Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
الحُقُوْقُ بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ
Haki Za Kutendeana Kati Ya Mke Na Mume
Alhidaaya.com [1]
14: Haki Zinazompasa Mume Kumtendea Mkewe: 11-Amshibishe Vizuri Tendo La Ndoa:
Mume anatakiwa amtosheleze mkewe hamu yake ya jimai ili asije kuwazia kwenda nje kwenye haramu. Na kwa ajili hiyo, Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwelekeza ‘Uthmaan bin Madh-’uwn kuhusu haki ya jimai anayopaswa kumtendea mkewe wakati alipojitenga naye kwa ajili ya swalah za usiku. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia:
"فَإِنَّ لأَهْلِكَ عَلَيْكَ حَقًّا"
“Na hakika mkeo ana haki juu yako (ya jimai)”. [Al-Bukhaariy (1977) na Muslim (1159)]
Kumuingilia mke ni waajib kwa mume kwa kauli yenye nguvu ya ‘Ulamaa. Ni madhehebu ya Abu Haniyfah na Ahmad. Sheikh wa Uislamu ameukhitari mwelekeo huu na akauwekea mpaka wajibu wake. Mpaka huo ni kiasi cha haja ya mke na kutosheka, na pia uwezo wa mume kwa namna isiyouchosha sana mwili akashindwa kufanya kazi.
Ama yaliyosemwa na Fuqahaa kwamba mpaka wa jimai ya waajib ni mara moja kila baada ya miezi minne, hayo hayazingatiwi, bali sahihi ni nguvu za mwanaume na kutosheka mwanamke.
Links
[1] http://www.alhidaaya.com/
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12046&title=15-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Haki%20Za%20Kutendeana%20Kati%20Ya%20Mke%20Na%20Mume%3A%20%28ii%29%20Haki%20Zinazompasa%20Mume%20Kumtendea%20Mkewe%3A%20Amshibishe%20Vizuri%20Tendo%20La%20Ndoa%20