Alhidaaya.com
Published on Alhidaaya.com (https://www.alhidaaya.com/sw)

Ukurasa Wa Kwanza > 10H(ii)-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: كتاب الزواج Kitabu Cha Ndoa: الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: (ii) Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe

10H(ii)-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: كتاب الزواج Kitabu Cha Ndoa: الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: (ii) Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe

Swahiyh Fiqh As-Sunnah [1]

 

 

كتاب الزواج

 

Kitabu Cha Ndoa

 

 

 

الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ

 

 

 Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume

(ii) Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe

 

 

Abu Maalik Kamaal Bin As-Sayyid Saalim

 

Imetarjumiwa na 'Abdullaah Mu'aawiyah (Abu Baasim)

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

Share [2]

01-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: (ii) Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: Utangulizi:

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ

 

Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume

 

Alhidaaya.com [3]

 

 

Pili:  Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe:  Utangulizi:

 

Haki hizi, kwanza ni haki za kimali kama ilivyotangulia nyuma na pesa za matumizi.   Pili, ni haki zisizo za kifedha, nazo ni hizi zitakazotajwa kwa mlolongo wa nambari.

 

 

 

Share [4]

02-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: (ii) Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: Atangamane Naye Kwa Wema:

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ

 

Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume

 

Alhidaaya.com [3]

 

 

 

01:  Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: 1-Atangamane Naye Kwa Wema:

 

Hii inajumuisha kuishi naye kwa wema, kumlinda na madhara, kumfurahikia, kumkunjukia na kumhisisha uhuru ndani ya wigo wa maisha yao ya ndoa.  Na hii ni kutokana na Kauli Yake Ta’aalaa:

 

"وَعَاشِرُوهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ"

 

“Na kaeni nao kwa wema”.  [An-Nisaa: 19]

 

Na Kauli Yake Ta’aalaa:

 

"وَلَهُنَّ مِثْلُ الَّذِي عَلَيْهِنَّ بِالْمَعْرُوفِ"

 

“Nao wake wana haki kama ambayo (ya waume zao) iliyo juu yao kwa mujibu wa shariy’ah”.  [Al-Baqarah: 228]

 

Na Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

"خَيْرُكُمْ خَيْرُكُمْ لِأَهْلِهِ وَأَنَا خَيْرُكُمْ لِأَهْلِي"

 

“Mbora wenu zaidi ni yule aliye mwema zaidi kwa mkewe, na mimi ndiye mwema zaidi kuliko nyinyi kwa wake zangu”.   [Hadiyth Swahiyh.  At-Tirmidhiy (3892), na Ibn Hibaan (1312)]

 

Mtangamano mwema ni neno jumuishi ambalo haki zote zinaingia ndani yake.  Haki zinazofuatia ni sehemu tu ya mtangamano huo, nasi tunazitaja moja baada ya nyingine ili wanaume wazizingatie kwa uangalifu zaidi.  

 

 

Share [5]

03-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: (ii) Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: Matumizi: Maana Ya Matumizi

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ

 

Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume

 

Alhidaaya.com [3]

 

 

 

02: Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: 2-Matumizi: (a) Maana Ya Matumizi:

 

Makusudio ya matumizi hapa ni gharama anazozitoa mume kwa mkewe na wanawe kwa ajili ya chakula, mavazi, sehemu ya kuishi na mfano wa hayo.  Matumizi haya ambayo mume anayatoa ni lazima kwake kwa mujibu wa Qur-aan, Sunnah, ‘Ijmaa na kiakili.

 

Kwenye Qur-aan, ni:

 

1-Kauli Yake Ta’aalaa:

 

"لِيُنفِقْ ذُو سَعَةٍ مِّن سَعَتِهِ ۖ وَمَن قُدِرَ عَلَيْهِ رِزْقُهُ فَلْيُنفِقْ مِمَّا آتَاهُ اللَّـهُ ۚ لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا مَا آتَاهَا ۚ سَيَجْعَلُ اللَّـهُ بَعْدَ عُسْرٍ يُسْرًا"

 

“Ili mwenye wasaa agharimu kwa wasaa wake, na aliyebaniwa riziki yake, basi agharimie katika kile Alichompa Allaah.  Allaah Haikalifishi nafsi yeyote ile isipokuwa kwa kile Alichoipa.  Allaah Atajaalia baada ya ugumu kuwa wepesi”.  [At-Twalaaq: 07]

 

2-  Na Kauli Yake Ta’aalaa:

 

 

"وَعَلَى الْمَوْلُودِ لَهُ رِزْقُهُنَّ وَكِسْوَتُهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ"

 

“Na ni juu ya mzazi wa kiume kuwapatia chakula chao na nguo kwa mujibu wa ada”.  [Al-Baqarah: 233]

 

Ibn Kathiyr (Rahimahul Laah) amesema:  “Ni juu ya baba wa mtoto kutoa matumizi kwa mama mtoto na mavazi kwa mujibu wa ada na mazingira, bila kufuja wala kubana kwa mujibu wa uwezo wa baba mtoto”.

 

Ama Sunnah, ni Hadiyth hizi:

 

1-  Hadiyth ya Jaabir akielezea Hijja ya Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambapo Rasuli alisema:

 

"اتَّقوا اللهَ في النِّسَاءِ، فإنَّهُنَّ عَوَانٍ عِنْدَكُمْ، أَخَذْتُمُوْهُنَّ بِأمَانةِ اللهِ، وَاسْتَحْلَلْتُمْ فُرُوْجَهُنَّ بِكَلِمَةِ الله، َوَلَهُنَّ عَلَيْكُمْ رِزْقُهُنَّ وكِسْوَتُهنَّ بِالمعْرُوْفِ"

 

“Mcheni Allaah katika kuamiliana kwenu na wanawake, kwani wao ni mateka walio mikononi mwenu, mmewachukua kwa Dhamana ya Allaah, mmehalalikiwa tupu zao kwa Neno la Allaah, nanyi ni wajibu wenu kuwalisha na kuwavisha kwa mujibu wa ada”.  [Hadiyth Swahiyh.  Muslim (1218)]

 

2-  Hadiyth ya Mu’aawiyah Al-Qushayriy (Radhwiya Allaah ‘anhu), amesema:

 

"قُلْتُ: يَا رَسُولَ اَللَّهِ! مَا حَقُّ زَوْجَةِ أَحَدِنَا عَلَيْهِ? قَالَ: "أَنْ تُطْعِمَهَا إِذَا طَعِمْتَ، وَتَكْسُوَهَا إِذَا اِكْتَسَيْتَ، وَلَا تَضْرِبِ اَلْوَجْهَ، وَلَا تُقَبِّحْ، ولا تَهْجُرْ إِلا في البَيْتِ"

