Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ
Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume
Alhidaaya.com [1]
16: Haki Zinazompasa Mke Kumtendea Mumewe: 16-Mumewe Akifa Amkalie Eda Kwa Muda Wa Miezi Minne Na Siku Kumi:
Mwanamke aliyefiwa na mumewe wa ndoa sahihi, ni lazima akae eda kwa muda wa miezi minne na siku kumi, ni sawa ikiwa alimuingilia au hakumuingilia, au ni katika wanaopata hedhi au waliokatikiwa. Na hii ni kwa Neno Lake Ta’aalaa:
"وَالَّذِينَ يُتَوَفَّوْنَ مِنكُمْ وَيَذَرُونَ أَزْوَاجًا يَتَرَبَّصْنَ بِأَنفُسِهِنَّ أَرْبَعَةَ أَشْهُرٍ وَعَشْرًا"
“Na wale wanaofishwa miongoni mwenu na wakaacha wake, hao wake wajisubirishe wenyewe (kwa kukaa eda) miezi minne na siku kumi”. [Al-Baqarah: 234]
Links
[1] http://www.alhidaaya.com/
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12029&title=17-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20Haki%20Zinazompasa%20Mke%20Kumtendea%20Mumewe%3A16-Mumewe%20Akifa%20Amkalie%20Eda%20Kwa%20Muda%20Wa%20Miezi%20Minne%20Na%20Siku%20Kumi