كتاب الزواج
Kitabu Cha Ndoa
الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ
Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume
Abu Maalik Kamaal Bin As-Sayyid Saalim
Imetarjumiwa na 'Abdullaah Mu'aawiyah (Abu Baasim)
Alhidaaya.com
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ
Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume
Alhidaaya.com [3]
Kwanza: Haki Zinazompasa Mke Kumtendea Mumewe: Baadhi Ya Dalili Kutoka Kwenye Qur-aan Na Hadiyth:
Asili ya haki hizi iko ndani ya Kauli Yake Ta’aalaa:
"الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاءِ بِمَا فَضَّلَ اللَّـهُ بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ وَبِمَا أَنفَقُوا مِنْ أَمْوَالِهِمْ ۚ فَالصَّالِحَاتُ قَانِتَاتٌ حَافِظَاتٌ لِّلْغَيْبِ بِمَا حَفِظَ اللَّـهُ ۚ وَاللَّاتِي تَخَافُونَ نُشُوزَهُنَّ فَعِظُوهُنَّ وَاهْجُرُوهُنَّ فِي الْمَضَاجِعِ وَاضْرِبُوهُنَّ ۖ فَإِنْ أَطَعْنَكُمْ فَلَا تَبْغُوا عَلَيْهِنَّ سَبِيلًا ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيًّا كَبِيرًا "
“Wanaume ni wasimamizi juu ya wanawake kwa kuwa Allaah Amefadhilisha baadhi yao kuliko wengine, na pia kwa ambayo wanatoa katika mali zao. Basi wanawake wema ni wale watiifu wenye kujihifadhi katika hali ya kutokuweko waume zao kwa kuwa Allaah Ameamrisha wajihifadhi. Na wale ambao mnakhofu uasi wao wa ndoa, basi wanasihini na wahameni katika malazi na wapigeni (kipigo kisichodhuru). Wakikutiini, basi msitafute njia dhidi yao (ya kuwaudhi). Hakika Allaah daima Ni Mwenye Uluwa, Mkubwa wa Dhati, Vitendo na Sifa”. [An-Nisaa: 34]
Haki anazopaswa mke kumtendea mumewe ni kubwa mno kama alivyosema Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"لا يَصْلُحُ لبَشَرٍ أنْ يَسْجُدَ لِبَشَرٍ، وَلَوْ صَلَحَ أَنْ يَسْجُدَ بَشَرٌ لِبَشَرٍ ، لَأَمَرْتُ المرْأَةَ أَنْ تَسْجُدَ لِزَوْجِهَا مِنْ عِظَمِ حَقِّهِ عَلَيْهَا ، وَالَّذِيْ نَفْسِيْ بِيَدِه ، لَوْ أَنَّ مِنْ قَدَمِهِ إلى مَفْرِقِ رَأْسِهِ قُرْحَةً تَنْبَجِسُ بالقَيْحِ والصَّدِيدِ ، ثم أَقْبَلَتْ تَلْحَسُه ، ما أَدَّتْ حَقَّه"
“Si haki kwa mwanadamu kumsujudia mwanadamu mwenzake. Na lau ingelikuwa ni haki kwa mwanadamu kumsujudia mwanadamu mwingine, basi ningelimwamuru mwanamke amsujudie mumewe kutokana na ukubwa wa haki anazopasa kumtendea. Basi naapa kwa Yule Ambaye nafsi yangu iko Mkononi Mwake, lau kama mume ana madonda yenye kutumbuka maji maji na usaha kuanzia miguuni hadi kichwani, kisha mke akawa anampangusa kwa ulimi wake, basi pia asingeliweza kuikamilisha haki yake”. [Hadiyth Swahiyh. Swahiyhul Jaami’i (7725)]
Kadhalika, mwanamke kumtii mumewe ni moja kati ya mambo yatakayomfanya aingie Peponi. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إِذَا صَلَّتْ الْمَرْأَةُ خَمْسَهَا، وَصَامَتْ شَهْرَهَا، وَأَحْصَنَتْ فَرْجَهَا، وَأَطَاعَتْ زَوْجَهَا، قِيْلَ لَهَا: ادْخُلِي الجَنَّةَ مِنْ أَيِّ اَبْوَابِهَا شِئْتِ"
“Mwanamke akiswali swalaah zake (tano), akafunga mwezi wake (wa Ramadhaan), akalinda utupu wake (na zinaa), na akamtii mumewe, ataambiwa (Siku ya Qiyaamah): Ingia Jannah kupitia mlango wake wowote uutakao”. [Hadiyth Swahiyh. Ibn Hibaan (4163)]
Ikiwa mambo ni hivi, basi ni vyema sana kwa mwanamke wa Kiislamu kuzijua vyema haki anazopaswa kumfanyia mumewe. Haki hizo ni hizi zitakazotajwa moja baada ya nyingi.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ
Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume
Alhidaaya.com [3]