“Nilisema:  Ee Rasuli wa Allaah!  Ni zipi haki ambazo mmoja wetu anapaswa kumfanyia mkewe?  Akasema:  Mlishe sawa na unachokula, mvishe kiwango sawa na unachovaa, wala usimpige usoni, wala usimkashifu kumwambia ni mbaya, wala usimsuse isipokuwa ndani ya nyumba tu”.  [Hadiyth Hasan.  Imechakatwa na Abu Daawuwd (2142), Ibn Maajah (1850), Ahmad (4/447) na An-Nasaaiy katika (Al-‘Ish-rah) (269)]

 

3-  Hadiyth ya ‘Aaishah (Radhwiya Allaah ‘anhaa) kwamba Hind bint ‘Utbah alimwambia Rasuli:

 

"يا رَسُولَ اللهِ! ِإِنَّ أَبَا سُفْيَانَ رَجُلٌ شَحِيحٌ، لا يُعْطِيْني مَا يَكْفِيْني وَوَلَدِي إلَّا مَا أَخَذْتُ مِنْ مَالِهِ وَهوَ لا يعلَمُ.‏ قَالَ: خُذِي مَا يَكْفِيكِ وَوَلَدَكِ بِالْمَعْرُوفِ"‏‏.‏

“Ee Rasuli wa Allaah!  Hakika Abu Sufyaan ni mtu bahili, na hanipi chochote wala watoto wangu isipokuwa kile ninachochukua katika pesa zake bila yeye kujua.  Akamwambia:  Chukua kinachokutosha wewe na wanao kwa mujibu wa mahitaji”.  [Hadiyth Swahiyh.  Imechakatwa na Al-Bukhaariy (5364) na Muslim (1714)]

 

Ama ‘Ijmaa, ni kwamba ‘Ulamaa wengi wamekubaliana kwa sauti moja kwamba ni lazima mume amkidhie mkewe matumizi -yote kama mume amebaleghe- ila tu kama mke atakuwa mwasi.

 

Na ama kiakili, ni kwamba mke huwa amefungika chini ya mamlaka ya mume ambaye humzuia asifanye atakalo au kuhangaikia maisha ili abakie na jukumu la kumtekelezea haki zake stahiki, na kwa ajili hiyo, ni lazima mume huyu amgharamikie matumizi yote ya lazima.

 

 

Share [6]

04-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: (ii) Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: Matumizi: Masharti Ya Matumizi Kuwa Wajibu

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ

 

Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume

 

Alhidaaya.com [3]

 

 

03:  Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: Matumizi: (b) Masharti Ya Matumizi Kuwa Wajibu:

 

Jumhuwr ya ‘Ulamaa wameweka masharti kwenye suala hili.  Masharti haya ni ya kabla ya kumuingilia na baada ya kumuingilia mke.

 

Masharti Ya Kabla Ya Kumuingilia:

 

1-  Mke amwezeshe mume kumuingilia kwa kumrahisishia kila kitu baada ya ndoa kufungwa.  Na kama hakufanya hivyo, au akakataa bila ya udhuru wa kukubalika, basi matumizi yatakuwa si wajibu juu ya mume.

 

2- Mke awe na uwezo wa kuingiliwa, kwa maana, asiwe bint mdogo sana au kuwepo kizuizi kinachozuia tendo kufanyika.

 

3-  ‘Aqdi iwe sahihi.  Ikiwa ni batili, basi hakuna matumizi juu ya mume, na mke hazingatiwi kwamba yuko chini ya mamlaka ya mume, kwa kuwa ndoa yenyewe ni batili.

 

Masharti Baada Ya Kumuingilia:

 

1-  Mume awe anajiweza kimali.  Kama hali yake ni ngumu hana cha kutoa, basi si juu yake kutoa katika muda wote wa kugandwa na hali hiyo.  Ni kwa Neno Lake Ta’aalaa:

 

"لِيُنفِقْ ذُو سَعَةٍ مِّن سَعَتِهِ ۖ وَمَن قُدِرَ عَلَيْهِ رِزْقُهُ فَلْيُنفِقْ مِمَّا آتَاهُ اللَّـهُ ۚ لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا مَا آتَاهَا ۚ سَيَجْعَلُ اللَّـهُ بَعْدَ عُسْرٍ يُسْرًا"

 

“Ili mwenye wasaa agharimu kwa wasaa wake, na aliyebaniwa riziki yake, basi agharimie katika kile Alichompa Allaah.  Allaah Haikalifishi nafsi yeyote ile isipokuwa kwa kile Alichoipa.  Allaah Atajaalia baada ya ugumu kuwa wepesi”.  [At-Twalaaq: 07]

 

2-  Awe chini ya mamlaka yake (asiwe ametoka nje ya mamlaka ya utiifu), akitoka, basi mume hana matumizi juu yake.

 

Faida:  Mwanamke Anayefanya Kazi, Je, Mume Anawajibikiwa Kumpa Matumizi?

 

Ikiwa atafanya kazi mbali na nyumba yake -kazi ya halali- na kwa ridhaa ya mume, basi ni lazima mume ampatie matumizi, kwa sababu yeye mwenyewe ameiachia haki ya mkewe kubaki nyumbani.  Na kama hakuridhia, akamkataza kutoka naye akatoka kwenda kufanya kazi, basi haki yake ya kupewa matumizi itadondoka, kwa kuwa haki kwa mumewe ya kubakia nyumbani katika hali hii inakuwa na pengo.  (Ibn ‘Aabidiyna (2/891)]

 

 

Share [7]

05-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: (ii) Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: Matumizi: Makadirio Ya Matumizi Kwa Mke

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ

 

Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume

 

Alhidaaya.com [3]

 

 

 

04:  Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: Matumizi: (c) Makadirio Ya Matumizi Kwa Mke:

 

Asili ya hili ni Kauli Yake Ta’aalaa:

 

"لِيُنفِقْ ذُوْ سَعَةٍ مِّنْ سَعَتِهِ"

 

“Ili mwenye wasaa agharimu kwa wasaa wake”.  [At-Twalaaq: 7]

 

Na Kauli Yake:

 

"وَمَتِّعُوهُنَّ عَلَى الْمُوسِعِ قَدَرُهُ وَعَلَى الْمُقْتِرِ قَدَرُهُ مَتَاعًا بِالْمَعْرُوفِ"

 

“Wapeni kiliwazo kwa mwenye wasaa kadiri ya uwezo wake na mwenye dhiki kadiri ya uwezo wake.  Maliwaza kwa mujibu wa ada, ni haki kwa wafanya ihsaan”.  [Al-Baqarah: 236]

 

Na pia Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipomwambia Hind (mke wa Abu Sufyaan):

"خُذِي مَا يَكْفِيكِ وَوَلَدَكِ بِالْمَعْرُوفِ"‏‏.‏

 

“Chukua kinachokutosha wewe na wanao kwa mujibu wa mahitaji”.  [Hadiyth Swahiyh.  Imechakatwa na Al-Bukhaariy (5364) na Muslim (1714)]

 

Linalozingatiwa hapa ni:

 

1-  Kumtosheleza mke na watoto mahitaji yao kwa mujibu wa ada, na hili linatofautiana kwa kupishana hali za watu, mwahala na zama.

