishi kumwoa.
Hali hii inakuja pale mwanamke anapokuwa mbali na mwanaume mchumbiaji. Pamoja na hivyo, inabidi kuzindusha hapa kwamba utumiaji wa picha unaweza ukawa njia ya udanganyifu na ghushi. Picha inaweza kuhadaa ikamwonyesha mwenye picha kinyume na alivyo. Na kwa mujibu wa teknolojia ya sasa, mwanamke mbaya anaweza kufanywa mzuri mrembo. Vile vile, mtu anaweza kutumiwa picha ya mwanamke mwingine asiye yule aliyemkusudia. Isitoshe, picha hiyo inaweza kuwafikia watu wengi na hatimaye kuwa madhara kwake na kwa familia yake. [Rawdhwat At-Twaalibiyna (7/21) na Mughnil Muhtaaj (2/85)]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الخِطْبَةُ وأَحْكَامُهَا
Posa Na Hukumu Zake
Alhidaaya.com [3]
19: Je, Mwanamke Naye Anaruhusiwa Kumwangalia Mwanaume?:
Hukmu ya mwanamke kumwangalia aliyemposa ni sawa na hukmu ya mwanaume kumwangalia yeye, kwa kuwa yanayompendeza kutoka kwa mwanaume ni yale yale yanayompendeza mwanaume kutoka kwake. Hili ni muhimu zaidi kwa mwanamke, kwa sababu mwanaume ana uwezo wa kumwacha mwanamke kama hakumpendeza baada ya kumwoa kinyume na mwanamke.
Hapa kiufupi tunaweza kusema kwamba sharia haikumwelekeza mwanamke kumwangalia aliyemchumbia, kwa kuwa wanaume ni rahisi kuwaona katika jamii, hawafichiki kama wanavyofichikana wanawake. Mwanamke anaweza kwa urahisi kumwona mwanaume aliyemposa. Na mpaka wa kumwangalia ni zaidi ya uso na viganja isipokuwa kati ya kitovu na magoti, sehemu hiyo ndio uchi wa mwanaume.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الخِطْبَةُ وأَحْكَامُهَا
Posa Na Hukumu Zake
Alhidaaya.com [3]
20: Kukaa Faragha Na Mchumba:
Ni haramu mposaji kukaa faragha na mchumba wake, ni sawa kwa ajili ya kumwangalia au kwa jambo jingine. Kukaa faragha kati ya wawili hawa hakusalimiki na hatari ya kutumbukia kwenye haramu.
Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kukaa faragha kati ya mwanamke na mwanaume akisema:
"لَا يَخْلُوَنَّ رَجُلٌ بِامْرَأَةٍ إِلَّا كَانَ ثَالِثُهُمَا الشَّيْطَان"
“Haipati kutokea mwanaume akakaa faragha na mwanamke isipokuwa shaytwaan anakuwa wa tatu wao”. [Hadiyth Swahiyh. Imechakatwa na Ahmad (1/18) na At-Tirmidhiy]
Na amesema tena:
"لَا يَخْلُوَنَّ رَجُلٌ بِاِمْرَأَةٍ إِلَّا مَعَ ذِي مَحْرَمٍ"
“Asithubutu mwanaume kukaa faragha na mwanamke isipokuwa aweko pamoja nao mahram yake”. [Hadiyth Swahiyh. Imechakatwa na Al-Bukhaariy (3006) na Muslim (1341)]
Waliotoka nje ya mstari wa Dini ya Allaah na Sharia Yake, wanadai kwamba mposaji kuongozana na mchumba wake, kukaa naye pamoja faraghani, na kusafiri naye, ni jambo lisilo na budi, eti kwa kuwa kila mmoja atapata kumjua na kumsoma mwenzake vizuri.
Na anayeutizama mwenendo wa nchi za magharibi katika suala hili, atakuta kwamba mwenendo huu haujaleta matokeo yoyote chanya ya kutambuana au kuvaana vilivyo kati ya wachumba wawili, bali zaidi ni mvulana kumhama mchumba wake baada ya kumvunja bikira. Kadhalika, anaweza kumwacha akiwa mja mzito, halafu baadaye msichana anakuja kutaabika peke yake katika kubeba jukumu la ulezi. Msichana huyu anaweza pia kuitoa mimba bila kujali chochote.
