Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ
Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume
Alhidaaya.com [1]
09: Haki Zinazompasa Mke Kumtendea Mumewe: 9-Amshukuru Mumewe, Asikanushe Wema Wake, Na Atangamane Naye Kwa Wema:
Toka kwa ‘Abdullaah bin ‘Umar kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"لاَ يَنْظُرُ اللهُ تبارك وتعالى إلى امْرَأَةٍ لا تَشْكُرُ لِزَوْجِهَا؛ وهيَ لا تَسْتَغْني عَنْهُ"
“Allaah Hamuangalii (kwa Jicho la Rahmah) mwanamke ambaye hamshukuru mumewe ilhali anamhitajia”. [Sanad yake ni Swahiyh]
Na Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema tena:
"وَرَأَيْتُ النَّارَ فَلَمْ أَرَ كَالْيَوْمِ مَنْظَرًا قَطُّ أَفْظَعَ وَرَأَيْتُ أَكْثَرَ أَهْلِهَا النِّسَاءَ. قَالُوا: لِمَ يَا رَسُولَ اللَّهِ؟ قَالَ: لِكُفْرِهِنَّ. قِيلَ: أَيَكْفُرْنَ بِاللَّهِ؟ قَالَ: يَكْفُرْنَ الْعَشِيرَ، وَيَكْفُرْنَ الإِحْسَانَ، لَوْ أَحْسَنْتَ إِلَى إِحْدَاهُنَّ الدَّهْرَ كُلَّهُ ثُمَّ رَأَتْ مِنْكَ شَيْئًا قَالَتْ: مَا رَأَيْتُ مِنْكَ خَيْرًا قَطُّ"
“Nikauona na moto. Sikupata kamwe kuona chochote kilicho kibaya na kirihishi zaidi kuliko nilichokiona leo. Na nikaona wengi wa watu wake ni wanawake. Wakamuuliza: Ni kwa nini ee Rasuli wa Allaah? Akasema: Kwa sababu ya kufuru yao. Wakauliza: Kumkufuru Allaah? Akasema: Wanamkufuru mume, wanakufuru wema waliotendewa. Lau utamfanyia wema mmoja wao umri wake wote, kisha akaona toka kwako chochote kisichompendeza, atasema: Sikuona kamwe kheri yoyote kutoka kwako”. [Al-Bukhaariy (29) na Muslim (884)]
Na hapa hatumaanishi shukurani ya ulimi tu, bali tunakusudia kwamba iende sambamba na kumwonyesha mume wake kuwa ana furaha na anahisi raha ya maisha akiwa ndani ya kumbatio lake mbali na kusimamia mambo yake na mambo ya watoto wake, kumhudumia, kutomtelekeza akiwa matatizoni, kutotoa malalamiko dhidi yake na mambo kama hayo.
Links
[1] http://www.alhidaaya.com/
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12022&title=10-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20Haki%20Zinazompasa%20Mke%20Kumtendea%20Mumewe%3A%209-Amshukuru%20Mumewe%2C%20Asikanushe%20Wema%20Wake%2C%20Na%20Atangamane%20Naye%20Kwa%20Wema