01: Haki Zinazompasa Mke Kumtendea Mumewe: 1- Amtii Kwa Mambo Yote Halali Anayomwamuru:
"عَنِ الْحُصَيْنِ بْنِ مِحْصَنٍ، أَنَّ عَمَّةً لَهُ أَتَتِ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي حَاجَةٍ، فَفَرَغَتْ مِنْ حَاجَتِهَا، فَقَالَ لَهَا النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: أَذَاتُ زَوْجٍ أَنْتِ؟ [5]قَالَتْ: نَعَمْ، قَالَ: كَيْفَ أَنْتِ لَهُ؟ [6]قَالَتْ: مَا آلُوهُ إِلَّا مَا عَجَزْتُ عَنْهُ، قَالَ: فَانْظُرِي أَيْنَ أَنْتِ مِنْهُ، فَإِنَّمَا هُوَ جَنَّتُكِ وَنَارُكِ" [7]
“Toka kwa Al-Huswayn bin Mihswan amesema kwamba: Shangazi yake alikwenda kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa ajili ya haja fulani. Alipomaliza kueleza haja yake, Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimuuliza: Una mume wewe? Akajibu: Na’am. Akamuuliza: Uko naye vipi? Akasema: Sizembei kwa lolote (analoniamuru) isipokuwa lile nisiloliweza. Akamwambia: Basi chunga nafasi yako kwake, kwani yeye ndiye (sababu ya) Pepo yako na moto wako”. [Hadiyth Hasan. An-Nasaaiy katika Al-‘Ishrah (uk. 106), Al-Haakim (2/189), Al-Bayhaqiy (7/291) na Ahmad (4/341)]
Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliulizwa kuhusu mwanamke aliye bora zaidi kuliko wengine akajibu:
“Ni yule anayemsikiliza mumewe anapomwamrisha, anamfurahisha anapomtazama, na anamlinda kwa kujichunga yeye mwenyewe na mali yake”. [Hadiyth Swahiyh. An-Nasaaiy (6/68)]
Angalizo:
Utiifu wa mke kwa mumewe una mipaka yake. Mwanamke anaruhusiwa kumtii mumewe kwa yote yanayokubalika kisharia. Ama kwa ya kumwasi Allaah Ta’aalaa, hayo hayaruhusiwi kumtii. Ni kama kumwamuru atoke nje bila hijabu, au asiswali, au amuingilie kinyume na maumbile au wakati akiwa katika hedhi na kadhalika. Kwa mambo kama haya haruhusiwi kumtii. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"لَا طَاعَةَ فِي مَعْصِيَةٍ إِنَّمَا الطَّاعَةُ فِي الْمَعْرُوف"
“Hakuna ruksa hata kidogo kutii jambo la uasi, bali utiifu ni katika jambo jema la halali”. [Al-Bukhaariy (7258) na Muslim (1840)]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ
Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume
Alhidaaya.com [3]
02: Haki Zinazompasa Mke Kumtendea Mumewe 2- Atulie Nyumbani Kwake, Asitoke Ila Kwa Ruksa Ya Mumewe:
Allaah Ta’aalaa Amesema:
"وَقَرْنَ فِي بُيُوتِكُنَّ وَلَا تَبَرَّجْنَ تَبَرُّجَ الْجَاهِلِيَّةِ الْأُولَىٰ"
“Na bakieni majumbani mwenu, na wala msionyeshe mapambo na uzuri kwa ajinabi kujishaua kama zama za ujahili”. [Al-Ahzaab: 33]
Sheikh wa Uislamu amesema: “Si halali kwa mke kutoka nyumbani kwake bila idhini ya mumewe. Na kama atatoka bila idhini, basi anakuwa amegomea haki ya mume, amemwasi Allaah na Rasuli Wake, na anastahili adhabu”. [Majmuw’ul Fataawaa (32/281)]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ
Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume
Alhidaaya.com [3]
03: Haki Zinazompasa Mke Kumtendea Mumewe: 3- Amkubalie Tendo La Jimai Kama Atataka:
Tendo la jimai ni haki mke ampatie mumewe ikiwa hali yake inaruhusu. Kama hairuhusu kwa kuwa mgonjwa, au kachoka sana, au hajisikii vizuri, basi anaweza kukataa, na ni lazima mume naye achunge hali ya mkewe. Kama hana lolote, basi anakuwa ni mwenye kumwasi Mola wake na anastahiki laana kama alivyosema Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"إِذَا دَعَا الرَّجُلُ امْرَأَتَهُ إِلَى فِرَاشِهِ فَأَبَتْ فَبَاتَ غَضْبَانَ عَلَيْهَا لَعَنَتْهَا الْمَلَائِكَةُ حَتَّى تُصْبِحَ"