Na hata wale ambao wanakaa muda mrefu kwenye posa na kisha kuoana, kila mmoja anakuja kugundua baadaye kwamba uchumba huo mrefu haukuweza kumfanya kila mmoja kumgundua mwenzake katika uhalisia wake. [Ahkaamuz Zawaaj cha Dk. ‘Umar Al-Ashqar (uk. 58)]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الخِطْبَةُ وأَحْكَامُهَا
Posa Na Hukumu Zake
Alhidaaya.com [3]
21: Mwanaume Haruhusiwi Kumpa Mkono Mchumba Wake Wala Kumgusa Sehemu Yoyote Ya Mwili Wake:
Hii ni hata bila matamanio, kwa kuwa msichana anakuwa bado ni ajnabiyya kwake. Dalili za uharamu huu ni hizi zifuatazo:
1- Ma’aqal bin Yasaar: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"لَأنْ يُطعَنَ في رأسِ رجلٍ بِمِخْيَطٍ من حديدٍ خيرٌ من أن يمَسَّ امرأةً لا تَحِلُّ له"
“Kudungwa mtu kichwani na sindano la chuma, ni nafuu zaidi kwake kuliko kumgusa mwanamke asiye halali kwake”. [Hadiyth Hasan. Imechakatwa na At-Twabaraaniy katika Al-Kabiyr (30/211). Angalia As-Swahiyhah (226)]
Na kwa ajili hii, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakuwa anawapa mkono wanawake wala kuchukua toka kwao ahadi ya utiifu kwake isipokuwa kwa maneno tu.
2- ‘Aaishah (Radhwiya Allaah ‘anhaa):
"كَانَ يَقُولُ للمَرْأَةِ المبَايِعَةِ: "قَدْ بَايَعْتُكِ" كَلَامًا. وقَالَتْ: وَاللَّهِ مَا مَسَّتْ يَدُهُ يَدَ امْرَأَةٍ قَطُّ فِي الْمُبَايَعَةِ، وَمَا بَايَعَهُنَّ إِلاَّ بِقَوْلِهِ: "قَدْ بَايَعْتُكِ"
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anamwambia kwa maneno mwanamke anayechukua toka kwake ahadi ya utiifu: “Nimechukua ahadi yako”. Na akasema: Wal Laah! Haukugusa kamwe mkono wake mkono wa mwanamke wakati wa kuchukua ahadi ya utiifu kwao isipokuwa kwa kumwambia mwanamke: Nimechukua ahadi ya utiifu kwako juu ya hilo”. [Hadiyth Swahiyh. Imechakatwa na Al-Bukhaariy (2713)]
Na katika riwaayah aliwaambia:
"إِنِّي لاَ أُصَافِحُ النِّسَاءَ"
“Mimi kwa hakika sipeani mikono na wanawake”. [Swahiyh. Imechakatwa na At-Tirmidhiy (1597), An-Nasaaiy (4181), Ibn Maajah (2874) na Ahmad (6/357)]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الخِطْبَةُ وأَحْكَامُهَا
Posa Na Hukumu Zake
Alhidaaya.com [3]
22: Kuzungumza Na Mchumba:
Inajuzu mposaji kuzungumza na mchumba wake kama atahitajia lakini kwa sharti ya uwepo wa mahram yake. Na hii ni ima kutaka kuijua sauti yake, au kuchukua rai yake kuhusiana na maisha yao yajayo ya ndoa. Mwanamke naye ana haki hiyo pia lakini kwa sharti ya kuwajibika na vidhibiti vya kisharia. Maneno yake yawe kwa mujibu wa haja, asilegeze sauti wala mwenyewe asijilainishe. Allaah Amesema:
"فَلَا تَخْضَعْنَ بِالْقَوْلِ فَيَطْمَعَ الَّذِي فِي قَلْبِهِ مَرَضٌ وَقُلْنَ قَوْلًا مَّعْرُوفًا"
“Basi msilegeze kauli asije akaingiwa tamaa ambaye moyoni mwake mna maradhi, na semeni kauli inayokubalika. [Al-Ahzaab: 32]
Na kati ya yanayoonyesha kujuzu kuzungumza kwa vidhibiti vya kisharia ni Kauli Yake Ta’aalaa:
"وَإِذَا سَأَلْتُمُوهُنَّ مَتَاعًا فَاسْأَلُوهُنَّ مِن وَرَاءِ حِجَابٍ"
“Na mnapowauliza wake zake haja, waulizeni nyuma ya pazia”. [Al-Ahzaab: 53]
Kadhalika, Nabiy Muwsaa (‘alayhis salaam) aliwasemesha wanawake wawili wa Madyan kama inavyoeleza Kauli Yake Ta’aalaa:
"وَلَمَّا وَرَدَ مَاءَ مَدْيَنَ وَجَدَ عَلَيْهِ أُمَّةً مِّنَ النَّاسِ يَسْقُونَ وَوَجَدَ مِن دُونِهِمُ امْرَأَتَيْنِ تَذُودَانِ ۖ قَالَ مَا خَطْبُكُمَا ۖ قَالَتَا لَا نَسْقِي حَتَّىٰ يُصْدِرَ الرِّعَاءُ ۖ وَأَبُونَا شَيْخٌ كَبِيرٌ"
“Alipofikia maji ya Madyan, alikuta kundi la watu linanywesha maji (wanyama wao), na akakuta kando yake wanawake wawili wanawazuia (wanyama wao). Akasema: Mna nini? Wakasema: Hatunyweshi mpaka waondoke wachungaji, na baba yetu ni mtu mzima sana”. [Al-Qaswas: 23]
Kadhalika, kuna Hadiyth nyingi zinazogusia suala hili. Kati yake ni ya Anas kuhusiana na kisa cha kufariki Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambayo sehemu yake inasema:
