Alhidaaya.com
Published on Alhidaaya.com (https://www.alhidaaya.com/sw)

Ukurasa Wa Kwanza > 10E-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: كتاب الزواج Kitabu Cha Ndoa: الصَّدَاقُ: Mahari > 11-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Mahari: Yanayopelekea Kudondoka Mahari Yote

11-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Mahari: Yanayopelekea Kudondoka Mahari Yote

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

 

الصَّدَاقُ

 

Mahari

 

 

Alhidaaya.com [1]

 

 

 

11:  Yanayopelekea Kudondoka Mahari Yote:

 

 

1-  Kutokea utengano -kwa matakwa ya mke- kabla ya kumuingilia. 

 

Ni kama mke kusilimu -na mumewe kubaki kafiri-, au mume kuvunja ndoa kutokana na kasoro aliyonayo mke, au mke kuritadi, au kugundulika kwamba mke aliwahi kumnyonyesha mume aliyemwoa, au mke kuvunja ndoa kutokana na kasoro aliyonayo mume, au mume kuwa masikini kupindukia na mfano wa hayo.  Hapo mahari iliyobainishwa na mahari ya mfano itadondoka.  Ni madhehebu ya Mashaafi’iy, Mahanbali, Mahanafiy na Wamaalik.  Lakini wao hawajatofautisha kati ya kuwa mtengano unatokana na mume au mke.

 

2-  Khulu’u (Mwanamke kudai talaka kwa kumlipa mume kitu au kumrejeshea mahari yake):  Ikiwa mume atakubali kuachana na mkewe kwa kuachia mahari yake, hapo mahari yote itadondoka.  Na kama mke bado hajapokea, basi mume hatotoa, na ikiwa amemkabidhi, basi mke atarejesha.

 

3-  Kusamehe mahari yote kabla ya kuingiliwa au baada ya kuingiliwa.

 

Mwanamke akisamehe mahari yake iliyobainishwa, na mahari hiyo ilikuwa ni deni katika shingo ya mume, basi mahari hiyo hudondoka, lakini kwa sharti mke awe na vigezo vya kusamehe na kutoa anachomiliki.

 

4-  Mwanamke kutunuku mahari yake yote kwa mume:

 

Madhali mke ana vigezo vya kutoa anachomiliki, na mume akakubali kutunukiwa mahari kwenye baraza ya kufunga ‘aqdi, ni sawa tunu hiyo ikawa kabla ya kukabidhi mahari au baada yake, basi mahari itadondoka.

 

 

Share [2]
www.alhidaaya.com

Source URL: https://www.alhidaaya.com/sw/node/11970

Links
[1] http://www.alhidaaya.com/
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11970&title=11-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Mahari%3A%20Yanayopelekea%20Kudondoka%20Mahari%20Yote