كِتَابُ اَلْجَنَائِزِ
Kitabu Cha Janaazah
Abu Maalik Kamaal Bin As-Sayyid Saalim
Imetarjumiwa na 'Abdullaah Mu'aawiyah (Abu Baasim)
Alhidaaya.com
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Janaazah
001-Wanayoyafanya Waliopo Kwa Aliyekaribia Kukata Roho
Alhidaaya.com [3]
1- Wamkumbushe Shahaadah
Imepokelewa toka kwa Abu Sa’iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu Anhu) akisema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Wakumbusheni watu wenu waliokaribia kukata roho “Laa ilaaha illa Allaah”)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (916), Abu Daawuud (3117), An-Nasaaiy (4/5), At-Tirmidhiy (976) na Ibn Maajah (1445)].
Makusudio ya Hadiyth ni kwamba mkumbusheni aliyekaribia kufa "لا إله إلا الله" ili liwe neno lake la mwisho. Ni kama ilivyo kwenye Hadiyth ya Anas ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliingia kwa mtu wa ukoo wa Bani Najjaar ili kumzuru. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: ((Ee khali! Sema "لا إله إلا الله")). Akasema: Je, ni khali mimi au ami? Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: ((Hapana, bali ni khali)). Akamwambia: ((Sema "لا إله إلا الله" )). Akasema: Je, ni bora kwangu? Akasema: ((Na’am)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (3/152, 154, 268)].
Na hii ni kwa matarajio ya kuwa neno lake la mwisho liwe "لا إله إلا الله" kabla ya kufa. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mtu ambaye neno lake la mwisho limekuwa "لا إله إلا الله" ataingia Peponi)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (3100)].
Maulamaa wote kwa pamoja wamekubaliana juu ya ukumbushaji huu. Ukumbushaji huu unatakikana ufanywe kwa upole na taratibu, na wala usikaririwe ili asidhikike. Akidhikika anaweza kulichukia hilo kwa moyo wake kisha akatamka yasiyofaa. Ikiwa atalitamka mara moja, basi asikaririwe tena isipokuwa tu kama atazungumza baada yake jambo jingine. Hapo atakumbushwa tena ili neno lake la mwisho liwe "لا إله إلا الله" . [Sharhu Muslim cha An-Nawawiy (2/580), Al-Majmu’u (5/110) na Al-Mughniy (2/450)].
· Zindusho
Maulamaa wamependezesha kuisoma Suwrat Yaasiyn kwa aliyekaribia kukata roho [Ibn ‘Aabidiyn (2/191), Ad-Dusuwqiy (1/423), Mughnil Muhtaaj (2/5) na Kash-Shaaful Qinaa (2/82)], wakitegemea yaliyosimuliwa kwa njia Marfu’u: ((Wasomeeni watu wenu waliokaribia kukata roho Suwrat Yaasiyn)), lakini ni Dhwa’iyf. Hivyo haiwezi kuruhusu hilo, na Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi.
2- Wamwelekeze Qiblah
Zimehadithiwa jumla ya Hadiyth Mursal zenye kutiliana nguvu kwa ujumla wake na kupanda kufikia ngazi ya Hasan ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipowasili Madiynah, alimuulizia Al-Barraa bin Ma’aruur na watu wakamwambia kwamba ameshafariki, na kwamba aliamuru theluthi ya mali yake apewe Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na aelekezwe Qiblah wakati alipokuwa karibu kukata roho. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Ameipata fitwrah, nami nimeirejesha theluthi yake kwa mwanaye)). Kisha akaenda akamswalia akasema: ((Ee Allaah! Mghufirie na Mrehemu, na Mwingize Pepo Yako, na hakika Ushafanya)). [Hadiyth Hasan kwa Sanad zake: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Haakim (1/353) na Al-Bayhaqiy (3/384). Sheikh wetu katika kitabu cha Al-Ghuslu wal Kafan amesema ni Hadiyth Hasan katika ukurasa wa 22].
Na katika riwaya ya kisa hiki toka kwa ‘Abdul Rahmaan bin ‘Abdullaah bin Ka’ab bin Maalik amesema: “Al-Barraa bin Ma’aruwr alikuwa mtu wa mwanzo kuelekea Qiblah akiwa hai na maiti”.
Kuelekezwa huku Qiblah ni jambo linalopendeza kwa Jamhuri ya Maulamaa, bali An Nawawiy amenukulu Ijma’a juu ya jambo hili, lakini Sa’iyd Al-Musayyib (Allaah Amrehemu) amelikataa. Walipotaka kumwelekeza Qiblah alighadhibika na kusema: “Je, siko Qiblah mimi?” [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na ‘Abdul Razzaaq katika Al-Muswannaf (3/391)].
Ingawa alipinga, lakini wengine walilikubali. Isitoshe, yeye hakupitisha kwa kukata kauli kwamba talqiyn kwa maiti ni bid-’a au ni haramu!! Kisha walichotaka kukifanya kwa Sa’iyd, ni dalili kwamba hilo lilikuwa mashuhuri kwao likifanywa na Waislamu wote kwa wafu wao. [Al-Mughniy (2/451), na Al-Ghuslu wal Kafan uk. 25].
· Namna Ya Kumwelekeza Qiblah
Maulamaa wana njia mbili kuhusiana na namna hii:
1- Alazwe chali miguu yake ikielekea Qiblah, na kichwa chake kinyanyuliwe kidogo ili kiwe mwelekeo wa Qiblah.
2- Alazwe kwa ubavu wake wa kulia uso ukielekezwa Qiblah. [Al-Majmu’u (5/116)].
Namna hii ndiyo yenye nguvu zaidi. Linaloitilia nguvu ni pale Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipomwambia Al-Barraa bin ‘Aazib: ((Ukienda kulala, basi tawadha kama unavyotawadha kwa ajili ya Swalaah, halafu lalia ubavu wako wa kulia. Ukifa, basi utakufa juu ya fitwrah)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (244) na Muslim (2710)].
Ninasema: “Hili linatolewa ushahidi vile vile na Hadiyth ya Ummu Salamah kuhusu kisa cha kufariki Faatimah (Radhwiya Allaahu Anhaa). Inasema: Akalazwa kwa ubavu na akaelekezwa Qiblah, naye akaweka mkono wake chini ya shavu lake. [Isnadi yake ni Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (6/461). Sanad yake ina udhwa’iyf].
Na hii haiwi isipokuwa amelala kwa ubavu. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi”.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Janaazah
002-Wanayoyafanya Waliopo Akishakufa Na Kukata Roho
Alhidaaya.com [3]
1- Wayafunge macho yake
Imepokelewa toka kwa Ummu Salamah akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliingia kwa Abu Salamah macho yake yakiwa yamefunguka, akayafunga, kisha akasema: ((Hakika roho inapotwaliwa, macho huifuatilia)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (920) na Abu Daawuud (3102) kwa ufupi].
Hikma ya kuyafunga macho ni kuwa kama hayakufungwa, uso wa maiti utatisha.
2- Mambo mengine waliyoyataja Mafuqahaa
[Al-Badaai-’i (1/300), Ibn ‘Aabidiyn (2/194), Mawaahibul Jaliyl (2/222), Al-Ummu (1/248), Al-Mughniy (2/451) na Al-Furu’u (2/192)].
(a) Akazwe taya zake mbili kwa kitambaa kipana kifungwe toka juu ya kichwa chake ili taya lake la chini lisilegee, mdomo ukafunguka na kukauka usiweze kufunga.
(b) Vilainishwe viungo vyake na vidole vyake kwa kuukunjia mkono wake kwenye kifupa panya, muundi wake kwenye paja lake, na paja lake kwenye tumbo lake, kisha litakaririwa hilo ili vilainike zaidi na iwe sahali kumwosha na kumsarifu.
(c) Avuliwe nguo ili kisije kikamtoka kitu kitakachomharibu kwa nguo hizo au kumchafua atakapovuliwa.
(d) Alazwe juu ya kitanda na mfano wake ili aweze kuhifadhika zaidi. Asiachwe juu ya ardhi kwani ataharibika haraka.
(e) Awekewe kitu kizito juu ya tumbo lake ili lisifure.
3- Aombewe du’aa
Ni kutokana na Hadiyth ya Ummu Salamah iliyotangulia inayomalizia kwa kusema: “Watu katika jamaa zake wakalalama kwa sauti akasema: Msijiombee wenyewe vibaya ila kwa kheri, kwani Malaika huitikia “aamiyn” kwa yale mnayoyasema”. Kisha akasema: “ Ee Allaah! Mghufirie Abu Salamah, Inyanyue daraja yake ndani ya walioongoka, na Umpe badali mwishoni mwake kwa wenye kubakia, na Utughufirie sisi na yeye ee Mola wa walimwengu wote, na Umkunjulie katika kaburi lake na Umnawirishie humo”.
4- Ufunikwe mwili wake wote kwa nguo
Imepokelewa toka kwa ‘Aaishah: “Kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipofariki, alifunikwa kwa burda la Kiyemen”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1241) na Muslim (942) na tamko ni lake].
5- Maiti ishughulikiwe haraka na itolewe
Imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: (( Iharakisheni jeneza. Ikiwa ni njema, basi ni kheri mnayoitanguliza kwake. Na kama si hivyo, basi ni shari mnayoitua toka shingoni mwenu)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1315) na Muslim (944)].
Kuishughulikia haraka maiti ni pamoja na kuiosha haraka, kuivisha sanda na kuitayarisha, na kuibeba kuipeleka haraka makaburini.
6- Kulipa haraka madeni yake
Ni kwa Hadiyth ya Abu Hurayrah ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Nafsi ya Muumini hufungiwa kwa sababu ya deni lake mpaka alipiwe)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (1078) na wengineo. Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh katika Al-Mishkaat (2915)].
Imepokelewa toka kwa Salamah bin Al-Akwa’a akisema: “ Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliletewa jeneza la maiti, na watu wakamwambia: Ee Rasuli wa Allaah liswalie. Akauliza: ((Je, ameacha deni analodaiwa?)) Wakasema: Ndio. Akauliza: (( Je, ameacha chochote?)) Wakasema: Hapana. Akasema: ((Mswalieni mwenzenu)). Mtu mmoja wa Kianswari aitwaye Abu Qataadah akasema: Mswalie, mimi nitalipa deni lake, naye akamswalia”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (2291) na An-Nasaaiy, na tamko ni lake].
· Yanayojuzu Kwa Waliopo Na Wengineo Kuyafanya Kwa Maiti
1- Kufunua uso wake na kuubusu
Imepokelewa toka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu Anha): “Ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliingia kwa ‘Uthmaan bin Madh’uun akiwa maiti, akaufunua uso wake, kisha akamwinamia na kuubusu. Alilia mpaka nikayaona machozi yakimiminika juu ya mashavu yake”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (3147), At-Tirmidhiy (994) na Ibn Maajah (1456)].
Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Abbaas: “Kwamba Abu Bakr alimbusu Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) baada ya kufariki”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (4457), An-Nasaaiy (4/11) na Ahmad (6/55)].
2- Kumlilia maiti kimya kimya bila sauti wala kelele, bila kulalama, bila kujipiga mashavu na mfano wa hayo
Katika Hadiyth ya Anas kuhusu kisa cha kufariki Ibrahiym mwana wa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamchukua Ibrahiym, akambusu na kumshumu. Kisha baadaye tukaingia hapo alipo na Ibrahiym anakaribia kukata roho, na macho ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) yakaanza kutoa machozi. ‘Abdul Rahmaan bin ‘Awf akasema: “ Na wewe pia (unalia) ee Rasuli wa Allaah?!” Akasema: ((Ibn ‘Awf! Hakika hii ni rahma)). Kisha akaongeza akisema: ((Hakika jicho linatoa machozi, na moyo wahuzunika, nasi hatusemi isipokuwa lenye kumridhisha Mola wetu, na sisi kwa kuondoka kwako ee Ibrahiym, hakika ni wenye kuhuzunishwa)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1303)].
Na alipougua Sa’ad bin ‘Ubaadah, Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alilia, na watu walipomwona analia, nao walilia akasema: ((Hivi hamsikii? Hakika Allaah Haadhibu kwa chozi la jicho, wala kwa huzuni ya moyo, lakini Anaadhibu kwa huu - akaashiria ulimi wake- au Anarehemu. Na hakika maiti huadhibiwa kwa kuliliwa na watu wake)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1304) na Muslim (924)].
Na Jaabir bin ‘Abdullaah aliufunua uso wa baba yake, akamlilia na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) yuko hapo. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy na Muslim].
· Faida Mbili
1- Hakuna ubaya kumlilia tu maiti
Bali linalokatazwa ni kutamka maneno ya kutoridhia Qadari ya Allaah na maombolezo yaliyoharamishwa. Pia hakuna ubaya kuungulika kwa ajili ya maiti wakati anapokaribia kukata roho. Ni kama alivyosema Faatwimah Alayhas Salaam wakati Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuwa karibu kukata roho: Ooh! Masikini baba yangu!!”. Akasema Rasuli: ((Hakuna tena mateso kwa baba yako baada ya leo)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (4462) na Ibn Maajah (1630)].
Ikajulikana kwamba maneno ya Faatwimah si katika maombolezo mabaya, kwa kuwa Rasuli aliyaridhia. [Fat-hul Baariy (7/756). Maktabah ya Salafiyyah].
2- Je, maiti huadhibiwa akililiwa na watu wake au wakimwombolezea?
Katika hili, kuna mvutano kati ya Maulamaa katika Maswahaba na waliofuatia baada yao. ‘Umar bin Al-Khatwwaab na mwanawe ‘Abdullaah na wengineo, walikuwa wanaona kwamba maiti huadhibiwa kwa kuliliwa na watu wake. Lakini ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu Anhaa) amekhalifiana nao akisema: “Rasuli wa Allaah alipita kwa mwanamke wa Kiyahudi ambaye watu wake wanamlilia akasema: ((Hakika wao wanamlilia, naye bila shaka anaadhibiwa ndani ya kaburi lake)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1289) na Muslim (932)].
Nao Jamhuri wanasema kwamba anayeadhibiwa kwa kuliliwa na watu wake, ni yule aliyeusia kwamba aliliwe na aombolezewe baada ya kufa, na wasiya wake ukatekelezwa. Ama anayeombolezewa bila kutoa wasiya, basi huyo haadhibiwi. Na wengine wanasema kwamba bali huadhibiwa kwa kuzembea kwake kuwaelimisha watu wake jambo lililowafanya kufanya hayo, kwani yeye ana jukumu juu ya watu wake. [Jaami’u Ahkaamin Nisaa (1/462) kwa muhtasari].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Janaazah
003-Yanayowapasa Jamaa Wa Maiti – Na Hususan Akina Mama- Inapowajia Habari Ya Kifo
Alhidaaya.com [3]
· Kusubiri, kulirejesha jambo kwa Allaah na kuiridhia Qadhwaa ya Allaah
Allaah Anasema:
(( وَلَنَبْلُوَنَّكُم بِشَيْءٍ مِّنَ الْخَوْفِ وَالْجُوعِ وَنَقْصٍ مِّنَ الْأَمْوَالِ وَالْأَنفُسِ وَالثَّمَرَاتِ ۗوَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ ● الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُم مُّصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّـهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ ● أُولَـٰئِكَ عَلَيْهِمْ صَلَوَاتٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَرَحْمَةٌۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُهْتَدُونَ ))
((Na bila shaka Tutakujaribuni kwa kitu katika khofu na njaa na upungufu wa mali na nafsi na mazao. Na wabashirie wenye kusubiri ● Wale ambao unapowafika msiba husema: “Hakika sisi ni wa Allaah na hakika sisi Kwake ni wenye kurejea” ● Hao zitakuwa juu yao Barakah kutoka kwa Rabb wao na rahmah, na hao ndio wenye kuongoka)). [Al-Baqarah (2:155-157)]
Dada yangu Muislamu! Jua kwamba subira ambayo mtu anastahiki kusifiwa kwayo, ni ile ya wakati anaposhtukizwa na msiba, kinyume na ya baada ya hapo, kwani kwa kupita muda, machungu hupoa. [Ameyanukuu katika Fat-hul Baariy (3/149) toka kwa Al-Khatwwaabiy].
Imepokelewa toka kwa Anas akisema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimpitia mwanamke mmoja akilia mbele ya kaburi akamwambia: ((Mche Allaah na fanya subira)). Akasema: “Achana na mimi, msiba wangu haukuhusu”. Hakumjua kwamba ni Rasuli. Akaambiwa kwamba huyo ni Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), naye moja kwa moja akamwendea na hakukuta kwake walinzi. Akamwambia: Sikukujua. Akasema: ((Hakika subira, ni kwenye kishindo cha mwanzo)). [Al-Bukhaariy (1283) na Muslim (926)].
Imepokelewa toka kwa Ummu Salamah akisema: “Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Hakuna Muislamu yeyote anayepatwa na msiba na akasema yale Aliyoamrishwa na Allaah: Innaa lil-Laahi wainnaa ilayhi raaji’uwna. Ee Allaah! Nilipe katika msiba wangu huu, na Unipe badali iliyo bora kuliko hiyo, isipokuwa Allaah Humpa badali bora zaidi kuliko hiyo)). [Muslim (918) na Abu Daawuud (3115)].
· Yaliyoharamishwa Kwa Wanawake Wa Jamaa Ya Maiti Na Wanawake Wengineo
1- Kuomboleza kwa vilio
Hili ni haramu, kwa sababu hukoleza huzuni na huondosha subira. Pia huenda kinyume na kuiridhia Qadhwaa na kuwa chini ya Amri ya Allaah Mtukufu. [Sharhu Muslim cha An-Nawawiy (2/598)].
Imepokelewa toka kwa Abu Maalik Al ‘Ash-ariy ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Manne katika Umma wangu ni katika mambo ya kijahiliya, hawayaachi: Kujifaharisha kwa aliyonayo mtu au ya wahenga, kudharau nasaba za wengine na kuiona yake ni bora, kuomba mvua kwa nyota na kuomboleza vibaya)). Na amesema: (( Mwanamke mwenye kuomboleza vibaya ikiwa hakutubia kabla hajafa, atasimamishwa Siku ya Qiyaamah avikwe guo la lami na deraya la pele)). [Muslim (934), Ahmad (5/342), Al-Haakim (1/383) na Al-Bayhaqiy (4/63)].
Imepokelewa toka kwa Ummu ‘Atwiyyah akisema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alichukua ahadi kwetu wakati wa bay-’a kwamba tusiomboleze vibaya kwa sauti. Hakulitekeleza hilo mwanamke yeyote kati yetu isipokuwa wanawake watano”. [Al-Bukhaariy (1306) na Muslim (936)].
2,3- Kupiga mashavu na kurarua nguo
Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: (( Si katika sisi aliyejipiga mashavu, aliyerarua nguo kifuani na akaomboleza maombolezo ya kijahilia)). [Al-Bukhaariy (1294) na Muslim (103)].
Kurarua nguo ni mwanamke kuipasua nguo yake kwenye mpasuo wa kifua, na maombolezo ya kijahilia ni kulia kwa sauti, kuelezea mazuri na sifa za aliyekufa na kuomba vibaya. [Hili ni maarufu kwa wanawake. Ni kama anavyosema mmoja wao: Ee simba wangu! Ee ngamia wangu! na mengineyo mashuhuri. Katika Al-Bukhaariy (4268) inaelezwa kwamba ‘Abdullah bin Rawwaah alipoteza fahamu, na dada yake akaanza kulia akisema: “Ee jabali langu! Ee kadha wa kadha!”. Alipozindukana alimwambia: Hakuna ulichosema ila niliambiwa: Je wewe ni kweli uko hivyo? Alipokufa, dada yake hakumlilia”].
4,5- Kunyoa nywele, kuzisambaza na kuzitawanya
Imepokelewa toka kwa Abu Burdah bin Abu Muusa akisema: “ Abu Muusa alihisi maumivu makubwa mno, akapoteza fahamu na kichwa chake kiko juu ya paja la mwanamke mmoja katika jamaa zake. Mwanamke mwingine katika jamaa zake akapiga ukelele, naye hakuweza kumjibisha kwa lolote. Alipozindukana alisema: Mimi niko mbali na yale aliyojiweka mbali nayo Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), kwani Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amejiweka mbali na mwanamke mwenye kupiga makelele wakati wa msiba, mwanamke mwenye kunyoa wakati wa msiba na mwanamke mwenye kurarua nguo wakati wa msiba”. [Al-Bukhaariy kaitolea maelezo (1296) na Muslim (103)].
Na mwanamke mmoja kati ya waliompa Bay-’a Rasuli amesema: “ Kati ya ahadi alizozichukua Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kutoka kwetu katika mema tuliyoyaahidi ya kwamba hatutomwasi, ilikuwa ni: tusiparuze uso, tusiombe mabaya, tusirarue nguo na tusivuruge nywele”. [Abu Daawuud (3131) kwa Sanad iliyo karibu na uzuri].
Kuvuruga nywele ni pamoja na kuzitimuatimua, kuzifumua fumua na kuzinyambuanyambua wakati wa msiba. Na haya pamoja na mengineyo yaliyotangulia ni haramu, inabidi akina mama watahadhari nayo.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Janaazah
004-Kumwosha Maiti
Alhidaaya.com [3]
· Hukmu yake
[Al-Majmu’u (5/128), Al-Ummu (1/243), Al-Muhalla (5/113) na Al Fat-h (3/125)]
Jamhuri ya Maulamaa wanasema kwamba kumwosha maiti ni Fardhi Kifaayah, bali An-Nawawiy kanukulu Ijma’a juu ya hilo!!
Al-Haafidh kasema: “ Na hili ni la kushangaza sana, kwani makhitilafiano katika mas-ala haya ni mashuhuri mno kwa Maalik”.
Dalili za Jamhuri ni hizi:
1- Ni pale Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipomwambia Ummu Salamah pamoja na wanawake walioshirikiana naye katika kumwosha binti yake: ((Mwosheni mara tatu au mara tano)). [Hadiyth Swahiyh: “Takhriyj” yake iko njiani].
2- Neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusiana na mtu aliyehirimia ambaye ngamia wake alimwangusha akavunjika shingo na kufa: ((Mwosheni kwa maji na mkunazi)). [Hadiyth Swahiyh: “Takhriyj” yake iko njiani].
Muktadha wa agizo katika Hadiyth hizi mbili ni wajibu, na hakuna kigeuzi cha kuifanya kuwa Sunnah, na anayesema kwamba ni Sunnah basi hasikilizwi.
3- Ndivyo Waislamu wanavyofanya toka enzi ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mpaka hivi leo
Ninasema: “ Maiti wote wa Kiislamu wa kiume na kike wako sawa katika hili la kuoshwa; mkubwa au mdogo, muungwana au mtumwa, isipokuwa kwa aliyeuawa kishahidi kwenye vita vya kupambana na makafiri kama itakavyokuja kuelezwa mbeleni”.
· Je, Mtoto Wa Mimba Iliyoharibika Ataoshwa?