“Mume akimtaka mkewe kitandani (kwa jimai) na mke akakataa, halafu mume akalala na hasira dhidi yake, basi Malaika watamlaani hadi kupambazuke”. [Al-Bukhaariy (3237) na Muslim (1436)]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ
Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume
Alhidaaya.com [3]
04-Haki Zinazompasa Mke Kumtendea Mumewe: 4-Asimruhusu Yeyote Kuingia Nyumbani Kwa Mumewe Ila Kwa Idhini Yake:
Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anawaambia akina mama:
"وَإِنَّ لَكُمْ عَلَيْهِنَّ أَلاَّ يُوطِئْنَ فُرُشَكُمْ مَنْ تَكْرَهُونَ "
“Na kwamba haki yao wao kukufanyieni nyinyi ni kwamba wasimuingize nyumbani kwenu yeyote msiyetaka aingie humo”. [Swahiyh Muslim (1218)]
Na anasema tena Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"وَلاَ تَأْذَنِ المَرْأَةُ فِي بَيْتِ زَوْجِهَا وَهُوَ شَاهِدٌ إِلاَّ بِإِذْنِهِ"
“Na mwanamke asiruhusu (kuwepo mtu) katika nyumba ya mumewe naye yupo isipokuwa kwa idhini yake”. [Swahiyh Muslim (1026)]
Hili linachukulika kwa yule ambaye mke hajui kama mumewe anaridhika uwepo wake nyumbani. Lakini kama atajua kwamba mume anaridhika, basi hakuna ubaya kumruhusu kama atakuwa ni katika watu wanaofaa kuingia kwake, na Allaah Ndiye Ajuaye zaidi.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ
Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume
Alhidaaya.com [3]
05: Haki Zinazompasa Mke Kumtendea Mumewe: 5-Asifunge Swawm Ya Sunnah Ilhali Mumewe Yuko Ila Kwa Ruhusa Yake:
Ni kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"لَا يَحِلُّ لِلْمَرْأَةِ أَنْ تَصُومَ وَزَوْجُهَا شَاهِدٌ إِلَّا بِإِذْنِهِ"
“Si halali mwanamke kufunga ilhali mumewe yuko ila kwa idhini yake”. [Al-Bukhaariy (5195), At-Tirmidhiy (782) na Ibn Maajah (1761)]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ
Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume
Alhidaaya.com [3]
06: Haki Zinazompasa Mke Kumtendea Mumewe: 6-Asitumie Mali Yake Isipokuwa Kwa Idhini Yake:
Ni kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"لَا تُنْفِقُ امْرَأَةٌ شَيْئًا مِنْ بَيْتِ زَوْجِهَا إِلَّا بِإِذْنِ زَوْجِهَا"
“Mwanamke asitoe chochote cha nyumba ya mumewe ila kwa ruhusa yake”. [Abu Daawuwd (3565), At-Tirmidhiy (670), Ibn Maajah (2295). Sanad yake ni Hasan]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ
Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume
Alhidaaya.com [3]
07: Haki Zinazompasa Mke Kumtendea Mumewe: 7-Amtumikie Mumewe Pamoja Na Wanawe:
"فَقَدْ كَانَتْ فَاطِمَةَ بِنْتِ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ تَخْدُمُ زَوْجَهَا حَتَّى اشْتَكَتْ إِلَى رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مَا تَلْقَى مِنَ الرَّحَى فِي يَدِهَا"
“Faatwimah binti Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anamtumikia mumewe mpaka akamshitakia Rasuli wa Allaah sugu ya mkono wake kutokana na jiwe la kusagia nafaka”. [Hadiyth Swahiyh. Al-Bukhaariy (361) na Muslim (2182)]
Naye Asmaa bint Abiy Bakr As-Swiddiyq (Radhwiya Allaah ‘anhu) amesema:
"كُنْتُ أَخْدُمُ الزُّبَيْرَ بن العَوَّامَ خِدْمَةَ الْبَيْتِ كُلّهِ، وَكَانَ لَهُ فَرَسٌ، وَكُنْتُ أَسُوسُهُ، وكُنْتُ أَحْتَشُّ لَهُ وَأَقُومُ عَلَيْهِ"
“Nilikuwa namtumikia Az Zubayr bin Al-‘Awwaam (mumewe) huduma zote za nyumbani. Alikuwa na farasi ambaye nilikuwa namfunza kutii maelekezo, nilikuwa namkatia majani ya malisho na kumsimamia kwa mambo yote”.