 

2-  Uwezo wa mume na wasaa wake:

 

‘Ulamaa (Rahimahumul Laahu) walizamia sana suala la kuainisha kiasi kilicho wajibu katika matumizi.  Wakachanganua kwenye hilo, na sisi tukaweza kuliona wakiwa wamelibainisha kwa mujibu wa ada na desturi za nyakati zao.

 

Katika suala hili la matumizi, je linalozingatiwa humo ni hali ya mume, au mke, au hali zao wote wawili?  Kwa mujibu wa aayaat zilizopita nyuma, linalozingatiwa ni hali ya mume; kama ana uwezo au hana uwezo.   ‘Ulamaa wa Kimaalik na Kishaafi’iy ndivyo wanavyoona.

 

 

Share [8]

06-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: (ii) Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: Matumizi: Je, Mume Anabeba Gharama Za Matibabu Ya Mke?

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ

 

Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume

 

Alhidaaya.com [3]

 

 

 

05: Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: Matumizi: (d) Je, Mume Anabeba Gharama Za Matibabu Ya Mke?

 

Madhehebu ya Maimamu wanne yanasema kwamba si wajibu kwa mume kugharamikia matibabu ya mkewe na kumuuguza!!  Lakini inavyoonekana ni kwamba msingi wa kauli yao hii ni kuwa huko nyuma zamani, kuuguza na kutibu halikuwa ni katika mambo ya kimsingi katika maisha ya watu, na halikuwa likihitajika kwa kiasi kikubwa, kwa kuwa zaidi kulikuwa na tiba za kijadi zisizo na gharama kubwa kama ilivyo leo. 

 

Lakini hivi leo, hitajio la matibabu limekuwa kama hitajio la chakula, bali limekuwa muhimu hata zaidi ya chakula, na hasa pia uwepo wa ongezeko kubwa la maradhi na magonjwa tofauti.  Na kama sote tunavyojua, mgonjwa huyapa matibabu yake kipaumbele zaidi kuliko kitu kingine chochote.  Itawezekana vipi akala chakula huku anateseka kwa maumivu yanayomchosha na kumtishia kifo!!

 

Kwa mantiki hii, tunaona kwamba ni wajibu kwa mume kugharamikia matibabu ya mkewe kama ilivyo wajibu kwa baba kugharamikia matibabu ya wanawe kwa mujibu wa ‘Ijmaa ya ‘Ulamaa.  Je, inaingia akilini mume astarehe na mkewe wakati akiwa mzima, kisha akiugua amrudishe kwao ili atibiwe na wazazi au ndugu zake?!  Atakuwa binadamu wa sampuli gani huyo!!  Itakuwa si uungwana wala mtangamano mwema, na pia itaua penzi la mke kwa mume kabisa na kuondosha imani yake kwake.

 

 

Share [9]

07-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: (ii) Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: Mavazi

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ

 

Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume

 

Alhidaaya.com [3]

 

 

 

 

06:  Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe:  3-Mavazi:  

 

‘Ulamaa kwa itifaki moja wamekubaliana kwamba ni wajibu kwa mume kumnunulia mavazi mkewe kutokana na Kauli Yake Ta’aalaa:

 

"وَعَلَى الْمَوْلُودِ لَهُ رِزْقُهُنَّ وَكِسْوَتُهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ"

 

“Na ni juu ya mzazi wa kiume kuwapatia chakula chao na nguo kwa mujibu wa ada”.  [Al-Baqarah: 233]

 

Na Hadiyth ya Jaabir (Radhwiya Allaah ‘anhu):

 

"اتَّقوا اللهَ في النِّسَاءِ، فإنَّهُنَّ عَوَانٍ عِنْدَكُمْ، أَخَذْتُمُوْهُنَّ بِأمَانةِ اللهِ، وَاسْتَحْلَلْتُمْ فُرُوْجَهُنَّ بِكَلِمَةِ اللهِ َوَلَهُنَّ عَلَيْكُمْ رِزْقُهُنَّ وكِسْوَتُهنَّ بِالمعْرُوْفِ"

 

“Mcheni Allaah katika kuamiliana na wanawake, kwani wao ni mateka walio mikononi mwenu, mmewachukua kwa Dhamana ya Allaah, mmehalalikiwa tupu zao kwa Neno la Allaah, nanyi ni wajibu wenu kuwalisha na kuwavisha kwa mujibu wa ada”.  [Hadiyth Swahiyh.  Muslim (1218)]

 

Mavazi ni jambo la kudumu, na kwa hivyo, ni lazima mume ampatie mkewe mavazi ya kutosha kuanzia mavazi ya ndani, ya kutokea, na ya minasaba kwa mujibu wa hali, na kwa mujibu wa urefu wake, ufupi wake, unene wake, wembamba wake na kadhalika.  Pia, yaendane na mazingira ya nchi waliyopo kama ni ya joto au baridi na kadhalika.

 

 

Share [10]

08-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: (ii) Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: Nyumba Ya Kuishi

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ

 

Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume

 

 

Alhidaaya.com [3]

 

 

07:  Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: 4-Nyumba Ya Kuishi:

 

Ni lazima mume ampatie mkewe nyumba ya kuishi au sehemu ya kukaa kwa ‘itifaki ya ‘Ulamaa kutokana na dalili zifuatazo:

 

1-  Kwa sababu Allaah Ta’alaa Amemwajibisha mume aliyemtaliki mkewe talaka rejea ampatie sehemu ya kukaa.  Hivyo basi, wakati wa uhai wa ndoa, nyumba ya kuishi mke ni wajibu zaidi kwa mume kumpatia mkewe.  Allaah Anasema:

 

"أَسْكِنُوهُنَّ مِنْ حَيْثُ سَكَنتُم مِّن وُجْدِكُمْ"

 

“Wawekeni wanawake (mliowataliki) kwenye majumba mnayokaa nyinyi kwa kadiri ya kipato chenu”.  [At-Twalaaq: 06]

 

2-  Allaah Ta’alaa Amewajibisha mtangamano mwema kati ya mke na mume kwa kusema:

 

"وَعَاشِرُوهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ"

 

“Na kaeni nao kwa wema”.  [An-Nisaa: 19]

 

Sehemu ya wema huo ulioamuriwa ni kumweka mahala ambapo patakuwa salama kwa yeye mwenyewe pamoja na mali yake.

 

3-  Mke ni lazima awe katika sehemu itakayomhifadhi asionekane na watu, aweze kustarehe na mumewe kwa faragha na kuhifadhi mali zake.  Hivyo ni lazima kwa mume ampatie sehemu kama hiyo.