Mwanamke akiharibikiwa na mimba ya zaidi ya miezi minne, basi kitoto kitaoshwa na kuswaliwa. Na kama ni chini ya miezi minne, basi hakioshwi wala kuswaliwa, bali hutatiwa kwenye kitambaa na kuzikwa. Hii ni kwa vile huwa kishapuliziwa roho baada ya miezi minne, na kabla ya hapo hakiwi ni kiumbe bali huwa kama kitu kisicho na roho na damu, hivyo hakiswaliwi. [Al-Majmu’u (5/256) na Al-Mughniy (2/522)].
· Shahidi Wa Vita Haoshwi
Imepokelewa toka kwa Jaabir bin ‘Abdullaah akisema: “ Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiwakusanya watu wawili katika nguo moja katika maiti wa vita vya Uhud kisha huuliza: (( Ni yupi kati yao aliyehifadhi zaidi Qur-aan?)) Anapoonyeshwa, humtanguliza kwenye mwanandani na husema: ((Mimi ni Shahidi kwa hawa Siku ya Qiyaamah)), kisha huamuru wazikwe na damu zao, hawakuoshwa wala hawakuswaliwa”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1343), Abu Daawuud (3135) na Ahmad (3/128)].
Sababu ya kutooshwa shahidi inaelezwa katika Hadiyth ya Jaabir toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu maiti wa Uhud aliposema: (( Msiwaoshe, kwani kila jeraha –au kila damu- litatoa harufu ya miski Siku ya Qiyaamah)). Hawakuswaliwa. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (3/399). Ina Hadiyth mweza kwa Al-Bayhaqiy (4/11)]. Shahidi asiyeoshwa ni yule aliyekufa akiwa kwenye vita ya kupambana na makafiri sawasawa kwa kuuliwa na kafiri, au kwa kupigwa kimakosa na silaha ya Muislamu, au kwa kudhuriwa na silaha yake mwenyewe, au kwa kuanguka toka juu ya farasi wake, au kwa kukanyagwa na mnyama wake au wanyama wa Waislamu wenzake. Pia kwa kukutwa amekufa baada ya vita kumalizika hata kama sababu ya kifo chake haikujulikana, ni sawa akikutwa na athari za damu au hakukutwa, au akifa papo hapo au akabakia muda hivi kisha akafariki kabla ya kumalizika vita. [Al-Majmu’u (5/261)].
· Shahidi Akiuawa Naye Ana Janaba
Haoshwi pia kwa mujibu wa kauli Swahiyh ya Maulamaa. [Al-Majmu’u (5/26) na Al-Mughniy (2/530)].
Na hii ni kwa mambo mawili:
1- Kwa ujumuishi wa dalili zilizotangulia wa kutooshwa shahidi.
2- Kuacha Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kumwosha Handhwalah bin Abiy ‘Aamir wakati alipouawa na kusema: ((Hakika mwenzenu anaoshwa na Malaika)). Wakamuuliza mkewe akasema: “Yeye alitoka aliposikia mbiu ya vita akiwa na janaba”. [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Haakim (3/204) na Al-Bayhaqiy (4/15). Angalia As-Swahiyhul Musnad Min Fadhwaaili As Swahaabati cha Sheikh wetu (Allaah Amhifadhi)].
Hadiyth hii imetolewa hoja kwamba inajuzu kumwosha kutokana na kitendo cha Malaika. Lakini haifichikani hapa kwamba hoja ni kuwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ndiye aliyeacha kumwosha na si kwa kuwa Malaika walimwosha. Kwa kuwa makusudio yake ni wanadamu kutaabudia kwa hilo, na kama kumwosha kungelikuwa ni wajibu, basi kusingetenguliwa kwa kuoshwa na Malaika.
· Je, Shahidi Aso Wa Vita Huoshwa?
Shahidi aso wa vita kama aliyekufa kwa ugonjwa wa tumbo, tauni, kughariki na kuporomokewa na nyumba, huoshwa na huswaliwa kama maiti wengineo. Hii ni kauli ya Jamhuri ya Maulamaa. [Al-Mughniy (2/536). Ikichelewa mwili wake kunyambuka kwa maji, hatooshwa kwa maji bali atatayamamishwa ikiwezekana. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi].
· Si Lazima Kumwosha Kafiri
Ni sawa akiwa dhimmiy (kafiri aishiye chini ya himaya ya Waislamu) au mwingineyo, kwa kuwa si mtu wa ‘ibaadah wala mtu wa kujitwaharisha.
Lakini inajuzu kwa Muislamu kuwaosha akaribu zake mapagani, au mkewe dhimmiyyat, na kusindikiza jeneza zao na kuwazika, lakini hawaswalii. Na akaribu zake makafiri wana haki zaidi kwake kuliko akaribu zake Waislamu. [Al-Majmu’u (5/144) na Al-Ummu (1/235)].
Ama yaliyosimuliwa kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwamuru ‘Aliy amwoshe baba yake, Sanad zote za Hadiyth hiyo hazina nguvu na hazina mashiko. [Angalia Al-Ghuslu wal Kafan cha Sheikh wetu Mustwafa bin Al-‘Adawiy – Allaah Ainyanyue hadhi yake uk 120].
· Nani Anastahiki Zaidi Kumwosha Maiti?
Imesuniwa maiti aoshwe na mtu wa karibu zaidi katika jamaa zake ikiwa ana sifa na ujuzi wa kuosha. “Kwa kuwa waliomwosha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni ‘Aliy na jamaa zake”. [Hadiyth Swahiyh: Ibn Maajah ameikhariji maana yake (1467), Al-Haakim (1/362) na Al-Bayhaqiy (3/388)].
Imepokelewa toka kwa Saalim bin ‘Ubayd Al-Ashja’iy ya kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipofariki, walimwambia Abu Bakr: “Ee swahibu wa Rasuli wa Allaah! Nani atamwosha?” Akasema: “Ni wanaume wa watu wa nyumba yake; wa karibu zaidi kisha wa karibu zaidi”. Wakauliza: “ Wapi tutamzika?” Akasema: “Mzikeni katika kiwanja ambacho Allaah Amemfisha, Hakumfisha isipokuwa katika kiwanja ambacho yeye anakipenda zaidi”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bayhaqiy (3/395). Katika Sanad yake yuko Suwadah bin Salamah bin Bunayt. Sheikh wetu kasema: “Sikuipitia sera ya maisha yake”].
Shughuli ya kumwosha inaweza kufanywa na wasio akaribu wake (na hasa wakiwa ni wajuzi wa kazi hiyo). Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakuwaamuru akaribu wa binti yake Zaynab kumwosha, bali waliomwosha ni Ummu ‘Atwiyya na wengineo kama itakavyokuja kuelezwa.
· Inajuzu Mume Kumwosha Mke Wake
[Al-Muhalla (5/174), Al-Majmu’u (5/132) na Al-Ummu (1/242)].
Ni kwa Hadiyth ya ‘Aaishah aliposema: “ Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alirejea kwangu siku hiyo toka Baqiy’i kwenye mazishi, nami nahisi maumivu ya kichwa na kulalama kwa maumivu. Akasema: (( Lau hilo likituka ukafa kabla yangu nikakuosha na kukuvika sanda, kisha nikakuswalia na kukuzika)). Nikasema: Lakini mimi au kana kwamba mimi kwako naapa kwa Allaah, laiti ungenifanyia hayo, ukarejea nyumbani kwangu, na ukalala humo na baadhi ya wakezo. Akasema: Rasuli wa Allaah akatabasamu, kisha yakamuanza maumivu yaliyokuwa sababu ya kifo chake”. [Swahiyhun Lighayrihi: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (6/228), Ibn Maajah (1465) Ad-daaramiy (1/37) na wengineo].
Na pia Allaah Mtukufu Amemwita mwanamke wa mtu kwa jina la mke baada ya kufariki Aliposema:
((وَإِن كَانَ رَجُلٌ يُورَثُ كَلَالَةً أَوِ امْرَأَةٌ وَلَهُ أَخٌ أَوْ أُخْتٌ فَلِكُلِّ وَاحِدٍ مِّنْهُمَا السُّدُسُ ۚ))
(( Na ikiwa mwanamume au mwanamke anayerithiwa hana mtoto wala wazazi, lakini anaye kaka au dada, basi kila mmoja kati yao atastahiki sudusi )). [An-Nisaa (4:12)]
Na kwa kuwa hakukuweko kizuizi cha kumwogesha wakati wa uhai wake, basi uhalali wa hilo unaendelea hata baada ya kufariki bila tofauti ya uhai na umauti isipokuwa kwa Aayah au Hadiyth, na hivyo havipo.
An-Nawawiy na Abu Haniyfah wanasema kwamba mwanamume hamwoshi mkewe, kwa kuwa angelitaka, angelimwoa dada yake wakati alipokufa!! Yaliyoelezwa ni hoja inayowarudi.
· Inajuzu Mke Kumwosha Mumewe [Vyanzo vya kifiqhi vilivyotangulia].
Ni kwa Hadiyth ya ‘Aaishah aliyesema: “ Laiti ningelijua jambo hili mwanzoni. Hawakumwosha Rasuli wa Allaah isipokuwa wakeze”. [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (3141) na Al-Bayhaqiy (3/398)].
Al-Bayhaqiy kasema (3/398): “ Nikahuzunishwa na hilo, na halihuzunikiwi ila lenye kujuzu”.
Imepokelewa kwa jumla ya Sanad ya kwamba wakeze Abu Bakri walimwosha kutokana na wasia alioutoa”. [Muswannaf ‘Abdul Razzaaq (6117-6119-6123-6124) na Ibn Abiy Shaybah. Angalia Jaami’u Ahkaamin Nisaa (1/466)].
·Je, Mtu Anaweza Kumwosha Binti Yake?
[Al-Majmu’u (5/151), Jaami’u Ahkaamin Nisaa cha Sheikh wetu (1/475) na nukuu kutoka kwake katika kitabu changu cha Fiqhu As-Sunnat Lin-Nisaa (ukurasa 186)].
Tumeshasema kwamba Ummu ‘Atwiyyah ndiye aliyemwosha binti ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na (Hadiyth itakuja kulizungumzia hilo). Lakini kama hakuna wanawake wa kumwosha maiti, au wakawepo lakini ujuzi wao ni mfinyu, basi hakuna kizuizi chochote kilichoripotiwa cha kumzuia mtu kumwosha binti yake. Mtu kwa binti yake ni kama mwanamume mwenzake kwa upande wa utupu na ufaragha. Haya yameelezewa na baadhi ya watangu wema. Imepokelewa toka kwa Abu Haashim kwamba Abu Qulaabah, alimwosha binti yake. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abiy Shaybah (3/251)].
Hili pia wamelisema Al-Awzaa’iy, Maalik na Ash-Shaafi’iy.
· Wanawake Wanaweza Kumwosha Mtoto Wa Kiume
[Al-Mughniy (2/455) na Al-Majmu’u (5/149)].
Ibn Al-Mundhir kasema: “Maulamaa wote wamekubaliana kwamba mwanamke anaweza kumwosha mtoto mdogo wa kiume”.
Imethibiti toka kwa Hasan kwamba yeye alikuwa haoni tatizo mwanamke kumwosha ghulamu kama asha acha kunyonya akiwa amesitiriwa na kitu. Pia limethibiti hilo toka kwa Ibn Syriyna. [Isnadi zote mbili ni Swahiyh: Zimefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abiy Shaybah (3/251)].
Ninasema: “Mahala pa kujuzu huku ni pale kama mtoto hajafikia umri wa kutamaniwa kimwili na mwanamke. Kama kafikia, basi wanawake hawamwoshi. Hivi ndivyo An Nawawiy alivyoliwekea kidhibiti”.
· Mwanamume Akifa Na Hakuna Wa Kumwosha Isipokuwa Wanawake Peke Yao, Au Mwanamke Na Hakuna Wa Kumwosha Ila Wanaume
Maulamaa wana kauli mbili kuhusiana na hili:
Ya kwanza: Ataoshwa akiwa na nguo.
Ya pili: Atatayamamishwa na haoshwi, kwa kuwa anakuwa katika hukmu ya mtu asiyepata maji.
Imepokelewa kwa njia Mursal toka kwa Makhuwl toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba kasema: ((Mwanamume akifa na hakuna isipokuwa wanawake tu, au mwanamke na hakuna isipokuwa wanaume tu, watatayamamishwa na kuzikwa, nao wako katika hukmu ya mtu asiyepata maji)). [Hadiyth Mursal: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abiy Shaybah (3/413) na Al-Bayhaqiy (3/398)].
Hadiyth hii inatiliwa nguvu na Hadiyth ya Sinaan bin Gharafah –alikuwa na usuhuba- toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusiana na mwanamke anayekufa akiwa na wanaume ambao si maharimu isemayo: ((Hutayamamishwa na haoshwi, na pia mwanaume)). [Al-Bayhaqiy kaitaja (3/398)].
· Sifa Za Mwoshaji
[Al-Ghuslu wal Kafan cha Sheikh wetu (ukurasa 62-65) kwa mabadilisho kidogo].
Mwenye kumwosha maiti ni lazima awe na sifa mbili:
1- Awe mwema mwenye maadili mema
Kwa kuwa mwenye sifa hii, anaijua vyema Mipaka ya Allaah na sharia ya dini yake. Na kwa sifa hii, ataisitiri aibu yoyote ya maiti. Ni kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Mwenye kumsitiri Muislamu, Allaah Atamsitiri Siku ya Qiyaamah)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (2442) na Muslim (2580)].
Pia hatamtusi na mfano wa haya. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Msiwatusi wafu, kwani hakika wao washayafikia waliyoyatanguliza)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1393)].
Kadhalika, atahifadhi siri yake na hatomsengenya. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema kuhusiana na kusengenya: ((Ni kumtaja nduguyo kwa analolichukia)). Na akasema: ((Ikiwa unalolisema analo, basi umemsengenya, na kama hanalo, basi umemzushia)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (2589)].
Imepokelewa toka kwa Raafi’i (Radhwiya Allaahu Anhu) akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mwenye kumwosha maiti akamsitiri aliyonayo, Hughufiriwa mara arobaini. Na mwenye kumkafini maiti, Allaah Atamvisha sun-dus na hariri nzito ya Peponi. Na mwenye kuchimba kaburi la maiti akamsitiri humo, hutiririshiwa malipo kama malipo ya nyumba aliyomweka aishi mpaka Siku ya Qiyaamah)). [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Haakim (1/354-362) na Al-Bayhaqiy (3/395)].
2- Awe mjuzi wa kuosha
Mwenye kuijua kazi ya kuosha, huitekeleza ipasavyo Sunnah ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Humtendea vyema maiti na humwosha itakikanavyo. Na kwa ajili hiyo, Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimpeleka Ummu ‘Atwiyyah ili amwoshe binti yake. An-Nawawiy ameeleza – kwa kumtaja bayana Ibn ‘Abdul Barr – kwamba Ummu ‘Atwiyya alikuwa mwosha maiti za wanawake.
Na hili linatiliwa nguvu ya kwamba: “ ‘Aliy alipotaka kumwosha Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), aliingiza mkono ili atoe uchafu anaotolewa maiti na hakuupata, akasema: Baba yangu ni fidia kwako. Wewe ni mtwaharifu. Ni mtwaharifu ukiwa hai, ni mtwaharifu ukiwa maiti”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Maajah (1467), Al-Haakim (1/362) na Al-Bayhaqiy (3/388)].
Na hapa kuna dalili kwamba ‘Aliy alikuwa ni mjuzi wa kuosha na anajua hali anayokuwa nayo maiti. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi.
Faida:
Mwenye janaba au hedhi anaweza kumwosha maiti kwa kuwa hakuna dalili ya kuzuia hilo. [Al-Majmu’u cha An-Nawawiy (5/187)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Janaazah
005-Sifa Ya Kumwosha Maiti
Alhidaaya.com [3]
Mhimili katika mlango huu ni Hadiyth ya Ummu ‘Atwiyyah (Radhwiya Allaahu Anhaa). Yeye alishiriki kumwosha binti ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), akalihadithia hilo na akalifanya kwa utimilivu. Maswahaba na Maulamaa wa Taabi’iyna huko Basrah, walikuwa wakipata maelekezo toka kwake juu ya namna ya kuosha maiti, na maimamu wakajifunza kutoka kwao.
Imepokelewa toka kwa Ummu ‘Atwiyyah akisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliingia kwetu nasi tunamwosha binti yake (Zaynab). Akatuambia: (( Mwosheni mara tatu au mara tano au zaidi ya hivyo kwa maji na mkunazi, na mwisho mtieni kafuri. Na mkimaliza, basi niiteni)). Tulipomaliza, tulimwita, akaturushia izari yake akisema: ((Mtatieni nayo mwilini)).
Katika tamko jingine: ((Mwosheni kiwitri)). Na jingine: ((Tatu, au tano au saba)). Pia: ((Anzeni kulia kwake na viungo vyake vya wudhuu)). Aidha, Ummu ‘Atwiyyah kasema: “Na tukamchana nywele makuruni matatu”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1254), Muslim (939), Abu Daawuud (3142), An-Nasaaiy (4/32) na Ibn Maajah (1458). Katika mlango huu, kuna Hadiyth ndefu Marfu’u katika konteksi ya sifa ya kuosha maiti toka kwa Ummu Sulaym ambayo iko kwa Al-Bayhaqiy (4/4), lakini ni Dhwa’iyf. Bali Abu Haatim kasema kwenye Al-‘Ilal (1/361): “Kana kwamba ni batili inayofanana kuwa maneno ya Ibn Syriyna. Pamoja na hivyo, washereheshaji wengi wameitegemea].
Vitendo vya kumwosha maiti vinaweza kuelezwa kiufupi kwa mujibu wa yaliyokuja katika Hadiyth ya Ummu ‘Atwiyyah na mengineyo yaliyoelezewa na Maulamaa katika haya yafuatayo: [Al-Ghuslu wal Kafan cha Sheikh wetu (uk. 67 – 105) kwa mabadilisho kidogo na kwa muhtasari].
1- Maiti avuliwe nguo zake na utupu wake usitiriwe
Imepokelewa toka kwa ‘Aaishah (kuhusiana na kisa cha kufariki Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)) akisema: “ Walipotaka kumwosha Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) walisema: Wal-Laahi hatujui. Je, tumvue nguo Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kama tunavyowavua maiti wetu, au tumwoshe na nguo zake?”. [Hadiyth Hasan: “Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (3141), Ahmad (6/267), Al-Haakim (3/59) na Al-Bayhaqiy (3/387)].
Hadiyth inakamilisha ikifahamisha kwamba walikuwa wakiwavua nguo maiti. Lakini pamoja na hivyo, uchi wa maiti ni lazima usitiriwe kutokana na ujumuishi wa neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Mwanaume asiutizame uchi wa mwanaume, wala mwanamke asiutizame uchi wa mwanamke)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (338)]
Na kwa haya, Ibn Syriyna, Abu Haniyfah, Maalik na Ahmad wanasema kwamba maiti husitiriwa uchi (kati ya kitovu na magoti). [Al-Mughniy (2/453)].
2- Mwanamke afumuliwe mistari ya nywele kama amesuka
Ni kwa aliyoyasema Ummu ‘Atwiyyah (katika riwaya ya Al-Bukhaariy 1260 na wengineo): “ Tulifunga makuruni matatu katika kichwa cha binti ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Tulizifumua nywele, tukaziosha, kisha tukaweka makuruni matatu”.
3- Kazi yote ya uoshaji ifanywe kwa upole na utuvu
Ni kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Hakika upole hauwepo katika kitu chochote ila hukipamba, na hauondoshwi kwenye kitu chochote isipokuwa hukiharibu)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (2594)].
Na kwa kuwa pia hishma ya maiti, ni sawa na hishma ya aliye hai. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Kuvunja mfupa wa maiti, ni kama kuvunja mfupa wa aliye hai)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (3207), Ibn Maajah (1616) na Ahmad (6/58)].
4- Maji yachanganywe na mkunazi au sabuni na mfano wake (katika majosho ya mwanzo)
Ni kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Mwosheni kwa maji na mkunazi)).
Na kama kutahitajika maji kupashwa moto ili uchafu uondoke vizuri na mfano wake, basi litafanywa lenye tija zaidi.
5- Uanze kuoshwa upande wake wa kulia na kwenye viungo vyake vya wudhuu baada ya niya na kupiga Bismil-Laah
Ni kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Anzeni kwa upande wake wa kulia, na kwenye viungo vyake vya wudhuu)).
Na hii ni pamoja na kumsukutusha, lakini kama itahofiwa maji kuingia ndani ya mwili na kusababisha mwili kuharibika au kutoka kwenye sanda yake, basi itakuwa bora kupangusa meno yake na pua yake kwa kitambaa cha maji mpaka visafike.
6- Kichwa kioshwe vizuri kwa maji na mkunazi (sabuni) mpaka kwenye maoteo ya nywele, na kisha nywele zichanwe kwa upole
[Al-Ummu (1/249) na Al-Mughniy (2/458)]
Kwa kuwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa katika josho la janaba akiteka mateko matatu na kukipachanisha kichwa chake hadi kufikia kwenye maoteo ya nywele kama ilivyotangulia kwenye mlango wa twahara.
7- Uoshwe upande wa kulia wa mwili wake
Ni kwa kummiminia maji toka ubapa wa kulia wa shingo yake mpaka kwenye unyayo wake wa kulia. Ataosha pia mkato wa kifua, ubavu wake, paja lake, na muundi wake wote wa kulia. Mtu mwingine atautaharakisha mguu ili maji yapenye vizuri kati ya mapaja yake, kisha atachukua maji aoshe upande wa kulia wa mgongo wake. [Al-Ummu (1/249)]
8- Upande wake wa kushoto utafanywa kama ulivyofanywa upande wa kulia
9- Ageuzwe kwa ubavu kisha aoshwe kichogo, mgongo na makalio mawili na yanayofuatia hayo ambayo haikuwezekanika kuoshwa kwa mbele.
10- Achanwe nywele, na nywele za mwanamke zisukwe mikia mitatu.
Mkia mmoja uwepo upande wa kulia wa kichwa, mwingine upande wa kushoto, na wa tatu utosini, na kwa mwanamke nywele zilazwe kwa nyuma. Usukaji mikia utakuwa katika josho la mwisho.
Katika Hadiyth ya Ummu ‘Atwiyya iliyoko kwa Al-Bukhaariy (263): “Tukamsuka makuruni matatu tukailazia kwa nyuma”.
11- Josho likaririwe mara nyingi
Ili asafike na anadhifike vizuri kutokana na neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): (( Au zaidi kama mtaona)). Na imesuniwa iwe kwa hisabu ya witr kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Mwosheni kwa witr)).
12- Kafuri (au miski na mfanowe) iongezwe katika osho la mwisho
Ni kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Na iwekeni mwisho kafuri)), isipokuwa kama maiti ni muhrim, hapo hatawekewa manukato kama itakavyokuja kubainishwa mbeleni.