Alikuwa pia anamlisha farasi majani, anachota maji, anashona ndoo ya ngozi, anakanda unga, anabeba kichwani kokwa za tende toka shamba la Az-Zubayr hadi nyumbani umbali wa kilometa nne”. [Al-Bukhaariy (5224) na Muslim (2182)]
Sheikh wa Uislamu amesema katika Al-Fataawaa (34/90-91):
“’Ulamaa wamevutana katika: Je, ni lazima mke amtumikie mumewe katika kuipanga nyumba, kumtayarishia chakula, kumletea majani ya malisho mnyama wake kama anaye na mfano wa hayo?
Kati yao kuna waliosema kwamba si wajibu kwake kumtumikia, lakini kauli hii ni dhaifu. Ni dhaifu mithili ya waliosema kwamba si wajibu kwake kumpa mumewe unyumba, kwa kuwa hili halileti maana ya kutangamana naye kwa wema. Mume ndiye mwenza wake katika safari yao ya maisha, na kama hakumsaidia kwenye maslaha yao ya pamoja, nyumba yao itakuwa katika hali gani?
‘Ulamaa wengine wamesema kwamba ni wajibu mke kumhudumia mumewe, kwani mume ndiye bwana wake kwa mujibu wa Kitabu cha Allaah, na mateka wa mume kwa mujibu wa Sunnah ya Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na mateka ni lazima atumikie, na huu ndio wema.
Kuna wengine pia wamesema ni lazima amtumikie huduma nyepesi nyepesi, na wengine wanasema amtumikie kwa mujibu wa ada na desturi, na hii ndio sawa. Ni wajibu kwake amtumikie huduma zinazofanana na mazingira yao na kwa mujibu wa hali. Huduma za mke wa vijijini kwa mumewe ni tofauti na za mjini, na hata mjini kwenyewe kunatofautiana kwa mujibu wa hali ya kila mmoja”.
Ninasema: “Kauli hii ndiyo iliyoungwa mkono na Abu Thawr, Abu Bakr bin Abi Shaybah, Abu Is-Haaq Al-Juwzajaaniy katika ‘Ulamaa wa Kihanbali.
Lakini Jumhuwr ya ‘Ulamaa wanasema kwamba si wajibu mke kumhudumia mume, bali ni lazima mume amwekee mhudumu wa kumtumikia haja zake!! Kwa sababu, kwa mujibu wa ‘aqdi ya ndoa, kipengele kinachohusika ni kustarehe naye tu kimwili, hivyo mke halazimiwi na mengineyo”.
Kiufupi, tunasema kwamba mke kumhudumia mume ni jambo la kimaumbile. Ni mwanamke gani ambaye yuko tayari kukaa tu ndani ya nyumba yake bila kujishughulisha kwa lolote, halafu asubiri mume aje amfanyie kazi za ndani pamoja na majukumu yake mengine ya kumtafutia riziki. Hakuna mwanamke wa aina hii kabisa. Isitoshe, Faatwimah binti Rasuli alikuwa akifanya kazi ngumu ya nyumbani kwake hadi kumlalamikia baba yake, na baba yake hakumwambia mumewe ‘Aliy kwamba mkewe asifanye tena kazi hizo na kwamba yeye ndiye afanye. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hampaki yeyote mafuta kwa lolote linalohusiana na hukmu au sharia. Kadhalika, Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipomwona Asmaa amebeba majani ya farasi kichwani akiwa pamoja na mumewe Az Zubayr, hakumwambia Az Zubayr kwa mfano: “Huyu asifanye tena kazi hizi, hii ni dhulma”, bali alinyamaza, na kunyamaza kwake ni kulikubalia na kuliridhia jambo kuwa liko sawa. Vile vile, aliwaachilia Maswahaba wengineo kuwatumikisha wake zao huku akijua kuwa baadhi ya wake wako radhi kwa hilo na wengine hawako radhi, na kuwa jambo hili halina shaka yoyote.