 

Hadhi Ya Nyumba Kisharia:

 

Hadhi ya nyumba ya mke kisharia inategemea uwezo wa mume na hali ya mke kwa kipimo kimoja na matumizi, kwa kuwa vyote viwili ni haki iliyofungamana na ‘aqdi ya ndoa.  Pia ni kutokana na Kauli Yake Ta’aalaa:

 

"أَسْكِنُوهُنَّ مِنْ حَيْثُ سَكَنتُم مِّن وُجْدِكُمْ"

 

“Wawekeni wanawake (mliowataliki) kwenye majumba mnayokaa nyinyi kwa kadiri ya kipato chenu”.  [At-Twalaaq: 06]

 

Na Neno Lake vile vile:

 

"لِيُنفِقْ ذُو سَعَةٍ مِّن سَعَتِهِ ۖ وَمَن قُدِرَ عَلَيْهِ رِزْقُهُ فَلْيُنفِقْ مِمَّا آتَاهُ اللَّـهُ ۚ لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا مَا آتَاهَا ۚ"

 

“Ili mwenye wasaa agharimu kwa wasaa wake, na aliyebaniwa riziki yake, basi agharimie katika kile Alichompa Allaah. Allaah Haikalifishi nafsi yeyote ile isipokuwa kwa kile Alichoipa”.  [At-Twalaaq: 07]

 

Wajibu wa matumizi kwa mke ni kwa mujibu wa hali ya mume ya uwezo wa kifedha; wa juu, au wa wastani, au wa chini.  Na ndivyo hivyo hivyo kwa upande wa nyumba au makazi.  Hii ni kauli ya Jumhuwr.

 

Faida:

 

1-  Mke Kuishi Nyumba Moja Pamoja Na Jamaa Za Mume Wake.

 

Wanaokusudiwa hapa ni wazazi wawili wa mume na mtoto wa mume aliyezaa na mke mwingine.  Jumhuwr ya ‘Ulamaa wanaona kwamba haijuzu kuwachanganya wazazi wa mume au jamaa zake pamoja na mke ndani ya nyumba moja.  Ni haki ya mke kukataa kukaa na watu hao isipokuwa kama mwenyewe ataridhika na hilo, kwa kuwa nyumba ni haki yake, na mume ni lazima asimshirikishe na mwingine yeyote ndani yake, kwani ni mara nyingi huzuka matatizo kwa uwepo wa watu wengine mbali na kukosekana umahususi kati ya mke na mume.

 

Ama Wanachuoni wa Kimaalik, wao wametofautisha kati ya mke mwenye hadhi na mke wa hali duni.  Wamesema haifai kumweka mke mwenye hadhi pamoja na wazazi wa mume, lakini kwa mke duni wameruhusu isipokuwa tu kama kutakuwa na madhara kwake.

 

Ama kuishi nyumba moja na mtoto wa kiume wa mume aliyezaa na mke mwingine, ikiwa ni mkubwa anafahamu jimai, basi haitofaa kwa itifaki ya ‘Ulamaa, kwa kuwa uwepo wake utasababisha madhara.  Lakini kama ni mdogo haelewi chochote kuhusu jimai, basi kukaa naye kunajuzu, na mke hana haki ya kukataa kukaa naye.

 

2-  Jamaa Wa Mke Kuishi Pamoja Na Mume:

 

Mwanamke hana haki ya kumweka yeyote katika maharimu zake kwenye nyumba ya mumewe, na mume ana haki ya kukataa, isipokuwa kama ataridhia, hapo hakuna ubaya.

 

Ama mtoto wake aliyezaa na mume mwingine, haijuzu kwake kukaa naye bila ya ridhaa ya mume wake kwa mujibu wa kauli ya Jumhuwr. 

 

3-  Je, Wake Wenza Wanaweza Kuwekwa Nyumba Moja?

 

Fuqahaa wamekubaliana kwamba haijuzu kuwaweka nyumba moja wake wenza wawili na zaidi kwa kuwa kufanya hivyo si katika mtangamano mwema.  Hilo mara nyingi husababisha magomvi ambayo Allaah Amekataza.  Kadhalika, kila mmoja kati yao anaweza kusikia kishindo cha mume wakati anapomuingilia mwenzake au akashuhudia tendo lenyewe,  na hilo bila shaka huchemsha uadui na wivu kati yao.  Ni haki yenye nguvu kwao kukataa kuwekwa nyumba moja isipokuwa kama wenyewe wataridhia hilo, au ikawa hapana budi kutokana na sababu zisizokwepeka.

 

Ninasema:  “Asili ya kila mke kuwekwa kwenye nyumba yake inayojitegemea, ni kitendo cha Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kama Anavyosema Allaah Ta’aalaa:

 

"يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَدْخُلُوا بُيُوتَ النَّبِيِّ إِلَّا أَن يُؤْذَنَ لَكُمْ إِلَىٰ طَعَامٍ غَيْرَ نَاظِرِينَ إِنَاهُ"

 

“Enyi walioamini!  Msiingie nyumba za Nabiy isipokuwa mkipewa idhini ya kwenda kula si kungojea kiive”.  [Al-Ahzaab: 53]

 

Katika aayah hii, Allaah Ta’aalaa Ameziita nyumba na si nyumba moja.  Lakini kama wenyewe wataridhia kutokana na mazingira, basi hakuna ubaya, hiyo ni haki yao pia. Allaah Ndiye Mjuzi zaidi”.

 

Share [11]

09-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: (ii) Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: Kumfanyia Upole Mke, Kucheza Naye Na Kuchunga Udogo Wa Umri Wake

 

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ

 

Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume

 

 

Alhidaaya.com [3]

 

 

08:  Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: 5-Kumfanyia Upole Mke, Kucheza Naye Na Kuchunga Udogo Wa Umri Wake:

 

Kwa mambo haya, mume inabidi amwige Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye ndiye kiigizo chema kwetu.  Imepokelewa toka kwa ‘Aaishah:

 

"كَانَ الْحَبَشُ يَلْعَبُونَ، فَسَتَرَنِي رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَأَنَا أَنْظُرُ، فَمَا زِلْتُ أَنْظُرُ حَتَّى كُنْتُ أَنَا أَنْصَرِفُ، فَاقْدُرُوا قَدْرَ الْجَارِيَةِ الْحَدِيثَةِ السِّنِّ الحَرِيْصَةِ عَلَى اللَّهْوَ"

 

“Wahabeshi walikuwa wanacheza (kwa mikuki).  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akanikinga nisionekane huku nawaangalia.  Niliendelea kuwaangalia mpaka nikaamua mwenyewe kuondoka.  Basi pimeni haja ya msichana mdogo mwenye kupenda pumbao”.  [Al-Bukhaariy (5190) na Muslim (892)]

 

Tunamwona pia Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akishindana mbio na ‘Aaishah akimwambia:

 

"تعالِيْ أُسَابِقُكِ فتَسْبِقُهُ، ثُمَّ يُسَابِقُهَا بَعْدَ أَنْ بَدَنَتْ وَحمَلَتِ اللَّحْمَ فيَسْبِقُهَا وَيَضْحَكُ وَيَقُوْلُ: هذِه بِتِلْكَ "

