كتاب الزواج
Kitabu Cha Ndoa
تَعَدُّدِ الزَّوْجّاتِ
Mke Zaidi Ya Mmoja
Abu Maalik Kamaal Bin As-Sayyid Saalim
Imetarjumiwa na 'Abdullaah Mu'aawiyah (Abu Baasim)
Alhidaaya.com
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
تَعَدُّدِ الزَّوْجّاتِ
Mke Zaidi Ya Mmoja
Alhidaaya.com [3]
01: Uhalali Wake:
Allaah Ta’aalaa Amesema:
"وَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تُقْسِطُوا فِي الْيَتَامَىٰ فَانكِحُوا مَا طَابَ لَكُم مِّنَ النِّسَاءِ مَثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ ۖ فَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تَعْدِلُوا فَوَاحِدَةً أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۚ ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَلَّا تَعُولُوا "
“Na mkikhofu kuwa hamtoweza kufanya uadilifu kwa mayatima, basi oeni waliokupendezeni katika wanawake wengine; wawili au watatu au wanne. Lakini mkikhofu kuwa hamtoweza kufanya uadilifu, basi mmoja tu, au ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki. Hivyo ni karibu zaidi kwamba hamtoelemea kudhulumu”. [An-Nisaa: 03].
Katika aayah hii, Allaah Ta’alaa Anawasemesha wasimamizi wa mayatima. Anawaambia: “Ikiwa binti yatima yuko chini ya ulezi na usimamizi wa mmoja wenu (naye akataka kumwoa), na akahofia kwamba hatompa mahari stahiki, basi ni vyema asimwoe, bali atafute mwanamke mwingine, kwani wanawake wa kuoa wako wengi tu. Na Allaah Hakumbana, bali Amemhalalishia kuoa kuanzia mmoja hadi wanne. Lakini ikiwa atakhofia kwamba hatoweza kuwatendea haki, basi ni lazima atosheke na mmoja tu, au vikajazi anaowamiliki”. [Hivi ndivyo alivyoifasiri aayah hii bibi ‘Aaishah (Radhwiya Allaah ‘anhaa) kama ilivyo kwenye Al-Bukhaariy (4576)]
Nyuma zimetajwa dalili nyingi zinazohimizia kuoa ili kuongeza kizazi na watoto. Sa’iyd bin Jubayr anasema:
"قَالَ لِي ابْنُ عَبَّاسٍ: هَلْ تَزَوَّجْتَ؟ قُلْتُ: لاَ. قَالَ: فَتَزَوَّجْ، فَإِنَّ خَيْرَ هَذِهِ الأُمَّةِ أَكْثَرُهَا نِسَاءً".
“Ibn ‘Abbaas aliniuliza: Je, umeoa? Nikamwambia: Hapana. Akaniambia: Oa, kwani mbora zaidi wa umma huu (Rasuli) ndiye aliye na wake wengi zaidi”. [Al-Bukhaariy (5069)]
Dalili hizi na nyinginezo, zinathibitisha kupendeza mwanaume wa Kiislamu kuoa zaidi ya mke mmoja, lakini kwa kuchunga masharti na vidhibiti maalum.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
تَعَدُّدِ الزَّوْجّاتِ
Mke Zaidi Ya Mmoja
Alhidaaya.com [3]
02: Masharti Ya Kuoa Mke Zaidi Ya Mmoja:
1- Awe mtu na uwezo wa kufanya uadilifu kati yao.
Ni kutokana na Kauli Yake Ta’aalaa:
"فَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تَعْدِلُوا فَوَاحِدَةً"
“Lakini mkikhofu kuwa hamtoweza kufanya uadilifu, basi mmoja tu”. [An-Nisaa: 03].
2- Ajijengee kinga ya kumlinda asije kufitinika akapoteza Haki za Allaah kwa sababu yao.
Ni kwa Kauli Yake Ta’aalaa:
"يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ مِنْ أَزْوَاجِكُمْ وَأَوْلَادِكُمْ عَدُوًّا لَّكُمْ فَاحْذَرُوهُمْ"
“Enyi walioamini! Hakika miongoni mwa wake zenu na watoto wenu ni maadui kwenu, basi tahadharini nao”. [At-Taghaabun: 14]
3- Awe na uwezo wa kuwatosheleza kimwili na kimahitaji.