13- Baadhi ya Maulamaa wanaona kuwa: [Al-Ummu (1/249) na Al-Majmu’u (5/168)].
Baada ya kumwosha, mikono na miguu irejeshwe na kuambatishwa na ubavu wa kulia na kushoto, nyayo zinyooshwe sawa, na kifundo kimoja kiambatishwe na kingine, mapaja yashikanishwe, kisha akaushwe kwa nguo. Wanaona pia akamuliwe kwa ulaini tumboni wakati wa kuoshwa ili kitoke kilichoko humo, na akalishwe mwisho wa kila josho.
14- Mwoshaji asiuguse utupu wa maiti kwa mkono mtupu ila kwa dharura
Aviringishe kitambaa kwenye mkono wake amfute nacho ili asipate kuugusa uchi wake, kwa kuwa kuangalia utupu wake ni haramu, na kuugusa ni haramu zaidi. [Al-Ummu (1/249) na Al-Mughniy (2/457)].
· Je, Kucha Za Maiti Hukatwa Na Nywele Za Kinena Hunyolewa?
[Al-Ghuslu wal Kafan (uk 97), Al-Ummu (1/248) na Al-Majmu’u (5/178)].
Maulamaa wana kauli mbili kuhusu hili:
Ya kwanza:
Linafanywa lile lililokuwa ni fitwrah katika maisha yake. Na kwa kuwa hilo ni usafi, basi ni haki yake ili kuondosha uchafu. Ash-Shaafi’iy kalisema hili katika madhehebu mapya.
Hili linaweza kutolewa dalili kwa Hadiyth ya Abu Hurayrah kuhusu kisa cha kuuawa Khubayb (Radhwiya Allaahu Anhu). Anasema: “ Khubayb akashikiliwa kwao mateka mpaka walipokata shauri la kumuua. Akaazima wembe wa kujinyolea kinena kutoka kwa binti mmoja wa Al-Haarith, naye akampa”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (3989), Ahmad (2/294), Abu Daawuud (2660) na wengineo].
Ni kana kwamba alijinyoa kinena kwa ajili ya kujiandaa na kifo, kwa kuwa yuko mikononi mwa washirikina ambao hawatamfanyia hilo baada ya kufa.
Imepokelewa toka kwa Abu Qulaabah: “Kwamba Sa’ad alimwosha maiti, akaitisha wembe akamnyoa”. [Wapokezi wake wanaaminika: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abiy Shaybah (3/247). Wapokezi wake ni watu madhubuti, na hakuna kinachochelewa isipokuwa Irsaal ya Abu Qulaabah].
Hadiyth kama hii imepokelewa toka kwa Bakr bin ‘Abdallah Al-Mazniy.
Ya pili:
Ni makruhu, kwa kuwa ni kukata sehemu ya mwili wake, ni kama kutahiri. Kayasema haya Al-Mazniy katika wafuasi wa Ash-Shaafi’iy. Na imepokelewa toka kwa Ibn Syriyn: “Kwamba ilikuwa inampendeza mgonjwa anapozidiwa sana, anyolewe sharubu zake, kucha zake na kinena chake. Na kama atafariki, asinyolewe chochote”. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abiy Shaybah (3/246)].
Ninasema: “Linaloonekana imara ni kuwa ikiwa itaonekana kwa maiti nywele iliyokaa vibaya ambayo imesuniwa kuinyoa, basi hakuna ubaya kuinyoa. Cha kuangaliwa katika hili, ni lenye kumfaa maiti. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi”.
· Faida: Zitafanywa Nini Nywele Alizonyolewa Maiti, Au Kucha Alizokatwa, Au Kilichotoka Katika Hivyo?
Maulamaa wengi wamesema kuwa vitawekwa pamoja na maiti na kuzikwa naye. Kuna jumla ya athar zinazozungumzia hili toka kwa Masalaf zilizopo kwa Ibn Abiy Shaybah (3/247). Unaweza kuzipitia.
· Mwanamke Akifariki Na Tumboni Kuna Kitoto Hai
Mwanamke akifariki na ujauzito, kama kuna matumaini ya kuwa kitoto ni hai, basi tumbo litafanyiwa upasuaji ili kitolewe. Na kama hakuna matumaini ya uhai, basi kitaachwa humo humo. Ni kauli ya Hanafiy, Ash-Shaafi’iy, Hanbali na baadhi ya wafuasi wa Maalik. [Al-Fataawaa Al-Hin-diyyah (1/157), Ghaayatul Muntahaa (1/254) na Bulghat As-Saalik (1/232)].
· Mwanamke Akifa Na Hedhi Au Janaba, Ataoshwa Josho Moja Tu
Kwa kuwa akifa, anakuwa hayuko tena ndani ya hukmu za makalifisho, na hana tena ‘ibaadah ya wajibu. Bali kumwosha maiti ni ‘ibaadah ya twa’a, na ili atoke hapa duniani akiwa msafi kabisa na maridadi. Na haya yote hupatikana kwa josho moja tu, na josho hili hutosheleza mawajibiko mawili aliyonayo maiti kama hedhi na janaba. [Al-Mughniy cha Ibn Qudaamah (2/463) kwa mabadilisho kidogo].
· Aliyeosha Maiti, Je Ataoga?
Imesimuliwa toka kwa Abu Hurayrah ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Aliyeosha maiti aoge, na aliyembeba atawadhe)). [Hadiyth Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (3161), Ahmad (2/433), Al-Bayhaqiy (1/303) na wengineo. Sanad zake zote zina kasoro. Angalia Al-Ghuslu wal Kafan (uk. 110 na zinazofuatia). Lakini pamoja na hayo, Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh. Kila mmoja na mtazamo wake].
Hadiyth hii ni Mudhtwarib. Maulamaa wa Hadiyth; Ibn Al-Madiyniy, Ahmad bin Hanbali, Muhammad bin Yahya, Ash-Shaafi’iy, Ibn Al-Mundhir, Al-Bayhaqiy na wengineo, wamesema ni Dhwa’iyf.
Na imesimuliwa toka kwa ‘Aaishah: “Kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akioga kwa mambo manne: Janaba, Siku ya Ijumaa, kuumikwa na kuosha maiti”. [Hii pia Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (3160), naye kasema Dhwa’iyf. Al-Bukhaariy kasema hivyo hivyo kama ilivyo kwa Al-Bayhaqiy (1/302)].
Na katika Hadiyth ya Naajiyah bin Ka’ab (kuhusu kisa cha kufa Abu Twaalib), na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kumwambia ‘Aliy: ((Nenda ukamzike baba yako, na usifanye kitu mpaka unijie)). Akasema: “ Nikaenda, nikamzika, kisha nikamjia. Akaniamuru, nikaoga na akaniombea”. [Kuna ulaini katika Sanad yake. Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (3214), An-Nasaaiy (4/79) na Ahmad. Sanad yake ni Layyin. Je yaweza kuwa Hasan kwa mjumuiko wa Sanad nyinginezo? Hili ni la kutafitiwa. Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh].
Kuna mvutano kuhusu kuizingatia Hadiyth Hasan kwa msingi kwamba haikuelezwa kuwa ‘Aliy alimwosha.
Na kwa haya yaliyotangulia, inabainika kwamba hakuna Hadiyth yoyote toka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) inayothibitisha wajibu wa kuoga baada ya kumwosha maiti, bali iko Hadiyth ya kinyume chake iliyopokelewa na Ibn ‘Abbaas anayesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Si lazima kwenu kuoga kwa kumwosha maiti wenu mtakapomwosha, kwa kuwa maiti wenu si najisi. Inawatosheni kuosha mikono yenu)). [Imetiwa kasoro kwa wakf. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Haakim (1/386) na Al-Bayhaqiy (1/306) ambaye kasema kuwa ni Dhwa’iyf. La sawa ni kuakifiwa kwa Ibn ‘Abbaas].
Hadiyth hii pia imetiwa kasoro, na sahihi ni kuakifiwa kwa Ibn ‘Abbaas.
Alaa kulli haal, Jamhuri ya Maulamaa katika Maswahaba na waliowafuatia, hawaoni wajibu wa kuoga kwa kumwosha maiti, bali wanaliona hilo kama ni jambo la Sunnah. [Al-Ummu (1/235), Al-Majmu’u (5/185) na Ma’alim As Sunan (3/512)].
Hili limethibiti toka kwa Ibn ‘Abbaas, Ibn Mas-’oud, Sa’ad bin Abiy Waqqaas, Ibn ‘Umar na ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu Anhum) kwa Sanad Swahiyh. [Angalia Al-Ghuslu wal Kafan (uk. 120-125)].
Baadhi ya wanachuoni kama Abu Daawuud wamesema kwamba hii ni mansukh baada ya kuileta Hadiyth ya Abu Hurayrah.
· Maji Yakikosekana, Au Yakawa Vigumu Kutumika, Je Maiti Atatayamamishwa
Kama itashindikana kumwosha maiti kwa kukosekana maji, au ikahofiwa kwamba akioshwa atanyumbuka kutokana na kuungua moto na mfano wake, basi atatayamamishwa. Tayamumi hii ni wajibu kwa kuwa ni utwaharisho usiohusiana na kuondosha najisi. Hivyo ni lazima kuuguria kama maji hakuna kama inavyokuwa katika josho la janaba. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Ardhi imefanywa kwangu Masjid na kitwaharishio tukikosa maji)). [Hadiyth Swahiyh: Imetajwa kwenye mlango wa tayammum].
· Maiti Akizikwa Bila Kuoshwa
Jamhuri wamesema ni lazima afukuliwe ili aoshwe kama bado hajaharibika.
Abu Haniyfah kasema kwamba si lazima afukuliwe baada ya kufukiwa!! [Al-Majmu’u (5/300) na Al-Muhalla].
Ninasema: “Hadiyth ya Jaabir inataarifu kwamba inajuzu kumtoa maiti kaburini kwa sababu ya kisharia. Anasema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliliendea kaburi la ‘Abdullah bin Ubayya baada ya kuingizwa shimoni. Akaamuru atolewe, akamweka kwenye magoti yake mawili, akampulizia cheche za mate kwa ulimi wake, na akamvisha nguo yake”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1350) na Muslim (2773)].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Janaazah
006-Kumkafini Maiti
Alhidaaya.com [3]
· Hukmu Yake
'Ulamaa wote wanakubaliana kwamba kumkafini maiti kwa kinachomsitiri ni fardhi ya kutoshelezana. Kuna Hadiyth zenye kutaarifu hilo:
1- Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Abbaas kwamba mtu mmoja aliyehirimia, ngamia wake alimwangusha akavunjika shingo na kufa, na sisi tuko pamoja na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Rasuli akasema: ((Mwosheni kwa maji na mkunazi, mkafinini ndani ya nguo mbili, msimtie manukato na wala msikifunike kichwa chake, kwani Allaah Atamfufua Siku ya Qiyaamah akiitikia talbiyah)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1267) na Muslim (1206)]
2- Khabbaab bin Al-Arath anasema katika Hadiyth yake: “Tulihama pamoja na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa ajili ya Allaah, na malipo yetu yakawa juu ya Allaah. Kati yetu kuna aliyekufa hakula chochote katika malipo yake akiwemo Mus’ab bin ‘Umayr –na kuna mwingine tunda lake limeiva analichuma– aliuawa siku ya Uhud. Hatukupata cha kumkafinia isipokuwa burdah. Tukimsitiria kichwa, miguu yake inabakia wazi, na tukimsitiria miguu, kichwa kinabaki wazi. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akatuamuru tukisitiri kichwa chake na tuweke juu ya miguu yake majani ya mnanaa”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1276) na Muslim (940)].
3- Imepokelewa toka kwa Jaabir bin ‘Abdullah ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikhutubu siku moja. Akamtaja mtu mmoja katika Maswahaba wake aliyekufa na kukafiniwa kwa sanda isiyomwenea, kisha akazikwa usiku. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akakemea kuzikwa mtu usiku mpaka aswaliwe, isipokuwa kama itabidi watu wafanye hivyo. Na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Akimkafini mmoja wenu nduguye, basi amkafini vizuri)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (943), Abu Daawuud (3148) na An Nasaaiy (4/33). Muradi wa kumkafini vizuri ni sanda iwe safi, nzito na yenye kusitiri mwili wote. Haikusudiwi kufuja, kuvuka kiwango kinachotakiwa na kuwa na thamani ya juu sana. Yameelezwa na An-Nawawiy].
· Nani Anayegharamia Sanda?
Maulamaa wengi wanasema kwamba fedha za kugharamia sanda, kumwosha maiti na kuzika, hutolewa toka kwenye mali ya maiti mwenyewe.. Baadhi yao wamelitolea ushahidi hilo kwa Hadiyth ya ‘Abdul Rahmaan bin ‘Awf: “Kwamba siku moja aliletewa chakula chake akasema: Mus-‘ab bin ‘Umayr aliuliwa – naye alikuwa ni mbora kuliko mimi – hakikupatikana anachokimiliki cha kumkafinia isipokuwa burdah”. [Al-Ummu (1/236), Al-Majmu’u (5/188), Al-Muhalla (5/121) na Al-Ghuslu wal Kafan (uk 150)].
Wengi wamesema kwamba itaanzwa sanda, kisha deni halafu wasia, kwa kuwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema kuhusiana na mtu aliyeangushwa na ngamia wake akafa: ((Na mkafinini ndani ya nguo mbili)), na wala hakusaili kama ana deni au la. Hivyo Hadiyth inataarifu kwamba kinachotangulizwa ni sanda kabla ya deni, na wenye kumdai na warithi wake hawana haki ya kuzuia hilo. Na kama hana kitu, basi watatoa wale wenye kumkimu kimaisha, na kama hawako, basi itachukuliwa toka kwenye Baytul Maal. Kama hakuna, basi Waislamu watatoa na imamu atawachangisha wenye uwezo na wale anaoweza kuwasemesha.
Lakini wengine wamesema kwamba deni ndilo linalotangulizwa, kwa kuwa Allaah Hakujaalia mirathi wala wasia isipokuwa katika kile anachokibakisha mtu baada ya kutolewa deni lake. Na kama hana mali, itawalazimu Waislamu wamkafini. Ama kutolea dalili kwa huyo aliyeuawa na ngamia, hili linajibiwa kwa kusema kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa ni mdhamini wa kulipa madeni ya Waislamu kwa neno lake: (( Mimi nawastahikia zaidi Waumini kuliko nafsi zao. Basi mwenye kufa na deni na hakuacha cha kulipia, basi kulipa ni juu yetu sisi, na mwenye kuacha mali, basi ni za warithi wake)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (6731) na wengineo].
Na hii ni kauli ya Abu Muhammad bin Hazm.
· Gharama Za Mke Wa Mtu
Baadhi ya Maulamaa wanasema kwamba gharama za kumkafini na za matayarisho mengineyo zitatolewa na mume wake. [Al-Majmu’u (5/188). Angalia kitabu changu cha Fiqh as Sunnah Lin Nisaai (uk. 189) chapa ya At-Tawfiyqiyyah].
Wengine wamesema kwamba bali hutolewa katika mali yake kama ameacha mali, na mume halazimiki, kwa kuwa mali za Waislamu ni marufuku kuzigusa ila kwa idhini toka kwenye Qur-aan au Hadiyth. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: (( Hakika damu zenu na mali zenu ni haramu juu yenu)). [Hadiyth Swahiyh: Itakuja kwa urefu wake na takhriyj yake kwenye mlango wa Hijjah].
Kilicho wajibu juu ya mume kwa mkewe ni pesa za matumizi ya kila siku, nguo na nyumba. Na kwa lugha Aliyotusemesha nayo Allaah Mtukufu, sanda haiitwi nguo, wala kaburi nyumba. [Al-Muhalla cha Ibn Hazm (5/122)].
Ninasema: “Kauli hii ndiyo yenye nguvu. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi”.
Faida: Inajuzu Mtu Kutayarisha Sanda Yake Kabla Ya Kufa
Imepokelewa toka kwa Sahl bin Sa’ad: “Kwamba mwanamke mmoja alikuja kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na burdah iliyofumwa ikiwa na kitambaa chake cha pembeni na akasema: Nimeisuka kwa mkono wangu na nimekuja ili nikuvike. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaichukua hali ya kuwa anaihitajia. Halafu akatutokea akiwa amejifunga kwa chini, na mtu mmoja akaisifia akisema: Nivishe mimi, ni nzuri mno. Watu wakamwambia: Umefanya vibaya. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kaivaa kwa kuihitajia, na wewe unamwomba na huku unajua kwamba yeye hamkatalii mtu?! Akasema: Mimi wal-Laahi sikumwomba ili niivae, bali nimemwomba ili iwe ni sanda yangu”. Sahl akasema: “Na ikawa ni sanda yake”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1277) na Ibn Maajah (3555)].
· Sifa Ya Sanda:
(a) Sanda ya mwanaume
Imepokelewa toka kwa ‘Aaishah: “Kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikafiniwa kwa nguo tatu nyeupe za Kiyemen toka kijiji cha Sahuol zilizotengenezwa kwa pamba. Hakuna kati yake kanzu wala kilemba”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1264) na Muslim (941)].
Tunajifunza kutokana na Hadiyth hii na nyinginezo kwamba yaliyosuniwa katika sanda ni haya yafuatayo:
1- Iwe nyeupe
Ni kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Vaeni nyeupe katika nguo zenu, kwani hizo ndizo bora ya nguo zenu, na wakafinini kwazo maiti wenu)). [Hadiyth Swahiyh Lighayrihi: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (3878), At-Tirmidhiy (994), Ibn Maajah (1472) na wengineo].
2- Mwanamume akafiniwe kwa nguo tatu.
3- Sanda iwe ya pamba.
4- Isiwepo kanzu wala kilemba.
Hakuna ubaya akikafiniwa kwa kanzu ingawa kuacha ni bora zaidi. Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Umar kwamba alipofariki ‘Abdullah bin Ubayya, mwanawe alikuja kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Nipe kanzu yako nimkafinie, mwombee na mtakie maghfirah. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akampa kanzu yake”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1269) na Muslim (2774)].
Ash-Shaafi’iy kasema katika Al-Ummu (1/236): “ Kama atakafiniwa kwenye kanzu, kanzu itakuwa chini ya nguo, na nguo juu ya kanzu”.
5- Iwe nguo moja kati ya nguo hizo ya mistari au ya rangi.
Imepokelewa toka kwa Jaabir ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Akifa mmoja wenu na akapata chochote, basi akafiniwe kwenye nguo ya mistari)) [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (3150) na Al-Bayhaqiy (3/403). Ibn Ma’iyn kaitia doa kwa aliyojibishiwa. Iko Hadiyth mwenza kwa Ahmad (3/335), na Ibn Abiy Shaybah (3/266) kwa njia nyingine mbili na kuiweka Hadiyth katika hali ya uSwahiyh. Iko kwenye Swahiyh Al-Jaami’i (455)].
6- Sanda itiwe manukato
Imepokelewa toka kwa Jaabir akisema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: (( Mkimfukiza maiti, basi mfukizeni mara tatu)). [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (3/331), Ibn Abiy Shaybah (3/265), Al-Haakim (1/355) na Al-Bayhaqiy (3/405)].
Hili wamelipendelea Maulamaa wengi. Wamesema: “Na kwa vile hii ni ada ya aliye hai ya kujifukiza kwa manukato baada ya kuoga na kubadili nguo, ni hivyo hivyo kwa maiti”. [Al-Mughniy (2/464). Angalia Al-Majmu’u (5/197)].
· Kama Nguo Haikutosha Kusitiri Mwili Wote
Tushaeleza katika Hadiyth ya Khabbaab ikisema : Mus’ab bin ‘Umayr aliuawa siku ya Uhud. Hatukupata cha kumkafinia isipokuwa burdah. Tukimsitiria kichwa, miguu yake inabaki wazi, na tukimsitiria miguu, kichwa kinabaki wazi. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akatuamuru tukisitiri kichwa chake na tuweke juu ya miguu yake majani ya mnanaa”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1276). Tushaieleza nyuma].
Hadiyth hii inatufunza kwamba kama hakikupatikana kabisa cha kumsitiri, basi atasitiriwa mwili wote kwa majani ya mnanaa. Kama hayakupatikana, atasitiriwa kwa majani yaliyopo. [Fat-hul Baariy (3/142)].
· Aliyehirimia Hukafiniwa Kwa Nguo Zake Za Ihraam, Na Kichwa Hakifunikwi
Ni kwa Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas iliyotangulia nyuma. Anasema: “Wakati mtu mmoja akiwa amesimama pamoja na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Arafah, ghafla alianguka toka juu ya ngamia wake akavunjika shingo na kufa. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Mwosheni kwa maji na mkunazi, na mkafinini ndani ya nguo mbili, - au alisema: Ndani ya nguo zake mbili - na wala msikifunike kichwa chake, kwani Allaah Atamfufua Siku ya Qiyaamah akiitikia talbiyah)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1849). Ishaelezwa nyuma].
· Shahidi (Wa Jihaad) Hukafiniwa Kwa Nguo Yake Aliyouawa Nayo Au Nguo Nyingine
Imepokelewa toka kwa ‘Abdullah bin Tha’alabah bin Swafiyr kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema siku ya Uhud: ((Wafunikeni kwenye nguo zao)). [Hasan kwa Sanad zake tofauti: Imefanyiwa “ikhraaj” kwa tamshi hili na Ahmad (5/431) kwa Sanad Layyin. Baadhi ya Maulamaa wamesema ni Dhwa’iyf kwa kuwa inakwendana kinyume na riwaya zake nyinginezo (5/431), na An-Nasaaiy (4/78-6/28) kwa tamshi la: “Wafunikeni na majeraha yao na damu zao”. Ninasema: “Hakuna kuendana kinyume, kwa kuwa matokeo ya matamshi mawili ni mamoja kama inavyoonekana. Isitoshe, Hadiyth hii ina mwenza ya Jaabir kwa Abu Daawuud (3133), na nyingine toka kwa Ibn ‘Abbaas (3134), Ibn Maajah (1515) na wengineo. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi”].
Maulamaa wamekubaliana kwamba inapendeza kuwakafini Mashahidi kwa nguo zao zile zile walizouawa nazo. Na wengi wao wamesema: “Watavuliwa nguo zao endapo kama si desturi ya watu kuzivaa kama ngozi, manyoa na chuma”. [Al-Mughniy (2/531)].
Kati ya yanayotaarifu kwamba inapendeza kuwakafini Mashahidi kwa nguo walizofia nazo lakini si wajibu wa lazima, ni Hadiyth ya Az-Zubayr asemaye kwamba Swafiyyah alipeleka nguo mbili kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) za kumkafinia Hamzah (Radhwiya Allaahu Anhu). Moja akamkafinia Hamza, na nyingine akamkafinia M-answaar ambaye hakuwa na sanda. [Hadiyth Swahiyh kwa Sanad zake tofauti: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (1/165), Al-Bayhaqiy (3/401) na wengineo].
Hadiyth inataarifu kwamba msimamizi ana khiyari. Pia Hadiyth iliyotangulia ya kukafiniwa Musw’ab bin ‘Umayr aliyeuawa katika vita vya Uhud.