 

“Njoo tushindane mbio, na ‘Aaishah akamshinda.  Kisha baada ya ‘Aaishah kunenepa na kupata mwili, alishindana naye, na (Rasuli) akamshinda na kucheka akimwambia:  Hii nimelipiza kwa ile”.  [Musnad ya Ahmad (6/264) kwa Sanad Swahiyh]

 

‘Aaishah amesema tena:

 

"كُنْتُ أَلْعَبُ بِالْبَنَاتِ عِنْدَ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَكَانَ لِي صَوَاحِبُ يَلْعَبْنَ مَعِي، فَكَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا دَخَلَ يَتَقَمَّعْنَ فيُسَرِّبُهُنَّ َإِلَيّ فَيَلْعَبْنَ مَعِيْ"

 

“Nilikuwa nacheza na vidoli kwa Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) pamoja na marafiki zangu.  Na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuwa anaingia, wao hujificha, na Rasuli anawatoa na kuwasukuma waje kwangu waendelee kucheza nami”.  [Al-Bukhaariy (6130) na Muslim (2440)]

                                                

 

Share [12]

10-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: (ii) Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: Akae Kuzungumza Na Mkewe Na Asikilize Mazungumzo Yake Kwa Hima

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

 

الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ

 

Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume

 

 

Alhidaaya.com [3]

 

 

 

09:  Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: 6-Akae Kuzungumza Na Mkewe Na Asikilize Mazungumzo Yake Kwa Hima:

 

Tunamwona Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anakaa kumsikiliza Mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhwiya Allaah ‘anhaa) akimhadithia mazungumzo ya wanawake 11 waliokuwa wamekaa na kupeana ahadi ya kwamba hakuna yeyote kati yao atakayeficha habari yoyote ya mumewe na maisha wanayoishi.  Mazungumzo haya yanajulikana kama kisa cha “Ummu Zar’i" ambacho ni kirefu.   Lakini pamoja na urefu wake, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakuchoka kumsikiliza ‘Aaishah akimhadithia visa vya wanawake hao 11 kuhusu waume zao mmoja baada ya mwingine hadi mwisho.

 

[Yaliyozungumzwa na wanawake hao kuhusu waume zao na hali wanayoishi nao, ndani yake kuna ahkaam za kisharia, adabu za unyumba, na mtangamano mwema wa mume kwa mkewe kwa mujibu wa Hadiyth hiyo ya ‘Aaishah ambayo tunasikitika kwamba hatukuifasiri kutokana na urefu wake].

 

 

Share [13]

11-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: (ii) Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: Amfundishe Mkewe Mambo Ya Dini Yake Na Amhimize Kuwajibika Na Kumtii Allaah

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ

 

Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume

 

 

Alhidaaya.com [3]

 

 

10:  Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: 7-Amfundishe Mkewe Mambo Ya Dini Yake Na Amhimize Kuwajibika Na Kumtii Allaah:

 

Kama ambavyo mume anatakiwa atangamane vyema na mkewe kwa kumfanyia upole kama ilivyotangulia, vile vile anatakiwa asichoke kumfundisha dini na kumhimiza kumtii Allaah Ta’aalaa.

 

Allaah Ta’aalaa Amesema:

 

"يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوا أَنفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَارًا وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ"

 

“Enyi walioamini!  Jikingeni nafsi zenu pamoja na ahli zenu na moto ambao kuni zake ni watu na mawe.”  [At-Tahriym:  06]

 

Imepokelewa toka kwa Ummu Salamah, amesema:

 

“Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliamka usiku mmoja akasema:

 

"سُبْحَانَ اللَّهِ مَاذَا أُنْزِلَ اللَّيْلَةَ مِنَ الْفِتَنِ؟ وَمَاذَا فُتِحَ مِنَ الْخَزَائِنِ؟ أَيْقِظُوا صَوَاحِبَ الْحُجَرِ، فَرُبَّ كَاسِيَةٍ فِي الدُّنْيَا عَارِيَةٍ فِي الْآخِرَة"

 

“Utakasifu ni Wake Allaah!  Ni fitna zilizoje zilizoteremshwa usiku!!  Na ukubwa ulioje wa hazina zilizofunguliwa!!  Waamsheni walio vyumbani (wakeze wapate kuswali).  Kwa hakika ni wengi wenye kuvaa duniani lakini aakhirah ni watupu”.  [Swahiyh Al-Bukhaariy (115)]

 

Toka kwa Abu Hurayrah, amesema:  “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

 

"رَحِمَ اللَّهُ رَجُلًا قَامَ مِنَ اللَّيْلِ فَصَلَّى وَأَيْقَظَ امْرَأَتَهُ فَصَلَّتْ فَإِنْ أَبَتْ نَضَحَ فِي وَجْهِهَا الْمَاءَ. رَحِمَ اللَّهُ امْرَأَةً قَامَتْ مِنَ اللَّيْلِ فَصَلَّتْ وَأَيْقَظَتْ زَوْجَهَا فَصَلَّى فَإِنْ أَبَى نَضَحَتْ فِي وَجْهِهِ المَاء"

 

“Allaah Amrehemu mwanaume aliyeamka usiku akaswali na akamwamsha mkewe naye akaswali.  Na kama atakataa (kwa uvivu), atamnyunyizia maji usoni (kumchangamsha aamke).  Allaah Amrehemu mwanamke aliyeamka usiku akaswali na akamwamsha mumewe naye akaswali.  Na kama atakataa (kwa uvivu), atamnyunyizia maji usoni (kumchangamsha aamke)”.  [Musnad Ahmad (2/250) kwa Sanad Hasan]

 

 

Share [14]

12-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: (ii) Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: Ayafumbie Macho Baadhi Ya Makosa Ya Mkewe Madhali Si Yenye Kukiuka Maagizo Ya Allaah

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ

 

Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume

 

 

Alhidaaya.com [3]

 

 

 

11:  Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: 8-Ayafumbie Macho Baadhi Ya Makosa Ya Mkewe Madhali Si Yenye Kukiuka Maagizo Ya Allaah:

 

 

Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametuongoza katika hili akituambia:

 

"لَا يَفْرَكْ مُؤْمِنٌ مُؤْمِنَةً إِنْ كَرِهَ مِنْهَا خُلُقًا رَضِيَ مِنْهَا آخَرَ"

 

“Muumini wa kiume (mume) asimbughudhikie Muumini mwanamke (mkewe).  Kama atachukizwa na baadhi ya tabia zake, basi zingine zitamfurahisha”.  [Swahiyh Muslim (1469)]

 

 

Share [15]

13-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: (ii) Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: Asimpige Akamjeruhi Usoni Au Kumwambia Ni Mbaya

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ

 

Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume

 

 

Alhidaaya.com [3]

 

 