Na hii ni ili wasivutike kwenda kwenye yaliyoharamishwa na machafu, kwani Allaah Hapendi mambo kama hayo. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"يَا مَعْشَرَ الشَّبَابِ، مَنِ اسْتَطَاعَ مِنْكُمُ الْبَاءَةَ فَلْيَتَزَوَّجْ"
“Enyi rika la vijana! Atakayeweza miongoni mwenu kupata gharama za kuolea na kuendeshea maisha, basi na aoe”. [Al-Bukhaariy na Muslim]
Na Allaah Ta’aalaa Anasema:
"وَلْيَسْتَعْفِفِ الَّذِينَ لَا يَجِدُونَ نِكَاحًا حَتَّىٰ يُغْنِيَهُمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ"
“Na wajizuie (yaliyoharamishwa) wale ambao hawapati uwezo wa ndoa mpaka Allaah Awatajirishe kwa Fadhila Zake”. [An-Nuwr: 33]
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
تَعَدُّدِ الزَّوْجّاتِ
Mke Zaidi Ya Mmoja
Alhidaaya.com [3]
03: Dhana Ya Kuoa Mke Zaidi Ya Mmoja:
Hakuna shaka yoyote kwamba kuoa mke zaidi ya mmoja ndio njia nyoofu zaidi kwa mwanaume kutokana na mambo ambayo yako wazi kabisa kwa kila mwenye akili. Mambo hayo ni:
1- Mwanamke kimaumbile hupata hedhi na nifasi, huugua na kupatwa na mengineyo yanayozuia tendo la ndoa. Na mwanaume wakati wote anakuwa hana kizuizi cha tendo hilo ila kwa nadra sana, na anakuwa tayari kwalo wakati wowote, saa yoyote. Sasa ikiwa mke ni mmoja, bila shaka inakuwa ni uzito sana kwa mume.
2- Allaah Amepitisha Qadari Yake ya idadi ya wanaume kuwa kidogo kuliko ya wanawake katika mataifa yote. Wanaume ndio wanaokabiliwa zaidi na vifo kwenye medani nyingi za maisha na hususan kwenye vita. Ikiwa mwanaume atatosheka na mke mmoja tu, basi idadi kubwa mno ya wanawake watabakia bila ndoa, na matokeo yake ni kufanya machafu.
Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amelihesabu hilo kuwa moja kati ya alama za kukurubia Qiyaamah. Anasema:
إِنَّ مِنْ أَشْرَاطِ السَّاعَةِ، أَنْ يُرْفَعَ الْعِلْمُ، وَيَكْثُرَ الْجَهْلُ، وَيَكْثُرَ الزِّنَا، وَيَكْثُرَ شُرْبُ الْخَمْرِ، وَيَقِلَّ الرِّجَالُ، وَيَكْثُرَ النِّسَاءُ حَتَّى يَكُونَ لِخَمْسِينَ امْرَأَةً الْقَيِّمُ الْوَاحِدُ
“Miongoni mwa alama za (kukurubia) Qiyaamah, ni kuondoshwa ‘ilmu (ya dini kwa kufa ‘Ulamaa wachamungu), kukithiri ujinga (wa mambo ya dini), kukithiri zinaa, kukithiri unywaji pombe, wanaume kupungua na wanawake kuwa wengi hadi kufikia wanawake 50 kusimamiwa kwa huduma na mwanaume mmoja”. [Al-Bukhaariy (5231) na Muslim (2671)]
3- Wanawake wote wako tayari kuolewa, lakini wanaume wengi kutokana na umasikini, hawana uwezo wa kupata mahitajio ya ndoa. Hivyo basi, wanaume walio tayari kwa ndoa ni kidogo kulinganisha na wanawake walio tayari kwayo. Na hawa walio tayari, ni vyema waongeze wake ili kupunguza pengo la idadi.
4- Kuna baadhi ya wanaume ambao kwa mujibu wa maumbile yao ya kisaikolojia na kimwili, wana kiu kali sana ya tendo la ndoa, mwanamke mmoja hamtoshelezi. Hivyo sharia imemfungulia milango ya kuwa na mke zaidi ya mmoja ili kushibisha utashi wake kwa njia halali badala ya kuhangaika na wanawake wa pembeni watakaomharibu tabia na kumletea maafa.