"فَلَمَّا دُفِنَ، قَالَتْ فَاطِمَةُ عَلَيْهَا السَّلاَمُ: يَا أَنَسُ، أَطَابَتْ أَنْفُسُكُمْ أَنْ تَحْثُوا عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم التُّرَابَ"
“Alipozikwa, Faatwimah (‘alayhas Salaam) alimwambia Anas: Ee Anas! Hivi kweli mmejisikia vizuri kummiminia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mchanga!”. [Hadiyth Swahiyh. Imechakatwa na Al-Bukhaariy (4462)]
Baadhi ya nyakati anaweza kuhitaji kuzungumza naye kwa njia ya simu. Hili halikatazwi ila tu la muhimu ni kuchunga vidhibiti vya kisharia, watu wa mchumba wajue kwamba atazungumza naye, na yawe kwa mujibu wa haja. Ama ikiwa simu hiyo itajenga kati yao mazingira yanayofanana na yale ya ufaragha ambayo kisharia yamekatazwa, na yakaweza kuwakokota taratibu kuingia kwenye haramu, basi kuachana nayo ni wajibu. Allaah Ndiye Ajuaye zaidi.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الخِطْبَةُ وأَحْكَامُهَا
Posa Na Hukumu Zake
Alhidaaya.com [3]
23: Pete Ya Uchumba:
Watu siku hizi wameingia bila kujijua kwenye tabia ya kijana mposaji kumvalisha pete ya posa mchumba wake. Ataukamata mkono wake -naye bado ni ajnabiy kwake- na kumvisha pete, na msichana naye atafanya hivyo hivyo. Pete hiyo anayovishwa mwanaume inaweza pia kuwa ni ya dhahabu!! Na baya zaidi, hilo linafanyika kwenye hafla yenye mvumo mkubwa huku wanaume na wanawake wakichanganyika pamoja. Haya yote ni katika munkari mbali na kwamba katika Uislamu hakuna chochote kinachogusia posa kufanyika kwa picha hii. Ni mambo ya kuiga yaliyoanzishwa na Mafarao au Manaswara, na kuyafanya ni sawa na kuiga kibubusa na kujifananisha na makafiri. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"مَنْ تَشَبَّهَ بِقَوْمٍ فَهُوَ مِنْهُمْ"
“Mwenye kujifananisha na watu basi yeye ni katika wao”. [Hadiyth Hasan. Imechakatwa na Abu Daawuwd (4031), Ahmad (2/50) na wengineo]
Yote ni mamoja katika uharamu ni sawa pete ikiwa ya dhahabu au silva, lakini uharamu unakuwa ni mkubwa zaidi ikiwa ni ya dhahabu. Allaah Ndiye Ajuaye zaidi.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الخِطْبَةُ وأَحْكَامُهَا
Posa Na Hukumu Zake
Alhidaaya.com [3]
24: Kuvunja Uchumba:
Posa haimaanishi kwamba ndoa ndiyo tayari, bali ni ahadi ya kuja kufungwa ndoa, na ahadi hii sio wajibishi kwa mujibu wa kauli ya Jumhuwr ya ‘Ulamaa. Walii wa binti halazimishwi kutekeleza ahadi hiyo baada ya kuikubali posa, na anaweza kuitengua kama ataona maslaha ya binti yake katika hilo, na hata binti pia ikiwa atamchukia mposaji. Sababu ni kuwa ndoa ni fungamano la maisha, na kama yako madhara ndani yake, basi yatakuwa ni ya kudumu.
Ninasema: “Allaah Ta’aalaa Amesema:
"كَبُرَ مَقْتًا عِندَ اللَّـهِ أَن تَقُولُوا مَا لَا تَفْعَلُونَ"
“Ni chukizo kubwa mno mbele ya Allaah kwamba mnasema yale msiyoyafanya”. [As-Swaff: 03]
Na katika Hadiyth ya Abu Hurayra (Radhwiya Allaah ‘anhu), Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"آيَةُ اَلْمُنَافِقِ ثَلَاثٌ: إِذَا حَدَّثَ كَذَبَ، وَإِذَا وَعَدَ أَخْلَفَ، وَإِذَا ائْتُمِنَ خَانَ"
“Alama za mnafiki ni tatu: Akizungumza husema uongo, akiahidi hatekelezi, na akiaminiwa husaliti”. [Hadiyth Swahiyh. Imechakatwa na Al-Bukhaariy na Muslim]
Aayaat na Hadiyth kama hizi, ni dalili za nguvu zenye kuashiria wajibu wa kutekeleza ahadi na kutoivunja bila ya udhuru unaokubalika.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الخِطْبَةُ وأَحْكَامُهَا
Posa Na Hukumu Zake
Alhidaaya.com [3]
25: Posa Ikivunjwa, Nini Hatima Ya Zawadi Zilizotolewa?:
Ikiwa mposaji atampa zawadi mchumba wake au akamgharamikia -wakati wa kipindi cha posa- kisha ndoa isifungwe, basi zawadi na gharama hizo hazikosi kuwa: ima sehemu ya mahari, au zawadi ya kuimarisha mapenzi na utangamano kati ya wachumba wawili.