12:  Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: 9-Asimpige Akamjeruhi Usoni Au Kumwambia Ni Mbaya:

 

 

Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

"وَلَا تَضْرِبِ اَلْوَجْهَ، وَلَا تُقَبِّحْ"

 

“Wala usipige uso, na wala usimkashifu (kumwambia) ni mbaya”.  [Hadiyth Hasan.  Imechakatwa na Abu Daawuwd (2142), Ibn Maajah (1850), Ahmad (4/447) na An-Nasaaiy katika (Al-‘Ishrah) (269)]

 

Na anasema tena Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam):

 

"لَا يَجْلِدْ أَحَدُكُمُ امْرَأَتَهُ جَلْدَ الْعَبْدِ ثُمَّ يُجَامِعْهَا فِي آخِرِ الْيَوْمِ"

 

“Asimpige mmoja wenu mkewe kama anavyompiga mtumwa wake, kisha tena aje amuingilie usiku (linawezekana kweli hilo!!)”.  [Al-Bukhaariy (4942) na Muslim (2855)]

 

Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakuwahi kamwe kumpiga yeyote katika wake zake wala mtu yeyote ila vitani.  ‘Aaishah amesema:

 

"ما رَأَيْتُ رسولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَضْرِبُ خادمًا لَه قَطّ ولا امرأةً، ولا ضربَ بيدِهِ شيئًا قَطّ إلَّا أَنْ يُجَاهِدَ في سَبيلِ اللهِ"

 

“Sikuwahi kumwona kamwe Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akimpiga mtumishi wake wala mwanamke, na hakupiga kwa mkono wake kamwe kitu chochote isipokuwa anapokuwa kwenye Jihaad ya Allaah”.  [Muslim (2328), At-Tirmidhiy katika Ash-Shamaail (331), An-Nasaaiy katika Al-‘Ishrah (281) na Ibn Maajah (1984)]

 

Faida:

 

Kumpiga mke ni jambo lililoruhusiwa kisharia ikiwa atakuwa mkorofi na akaacha kumsikiliza mumewe.  Na hili linakuwa kwa mtiririko wa hatua zilizoelezewa na Allaah Ta’aalaa katika Kauli Yake:

 

وَاللَّاتِي تَخَافُونَ نُشُوزَهُنَّ فَعِظُوهُنَّ وَاهْجُرُوهُنَّ فِي الْمَضَاجِعِ وَاضْرِبُوهُنَّ ۖ فَإِنْ أَطَعْنَكُمْ فَلَا تَبْغُوا عَلَيْهِنَّ سَبِيلًا ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيًّا كَبِيرًا "

 

“Na wale ambao mnakhofu uasi wao wa ndoa, basi wanasihini na wahameni katika malazi na wapigeni (kipigo kisichodhuru).  Wakikutiini, basi msitafute njia dhidi yao (ya kuwaudhi).  Hakika Allaah daima Ni Mwenye Uluwa, Mkubwa wa Dhati, Vitendo na Sifa”.  [An-Nisaa: 34]

 

Katika aayah hii, kupiga huko kuna vidhibiti vitatu:

 

1-  Kuje baada ya kufeli kumwonya na kumhama kitanda.

 

2-  Liwe pigo dogo la kuadabisha na si kubwa la kuvunja mfupa au saikolojia yake.

 

3-  Mume aache kumpiga kama atatii amri.

 

Share [16]

14-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: (ii) Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: Asimsuse Na Ikibidi Basi Yaishilie Ndani Ya Nyumba Tu

 

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ

 

Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume

 

 

Alhidaaya.com [3]

 

 

13:  Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe:  10-Asimsuse Na Ikibidi Basi Yaishilie Ndani Ya Nyumba Tu:

 

Ni kama ilivyoeleza Hadiyth iliyotangulia nyuma:

 

"وَلَا تَضْرِبِ اَلْوَجْهَ، وَلَا تُقَبِّحْ، ولا تَهْجُرْ إِلا في البَيْتِ"

 

“Wala usipige uso, wala usimkashifu (kumwambia) ni mbaya, wala usimhame isipokuwa ndani ya nyumba tu”.  [Hadiyth Hasan.  Imechakatwa na Abu Daawuwd (2142), Ibn Maajah (1850), Ahmad (4/447) na An-Nasaaiy katika (Al-‘Ishrah) (269)]

 

Lakini kama kuna maslaha ya kisharia ya kumhama na kumsusa nje ya nyumba, basi atafanya hivyo kama alivyowahama Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wakeze nje ya nyumba zao kwa muda wa mwezi mzima.

 

 

Share [17]

15-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: (ii) Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: Amshibishe Vizuri Tendo La Ndoa

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ

 

Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume

 

 

Alhidaaya.com [3]

 

 

14:  Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe:  11-Amshibishe Vizuri Tendo La Ndoa: 

 

Mume anatakiwa amtosheleze mkewe hamu yake ya jimai ili asije kuwazia kwenda nje kwenye haramu.  Na kwa ajili hiyo, Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwelekeza ‘Uthmaan bin Madh-’uwn kuhusu haki ya jimai anayopaswa kumtendea mkewe wakati alipojitenga naye kwa ajili ya swalah za usiku.  Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: 

 

"فَإِنَّ لأَهْلِكَ عَلَيْكَ حَقًّا"

 

“Na hakika mkeo ana haki juu yako (ya jimai)”.  [Al-Bukhaariy (1977) na Muslim (1159)]

 

Kumuingilia mke ni waajib kwa mume kwa kauli yenye nguvu ya ‘Ulamaa.  Ni madhehebu ya Abu Haniyfah na Ahmad.  Sheikh wa Uislamu ameukhitari mwelekeo huu na akauwekea mpaka wajibu wake.  Mpaka huo ni kiasi cha haja ya mke na kutosheka, na pia uwezo wa mume kwa namna isiyouchosha sana mwili akashindwa kufanya kazi.

 

Ama yaliyosemwa na Fuqahaa kwamba mpaka wa jimai ya waajib ni mara moja kila baada ya miezi minne, hayo hayazingatiwi, bali sahihi ni nguvu za mwanaume na kutosheka mwanamke.

 

Share [18]

16-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: (ii) Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: Amruhusu Kutoka Kama Atamwomba Ruksa Kwenda Kwenye Swalaah Ya Jamaa Au Kuwatembelea Jamaa Zake Nk Ikiwa Mazingira Yako Salama

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ

 

Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume

 

 

Alhidaaya.com [3]

 

 

15:  Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: 12-Amruhusu Kutoka Kama Atamwomba Ruksa Kwenda Kwenye Swalaah Ya Jamaa, Au Kuwatembelea Jamaa Zake Na Kadhalika Ikiwa Mazingira Yako Salama:

 

Ikiwa mazingira yako salama kutoka, basi ni vyema mume amruhusu.  Kutoka kwenda kwenye mambo hayo, kuna faida kubwa kwa mwanamke na hata kwa mumewe pia.

