Achari Ya Papai Bichi, Embe Mbichi Na Karoti

Achari Ya Papai Bichi, Embe Mbichi Na Karoti 

Vipimo

Papai bichi - 1

Embe mbichi - 3

Karoti - 3

Pilipili mbichi - 7

Pilipili nyekundu ya masala/unga - 1 kijiko cha supu

Nyanya iliyosagwa (crushed) - 3 vijiko vya supu

Rai/chembe za hardali (mustard seeds) - ¼ kikombe

Majani ya mchuzi (curry leaves) - 2 miche

Methi (uwatu uliosagwa) - 2 vijiko vya cha chai

Haldi (bizari ya manjano) - 2 vijiko vya chai

Chumvi - kiasi

Ndimu - 3 (kamua maji)

Mafuta - ½ kikombe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Menya papai, embe na karoti kisha katakata vipande virefu virefu kama vinavyoonekana katika picha.
  2. Katakata pilipili mbichi weka kando.
  3. Katika karai, weka mafuta yashike moto. Kisha tia rai zikaangike kidogo.
  4. Zinapoanza kurukaruka na kugeuka rangi, tia methi, majani ya mchuzi, pilipili mbichi, pilipili nyekundu ya masala ya unga na haldi na endelea kukaanga kidogo.
  5. Tia nyanya iliyosagwa endelea kukaanga kidogo.
  6. Tia papai, embe na karoti, endelea kukaanga, kisha punguza moto uwe mdogo mdogo.     
  7. Mimina maji ya ndimu, ongeza kidogo maji yakihitajika yapate kuivisha papai, embe na karoti. Tia chumvi.
  8. Funika huku kila mara unafungua kugeuza geuza hadi iive. Onja, chumvi na viungo, ikiwa tayari.   
  9. Kidokezo:
  10. Ukipenda ongezea achari ya embe ya mafuta ya tayari kijiko kimoja cha supuu izidi kutoa ladha ya achari.

 

 

 

Share