Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ
Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume
Alhidaaya.com [1]
08: Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: 5-Kumfanyia Upole Mke, Kucheza Naye Na Kuchunga Udogo Wa Umri Wake:
Kwa mambo haya, mume inabidi amwige Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye ndiye kiigizo chema kwetu. Imepokelewa toka kwa ‘Aaishah:
"كَانَ الْحَبَشُ يَلْعَبُونَ، فَسَتَرَنِي رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَأَنَا أَنْظُرُ، فَمَا زِلْتُ أَنْظُرُ حَتَّى كُنْتُ أَنَا أَنْصَرِفُ، فَاقْدُرُوا قَدْرَ الْجَارِيَةِ الْحَدِيثَةِ السِّنِّ الحَرِيْصَةِ عَلَى اللَّهْوَ"
“Wahabeshi walikuwa wanacheza (kwa mikuki). Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akanikinga nisionekane huku nawaangalia. Niliendelea kuwaangalia mpaka nikaamua mwenyewe kuondoka. Basi pimeni haja ya msichana mdogo mwenye kupenda pumbao”. [Al-Bukhaariy (5190) na Muslim (892)]
Tunamwona pia Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akishindana mbio na ‘Aaishah akimwambia:
"تعالِيْ أُسَابِقُكِ فتَسْبِقُهُ، ثُمَّ يُسَابِقُهَا بَعْدَ أَنْ بَدَنَتْ وَحمَلَتِ اللَّحْمَ فيَسْبِقُهَا وَيَضْحَكُ وَيَقُوْلُ: هذِه بِتِلْكَ "
“Njoo tushindane mbio, na ‘Aaishah akamshinda. Kisha baada ya ‘Aaishah kunenepa na kupata mwili, alishindana naye, na (Rasuli) akamshinda na kucheka akimwambia: Hii nimelipiza kwa ile”. [Musnad ya Ahmad (6/264) kwa Sanad Swahiyh]
‘Aaishah amesema tena:
"كُنْتُ أَلْعَبُ بِالْبَنَاتِ عِنْدَ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَكَانَ لِي صَوَاحِبُ يَلْعَبْنَ مَعِي، فَكَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا دَخَلَ يَتَقَمَّعْنَ فيُسَرِّبُهُنَّ َإِلَيّ فَيَلْعَبْنَ مَعِيْ"
“Nilikuwa nacheza na vidoli kwa Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) pamoja na marafiki zangu. Na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuwa anaingia, wao hujificha, na Rasuli anawatoa na kuwasukuma waje kwangu waendelee kucheza nami”. [Al-Bukhaariy (6130) na Muslim (2440)]
Links
[1] http://www.alhidaaya.com/
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12040&title=09-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20%28ii%29%20Haki%20Zinazompasa%20Mume%20Kumtendea%20Mkewe%3A%20Kumfanyia%20Upole%20Mke%2C%20Kucheza%20Naye%20Na%20Kuchunga%20Udogo%20Wa%20Umri%20Wake