Alhidaaya.com
Published on Alhidaaya.com (https://www.alhidaaya.com/sw)

Ukurasa Wa Kwanza > 10H(ii)-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: كتاب الزواج Kitabu Cha Ndoa: الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: (ii) Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe > 06-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: (ii) Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: Matumizi: Je, Mume Anabeba Gharama Za Matibabu Ya Mke?

06-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume: (ii) Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: Matumizi: Je, Mume Anabeba Gharama Za Matibabu Ya Mke?

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ

 

Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume

 

Alhidaaya.com [1]

 

 

 

05: Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: Matumizi: (d) Je, Mume Anabeba Gharama Za Matibabu Ya Mke?

 

Madhehebu ya Maimamu wanne yanasema kwamba si wajibu kwa mume kugharamikia matibabu ya mkewe na kumuuguza!!  Lakini inavyoonekana ni kwamba msingi wa kauli yao hii ni kuwa huko nyuma zamani, kuuguza na kutibu halikuwa ni katika mambo ya kimsingi katika maisha ya watu, na halikuwa likihitajika kwa kiasi kikubwa, kwa kuwa zaidi kulikuwa na tiba za kijadi zisizo na gharama kubwa kama ilivyo leo. 

 

Lakini hivi leo, hitajio la matibabu limekuwa kama hitajio la chakula, bali limekuwa muhimu hata zaidi ya chakula, na hasa pia uwepo wa ongezeko kubwa la maradhi na magonjwa tofauti.  Na kama sote tunavyojua, mgonjwa huyapa matibabu yake kipaumbele zaidi kuliko kitu kingine chochote.  Itawezekana vipi akala chakula huku anateseka kwa maumivu yanayomchosha na kumtishia kifo!!

 

Kwa mantiki hii, tunaona kwamba ni wajibu kwa mume kugharamikia matibabu ya mkewe kama ilivyo wajibu kwa baba kugharamikia matibabu ya wanawe kwa mujibu wa ‘Ijmaa ya ‘Ulamaa.  Je, inaingia akilini mume astarehe na mkewe wakati akiwa mzima, kisha akiugua amrudishe kwao ili atibiwe na wazazi au ndugu zake?!  Atakuwa binadamu wa sampuli gani huyo!!  Itakuwa si uungwana wala mtangamano mwema, na pia itaua penzi la mke kwa mume kabisa na kuondosha imani yake kwake.

 

 

Share [2]
www.alhidaaya.com

Source URL: https://www.alhidaaya.com/sw/node/12037

Links
[1] http://www.alhidaaya.com/
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12037&title=06-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20%28ii%29%20Haki%20Zinazompasa%20Mume%20Kumtendea%20Mkewe%3A%20Matumizi%3A%20Je%2C%20Mume%20Anabeba%20Gharama%20Za%20Matibabu%20Ya%20Mke%3F