(b) Sanda Ya Mwanamke
Sanda ya mwanamke ni sawa na sanda ya mwanamume isipokuwa linalopendelewa zaidi iwe ni nguo tano kwa mujibu wa kauli ya Maulamaa wengi. Hadiyth yenye Isnadi Dhwa’iyf imesimuliwa kuhusiana na hili isemayo kwamba Laylaa binti Qaaif Ath-Thaqafiyyah amesema: “Nilikuwa miongoni mwa waliomwosha Ummu Kulthum binti ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipofariki. Cha kwanza alichotupa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni nguo ya chini (izari), kisha kanzu, halafu mtandio, halafu shuka kisha akaingizwa kwenye nguo ya mwisho. Akasema: “ Na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekaa kwenye mlango akiwa na sanda yake na kuwapa nguo moja baada ya nyingine”. [Hadiyth Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (3157) kwa Sanad Dhwa’iyf].
Ibn Al-Mundhir kasema: “Wengi katika Maulamaa tunaowajua vyema wanasema kwamba mwanamke hukafiniwa kwa nguo tano, na hilo linapendeza kwa kuwa mwanamke katika uhai wake hujisitiri zaidi ya anavyojisitiri mwanaume kutokana na uchi wake kuuzidi uchi wa mwanaume. Na hali ni hivyo hivyo baada ya kufa”. [Al-Mughniy (2/470). Angalia Al-Majmu’u (5/205)].
· Kukafiniwa Mwanamke Kwa Hariri
Inajuzu, kwa vile anaruhusiwa kuivaa wakati wa maisha yake. Lakini ni makruhu kumkafinia kwa kuwa ni israfu inayofanana na ufujaji mali kinyume na anapoivaa wakati yu hai, kwani hujipambia nayo kwa ajili ya mumewe. [Al-Majmu’u (5/197) cha An-Nawawiy].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Janaazah
007-Kubeba Jeneza Na Kulisindikiza
Alhidaaya.com [3]
Kubeba jeneza na kulisindikiza ni kati ya haki za maiti juu ya Waislamu. Ni kwa Hadiyth ya Abu Hurayrah kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Haki za Muislamu juu ya Muislamu ni tano: Kujibu maamkizi, kumzuru mgonjwa, kwenda kuzika, kuitikia wito, na kumtakia rahma aliyekwenda chafya)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1240) na Muslim (2162)].
Na imepokelewa toka kwa Abu Sa’iyd Al-Khudriy kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mtembeleeni mgonjwa, na sindikizeni jeneza, litawakumbusheni aakhirah)). [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (3/27), Al-Bukhaariy katika Al-Adab Al-Mufrad (518), Ibn Abiy Shaybah (4/73) na wengineo].
Maulamaa wamekubaliana kwamba kwenda kuzika ni Fardhi ya Kutoshelezana, wakifanya baadhi, basi wengine waliobaki huwapomokea. Na wengi wao wanasema kwamba kuisindikiza na kuzika ni Sunnah. [Ibn ‘Aabidiyn (1/624), Al-Fataawaa Al-Hin-diyyah (1/159), Al-Fat-hu (3/112) na Sharhu Muslim (1/188)].
Na hii ni kutokana na Hadiyth ya Al-Barraa bin ‘Aazib aliyesema: “ Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alituamuru tusindikize jeneza”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1239) na Muslim (2066)]. Wanasema kwamba agizo hili ni la Sunnah na si la wajibu, kwa Ijma’a!!
Ninasema: “Ikiwa Ijma’a imethibiti, basi imethibiti, na kama haikuthibiti basi hakuna tofauti kati ya hukmu ya kubeba na kuzika, na linaloonekana ni kuwa yote mawili ni Fardhi ya Kutoshelezana. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi”.
· Jeneza Hubebwa Mabegani Mwa Wanaume
Sunnah ni kubebwa jeneza juu ya mabega ya wanaume. Imepokelewa na Abu Sa’iyd Al-Khudriy kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Linapowekwa jeneza, na wanaume wakalibeba juu ya mabega yao, ikiwa ni la mtu mwema husema: Niwahisheni, na kama si la mtu mwema husema: Eh ole wake! Mnakwenda nalo wapi?! Kila kitu huisikia sauti yake isipokuwa mwanadamu, na lau angeisikia angekufa)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1314), An-Nasaaiy (1/270) na Ahmad (3/41)].
Hadiyth hii inatutaarifu kwamba si sharia kwa wanawake kubeba jeneza ni sawa maiti akiwa mwanaume au mwanamke. Hakuna makhitalifiano kabisa katika hili. Kwa kuwa wanawake wanahemewa katika kubeba, na pia kinaweza kuonekana chochote cha miili yao wakati wa kubeba. Zaidi ya haya, wanaweza kulia kwa kelele wakati wa kulibeba na kulitua. Isitoshe, wangeruhusiwa kulibeba, ingelipatikana njia ya kuchanganyika wao na wanaume na kuzua fitna. Hivyo imekuwa ni lazima kwa wanaume tu. [Al-Majmu’u (5/270), Al Fat-hu (3/217) na Jaami’u Ahkaamin Nisaa (1/535)].
· Kuiharakisha Jeneza
Imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: (( Iharakisheni jeneza. Ikiwa ni njema, basi ni kheri mnayoitanguliza kwake. Na kama si hivyo, basi ni shari mnayoitua toka shingoni mwenu)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1315) na Muslim (944)].
Muradi wa kuiharakisha ni kuzidisha zaidi ya mwendo wa kawaida, lakini si kwa kasi inayoweza kuleta madhara kwa maiti, au uzito kwa mbebaji au msindikizaji.
Angalizo:
Si Sharia Kubeba Jeneza Kwa Gari Bali Inatosha Kulibeba Mabegani Kwa Haya Yafuatayo: [Angalia: Ahkaamul Janaaiz cha Al-Imaam Al-Albaaniy – Allaah Amrehemu- (uk. 99) chapa ya Al-Ma’aarif].
1- Hili ni katika ada za makafiri, nasi tumeamuriwa kwenda nao kinyume.
2- Ni bid-’a katika ‘ibaadah sambamba na kukinzana kwake na Sunnah ya kivitendo katika kubeba jeneza.
3- Kunapoteza lengo la kuibeba na kuisindikiza, nalo ni kukumbuka aakhirah.
4- Ni sababu ya kupungua idadi ya wasindikizaji na hususan wasindikizaji hao wakiwa kwenye magari yao.
5- Picha hii haiendani na yaliyo maarufu kuhusu sharia twaharifu samehevu ya kujiweka mbali na urasmi na mwonekano, na hususan kwenye mfano wa jambo hili hatari; mauti.
Ninasema: “Mafuqahaa wameeleza kwamba ni makruhu kubeba jeneza juu ya mgongo wa mnyama bila udhuru. Ama ikiwa ni kwa udhuru kama makaburi kuwa mbali na ikawa uzito kwa watu kulibeba, basi inajuzu. [Ibn ‘Aabidiyn (1/623) na Al-Majmu’u (5/270)].
Na ninasema: “ Inatakikana wakati huo wasimamishe magari na walibebe jeneza wanapofika umbali mwafaka kwa ajili ya kuipata Sunnah na kusudio lake”.
· Kusindikiza Jeneza Kuna Ngazi Mbili
1- Kulisindikiza toka linapotolewa nyumbani kwa watu wa maiti mpaka atakaposwaliwa.
2- Kulisindikiza toka linapotolewa kwa jamaa wa maiti mpaka atakapozikwa. Yote haya mawili Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameyafanya. [Angalia Ahkaamul Janaaiz (uk. 87-88)].
Na bila shaka, ngazi ya pili ni bora zaidi. Imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mwenye kulifuata jeneza [toka nyumbani kwake] mpaka likaswaliwa, basi ana qiyraatw, na mwenye kulifuata mpaka maiti akazikwa, basi ana qiyraatw mbili [za thawabu]. Ikasemwa: Ee Rasuli wa Allaah! Ni nini qiyraatw mbili? Akasema: ((Ni mfano wa milima miwili mikubwa)). Na katika riwaya nyingine: ((Kila qiyraatw ni mfano wa Uhud)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1325) na Muslim (945)].
· Ni Marufuku Wanawake Kusindikiza Jeneza
Fadhla hiyo iliyotajwa ya kusindikiza jeneza ni kwa wanaume tu na si kwa wanawake, kwa kuwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amewakataza kufanya hivyo. Ummu ‘Atwiyyah amesema: “Tulikatazwa kusindikiza jeneza, lakini hatukukaziwa sana”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1278) na Muslin (938)].
Jamhuri ya Maulamaa wamelichukulia katazo hili juu ya ukaraha na si uharamu. [Al-Majmu’u (5/277), Fat-hul Baariy (2/599) na Ibn ‘Aabidiyn (1/208)] Ni kutokana na neno lake: “Hatukukaziwa sana”.
Lakini, Sheikh wa Uislamu katika Al-Fataawaa (24/355) amesema: “Huenda muradi wake ni kuwa katazo halijasisitizwa kwa uzito, na hii haikanushi uharamishaji. Huenda yeye amedhani kwamba si katazo la uharamishaji, lakini nguvu ya hoja inabakia ndani ya kauli ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na si kwenye dhana ya mtu”.
· Ni Upande Gani Wa Jeneza Wasindikizaji Wanakuwa?
Inafaa kwenda nyuma au mbele ya jeneza, kuliani au kushotoni karibu nalo. Anas (Radhwiya Allaahu Anhu) anasema: “ Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), Abu Bakr na ‘Umar, walikuwa wakitembea mbele ya jeneza na nyuma yake”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Maajah (1483), At-Twahaawiy (1/278), nayo iko kwa Abu Daawuud (3179), At-Tirmidhiy (1007) na An-Nasaaiy (4/56) bila ya (nyuma yake). Angalia Al-Irwaa (739)].
Lakini bora ni kutembea nyuma yake kwa mujibu wa Hadiyth zenye kuamuru kusindikiza jeneza. Linatiliwa nguvu na kauli ya ‘Aliy bin Abi Twaalib (Radhwiya Allaahu Anhu) isemayo: “ Kutembea nyuma yake ni bora kuliko kutembea mbele yake, ni kama fadhla ya Swalaah ya mtu kwa Jamaa na kuswali peke yake”. [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abiy Shaybah, (4/101), Ahmad (1/97) na Al-Bayhaqiy (4/25). Al-Haafidh kasema ni Hasan, na ina hukmu ya Umarfu’u].
Na hii ni kauli ya ya Al-Awzaa’iy, Abu Haniyfah na Is-Haaq kinyume na Jamhuri. [Al-Ummu (1/240), Bidaayatul Mujtahid (1/344), na Fat-hul Baariy (3/219)].
Inajuzu kwa wasindikizaji kupanda lakini wawe nyuma ya jeneza kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Mwenye kupanda atembee nyuma ya jeneza, na mwenye kutembea popote atakapo pa jeneza)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (3180), At-Tirmidhiy (1031), An-Nasaaiy (1/275) na Ahmad (4/247)].
Ingawa kupanda kunajuzu, lakini kutembea ni bora zaidi kwa kuwa hilo limezoeleka kufanywa na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Thawbaan (Radhwiya Allaahu Anhu) anasimulia: “Kwamba Rasuli wa Allaah aliletewa mnyama – akiwa na jeneza – akakataa kumpanda. Alipomaliza, aliletewa mnyama akampanda, akaulizwa akasema: (( Hakika Malaika walikuwa wanatembea, na haikunifalia kupanda na wao wanatembea. Walipoondoka, nilipanda)). [Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (3177), Al-Haakim (1/355) na Al-Bayhaqiy (4/23). Angalia Ahkaamul Janaaiz (uk. 97)].
· Adabu Za Kusindikiza Jeneza
1- Kutolisindikiza kwa chetezo au moto
Mafuqahaa wamekubaliana kwamba jeneza halisindikizwi kwa moto wa mwenge (chetezo) wala mshumaa au mfano wa hivyo ila kama vitahitajika kwa ajili ya mwanga. Ni kwa Hadiyth ya Abu Hurayrah toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) isemayo: ((Jeneza halisindikizwi kwa sauti wala moto)). [Al-Albaaniy kaipa nguvu kwa Hadiyth wenza: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (3171) na Ahmad (2/427). Angalia Ahkaamul Janaaiz (uk. 91)].
Sanad yake ina walakin isipokuwa inapata nguvu kwa aliyoyasema ‘Amri bin Al-‘Aaswiy katika wasia wake: “Nikifa, asinisindikize mwanamke mwombolezaji wala moto”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (121) na Ahmad (4/199)].
Imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu Anhu) kwamba alisema mauti yalipomwadilia: “Msinijengee hema, wala msinisindikize kwa mwenge (na katika riwaya nyingine: Kwa moto)”. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (2/292)].
Na imepokelewa toka kwa Abu Muusa kwamba aliusiua wakati mauti yalipomwadilia akisema: “ Mkiondoka na jeneza langu, basi nikazieni mwendo, na wala msinisindikize kwa kijinga cha moto”. [Isnadi yake ni Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Maajah (1487), Ahmad (4/397) na Al-Bayhaqiy (3/395)].
2- Kulisindikiza kimya kimya
Haijuzu kulisindikiza jeneza kwa sauti, si kwa dhikri wala kwa jingine lolote. Imepokelewa toka kwa Qays bin ‘Ubbaad akisema: “Maswahaba wa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) walikuwa wanachukia sauti kunyanyuliwa kwenye majeneza”. [Wapokezi wake wanaaminika: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bayhaqiy (4/74) na Ibn Mubaarak katika Az-Zuhd (83)].
Kunyanyua sauti ni kujishabihishana Manaswara. Wao hunyanyua sauti kw kusoma sehemu ya Biblia yao na nyiradi zao kwa kuvuta sauti, kwa mahadhi na kwa mdundo wa kugusa huzuni.
An-Nawawiy kasema kwenye Al-dhkaar (uk. 203): “Jua kwamba sahihi ni lililokhitariwa, na ukimya waliokuwa wakiufanya Masalaf (Radhwiya Allaahu Anhum) wakati walipokuwa wakilipeleka jeneza. Sauti hainyanyuliwi kwa kisomo, wala dhikri wala kwa jingine lolote lile. Na hikma ya hilo iko wazi, nayo ni kuwa ukimya hutuliza mawazo ya mtu, na huijumuisha akili yake kufikiria kuhusu mauti. Na hili ndilo linalotakikana katika hali hii, na hii ndio haki. Basi usidanganyike na wengi wenye kwenda kinyume na hili”.
Ninasema: “Ama waliyoyazoea watu ya kuleta dhikr mbele ya jeneza katika zama zetu za leo, au mmoja wao kusema: “Wahhiduuh” (Mpwekesheni!) na wasindikizaji kumwitikia, au kusema: “Mshuhudilieni!!”, hayo ni bid-’a kama walivyoeleza Mafuqahaa. [Ibn ‘Aabidiyn (1/608), Ash-Sharhu As-Swaghiyr (1/229), na Mughnil Muhtaaj (1/247)].
Al-Albaaniy kasema: [Ahkaamul Janaaiz (uk. 92) chapa ya Al-Ma’aarif (1412H = 1992)] “Baya zaidi ya hilo, ni kusindikiza jeneza kwa kupiga ala za muziki mbele yake kwa mahadhi ya mguso wa huzuni kama inavyofanywa katika baadhi ya nchi za Kiislamu kwa kuwaiga makafiri. Allaahul-Musta’anu”.
3- Wasindikizaji wasiketi kabla ya jeneza kuwekwa chini
Imepokelewa toka kwa Abu Sa’iyd kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mkiliona jeneza basi simameni, na mwenye kulisindikiza asikae mpaka liwekwe)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1310) na Muslim (959)].
Muradi ni mpaka walitue toka mabegani kuliweka chini, na wengine wanasema mpaka maiti atiwe kwenye mwanandani.
Maswahaba wengi pamoja na Taabi’iyna wamesema ni vizuri zaidi watu wasimame mpaka jeneza iwekwe chini kama alivyonukuu Ibn Al-Mundhir. Ni kauli ya Al-Awzaa’iy, Ahmad, Is-Haaq na Muhammad bin Al-Hasan. Imekhitariwa na Ash-Shaafi’iy. [Fat-hul Baariy (3/213), Al-Majmu’u (5/280) na Al I-’itibaar cha Al-Haazimiy (uk. 138)].
4- Je, mtu asimame jeneza likipita?
[Fat-hul Baariy (3/216), Al-Majmu’u (5/280), Al I-‘itibaar (uk. 138), Al-Fataawaa Al-Hin-diyyah (1/160) na Al-Muhalla (5/…)].
Imepokelewa toka kwa ‘Aamir bin Rabiy-’ah toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Mkiliona jeneza basi simameni mpaka liwapite [au liwekwe chini] )). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1307) na Muslim (958)].
Na Jaabir bin ‘Abdullah amesema: “ Lilitupitia jeneza, na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akalisimamia, nasi pia tukalisimamia. Tukasema: Ee Rasuli wa Allaah! Ni jeneza la Myahudi. Akasema: ((Mkiliona jeneza, basi simameni)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1311) na Muslim (960)].
Na katika tamshi toka kwa Sahl bin Haniyf na Qays bin Sa’ad: ((Je, si nafsi?)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1312) na Muslim (961)].
Lakini, Maulamaa wengi wakiwemo Maimamu wanne na wengineo, wanasema kwamba kulisimamia jeneza kumenasikhiwa na Hadiyth ya ‘Aliy bin Abiy Twaalib aliyesema: “Rasuli wa Allaah alilisimamia jeneza nasi tukasimama, kisha akakaa nasi tukakaa”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (962), Ibn Maajah (1544) na Ahmad (1/13)].
Na katika tamshi jingine: “Kisha alikaa baada ya hapo, na akatuamuru tukae”. [Al-Albaaniy kasema ni Hadiyth Hasan. Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (1/82) na At-Twahaawiy (1/282). Angalia Ahkaamul Janaaiz (uk. 101)].
Ibn Hazm, Ibn Habiyb na Ibn Al-Maajithuna katika wafuasi wa Maalik na baadhi ya wafuasi wa Ash-Shaafi’iy ikiwa pia ni chaguo la An-Nawawiy, wanasema kwamba kukaa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) baada ya kuamuru kusimama, ni kubainisha kujuzu, na kwamba amri ilikuwa ni ya Sunnah, na naskh haifanyi kazi hapa isipokuwa ikishindikana kukusanya, na hapa inawezekana.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Janaazah
008-Swalaah Ya Janaazah
Alhidaaya.com [3]
· Hukmu Yake:
Kumswalia maiti ni Fardhi ya Kutoshelezana (wakiifanya baadhi ya Waislamu, itawapomokea wengine), Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameliamuru hilo. Imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiletewa mtu aliyefariki mwenye deni naye anauliza: ((Je, ameacha ziada kwa deni lake?)) Akiambiwa kwamba ameacha cha kulipia humswalia, na kama hakuacha, huwaambia Waislamu: ((Mswalieni mwenzenu)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1251) na An-Nasaaiy (1960)].
Imepokelewa toka kwa Zayd bin Khalid Al-Juhaniy: "Kwamba mtu mmoja katika Maswahaba wa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alifariki Siku ya Khaybar, wakaitaja habari ya kifo kwa Rasuli, naye akasema: ((Mswalieni mwenzenu)). Nyuso za watu zikabadilika kwa kauli hiyo. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Hakika mwenzenu amedokoa katika mali ya Allaah)). Tukapekua mzigo wake, tukakuta sindano katika sindano za Mayahudi za kushonea ngozi haifiki dirhamu mbili. [Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Maalik katika Al-Muwattwaa (2/14), Abu Daawuud (2710), An-Nasaaiy (4/64), Ibn Maajah (2848) na Ahmad (4/114, 5/192). Angalia Al-Irwaa (726)].
· Fadhla Yake:
Imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mwenye kuhudhuria Swalaah mpaka janazah ikaswaliwa, basi huyo ana qiyraatw. Na mwenye kuihudhuria mpaka akazikwa, basi ana qiyraatw mbili)). Akaulizwa: "Ni nini qiyraatw mbili?" Akasema: (( Ni mfano wa milima miwili mikubwa)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (945)].
Imepokelewa toka kwa ‘Abdullah bin ‘Abbaas: “Kwamba mwanawe alifariki huko Qudayd – au ‘Asafaan – akasema: Ee Kurayb! Angalia watu waliomkusanyikia. Nikatoka, na nikawakuta watu wamekusanyika kwa ajili yake nikamweleza. Akasema: Unasema wao ni arobaini? Nikasema: Na’am. Akasema: Basi mtoeni, kwani mimi nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Hakuna mtu yeyote Muislamu anayekufa, wakasimama watu arobaini wasiomshirikisha Allaah na chochote kumswalia, isipokuwa Allaah Huwakubalia shufaa yao kwake)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (948)].
Na imepokelewa toka kwa ‘Aaishah toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Hakuna maiti yeyote anayeswaliwa na Umma wa Waislamu wanaofikia mia moja wote wanamtakia shufaa, isipokuwa hukubaliwa shufaa yao kwake)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (947)].
· Wapi Asimame Imamu Kulielekea Jeneza
Kauli ya kwanza:
Asimame imamu mkabala wa kichwa cha mwanamume, na mkabala wa kiuno cha mwanamke. Ni kauli ya Ash-Shaafi’iy, Ahmad na Is-Haaq. [Al-Majmu’u cha An-Nawawiy (5/225)].
Baadhi ya Mahanafi wameikhitari kauli hii. [Al-Hidaaya (1/462), na Sharhul Ma’aaniy (1/284)].
Ash-shawkaaniy kasema ni haki.
Wametoa dalili kwa Hadiyth ya Anas bin Maalik: "Ya kwamba Abu Ghaalib Al-Khayyaat alisema: Nilimshuhudia Anas bin Maalik akiliswalia jeneza la mtu. Akasimama mkabala wa kichwa chake (katika riwaya nyingine: [Kichwa cha As Surayr]. Lilipoondoshwa, lililetwa jeneza la mwanamke wa Kikureshi – au wa Kianswaar - akaambiwa: Ee Abu Hamzah! Hili ni jeneza la fulanah binti fulanah, basi mswalie. Akamswalia na akasimama mkabala wa kiuno chake. [Na katika riwaya nyingine: Kwenye bamba lake, na amefunikwa jeneza la kijani]. Alikuwa pamoja nasi Al-'Alaa bin Ziyaad Al-'adawiy. Alipoona kutofautiana sehemu aliposimama Anas kwa mwanamke na mwanamume alisema: Ee Abu Hamzah! Je, ndivyo hivi alikuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anasimama hapo uliposimama, na kwa mwanamke uliposimama? Akasema: Na’am. Al-'Alaa akatugeukia akasema: Hifadhini”. [Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (3194) na At-Tirmidhiy (1034). Waliosema ni Hasan ni Ibn Maajah (1494), Ahmad (3/118, 204), Al-Bayhaqiy (4/33) na At-Twayaalsiy (2149). Angalia Ahkaamul Janaaiz cha Al-Albaaniy (uk. 138)].
