Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ
Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume
Alhidaaya.com [1]
10: Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: 7-Amfundishe Mkewe Mambo Ya Dini Yake Na Amhimize Kuwajibika Na Kumtii Allaah:
Kama ambavyo mume anatakiwa atangamane vyema na mkewe kwa kumfanyia upole kama ilivyotangulia, vile vile anatakiwa asichoke kumfundisha dini na kumhimiza kumtii Allaah Ta’aalaa.
Allaah Ta’aalaa Amesema:
"يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوا أَنفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَارًا وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ"
“Enyi walioamini! Jikingeni nafsi zenu pamoja na ahli zenu na moto ambao kuni zake ni watu na mawe.” [At-Tahriym: 06]
Imepokelewa toka kwa Ummu Salamah, amesema:
“Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliamka usiku mmoja akasema:
"سُبْحَانَ اللَّهِ مَاذَا أُنْزِلَ اللَّيْلَةَ مِنَ الْفِتَنِ؟ وَمَاذَا فُتِحَ مِنَ الْخَزَائِنِ؟ أَيْقِظُوا صَوَاحِبَ الْحُجَرِ، فَرُبَّ كَاسِيَةٍ فِي الدُّنْيَا عَارِيَةٍ فِي الْآخِرَة"
“Utakasifu ni Wake Allaah! Ni fitna zilizoje zilizoteremshwa usiku!! Na ukubwa ulioje wa hazina zilizofunguliwa!! Waamsheni walio vyumbani (wakeze wapate kuswali). Kwa hakika ni wengi wenye kuvaa duniani lakini aakhirah ni watupu”. [Swahiyh Al-Bukhaariy (115)]
Toka kwa Abu Hurayrah, amesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"رَحِمَ اللَّهُ رَجُلًا قَامَ مِنَ اللَّيْلِ فَصَلَّى وَأَيْقَظَ امْرَأَتَهُ فَصَلَّتْ فَإِنْ أَبَتْ نَضَحَ فِي وَجْهِهَا الْمَاءَ. رَحِمَ اللَّهُ امْرَأَةً قَامَتْ مِنَ اللَّيْلِ فَصَلَّتْ وَأَيْقَظَتْ زَوْجَهَا فَصَلَّى فَإِنْ أَبَى نَضَحَتْ فِي وَجْهِهِ المَاء"
“Allaah Amrehemu mwanaume aliyeamka usiku akaswali na akamwamsha mkewe naye akaswali. Na kama atakataa (kwa uvivu), atamnyunyizia maji usoni (kumchangamsha aamke). Allaah Amrehemu mwanamke aliyeamka usiku akaswali na akamwamsha mumewe naye akaswali. Na kama atakataa (kwa uvivu), atamnyunyizia maji usoni (kumchangamsha aamke)”. [Musnad Ahmad (2/250) kwa Sanad Hasan]
Links
[1] http://www.alhidaaya.com/
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12042&title=11-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20%28ii%29%20Haki%20Zinazompasa%20Mume%20Kumtendea%20Mkewe%3A%20Amfundishe%20Mkewe%20Mambo%20Ya%20Dini%20Yake%20Na%20Amhimize%20Kuwajibika%20Na%20Kumtii%20Allaah%20