5- Kunaweza kuwa ni msaada mzuri kwa mmoja wa jamaa au ndugu ambaye amefiliwa na mumewe au ametalikiwa. Kumwoa huyu kutamwokoa na mahangaiko ya kimaisha, na atakidhiwa hitajio lake la hamu ya tendo la ndoa.
Ninasema: “Ingawa jambo hili limesuniwa na linapendeza, na ni sehemu ya sharia samehevu ya Kiislamu, lakini kutokana na kutumiwa vibaya na baadhi ya watu, limekuwa kwenye mwono wa watu wengi kama ni uhalifu, uovu na utovu wa wema pamoja na tuhuma nyinginezo nyingi batili”.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
تَعَدُّدِ الزَّوْجّاتِ
Mke Zaidi Ya Mmoja
Alhidaaya.com [3]
04: Baadhi Ya Faida Za Kifiqhi Za Ndoa Ya Wake Wengi:
1- Inajuzu mahari kutofautiana kati ya mke na mke na hata chakula cha walima.
Nyuma tulieleza kwamba Mfalme Najaashiy (Negus) alimwozesha Ummu Habiybah kwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na akamlipia mahari ya dirham 4,000. Na mahari ya Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa wakeze ilikuwa ni dirham 400 tu.
Anas akizungumzia walima aliofanya Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipomwoa Zaynab binti Jahsh amesema:
"مَا رَأَيْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَوْلَمَ عَلَى أَحَدٍ مِنْ نِسَائِهِ مَا أَوْلَمَ عَلَيْهَا"
“Sikumwona Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akimfanyia walima yeyote kati ya wake zake, kama aliyomfanyia Zaynab”. [Imetajwa nyuma]
2- Haijuzu mwanaume kuwaweka wake wenza nyumba moja ila kwa ridhaa yao.
Kila mke ni lazima awe na nyumba yake kando kama alivyofanya Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Allaah Ta’aalaa Amesema:
"يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَدْخُلُوا بُيُوتَ النَّبِيِّ إِلَّا أَن يُؤْذَنَ لَكُمْ إِلَىٰ طَعَامٍ"
“Enyi walioamini! Msiingie nyumba za Nabiy isipokuwa mkipewa idhini ya kwenda kula, si kungojea kiive”. [Al-Ahzaab: 53]
Allaah Amezielezea hapa kama nyumba nyingi, na si nyumba moja, kama ilivyoelezwa kwenye milango ya nyuma.
3- Mgawo wa zamu kati ya wake.
Jumhuwr ya ‘Ulamaa wanasema kwamba mtu akioa bikra kwa mke mkubwa “thayyib” (aliyekwisha ingiliwa), basi atakaa kwa bikra kwa muda wa siku saba, kisha baada ya hapo, atagawa siku za zamu za kulala kwao sawa kwa sawa.
Ama akioa “thayyib” kwa mke bikra, basi atakaa kwake kwa siku tatu, kisha atagawa siku za zamu za kulala kwao sawa kwa sawa.
Ni kutokana na Hadiyth ya Anas aliyesema:
"مِنَ اَلسُّنَّةِ إِذَا تَزَوَّجَ اَلرَّجُلُ اَلْبِكْرَ عَلَى اَلثَّيِّبِ أَقَامَ عِنْدَهَا سَبْعًا، ثُمَّ قَسَمَ، وَإِذَا تَزَوَّجَ اَلثَّيِّبَ أَقَامَ عِنْدَهَا ثَلَاثًا، ثُمَّ قَسَمَ "
“Ni katika Sunnah mtu akioa bikra kwa “thayyib”, akae kwa bikra siku saba, kisha agawe zamu (sawa kwa sawa). Na akioa “thayyib” kwa bikra, akae kwa “thayyib” siku tatu, kisha agawe zamu (sawa kwa sawa)”. [Al-Bukhaariy 5214) na Muslim (1461)]
Angalizo:
Baadhi ya watu wameifahamu vibaya Hadiyth hii. Wanadhani kwamba mume anapooa bikra, basi ajifungie naye ndani siku hizo saba na asitoke hata kwenda kuswali jamaa msikitini. Huu ni ufahamu batili usio na dalili yoyote. Hatakikani akose jamaa kama ilivyo kwa watu wengine.