 

 

Share [19]

17-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: (ii) Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: Asieneze Siri Zake Au Kutaja Kasoro Zake

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

 

الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ

 

Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume

 

 

Alhidaaya.com [3]

 

16:  Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: 13-Asieneze Siri Zake Au Kutaja Kasoro Zake:

 

Kutaja siri za mke kwa watu wa nje ni haramu na hususan ikiwa siri zenyewe zinahusiana na maisha yao ya unyumba.  Na dhambi inakuwa kubwa zaidi ikiwa siri yenyewe inahusiana na tendo la jimai. 

 

Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

 "إِنَّ مِنْ أَشَرِّ النَّاسِ عِنْدَ اللَّهِ مَنْزِلَةً يَوْمَ الْقِيَامَةِ الرَّجُلَ يُفْضِي إِلَى امْرَأَتِهِ وَتُفْضِي إِلَيْهِ ثُمَّ يَنْشُرُ سِرَّهَا ‏"‏‏.‏

 

“Hakika miongoni mwa watu wenye hadhi mbaya zaidi mbele ya Allaah Siku ya Qiyaamah, ni mtu anayemvaa mkewe kimwili na mkewe akamvaa, kisha akaja kuelezea siri yake kwa watu”.  [Muslim (1437) na Abu Daawuwd (4870)]

 

 

Share [20]

18-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: (ii) Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: Mume Ajipambe Kwa Mkewe Kama Mkewe Anavyojipamba Kwa Ajili Yake

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ

 

Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume

 

 

Alhidaaya.com [3]

 

 

17: Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: 14-Mume Ajipambe Kwa Mkewe Kama Mkewe Anavyojipamba Kwa Ajili Yake:

 

Ibn ‘Abbaas amesema: 

 

"إني لأحِبُّ أَنْ أَتَزَيَّنَ لِلْمَرْأَةِ كَمَا أُحِبُّ أَنْ تَتَزَيَّنَ لِيْ، لأَنَّ اللهَ تعالى يَقُوْلُ":

 

“Mimi kwa hakika ninapenda kujipamba kwa mke wangu kama ninavyopenda yeye kujipamba kwa ajili yangu.  Kwa sababu Allaah Ta’aalaa Anasema:

 

"وَلَهُنَّ مِثْلُ الَّذِي عَلَيْهِنَّ بِالْمَعْرُوفِ"

 

“Nao wake wana haki kama ambayo (ya waume zao) iliyo juu yao kwa mujibu wa shariy’ah”.  [Al-Baqarah: 228]

 

 

Share [21]

19-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: (ii) Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: Amjengee Dhana Njema

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

 

الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ

 

Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume

 

Alhidaaya.com [3]

 

 

 

18: Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: 15-Amjengee Dhana Njema:

 

Allaah Ta’aalaa Amesema:

 

"لَّوْلَا إِذْ سَمِعْتُمُوهُ ظَنَّ الْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بِأَنفُسِهِمْ خَيْرًا"

“Kwa nini mlipoisikia (kashfa ya kusingiziwa), Waumini wanaume na Waumini wanawake wasiwadhanie wenzao khayr?”  [An-Nuwr: 12]

 

Na Amesema tena Allaah: 

 

"يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اجْتَنِبُوا كَثِيرًا مِّنَ الظَّنِّ إِنَّ بَعْضَ الظَّنِّ إِثْمٌ"

 

“Enyi walioamini!   Jiepusheni sana na dhana, kwani hakika baadhi ya dhana ni dhambi”.  [Al-Hujuraat: 12]

 

Na Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

 "إِذَا أَطَالَ أَحَدُكُمُ الْغَيْبَةَ فَلاَ يَطْرُقْ أَهْلَهُ لَيْلاً"

 

“Mmoja wenu akiwa mbali kwa muda mrefu, basi asimjie mkewe usiku”.   [Hadiyth Swahiyh.  Al-Bukhaariy (5244)]

 

Lakini, pamoja na dhana njema, mume anatakiwa awe chonjo, lakini pia azuie visababisho vya uharibifu na makosa ya kisharia. 

 

Wanaume toka ukoo wa Haashim walipoingia nyumbani kwa Asmaa bint ‘Umays (Radhwiya Allaah ‘anhaa) ambaye ni mke wa Abu Bakr, na Abu Bakr alipoingia akachukizwa na hilo, alikwenda kwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kumweleza hilo, lakini alimwambia:  “Sijaona lolote ila kheri”.  Na Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: 

 

"إِنَّ اللَّهَ قَدْ بَرَّأَهَا مِنْ ذَلِكَ"

 

“Hakika Allaah Amemtakasa kutokana na hayo (uchafu)”.  Kisha akasimama juu ya mimbari akasema:

 

"لاَ يَدْخُلَنَّ رَجُلٌ بَعْدَ يَوْمِي هَذَا عَلَى مُغِيبَةٍ إِلاَّ وَمَعَهُ رَجُلٌ أَوِ اثْنَانِ"

 

“Baada ya leo hii, asiingie mtu yeyote kwenye nyumba ya mwingine naye hayuko, ila akiwa pamoja naye mtu mmoja au wawili”.  [Hadiyth Swahiyh.  Muslim (2173)]

 

Ushahidi hapa ni kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimkanushia Asmaa uovu na akamwekea dhana njema, lakini pamoja na hivyo, aliwawekea wanaume marufuku ya kuingia nyumba za wengine wakati wao hawako ila wakiwa wamesuhubiana na mtu mwingine ili kutomruhusu shaytwaan kuvuruga mambo.

 

 

Share [22]

20-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: (ii) Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: Afanye Usawa Kati Yake Na Wake Wenza Wenzake Katika Chakula, Vinywaji, Mavazi Na Malazi

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

 

الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ

 

Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume

 

 

Alhidaaya.com [3]

 

 

19:  Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: 16-Afanye Usawa Kati Yake Na Wake Wenza Wenzake Katika Chakula, Vinywaji, Mavazi Na Malazi:

 

Kutenda usawa kati ya wake ni jambo la waajib katika chakula, mavazi, nyumba na zamu za kulala.  Ama penzi, hilo liko nje ya uwezo wa kibinadamu, halidhibitiki.

 

 

 

Share [23]

21-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: (ii) Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: Haki Za Pamoja Kati Ya Mke Na Mume

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

 

الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ

 

Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume

 

 

Alhidaaya.com [3]

 

 

 

 

20:  Haki Za Pamoja Kati Ya Mke Na Mume:

 

1-  Kustarehe kila mmoja na mwenzake:

 

Hili linafanyika baada ya ‘aqdi kufungwa na masharti yakatimia ikiwa ni pamoja na mke kukabidhiwa kwa mumewe, kupatiwa mahala pa kukaa na kupatiwa matumizi.  Kadhalika, kukosekana vizuizi kama kuhirimia na kadhalika.  Yakitimu haya, basi kila mmoja ana haki ya kustarehe na mwenzake kwa mujibu wa maelekezo ya kisharia yaliyoelezewa nyuma.