(a) Alichokitoa kama sehemu ya mahari, hiki kina hali mbili:
Hali ya kwanza:
Kitu chenyewe kiwepo kwa dhati yake. Ni kama seti ya mkufu, pete, na bangili za dhahabu au vito ambayo mposaji anamnunulia mchumba wake baada ya posa kukubaliwa, na seti hii inajulikana kama “shabkah” (kwenye baadhi ya nchi za Kiarabu). Anaweza kumnunulia kabla ya ndoa kufungwa au baada yake kwa mujibu wa ada na desturi za eneo husika. Hii na mfano wake, ni haki ya mposaji kudai kama posa itavunjwa kwa itifaki ya ‘Ulamaa, ni sawa awe yeye kaivunja au msichana, au kwa sababu yoyote iliyo nje ya uwezo.
Hali ya pili:
Awe amenunua kifaa au chombo ili kitumike baada ya kuoana. Kuhusu hukmu ya kurejesha thamani ya mahari au chombo alichonunua, Fuqahaa wana kauli mbili:
Kauli ya kwanza:
Ni lazima arejeshewe mahari aliyolipa, kwa sababu mahari ni fidia kwa mkabala wa kustarehe na mke, na starehe haijapatikana. Hivyo ni lazima arejeshewe kitu chenyewe kama kipo, au thamani yake kama kimeharibika au kimechakaa. Haya ni madhehebu ya Jumhuwr.
Kauli ya pili:
Mwanamke hatotakwa arejeshe chombo alichokinunua ikiwa mposaji alimruhusu kununua, au alijua kimenunuliwa, au ikawa hiyo ndio ada na desturi. Na kama si hivyo, atatakiwa arejeshe mahari ambayo mposaji amelipa.
Ninaloliona kuwa lina nguvu ni kwamba ikiwa mwanaume ndiye aliyevunja posa na akawa amejua kwamba chombo kimenunuliwa kutokana na pesa ya mahari, au ikawa hiyo ndiyo ada, hapo atachukua chombo hicho, lakini haruhusiwi kumlazimisha mwanamke huyo akiuze ili amkabidhi pesa ya mauzo. Ama ikiwa mwanamke ndiye aliyevunja posa, basi atalazimika kurejesha pesa ya mahari, na kama kanunulia chombo, itabidi akiuze na arejeshe pesa.
(b) Alichokitoa kama zawadi, hiki ‘Ulamaa wana kauli nne kuhusiana na hukmu ya kurejeshewa mposaji:
Ya kwanza:
Inajuzu kukidai ikiwa bado kiko katika umiliki wa mwanamke, kiwe ni kile kile na si chingine, na asiwe amefanya lolote la kukitoa nje ya umiliki wake. Na kama kitakuwa kimeharibika au kimebadilika hali yake, hapo hawezi kukidai.
Ya pili:
Hakirejeshwi chochote hata kama sababu ya kuvunjika posa ni mwanamke isipokuwa kama waliwekeana sharti hilo. Hoja ya msingi ya kauli hii ni kwamba zawadi inabeba maana ya tunu, na mtoaji tunu haruhusiwi kisharia kuitaka tena tunu yake kutokana na neno lake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
" لَيْسَ لَنَا مَثَلُ اَلسَّوْءِ، اَلَّذِي يَعُودُ فِي هِبَتِهِ كَالْكَلْبِ يَرْجِعُ فِي قَيْئِهِ"
“Haitakikani kwetu (sisi Waislamu) kuwa mfano wa sifa mbovu. Mwenye kurejelea zawadi aliyotoa ni kama mbwa anayerejea kula matapishi yake”. [Hadiyth Swahiyh. Imechakatwa na Al-Bukhaariy (2622) na Muslim]
Wakati ‘Umar bin Al-Khattwaab (Radhwiya Allaah ‘anhu) alipojitolea farasi wake na kumpa mtu mmoja ili amtumie katika Jihaad na mtu yule akashindwa kumtunza ipasavyo, ‘Umar alitaka kumnunua. Lakini Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia:
"لاَ تَشْتَرِهِ، وَإِنْ أَعْطَاكَهُ بِدِرْهَمٍ وَاحِدٍ، فَإِنَّ الْعَائِدَ فِي صَدَقَتِهِ كَالْكَلْبِ يَعُودُ فِي قَيْئِهِ"
“Usimnunue, hata akikupa kwa dirham moja, kwani mwenye kuirejea swadaqah yake ni mfano wa mbwa anayelamba matapishi yake mwenyewe”. [Hadiyth Swahiyh. Imechakatwa na Al-Bukhaariy (2623)]
Ya tatu:
Zawadi itarejeshwa vyovyote aina yake iwavyo. Ikiwa bado iko kama ilivyo, itarejeshwa hivyo hivyo, na kama imechakaa, basi itarejeshwa thamani yake. Hii ni kauli ya Jumhuwr ambayo maana yake ni kwamba zawadi hizi si kama tunu, kwa kuwa miongoni mwa masharti ya tunu kwao ni kwamba isiwe na mkabala, na mtoaji (mposaji) alitoa tunu hiyo wakati wa posa kwa mkabala wa kupatikana ndoa, na ndoa haikufanyika.
