Mchanganyiko Wa Mboga Za Kuchoma (Baked)

Mchanganyiko Wa Mboga Za Kuchoma (Baked)

 

Vipimo 

 

Viazi - 5 

Karoti - 2 

Koliflawa (cauliflower) - ½ 

Brokoli - 3 misongo (bunch) 

Pilipili mboga ya kijani - 1 

Pilipili mboga nyekundu - 1 

Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa - 1 kijiko cha supu 

Pilipili manga iliyosagwa - 1 kijiko cha chai 

*Kidonge cha supu (stock) - 1 

Parsley kavu iliyokatwa ndogo ndogo (chopped) - 2 vijiko vya supu  

Chumvi - kiasi 

Mafuta ya zaytuni (olive oil) - 3 vijiko vya supu  

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika  

  1. Menya viazi katakata vipande vya mchemraba (cubes)
  2. Katakata karoti vipande virefu virefu vya kiasi
  3. Katakata mapilipili mboga vipande vya kiasi kiasi
  4. Chambua koliflawa na brokoli
  5. Tia mafuta katika karai, kaanga thomu kidogo kisha tia chumvi, pilipili manga, epua weka kando.
  6. Weka  kidonge cha supu katika kibakuli kidogo, tia maji ya moto kiasi vijiko 3 vya supu, koroga kipate kuyayuka iwe supu.  Tia katika sufuria uliyokaangakia thomu.
  7. Weka mboga zote katika bakuli kisha mimina mchanganyiko wa thomu na supu uchanganye vizuri.
  8. Tia katika treya ya kupikia ndani ya oveni. Zipike mboga (bake) kwa moto wa takriban 350°C kwa muda wa dakika 15-20.
  9. Epua kisha mwagia parsely na uchanganye kisha mimina katika bakuli la kupakulia ikiwa tayari kuliwa kwa aina za mikate.  

 

* kidonge cha supu ikiwa ni chicken stock au beef stock.

 

Share