Alhidaaya.com
Published on Alhidaaya.com (https://www.alhidaaya.com/sw)

Ukurasa Wa Kwanza > 10H(ii)-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: كتاب الزواج Kitabu Cha Ndoa: الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: (ii) Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe > 03-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: (ii) Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: Matumizi: Maana Ya Matumizi

03-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: (ii) Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: Matumizi: Maana Ya Matumizi

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ

 

Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume

 

Alhidaaya.com [1]

 

 

 

02: Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: 2-Matumizi: (a) Maana Ya Matumizi:

 

Makusudio ya matumizi hapa ni gharama anazozitoa mume kwa mkewe na wanawe kwa ajili ya chakula, mavazi, sehemu ya kuishi na mfano wa hayo.  Matumizi haya ambayo mume anayatoa ni lazima kwake kwa mujibu wa Qur-aan, Sunnah, ‘Ijmaa na kiakili.

 

Kwenye Qur-aan, ni:

 

1-Kauli Yake Ta’aalaa:

 

"لِيُنفِقْ ذُو سَعَةٍ مِّن سَعَتِهِ ۖ وَمَن قُدِرَ عَلَيْهِ رِزْقُهُ فَلْيُنفِقْ مِمَّا آتَاهُ اللَّـهُ ۚ لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا مَا آتَاهَا ۚ سَيَجْعَلُ اللَّـهُ بَعْدَ عُسْرٍ يُسْرًا"

 

“Ili mwenye wasaa agharimu kwa wasaa wake, na aliyebaniwa riziki yake, basi agharimie katika kile Alichompa Allaah.  Allaah Haikalifishi nafsi yeyote ile isipokuwa kwa kile Alichoipa.  Allaah Atajaalia baada ya ugumu kuwa wepesi”.  [At-Twalaaq: 07]

 

2-  Na Kauli Yake Ta’aalaa:

 

 

"وَعَلَى الْمَوْلُودِ لَهُ رِزْقُهُنَّ وَكِسْوَتُهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ"

 

“Na ni juu ya mzazi wa kiume kuwapatia chakula chao na nguo kwa mujibu wa ada”.  [Al-Baqarah: 233]

 

Ibn Kathiyr (Rahimahul Laah) amesema:  “Ni juu ya baba wa mtoto kutoa matumizi kwa mama mtoto na mavazi kwa mujibu wa ada na mazingira, bila kufuja wala kubana kwa mujibu wa uwezo wa baba mtoto”.

 

Ama Sunnah, ni Hadiyth hizi:

 

1-  Hadiyth ya Jaabir akielezea Hijja ya Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambapo Rasuli alisema:

 

"اتَّقوا اللهَ في النِّسَاءِ، فإنَّهُنَّ عَوَانٍ عِنْدَكُمْ، أَخَذْتُمُوْهُنَّ بِأمَانةِ اللهِ، وَاسْتَحْلَلْتُمْ فُرُوْجَهُنَّ بِكَلِمَةِ الله، َوَلَهُنَّ عَلَيْكُمْ رِزْقُهُنَّ وكِسْوَتُهنَّ بِالمعْرُوْفِ"

 

“Mcheni Allaah katika kuamiliana kwenu na wanawake, kwani wao ni mateka walio mikononi mwenu, mmewachukua kwa Dhamana ya Allaah, mmehalalikiwa tupu zao kwa Neno la Allaah, nanyi ni wajibu wenu kuwalisha na kuwavisha kwa mujibu wa ada”.  [Hadiyth Swahiyh.  Muslim (1218)]

 

2-  Hadiyth ya Mu’aawiyah Al-Qushayriy (Radhwiya Allaah ‘anhu), amesema:

 

"قُلْتُ: يَا رَسُولَ اَللَّهِ! مَا حَقُّ زَوْجَةِ أَحَدِنَا عَلَيْهِ? قَالَ: "أَنْ تُطْعِمَهَا إِذَا طَعِمْتَ، وَتَكْسُوَهَا إِذَا اِكْتَسَيْتَ، وَلَا تَضْرِبِ اَلْوَجْهَ، وَلَا تُقَبِّحْ، ولا تَهْجُرْ إِلا في البَيْتِ"

“Nilisema:  Ee Rasuli wa Allaah!  Ni zipi haki ambazo mmoja wetu anapaswa kumfanyia mkewe?  Akasema:  Mlishe sawa na unachokula, mvishe kiwango sawa na unachovaa, wala usimpige usoni, wala usimkashifu kumwambia ni mbaya, wala usimsuse isipokuwa ndani ya nyumba tu”.  [Hadiyth Hasan.  Imechakatwa na Abu Daawuwd (2142), Ibn Maajah (1850), Ahmad (4/447) na An-Nasaaiy katika (Al-‘Ish-rah) (269)]

 

3-  Hadiyth ya ‘Aaishah (Radhwiya Allaah ‘anhaa) kwamba Hind bint ‘Utbah alimwambia Rasuli:

 

"يا رَسُولَ اللهِ! ِإِنَّ أَبَا سُفْيَانَ رَجُلٌ شَحِيحٌ، لا يُعْطِيْني مَا يَكْفِيْني وَوَلَدِي إلَّا مَا أَخَذْتُ مِنْ مَالِهِ وَهوَ لا يعلَمُ.‏ قَالَ: خُذِي مَا يَكْفِيكِ وَوَلَدَكِ بِالْمَعْرُوفِ"‏‏.‏

“Ee Rasuli wa Allaah!  Hakika Abu Sufyaan ni mtu bahili, na hanipi chochote wala watoto wangu isipokuwa kile ninachochukua katika pesa zake bila yeye kujua.  Akamwambia:  Chukua kinachokutosha wewe na wanao kwa mujibu wa mahitaji”.  [Hadiyth Swahiyh.  Imechakatwa na Al-Bukhaariy (5364) na Muslim (1714)]

 

Ama ‘Ijmaa, ni kwamba ‘Ulamaa wengi wamekubaliana kwa sauti moja kwamba ni lazima mume amkidhie mkewe matumizi -yote kama mume amebaleghe- ila tu kama mke atakuwa mwasi.

 

Na ama kiakili, ni kwamba mke huwa amefungika chini ya mamlaka ya mume ambaye humzuia asifanye atakalo au kuhangaikia maisha ili abakie na jukumu la kumtekelezea haki zake stahiki, na kwa ajili hiyo, ni lazima mume huyu amgharamikie matumizi yote ya lazima.

 

 

Share [2]
www.alhidaaya.com

Source URL: https://www.alhidaaya.com/sw/node/12034

Links
[1] http://www.alhidaaya.com/
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12034&title=03-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20%28ii%29%20Haki%20Zinazompasa%20Mume%20Kumtendea%20Mkewe%3A%20Matumizi%3A%20Maana%20Ya%20Matumizi%20