Kadhalika, hayo yote yako ndani ya wigo wa kusaidiana katika wema na taqwa. Lakini pamoja na hivyo, haina maana ya kuwa mume asimsaidie mkewe kwenye baadhi ya majukumu ya nyumbani na mengineyo kama alivyokuwa akifanya Rasuli, kwani hilo linaongeza pia penzi na huruma kati ya mke na mume.
Bibi ‘Aaishah (Radhwiya Allaah ‘anhaa) alipoulizwa nini anafanya Rasuli anapokuwa nyumbani, alijibu:
"كَانَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي مِهْنَةِ أَهْلِهِ، فَإِذَا حَضَرتِ الصَّلَاةُ خَرَجَ إِلَى الصَّلَاة"
“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anawasaidia wake zake na kuwahudumia, na wakati wa swalaah unapofika, hutoka akaenda kuswali”. [Hadiyth Swahiyh. Al-Bukhaariy (676)]
Mume anatakiwa achunge hali ya mkewe, asimchoshe au kumbebesha asiyoyaweza.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ
Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume
Alhidaaya.com [3]
08: Haki Zinazompasa Mke Kumtendea Mumewe: 8-Amlinde Kwa Kujichunga Yeye Mwenyewe, Watoto Wa Mumewe Na Mali Yake:
Allaah Ta’alaa Amesema:
"فَالصَّالِحَاتُ قَانِتَاتٌ حَافِظَاتٌ لِّلْغَيْبِ بِمَا حَفِظَ اللَّـهُ"
Basi wanawake wema ni wale watiifu wenye kujihifadhi katika hali ya kutokuweko waume zao kwa kuwa Allaah Ameamrisha wajihifadhi. [An-Nisaa: 34]
At-Twabariy akiifasiri aayah hii amesema: “Yaani, wanajihifadhi wenyewe wakati waume zao wanapokuwa hawapo, kwa kuzilinda tupu zao na mali za waume zao”.
Nyuma tumeitaja Hadiyth hii isemayo kuhusu mwanamke bora zaidi isemayo:
“Ni yule anayemsikiliza mumewe anapomwamrisha, anamfurahisha anapomtazama, na anamlinda kwa kujichunga yeye mwenyewe na mali ya mumewe”. [Hadiyth Swahiyh. An-Nasaaiy (6/68)]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ
Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume
Alhidaaya.com [3]
09: Haki Zinazompasa Mke Kumtendea Mumewe: 9-Amshukuru Mumewe, Asikanushe Wema Wake, Na Atangamane Naye Kwa Wema:
Toka kwa ‘Abdullaah bin ‘Umar kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"لاَ يَنْظُرُ اللهُ تبارك وتعالى إلى امْرَأَةٍ لا تَشْكُرُ لِزَوْجِهَا؛ وهيَ لا تَسْتَغْني عَنْهُ"
“Allaah Hamuangalii (kwa Jicho la Rahmah) mwanamke ambaye hamshukuru mumewe ilhali anamhitajia”. [Sanad yake ni Swahiyh]
Na Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema tena:
"وَرَأَيْتُ النَّارَ فَلَمْ أَرَ كَالْيَوْمِ مَنْظَرًا قَطُّ أَفْظَعَ وَرَأَيْتُ أَكْثَرَ أَهْلِهَا النِّسَاءَ. قَالُوا: لِمَ يَا رَسُولَ اللَّهِ؟ قَالَ: لِكُفْرِهِنَّ. قِيلَ: أَيَكْفُرْنَ بِاللَّهِ؟ قَالَ: يَكْفُرْنَ الْعَشِيرَ، وَيَكْفُرْنَ الإِحْسَانَ، لَوْ أَحْسَنْتَ إِلَى إِحْدَاهُنَّ الدَّهْرَ كُلَّهُ ثُمَّ رَأَتْ مِنْكَ شَيْئًا قَالَتْ: مَا رَأَيْتُ مِنْكَ خَيْرًا قَطُّ"
“Nikauona na moto. Sikupata kamwe kuona chochote kilicho kibaya na kirihishi zaidi kuliko nilichokiona leo. Na nikaona wengi wa watu wake ni wanawake. Wakamuuliza: Ni kwa nini ee Rasuli wa Allaah? Akasema: Kwa sababu ya kufuru yao. Wakauliza: Kumkufuru Allaah? Akasema: Wanamkufuru mume, wanakufuru wema waliotendewa. Lau utamfanyia wema mmoja wao umri wake wote, kisha akaona toka kwako chochote kisichompendeza, atasema: Sikuona kamwe kheri yoyote kutoka kwako”. [Al-Bukhaariy (29) na Muslim (884)]
Na hapa hatumaanishi shukurani ya ulimi tu, bali tunakusudia kwamba iende sambamba na kumwonyesha mume wake kuwa ana furaha na anahisi raha ya maisha akiwa ndani ya kumbatio lake mbali na kusimamia mambo yake na mambo ya watoto wake, kumhudumia, kutomtelekeza akiwa matatizoni, kutotoa malalamiko dhidi yake na mambo kama hayo.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ
Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume
Alhidaaya.com [3]
10: Haki Zinazompasa Mke Kumtendea Mumewe: 10-Ajipambe Na Ajitengeneze Kwa Ajili Yake:
Kama ilivyotangulia nyuma kwenye Hadiyth, mwanamke bora zaidi ni yule ambaye mumewe akimuangalia anafurahika kutokana na anavyojiweka katika hali ya usafi na umaridadi nyakati zote.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ
Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume
Alhidaaya.com [3]
11: Haki Zinazompasa Mke Kumtendea Mumewe: 11-Asimsimbulie Kama Atatumia Mali Yake Kwa Ajili Yake Na Watoto Wake:
Kusimbulia kunaharibu thawabu na ajri kutoka kwa Allaah Anayesema:
"يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُبْطِلُوا صَدَقَاتِكُم بِالْمَنِّ وَالْأَذَىٰ"
“Enyi walioamini! Msibatilishe swadaqah zenu kwa masimbulizi na udhia”. [Al-Baqarah: 264]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ
Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume
Alhidaaya.com [3]
12: Haki Zinazompasa Mke Kumtendea Mumewe: 12-Aridhike Kwa Kidogo Na Atosheke Nacho, Na Wala Asimbebeshe Yaliyo Juu Ya Uwezo Wake:
Allaah Ta’alaa Amesema:
"لِيُنفِقْ ذُو سَعَةٍ مِّن سَعَتِهِ ۖ وَمَن قُدِرَ عَلَيْهِ رِزْقُهُ فَلْيُنفِقْ مِمَّا آتَاهُ اللَّـهُ ۚ لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا مَا آتَاهَا ۚ سَيَجْعَلُ اللَّـهُ بَعْدَ عُسْرٍ يُسْرًا"
“Ili mwenye wasaa agharimu kwa wasaa wake, na aliyebaniwa riziki yake, basi agharimie katika kile Alichompa Allaah. Allaah Haikalifishi nafsi yeyote ile isipokuwa kwa kile Alichoipa. Allaah Atajaalia baada ya ugumu kuwa wepesi”. [At-Twalaaq: 7]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ
Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume
Alhidaaya.com [3]
13: Haki Zinazompasa Mke Kumtendea Mumewe: 13-Asifanye Lolote Linalomuudhi Au Kumkasirisha:
Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"لَا تُؤْذِي امْرَأَةٌ زَوْجَهَا فِي الدُّنْيَا إِلَّا قَالَتْ زَوْجَتُهُ مِنَ الْحُورِ الْعِينِ: لَا تُؤْذِيهِ قَاتَلَكِ اللَّهُ، فَإِنَّمَا هُوَ عِنْدَكِ دَخِيلٌ يُوشِكُ أَنْ يُفَارِقَكِ إِلَيْنَا"
“Hakuna mwanamke yeyote anayemkera mumewe hapa duniani, isipokuwa mke wake mmoja katika mahurul-‘ayn humwambia: Usimsumbue, Allaah Akulaani, huyo kwako ni mgeni wa kupita tu, karibuni atakuacha aje kwetu”. [At-Tirmidhiy (1184) na Ibn Maajah (2014) kwa Sanad Hasan]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ
Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume
Alhidaaya.com [3]
14: Haki Zinazompasa Mke Kumtendea Mumewe: 14-Aamiliane Vyema Na Wazazi Wake Na Jamaa Zake:
Hili bila shaka litazidisha heshima na penzi toka kwa mumewe na kutoka kwa wazazi wake na jamaa zake kiujumla. Na hii pia ni dalili ya kuwa huyo ni mke mwema aliyeleleka juu ya maadili mema ya kidini.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ
Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume
Alhidaaya.com [3]
15: Haki Zinazompasa Mke Kumtendea Mumewe: 15-Awe Na Hima Ya Kuendelea Kuishi Naye Hadi Mwisho, Na Asiombe Talaka Isipokuwa Kwa Sababu Za Kisharia:
Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"أَيُّمَا امْرَأَةٍ سَأَلَتْ زَوْجَهَا طَلَاقًا فِي غَيْرِ مَا بَأْسٍ فَحَرَامٌ عَلَيْهَا رَائِحَةُ الْجَنَّةِ"
