Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ
Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume
Alhidaaya.com [1]
01: Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: 1-Atangamane Naye Kwa Wema:
Hii inajumuisha kuishi naye kwa wema, kumlinda na madhara, kumfurahikia, kumkunjukia na kumhisisha uhuru ndani ya wigo wa maisha yao ya ndoa. Na hii ni kutokana na Kauli Yake Ta’aalaa:
"وَعَاشِرُوهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ"
“Na kaeni nao kwa wema”. [An-Nisaa: 19]
Na Kauli Yake Ta’aalaa:
"وَلَهُنَّ مِثْلُ الَّذِي عَلَيْهِنَّ بِالْمَعْرُوفِ"
“Nao wake wana haki kama ambayo (ya waume zao) iliyo juu yao kwa mujibu wa shariy’ah”. [Al-Baqarah: 228]
Na Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"خَيْرُكُمْ خَيْرُكُمْ لِأَهْلِهِ وَأَنَا خَيْرُكُمْ لِأَهْلِي"
“Mbora wenu zaidi ni yule aliye mwema zaidi kwa mkewe, na mimi ndiye mwema zaidi kuliko nyinyi kwa wake zangu”. [Hadiyth Swahiyh. At-Tirmidhiy (3892), na Ibn Hibaan (1312)]
Mtangamano mwema ni neno jumuishi ambalo haki zote zinaingia ndani yake. Haki zinazofuatia ni sehemu tu ya mtangamano huo, nasi tunazitaja moja baada ya nyingine ili wanaume wazizingatie kwa uangalifu zaidi.
Links
[1] http://www.alhidaaya.com/
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12033&title=02-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20%28ii%29%20Haki%20Zinazompasa%20Mume%20Kumtendea%20Mkewe%3A%20Atangamane%20Naye%20Kwa%20Wema%3A