Pia kuna Hadiyth ya Samrah bin Jun-dub aliyesema: "Niliswali nyuma ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), akamswalia Ummu Ka'ab ambaye alikufa akiwa na nifasi, Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasimama kiunoni mwake kumswalia". [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1332) na Muslim (964) na tamko ni lake].
Ya pili:
Asimame mkabala wa kifua cha maiti sawasawa akiwa mwanamume au mwanamke. Wameijibu Hadiyth ya Anas iliyotangulia wakisema kwamba sababu ya wao kusimama mkabala wa kiuno cha mwanamke ni sitara kwa kuwa hakukuweko majeneza. Wametolea ushahidi hilo kwa ziada aliyoisimulia Abu Daawuud katika Hadiyth ya Anas. Ziada inasema: " Abu Ghaalib akasema: Nikauliza kuhusu kitendo cha Anas cha kusimama mkabala wa kiuno cha mwanamke. Wakanieleza kwamba sababu ni kutokuweko majeneza, imamu alikuwa anasimama mkabala wa kiuno chake ili kumsitiri na wanaume". [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (3194)].
Sheikh Al-Albaaniy ameijibu kauli ya Mahanafi akisema kwamba sababu waliyoitoa inakataliwa kwa hoja zifuatazo:
Kwanza: Aliyeleta sababu hiyo hajulikani, na linalokuwa hivyo halina thamani.
Pili: Inapingana na aliyoyafanya msimulizi mwenyewe wa Hadiyth ambaye ni Anas (Radhwiya Allaahu Anhu). Yeye alisimama mkabala wa kiuno na maiti yuko ndani ya jeneza, na hili linaonyesha kwamba sababu hiyo ni batili. [Angalia Ahkaamul Janaaiz Wabidaaihaa cha Al-Albaaniy ukurasa wa 139 kwenye footnote].
Ibn Hazm kasema kwenye Al-Muhalla: "Maiti huswaliwa na imamu anayesimama na kuelekea Qiblah, na nyuma yake watu katika safu. Kwa mwanamume anasimama kwenye kichwa chake, na kwa mwanamke kwenye kiuno". [Al-Muhalla cha Ibn Hazm (5/123)].
· Imesuniwa Wapange Safu Tatu Nyuma Ya Imamu Hata Kama Watu Ni Kidogo
Ni kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): (( Hakuna maiti yeyote anayekufa na akaswaliwa na safu tatu za Waislamu, isipokuwa [Allah] Huwajibisha [Pepo]). [Al-Albaaniy kasema ni Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (3150), At-Tirmidhiy (1033), na Ibn Maajah (1490)].
Na kila watu wanavyozidi, ndivyo inavyokuwa faida zaidi kwa maiti kwa neno lake Rasuli: ((Hakuna maiti yeyote anayeswaliwa na Umma wa Waislamu wanaofikia mia moja wote wanamtakia shufaa, isipokuwa hukubaliwa shufaa yao kwake)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (947), At-Tirmidhiy (1034), na An-Nasaaiy (4/75)].
· Maiti Za Wanaume Na Wanawake Zikikusanyika Wakati Mmoja
Ikikusanyika maiti zaidi ya moja kati ya wanaume na wanawake, imamu anaweza kuiswalia kila maiti peke yake, na pia inajuzu kuwaswalia wote kwa Swalaah moja. Majeneza yatapangwa moja baada ya jingine ili maiti wote wawe mbele ya imamu. Maiti za wanaume zitawekwa mbele yake, na za wanawake zitafuatia upande wa Qiblah.
Imepokelewa toka kwa Naafi'i ya kwamba Ibn 'Umar aliswalia majeneza tisa kwa pamoja. Akazipanga maiti za wanaume mbele ya imamu na za wanawake safu moja upande wa Qiblah. Majeneza ya Ummu Kulthum bint 'Aliy mke wa 'Umar bin Al-Khattwaab na mwanawe aitwaye Zayd yaliwekwa pamoja, na imamu siku hiyo alikuwa ni Sa'iyd bin Al-'Aaswiy, na watu wengine ni pamoja na Ibn 'Umar, Abu Hurayrah, Abu Sa'iyd, na Abu Qataadah. Maiti ya Zayd ikawekwa mbele ya imamu na mtu mmoja akasema: Nikalipinga hilo. Nikamwangalia Ibn 'Abbaas, Abu Hurayrah, Abu Sa'iyd na Abu Qataadah nikawauliza: "Nini hii?". Wakaniambia: "Ni Sunnah". [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na An-Nasaaiy (4/71), Ad-daaraqutwniy (2/79), Al-Bayhaqiy (4/33) na ‘Abdul Razzaaq (6337)].
· Inajuzu Wanawake Kuswalia Maiti
Inajuzu wanawake kumswalia maiti ikiwa hawataifuata kule iliko, bali ikasadifiana kuwepo kwao pale anaposwaliwa maiti. Imepokelewa toka kwa ‘Abdullah bin Az Zubayr: "Kwamba 'Aaishah aliamuru jeneza la Sa'ad bin Abi Waqqaas lipitishwe Msikitini ili apate kumswalia. Watu wakampinga hilo, naye akasema: Watu wanasahau haraka hivyo! Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakumswalia Suhayl bin Al-Baydhwaa isipokuwa Msikitini". [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (973), Abu Daawuud (3173) na An-Nasaaiy (4/68)].
· Faida
Hadiyth hii inatueleza kwamba inajuzu kumswalia maiti ndani ya Msikiti, lakini lililo bora zaidi ni kumswalia nje ya Msikiti kwenye sehemu maalumu iliyoandaliwa kwa hilo. Hii ilikuwa ndio hadyi ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na alikuwa akifanya hivyo mara nyingi. [Al-Wajiyz (uk. 174)].
· Je, Baadhi Ya Viungo Vya Maiti Huswaliwa?
Kuna athar zilizosimuliwa ambazo ziko kati ya udhwa’iyf na irsaal toka kwa baadhi ya Maswahaba ya kwamba waliviswalia baadhi ya viungo vya maiti.
Khalid bin Mu'udaan anasema kwamba Abu 'Ubaydah aliviswalia vichwa huko Sham. [Mursal: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abiy Shaybah (4013) na Al-Bayhaqiy (4/18)].
Inasimuliwa toka kwa Abu Ayyuub kwamba aliuswalia mguu. [Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abiy Shaybah (3/40)].
Inasimuliwa kuwa 'Umar aliiswalia mifupa huko Sham. [Mursal: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abiy Shaybah (3/41)].
Kuna jumla ya kauli tatu zilizosemwa na Maulamaa katika mas-ala haya:
Ya kwanza: Huswaliwa, sawasawa vikiwa ni kidogo au vingi. Ni kauli ya Ash-Shaafi'iy na Ahmad. [Al-Majmu’u cha An-Nawawiy (5/214)]. Ibn Hazm kasema hivyo hivyo. [Al-Muhalla cha Ibn Hazm (5/214)].
Ya pili: Ikiwa itapatikana zaidi ya nusu ya mwili wake, basi itaoshwa na kuswaliwa. Na kama itapatikana nusu tu, basi haioshwi wala kuswaliwa. Ni kauli ya Abu Haniyfah.
Kauli ya Maalik iko karibu na hii. Anasema kwamba viungo vichache haviswaliwi. [Al-Majmu’u cha An-Nawawiy (5/214)].
Ya tatu: Haviswaliwi kwa hali yoyote ile. Ni kauli ya Daawuud. [Al-Majmu’u cha An-Nawawiy (5/214)].
Ninasema: " Naona nafsi yangu inanivuta kuniambia kuwa ikiwa hakuswaliwa, basi vitaoshwa, vitaswaliwa na vitazikwa. Na ikiwa maiti aliswaliwa kisha baadhi ya viungo vyake vikapatikana, basi havitaswaliwa, bali vitaoshwa na kuzikwa. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi".
· Kiungo Cha Aliye Hai Hakiswaliwi
Haikunukuliwa toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) au Maswahaba kwamba walikiswalia kiungo kilichokatika cha mtu hai. Kuna habari nyingi za uhakika kutoka kizazi hadi kizazi zinazoeleza kwamba adhabu zilitekelezwa wakati wa enzi ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Maswahaba baada yake, na mikono ilikatwa. Haikuelezwa kwamba waliosha au kuswalia kiungo chochote katika hivyo. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi.
· Kumswalia Mtoto Wa Mimba Iliyoharibika Na Mtoto Mdogo
Kwanza: Mtoto
Tunamaanisha ambaye bado kubaleghe, huyu ni sharia kumswalia. Imepokelewa toka kwa 'Aaishah akisema: " Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliletewa mtoto mdogo katika watoto wa wakazi wa Madiynah akamswalia. Nikasema: Pepo imthibitikie huyu. Ndege katika ndege wa Peponi, hakufanya baya na wala hakubaleghe. Akasema: ((Au lipo jingine ya hilo ee ‘Aaishah? Allaah 'Azza wa Jalla Ameumba Pepo, na Akaiumbia watu wake, na Akawaumba kwenye migongo ya baba zao, na Akaumba moto, na Akauumbia watu wake, na Akawaumba kwenye migongo ya baba zao)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (2662), An-Nasaaiy (1/76) na tamko ni lake, na Ahmad (6/208)].
Pili: Mtoto wa mimba iliyoharibika
Hakuna makhitalifiano kati ya Maulamaa kwamba mtoto wa mimba iliyoharibika akilia wakati anazaliwa au akapiga chafya, huswaliwa. Ibn Al-Mundhir kasema: "Wamekubaliana wote kwamba mtoto akijulikana yu hai au akilia wakati anazaliwa, basi huswaliwa. [Al-Ijma’a ukurasa wa 30].
Lakini makhitalifiano yako kati yao ikiwa mtoto hakulia wakati anazaliwa:
Baadhi yao wamesema kwamba haswaliwi. Hilo limesimuliwa toka kwa Jaabir bin ‘Abdullaah. Pia ni kauli ya Az-Zuhriy, Ath-Thawriy, Al-Awzaa'iy, Maalik, Ash-Shaafi'iy na Aswhaab ar raay. [Sharhu As-Sunnah cha Al-Baghawiy (5/373)].
Wanatoa dalili kwa yaliyosimuliwa na Jaabir bin ‘Abdullah na Al-Musuur bin Makhramah kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: (( Mtoto harithi mpaka alie anapozaliwa)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (1032), An-Nasaaiy katika Al-Kubraa (6358, 6359), Ibn Maajah (1508, 2750, 2751), Ad-daaramiy (4126), Ibn Abiy Shaybah (11603), ‘Abdul Razzaaq (6608), Ibn Hibaan (6032), Al-Haakim (4/348), (1/363) na Al-Bayhaqiy (4/8)].
Na Hadiyth ya Abu Hurayrah kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mtoto akilia anapozaliwa, hurithi)). [Kuna udhwa’iyf katika isnadi yake: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (2920)].
Lakini Maulamaa wengine wamesema kwamba huswaliwa. Linasimuliwa hilo toka kwa Ibn 'Umar na Abu Hurayrah. Pia limesemwa na Ibn Syriyna, Ibn Al-Musayyib, Ahmad na Is-Haaq. [Sharhus Sunnah cha Al-Baghawiy (5/373)]. Wametoa dalili kwa Hadiyth ya Al-Mughiyrah bin Shu-'ubah ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mtoto wa mimba iliyoharibika huswaliwa, na mzazi wake huombewa maghfirah na rahma)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (1031), An-Nasaaiy (4/358,360), Ibn Maajah (1507), Ahmad (4/247, 249) na wengineo].
Is-Haaq ameijibu dalili ya kundi la kwanza akisema: "Hakika mirathi ni kwa kulia mtoto anapozaliwa. Ama Swalaah, bila shaka huswaliwa kwa kuwa ni kiumbe kilichoandikiwa hatima mbaya ya naqama au hatima njema ya furaha.” [Sharhu As-Sunnah cha Al-Baghawiy (5/373)].
Al-Khattwaabiy kanukuu toka kwa Ahmad bin Hanbali na Is-Haaq bin Raahaawiyyah ya kwamba wawili hao wamesema: "Huswaliwa kila kilichopuliziwa roho na kikakamilisha miezi minne na siku kumi". [Maalim As-Sunan cha Al-Khattwaabiy (1/268-269)].
An-Nawawiy (Rahimahul Laahu) amesema: " Lenye nguvu ni kwamba mtoto wa mimba iliyoharibika huswaliwa ikiwa ameshapuliziwa roho, na hii ni pale anapotimiza miezi minne, kisha akafa. Ama ikiwa atatoka kabla ya muda huo basi haswaliwi, kwa kuwa si maiti kama inavyodhihiri. Na asili ya hilo ni Hadiyth Marfu’u ya ‘Abdullah bin Mas-’oud isemayo: ((Hakika kuumbwa mmoja wenu, hukusanywa kwenye tumbo la mama yake siku arobaini, kisha huwa pande la damu mfano wa hivyo, kisha huwa pande la nyama mfano wa hivyo, halafu hupelekwa Malaika akampulizia roho)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (3208) na Muslim (2643)].
· Kuwaswalia Watu Wa Bid-'a, Wenye Madhambi Makubwa Makubwa Na Wafanyaji Maasi
Mjumuisho wa maneno waliyosema Maulamaa ni kuwa kila Muislamu huswaliwa hata akiwa ni mfanyaji madhambi makubwa makubwa, au fasiki, au mtu wa bid-'a - madhali hakukufuru kwa bid-'a yake -. Lakini ikiwa Maulamaa na watu wenye hadhi na ushawishi wataacha kumswalia yeyote katika hao ili iwe onyo kwa wengineo wenye kufanya hayo, basi itakuwa ni vizuri. Ni kama alivyokataa Rasuli kumswalia mtu aliyejiua na akawaambia Maswahaba wake: ((Mswalieni)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (978) na wengineo].
Haya yamesemwa na Maalik, Ahmad na maimamu wengineo. [Al-Mudawwanah (1/165), Al-Mughniy (2/355), na Majmu’u Al-Fataawaa (24/289)].
· Kumswalia Mwenye Deni
Imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiletewa mtu aliyefariki na anadaiwa, na alikuwa anauliza: ((Je ameacha cha kulipia deni lake?)). Akiambiwa ameacha cha kulipia humswalia, na kama hakuacha husema: ((Mswalieni mwenzenu)). Na Allaah Alipomfungulia kombozi za nchi mbalimbali alisema: (( Mimi nawastahikia zaidi Waumini kuliko nafsi zao. Basi mwenye kufa na deni na hakuacha cha kulipia, basi kulipa ni juu yetu sisi, na mwenye kuacha mali, basi ni za warithi wake)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (2298) na Muslim (1619)].
An-Nawawiy kasema: " Alikuwa anaacha kumswalia ili awahimize watu juu ya umuhimu wa kulipa deni kabla ya kifo, na kujihimu kutokuwa nalo ili mtu asije akakosa kuswaliwa na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Na Allaah Alipomfungulia kombozi za nchi, alirudi kuwaswalia na kulipa deni la mtu ambaye hakuacha cha kulipia". [Muslim Sharhu An Nawawiy (11/60)].
Juu ya msingi wa haya, haitakikani kwa Muislamu yeyote aache kumswalia mdaiwa eti kwa kuwa ana deni. Shukrani ni za Allaah Bwana wa ‘alamina.
· Kumswalia Aliyejiua
Maulamaa wana kauli tatu kuhusiana na hili:
Ya kwanza:
Haswaliwi. Hii ni kauli ya 'Umar bin ‘Abdul 'Aziyz na Al-Awzaa'iy. [Muslim Sharhu An Nawawiy (7/47)].
Hoja yao ni ni Hadiyth ya Jaabir bin Samurah aliyesema: "Rasuli aliletewa mtu mmoja aliyejiua kwa ncha ya mshale, hakumswalia”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (978)].
Ya pili:
Huswaliwa. Ni kauli ya Jamhuri ya Maulamaa, Al-Hasan, An-Nakh'iy, Qataadah, Maalik, Abu Haniyfah na Ash-Shaafi'iy. Wameijibu Hadiyth iliyotangulia ya Jaabir kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakumswalia yeye binafsi ili iwe onyo kwa watu wasije kufanya kitendo kama hicho, lakini Maswahaba walimswalia. Na ndivyo kama Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alivyoacha kumswalia mwenye deni mwanzoni ili kuwaonya wasitasahali kukopa na kuzembea kulipa deni, lakini aliwaamuru Maswahaba wamswalie kwa kuwaambia: ((Mswalieni mwenzenu)).
Al-Qaadhwiy amesema: "Kauli ya Maulamaa wote ni kumswalia kila Muislamu aliyekufa kwa kutekelezewa adhabu ya kisharia, aliyepigwa mawe kwa kuzini, aliyejiua na mtoto wa zinaa". [Angalia Sharhu Muslim (7/47) cha An-Nawawiy].
Ya tatu:
Waheshimiwa wenye hadhi na wenye madaraka waache kumswalia. Hili limesimuliwa toka kwa Maalik na wengineo, nalo ndilo lenye nguvu. [Sharhu Muslim (7/47) cha An-Nawawiy].
Ibn Taymiyah amepondokea kwenye kauli hii aliposema: "Inafaa kwa watu wa kawaida kumswalia. Ama Maulamaa wa dini wenye sauti na ushawishi, kama wakiacha kumswalia ili iwe onyo kwa wengineo na kukiiga kitendo cha Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), basi hii ni haki. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi". [Maajmu’u Al-Fataawaa (24/289)].
· Je, Shahidi Wa Vita Huswaliwa?
Maulamaa wamekhitalifiana juu ya hili katika kauli tatu:
Ya kwanza:
Haswaliwi. Ni kauli ya Maalik, Ash-Shaafi'iy, Is-Haaq na moja ya riwaya toka kwa Ahmad. [Naylul Awtwaar (4/54) na Al-Afnaan An-Nadiyyah (2/295)].
Wametoa dalili kwa jumla ya Hadiyth ambazo baadhi yake ni:
1- Hadiyth Marfu’u ya Jaabir kuhusu maiti wa Uhud ambapo alisema: "Akaamuru wazikwe na damu zao, hawakuoshwa, na wala hawakuswaliwa". [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1343)].
2- Hadiyth ya Anas ya kwamba Mashahidi wa Uhud hawakuoshwa, wakazikwa na damu zao, na wala hawakuswaliwa [isipokuwa Hamzah]. [Al-Albaaniy kasema ni Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (3137), na ziada ni yake, Al-Haakim (1/520) na Al-Bayhaqiy (4/10-11). Angalia Ahkaamul Janaaiz cha Al-Albaaniy (73)].
3- Hadiyth ya Abu Barzah kuhusiana na kuuawa Julaybiyb ambapo anasema: " Akamweka kwenye mikono yake miwili, hana kitanda isipokuwa mikono ya Rasuli. Akachimbiwa shimo, akawekwa kwenye kaburi lake na hakutaja osho". [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (2472), At-Twayalsiy (924), Ahmad (4/421, 422, 425) na Al-Bayhaqiy (4/21)].
Ya pili:
Ni lazima Shahidi aswaliwe. Ni kauli ya Abu Haniyfah, Ath-Thawriy, Ibn Al-Musayyib na Al-Hasan. Imeungwa mkono na Al-'Utrah. [Naylul Awtwaar (4/54) na Al-Afnaan An-Nadiyyah (2/295)].
Wametoa dalili kwa jumla ya Hadiyth ambazo miongoni mwazo ni:
1- Hadiyth ya Shaddaad bin Al-Haad ya kwamba mtu mmoja bedui alikuja kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwamini na kumfuata. Hadiyth inasema: " Walikaa kidogo, kisha wakanyanyuka kwenda kupambana na adui. Bedui akaletwa kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa amebebwa baada ya kupigwa mshale, na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Ni huyu ndiye?)). Wakasema: Ndiye. Akasema: ((Amemsadiki Allaah, na Yeye Akamsadikisha)). Kisha Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamkafini kwa juba lake, halafu akamweka mbele na kumswalia. Halafu ikawa kati ya aliyomwombea Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni: Ee Allaah! Huyu ni mja Wako, ametoka akihajiri katika Njia Yako akauawa kishahidi, na mimi ni shahidi juu ya hilo". [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na An-Nasaaiy (4/60), ‘Abdul Razzaaq kwenye Al-Muswannaf (9597), Al-Haakim kwenye Al-Mustadrak (3/595/596) na Al-Bayhaqiy (4/15-16)].
2- Hadiyth ya 'Uqbah bin 'Aamir ya kwamba Rasuli aliwaswalia maiti wa Uhud baada ya miaka minane. Swalaah yake kwa maiti ni kama mwenye kuwaaga walio hai na waliokufa. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (4042) na Muslim (2296)].
Wana jumla ya Hadiyth nyinginezo ambazo Sanad zake hazikosi kosoleo.
Ya tatu:
Hii ina nguvu na nafsi inapondokea kwayo. Inasema kwamba inajuzu kumswalia au kutomswalia. Ikiwa ataswaliwa aliyeuawa vitani basi ni vizuri, na kama hakuswaliwa pia ni vizuri. Hii ni rai ya Ibn Hazm [Al-Muhalla cha Ibn Hazm (5/115)], na riwaya moja toka kwa Ahmad. Ibn Al-Qayyim kasema iko barabara. [Angalia Al-Afnaan An-Nadiyyah (2/294)].
Kauli hii inafanya kazi kwa Hadiyth na nususi zote zilizothibiti.
Faida: Ama Shahidi ambaye si wa vitani, huyu huoshwa, na huswaliwa kama maiti wengineo. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi.
· Kumswalia Maiti Wa Mbali Asiyekuwepo
Maulamaa wana kauli tatu kuhusiana na hili:
Ya kwanza: Inajuzu kumswalia maiti wa mbali. Ni kauli ya Ash-Shaafi'iy, na Ahmad katika moja ya riwaya zake mbili. [Zaadul Ma’ad cha Ibn Al-Qayyim (1/197)].
Mhimili wa hoja yao katika hili ni kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwatangazia watu maombolezo ya kifo cha Negus katika siku aliyofariki, akatoka nao hadi kwenye muswalla, akapiga takbiyrah nne". [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (951) toka Hadiyth Marfu’u ya Abu Hurayrah].
Ya pili: Haijuzu kumswalia maiti wa mbali, na kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kumswalia Negus kimahususi, hakuwezi kufanywa kwa wote. Ni kauli ya Maalik na Abu Haniyfah. [Al-Muhalla cha Ibn Hazm (5/139)].
Ya tatu: Ina uchanganuo kidogo. Ni kwamba inajuzu kumswalia maiti wa mbali aliyekufa katika nchi ambayo hakuswaliwa na yeyote, na kama ameswaliwa huko alikofia, basi hatoswaliwa Swalaah ya maiti wa mbali kwa kuwa faradhi inakuwa ishaondoka kwa kuswaliwa na Waislamu. Huu ni msimamo wa Sheikh wa Uislamu Ibn Taymiyah [Zaadul Ma’ad cha Ibn Al-Qayyim (1/197)].
