Alhidaaya.com
Published on Alhidaaya.com (https://www.alhidaaya.com/sw)

Ukurasa Wa Kwanza > 10J-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: كتاب الزواج Kitabu Cha Ndoa: مِنْ أَحْكَامِ المَوْلُودِ Hukumu Zinazohusiana Na Mtoto Anayezaliwa

10J-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: كتاب الزواج Kitabu Cha Ndoa: مِنْ أَحْكَامِ المَوْلُودِ Hukumu Zinazohusiana Na Mtoto Anayezaliwa

Swahiyh Fiqh As-Sunnah [1]

 

 

كتاب الزواج

 

Kitabu Cha Ndoa

 

 

 

مِنْ أَحْكَامِ المَوْلُودِ

 

Hukumu Zinazohusiana Na Mtoto Anayezaliwa

 

 

Abu Maalik Kamaal Bin As-Sayyid Saalim

 

Imetarjumiwa na 'Abdullaah Mu'aawiyah (Abu Baasim)

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

Share [2]

01-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa:Hukumu Zinazohusiana Na Mtoto Anayezaliwa: Anayezalisha Na Kuwapa Watu Habari Ya Kuzaliwa

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

مِنْ أَحْكَامِ المَوْلُودِ

 

Hukumu Zinazohusiana Na Mtoto Anayezaliwa:

 

Alhidaaya.com [3]

 

 

 

01:  Anayezalisha Na Kuwapa Watu Habari Ya Kuzaliwa:

 

 

Mwanamke mwenye utaalamu wa kuzalisha, ndiye anayetakiwa kusimamia shughuli ya kumzalisha mwanamke mwenzake.  Awe na wanawake wenzake watakaomsaidia kufanikisha zoezi hilo.  Kazi hii kufanywa na wanawake ni jambo la waajib, ila tu kama kuna udharura usioepukika, kama kutopatikana wanawake wenye utaalamu wa kazi hii.  Wasipopatikana, basi daktari mwanaume wa Kiislamu atasimamia jukumu, lakini kwa kuchunga vidhibiti vilivyotajwa kwenye mlango wa Hukumu Za Kuangalia.

 

Inapendeza Kuwapa Watu Habari Ya Furaha Ya Kuzaliwa Mtoto Na Kuwapongeza Wahusika:

 

Mara mtoto anapozaliwa akatoa sauti ya kilio, imesuniwa kwa mwanamke aliyepo kwenye tukio, au yeyote aliye karibu, atoe habari ya furaha kwa baba yake, kwani hilo bila shaka linaingiza furaha moyoni.  Imesuniwa Muislamu kuharakia kumfurahisha nduguye na kumjulisha jambo lolote la kumfurahisha.

 

Allaah Ta’aalaa Akizungumzia kisa cha Nabiy Ibraahiym (‘Alayhis Salaam) Anasema:

 

"فَبَشَّرْنَاهُ بِغُلَامٍ حَلِيمٍ"

 

 

“Basi Tukambashiria ghulamu mvumilivu”.  [As-Swaaffaat: 101]

 

Na Anasema tena:

 

"قَالُوا لَا تَوْجَلْ إِنَّا نُبَشِّرُكَ بِغُلَامٍ عَلِيمٍ"

 

“(Malaika) wakasema:  Usiogope!  Hakika sisi tunakubashiria ghulamu mjuzi”.  [Al-Hijr: 53]

 

Vile vile Anasema:

 

"يَا زَكَرِيَّا إِنَّا نُبَشِّرُكَ بِغُلَامٍ اسْمُهُ يَحْيَىٰ لَمْ نَجْعَل لَّهُ مِن قَبْلُ سَمِيًّا"

 

“(Akaambiwa):  Ee Zakariyyaa!  Hakika Sisi Tunakubashiria ghulamu jina lake Yahyaa, Hatukupata kabla kumpa jina hilo yeyote.   [Maryam:  07]

 

Ikiwa mtu atapitwa na habari hiyo ya furaha, basi imesuniwa ampongeze mzazi kwa kukiombea kichanga chake kheri.

 

 

Share [4]

02-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa:Hukumu Zinazohusiana Na Mtoto Anayezaliwa: Je, Kichanga Huadhiniwa Kwenye Sikio Lake La Kulia Na Kuqimiwa Kwenye Sikio Lake La Kushoto?

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

مِنْ أَحْكَامِ المَوْلُودِ

 

Hukumu Zinazohusiana Na Mtoto Anayezaliwa

 

 

Alhidaaya.com [3]

 

 

 

02:   Je, Kichanga Huadhiniwa Kwenye Sikio Lake La Kulia Na Kuqimiwa Kwenye Sikio Lake La Kushoto?

 

Suala hili limetajwa kwenye baadhi ya Hadiyth, lakini sanadi zake ni dhwa’iyf.  Kati yake ni Hadiyth ya Abu Raafi’u aliyesema:

 

"رَأَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أذَّنَ فِي أُذُنِ الحَسَنِ ابنِ عليٍّ حِينَ وَلَدَتْهُ فَاطِمَةُ"

 

“Nilimwona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akimwadhinia Al-Hasan bin ‘Aliy kwenye sikio lake wakati alipozaliwa na Faatwimah”.  [Abu Daawuwd (5105), At-Tirmidhiy (1514) na Al-Haakim (3/179) kwa Sanad Dhwa’iyf).  Al-Albaaniy alisema kwamba Hadiyth hii ina hadhi ya “Hasan Lighayrihi” katika Al-Irwaa (1173), lakini alijirudi baadaye na kusema ni Hadiyth  Dhwa’iyf]

 

Kwa muktadha huu, Hadiyth hii ya Abu Raafi’u ni Dhwa’iyf, haifai kutumika mpaka ipatikane nyingine ya kuitilia nguvu.  Ibn Al-Qayyim aliitaja Hadiyth hii  pamoja na Hadiyth nyingine mbili katika Kitabu cha Tuhfatul Mawluwd (ukurasa wa 101), lakini Hadiyth hizo mbili pia ni Dhwa’iyf.

 

Imesuniwa Kukilambisha Kichanga Kitu Tamu:

 

Ni vizuri kuitafuna au kuisaga tende na kumsugulia kwayo kichanga ndani ya kinywa.  Toka kwa Abu Muwsaa amesema:

 

"وُلِدَ لِي غُلاَمٌ، فَأَتَيْتُ بِهِ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ، فَسَمَّاهُ إِبْرَاهِيمَ، فَحَنَّكَهُ بِتَمْرَةٍ، وَدَعَا لَهُ بِالْبَرَكَةِ، وَدَفَعَهُ إِلَيَّ "

 

“Niliruzukiwa mtoto wa kiume, nikaenda naye kwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam), (akamchukua) na akampa jina la Ibraahiym kisha akamlambisha tende.  Lakini pia alimwombea barakah, halafu akanirudishia”.  [Mtoto alikuwa wa kwanza wa Abu Muwsaa].

 

 

Share [5]

03-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa:Hukumu Zinazohusiana Na Mtoto Anayezaliwa: Imesuniwa Kumfanyia ‘Aqiyqah

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

مِنْ أَحْكَامِ المَوْلُودِ

 

Hukumu Zinazohusiana Na Mtoto Anayezaliwa:

 

Alhidaaya.com [3]

 

 

03:   Imesuniwa Kumfanyia ‘Aqiyqah:

 

Asili ya neno “Aqiyqah”, ni nywele zinazokuwepo kwenye kichwa cha mtoto baada ya kuzaliwa.  Na mbuzi au kondoo anayechinjwa kwa ajili yake anaitwa ‘aqiyqah.  Kadhalika, chinjo lenyewe la mbuzi au kondoo linaitwa ‘aqiyqah.

 

‘Aqiyqah hii imesuniwa kufanywa siku ya saba ya kuzaliwa mtoto.  Baba yake atamchinjia kondoo au mbuzi wawili kama ni wa kiume, na mbuzi mmoja au kondoo mmoja kama ni wa kike.

 

Toka kwa Salmaan bin ‘Aamir Ad-Dhwabiy amesema:  Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

"مَعَ الْغُلاَمِ عَقِيقَتُهُ، فَأَهْرِيقُوا عَنْهُ دَمًا، وَأَمِيطُوا عَنْهُ الأَذَى‏"

‏

”Sambamba na kila mtoto (anayezaliwa), pana mnyama wake wa ‘aqiyqah.  Basi mwageni damu kwa niaba yake, na mwondosheeni adha”.  [Hadiyth Swahiyh.  Imetajwa nyuma].

.

 

Naye ‘Aaishah (Radhwiya Allaah ‘anhaa), amesema:

 

عَنِ اَلْغُلَامِ شَاتَانِ مُكَافِئَتَانِ، وَعَنْ اَلْجَارِيَةِ شَاةٌ "

 

“Mtoto wa kiume achinjiwe kondoo wawili wenye umri sawa, na wa kike kondoo mmoja”.  [At-Tirmidhiy (1513) na Ahmad (6/31).  Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh katika Al-Irwaa (1166)]   

 

Kadhalika,  Samurah amesema:  Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: 

 

"الغُلاَمُ رَهِينَةٌ بِعَقِيقَتِهِ ، تُذْبَحُ عَنْهُ يَوْمَ سَابِعِهِ ، وَيُحْلَقُ ، وَيُسَمَّى"

 

“Mtoto ni rehani kwa mnyama wake wa aqiyqah, huchinjiwa siku yake ya saba, hunyolewa, na hupewa jina”.   [Hadiyth Swahiyh.  Imekharijiwa na Abu Daawuwd (2838), An Nasaaiy (7/166), At-Tirmidhiy (1522), Ibn Maajah (3165) na wengineo].

 

 

Imesuniwa Kuila, Kulisha Na Kuigawa Nyama Aa ‘Aqiyqah.

 

Mnyama wa ‘aqiyqah ni lazima awe na vigezo sawa na mnyama wa ‘udh-hiyah kama kuwa mbuzi au kondoo asiye na kasoro yoyote na mfano wa hayo.

 

Share [6]

04-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa:Hukumu Zinazohusiana Na Mtoto Anayezaliwa: Kunyoa Kichwa Cha Mtoto Na Kutoa Swadaqah Ya Silver Ya Uzito Wa Nywele Zake Na Kumtahiri

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

مِنْ أَحْكَامِ المَوْلُودِ

 

Hukumu Zinazohusiana Na Mtoto Anayezaliwa:

 

Alhidaaya.com [3]

 

 

 

 

04:   Kunyoa Kichwa Cha Mtoto Na Kutoa Swadaqah Ya Silver Ya Uzito Wa Nywele Zake Na Kumtahiri:

 

Toka kwa Anas bin Maalik:

 

"أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَمَرَ بِرَأْسِ الحَسَنِ والحُسَيْنِ يَوْمَ سَابِعِهِمَا، فَحُلِقَا، وَتَصَدَّقَ بِوَزْنَهِ فِضّة"

 

“Kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliamuru Al-Hasan na Al-Husayn waletwe kwake siku ya saba ya kuzaliwa kwao, akawanyoa, na akatoa swadaqah silver ya uzito wa nywele zao”.  [Hadiyth Swahiyh.  At-Tirmidhiy (1519), Al-Haakim (4/237) na Al-Bayhaqiy (9/304)]

 

Angalizo:

 

Haijuzu kunyoa kichwa cha mtoto sehemu na kuacha nyingine mfano wa panki, denge na kadhalika.  Toka kwa Ibn ‘Umar (Radhwiya Allaah ‘anhumaa) amesema:

 

"نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنِ الْقَزَعِ"

 

“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kunyoa denge (panki)”.  [Al-Bukhaariy (5920) na Muslim (113)]

                                                           

 

Kumfanyia Sunnah (Kumtahiri):

 

Kuna baadhi ya Hadiyth zilizotajwa kuhusiana na kusuniwa kumfanyia mtoto wa kiume sunnah siku ya saba ya kuzaliwa kwake.  Lakini sanadi za Hadiyth hizi ni dhwa’iyf, ingawa zinaweza kuzatitiana zenyewe kwa zenyewe.  Kati yake ni:

 

"أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَقَّ عَنِ الحَسَنِ وَالحُسَيْنِ وَخَتَنَهُمَا لِسَبْعَةِ أَيَّام"

 

“Kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwafanyia Al-Hasan na Al-Husayn ‘aqiyqah na akawatahiri siku ya saba (ya kuzaliwa)”.  [At-Twabaraaniy katika As-Swaghiyr (891) na Al-Bayhaqiy (8/324).  Sanad yake ni dhwa’iyf] 

 

 

 

Share [7]

05-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa:Hukumu Zinazohusiana Na Mtoto Anayezaliwa: Kumpa Jina

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

مِنْ أَحْكَامِ المَوْلُودِ

 

Hukumu Zinazohusiana Na Mtoto Anayezaliwa

 

 

Alhidaaya.com [3]

 

 

 

05:   Kumpa Jina:

 

(a)  Baba ndiye mwenye haki ya kutoa jina la mtoto, na mama hana haki ya kupinga.  Lakini pamoja na hivyo, ni vizuri sana washauriane na wakubaliane jina.  Kama watavutana, basi haki inabakia kwa baba.

 

(b)  Baba anatakiwa achague jina zuri kwa upande wa maana na linavyotamkwa.  Liwe zuri, tamu kwenye ulimi, linakubalika kwenye sikio, na halikuharamishwa au kukirihishwa kwa mujibu wa maelekezo ya Allaah na Rasuli Wake.

 

(c)  Majina Mazuri Yanayopendeza:

 

Majina yanayopendeza ni mengi.  Tunaweza kuyaweka katika utaratibu ufuatao:

 

1-  ‘Abdullaah na ‘Abdulrahmaan.  Ni kwa neno la Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

 

"أَحَبُّ الأَسْمَاءِ إِلَى اللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ عَبْدُ اللَّهِ وَعَبْدُ الرَّحْمَنِ ‏"‏

 

“Majina yanayopendeza zaidi kwa Allaah ‘Azza wa Jalla ni ‘Abdullaah na ‘Abdulrahmaan”.  [Swahiyh Muslim]

 

2-  Majina yenye kuanziwa na ‘Abdu (Mja) na kufuatiwa na Jina lolote Zuri la Allaah kama ‘Abdul ‘Aziyz, ‘Abdul Kariym, ‘Abdul Malik na kadhalika.

 

3-  Majina ya Manabii na Mitume.

 

4-  Majina ya Waislamu walio wema wakiongozwa na Maswahaba.

 

Imepokelewa toka kwa Al-Mughiyrah bin Shu-‘ubah (Radhwiya Allaah ‘anhu) kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) (akiwazungumzia Baniy Israaiyl) amesema:

 

"إِنَّهُمْ كَانُوا يُسَمُّونَ بِأَنْبِيَائِهِمْ وَالصَّالِحِينَ قَبْلَهُمْ ‏"‏

 

“Hakika wao walikuwa wakiita (watoto wao) majina ya Manabii na wema wao waliotangulia”.  [Swahiyh Muslim]

 

5-  Yenye kubeba sifa ya kweli aliyonayo binadamu kwa masharti yafuatayo:

 

(a)  Yawe na asili ya Kiarabu.  Yasiyo na asili ya Kiarabu kama vile Diana, Haidey, Sherihan na kadhalika hayafai.

 

(b)  Yawe na maana nzuri na muundo murua.

 

(c)  Yawe na herufi chache kiasi iwezekanavyo.

 

(d)  Yatamkike kwa wepesi.

 

Majina Yaliyoharamishwa:

 

(a) Kila jina linalotanguliwa na “Abdu bila kufuatiliwa na Jina la Allaah kama vile ‘Abdul Rasuwl"عَبْدُ الرَّسُول" , ‘Abdul Hasan  "عَبْدُ الحَسَن"na kadhalika.

 

(b)  Kila jina linalohusiana na Allaah Pekee kama Ar-Rahmaan"الرَّحْمن" , Al-Khaaliq "الخَالِق"na kadhalika.

 

(c)  Majina ambayo ni mahsusi kwa makafiri kama George, Diana, Suzan na kadhalika.

 

(d) Majina ya masanamu yanayoabudiwa badala ya Allaah kama vile Al-Laata, Al-‘Uzza na kadhalika.

 

(e)  Majina yasiyo ya Kiarabu ambayo hayana nafasi katika Lugha ya Kiarabu kama Neriman, Jehan, Nevin na kadhalika.

 

(f)  Majina yenye kubeba sifa njema au mbaya asiyokuwa nayo mwitwaji.

 

(g)  Majina ya mashetani kama Khinzab"خِنْزَب" , Al A-’awar"الأَعْوَر"  na kadhalika.

 

Majina Yaliyokirihishwa:

 

1-  Majina yote yenye kuchukiza moyoni kutokana na maana zake au kutamkwa kwake kunakopelekea kuchezwa shere na watu, au wenye majina hayo kuhisi dhiki, au kuathirika vibaya kisaikolojia.

 

Majina hayo ni kama Khan-jar  "خَنْجَر"(aina ya kisu), Faadhwih  "فَاضِح"(mtovu wa hishma), Huyaam na Suhaam  "هُيَام" "سُهَام"(magonjwa ya ngamia) na kadhalika.

 

2-  Majina yenye maana laini yenye kuchemsha matamanio kama Ahlaam"أَحْلَام"  (ndoto), Ghaadah "غَادَة"  (msichana mzuri laini), Faatin "فَاتِن" (msichana mzuri anayevutia) na kadhalika.

 

3-  Majina ya waigizaji, waimbaji na wasanii wasio na chembe ya hofu kwa Allaah.  Na hii ni kwa kukusudia kumpa mtoto jina la watu hao kwa kuwa mtu anawapenda na kuwashabikia.

 

4-  Majina yenye kubeba maana ya dhambi na maasi kama Dhalimu "ظَالِم" , Mwizi  mbobezi  "سَرَّاق"na kadhalika.

 

5-  Majina ya mafirauni, madikteta, watawala madhalimu na watu makatili kama Firauni, Haamaan, Qaaruwn na kadhalika.

 

6-  Majina ya wanyama wenye sifa za kuchukiza kama punda, mbwa, nungu na kadhalika. 

 

7-  Majina yenye kuegemezewa kwenye dini au Uislamu kama vile Nuwrud Diyn  "نُوْرُ الدِّيْن"(Nuru ya dini),  Shihaabud Diyn "شِهَابُ الدِّيْن"  (Kimondo cha dini), Sayful Islaam "سَيْفُ الإِسْلَام"(Upanga wa Uislamu) na kadhalika.

 

8-  Majina ambatano (mawili kwa mpigo) kama Muhammad Ahmad na kadhalika.  Majina haya huchanganya watu.

 

9-  Majina ya Malaika kama vile Jibriyl, Miykaaiyl na kadhalika.

 

Share [8]
www.alhidaaya.com

Source URL: https://www.alhidaaya.com/sw/node/12055

Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/284
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12055&title=10J-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20%D9%83%D8%AA%D8%A7%D8%A8%20%D8%A7%D9%84%D8%B2%D9%88%D8%A7%D8%AC%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3A%20%D9%85%D9%90%D9%86%D9%92%20%D8%A3%D9%8E%D8%AD%D9%92%D9%83%D9%8E%D8%A7%D9%85%D9%90%20%D8%A7%D9%84%D9%85%D9%8E%D9%88%D9%92%D9%84%D9%8F%D9%88%D8%AF%D9%90%20Hukumu%20Zinazohusiana%20Na%20Mtoto%20Anayezaliwa
[3] http://www.alhidaaya.com/
[4] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12060&title=01-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3AHukumu%20Zinazohusiana%20Na%20Mtoto%20Anayezaliwa%3A%20Anayezalisha%20Na%20Kuwapa%20Watu%20Habari%20Ya%20Kuzaliwa%20
[5] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12061&title=02-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3AHukumu%20Zinazohusiana%20Na%20Mtoto%20Anayezaliwa%3A%20Je%2C%20Kichanga%20Huadhiniwa%20Kwenye%20Sikio%20Lake%20La%20Kulia%20Na%20Kuqimiwa%20Kwenye%20Sikio%20Lake%20La%20Kushoto%3F
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12062&title=03-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3AHukumu%20Zinazohusiana%20Na%20Mtoto%20Anayezaliwa%3A%20Imesuniwa%20Kumfanyia%20%E2%80%98Aqiyqah
[7] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12063&title=04-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3AHukumu%20Zinazohusiana%20Na%20Mtoto%20Anayezaliwa%3A%20Kunyoa%20Kichwa%20Cha%20Mtoto%20Na%20Kutoa%20Swadaqah%20Ya%20Silver%20Ya%20Uzito%20Wa%20Nywele%20Zake%20Na%20Kumtahiri%20
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F12064&title=05-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Kitabu%20Cha%20Ndoa%3AHukumu%20Zinazohusiana%20Na%20Mtoto%20Anayezaliwa%3A%20Kumpa%20Jina%20