Alhidaaya.com
Published on Alhidaaya.com (https://www.alhidaaya.com/sw)

Ukurasa Wa Kwanza > Fataawaa: Kulipa Swawm Na Kafara > 01-Al-Lajnah Ad-Daaimah: Ameamka Huku Anasinzia Akala Chakula Kisha Akatambua Kuwa Alfajiri Imeshaingia

01-Al-Lajnah Ad-Daaimah: Ameamka Huku Anasinzia Akala Chakula Kisha Akatambua Kuwa Alfajiri Imeshaingia

Ameamka Huku Anasinzia Akala Chakula Kisha Akatambua Kuwa Alfajiri Imeshaingia

 

Al-Lajnah Ad-Daaimah

 

www.alhidaaya.com [1]

 

 

 

SWALI:

 

Niliamka asubuhi moja huku bado nusu nimelala (nasinzia) nikaenda jikoni haraka na kula chakula, lakini nilivyoanza kula, nimetazama saa nikaona kuwa ni saa 10: 45 Alfajiri  Na wakati wa Alfajiri  huku Tabuk (Kaskakazini Saudi Arabia) ni 10: 15 Alfajiri. Kwa hiyo nikasimama kula na kuanza kufunga, nikijua kuwa nimekula kama vijiko vitatu au vinne. Je, Sheikh inanipasa nilipe Swawm hii au hainipasi?

 

 

JIBU:

 

Kama hali ni kama ulivyoeleza, basi inakupasa ulipe siku hiyo kwani ulikula baada ya wakati wa Alfajiri kupita.

 

Allaah Atujaalie At-Tawfiyq.  Swalah na Salaam ziwe juu ya Nabiy wetu Muhammad, familia yake, na Maswahaba zake.

 

 

[Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah lil-Buhuwth Al-'Ilmiyyah wal-Iftaa. - Fataawaa Ramadhwaan - Mjalada 2, Uk 569, Fatwa Namba 552]
 

 

 

Share [2]
www.alhidaaya.com

Source URL: https://www.alhidaaya.com/sw/node/8455

Links
[1] http://www.alhidaaya.com
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8455&title=01-Al-Lajnah%20Ad-Daaimah%3A%20Ameamka%20Huku%20Anasinzia%20Akala%20Chakula%20Kisha%20Akatambua%20Kuwa%20Alfajiri%20Imeshaingia