Mitai 1

Mitai 1

 

 

 

VIPIMO

 
Unga wa ngano   1 1/2 Kikombe

Baking powder  1 Kijiko cha chai

Baking soda  ¼ Kijiko cha chai

Chumvi    ½  kijiko cha chai

Sukari  1 kijiko cha supu

Hamira   1/2 Kijiko cha supu

Yai   1

Maziwa ½  Kikombe

Mafuta ya kukaangia

 

SHIRA

Sukari  1 Kikombe

Maji  ½  Kikombe

Iliki au Mdalasini ¼   kijiko cha chai (ya unga)

 

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

 

1.  Kwenye bakuli, changanya pamoja unga, baking powder, baking soda,  chumvi, sukari na hamira.

2.  Katika kibakuli, piga mayai na maziwa pamoja.

3.  Changanya mchanganyiko wa mayai na wa unga ; na ukande kama unga wa maandazi.

4.  Ikisha fura, sukuma unga kama wa maandazi na ukate mitai .

5.  Pasha moto mafuta na uchome hadi iwe rangi ya dhahabu, upande zote  mbili.

6.  Ipikie shira lakini isiwe nzito .

7.  Tia mitai na upepete hadi sukari ienee kote na zitakuwa tayari kuliwa.

 

 

 

 

Share