Ya nne:
Ikiwa aliyevunja posa ni mwanaume, basi hana haki ya kuidai, na ikiwa ni mwanamke, basi mwanaume ana haki ya kuidai, kwa kuwa lengo la kutoa zawadi hiyo halikufikiwa. Hii ni kauli ya Ar-Raafi’iy na Ibn Arshad, na ni chaguo la Sheikh wa Uislamu Ibn Taymiyah, nayo ndiyo kauli iliyo na uadilifu zaidi. Kwa sababu, kulazimisha kurejesha zawadi kama mposaji mwenyewe ameivunja posa kunasababisha machungu mawili kwa mwanamke; uchungu wa posa kuvunjika na uchungu wa kurejesha zawadi alizopewa. Kadhalika, kuzuia zawadi zisirejeshwe kama aliyevunja posa ni mwanamke, kunaleta machungu mawili; uchungu wa kuvunjika posa na uchungu wa gharama za zawadi hizo.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الخِطْبَةُ وأَحْكَامُهَا
Posa Na Hukumu Zake
Alhidaaya.com [3]
26: Kumfidia Aliyedhurika Kutokana Na Kuvunjika Posa:
Baadhi ya wasomi wa kileo wanaona kwamba kuvunja posa kunawajibisha fidia ya fedha kama ilivyo kwa baadhi ya makundi ya Kinaswara wakati ambapo Fuqahaa hapo nyuma pamoja na kutofautiana kwao kimaoni, hawakupanga malipo yoyote ya fidia kwa upande uliosababisha posa kuvunjwa. Na hili ndilo lililo sahihi kwa haya yafuatayo:
1- Fidia inazidisha tatizo juu ya tatizo, na wala hailitatui. Lakini pia, madhara yanayotokana na kuvunja posa yanazalikana kutokana na watu kuipa posa uzito mkubwa zaidi ya inavyostahili. Posa ni ahadi tu, na haijuzu watu waijengee hali ambayo italeta madhara kwao. Na gharama ambazo waposaji wanazibeba, manunuzi na mfano wa hayo kwa wachumba, ni kuharakia jambo ambalo lina wasaa na muda wa kutosha.
2- Fidia inafungua mlango kwa pande zote mbili wa kulipiziana na kutiana hasara kwa nguvu na hila zote kutokana na machungu na maumivu ya rohoni. Na idadi ya kesi kama hizi kwenye jamii zetu ni nyingi mno kuzidi uwezo wa mahakama.
3- Fidia inakwenda kinyume na uhalisia wa posa ambayo ni ahadi na makubaliano ya awali ya matayarisho ya ndoa.
4- Fidia inakhalifu Ijmaa ya Umma na si uadilifu.
5- Inaweza kulazimisha posa kurejeshwa upya na ndoa kufungwa huku chuki ikiwa imetamalaki, na hili ni jambo la hatari kabisa.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الخِطْبَةُ وأَحْكَامُهَا
Posa Na Hukumu Zake
Alhidaaya.com [3]
27: Kufanya Vipimo Vya Kitiba Kabla Ya Ndoa:
Jambo hili halikuweko zamani. Lakini hivi leo, ukweli na uaminifu umekuwa ni nadra sana. Watu wanaficha kasoro zao za kisaikolojia na za kimwili kabla ya kuoana. Na kwa msingi huu, kutokana na mapinduzi makubwa katika nyanja ya tiba, wachumba wawili wanaweza kufanyiwa vipimo vya kitiba ili kujua kama wana magonjwa ya kurithi, au ambukizi, au tatizo la tendo la ndoa au matendo ya kila siku ambayo yataathiri kwa siku za usoni afya ya wanandoa wawili au watoto wao.
Rai mashuhuri zaidi ya kitiba kuhusiana na vipimo kwa wanandoa kabla ya kuoana inasema kwamba suala hili lina hali chanya na hasi inayoelezewa kwa muhtasari katika haya yafuatayo:
(a) Yaliyo chanya:
1- Ni katika njia bora zaidi za kinga za kuzuia magonjwa hatari ya urithi na ambukizi.
2- Vinaunda kinga kwa jamii, na kinga hii inazuia kuenea kwa magonjwa lakini pia inapunguza idadi ya walemavu. Hili likifanikiwa linaistawisha jamii kiuchumi na kiutu.
3- Vinatoa dhamana ya kuzaliwa watoto wenye afya kamili na wasio na kasoro zozote za kiakili au kimwili mbali na kutohama magonjwa ya urithi anayoweza kuwa nayo mmoja wa walioposana au wote wawili.