4- Je, ni lazima mume afanye usawa kati ya wakeze katika penzi na jimai?
Penzi na mahaba mahala pake ni moyoni. Allaah Ta’aalaa Amesema:
"وَلَن تَسْتَطِيعُوا أَن تَعْدِلُوا بَيْنَ النِّسَاءِ وَلَوْ حَرَصْتُمْ"
“Na wala hamtoweza kuadilisha baina ya wake japokuwa mtapania”. [An-Nisaa: 129]
Makusudio ya kutokuweza hapa ni katika mahaba, jimai na matamanio, haya ni mambo ambayo mtu hawezi kuyadhibiti.
Na katika Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas, ‘Umar aliingia kwa Hafswah na kumwambia:
"يَا بُنَيَّةِ، لاَ يَغُرَّنَّكِ هَذِهِ الَّتِي أَعْجَبَهَا حُسْنُهَا حُبُّ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِيَّاهَا ـ يُرِيدُ عَائِشَةَ ـ فَقَصَصْتُ عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَتَبَسَّمَ"
“Ewe binti yangu! Angalia sana usije kuhadaika na huyu anayeringia uzuri wake na kupendwa zaidi na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) -anamkusudia ‘Aaishah-. Nikamhadithia hilo Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam), naye akatabasamu”. [Al-Bukhaariy (49/3) na Muslim (1479)]
Na Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliulizwa:
"أَىُّ النَّاسِ أَحَبُّ إِلَيْكَ؟ قَالَ: عَائِشَةُ"
“Ni yupi kati ya watu umpendaye zaidi? Akajibu: ‘Aaishah”. [Sunan Ibn Maajah: 101]
Ibn Qudaamah amesema: “Hatujui mvutano wowote kati ya ‘Ulamaa kuhusiana na suala la kuwa si wajibu kufanya usawa kati ya wake katika tendo la jimai, kwa sababu, chanzo cha jimai ni matamanio na msisimko, na hili halina ujanja wa kuweza kufanya usawa ndani yake. Moyo wa mume unaweza kulemea zaidi kwa mmoja wao pasi na mwengine (bila kuwa na uwezo wa kudhibiti hilo)”.
Ama kwa upande wa matumizi ya kawaida, hilo bila shaka ni wajibu kwa mume kufanya usawa kati yao.
5- Haijuzu kwa mwanamke kumtaka mume amtaliki mke mwenzake ili abaki peke yake na mumewe.
Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"لَا تَسْأَلِ الْمَرْأَةُ طَلَاقَ أُخْتِهَا لِتَسْتَفْرِغَ صَحْفَتَهَا وَلِتَنْكِحَ فَإِنَّ لَهَا مَا قُدِّرَ لَهَا"
“Mwanamke asishawishi mwenzake atalikiwe ili yeye aolewe na atwaye nafasi yake, kwani hakika atapata kile tu alichokadiriwa (na Allaah)”. [Al-Bukhaariy (5152), na Muslim (1408)]
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/284
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12054&title=10I-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20%D9%83%D8%AA%D8%A7%D8%A8%20%D8%A7%D9%84%D8%B2%D9%88%D8%A7%D8%AC%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20%D8%AA%D9%8E%D8%B9%D9%8E%D8%AF%D9%91%D9%8F%D8%AF%D9%90%20%D8%A7%D9%84%D8%B2%D9%91%D9%8E%D9%88%D9%92%D8%AC%D9%91%D8%A7%D8%AA%D9%90%20Mke%20Zaidi%20Ya%20Mmoja
[3] http://www.alhidaaya.com/
[4] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12056&title=01-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Mke%20Zaidi%20Ya%20Mmoja%3A%20Uhalali%20Wake
[5] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12057&title=02-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Mke%20Zaidi%20Ya%20Mmoja%3A%20Masharti%20Ya%20Kuoa%20Mke%20Zaidi%20Ya%20Mmoja
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12058&title=03-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Mke%20Zaidi%20Ya%20Mmoja%3A%20Dhana%20Ya%20Kuoa%20Mke%20Zaidi%20Ya%20Mmoja
[7] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12059&title=04-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20Mke%20Zaidi%20Ya%20Mmoja%3A%20Baadhi%20Ya%20Faida%20Za%20Kifiqhi%20Za%20Ndoa%20Ya%20Wake%20Wengi