Nyama Ya Kukaanga Na Mboga Ya Mchicha (Spinach)

Nyama Ya Kukaanga Na Mboga Ya Mchicha (Spinach)

      

Vipimo:

Nyama isiyo na mifupa - 1 Ratili (LB)

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi iliyosagwa - 1 Kijiko cha supu

Kitunguu - 1 kikubwa

Pilipili manga ya unga -  1/2 Kijiko cha chai

Bizari ya unga(Garam masala) - 1 Kijiko cha chai

Chumvi - Kiasi

Sosi ya soya(soy sauce) - 2 Vijiko vya supu

Mboga(Spinach) ya barafu iliyokatwa - 1 pakiti

Hummus(Chick peas)  - 1 Kopo

Mafuta ya kukaangia  -  1/4 kikombe 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

1. Katakata nyama vipande vidogo. 

2. Weka mafuta katika sufuria na kaanga kitunguu hadi iwe rangi ya brauni.

3. Kisha kaanga thomu na tangawizi na vyote vilivyo baki ,pamoja na nyama isipokuwa spinach na hummus.

4. Nyama ikishakuwa si nyekundu tena, weka maji kiasi ya kuiivisha.

5. Nyama ikishaiva na karibu kukauka, tia hummus na spinach na iwache dakika chache.

6. Epua na tayari kuliwa na wali.

 

Share