4- Vinafichua uwezekano wa kuzaa au kutokuzaa. Kuwa tasa kwa mmoja wa wanandoa, kunaweza kuja kuwa miongoni mwa sababu za mivutano na mkorogano kati yao.
5- Vinahakikisha kutokuwepo kasoro za kifisiolojia au za viungo. Tatizo hili kama liko, litakuwa ni kikwazo kwa kila mwanandoa la kufanya tendo salama la ndoa.
6- Vinahakikisha kutokuweko magonjwa yoyote sugu ambayo ni tishio la utulivu wa maisha ya ndoa.
7- Ni dhamana ya kutodhurika mmoja wao kutoka kwa mwenzake katika kufanya tendo la ndoa, au wakati wa ujauzito au baada ya kuzaa.
(b) Yaliyo hasi:
1- Vinaweza kuleta hali ya kuvunjikwa moyo na kupoteza matumaini. Lakini ikiwa pia vipimo vitaonyesha uwezekano kwa mwanamke kupata utasa au saratani ya titi, halafu wengine wakajua hilo, hili bila shaka litamsababishia madhara ya kisaikolojia na kutoka kwa jamii yake. Kwa hali hii, atahisi mustakbali wake umekwisha ingawa mambo ya kitiba hupatia na kukosea.
2- Vinayafanya maisha ya baadhi ya watu kutawaliwa na wasiwasi, huzuni na kukata tamaa anapoelezwa kwamba atakuja kupatwa na maradhi mabaya yasiyoweza kupona.
3- Matokeo ya vipimo hubakia katika hali isiyo ya uhakika kamili katika magonjwa mengi, na si dalili thibitishi ya kugundua na kutabiria magonjwa ya siku za mbeleni.
4- Vinaweza kuwanyima baadhi nafasi ya ndoa kutokana na matokeo ambayo hayana uhakika ndani yake.
5- Ni nadra sana kumkuta mtu bila maradhi yoyote na hususan ya kuthibitishwa uwepo wa magonjwa ya urithi zaidi ya 3000 yaliyo orodheshwa na kuthibitishwa.
6- Kuharakia kutoa ushauri tiba baada ya vipimo kunasababisha matatizo zaidi kuliko kunavyoyatatua.
7- Waliofanya vipimo wanaweza kutendewa vibaya ikiwa siri ya matokeo ya vipimo vyao itafichuliwa na kutumiwa kwa njia ya kuwadhuru.
Huu ndio muhtasari wa rai ya tiba kuhusiana na vipimo kabla ya ndoa. Sasa vipi kwa upande wa msimamo wa sharia ya Kiislamu? Je, inajuzu kuwalazimisha wanandoa watarajiwa kufanya?
Hakuna shaka kwamba hapo zamani hakukuweko haja ya kufanya haya kwa sababu Waislamu enzi hizo walikuwa na sifa kubwa ya uaminifu katika kueleza kasoro za watu, lakini pia hakukuweko maendeleo ya kisayansi ya kuwawezesha kufanya vipimo kama hivi. Ama ‘Ulamaa wa enzi yetu ya leo, wao wana mielekeo miwili:
Mwelekeo wa kwanza:
Vipimo hivi haviruhusiwi na havina haja. Kati ya wenye msimamo huu, ni Al-‘Allaamah bin Baaz (Rahimahul Laah). Sababu ni kuwa kufanya hivyo kunakinzana na kumfanyia Allaah dhana njema, na pia matokeo ya vipimo yanaweza kuwa si sahihi.
Mwelekeo wa pili:
Vinajuzu na wala havipingani na sharia ya Kiislamu. Hii ni kauli ya ‘Ulamaa wengi wanaosema kwamba hilo halipingani na sharia wala halipingani na kuwa na Imani na Allaah, kwa kuwa mtu anatumia nyenzo alizonazo. ‘Umar (Radhwiya Allaah ‘anhu) alisema wakati ugonjwa wa tauni ulipoibuka huko Sham:
"أَفِرُّ مِن قَدَرِ اللَّهِ إلى قَدَرِ اللَّه"
“Ninakimbia toka kwenye Qadari ya Allaah kwenda kwenye Qadari ya Allaah”. [Hadiyth Swahiyh. Imechakatwa na Al-Bukhaariy]
Ninasema: “Huenda mwelekeo huu pamoja na hadhari na kuweka maneno akiba, ndio ulio karibu zaidi. Na unaweza kutolewa dalili ya kujuzu kwake kwa haya yafuatayo:
1- Kukilinda kizazi ni katika mihimili mikuu mitano ambayo Aayaat na Hadiyth nyingi zimeipa umuhimu na kutoa wito wa kuichunga na kuisimamia vyema.