 

2-  Kurithiana:

 

Baada tu ya kufungwa ‘aqdi, basi haki ya kurithiana inathibiti kati yao akifa mmoja wao.

 

3-  Kutangamana na kuamiliana kwa wema kama ilivyobainishwa nyuma.

 

4-  Uharamu wa ukwe unathibiti kama ilivyobainishwa kwenye mlango wa wanawake walioharamishwa kwa sababu ya ukwe.

 

 

Share [24]
www.alhidaaya.com

Source URL: https://www.alhidaaya.com/sw/node/12031

Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/284
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12031&title=10H%28ii%29-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20%D9%83%D8%AA%D8%A7%D8%A8%20%D8%A7%D9%84%D8%B2%D9%88%D8%A7%D8%AC%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20%D8%A7%D9%84%D8%AD%D9%8F%D9%82%D9%8F%D9%88%D9%92%D9%82%D9%8F%20%D8%A8%D9%8E%D9%8A%D9%92%D9%86%D9%8E%20%D8%A7%D9%84%D8%B2%D9%91%D9%8E%D9%88%D9%92%D8%AC%D9%8E%D9%8A%D9%92%D9%86%D9%90%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20%28ii%29%20Haki%20Zinazompasa%20Mume%20Kumtendea%20Mkewe
[3] http://www.alhidaaya.com/
[4] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12032&title=01-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20%28ii%29%20Haki%20Zinazompasa%20Mume%20Kumtendea%20Mkewe%3A%20Utangulizi%3A
[5] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12033&title=02-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20%28ii%29%20Haki%20Zinazompasa%20Mume%20Kumtendea%20Mkewe%3A%20Atangamane%20Naye%20Kwa%20Wema%3A
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12034&title=03-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20%28ii%29%20Haki%20Zinazompasa%20Mume%20Kumtendea%20Mkewe%3A%20Matumizi%3A%20Maana%20Ya%20Matumizi%20
[7] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12035&title=04-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20%28ii%29%20Haki%20Zinazompasa%20Mume%20Kumtendea%20Mkewe%3A%20Matumizi%3A%20Masharti%20Ya%20Matumizi%20Kuwa%20Wajibu%20
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12036&title=05-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20%28ii%29%20Haki%20Zinazompasa%20Mume%20Kumtendea%20Mkewe%3A%20Matumizi%3A%20Makadirio%20Ya%20Matumizi%20Kwa%20Mke%20
[9] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12037&title=06-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20%28ii%29%20Haki%20Zinazompasa%20Mume%20Kumtendea%20Mkewe%3A%20Matumizi%3A%20Je%2C%20Mume%20Anabeba%20Gharama%20Za%20Matibabu%20Ya%20Mke%3F
[10] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12038&title=07-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20%28ii%29%20Haki%20Zinazompasa%20Mume%20Kumtendea%20Mkewe%3A%20Mavazi
[11] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12039&title=08-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20%28ii%29%20Haki%20Zinazompasa%20Mume%20Kumtendea%20Mkewe%3A%20Nyumba%20Ya%20Kuishi
[12] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12040&title=09-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20%28ii%29%20Haki%20Zinazompasa%20Mume%20Kumtendea%20Mkewe%3A%20Kumfanyia%20Upole%20Mke%2C%20Kucheza%20Naye%20Na%20Kuchunga%20Udogo%20Wa%20Umri%20Wake
[13] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12041&title=10-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20%28ii%29%20Haki%20Zinazompasa%20Mume%20Kumtendea%20Mkewe%3A%20Akae%20Kuzungumza%20Na%20Mkewe%20Na%20Asikilize%20Mazungumzo%20Yake%20Kwa%20Hima
[14] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12042&title=11-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20%28ii%29%20Haki%20Zinazompasa%20Mume%20Kumtendea%20Mkewe%3A%20Amfundishe%20Mkewe%20Mambo%20Ya%20Dini%20Yake%20Na%20Amhimize%20Kuwajibika%20Na%20Kumtii%20Allaah%20
[15] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12043&title=12-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20%28ii%29%20Haki%20Zinazompasa%20Mume%20Kumtendea%20Mkewe%3A%20Ayafumbie%20Macho%20Baadhi%20Ya%20Makosa%20Ya%20Mkewe%20Madhali%20Si%20Yenye%20Kukiuka%20Maagizo%20Ya%20Allaah
[16] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12044&title=13-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20%28ii%29%20Haki%20Zinazompasa%20Mume%20Kumtendea%20Mkewe%3A%20Asimpige%20Akamjeruhi%20Usoni%20Au%20Kumwambia%20Ni%20Mbaya
[17] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12045&title=14-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20%28ii%29%20Haki%20Zinazompasa%20Mume%20Kumtendea%20Mkewe%3A%20Asimsuse%20Na%20Ikibidi%20Basi%20Yaishilie%20Ndani%20Ya%20Nyumba%20Tu
[18] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12046&title=15-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20%28ii%29%20Haki%20Zinazompasa%20Mume%20Kumtendea%20Mkewe%3A%20Amshibishe%20Vizuri%20Tendo%20La%20Ndoa%20
[19] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12047&title=16-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20%28ii%29%20Haki%20Zinazompasa%20Mume%20Kumtendea%20Mkewe%3A%20Amruhusu%20Kutoka%20Kama%20Atamwomba%20Ruksa%20Kwenda%20Kwenye%20Swalaah%20Ya%20Jamaa%20Au%20Kuwatembelea%20Jamaa%20Zake%20Nk%20Ikiwa%20Mazingira%20Yako%20Salama%20
[20] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12048&title=17-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20%28ii%29%20Haki%20Zinazompasa%20Mume%20Kumtendea%20Mkewe%3A%20Asieneze%20Siri%20Zake%20Au%20Kutaja%20Kasoro%20Zake
[21] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12049&title=18-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20%28ii%29%20Haki%20Zinazompasa%20Mume%20Kumtendea%20Mkewe%3A%20Mume%20Ajipambe%20Kwa%20Mkewe%20Kama%20Mkewe%20Anavyojipamba%20Kwa%20Ajili%20Yake
[22] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12050&title=19-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20%28ii%29%20Haki%20Zinazompasa%20Mume%20Kumtendea%20Mkewe%3A%20Amjengee%20Dhana%20Njema
[23] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12051&title=20-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20%28ii%29%20Haki%20Zinazompasa%20Mume%20Kumtendea%20Mkewe%3A%20Afanye%20Usawa%20Kati%20Yake%20Na%20Wake%20Wenza%20Wenzake%20Katika%20Chakula%2C%20Vinywaji%2C%20Mavazi%20Na%20Malazi
[24] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12052&title=21-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20%28ii%29%20Haki%20Zinazompasa%20Mume%20Kumtendea%20Mkewe%3A%20Haki%20Za%20Pamoja%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume