Alhidaaya.com
Published on Alhidaaya.com (https://www.alhidaaya.com/sw)

Ukurasa Wa Kwanza > Fataawaa: Suhuwr (Daku) Na Kufuturu

Fataawaa: Suhuwr (Daku) Na Kufuturu

Fataawa Za Ramadhwaan-'Iyd [1]

 

 

 

 

www.alhidaaya.com [2]

 

 

 

Share [3]

01-Imaam Bin Baaz: Kula Suhuwr (Daku) Wakati Muadhini Anaadhini

Kula Suhuwr (Daku) Wakati Muadhini Anaadhini

 

Imaam Bin Baaz (Rahimahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com [4]

 

SWALI:

 

Je, Unaruhusiwa kuendelea kula daku wakati Muadhini anaadhini adhaan ya pili au aache?

 

JIBU:

 

Hii ina maelezo.

Inategemea kama Muadhini anaadhini kwa ajili ya Alfajiri (anatoa Adhaan ya kuwa Alfajiri imeshaanza (Adhaan ya pili), basi lazima usimame kula na kunywa kwa sababu Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema, ((Msisimamishe daku yenu mnaposikia adhaan ya Bilaal, kwani yeye anaadhini usiku, kwa hiyo kuleni na kunyweni mpaka Ibn Umm Maktuum aadhini)) Na hii ni kutokana na aya (ambayo inaleta maana hiyo)

 

“Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu uzi mweupe (mapambazuko) wa Alfajiri kutokana na uzi mweusi (wa kiza cha usiku).” [Al-Baqarah: 2:187]

 

Vile vile ikijulikana kama Alfajiri imeingia kama mfano mtu akiwa kwenye jangwa basi aache kula na kunywa hata kama hakusikia adhaan (mahali ambapo adhana haisikiki).

Lakini kama Muadhini anaadhini mapema au kama kuna shaka na adhaan yake kama imewafikiana na Asubuhi au sio, basi unaweza kula na kunywa mpaka utakapokuwa na uhakika kuwa Alfajiri imeshaanza, ikiwa inajulikana hivyo kutokana na saa maarufu zinazothibitisha kuanza Alfajiri au  kutokana na Muadhini mwenye kuaminika anayejulikana kuwa anaadhini wakati wa Alfajiri. Kwa hali hii (ikiwa adhaan imeadhiniwa mapema sana) unaweza kula wakati adhaan inaadhiniwa, ule au unywe kilichokuweko mkononi mwako kwa sababu hakuna hakika kama adhaan inaadhiniwa kwa wakati wake ulio sahihi, bali huenda kulikuwa tu ni kwa makisio na si kwa uhakika.  

 

[Majmuw' Fataawa ash-Shaykh Ibn Baaz, mjalada 15, ukurasa 282].

Share [5]

02-Imaam Ibn ‘Uthyamiyn: Kufuturu Tende Kwa Idadi Ya Witr

Kufuturu Tende Kwa Idadi Ya Witr

 

Imaam Ibn ‘Uthyamiyn (Rahimahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com [4]

 

SWALI:

 

Nimesikia kwammba mwenye swawm anawajibika pale anapofuturu tende, iwe ni idadi ya witr yaani iwe tano au saba  na kadhaalika Je ni waajib?

 

JIBU:

 

Si waajib, bali hata sio Sunnah mtu afuturu kwa witr; tatu au tano au saba au tisa isipokuwa Siku ya ‘Iyd kwani imethibiti kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa hatoki kwenda Swalaah Siku ya ‘Iydul-Fitwr mpaka ale kwanza tamar (tende) na alikuwa akila kwa witr. 

Ama nje ya hayo Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakukusudia kula tende kwa witr.

 [Fataawa Nuwr ‘Alad-Darb 11/2]

 

 

 

Share [6]
www.alhidaaya.com

Source URL: https://www.alhidaaya.com/sw/node/8401

Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/261
[2] http://www.alhidaaya.com/sw/
[3] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8401&title=Fataawaa%3A%20Suhuwr%20%28Daku%29%20Na%20Kufuturu
[4] http://www.alhidaaya.com
[5] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8402&title=01-Imaam%20Bin%20Baaz%3A%20Kula%20Suhuwr%20%28Daku%29%20Wakati%20Muadhini%20Anaadhini
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8404&title=02-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthyamiyn%3A%20Kufuturu%20Tende%20Kwa%20Idadi%20Ya%20Witr