“Mwanamke yeyote anayemdai mumewe talaka bila kuwepo madhara yoyote, basi ni marufuku kwake harufu ya Pepo”. [Hadiyth Swahiyh. At-Tirmidhiy (1199), Abu Daawuwd (2209) na Ibn Maajah (2055)]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ
Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume
Alhidaaya.com [3]
16: Haki Zinazompasa Mke Kumtendea Mumewe: 16-Mumewe Akifa Amkalie Eda Kwa Muda Wa Miezi Minne Na Siku Kumi:
Mwanamke aliyefiwa na mumewe wa ndoa sahihi, ni lazima akae eda kwa muda wa miezi minne na siku kumi, ni sawa ikiwa alimuingilia au hakumuingilia, au ni katika wanaopata hedhi au waliokatikiwa. Na hii ni kwa Neno Lake Ta’aalaa:
"وَالَّذِينَ يُتَوَفَّوْنَ مِنكُمْ وَيَذَرُونَ أَزْوَاجًا يَتَرَبَّصْنَ بِأَنفُسِهِنَّ أَرْبَعَةَ أَشْهُرٍ وَعَشْرًا"
“Na wale wanaofishwa miongoni mwenu na wakaacha wake, hao wake wajisubirishe wenyewe (kwa kukaa eda) miezi minne na siku kumi”. [Al-Baqarah: 234]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ
Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume
Alhidaaya.com [3]
Pili: Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: Utangulizi:
Haki hizi, kwanza ni haki za kimali kama ilivyotangulia nyuma na pesa za matumizi. Pili, ni haki zisizo za kifedha, nazo ni hizi zitakazotajwa kwa mlolongo wa nambari.
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/284
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12012&title=10H-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20%D9%83%D8%AA%D8%A7%D8%A8%20%D8%A7%D9%84%D8%B2%D9%88%D8%A7%D8%AC%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20%D8%A7%D9%84%D8%AD%D9%8F%D9%82%D9%8F%D9%88%D9%92%D9%82%D9%8F%20%D8%A8%D9%8E%D9%8A%D9%92%D9%86%D9%8E%20%D8%A7%D9%84%D8%B2%D9%91%D9%8E%D9%88%D9%92%D8%AC%D9%8E%D9%8A%D9%92%D9%86%D9%90%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume
[3] http://www.alhidaaya.com/
[4] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12013&title=01-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20Kwanza%3A%20%20Haki%20Zinazompasa%20Mke%20Kumtendea%20Mumewe
[5] https://alsunniah.com/search/content?query=%D8%A3%D8%B0%D8%A7%D8%AA+%D8%B2%D9%88%D8%AC+%D8%A3%D9%86%D8%AA
[6] https://alsunniah.com/search/content?query=%D9%83%D9%8A%D9%81+%D8%A3%D9%86%D8%AA+%D9%84%D9%87
[7] https://alsunniah.com/search/content?query=%D9%81%D8%A7%D9%86%D8%B8%D8%B1%D9%8A+%D8%A3%D9%8A%D9%86+%D8%A3%D9%86%D8%AA+%D9%85%D9%86%D9%87+%D9%81%D8%A5%D9%86%D9%85%D8%A7+%D9%87%D9%88+%D8%AC%D9%86%D8%AA%D9%83+%D9%88%D9%86%D8%A7%D8%B1%D9%83
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12014&title=02-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20Haki%20Zinazompasa%20Mke%20Kumtendea%20Mumewe%3A%201-%20Amtii%20Kwa%20Mambo%20Yote%20Halali%20Anayomwamuru
[9] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12015&title=03-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20Haki%20Zinazompasa%20Mke%20Kumtendea%20Mumewe%20%202-%20%20Atulie%20Nyumbani%20Kwake%2C%20Asitoke%20Ila%20Kwa%20Ruksa%20Ya%20Mumewe
[10] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12016&title=04-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20Haki%20Zinazompasa%20Mke%20Kumtendea%20Mumewe%3A%20%203-%20Amkubalie%20Tendo%20La%20Jimai%20Kama%20Atataka
[11] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12017&title=05-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20Haki%20Zinazompasa%20Mke%20Kumtendea%20Mumewe%3A%204-Asimruhusu%20Yeyote%20Kuingia%20Nyumbani%20Kwa%20Mumewe%20Ila%20Kwa%20Idhini%20Yake