Ni chaguo pia la Sheikh 'Uthaymiyn. Hoja yao ni kwamba Rasuli hakumswalia mwingine yeyote Swalaah ya maiti wa mbali isipokuwa Negus peke yake, kwa kuwa alikufa kwenye umma wa kipagani usio na Swalaah. Na kama alikuwepo kati yao aliyeamini, basi hakuna chochote kijulikanacho kuhusu Swalaah hiyo. [Ash-Sharhul Mumti’i cha Ibn ‘Uthaymiyn (5/439)].
· Haijuzu Kumswalia Kafiri
Haijuzu kumswalia kafiri kutokana na Neno Lake Ta’alaa:
(( وَلَا تُصَلِّ عَلَىٰ أَحَدٍ مِّنْهُم مَّاتَ أَبَدًا وَلَا تَقُمْ عَلَىٰ قَبْرِهِ ۖ إِنَّهُمْ كَفَرُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَمَاتُوا وَهُمْ فَاسِقُونَ))
((Na wala usimswalie yeyote abadani miongoni mwao akifa; na wala usisimame kaburini kwake. Hakika wao wamemkufuru Allaah na Rasuli Wake, na wakafa hali wao ni mafasiki)). [At-Tawbah (9:84)]
Na Neno Lake Ta’alaa:
(( مَا كَانَ لِلنَّبِيِّ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَن يَسْتَغْفِرُوا لِلْمُشْرِكِينَ وَلَوْ كَانُوا أُولِي قُرْبَىٰ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُمْ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ • وَمَا كَانَ اسْتِغْفَارُ إِبْرَاهِيمَ لِأَبِيهِ إِلَّا عَن مَّوْعِدَةٍ وَعَدَهَا إِيَّاهُ فَلَمَّا تَبَيَّنَ لَهُ أَنَّهُ عَدُوٌّ لِّلَّـهِ تَبَرَّأَ مِنْهُ ۚ إِنَّ إِبْرَاهِيمَ لَأَوَّاهٌ حَلِيمٌ))
((Haimpasi Nabiy na wale walioamini kuwaombea maghfirah washirikina japokuwa ni jamaa zao wa karibu baada ya kuwabainikia kwamba wao ni watu wa moto uwakao vikali mno • Na haikuwa Ibraahiym kumuombea maghfirah baba yake isipokuwa kwa sababu ya ahadi aliyoahidiana naye. Lakini ilipombainikia kwamba yeye ni adui wa Allaah, alijiepusha naye. Hakika Ibraahiym ni mwenye huruma mno na mvumilivu)). [At-Tawbah (9:113 na 114)]
· Kuwaswalia Watoto Wa Mapagani
Haijuzu kuwaswalia watoto wa kipagani, kwa kuwa wanafuata hukmu ya wazazi wao ila kwa mtoto tunayemhukumu kuwa ni Muislamu. Ni kama kusilimu mmoja wa wazazi wake, au mtoto huyo kufa au kutekwa akiwa peke yake bila wazazi. Kama atakuwa hivyo, basi ataswaliwa. [Al-Mughniy cha Ibn Qudaamah (3/507, 508)].
· Hukmu Ya Mtu Aliyekutwa Amekufa Bila Kutambulika Kama Ni Muislamu Au Kafiri
Maulama wanasema kwamba zitaangaliwa alama za Uislamu kama kutahiriwa, nguo zake, mpako wa hina na kadhalika. Kama zitapatikana, ataoshwa na kuswaliwa. Na kama hakuna na maiti yuko katika nchi ya Kiislamu, basi ataoshwa na kuswaliwa. Na kama yuko katika nchi ya kikafiri, hatooshwa wala kuswaliwa. Haya kayaeleza Ahmad. [Al-Mughniy cha Ibn Qudaamah (3/478). Angalia Al-Mabsuutw cha As-Sarkhasiy (1/54) na Al-Majmu’u cha An-Nawawiy (5/213)].
· Zikichanganyika Maiti Za Waislamu Na Makafiri
Maulamaa wamekhitalifiana juu ya hili katika kauli mbili:
Ya kwanza: Zikichanganyika bila kuweza kutofautisha kati ya Waislamu na makafiri, wataswaliwa wote kama Waislamu. Ni kauli ya Maalik, Ash-Shaafi’i na Ahmad. [Al-Mughniy cha Ibn Qudaamah (3/477)].
Ya pili: Ikiwa maiti nyingi ni za Waislamu, wataoshwa na kuswaliwa wote kwa kuzingatia wingi isipokuwa kwa maiti itakayojulikana ni ya kafiri. Na kama nyingi ni za makafiri, haziswaliwi isipokuwa maiti zitakazojulikana kama ni za Waislamu kwa alama. Kama idadi italingana, hawataswaliwa kwa kuwa kuwaswalia makafiri ni marufuku, na pia inajuzu kuacha kuwaswalia baadhi ya Waislamu. Hii ni kauli ya Abu Haniyfah. [Al-Mughniy cha Ibn Qudaamah (3/477) na Al-Mabsuutw cha As-Sarkhasiy (1/54-55)].
· Ni Wapi Maiti Huswaliwa?
Kuswalia maiti kwenye muswallah
Imesuniwa kuswalia maiti katika muswallah, kwa kuwa Swalaah nyingi za maiti alizoziswali Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) zilikuwa katika muswallah, nayo ni sehemu maalumu kwa ajili hiyo kama ilivyosimuliwa:
- Imepokewa toka kwa Ibn Habiyb kwamba muswallah wa maiti Madiynah, ulikuwa umeshikana na Msikiti wa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa upande wa mashariki. [Fat-hul Baariy (3/237)].
- Abu Hurayrah kuhusu Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kumswalia Negus amesema: “Rasuli aliwapanga safu katika muswallah, akampigia takbiyrah nne”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1328) na Muslim (952)].
- ‘Abdullah bin ‘Umar kasema: “Mayahudi walimleta mwanamume kati yao na mwanamke waliozini kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Rasuli akaamuru wapigwe mawe karibu na muswallah wa maiti mbele ya Msikiti”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1329)].
Ibn Hajar kasema: “Hadiyth iliyotajwa ya Ibn ‘Umar inaonyesha kwamba Swalaah za maiti zilikuwa na sehemu yake maalum iliyoandaliwa” [Fat-hul Baariy (3/237)].
· Kuswalia Maiti Ndani Ya Msikiti
Maulamaa wana kauli tatu kuhusu hili:
Ya kwanza: Ni makruhu. Ni mwelekeo wa Hanafi na Maalik. [Fat-hul Baariy (3/224)].
Hoja yao ni dalili tulizozitoa za kumswalia maiti kwenye muswallah. Pia wanatolea dalili Hadiyth ya Abu Hurayrah aliyesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mwenye kumswalia maiti Msikitini, basi hana kitu)). [Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (3191), Ibn Maajah (1517), Ahmad (2/444, 455, na 505). Angalia As-Silsilat As-Swahiyhah (2352)].
Ya pili: Inajuzu. Ni kauli a Mahanbali. [Al-Mawsuw’at Al-Fiqhiyyah (16/36)].
Wametoa dalili kwa Hadiyth ya ‘Aaishah aliyesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakumswalia Suhayl bin Baydhwaa isipokuwa Msikitini”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (973)].
Ya tatu: Ni Sunnah kama uko usalama wa Msikiti kutochafuliwa. Ni kauli ya Mashaafi’iy. [Al-Mawsuw’at Al-Fiqhiyyah (16/36)].
Wametoa dalili kwa Hadiyth ya ‘Aaishah iliyotangulia, na wanasema pia kumswalia Msikitini ni utukufu zaidi.
· Kumswalia Maiti Kwenye Kaburi
Maulamaa wamekhitalifiana kuhusu hili kwa aliyepitwa na Swalaah katika kauli tatu: [Al-Ummu (1/414), Al-Majmu’u (5/210), Al-Mudawwanah (1/170), Al-Mughniy (3/500) Naylul Maarib (1/66), Sunan At-Tirmidhiy nambari 1037, Al-Muhalla (5/139) na Al-Badaai-’i (1/314)].
Ya kwanza: Huswaliwa. Ni kauli ya Maulamaa wengi katika Maswahaba wa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na waliofuatia baada yao. Pia ni kauli ya Ibn Mubaarak, Ash-Shaafi’iy, Ahmad, Is-Haaq, Ibn Hazm na wengineo. Wametoa dalili kwa:
1- Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas: “Kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliswali kwenye kaburi baada ya maiti kuzikwa, akapiga takbiyrah nne”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy kwa urefu (1247) na Muslim (954), na tamko ni lake].
2- Hadiyth ya Abu Hurayrah: “Kwamba mtu mweusi – mwanaume au mwanamke – alikuwa akisafisha Msikiti na akafariki. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakujua habari ya kifo chake, na siku moja akamkumbuka na kusema: (( Kitu gani kimemsibu mtu yule?)). Wakasema: Amekufa ee Rasuli wa Allaah. Akasema: ((Kwa nini msinijulishe?)). Wakasema: Alikuwa hivi na hivi – kisa chake – wakamdunisha. Akasema: (( Nionyesheni wapi kaburi lake)), akaenda kwenye kaburi hilo na kumswalia”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1337)].
Wenye kauli hii, wako baadhi yao waliojuzisha kuswali kwenye kaburi mpaka siku tatu na zikipita basi, wengine wamejuzisha mpaka mwezi, wengine wanasema mpaka mwili uharibike, na wengine milele.
Ya pili: Haijuzu kabisa kumswalia kwenye kaburi.
Ya tatu: Haijuzu kumswalia kwenye kaburi isipokuwa kama alizikwa kabla ya kuswaliwa. Kauli hizi mbili (ya pili na ya tatu) zimesimuliwa toka kwa An-Nakh'iy, Abu Haniyfah na Maalik. Na hoja yao ni:
1- Hadiyth zenye kukataza kuswali kwenye makaburi na kuswali kulielekea kaburi.
2- Nyongeza iliyopo kwenye Hadiyth ya Abu Hurayrah inayozungumzia Rasuli kumswalia mwanaume au mwanamke mweusi. Inasema: ((Hakika makaburi haya yamejaa giza kwa watu wake, na hakika Allaah Huyatia nuru kwa mimi kuwaswalia)). [Imefanyiwa "ikhraaj" kwa nyongeza hii na Muslim (956) kwa njia ya Abu Ar-Rabiy'i na Abu Kaamil Thanaa Hammaad toka kwa Thaabit toka kwa Abu Raafi'i toka kwa Abu Hurayrah].
Wamesema: "Kumswalia maiti kwenye makaburi ni katika mambo mahsusi yanayomhusu Rasuli peke yake".
· Kauli Yenye Nguvu:
Dalili za kumswalia maiti kwenye kaburi zimethibiti uthibiti usiokabilika ila mtu kusalimu amri tu. Ama kwa maiti ambaye hakuswaliwa, bila shaka jambo liko wazi bayana, na uhalali wa kumswalia utaendelea kuwepo madhali watu wanajua kwamba hakuna aliyemswalia. Ama kwa ambaye ameswaliwa, Hadiyth iliyotangulia kuhusu mwanaume au mwanamke mweusi inaweka wazi. Na ni maarufu kwamba katika enzi yake Rasuli, maiti alikuwa hazikwi bila ya kuswaliwa. [Ar-Rawdhwah An-Nadiyyah (1/171)].
Ama Hadiyth zenye kukataza kuswali kwenye makaburi na kuswali kuyaelekea, bila shaka katazo hili ni mahususi kwa Swalaah nyinginezo zisizo za maiti. Kwani aliyekataza hilo ndiye huyo huyo aliyeswalia maiti kwenye kaburi. Hii ni kauli yake na hiki ni kitendo chake, na viwili hivi havipingani. [Al-Muhalla (5/139) na Zaadul Ma’ad (1/195)].
Ama madai ya umahususi, haya hayana mashiko. Yanakhitilafiana na asili, na hayawezi kuthibiti ila kwa dalili. Ama ziada walioitumia kama hoja, la sawa ni kuwa imeingizwa katika Isnadi hii, nayo ni katika Mursali za Thaabit. Limebainishwa hili na Maswahiba wengi wa Hammaad bin Zayd. Na kwa ajili hiyo, Al-Bukhaariy hakuikhariji nyongeza hiyo. [Fat-hul Baariy (baada ya Hadiyth 458), na Sunan Al-Bayhaqiy (4/47)].
Na hata tukijaalia kwamba imethibiti, basi kuwa tu kwamba Allaah Anayatia nuru makaburi kutokana na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwaswalia waliomo humo, hakukanushi uhalali wa mtu mwingine kumswalia mtu kwenye kaburi na hasahasa baada ya neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Swalini kama mnavyoniona nikiswali)). [Naylul Awtwaar (4/64) chapa ya Al-Hadiyth].
Isitoshe, baadhi ya Maswahaba waliswali kwenye kaburi nyuma ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na yeye hakuwakataza. Hivyo basi, la sahihi ni kuwa inajuzu kuswali kwenye kaburi kwa ambaye hakumswalia maiti na hususan akiwa ni katika wahishimiwa wenye sifa ya wema. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Janaazah
009-Vitendo Vya Swalaah Ya Maiti
Alhidaaya.com [3]
1- Takbiyrah
(a) Idadi ya takbiyrah:
Zimepokelewa picha tofauti za takbiyrah toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
Ya kwanza: Takbiyrah nne
- Imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwombolezea Negus siku aliyokufa. Alitoka nao kwenda sehemu ya kuswalia, akapanga nao safu, kisha akampigia takbiyrah nne. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa "ikhraaj" na Al-Bukhaariy (1333) na Muslim (951)].
- Imepokelewa toka kwa Jaabir: "Kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliswalia Ashamah Negus, akapiga takbiyrah nne". [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa "ikhraaj" na Al-Bukhaariy (1334)].
- Imepokelewa toka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu Anhumaa) akisema: "Mtu mmoja alikufa, na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akimzuru, wakamzika usiku. Kulipopambazuka, walimjulisha naye akawauliza: Nini kiliwazuia msinijulishe? Wakasema: Ilikuwa ni usiku na giza, tukahisi tabu kukupa uzito. Akaliendea kaburi lake, akamswalia na akapiga takbiyrah nne”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa "ikhraaj" na Muslim (954) na An-Nasaaiy (1/284)].
Haya haya yamesemwa na ‘Umar bin Al-Khattwaab, Ibn ‘Umar, Zayd bin Thaabit, Al-Hasan bin ‘Aliy, Ibn Abiy Awfaa, Al-Barraa bin ‘Aazib, Abu Hurayrah, Ibn ‘Aamir, Muhammad bin Al-Hanafiyyah, ‘Atwaa, Ath-Thawriy, Al-Awzaa’iy, Ahmad, Is-Haaq, Maalik, Asw-haab Ar-Raay, Ibn Al-Mubaarak na Ash-Shaafi’iy. [Al-Majmu’u cha An-Nawawiy (5/189), Sharhu As-Sunnah cha Al-Baghawiy (5/342, 343), Al-Ummu cha Ash-Shaafi’iy (1/413), Ad-Dusuwqiy (1/414), na Kash-Shaaful Qina’a (2/112)].
Ya pili: Takbiyrah tano
- Imepokelewa na ‘Abdul Rahmaan bin Abiy Ya’alaa akisema: “ Zayd alikuwa akipiga takbiyrah nne kwa Swalaah za maiti wetu, na alipiga takbiyrah tano kwenye Swalaah fulani ya maiti, nami nikamuuliza sababu akasema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akizipiga”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa "ikhraaj" na Muslim (957)].
- Imesimuliwa kwamba ‘Aliy alikuwa akipiga takbiyrah sita kwa watu wa Badr, tano kwa Maswahaba wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na nne kwa watu wengineo. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa "ikhraaj" na Ibn Abiy Shaybah (11454)].
- Imam At-Tirmidhiy amesema kuhusu takbiyrah tano: “ Baadhi ya wasomi katika Maswahaba wa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na wengineo wameliafiki hili. Wanaona ni takbiyrah tano kwa Swalaah ya Janaazah”. [Angalia Hadiyth nambari (1023)].
Ya tatu: Takbiyrah saba
Picha hii ina Hadiyth Dhwa’iyf. Nimeitaja ili kuashiria udhwa’iyf wa Hadiyth yake. Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu Anhumaa) akisema: “ Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliamuru siku ya Uhud waletwe waliouawa, akaanza kuwaswalia. Wakawekwa tisa pamoja na Hamzah, akawapigia takbiyrah saba, kisha wakaondoshwa akabakishwa Hamzah. Kisha wakaletwa wengine tisa akawapigia takbiyrah saba mpaka akawamaliza”. [Hadiyth Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Twahaawiy katika Sharhu Ma’aanil Aathaar (1/503)].
Ya nne:
Imepokelewa toka kwa ‘Abdullah bin Az Zubayr (Radhwiya Allaahu Anhu) ya kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliamuru Hamzah afunikwe kwa burdah siku ya Uhud. Kisha akamswalia, akapiga takbiyrah tisa, kisha wakaletwa waliouawa wakapangwa safu, akawaswalia na akamswalia Hamzah pamoja nao”. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Twahaawiy katika Sharhu Ma’aanil Aathaar (1/503)].
· Faida
Imepokelewa toka kwa Maswahaba (Radhwiya Allaahu Anhum) athari Swahiyh kuhusu takbiyrah za Swalaah ya maiti tatu, nne, tano, sita, na saba. [Al-Awsatw (5/429), Ibn Abiy Shaybah (1/497), Sharhul Ma’aaniy (1/497) na Al-Muhalla (5/128)].
An-Nawawiy (Rahimahul Laahu) ameiashiria tofauti hii kisha akasema: “ Halafu tofauti hiyo ilitoweka, na Umma kwa sasa umekubaliana kwa pamoja kwamba ni takbiyrah nne bila kuongeza wala kupunguza”. [Al-Majmu’u (5/187). Ibn Hazm kaikadhibisha Ijma’a hii katika Al-Muhalla (5/126) kwa namna niliyoitaja hapo juu].
Ninasema: “ Haitolewi hoja ambayo wamo humo akina ‘Aliy, Ibn Mas-’oud, Anas, Ibn ‘Abbaas, Maswahaba wa Sham na Taabi’iyna. La sahihi ni kuwa kila lililothibiti toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ndilo litumikalo, na mwenye kupinga hatiwi maanani. Ijapokuwa linaloonekana kuwa na uzito zaidi katika Hadiyth zilizotajwa kwenye mlango huu ni kuwa, kuongeza zaidi ya takbiyrah nne ni jambo linalowahusu wanachuoni wenye kuheshimika kama alivyolizungumzia hilo At-Twahaawiy kwenye mlango maalumu. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi”.
· Akiacha Takbiyrah Moja Kati Ya Takbiyrah
[Al-Mughniy (3/451), Ibn ‘Aabidiyn (1/613), na Ad-Dusuwqiy (1/411)].
Mwenye kuacha takbiyrah moja kati ya takbiyrah za Swalaah ya maiti, kama ameiacha kwa kusahau, ataipiga kisha atatoa tasliym. Imeripotiwa kwamba Anas alipiga takbiyrah tatu kwenye Swalaah ya maiti, kisha akaondoka. Akazungumza, na watu wakazungumza, wakasema: “ Ee Abu Hamzah! Umepiga takbiyrah tatu tu! Akasema: Pangeni safu. Wakapanga, akapiga ya nne. [Kuna maneno kuhusu isnadi yake. Imefanyiwa “ikhraaj” na ‘Abdul Razzaaq (6417) kupitia kwa Mu’ammar toka kwa Qataadah. Kuna walakini kwenye riwaya hii].
Na kama imamu ataiacha kwa kusudi, Swalaah yake itabatilika, na sijdah ya sahau hairuhusiwi kwa hali yoyote.
· Je, Atanyanyua Mikono Yake Sambamba Na Takbiyrah?
Hakuna Hadiyth yoyote Marfu’u ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) inayogusia hili, lakini Maulamaa wamegawanyika makundi mawili: [Al-Mabsuwt (2/46), Al-Mudawwanah (1/160), Al-Majmu’u (5/232), Kash-Shaaful Qina’a (2/72), Al-Awsatw (5/426), Al-Muhalla (5/128), Kitabu cha Raf-’u Al Yadayn cha Al-Bukhaariy (uk. 175) na Ahkaamul Janaaiz (uk. 148)].
La kwanza: Wanasema atanyanyua mikono yake katika takbiyrah ya kwanza tu. Ni kauli ya Ath-Thawriy, na riwaya toka kwa Abu Haniyfah, Malik na Ibn Hazm. Al-Albaaniy kaikhitari. Dalili yao ni:
1- Yaliyoripotiwa Marfu’u toka kwa Abu Hurayrah: “Kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipiga takbiyrah katika Swalaah ya maiti, akanyanyua mikono yake kwenye takbiyrah ya kwanza, na akaweka mkono wa kulia juu ya wa kushoto”. [Ni Dhwa’iyf mno: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (1077), Ad-daaraqutwniy (2/75), na Al-Bayhaqiy (4/38)].
Sanad yake pia ni mbovu.
2- Yaliyoripotiwa toka kwa Ibn ‘Abbaas: “ Kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa ananyanyua mikono yake katika Swalaah ya maiti katika takbiyrah ya kwanza, kisha hafanyi tena”. [Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ad-daaraqutwniy (2/75) na Al-Uqayliy (3/449)].
Sanad yake pia ni Dhwa’iyf.
3- Wote wameitafikiana kunyanyua mkono katika takbiyrah ya kwanza. Hakuna jingine zaidi ya hilo lililofanywa na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Hivyo, haifai kufanya ambalo hakulifanya.
La pili: Wanasema atanyanyua mikono yake katika takbiyrah zote. Hili wamelisema Maulamaa wengi kama Ash-Shaafi’iy, Ahmad, Is-Haaq na riwaya toka kwa Abu Haniyfah na Maalik. Dalili yao ni:
1-Yanayosimuliwa toka kwa Ibn 'Umar: "Kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anaposwalia maiti, ananyanyua mikono yake miwili kwa kila takbiyrah". [Imetiwa dosari kwa waqfu. Imefanyiwa "ikhraaj" na Ad-daaraqutwniy katika Al-'Ilal].
La sahihi ni kuakifishiwa Ibn ‘Umar, nalo ni lenye kufuatia.
2- Yaliyothibiti toka kwa Ibn 'Umar: "Kwamba alikuwa akinyanyua mikono yake miwili katika kila takbiyrah katika Swalaah ya maiti, na anaposimama toka kwenye rakaa mbili". [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa "ikhraaj" na Al-Bukhaariy katika Kitabu cha Raf-'u Al Yadayn (110) na Al-Bayhaqiy (4/44)].
3- Na mfano wa Hadiyth hii toka kwa Ibn 'Abbaas, Al-Haafidh ameiashiria kwenye At-Talkhiysw (2/147), na amesema kuwa ni Swahiyh.
