Kulipa Kibaba Kwa Ajili ya Swawm
SWALI:
Ni vipi namna ya kutoa vibaba kwa ajili ya mtu asiyeweza kufunga. Unatoa kiasi chote kinachostahili kwa mara moja au unatoa kila siku moja
na kiasi chake?
JIBU:
Shukrani kwa dada yetu ambaye ameuliza maswali haya ambayo ni muhimu
1. Kibaba kwa mtu asiyeweza kufunga wakati wa Ramadhan wala kulipa baada ya Ramadhan. Ikiwa mtu ni mgonjwa mtu na anatarajiwa kuwa atapona na hivyo kuweza kufunga itabidi anapokuwa mzima alipe siku alizokula. Lakini ikiwa ni mkongwe au ana ugonjwa asiotarajia kuwa atapata sahali basi itabidi atowe kibaba kimoja kwa kila siku aliyokula. Allah anasema: “Na wale wasioweza, watoe fidiya kwa kumlisha masikini” (2: 184).
Aya hii inatueleza kutoa fidia kwa kutoweza kulipa siku ulizokula kwa kumlisha masikini mmoja kwa kila siku. Hapa unaweza ima ukamwalika masikini aje ale nanyi kwa mwezi mzima wa Ramadhan au pia unaweza kuwaalika masikini sawa na idadi ambayo hukufunga. Wanazuoni wametofautiana kuhusu hichi kibaba, je, ni saa’ (sawa na kilo 2.5 hadi 3) au ni nusu saa’ au ni mudd (gramu 700). Ikiwa unataka kumpatia chakula unaweza kuchagua kima ambacho unaweza kumpatia masikini au ukakisia mwenyewe chakula cha masikini mmoja kwa siku moja. Kwa mfano ikiwa ni mchele mtu wa kawaida huweza kula gramu 250, kwa hivyo kwa siku moja
Na Allah Anajua zaidi.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