Nabiy Zakariyya (‘alayhis salaam) alimwomba Allaah akisema:
"قَالَ رَبِّ هَبْ لِي مِن لَّدُنكَ ذُرِّيَّةً طَيِّبَةً"
“Rabb wangu! Nitunukie kutoka Kwako kizazi chema”. [Aal ‘Imraan: 38]
Na Waumini pia walimwomba Rabbi wao wakisema:
"رَبَّنَا هَبْ لَنَا مِنْ أَزْوَاجِنَا وَذُرِّيَّاتِنَا قُرَّةَ أَعْيُنٍ"
“Rabb wetu! Tutunukie kutoka wake zetu na dhuria wetu viburudisho vya macho yetu”. [Al-Furqaan: 74]
2- Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amemhimiza Muislamu achague mke toka familia ambayo mabanati zake wana sifa ya uzazi. Akasema:
"تَزَوَّجُوا الْوَدُودَ الْوَلُودَ فَإِنِّي مُكَاثِرٌ بِكُمُ الْأُمَم"
“Oeni mwanamke mwenye penzi, mwenye uzazi mwingi, kwani hakika mimi nitajifaharisha kwa wingi wenu kwa umma nyinginezo”. [Hadiyth Swahiyh]
Hadiyth hii inaonyesha umuhimu wa kuchagua kwa kuzingatia afya ya kizazi na uzazi wenyewe.
3- ‘Umar (Radhwiya Allaah ‘anhu) amesema:
"أَيُّمَا رَجُلٍ تَزَوَّجَ اِمْرَأَةً فَدَخَلَ بِهَا، فَوَجَدَهَا بَرْصَاءَ، أَوْ مَجْنُونَةً، أَوْ مَجْذُومَةً، فَلَهَا اَلصَّدَاقُ بِمَسِيسِهِ إِيَّاهَا، وَهُوَ لَهُ عَلَى مَنْ غَرَّهُ مِنْهَا"
“Ikiwa mwanaume yeyote ameoa mwanamke kisha akamwingilia, halafu akamkuta ana mbalanga, au wazimu, au ukoma, basi mwanamke ana haki ya mahari kwa kuwa amemuingilia. Ikiwa alihadaiwa na mtu ili amwoe (mwanamke huyo), basi mtu huyo atamrejeshea mahari hiyo”.
4- Hadiyth zinazomhimiza mwanaume kumkagua vyema mke mtarajiwa ili kujua kasoro zake. Ni kama Hadiyth ya Abu Hurayrah isemayo kwamba mtu mmoja alimchumbia mwanamke na Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia:
"انْظُرْ إِلَيْهَا فَإِنَّ فِي أَعْيُنِ الْأَنْصَارِ شَيْئًا"
“Nenda ukamwangalie, kwani hakika kwenye macho ya Maanswaar kuna ila fulani”. [Hadiyth Swahiyh. Imechakatwa na Muslim]
5- Dalili jumuishi zinazohimizia kuwaepuka wenye magonjwa ambukizi kama kauli yake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"لا تُورِدُوا المُمْرِضَ على المُصِحِّ"
“Msiwaweke pamoja mgonjwa na mzima”.
Na Hadiyth yake:
" وَفِرَّ مِنَ الْمَجْذُومِ كَمَا تَفِرُّ مِنَ الأَسَدِ"
“Na mkimbie mwenye ukoma kama unavyomkimbia simba”. [Hadiyth Swahiyh. Imechakatwa na Al-Bukhaariy (5380), Ahmad (2/443) na Al-Bayhaqiy (7/217)]
6- Dalili kiujumla zinazokataza kujiingiza kwenye madhara.
Na kwa haya tuliyoyataja, tunaweza kusema kwamba kufanya vipimo vya tiba kabla ya ndoa hakupingani na sharia bali kunaendana na makusudio yake. Na kwa muktadha huu, ikiwa walii wa msichana ataona kuna ulazima na hususan wakati wa kuenea magonjwa, basi itajuzu. Na vipimo hivi havina taathira yoyote katika kuswihi ndoa.