Ninasema: " Uwanja katika suala hili ni mpana ingawa kauli ya pili ndiyo yenye nguvu zaidi kutokana na kitendo cha Ibn 'Umar – kwa kuwa ndiye Swahaba mwenye kufuata zaidi Sunnah ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) – na hususan kwa anayeona kwamba yeye hafanyi hilo ila kwa tawqiyf".
· Je, Du’aa Ya Ufunguzi Wa Swalaah Ipo Katika Swalaah Ya Maiti?
[Al-Majmu'u (5/193), na Al-Mughniy (3/410)].
Jamhuri ya Maulamaa wanasema kwamba du’aa ya ufunguzi wa Swalaah haipo katika Swalaah ya maiti. Bali Ash-Shaafi'iy na Hanbali wamesema: Hupiga takbiyrah, kisha husoma isti'aadhah, na halafu husoma.
Ath-Thawriy kasema: "Atasoma du’aa ya ufunguzi wa Swalaah kwenye Swalaah hiyo, na imesimuliwa mfano wa kauli hiyo toka kwa Ahmad".
Ninasema: "Kauli yenye nguvu ni kuwa du’aa hiyo haikatazwi".
· Kusoma Al-Faatihahh Kwenye Swalaah Ya Maiti
Maulamaa wana kauli mbili kuhusiana na hukmu ya kusoma Suwrat Al-Faatihahh katika Swalaah ya maiti: [Al-Majmu'u (5/191), na Al-Mughniy (3/411), Al-Muhalla (5/131), Ibn 'Aabidiyn (1/611), Zaadul Ma'aad (1/192), na Bidaayatul Mujtahid (1/188)].
Ya kwanza: Ni lazima kuisoma. Hii ni kauli ya Ash-Shaafi'iy, Ahmad, Is-Haaq, Daawuud na Ibn Hazm. Pia kaisema Ibn 'Abbaas na Abu Umaamah. Dalili yao ni:
1- Ujumuishi wa kauli ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Hana Swalaah ambaye hakusoma Faatihahtul Kitaab)). [Hadiyth Swahiyh: Imetajwa mara nyingi katika mlango wa Swalaah].
Wamesema: Jina Swalaah ni pamoja na Swalaah ya maiti.
2- Imepokelewa toka kwa Abu Umaamah akisema: " Sunnah katika Swalaah ya maiti, asome mtu katika takbiyrah ya kwanza Ummul Kitaab kwa sauti ya chini, kisha apige takbiyrah mara tatu, na atoe tasliym wakati wa takbiyrah ya mwisho". [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa "ikhraaj" na An-Nasaaiy (4/75), ‘Abdul Razzaaq (6428) na Al-Bayhaqiy (4/39)].
3-Twalha bin ‘Abdallah bin 'Awf amesema: " Niliswali Swalaah ya maiti nyuma ya Ibn 'Abbaas, akasoma Faatihahtul Kitaab, na akasema: "Ili mjue kwamba ni Sunnah". [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa "ikhraaj" na Al-Bukhaariy (1335), Abu Daawuud (3182), At-Tirmidhiy (1032) An-Nasaaiy (4/75) na Ibn Maajah (2495)].
Ama kwa upande wa Sheikh wa Uislamu, yeye anaona kwamba kuisoma ni Sunnah na si wajibu katika Swalaah ya maiti.
Ya pili: Hakisomwi chochote katika Qur-aan katika Swalaah ya maiti. Ni madhehebu ya Ath-Thawriy, Al-Awzaaiy, Abu Haniyfah, na Maalik. Ni kauli pia ya Ibn 'Umar na 'Ubaadah bin As-Swaamit katika Maswahaba. Hoja yao ni:
1- Watu wa Madiynah hawasomi katika Swalaah ya maiti (kwa mujibu wa Maalik).
2- Yaliyothibiti kwa Ibn 'Umar kwamba yeye: "Alikuwa hasomi akimswalia maiti". [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa "ikhraaj" na Ibn Abiy Shaybah katika Muswannaf wake (11404)].
3- Imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah ya kwamba alimuuliza 'Ubaadah bin As-Swaamit kuhusiana na Swalaah ya maiti, naye akajibu: " Mimi Wal-Laahi nitakueleza: Utaanza kwa takbiyrah, kisha utamswalia Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), halafu utasema: Allaahumma, inna ‘Abdallah fulaan kaana laa yushriku bika shay-an, Anta A-'alamu bihi. In kaana muhsinan Fazid fiy ihsaanihii, wain kaana musiy-an Fatajaawaz anhu. Allaahumma laa Tahrimnaa ajrahu, wala Tudhwillanaa ba'adahu". [Isnadi yake ni Hasan: Imefanyiwa "ikhraaj" na Al-Bayhaqiy (4/40)].
Ninasema: " Kauli ya kwanza ndio yenye nguvu kutokana na yaliyotangulia. Ama athar ya Ibn 'Umar, inawezekana ikachukulika kama yeye hasomi kingine chochote isipokuwa Ummul Qur-aan. Aidha, athar ya 'Ubaadah, hakuna ndani yake hoja na hususan kutokutajwa takbiyrah nyinginezo na tasliym. Je, itasemwa si wajibu?! La sahihi ni kwamba inasomwa. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi”.
· Kumswalia Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Baada Ya Takbiyrah Ya Pili
Imesuniwa kumswalia Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) baada ya takbiyrah ya pili kutokana na Hadiyth ya Abu Umaamah ya kwamba mtu mmoja katika Maswahaba wa Rasuli alimjulisha: "Ya kwamba Sunnah katika Swalaah ya maiti ni imamu kupiga takbiyrah, kisha asome kimya kimya mwenyewe Faatihahtul Kitaab baada ya takbiyrah ya kwanza, halafu amswalie Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na amwombee du’aa maiti katika takbiyrah ya tatu, hasomi chochote katika takbiyrah hizo, kisha atoe tasliym kimya kimya ". [Ash-Shaafi'iy katika Al-Ummu (1/270) na Al-Bayhaqiy (4/39). Al-Haafidh ameipasisha isnadi yake].
Ukamilifu wa kumswalia Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni kwa tamko lile la tashah-hud.
· Kumwombea Maiti Du’aa Baada Ya Kumswalia
Ni Sunnah kwa kila mmoja kumwombea maiti du’aa baada ya kumswalia. Imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah akisema: "Nimemsikia Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Mkimswalia maiti, basi kila mmoja amwombee du’aa)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa "ikhraaj" na Abu Daawuud (3197), Ibn Maajah (1497), Al-Bayhaqiy (4/40 na Ibn Hibaan (3077)].
· Miundo Ya Du’aa Katika Swalaah Ya Maiti
- (( Allaahumma Ighfir lahuu wa R-hamhu wa 'Aafihii wa 'Afu anhu, wa Akrim nuzulahu wa Wassi'i madkhalahu, wa Ghsilhu bilmaai wath-thalji wal barad, wa Naqqihii minal khatwaayaa kamaa Naqqayta ath-thawba al abyadh minad danas, wa ‘Abdilhu daaran khayran min daarihii, wa ahlan khayran min ahlihi, wa zawjan khayran min zawjihi, wa Adkhilhul Jannah, wa A'idh-hu min 'adhaabil qabri, aw min 'adhaabin naar)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa "ikhraaj" na Muslim (963)].
- ((Allaahumma Ighfir lihayyinaa wa mayyitinaa, wa shaahidinaa wa ghaaibinaa, wa swaghiyrinaa wa kabiyrinaa, wa dhakarinaa wa unthaanaa. Allaahumma man Ahyaytahuu minnaa fa Ahyihii 'alal Islaam, waman Tawaffaytahuu minna fa Tawaffahuu 'alal iymaan. Allaahumma laa Tahrimnaa ajrahuu walaa Tudwillanaa ba'adahuu)). [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa "ikhraaj" na Abu Daawuud (3201), At-Tirmidhiy (1024), Ibn Maajah (1498)].
Faida: Kisomo na du’aa ni kimya kimya
Kisomo na du’aa ni kimya kimya katika Swalaah ya maiti, ingawa imepokelewa toka kwa Ibn 'Abbaas [Al-Bukhaariy (1335). Imetajwa nyuma] kwamba alisoma kwa sauti Faatihahtul Kitaab isipokuwa hilo lilikuwa kwa lengo la kuwafunza watu kama alivyosema Ahmad kuwa alifanya hivyo ili kuwafundisha. [Al-Mughniy cha Ibn Qudaamah (3/412)].
· Kutoa Tasliym
Maulamaa wamekhitalifiana; je ni tasliym moja au mbili?
Wenye kusema tasliym moja: Imepokelewa kwa njia sahihi toka kwa Ibn 'Umar [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa "ikhraaj" na Ibn Abiy Shaybah (11491)] na Waailah bin Al-Asqu'i [Sanad yake ni Hasan: Imefanyiwa "ikhraaj" na Ibn Abiy Shaybah (11505)] kwamba walikuwa wakitoa tasliym moja.
Pia limesimuliwa hilo toka kwa 'Aliy, Ibn 'Abbaas, Jaabir, Abu Hurayrah, Anas bin Maalik na Ibn Abiy Awfaa. Kadhalika, limesemwa na Sa'iyd bin Jubayr, Al-Hasan, Ibn Syriyna, Abu Umaamah bin Sahl, Al-Qaasim bin Muhammad, Al-Haarith, Ibrahiym An-Nakh'iy, Ath-Thawriy, Ibn 'Uyaynah, Ibn Al-Mubaarak, ‘Abdul Rahmaan bin Mahdiy, Maalik, Ahmad na Is-Haaq. [Al-Mughniy cha Ibn Qudaamah (3/418) na Al-Mudawwanatul Kubraa (1/170)].
Nayo ni kauli iliyosimuliwa toka kwa Ash-Shaafi'iy. [Al-Majmu'u cha An-Nawawiy (5/198-200)].
Wenye kusema tasliym mbili: Hili kalisema Ash-Shaafi'iy na Aswhaabu Ar Raay, na limwekhitariwa hili na Al-Qaadhwiy. [Al-Mughniy cha Ibn Qudaamah (3/418)].
Pia Abu Haniyfah ana msimamo huu. [Al-Mawsuu'at Al-Fiqhiyyah (16/28)].
Hoja yao katika hili ni kauli yake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Swalini kama mnavyoniona naswali)).
Na Hadiyth ya ‘Abdullah bin Abiy Awfaa ya kwamba alimswalia binti yake akapiga takbiyrah nne, kisha akatoa tasliym kulia kwake na kushoto kwake. [Hadiyth Dhwa’iyf: Imefanyiwa "ikhraaj" na Al-Bayhaqiy katika Sunani zake (4/43)].
Hadiyth hii imerufaishwa kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
Ninasema: "Hadiyth hii ni Dhwa’iyf".
· Aliyepitwa Na Baadhi Ya Takbiyrah
Baadhi ya Maulamaa wanaona kwamba maamuma akipitwa na baadhi ya takbiyrah, basi atazilipa zilizompita. Limesimuliwa hilo toka kwa Sa'iyd bin Al-Musayyib, 'Atwaa, An-Nakh'iy, Az-Zuhriy, Ibn Syriyn, Qataadah, Maalik, Ath-Thawriy, Ash-Shaafi'iy, Is-Haaq, Asw-Haab Ar Raay, na Ibn Hazm. [Al-Mughniy cha Ibn Qudaamah (3/423), Al-Muhalla cha Ibn Hazm (5/179)].
Lakini wamekhitalifiana kama atalipa; je ataomba du’aa kati ya takbiyrah au haombi? Abu Haniyfah anasema kwamba ataomba kati ya takbiyrah inayolipwa, lakini Maalik na Ash-Shaafi'iy wanaona kwamba atailipa bila kusoma au kuomba chochote. [Bidaayatul Mujtahid cha Ibn Rushd (1/190)].
Na hoja ya wanaosema kwamba alipe ni kauli ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Mlichokipata kiswalini, na kilichowapiteni kikamilisheni)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa "ikhraaj" na Al-Bukhaariy (635), na Muslim (602)].
Baadhi ya Maulamaa wanaona kwamba halipi takbiyrah zilizompita. Yameelezwa hayo kwa njia sahihi toka kwa Al-Hasan. [Hadiyth Swahiyh: ‘Abdul Razzaaq (5/64)].
Na inasimuliwa kuwa Ibn 'Umar hakuwa akilipa takbiyrah. Na kama atapiga takbiyrah mfululizo, basi hakuna ubaya. [Al-Mughniy cha Ibn Qudaamah (3/423)].
Imepokelewa toka kwa Ahmad akisema: "Kama hakulipa, basi hakuna ubaya". [As-Saabiq].
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Janaazah
010-Kuzika Maiti Na Yanayohusiana
Alhidaaya.com [3]
Kuzika maiti ni Fardhi ya Kutoshelezana hata kama maiti ni kafiri:
1- Ni kwa Hadiyth ya Abu Twalha: "Kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliamuru Siku ya Badr vigogo ishirini na nne wa Kikureshi watiwe kwenye kisima kati ya visima vya Badr". [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa "ikhraaj" na Al-Bukhaariy (3976) na Muslim (2875)].
2- Tumezungumza nyuma kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia 'Aliy wakati Abu Twaalib alipokufa – kafiri -: ((Nenda ukamzike)). [Isnadi yake ni Laini: Takhriyj yake ishatajwa].
Muislamu hazikwi pamoja na kafiri, wala kafiri pamoja na Muislamu, bali Muislamu huzikwa kwenye makaburi ya Waislamu, na kafiri kwenye makaburi ya washirikina. Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa katika enzi ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na yakaendelea mpaka enzi yetu ya leo. [Angalia dalili za hilo kwenye mlango wa Hukmu Za Janazah].
· Akifa Mwanamke Mjamzito Wa Ahlul Kitaab Na Aliyemtia Mimba Ni Muislamu, Wapi Atazikwa?
Imamu Ahmad kasema: " Atazikwa kati ya makaburi ya Waislamu na makaburi ya Ahlul Kitaab. Yeye ni kafiri na hazikwi kwenye makaburi ya Waislamu, kwa kuwa watapata adha kutokana na kuadhibiwa kwake, na hazikwi kwenye makaburi ya makafiri, kwa kuwa mwanaye ni Muislamu atapata adha ya kuadhibiwa kwao. Hivyo atazikwa sehemu yake peke yake".
Wamesema: "Mgongo wake utaelekezwa Qiblah kwa kulazwa kwa ubavu ili uso wa mtoto uelekee Qiblah juu ya ubavu wake wa kulia, kwa kuwa uso wa mtoto unaelekea mgongo wa mama yake". [Al-Mughniy (2/563)].
· Sunnah, Ni Kuzikwa Kwenye Makaburi
[Ahkaamul Janaazah (uk 173 na zinazofuatia)]
Hii ni kwa vile Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anazika maiti kwenye makaburi ya Al-Baqiy’i kama habari yakini zilivyotangaa kwa hilo kizazi kwa kizazi, na haikunukuliwa kuwa kuna Salaf yeyote aliyezikwa sehemu isiyo makaburi, isipokuwa tu habari yakini zilizotangaa kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) [na Maswahiba wake wawili] alizikwa kwenye chumba cha 'Aaishah (Radhwiya Allaahu Anha), na hili ni spesheli kwao.
Pia, Mashuhadaa wa vita hawazikwi kwenye makaburi bali huzikwa mahala walipouawa, na hawapelekwi kuzikwa kwenye makaburi. Ni kwa Hadiyth ya Jaabir ya kwamba amati yake alimleta baba yake Jaabir na khali yake – baada ya kuuliwa vitani kishahidi- ili awazike kwenye makaburi. Akashtukiziwa na mtu ananadi: Ee! Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anawaamuruni muwarejeshe maiti muwazike pale walipofia. Akarudi nao, akawazika pale walipouawa. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa "ikhraaj" na Abu Daawuud (3149), An-Nasaaiy (4/79), At-Tirmidhiy (1771) na Ahmad (3/397)].
· Ni Karaha Kumzika Maiti Katika Nyakati Hizi Ila Kwa Dharura
1,2,3- Jua linapochomoza, linapokua utosini na linapozama
Ni kwa Hadiyth ya 'Uqbah bin 'Aamir aliyesema: "Nyakati tatu Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anatukataza kuswali au kuwazika maiti wetu: Wakati jua linapochomoza dhahiri bayana mpaka linaponyanyuka, jua linapolingamana sawasawa katikati ya mbingu mpaka lipinduke, na jua linapokurubia kuzama mpaka lizame". [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa "ikhraaj" na Muslim (831), Abu Daawuud (3176), At-Tirmidhiy (1035) An-Nasaaiy (1/275), Ibn Maajah (1519)].
4- Wakati wa usiku bila dharura
Ni kwa Hadiyth ya Jaabir: " Kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimtaja mtu mmoja katika Maswahaba wake aliyekufa, akavikwa sanda isiyomtosha, akazikwa usiku. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akakemea mtu kuzikwa usiku mpaka aswaliwe isipokuwa mtu akilazimika kufanya hivyo". [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa "ikhraaj" na Muslim (943), Abu Daawuud (3148) na Ahmad (3/295-329)].
Sababu ni kuwa kuzika usiku kuna uhakika mkubwa wa kupatikana idadi ndogo ya wenye kumswalia maiti. Na kwa ajili hiyo, imekatazwa kuzika usiku ili aswaliwe mchana, kwa kuwa mchana watu wanakuwa na uchangamfu wa kumswalia maiti. Ikiwa watalazimika kumzika usiku kutokana na kuchelea kuharibika kutokana na joto au mfano wake, basi itajuzu kumzika hata kwa kutumia taa na kuteremka nayo kaburini. Ni kwa Hadiyth ya Ibn 'Abbaas: "Kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimzika mtu kwenye kaburi lake usiku, na taa ikawashwa katika kaburi lake" [Al-Albaaniy kasema ni Hasan: Imefanyiwa "ikhraaj" na At-Tirmidhiy (1064)].
· Sifa Ya Kaburi
1- Ni vizuri kaburi liwe na kina cha kutosha, pana na zuri
Ni kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu maiti wa Uhud: (( Chimbeni, panueni, nendeni chini na tengenezeni vizuri)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa "ikhraaj" na Abu Daawuud (3199), At-Tirmidhiy (1766) na An-Nasaai (4/8)].
2- Inajuzu kuchimba mwanandani au “shaqqu” kwenye kaburi, na mwanandani ni bora zaidi
Mwanandani ni mpasuo pembeni ya kaburi mwelekeo wa Qiblah. Na “shaqqu” ni kaburi au shimo lichimbwalo kwenda chini (kama mto).
Yote mawili yalifanywa wakati wa enzi ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Na mwanandani ni bora zaidi, nayo ndiyo Allaah Aliomchagulia Rasuli Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Imepokelewa toka kwa Anas akisema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipofariki, Madiynah kulikuwa na mtu anayechimba mwanandani na mwingine shaqqu. Wakasema: Tumtake istikhaarah Mola wetu, na tutume watu wawaite, na yeyote atakayekuja mwanzo, basi tutamwachia. Wakaenda kuitwa, na mwenye kuchimba mwanandani akawahi kuja, nao wakamchimbia Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mwanandani”. [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa "ikhraaj" na Ibn Maajah (1557) na Ahmad (3/99)].
Na imepokelewa toka kwa Sa’iyd bin Abiy Waqqaas kwamba amesema: “Nichimbieni mwanandani, na nisimikieni tofali juu ya kaburi langu kama alivyofanyiwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa "ikhraaj" na Muslim (966), An-Nasaaiy (1998) na Ibn Maajah (1556)].
An Nawawiy kasema: “ Maulamaa wamekubaliana kwamba kuzika kwenye mwanandani na shaqqu kunajuzu. Ikiwa ardhi ni ngumu udongo wake hauporomoki, basi mwanandani ni bora kutokana na dalili zilizotangulia, na kama ni laini unaoporomoka, basi shaqqu ni bora”. [Al-Majmu’u Sharhul Muhadh-dhab (5/287)].
· Ni Nani Anayezika?
1- Wanawake haifai kuzika wafu:
[Kutoka kitabu changu cha Fiqhu As Sunnah Lin Nisaai (uk. 198) chapa ya At-Tawfiyqiyyah].
Lililozoeleka wakati wa enzi ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na ambalo Waislamu wamekuwa wakilifanya mpaka hivi leo, ni wanaume kusimamia kazi ya kuzika. Wanaume ndio wenye uwezo zaidi wa kulifanya hilo, na kama wanawake watalifanya, basi inaweza kusababisha kufichuka sehemu za mwili wao mbele ya ajanibu, na hili halijuzu. Lililowazi zaidi kuliko haya yote ni kuwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimtanguliza Abu Twalha ili amzike binti yake – na Abu Twalha si maharimu yake – kama itakavyokuja mbele, na Rasuli hakuwatanguliza wanawake. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi”.
2- Ni nani mwenye haki zaidi ya kuzika maiti?
Mawalii wa maiti na akaribu zake ndio wenye haki zaidi ya kumteremsha kaburini. Na hii ni kwa ujumuishi wa Neno Lake Ta’alaa:
((وَالَّذِينَ آمَنُوا مِن بَعْدُ وَهَاجَرُوا وَجَاهَدُوا مَعَكُمْ فَأُولَـٰئِكَ مِنكُمْ ۚ وَأُولُو الْأَرْحَامِ بَعْضُهُمْ أَوْلَىٰ بِبَعْضٍ فِي كِتَابِ اللَّـهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ))
((Na wale walioamini baada (ya hijra) na wakahajiri na wakafanya jihaad pamoja nanyi; basi hao ni miongoni mwenu. Na ndugu wa uhusiano wa damu wanastahikiana wenyewe kwa wenyewe (kwa kurithiana), katika shariy’ah ya Allaah. Hakika Allaah ni Mjuzi wa kila kitu)). [Al-Anfaal (8:75)].
Na kwa Hadiyth ya ‘Aliy (Radhwiya Allaahu Anhu) aliyesema: “Nilimwosha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), nikaanza kuangalia uchafu anaokuwa nao maiti, nami sikuona kitu. Alikuwa msafi akiwa hai na maiti. Na waliosimama kumzika na kumteremsha kaburini ni watu wanne tu: ’Aliy, Al-Abbaas, Al-Fadhwl, na Swaaleh mwachwa huru wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Rasuli wa Allaah alichimbiwa mwanandani, na alisimikiwa tofali juu ya kaburi lake”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa "ikhraaj" na Al-Haakim (1/362), na kutoka kwake Al-Bayhaqiy (4/53). Ina Hadiyth wenza].
3- Nani wa kumwingiza mwanamke kwenye kaburi lake?
(a) Maharimu wake: Ni kwa ujumuishi wa Aayah iliyotangulia, na kwa Hadiyth ya ‘Abdul Rahmaan bin Abziy: “Kwamba ‘Umar bin Al-Khattwaab (Radhwiya Allaahu Anhu) alipiga takbiyrah nne kumswalia Zaynab binti Jahsh, kisha akatuma mtu kwenda kuwauliza wake wa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni nani atakayemwingiza Zaynab kwenye kaburi. Wakamjibu: Ni yule aliyekuwa akiingia nyumbani kwake bila kizuizi wakati wa uhai wake”. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa "ikhraaj" na Ibn Abiy Shaybah (3/324) na Al-Bayhaqiy (4/53)].
(b) Mumewe: Ana haki zaidi kuliko mtu wa kando. Tumetangulia kusema nyuma kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia ‘Aaishah: (( Nimependa kwamba hilo liwe nami ni hai, nikakuosha na kukukafini, na nikakuzika)). [Hadiyth Swahiyh: “Takhriyj” yake ishatajwa kwenye mlango wa mwanamume kumwosha mkewe].
3- Ni sharti kwa anayemzika maiti asiwe amemwingilia mkewe usiku huo
Mwanamume wa kando ajnabi atatangulizwa kumzika maiti badala ya maharimu au mume kama alimwingilia mkewe usiku huo. Imepokelewa toka kwa Anas akisema: “ Tulihudhuria mazishi ya binti ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekaa juu ya kaburi, nikaona macho yake yanatoa machozi, naye akasema: ((Je, kuna yeyote kati yenu hakumwingilia mkewe usiku?)). Abu Twalha akasema: Mimi. Akasema: ((Basi teremka kwenye kaburi lake)). Akateremka kwenye kaburi lake, akamzika”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa "ikhraaj" na Al-Bukhaariy (1342) na Ahmad (3/126)].
Imepokelewa toka kwa Anas kwamba: “Ruqayya alipokufa, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema: ((Asiingie kaburini mtu aliyemwingilia mkewe usiku)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa "ikhraaj" na Ahmad (3/370), na Al-Haakim (4/47) kwa Sanad Swahiyh].
· Namna Ya Kumlaza Maiti Kaburini
1- Sunnah ni kumwingiza maiti kwa upande wa inakolala miguu yake
Ni kwa Hadiyth ya Ibn Is-Haaq aliyesema: “Al-Haarith aliusia ‘Abdullah bin Yaziyd amswalie. Alimswalia kisha akamwingiza kaburini kwa upande wa inakolala miguu yake, na akasema: “Hii ni katika Sunnah”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa "ikhraaj" na Abu Daawuud (3195) kwa Sanad Swahiyh].
2- Alazwe maiti katika kaburi lake juu ya ubavu wake wa kulia, na uso wake uelekezwe Qiblah.
Haya ndiyo waliyoyafanya Waislamu tokea enzi ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mpaka hivi leo.
3- Aseme anayemlaza kwenye mwanandani: “Bismil-Laahi, wa’alaa Sunnat (au ‘alaa millati) Rasuwlil-Laah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa "ikhraaj" na Abu Daawuud (3197), At-Tirmidhiy (1051) na Ibn Maajah (1550) kwa Sanad Swahiyh].
4- Je kaburi la mwanamke lisitiriwe kwa nguo watu wasione mpaka afukiwe?
Kuna Hadiyth Dhwa’iyf iliyosimuliwa kuhusiana na hili, lakini Ibn Qudaamah amesema katika Al-Mughniy (2/501): “Na je mwanamke kaburi lake hufunikwa kwa nguo? Hatujui makhitalifiano kati ya Maulamaa kuhusiana na kusuniwa hili [Kisha akaleta athar kuhusiana na hili toka kwa ‘Umar na Anas, halafu akasema:] Kwa kuwa mwanamke ni uchi, na hakuna dhamana ya kufichuka sehemu yake yoyote wakaiona waliopo…”.
5- Ni Sunnah kutupia mateko matatu ya mchanga baada ya kumaliza kuziba mwanandani
Ni kwa Hadiyth ya Abu Hurayrah: “Kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimswalia maiti, kisha akamwendea maiti na akatupia mateko matatu upande wa kichwa chake”. [Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh: Imefanyiwa "ikhraaj" na Ibn Maajah (1565), na katika Al-Irwaa (751) kapitisha uSwahiyh wake].
6- Kaburi inyanyuliwe kidogo toka usawa wa ardhi ili ihifadhiwe, na ifanywe kuwa na mgongo
Ni kwa Hadiyth ya Jaabir: “Kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alichimbiwa mwanandani, na akasimikiwa tofali, na kaburi lake likanyanyuliwa kiasi cha shibri toka usawa wa ardhi”. [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa "ikhraaj" na Ibn Hibaan (2160) na Al-Bayhaqiy kwa Sanad safi].
Imepokelewa toka kwa Sufyaan At-Tammaar akisema: “Nilioona kaburi ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ikiwa na mgongo”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa "ikhraaj" na Al-Bukhaariy (1390)].
7- Kaburi itiwe alama kwa jiwe au mfano wake, ili azikwe mbele yake anayekufa katika jamaa wa maiti
Ni kwa Hadiyth ya Al-Muttwalib bin Hantwab aliyesema: “ Alipokufa ‘Uthmaan bin Madh-’uwn, jeneza lake lilitolewa akazikwa. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwamuru mtu mmoja amletee jiwe akashindwa kulibeba. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaliendea, akaikunja mikono yake…… kisha akalibeba na kuliweka kwenye kichwa chake. Akasema: “ “Unaliwekea kwalo alama ya kaburi ya ndugu yangu, nije kumzika atakayekufa katika jamaa zangu”. [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa "ikhraaj" na Abu Daawuud (3205) na Al-Bayhaqiy (3/412)].
· Inajuzu Kuzika Maiti Wawili Au Zaidi Katika Kaburi Moja Kwa Dharura
Imepokelewa toka kwa Jaabir bin ‘Abdillah akisema: “ Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anawakusanya wanaume wawili katika nguo moja katika maiti wa Uhud, kisha anauliza: “Ni yupi kati yao aliyehifadhi zaidi Qur-aan?” Anapoonyeshwa mmoja wa wawili hao, humtanguliza kwenye mwanandani na husema: (( Mimi ni shahidi juu ya hawa Siku ya Qiyaamah)), na huamuru wazikwe na damu zao, hawakuoshwa wala hawakuswaliwa”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa "ikhraaj" na Al-Bukhaariy (1343), An-Nasaaiy (1/277), At-Tirmidhiy (1036), Abu Daawuud (3138) na Ibn Maajah (1514)].
Pia yaelezwa kuwa wakizikwa wawili na zaidi, hutangulizwa mbora wao.
· Mwanamke Huzikwa Pamoja Na Mwanamume Kwa Dharura
Imepokelewa toka kwa Wailah bin Al-Asqa’a (Radhwiya Allaahu Anhu): “ Kwamba ilikuwa wanaume na wanawake wakizikwa pamoja, mwanamume hulazwa kwenye kaburi mwelekeo wa Qiblah, na mwanamke hulazwa nyuma yake kwenye kaburi”. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa "ikhraaj" na ‘Abdul Razzaaq (6378). Kuna athar nyinginezo ziangaliwe kwenye Jaami’i Ahkaamun Nisaa (1/556)].
Ash-Shaafi’iy kasema kwenye Al-Ummu (1/245): “ Sipendi kabisa mwanamke azikwe pamoja na mwanamume. Lakini kama ni lazima kufanya hivyo na hapana budi, mwanamume atakuwa mbele na mwanamke nyuma yake, na kitawekwa kizuizi cha mchanga kati ya mwanamke na mwanamume kwenye kaburi”.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Janaazah
011-Kuwapa Pole Wafiwa (Ta-‘aziyah)
Alhidaaya.com [3]
Inajuzu kisharia kwa watu – wanaume na wanawake- kuwapa ta-’aziyah (kuwafariji) jamaa wa maiti kwa maneno ya kuwaliwaza na kuwaondoshea huzuni, na kuwafanya waridhie na wasubiri kutokana na yale yaliyothibiti toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na hii ikiwa watawaendea. Na kama hawakuwaendea, basi watawaazi kwa namna yoyote itakayofanikisha hilo bila kwenda kinyume na sharia. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mwenye kumfariji nduguye Muumini katika msiba wake, Allaah Atamvika kipambo cha kijani afurahishwe kwacho Siku ya Qiyaamah)). Ikasemwa: Ee Rasuli wa Allaah! Nini maana ya kufurahishwa? Akasema: ((Watu watalitamania hilo)). [Al-Albaaniy kasema ni Hasan: Angalia Al-Irwaa (764)].
Kati ya yaliyothibiti ya kusemwa katika kumfariji mfiwa (kutoa pole) ni:
(( لله ما أخذ وله ما أعطى، وكل شيء عنده بأجل مسمى، فلتصبر وتحتسب ))
[Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1224) na Muslim (923)].
· Zindusho
Ni karaha kukusanyika sehemu maalumu kwa ajili ya kutaazia (kufanya matanga). [Al-Ummu cha Ash-Shaafi’iy (1/248) na Fiqhu As-Sunnah Lin Nisaai (uk. 202)].
Hii ni kwa vile kufanya hivyo hujadidisha huzuni na hugharimu. Imesimuliwa katika Hadiyth ya Jariyr bin ‘Abdillaah (Radhwiya Allaahu Anhu) akisema: “ Tulikuwa tunaona kukusanyika kwa jamaa wa maiti na kupikwa chakula, ni katika maombolezo mabaya”. [Isnadi yake ni Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (3132), At-Tirmidhiy (998) na Ibn Maajah (1610). Inatiliwa nguvu na yanayofuatia].
Hivyo mtu asikubali kwenda kwenye mjumuiko huu, bali atoe pole kwa mujibu wa itakavyowepesika kwake.
Ama vinavyoitwa khamiys na arubaini zinazofanywa kila mwaka na mfano wake, ni katika bid-’a zilizozushwa zenye kupingana na Dini ya Allaah Mtukufu.
· Kuwatayarishia Chakula Wafiwa
Ni Sunnah kwa jamaa wa maiti na majirani zake kuwatayarishia chakula wafiwa. Imeripotiwa toka kwa ‘Abdullah bin Ja’afar akisema: “ Rasuli wa Allaah amesema: (( Waandalieni watu wa Ja’afar chakula, kwani limewajilia wao jambo la kuwashughulisha)). [Isnadi yake ni Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Maajah (1612) na Ahmad (2/204)].
Hadiyth hii ni Dhwa’iyf, lakini inatiliwa nguvu na Hadiyth ya ‘Aaishah ya kwamba yeye alikuwa wakati anapokufa jamaa yake: “Huamuru liletwe jungu la “talbinah” ikapikwa, kisha uji wa shayiri ukatayarishwa, halafu “talbinah” ikamiminwa humo. Halafu husema: Kuleni, kwani mimi nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Talbinah hufariji moyo wa mgonjwa, na huondosha sehemu ya huzuni)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (5417) na Muslim (2216)].
“Talbinah”, ni chakula kinachopikwa kwa unga, na pia huweza kuongezewa asali.
· Zindusho:
Ama waliyoyazoea watu kinyume na Sunnah hii, na waliofiwa kuwatayarishia chakula watoaji pole, haya ni makruhu kwa kuwa yanapishana na Sunnah, na kwa Hadiyth iliyotangulia ya Jariyr.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Janaazah
012-Yananayomnufaisha Maiti Baada Ya Kufa
Alhidaaya.com [3]
1- Kuombewa du’aa na Waislamu
Allaah Mtukufu Anasema:
((وَالَّذِينَ جَاءُوا مِن بَعْدِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالْإِيمَانِ وَلَا تَجْعَلْ فِي قُلُوبِنَا غِلًّا لِّلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا إِنَّكَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ))
((Na wale waliokuja baada yao wanasema: “Rabb wetu! Tughufurie na ndugu zetu ambao wametutangulia kwa iymaan na wala Usijaalie katika nyoyo zetu mafundo ya chuki kwa wale walioamini; Rabb wetu! Hakika Wewe ni Mwenye huruma mno, Mwenye kurehemu)). [Al-Hashr (59:10)].
Na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anasema: (( Du’aa ya mtu Muislamu kwa nduguye kwa siri, inajibiwa)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (2733) na wengineo].
2- Kulipiwa deni lake na mtu yeyote
Ni kwa Hadiyth iliyoelezewa nyuma ya Abu Qataadah kumlipia deni mtu aliyekufa. [Hadiyth Swahiyh: Imetajwa mwanzoni mwa mlango huu].
3- Walii wake kumlipia Swawm
Ni kwa Hadiyth ya 'Aaishah (Radhwiya Allaahu Anhaa) ya kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: (( Aliyekufa na anadaiwa Swawm, basi walii wake atamfungia)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1952) na Muslim (1147)].
Na hii inajumuisha deni la Ramadhwaan na deni la Swawm ya nadhiri. Hii ndiyo kauli sahihi zaidi ya Maulamaa kama itakavyokuja kuelezwa kwenye mlango wa Swawm Apendapo Mola.
4- Kumlipia nadhiri ikiwa ni Swawm au jingine lolote
Sa'ad bin 'Ubaadah alimuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Mama yangu amefariki na nadhiri yake hajaitekeleza". Rasuli akamwambia: ((Mlipie wewe)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (2761) na Muslim (1638)].
5- Matendo mema anayoyafanya mtoto mwema
Allaah Anasema:
((وَأَن لَّيْسَ لِلْإِنسَانِ إِلَّا مَا سَعَىٰ))
((Na kwamba insani hatopata (jazaa) isipokuwa yale aliyoyafanyia juhudi)). [An-Najm (:39)]
Na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika chema zaidi akilacho mtu, ni kile alichokichuma mwenyewe, na hakika mtoto wake ni chumo lake)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (3511), At-Tirmidhiy (1369) An-Nasaaiy (7/241) na Ibn Maajah (2137)].
6- Anayoyaacha maiti kati ya mabaki mema na swadaqah endelevu
Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mwanadamu anapokufa, amali zake hukatika isipokuwa matatu: Swadaqah endelevu, au elimu yenye manufaa, au mtoto mwema anayemwombea)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (1631), Abu Daawuud (2863), At-Tirmidhiy (1390), na An-Nasaaiy (6/251)]
· Nini Hukmu Ya Kumtunuku Maiti Thawabu Za Kisomo Cha Qur-aan?
Allaah Amesema:
((وَأَن لَّيْسَ لِلْإِنسَانِ إِلَّا مَا سَعَىٰ))
((Na kwamba insani hatopata (jazaa) isipokuwa yale aliyoyafanyia juhudi)). [An-Najm (:39)]
Asili ni kuwa maiti hanufaiki na chochote kutokana na matendo ya walio hai isipokuwa kwa lile ambalo limehusishwa na dalili kutoka kwenye ujumuishi wa yaliyotajwa nyuma. Ama yasiyo hayo, hayo hubakia kwenye ujumuishi kama inavyoelezwa kwenye uswuul.
Na kwa sababu hii, Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakuuhimiza Umma kutoa thawabu za kisomo kwa wafu, na wala hakuwaelekeza kufanya hivyo, bali hili halikunukuliwa toka kwa Swahaba yeyote –kwa mujibu wa tujuavyo- lakini Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametuelekeza kumwombea maiti maghfirah akisema: ((Mtakieni maghfirah ndugu yenu, na mwombeeni uthibiti, kwani yeye hivi sasa anaulizwa)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (3221) na wengineo].
Kwa Hadiyth hii, tunapata kujua kwamba kisomo hakimnufaishi maiti. Lakini huu ni msimamo wa Ash-Shaafi'iy kinyume na Jamhuri.
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Janaazah
013-Kuyazuru Makaburi Na Yanayohusika
Alhidaaya.com [3]
Kuyazuru makaburi kunaruhusika kwa ajili ya kuwaidhika nayo na kuikumbuka aakhirah. Na hii ni kutokana na neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): (( Nilikuwa nimewakatazeni kuyazuru makaburi, basi yazuruni [yatawakumbusheni aakhirah])). [Hadiyth Swahiyh: “Takhriyj” yake yaja].
· Je, Wanawake Wanaruhusiwa Kuyazuru Makaburi?
Maulamaa wana kauli tatu kuhusu hili: Ya kwanza ni haramu, ya pili ni makruhu, na ya tatu ni mubaha bila karaha. Ni riwaya toka kwa Ahmad, na kauli ya Maalik na baadhi ya Mahanafi. [Tahdhiyb As-Sunan cha Ibn Al-Qayyim (9/58 –‘awn al ma’abuwd) kwa mabadilisho kidogo].
Kauli hii ndiyo yenye nguvu zaidi kwa sharti ziara iwe kwa ajili ya kukumbuka mauti na aakhirah pamoja na kujiepusha maharamisho. Na hii ni kwa dalili zifuatazo:
1- Hadiyth ya Anas –iliyotangulia- isemayo: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimpitia mwanamke mmoja anayelia mbele ya kaburi akamwambia: ((Mche Allaah na fanya subira)). [Hadiyth Swahiyh: Al-Bukhaariy (1283) na Muslim (926)]
Na hapa Rasuli hakumkataza kuzuru makaburi.
2- Bibi ‘Aaishah alilizuru kaburi la kaka yake. Imepokelewa toka kwa Ibn Abiy Mulaykah: “Kwamba ‘Aaishah alikuja siku moja akitokea makaburini. Nikamuuliza: Ee Mama wa Waumini! Umetokea wapi? Akasema: Natoka kwenye kaburi la kaka yangu ‘Abdul Rahmaan bin Abi Bakri. Nikamwambia: Si Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa amekataza kuyazuru makaburi? Akasema: Ndio, alikuwa amekataza, kisha akaamuru kuyazuru”. [Hadiyth Swahiyh: Al-Haakim (1/376), Al-Bayhaqiy (4/78), na asili yake ni kwa Ibn Maajah (1569) kwa ufupi, nayo ni Swahiyh].
3- Bibi ‘Aaishah alimuuliza Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Nitasema vipi ee Rasuli wa Allaah? [yaani akienda makaburini]. Akasema: ((Sema: As Salaam ‘alaa ahlid diyaar minal Mu-uminiyna wal Muslimiyna, wayarhamul Laahu al mustaqdimiyna minnaa wal musta-akhiriyna, wainnaa in shaa Allaah bikum lalaahiquwna)). [Hadiyth Swahiyh: Muslim (974), Ahmad (6/221), ‘Abdul Razzaaq (6712) na Al-Bayhaqiy (4/79)].
4- Ujumuishi wa neno lake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Nilikuwa nimewakatazeni kuyazuru makaburi, basi yazuruni)). [Hadiyth Swahiyh: Muslim (977), Abu Daawuud (3235) kwa ufupi, An-Nasaaiy (4/89) na At-Tirmidhiy (1054)].
· Zindushi
[Jaami’u Ahkaamin Nisaa (1/581) kwa mabadilisho kidogo. Pia kwenye kitabu changu cha Fiqhu Sunnat An Nisaaa (uk 204) nikiwa nimenukuu toka kitabu hicho].
1- Kukipatikana uhakika kwamba wanawake wakienda makaburini watalia kwa sauti, wataomboleza, watawalalamikia maiti, na watafanya bid-’a na maharamisho, hapo itakuwa ni haramu kwao kuzuru makaburi.
2- Kukipatikana uhakika kwamba wao wanayaendea makaburi ya wanaioitwa watu wema au mawalii ili kuwaomba wawaondoshee matatizo, wawakidhie haja zao na wawaondoshee ghamu, basi hii ni shirki, na hapo bila shaka watazuiliwa wasende.
3- Ikiwa wanawake wataiweka siku mahsusi kwa ajili ya kuyazuru makaburi kama inavyotokea siku za ijumaa, ‘Iyd na kadhalika, basi hii ni bid-’a.
4-Haijuzu wanawake kutoka kwenda makaburini na kwingineko wakiwa wamevalia mavazi yasiyo sitara, wamejipamba na kujitia manukato.
· Miongoni Mwa Adhkaar Zilizothibiti Wakati Wa Kuyazuru Makaburi
1- ((As Salaam ‘Alaykum daara qawmin Mu-uminiyna, wainnaa waiyyaakum wamaa tuw-’aduwna ghadan muajjaluwna, wainnaa in Shaa Allaahu bikum laahiquwna. Allaahumma Ghfir liahli (atataja makaburi)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (974), An Nasaaiy (1/287) na wengineo].
2- ((As Salaam ‘Alaykum Ahlad diyaar minal Mu-uminiyna wal Muslimiyna, wainnaa in Shaa Allaahu [bikum] lalaahiquwna. As-alul Laaha lanaa walakumul ‘aafiyah)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (975), An Nasaaiy (2040) na Ibn Maajah (1547)].
3- ((As Salaam ‘Alaa Ahlid diyaar minal Muuminiyna wal Muslimiyna, wa Yarhamul Laahu al mustaqdimiyna minnaa wal mustaakhiriyna, wainnaa in shaa Allaahu bikum lalaahiquwna)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (974) na Ahmad (6/221)].
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/284
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9949&title=03-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20%D9%83%D9%90%D8%AA%D9%8E%D8%A7%D8%A8%D9%8F%20%D8%A7%D9%8E%D9%84%D9%92%D8%AC%D9%8E%D9%86%D9%8E%D8%A7%D8%A6%D9%90%D8%B2%D9%90%20-%20Kitabu%20Cha%20Janaazah%20%20%20
[3] http://www.alhidaaya.com/
[4] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9950&title=001-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Janaazah%3A%20Wanayoyafanya%20Waliopo%20Kwa%20Aliyekaribia%20Kukata%20Roho
[5] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9951&title=002-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Janaazah%3A%20Wanayoyafanya%20Waliopo%20Akishakufa%20Na%20Kukata%20Roho
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9952&title=003-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Janaazah%3A%20Yanayowapasa%20Jamaa%20Wa%20Maiti%20%E2%80%93%20Na%20Hususan%20Akina%20Mama-%20Inapowajia%20Habari%20Ya%20Kifo
[7] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9956&title=004-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Janaazah%3A%20Kumwosha%20Maiti%20
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9957&title=005-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Janaazah%3A%20Sifa%20Ya%20Kumwosha%20Maiti
[9] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9964&title=006-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Janaazah%3A%20Kumkafini%20Maiti
[10] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9965&title=007-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Janaazah%3A%20Kubeba%20Jeneza%20Na%20Kulisindikiza
[11] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9966&title=008-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Janaazah%3A%20Swalaah%20Ya%20Janaazah
[12] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9967&title=009-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Janaazah%3A%20Vitendo%20Vya%20Swalaah%20Ya%20Maiti
[13] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9985&title=010-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Janaazah%3A%20Kuzika%20Maiti%20Na%20Yanayohusiana%20
[14] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9997&title=011-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Janaazah%3A%20Kuwapa%20Pole%20Wafiwa%20%28Ta-%E2%80%98aziyah%29
[15] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9998&title=012-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Janaazah%3A%20Yananayomnufaisha%20Maiti%20Baada%20Ya%20Kufa
[16] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F9999&title=013-Swahiyh%20Fiqh%20As-Sunnah%3A%20Mlango%20Wa%20Janaazah%3A%20Kuyazuru%20Makaburi%20Na%20Yanayohusika