[12] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12018&title=06-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20Haki%20Zinazompasa%20Mke%20Kumtendea%20Mumewe%3A%205-Asifunge%20Swawm%20Ya%20Sunnah%20Ilhali%20Mumewe%20Yuko%20Ila%20Kwa%20Ruhusa%20Yake%3A
[13] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12019&title=07-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20Haki%20Zinazompasa%20Mke%20Kumtendea%20Mumewe%3A%206-Asitumie%20Mali%20Yake%20Isipokuwa%20Kwa%20Idhini%20Yake
[14] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12020&title=08-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20Haki%20Zinazompasa%20Mke%20Kumtendea%20Mumewe%3A%207-Amtumikie%20Mumewe%20Pamoja%20Na%20Wanawe
[15] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12021&title=09-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20Haki%20Zinazompasa%20Mke%20Kumtendea%20Mumewe%3A%20%208-Amlinde%20Kwa%20Kujichunga%20Yeye%20Mwenyewe%2C%20Watoto%20Wa%20Mumewe%20Na%20Mali%20Yake
[16] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12022&title=10-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20Haki%20Zinazompasa%20Mke%20Kumtendea%20Mumewe%3A%209-Amshukuru%20Mumewe%2C%20Asikanushe%20Wema%20Wake%2C%20Na%20Atangamane%20Naye%20Kwa%20Wema
[17] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12023&title=11-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20Haki%20Zinazompasa%20Mke%20Kumtendea%20Mumewe%3A%2010-Ajipambe%20Na%20Ajitengeneze%20Kwa%20Ajili%20Yake
[18] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12024&title=12-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20Haki%20Zinazompasa%20Mke%20Kumtendea%20Mumewe%3A%2011-Asimsimbulie%20Kama%20Atatumia%20Mali%20Yake%20Kwa%20Ajili%20Yake%20Na%20Watoto%20Wake
[19] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12025&title=13-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20Haki%20Zinazompasa%20Mke%20Kumtendea%20Mumewe%3A%20%2012-Aridhike%20Kwa%20Kidogo%20Na%20Atosheke%20Nacho%2C%20Na%20Wala%20Asimbebeshe%20Yaliyo%20Juu%20Ya%20Uwezo%20Wake
[20] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12026&title=14-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20Haki%20Zinazompasa%20Mke%20Kumtendea%20Mumewe%3A%2013-Asifanye%20Lolote%20Linalomuudhi%20Au%20Kumkasirisha
[21] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12027&title=15-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20Haki%20Zinazompasa%20Mke%20Kumtendea%20Mumewe%2014-Aamiliane%20Vyema%20Na%20Wazazi%20Wake%20Na%20Jamaa%20Zake
[22] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12028&title=16-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20Haki%20Zinazompasa%20Mke%20Kumtendea%20Mumewe%3A%2015-Awe%20Na%20Hima%20Ya%20Kuendelea%20Kuishi%20Naye%20Hadi%20Mwisho%2C%20Na%20Asiombe%20Talaka%20Isipokuwa%20Kwa%20Sababu%20Za%20Kisharia
[23] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12029&title=17-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20Haki%20Zinazompasa%20Mke%20Kumtendea%20Mumewe%3A16-Mumewe%20Akifa%20Amkalie%20Eda%20Kwa%20Muda%20Wa%20Miezi%20Minne%20Na%20Siku%20Kumi
[24] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12030&title=18-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20Pili%3A%20Haki%20Zinazompasa%20Mume%20Kumtendea%20Mkewe%3A%20Utangulizi%3A