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/284
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11862&title=10B-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20%D9%83%D8%AA%D8%A7%D8%A8%20%D8%A7%D9%84%D8%B2%D9%88%D8%A7%D8%AC%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20%D8%A7%D9%84%D8%AE%D9%90%D8%B7%D9%92%D8%A8%D9%8E%D8%A9%D9%8F%20%D9%88%D8%A3%D9%8E%D8%AD%D9%92%D9%83%D9%8E%D8%A7%D9%85%D9%8F%D9%87%D9%8E%D8%A7%20Posa%20Na%20Hukumu%20Zake
[3] http://www.alhidaaya.com/
[4] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11863&title=01-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Posa%20Na%20Hukumu%20Zake%3ATaarifu%20Na%20Hukmu%20Yake
[5] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11864&title=02-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Posa%20Na%20Hukumu%20Zake%3A%20Ni%20Nani%20Anayekabidhiwa%20Posa%3F%20%20
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11865&title=03-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Posa%20Na%20Hukumu%20Zake%3AInajuzu%20Walii%20Kumtangazia%20Bintiye%20Kwa%20Watu%20Anaowaona%20Kuwa%20Wana%20Vigezo%20Vya%20Kumwoa
[7] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11866&title=04-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Posa%20Na%20Hukumu%20Zake%3AMwanamke%20Anaruhusiwa%20Kisharia%20Kujinadia%20Mwenyewe%20Kwa%20Mtu%20Mwema%20Ili%20Amwoe
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11867&title=05-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Posa%20Na%20Hukumu%20Zake%3AWanawake%20Wasiofaa%20Kuchumbiwa
[9] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11868&title=06-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Posa%20Na%20Hukumu%20Zake%3AKumchumbia%20Mwanamke%20Ambaye%20Amekwishachumbiwa%20Na%20Muislamu
[10] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11869&title=07-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Posa%20Na%20Hukumu%20Zake%3ANi%20Upi%20Mpaka%20Wa%20Posa%20Ambayo%20Ni%20Haramu%20Kuiposea%3F
[11] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11870&title=08-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Posa%20Na%20Hukumu%20Zake%3AIkiwa%20Mtu%20Ataposa%20Juu%20Ya%20Posa%20Ya%20Mwingine%20Kisha%20Akamwoa%20Mwanamke%2C%20Je%2C%20Itaswihi%20Ndoa%3F
[12] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11871&title=09-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Posa%20Na%20Hukumu%20Zake%3APosa%20Juu%20Ya%20Posa%20Ya%20Kafiri
[13] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11872&title=10-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Posa%20Na%20Hukumu%20Zake%3A%20Kuulizwa%20Kuhusu%20Mposa%20Na%20Mposwa%20Na%20Kutaja%20Kasoro%20Zao
[14] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11873&title=11-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Posa%20Na%20Hukumu%20Zake%3A%20Istikhaarah%20Kwa%20Ajili%20Ya%20Posa
[15] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11874&title=12-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Posa%20Na%20Hukumu%20Zake%3AInajuzu%20Mtu%20Kuwa%20Mshenga
[16] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11875&title=13-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Posa%20Na%20Hukumu%20Zake%3AJe%2C%20Mwanaume%20Anaruhusiwa%20Kumwangalia%20Kikaguzi%20Mwanamke%20Aliyekusudia%20Kumposa%3F
[17] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11876&title=14-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Posa%20Na%20Hukumu%20Zake%3AMipaka%20Ya%20Kumwangalia
[18] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11877&title=15-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Posa%20Na%20Hukumu%20Zake%3AJe%2C%20Ni%20Sharti%20Mwanamke%20Anayeposwa%20Atakwe%20Idhini%20Ya%20Kuangaliwa%20Na%20Ajue%20Hilo%3F
[19] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11878&title=16-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Posa%20Na%20Hukumu%20Zake%3A%20Je%2C%20Mwanaume%20Anaruhusiwa%20Kumwangalia%20Kwa%20Matamanio%20Au%20Kwa%20Hisia%20Ya%20Ladha%3F%20%20
[20] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11879&title=17-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Posa%20Na%20Hukumu%20Zake%3AKama%20Mwanaume%20Hajapendezwa%20Na%20Mwanamke%2C%20Nini%20Afanye%3F
[21] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11880&title=18-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Posa%20Na%20Hukumu%20Zake%3AJe%2C%20Inatosha%20Kuangalia%20Picha%20Ya%20Mchumba%3F
[22] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11881&title=19-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Posa%20Na%20Hukumu%20Zake%3AJe%2C%20Mwanamke%20Naye%20Anaruhusiwa%20Kumwangalia%20Mwanaume
[23] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11882&title=20-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Posa%20Na%20Hukumu%20Zake%3A%20Kukaa%20Faragha%20Na%20Mchumba
[24] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11883&title=21-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Posa%20Na%20Hukumu%20Zake%3AMwanaume%20Haruhusiwi%20Kumpa%20Mkono%20Mchumba%20Wake%20Wala%20Kumgusa%20Sehemu%20Yoyote%20Ya%20Mwili%20Wake
[25] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11884&title=22-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Posa%20Na%20Hukumu%20Zake%3AKuzungumza%20Na%20Mchumba
[26] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11885&title=23-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Posa%20Na%20Hukumu%20Zake%3A%20Pete%20Ya%20Uchumba
[27] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11886&title=24-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Posa%20Na%20Hukumu%20Zake%3AKuvunja%20Uchumba
[28] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11887&title=25-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Posa%20Na%20Hukumu%20Zake%3APosa%20Ikivunjwa%2C%20Nini%20Hatima%20Ya%20Zawadi%20Zilizotolewa%3F
[29] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11888&title=26-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Posa%20Na%20Hukumu%20Zake%3A%20Kumfidia%20Aliyedhurika%20Kutokana%20Na%20Kuvunjika%20Posa
[30] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11889&title=27-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Posa%20Na%20Hukumu%20Zake%3AKufanya%20Vipimo%20Vya%20Kitiba%20Kabla%20Ya%20Ndoa